KAMA kuna picha ya Kiswahili ambayo niliipenda kwa angle na twist , filamu iliyotoka karibuni ya The Lost Twins sehemu ya kwanza na ya pili,...
KAMA kuna picha ya Kiswahili ambayo niliipenda kwa angle na twist , filamu iliyotoka karibuni ya The Lost Twins sehemu ya kwanza na ya pili, ndiyo yenyewe, Waswahili wangesema habari ndiyo hiyo.
Filamu hii inamuweka Kanumba katika udereva imempika vyema Lucy Peter aliyecheza nafasi ya upacha ya Mary na Anita.
Waigizaji wengine waliomsindikiza staa wetu ukimwacha mbali Kanumba, Suzan Lewis, Elizabeth Chijumba na Mzee Chilo wamefanikiwa kutengeneza kitu kwa uhalisia wake na kukifanya kiwe chakula bora katika ulimwengu wetu wa filamu unaozidi kushika chati hapa nchini.
Naam ni habari ya mama aliyezaa wawili akapokonywa mmoja na kisha wakaa tofauti kwa miaka ipatayo 20, jamaa wamepatia muda, hasa kwa kufunika kivuli.
Ni hadithi ya Susan Lewis kununua mtoto ili kuongeza mapenzi kwa mume wake, kuamua kuua mume kwa kumtwanga na sumu na kupoteza urithi ambao alidhani utakuwapo.
Ni kama vile hadithi za hapa kwetu ukiingia katika utajiri unaua mume ili 'ufitike' stauti na urithi wake. Si kwa Susan ambaye aliua na kisha kukosa utajiri.
Ni hadithi ya mapacha wawili waliolelewa katika sehemu tofauti tabia tofauti wakapambana na mikasa tofauti kwa kufanana kwao lakini mwishoni wanakuwa pamoja.
Ni hadithi ileile ya kumrejea Mungu kwa sababu tofauti huku mama Nelson akisema ukweli kwa sababu ya hasira.
Mwishoni kila kitu kilikaa mahali pake, lakini ni hadithi yenye utamu wa aina yake kwani angle na twisti Mtitu kazipatia, na mtu wa kontinuiti alifanya kazi yake kwani kasoro unazitafuta, hazionekani wazi.
Game 1st Quality Tz Limited kwa sinema hii ya Mtitu, si tu kwamba wamekusanya wenye majina bali wametoa nafasi ya watu kuonyesha kwamba wanaweza.
Naam walikwenda Extreme maeneo fulani hasa katika maleba lakini unaweza kuona kabisa pamoja na uchache wa dayologu kazi kubwa imefanyika na una haki ya kuipenda kazi hii. Ninaweza kusema moja ya kazi ninayoiheshimu kutokana na kujituma kwa watu wake.
Ule ukakasi wa title za Kiingereza ni kawaida kwani kwetu sisi si tunakienzi Kiswahili bali ni kuukubali ule ukweli kuwa kizazi cha sasa ni Kiswaenglish.
Mimi natoa tano kwa filamu hii na salamu zenye kuheshimika kwa wahusika.
Pamoja na filamu hii kuwa ndiyo imeingia Salamander bado chati ya Salamander haikubadilika kwa wiki iliyopita.

Kaka Sempa wa Salamander amesema hali imebaki vilevile, hii ndivyo ilivyo:
Ifuatayo ni misimamo mbalimbali ya filamu kwa wiki iliyopita.

Msimamo wa filamu katika maktaba ya Salamander( kasi ya kuazima) na pia majuu katika Top ten za USA.
Filamu za Kiswahili
1--- COPY
2--- MISS BONGO
3--- POINT OF NO RETURN
4--- SHE IS MY SISTER
5--- DAR TO LAGOS
6--- THE GREENA
7--- AGANO LA URITHI
8--- I CANT FORGET
9--- DIVERSION OF LOVE
10-- MAHABUBA
Filamu za Kiingereza
1--- THE RANDIOTION
Filamu za Kiingereza
1--- THE RANDIOTION
2--- BATTLE TO HADITHIA
3--- THE TAKE
4--- 10.000 BC
5--- WHY DID I GET MARRIED
6--- SHOOT THEM UP
7--- FORBIDEN KINGDOM
8--- RAMBO IV
9--- WE OWN THE NIGHT
10-- NO COUNTRY FOR OLD MAN
Filamu za Hollywood (Top Office Box)
1.The Incredible Hulk
2.Kung Fu Panda
3.The Happening
4.You Don't Mess With the Zohan
5.Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull
6.Sex and the City
7.Iron Man
8.The Strangers
9.The Chronicles of Narnia: Prince Caspian
10.What Happens in Vegas View
COMMENTS