WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema tatizo la ubovu wa miundombinu hasa nyakati za mvua jijini Dar es Salaam, linahitaji kupewa kipaumbele na ...
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema tatizo la ubovu wa miundombinu hasa nyakati za mvua jijini Dar es Salaam, linahitaji kupewa kipaumbele na serikali na si kuachiwa Halmashauri za Manispaa kulitatua.
Akizungumza bungeni wakati akimsaidia kujibu swali la nyongeza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri leo Juni 10, alisema ni wazi kuwa tatizo hilo linahitaji kutatuliwa kwa ushirikiano.
“Juzi nilikutana na madiwani nikawaahidi kuwa itabidi suala hili tulirejeshe serikalini na tulishughulikie kwa pamoja na manispaa, hatuwezi kulifanikisha kwa kutegemea manispaa pekee,” alisema Pinda.
Katika swali lake la msingi, Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan (CCM), alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kusaidia Halmashauri ya Kinondoni kuondoa kero za ukosefu wa mifereji ya kuondoa maji kwenye barabara katika kata za Mwananyamala, Makumbusho, Kinondoni, Tandale na Hananasif.
Akijibu swali hilo, Mwanri alikiri kuwa mvua zilizonyesha Dar es Salaam mwaka huu, zilisababisha mafuriko sehemu mbalimbali likiwamo Jimbo la Kinondoni na kwamba katika manispaa hiyo, mafuriko yalisababishwa na baadhi ya maeneo kutokuwa na mifereji ya maji ya mvua.
Naibu Waziri alisema pia kuwapo kwa miundombinu ya maji ya mvua chini kwa chini ambayo ilijengwa mwaka 1950 hasa maeneo ya Mwananyamala na Kinondoni ambayo sasa imechakaa na kuzidiwa uwezo yakiwamo maeneo yanayojaa maji na kusababisha mafuriko, akitolea mfano bwawa la Msisiri A na Shoppers Plaza.
Alisema baadhi ya maeneo yamekuwa na mifereji ya mvua ambayo haikidhi utiririkaji na usafirishaji wa maji ya mvua na hivyo kuhitaji upanuzi wa baada ya maeneo kuendelezwa na pia tatizo la mikondo ya maji ya asili kubadilishwa na wananchi na kuwa viwanja nalo huchangia mafuriko.
Katika kukabiliana na tatizo hilo, tayari Manispaa ya Kinondoni katika bajeti ya mwaka 2007/2008, ilipeleka fedha wastani wa Sh 100,000 hadi Sh 300,000 kwa kata 16 kwa ajili ya kusafisha mifereji ya maji ya mvua iliyopo kwenye kata hizo kwa mpango shirikishi jamii, alisema.
Alisema pia katika bajeti ya matengenezo ya barabara mwaka 2008/2009, Manispaa ya Kinondoni imeomba kupatiwa Sh milioni 491 kwa ajili ya kujenga mifereji mipya ya maji ya mvua katika maeneo korofi ambayo ni Makumbusho, Mwananyamala, Kinondoni na Msasani.
Mwanri pia alisema manispaa hiyo ina mikakati ya upanuzi wa mifereji ya maji ya mvua eneo la Tandale kwa Mtogole, ukarabati na uzibuaji mifereji ya maji ya mvua na makalavati maeneo ya Hananasif, Mwananyamala sekondari, katika shule za Turiani na Kijitonyama.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), ambaye alitaka kujua kama serikali iko tayari kuziruhusu manispaa kukopa ili kukabiliana na tatizo hilo, Mwanri alisema suala la Dar es Salaam linamuumiza kila mtu ikiwamo serikali.
Alisema suala la manispaa kukopa, upo utaratibu unaoruhusu halmashauri kukopa ila kama hali itakuwa mbaya na kufanya halmashauri hizo kukopa, basi serikali inabidi iangalie suala hilo.

Pichani waziri mkuu akizungumza bungeni.
COMMENTS