Nani anasema ukweli kuhusu Sekondari Mwakaleli?

Hii ni barua pepe ambayo imefikia blogu hii.haikuhaririwa wala kitu chochote imetolewa kama ilivyoandikwa. Je ni nani hasa anahusika? Nini h...

Hii ni barua pepe ambayo imefikia blogu hii.haikuhaririwa wala kitu chochote imetolewa kama ilivyoandikwa. Je ni nani hasa anahusika? Nini hasa kinastahili kufanywa. Je hii ndiyo adhabu rekebishi?Angalau mtu mmoja anatakiwa kuangalia haya!

Soma haya kama yalivyoletwa.


YAH: KUOMBA KURUDISHWA KWA KIDATO CHA SITA
SHULENI MWAKALELI SEKONDARI.
WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA.


Sisi wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Mwakaleli ambao ni wahusika wa tatizo la uharibifu uliofanyika shuleni tarehe 30/may 2008 siku ya Ijumaa tumeamua kufikisha madai yetu kwako ili tusaidiwe kulingana na adhabu iliyotolewa na bodi ya shule kuwa uharibifu uliofanyika ulifikia thamani ya shillingi za kitanzania milioni Arobaini (Tsh 40miliom ) wakati kitu ambacho hatujakubaliana nacho na adhabu iliyotolewa ni kuwafukuza wanafunzi themanini na watatu na Viongozi wote wa serikali ya wanafunzi. Pia wanafunzi waliorudishwa ni sabini na watatu na watalipa fidia ya shilingi za kitanzania laki nne na elfu Hamsini ( 450,000/=) Adhabu iliyotolewa na bodi ya shule haijazingatia kurekebisha matatizo yaliyosababisha uharibifu uliofanyika na vurugu zote za siku hiyo. Pia sisi kama walengwa wa shutuma (tatizo) hilo hatujapewa nafasi ya kujieleza na kusikilizwa, Hivyo tumeamuwa kuitaarifu ofisi yako ili ishughulikie shauri letu.

Sisi kama wahusika wa tatizo hilo tunakubali kuwa uharibifu ulitokea ila kuna sababu zilizo sababisha yote hayo kufikiwa. Sababu za matatizo yote hayo zimegawanyika zimegawanyika katika sehemu mbili ni kama hizi zifuatazo.
Sababu za muda mrefu na sababu za muda mfupi (wakati wa tatizo) kati ya sababu za muda mrefu ni hizi zifuatazo
(walimu wa masomo ya uchumi na geography)
Walimu kutokuingia madarasani katika vipindi kwa madai kuwa wanamajukumu mengine tofauti ya kiofisi tofauti na ufundishaji. Hivyo tulihitaji kuongea na mkuu wa shule ili suala hilo litatuliwe haraka iwezekanavyo kwani sisi ni watahiniwa. Kwani tayari tulishindwa kuelewana na walimu husika kwani walitujibu kwa kauli ambazo si nzuri mfano mwalimu Elicko sanga alitupa kauli hii” uwezo wa kuacha kufundisha ninao, nikawepo mazingira ya shule nikaotea jua na mwisho wa mwezi mshahara wangu ukawa palepale.”mwalimu huyu alikuwa akifundisha masomo ya historia na geographia ambayo ni viungo kwa wanafunzi wa Lugha na Wauchumi. Hivyo ni dhahiri kuwa shule haikuwa tayari kutusikiliza madai yetu sisi kama wanafunzi.
Pia sisi kama wanafunzi tuliodhaminiwa na Serikali kuishi maisha ya Bweni tulihitaji kuhoji uhalali wa wanafunzi wa O’level wanaoishi mabwenini shuleni hapo. Nafasi hiyo ya kujieleza na kuuhoji uongozi wa shule tulinyimwa (hatukupewa). Hiyo ikawa ni sababu nyingine iliyotuweka sisi wanafunzi katika wakati mgumu. Na tukiamini mkuu wa shule ndiye kimbilio letu lakini hakuwa tayari kutusikiliza.

Uhaba wa chakula shuleni ni tatizo jingine ambalo liliikabiri shule yetu kwa wakati huu. Ili kukabiliana na tatizo hilo pia tulihitaji kuwasiliana na Mkuu wa Shule ili tujue mstakabali wa chakula kulingana na tatizo hilo. Kunyimwa nafasi ya kuongea na mkuu wa shule ni sababu ya muda mrefu iliyotukabili shuleni kwetu.

