FILAMU 50 zinatarajia kushindanishwa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar-ZIFF- linalotarajiwa kuanza Julai 11 hadi 20. Taarifa...
FILAMU 50 zinatarajia kushindanishwa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar-ZIFF- linalotarajiwa kuanza Julai 11 hadi 20.
Taarifa ambazo HabariLeo imezipata jana zinasema kwamba mwaka huu Watanzania wachache walipeleka filamu zao kwa ajili ya kuzishindanisha.
Kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wa ZIFF, Khadija Mohammed ‘Deddah’ ni filamu sita ikiwamo Bongoland 11, na Jando ndizo zilizowasilishwa kwenye ushindani ingawa muda wa kuingiza filamu katika tamasha hilo kwa Watanzania uliongezwa mara mbili.
Tamasha la mwaka huu lina zaidi ya filamu 50 zinazotarajia kuonyeshwa kiushindani.
Miongoni mwa filamu hizo kutoka nje ni pamoja na Behind this Convent (2008) iliyotengenezwa Rwanda, Hero - Wings are Not Necessary to Fly (Hispania) ya mwaka 2007, Pukwa (2008) nchini Kenya, The Great Silence (2008) USA, One Day (2006) Norway, Jando (2006) Tanzania, An Islamic Conscience the Aga Khan and the Ismailis (2008) Uingereza na The Princess from Zanzibar (2007) ya Ujerumani.
Deddah alisema kwamba mbali ya filamu katika tamasha la mwaka huu pia kutakuwa na vikundi zaidi ya 30 kutoka Tanzania, Msumbiji, Malawi, Comoro, Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe na kutoka bara la Asia.
Tamasha la mwaka huu ambalo linabeba ujumbe wa ‘mikinzano ya utamaduni’ mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Ramsey Noah, msanii maarufu wa maigizo kutoka Nigeria.
Katika tamasha hilo pia kutakuwa na jukwaa la vijijini, wanawake na watoto ambapo filamu, warsha na maonyesho kadhaa yatafanyika katika majukwaa hayo.
Tamasha la Nchi ya Jahazi ni kubwa la utamaduni na filamu katika Afrika Mashariki na Kati linalofanyika kila mwaka mara moja tangu mwaka 1998.
Tamasha la mwaka huu linatarajia pia kuhudhuriwa na wakali wengi wa mambo ya sinema kama Newton Aduaka kutoka Nigeria ambaye alitwaa tuzo katika Tamasha la Fesapaco mwaka jana, Danny Golver na Charles Burnett kutoka Hollywood Marekani ambao filamu yao ya Namibia: Struggle for Independence inatarajia kufungua pazia la tamasha hilo la 11.
Mtengeneza sinema Aduaka amethibitisha ushiriki wake.
Wakati huohuo, Ofisa Mtendaji wa ZIFF, Dk. Martin Mhando amesema mwaka huu utakuwa wa kukumbukwa kutokana na ukweli kuwa masuala ya utamaduni Zanzibar yamezingatiwa na wageni watapata fursa ya kuona utamaduni wa Kizanzibari katika mfumo wa fensi ya Zanzibar.
Pia alisema pia kutakuwa na filamu za Kinaijeria ambazo zitakuwa zinaonyeshwa.
"Huwezi kudharau mchango mkubwa wa sinema za Kinaijeria katika ukuaji wa sinema bara la Afrika" alisema Dk. Mhando.
Kutakuwa pia na sinema nne zitakazoonyeshwa kwa mara ya kwanza (primia).

Pichani ni CEO wa ZIFF Dk Martin Mhando (kushoto) na afisa habari Deddah wakiwa katika ofisi za ZIFF Ngome Kongwe, Unguja.
COMMENTS