MUFTI wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa Shaaban bin Simba amewataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini, kutohusisha magonjwa yake na imani za ki...
MUFTI wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa Shaaban bin Simba amewataka waumini wa dini ya Kiislamu nchini, kutohusisha magonjwa yake na imani za kishirikina.
Badala yake, ameeleza kuwa anaumwa ugonjwa wa kisukari kwa miaka 24 sasa, na pia hivi karibuni, moyo wake ulijaa maji, hivyo akalazimika kupelekwa matibabuni India. Pia mguu wake umegundulika kuwa na vijidudu vya bakteria.
Akizungumza rasmi kwa mara ya kwanza na waumini wake tangu arejee nchini kutoka kwenye matibabu India, Mufti alisema amekuwa akiumwa ugonjwa wa kisukari kwa miaka 24 sasa, hivyo aliwataka waumini wasiyahusishe matatizo yake ya kiafya na imani za kishirikina.
“Ugonjwa ni sehemu ya kawaida ya maisha ya mwanadamu…hata uwe sheikh, uwe mtu wa kawaida, ni lazima utaumwa tu. Msifikirie kwamba nimepigwa mzinga, wala nilipokuwa Arusha sikuwa nimefichwa,” alisema Mufti alipojibu maswali ya waandishi wa habari kwenye hadhara ya waumini wa Kiislamu kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu, Kinondoni, Dar es Salaam Juni 13.
Aidha, Mufti Simba alisema pia kuwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo kujaa maji, kisukari na wingi wa vijidudu vya bacteria katika mguu wake wa kulia.
Mufti ambaye alikuwa matibabuni India kwa takribani miezi miwili, alisema anatarajia kurudi tena katika Hospitali ya Tiba ya Madrasa iliyopo India baada ya miezi mitatu kwa matibabu zaidi.
Alisema hakukuwa na ugumu kwa vyombo vya habari nchini kupata habari kuhusu afya yake, kwani alikuwa akipatikana kwa simu, hivyo hakukua na sababu ya kuripoti tofauti na hali halisi ilivyokuwa.
Akiwa India, kumekuwapo na uvumi mwingi ukihusisha ugonjwa wa kiongozi huyo Mkuu wa Waislamu nchini, zikiwamo habari kwamba amelogwa na wengine wakisema alikuwa amekatwa mguu wake mmoja.
Mufti leo alikuwa akitembea kwa msaada wa kifaa cha kutembelea huku akisaidiwa na msaidizi wake kushuka na kutembea huku miguu yake miwili ikiwa mizima, tofauti na baadhi ya vyombo vya habari vilivyodai akiwa India kwamba amekatwa mguu.
Aidha, Mufti aliwaeleza waumini hao wa Kiislamu kwamba atafuatilia tuhuma za migogoro ndani ya dini hiyo na kuchukua hatua mbadala dhidi ya hali hiyo.
Mufti alisema anahitaji muda zaidi kuyashughulikia matatizo yanayohusu dini hiyo ikiwamo kufuatilia barua zilizoandikwa kwa jina lake, zikisisitiza kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi wa dini hiyo.

COMMENTS