Dk Mwakyembe afanya balaa bungeni

ALIYEKUWA mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond Dk Harrison Mwakyembe ame...


ALIYEKUWA mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond Dk Harrison Mwakyembe amevunja mzizi wa fitna na kuwapasha baadhi ya Wabunge wanaowasafisha viongozi waliojizulu kutokana na kashfa ya Richmond kuwa wanapoteza muda kwani Watanzania sio mabwege.
Dk Mwakyembe alilimbia Bunge Leo kuwa kuna kundi la Wabunge ambao wameandaliwa kuwasafisha viongozi waliotuhumiwa kuhusuka kwenye ufisadi wa Richmond na kusababisha wajiuzulu ili kamati aliyokuwa anaiongoza yeye ionekena kama iliwaonea kwenye ripoti yake.
Mbunge huyo ambaye alizungumza suala hilo kwa hisia kali alitamka bayana kuwa jaribio hilo la kuwasafisha viongozi wanaotuhumiwa katika ufisadi wa Richmond ni kujidhalilisha.
Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu, Dk Mwakyembe alisema kama kuna Wabunge ambao wanaamini kuwa kamati iliwaonea mawaziri na wabunge waliotajwa kwenye ripoti hiyo kuhusika na mkataba mbovu wa Richmond ni vyema waombe Spika avunje kanuni za Bunge ili suala hilo liweze kujadiliwa tena bungeni.
Alisema analazimika kusema maneno hayo kwani suala hilo licha ya kujadiliwa kwa kina bungeni na kasha kutolewa maamuzi kadhaa na chombo hicho; lakini bado kuna baadhi ya Wabunge ambao wameandaliwa kujaribu kuwasafisha viongozi waliotajwa kwenye ripoti hiyo jambo alilodai yeye kama mwenyekiti wa kamati ile hawezi kulivumilia.
Viongozi ambao walijiuzulu nyadhifa zao baada ya kutajwa kuhusika kwenye mkataba mbovu wa Richmond ni aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa, aliyekuwa waziri wa nishati na madini Naziri Karamagi, aliyekuwa waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Ibrahim Msabaha.
Ripoti hiyo pia ilimtaja Mbunge wa Igunga Rostam Aziz kuhusika na umiliki wa Richmond kampuni inayodaiwa kuwa haipo na haikuwahikusajiliwa huko Marekani kama ilivyoonyeshwa kwenye anuani yake.
Dk Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela alisema juhudi za kuwasafisha vigogo hao ni kujidhalilisha kwani Watanzania kwa saa sio tena mabwege wa kuendelea kudanganywa na kuwashawishi waamini kwamba viongozi waliotajwa kwenye ripoti wamesingiziwa na kuonewa.
Alisema Wabunge wanaomini hivyo wawasilishe maombi kwa Spika ili kanuni namba 53 na 54 za Bunge zivunjwe na kamati yake iko tayari suala hilo lijadiliwe tena bungeni na iwapo wanakamati watabainika kuwa waliwasingizia viongozi waliotajwa kuhusika na mkataba huo mbovu wa Richmond wako tayari kujiuzulu Ubunge.
Lakini akaonya kuwa kama suala hilo litajadiliwa tena na ikabainika kuwa viongozi waliotajwa na kujiuzulu walihusika kuingiza nchi kwenye mkataba wenye utata nao wawe tayari kujiuzulu na kuachia ngazi nyadhifa zote za utumishi wa umma walizonazo.
Aliongeza kuwa kamati yake iko tayari kutaja hata yale mambo ambayo waliyaficha kuyatoa hadharani kwenye ripoti hiyo ili kulinda heshima ya serikali ya CCM. Alisema hatua hiyo peke yake ndio itasaidia kuliepusha Bunge ili lisiwe sehemu ya malumbano.
"Hapa tuko busy tu kukashfiana, kwa kweli jambo hili linanikera," alisema na kusisitiza kwa mwenyekiti aliyekuwa anashikilia kiti cha Spika Jenesta Mhagama kuwa aruhusu kanuni ya 53 na 54 ivunjwe ili ibainike yupi mkweli.
Kanuni hizo za Bunge zinamkataza mbunge yeyote kuibua jambo ambalo lilishatolewa uamuzi na Bunge. Kutokana na kitendo cha baadhi ya wabunge kuliibua katika hoja mbalimbali wanazozitoa wakati wa kuchangia hotuba za bajeti na ile hotuba ya makadirio ya ofisi ya waziri mkuu, Dk Mwakyembe alisema kitendo hicho ni kuvunja kanuni hiyo.
Aliongeza kuwa baadhi ya wabunge hao wanadhani kuwa uamuzi huo ulikuwa wanakamati wakati suala hilo baada ya kuwasilishwa bungeni lilijadiliwa kwa kina na kuamriwa katika vipengele zaidi ya 50 ambavyo vinahitaji kutekelezwa na Serikali.
"Kuna wabunge hapa wanadhani uamuzi ule ulikuwa wa Mwakyembe (Harrison), Manyanya (Stella), Mnyaa (Mohamed), Selelii (Lucas), Mtangi (Herbet), hapana ule ni uamuzi wa Bunge," alisema Dk Mwakyembe ambaye mara tu baada ya kikao cha Bunge kuanza aliripotiwa kuugua ghafla.
Alisema ni vyema kifungu hicho kitenguliwe ili wenye mashaka na maamuzi yale watoe dukuduku zao na wao watasema yale yote wanayoyajua kwa namna viongozi waliotajwa kwenye ripoti hiyo walivyohusika kuiingiza nchi kwenye mkataba mbovu na kampuni hewa.
Dk Mwakyembe alisema Bunge haliwezi kugeuka la malumbano "Waje hapa waseme nasi tuko tayari kusema na mengine ambayo hatukuyataja...hatuwezi kuja hapa kila siku tukakumbushia mambo yaliyokwisha amriwa."
Alisema kitendo hicho kinachofanywa na baadhi ya Wabunge ni cha kujidhalilisha mbele ya uso wa Watanzania. Aliongeza kuwa Wabunge walishaanza kupata heshima mbele ya wananchi; lakini kwa vitendo vinavyofanywa na baadhi yao kujaribu kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi wa Richmond ni kujidhalilisha na heshima hiyo inapotea.
Mara tu baada ya Dk Mwakyembekumalizia kuchangia, Lowassa ambaye kwa muda wote alikuwa anamwangalia alitoka nje ya ukumbi wa Bunge na hakurudi tena hadi Jenesta alipositisha shughuli za Bunge hadi jioni.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Dk Mwakyembe afanya balaa bungeni
Dk Mwakyembe afanya balaa bungeni
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDGIHnGVl0k21FHRYTOaLWih-COdNAJecblTkk35iPUt5ogyo1gMFwNYftkV-4R1disuvjYNrYUnRIKl7z-KgEDTOJ6P7VOUrLBQdkjMHRESBWiJVGbjtJslUl9ExfUMagXfabs_Fxv7YM/s320/mwakyembe01bc.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiDGIHnGVl0k21FHRYTOaLWih-COdNAJecblTkk35iPUt5ogyo1gMFwNYftkV-4R1disuvjYNrYUnRIKl7z-KgEDTOJ6P7VOUrLBQdkjMHRESBWiJVGbjtJslUl9ExfUMagXfabs_Fxv7YM/s72-c/mwakyembe01bc.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/dk-mwakyembe-afanya-balaa-bungeni.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/dk-mwakyembe-afanya-balaa-bungeni.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy