Si kejeli lakini ni kweli kuwa Bunge limeambiwa kuwa uamuzi wa kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma upo palepale. Serikali ikijieleza Bungeni...
Si kejeli lakini ni kweli kuwa Bunge limeambiwa kuwa uamuzi wa kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma upo palepale.
Serikali ikijieleza Bungeni leo Juni 19,2008 imesema kwamba bado ina mpango wa kuhamisha makao ya nchi Dodoma na kwamba uhamiaji utafanyika kwa haraka endapo miundombinu na huduma nyingine muhimu zitakapokamilika.
Akijibu swali la Mbunge wa Nkasi, Ponsiano Nyami (CCM), aliyetaka kufahamu ni lini serikali inakusudia kuhamia Dodoma na mwaka gani au karne gani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo alisema jambo linalokwamisha kwa sasa ni hali halisi ya fedha.
“Namhakikishia Mbunge mbele ya Bunge hili tukufu kwamba dhamira ya serikali iko palepale ya kuhamia Dodoma isipokuwa tatizo ni fedha, kama ikipatikana utaratibu huo utakamilika mara moja,” alisema Marmo.
Nyami pia alitaka kufahamu kama kitendo cha serikali kuendelea kujenga majengo mapya kwenye ofisi za wizara na idara zake Dar es Salaam si kiini macho cha kuita Dodoma Makao Makuu ya Nchi.
Akijibu hoja hiyo, Marmo alisema serikali ilitenga hekta 53 katika mpango kabambe wa Mji wa Dodoma kwa ajili ya kujenga ofisi za serikali na huduma nyingine muhimu na kwamba eneo hilo linalojulikana kama ‘National Capital Centre’ lipo eneo la Mlimani, kusini mwa barabara inayojengwa sasa ya Chuo Kikuu cha Dodoma na tayari eneo hilo limesanifiwa katika mipango.
Usanifu wa eneo hilo ulimalizika mwaka 1980 na kinachosubiriwa ni kujengwa kwa miundombinu pamoja na usanifu wa majengo mbalimbali ya wizara. “Kazi ya kuufanya Mji wa Dodoma Makao Makuu ya Nchi inahitaji rasilimali nyingi na muda mrefu hili si jambo la mara moja,” alisema.
Alisema huduma muhimu kama nyumba za kuishi wafanyakazi na ofisi bado zinaendelea kuendelezwa kulingana na uwezo wa serikali na kwa sasa serikali inakusudia kushirikisha sekta binafsi katika uwekaji wa miundombinu na huduma badala ya dhana yake ya mwanzo kufanya hivyo yenyewe.
Kuhusu kuendelea kwa ujenzi wa wizara na idara Dar es Salaam, alisema ni kutokana na kuongezeka kwa shughuli za wizara pamoja na ongezeko la wafanyakazi hivyo kulazimu kupanua maeneo ya ofisi zao kwa kujenga majengo mapya ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi.
“Ujenzi wa majengo mapya Dar es Salaam, wala si kikwazo cha wizara hiyo kuhamia Dodoma maana hata zikihamia Dodoma, majengo hayo yanaweza kukodishwa kwa watu wengine kwa vile bado Dar es Salaam itaendelea kuwa Jiji la kibiashara,” alisema.

Pichani moja ya mitaa ya Dodoma, Kuu kama ilivyonaswa na mdau Albart Jackson wa The Football
COMMENTS