Hizo ni sababu matatizo yaliyokuwepo shuleni kwetu kwa muda mrefu. Licha ya matatizo hayo ya muda mrefu pia kuna sababu ambazo ndizo zilizochangia kwa kiasi kikubwa matatizo mengine ya uharibifu wa siku hiyo ya tarehe 30 may 2008. sababu hizo nihizi zifuatazo
- kauli chafu kwa wanafunzi wa kidato cha sita zilizotolewa na mwalimu charles Ntimi tarehe 29/may/2008 siku moja kabla ya matatizo hayo kutokea. Mwalimu huyo ambaye ndiye aliyepigwa alikuwa katika mtafaruku na wanafunzi hivyo tulihitaji kuongea na mkuu wa shule kumueleza suala hilo ili amrekebishe lakini ikaonekana bado hayuko tayari kutusikiliza hivyo kusababisha hasira kwa wanakidato cha sita.
- Mwalimu huyo kikazi alikua bado ni mgeni na alipanga kuwagawanya wanafunzi wa kidato cha sita kwa kutumia system ya devide and rule. Kitu ambacho kiliwakera wanakidato cha sita; kwa kuwaonyesha dhamira zake kikazi. Kwa maamuzi ya utendaji huo wa mwalimu huyo na viongozi wa serikali ya wanafunzi tuliwekwa katika wakati mgumu kimaamuzi) wakiwa katika nafasi ya kutengwa mbali na wanaowaongoza.

- Iliyokuwa serikali ya wanafunzi shuleni hapo haikupewa nafasi ya kusikilizwa na kuombwa ushauri katika maamuzi ya utawala viongozi hao katika wakati mgumu kiusalama na kuamua kujiudhuru ili kujisalimisha.
Kulingana na matatizo hayo pia tuliomba mkuu wa shule tuongee nae ili kumueleza matatizo yetu lakini alikataa hatua ya kutokukubali kuongea nasi na kutoa kauli ambayo ndiyo ilileta hasira kwetu na kuona hatuna mtetezi mwingine maeneo yale. Alisema “form six hadi sasa nimewatema, sio headmaster wao tena , bebeni vitu vyenu nendeni popote mnapo hisi mtasikilizwa” baada ya hapo ndipo wanafunzi wa kidato cha sita walipokasirka na kufanya uharibifu wakati mwalimu Charles Ntimi anatafutwa aliyekuwa amejificha katika jengo la utawala. Hivyo ilikuwa katika kumtafuta mwalimu huyo ambapo ndipo vioo vya jengo la utawala vilivunjwa, milango na mila ya umeme, Computer moja, Typing machine na kuvunja vitu vya stoo ya chakula. Hivyo ndivyo vitu ambavyo kwa mtazamo wetu tunatambua viriharibiwa na tunadhani vilihesabiwa katika uharibifu huo.
- kulingana na maamuzi ya bodi ya shule imetangaza kuwa hasara ya uharibifu huo ni wa thamani ya zaidi ya Tsh milioni arobaini, gharama ambayo hatujakubaliana nalo.
- Pia imedaiwa kuwa aliibiwa zaidi ya shilingi laki saba ambazo zilikuwa katika moja ya ofisi ya shule. Kwa sheria tunaamini kuwa hakuna sheria inayohusu pesa ya serikali kukaa ofisini zaidi ya kila moja. Hivyo tunapinga mashtaka ya bodi kwa kwa suala hilo.
- Bodi hiyo imetoa adhabu ya kuwafuta shule wanafunzi themanini na watatu (83), na kuwarudisha wanafunzi sabini na nne (78) ambao watalipa fidia ya shilingi laki nne na nusu (Tsh 450,000/=) pia hatujakubaliana na maamuzi hayo kwa upande wa bodi kwani hatujajua wametumia mbinu ipi kuwapata hao sabini na nne kuwa si waharifu katika tukio hilo, ilihali hawajatuhoji sisi kama wahusika. Hivyo tunaomba ofisi yako tukufu ifuatilie mashauri yaliyofanywa na bodi ya shule, kwani haijafuata haki. Pia adhabu iliyotolewa ni ngumu kwa wazazi wetu wa hali ya kati kiuchumi.
- Pia tunapingana na kauli iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa tulichapa walimu wetu viboko kama ilivyotangazwa. Mwalimu aliyepigwa ni mmoja tu Mwalimu Charles Ntimi na si walimu wote kama invyotangazwa. Hata mwalimu huyo alipigwa kulingana na hali tuliyojengewa na mkuu wa shule kwa kutotusikiliza.
- Pia tumedharirishwa na vyombo vya habari kuwa tulivuta bangi kwa takribani masaa manne. Shutuma hizo tunazipanga na tuko tayari kupimwa afya zetu ili kubaini kauli hiyo. Huo ni udhalilishwaji wa hari ya juu kwa wasomi kama sisi.
Ombi letu kwa Ofisi yako ni kwamba Tunaomba tume au ofisi teule iondoe ili ichunguze kwa undani sababu za matatizo hayo na wanafunzi waliofukuzwa shule warudishwe na uchunguzi ufanywe katika gharama za uharibifu, zitajwe upya baada ya kamati ya uchunguzi kumaliza kazi yake.


Wako Watiifu
Wana wa kidato cha sita shule ya sekondari Mwakaleli

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Nani anasema ukweli kuhusu Sekondari Mwakaleli?
Nani anasema ukweli kuhusu Sekondari Mwakaleli?
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/nani-anasema-ukweli-kuhusu-sekondari.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/nani-anasema-ukweli-kuhusu-sekondari.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy