LEO asubuhi gazeti moja la wiki linaloitwa Changamoto limetoka na habari hii ambayo mimi sitaki kuijadili ingawa nina maswali kibao juu yake...
LEO asubuhi gazeti moja la wiki linaloitwa Changamoto limetoka na habari hii ambayo mimi sitaki kuijadili ingawa nina maswali kibao juu yake. Lakini swala kuu (hapana, suala Kuu) ndani ya habari hiyo ni matumizi ya alama za kiserikali katika mambo binafsi. Halafu inakuwaje hasa nyumba ya PCCB kuuzwa na Wizara ya Miundo mbinu kupitia wakala wake wa majengo ,halafu unaona kitu kigumu kabisa imeuzwa baada ya ukarabati.Sina hakika, lakini huyu jamaa anayetakiwa kuzuia rushwa kama kweli amelipa mifedha yote hii kwa namna barua hii inavyoonyesha basi mambo ni mnega msega. Pata taarifa rasmi kwa Changamoto mimi nimekuchapia habari hii neno kwa neno hata likikosewa.
Kigogo Takukuru ajiuzia
hekalu kwa bei ya kutupa
· Lina thamani ya mil 500/=
· Alinyakua kwa 56/=
NA MWANDISHI WETU
WAKATI mzimu wa Richmond na EPA ukiwa bado unazunguka, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward Hosea anadaiwa kujiuzia nyumba ya taasisi hiyo kwa bei ya kutupa.
Habari za kuaminika kutoka TAKUKURU zinadai kuwa, nyumba hiyo namba 1/8 ya ghorofa moja iliyopo Mtaa wa Chisiza Oysterbay Dar es Salaam, imenunuliwa kinyume cha utaratibu.
Kulingana na chanzo chetu hicho cha habari, nyumba hiyo haikuwa miongoni mwa nyumba ambazo zilipaswa kuuzwa kwa watumishi kwa kuwa si mali ya Wizara ya Miundombinu, na kwamba ni mali ya (TAKUKURU).
Habari hizo zinadai kuwa, nyumba hiyo ilinunuliwa na TAKUKURU kutoka kampuni ya simu 2000 iliyokuwa ikisimamia mali za Kampuni ya Simu nchini (TTCL), ambapo inaelezwa kuwa gharama za kuinunua na kuifanyia ukarabati zinadaiwa kufikia shilingi milioni 500.
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, nyumba hiyo ilinunuliwa kati ya mwaka 2004/05 wakati wa uongozi wa Meja Jenerali Mstaafu Anatory Kamazima na kukarabatiwa maalum kwa ajili ya makazi ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo.
“Nyumba ile ilinunuliwa mahsusi kwa ajili ya makazi ya Mkurugenzi wa Mkuu wa Takukuru. Kwamba yeyote anayeteuliwa kushika wadhifa huo, angeishi pale,” kilibainisha chanzo chetu.
Hata hivyo ilidaiwa kuwa mara baada Mkurugenzi wa sasa kushika usukani wa kuongoza taasisi hiyo, mpango mkakati uliandaliwa kuhakikisha anamiliki nyumba hiyo.
Habari hizo zinadai kuwa, mpango huo wa kununua nyumba hiyo kwa bei ya kutupa, ulifanikiwa kutokana na msaada mkubwa Hosea aliopewa na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Miundombinu pamoja na Wakala wa Majengo nchini (TBA).
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, Mkurugenzi huyo anadaiwa kujiuzia nyumba kwa shilingi milioni 56/=, huku ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500/=.
Tayari Mkurugenzi huyo anadaiwa kulipa kiasi hicho cha fedha katika awamu mbili tofauti.
Katika awamu ya kwanza alilipa shilingi milioni 10 kwa risiti namba ERV 26051976 ya Februari 11, mwaka huu.
Aidha, katika awamu ya pili Mkurugenzi huyo alilipa shilingi milioni 46 kupitia risiti yenye namba ERV 26069612 ya April 9 mwaka huu.
Sakata la kigogo huyo kujiuzia nyumba hiyo, linadaiwa kupingwa na baadhi ya watendaji wa Makao Makuu ya taasisi hiyo kwa kile kinachodaiwa kwamba, kutaifanya taasisi hiyo kuingia gharama kubwa ya kununua au kujenga makazi ya mengine kwa ajili ya Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo nyeti nchini.
Mbali na hayo Mkurugenzi huyo anadaiwa kutumia nyaraka za ofisi katika mawasiliano yake ya kuuziwa nyumba hiyo, jambo ambalo kwa mujibu wa utumishi wa umma inadaiwa haliruhusiwi kwa kuwa hilo ni suala lake binafsi.
Inadaiwa kuwa, katika harakati za kuhakikisha anafanikiwa kuitwaa nyumba hiyo, tayari amemuandikia barua Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini kumfahamisha kufanikiwa kwake kumaliza deni lake la kununua nyumba hiyo na kuomba kuandaliwa hati ya kumiliki.
Barua hiyo ikiwa na mchanganuo wa malipo ya shilingi milioni 56, iliandikwa Aprili 8 mwaka huu kwenda kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo, ikiwa na kumbukumbu namba PCB/PF/EH/459.
Sehemu ya barua hiyo iliandikwa: “Napenda kukufahamisha rasmi kwamba nimelipa deni lote la Tshs. 56m/- ambalo ni gharama za kuuziwa nyumba tajwa hapo juu… Naomba niandaliwe hati miliki ya nyumba hii.”
Alipotafutwa na gazeti hili ili kufafanua madai hayo, Mkurugenzi Mkuu huyo wa Takukuru hakupatikana kwa kile kilichosemekana kuwepo safarini nje ya nchi.
Naye msemaji wa TAKUKURU Mary Mosha alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu suala hilo aliomba kupewa muda ili kulifanyia kazi.
“Naomba nipe muda nifanyie kazi, niletee taarifa kwa maandishi”, alisema Mosha.
Awali Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU Lilian Mashaka alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema yeye si msemaji wa taasisi hiyo na kushauri atafutwe msemaji wa taasisi ili azungumzie suala hilo.
Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Wakala wa Majengo Francis Segolina alisema taarifa za uhakika kuhusu suala hilo na kumtaka mwandishi wa gazeti hili amuone Mkurugenzi wa majengo au Afisa Mtendaji mkuu.
Gazeti hili lilipotaka kumuona Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa majengo (TBA) Makumba Kimweri, Katibu muhtasi wake alitaka aandikiwe maswali ili awasilishe kwa bosi wake.
Pamoja na CHANGAMOTO kuandika swali kutaka ufafanuzi, Afisa Mtendaji mkuu huyo alijibu kupitia katibu muhtasi wake kwamba hakuwa katika nafasi ya kujibu swali hilo na kumtaka mwandishi kufuatilia baada ya siku moja au mbili.

COMMENTS