Jamani kuna mdau alinitumia kitu hiki Mei 31, asubuhi lakini nikawa njiani. Kwa jinsi mambo yalivyo ni dhahiri kwamba hata wewe mdau unataki...
Jamani kuna mdau alinitumia kitu hiki Mei 31, asubuhi lakini nikawa njiani. Kwa jinsi mambo yalivyo ni dhahiri kwamba hata wewe mdau unatakiwa kuangalia kwa makini hii kitu manake nina hasara na hasira na mambo yanavyokuwa.
Shughuli iko mlangoni, kadi ya mwaliko ya nini?
Leo hii, Tanzania inatupa kete muhimu katika mchakato au mbio za kuwania kufuzu kwenda kwenye fainali za michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika Afrika ya Kusini mwaka 2010.
Bahati mbaya, wapo baadhi yetu wanaofikiri kuwa wanaowania tiketi hiyo ni Taifa stars na wala si nchi. Hapa ndipo kwenye maneno. Hii si sawa! kwa sababu Taifa Stars wanawania nafasi hiyo kama wawakilishi au askari wanaosimama kwa niaba ya Taifa.
Timu ya Taifa kama wapiganaji wao ndio wako msitari wa mbele uwanjani, lakini nyuma lipo Taifa, tupo sisi. Inaposemwa kuwa timu ya Taifa inawania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia ni sawa kwa upande mmoja kwa ile sababu ya kuwa wao ndio wanaocheza lakini kwa upande si sawa kwa sababu mpira unachezwa ndani na nje ya uwanja na pengine nje ya zile dakika 90 ndio kuna muda mrefu wa maandalizi yote muhimu.
Nakumbuka kuna wakati nchi hii ilipokuwa inapigana na Nduli Amini, Makamanda wetu Shujaa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Vikosi Vya Ulinzi na Usalama walimwambia Mwalimu asiwe na wasiwasi kuhusu hali ilivyo kule Kagera kwamba Idd Amin tutampiga kwa sababu alituchokoza mwenyewe. Ndivyo ilivyokuwa. Nasikia baadhi ya Makamanda walikuwa katika shughuli za kisiasa lakini waliposikia shughuli iko mlangoni, hawakusubiri kutafutwa au kuombwa! Walikwenda moja kwa moja mstari wa mbele. Mtu chake. Nenda Kampala utaambiwa kazi ya mashujaa hao ilikuwaje.
Naizungumzia vita ya Kagera kwa sababu, pengine ndio kipimo cha hamasa na ari ya hali ya juu niliyopata kuiona katika nchi hii kwa sababu harakati za kuikomboa nchi hii sikuziona kwa hiyo siwezi kuzisemea. Naizungumzia vita ya Kagera kwa jinsi ambavyo kila mtu alikuwa tayari kutoa alichonacho, wakati mapambano yanaendelea kuna watu walikuwa wanafanya mazoezi ya kujitolea kwenda mstari wa mbele. Tuliposhinda, ulikuwa ushindi mnono kwa sababu kila mtu alishiriki. Nakumbuka baada ya kumtokomeza nduli, Makamanda wetu walituma Ujumbe kwa Mwalimu wakimpa salamu za pongezi kwa ushindi. Kipimo kikuu cha upendo na utii na mapenzi kwa Taifa kwa sababu wao ndio walioenda vitani na wao ndio waliopigana lakini ni wao ndio waliotuma salamu za ushindi na pongezi kwa Rais na wananchi.
Sitaki hoja yangu kuigeuza kuwa kolamu ya mashujaa au historia. Nimeisema hii kwa sababu ya hiki ambacho kiko mlangoni kwetu leo hii. Safri ya kwenda Afrika ya kusini ndio hii, lakini nachelea kama kweli kila mmoja wetu yuko tayari.
Napenda kuwapongeza waliozindua kampeni ya kick the ball na ile ya zamani ya goo Tanzania goo. Kwa sasa kama kuna mtu ana ushauri au mchango wowote kuhusu namna ya kuiwezesha timu yetu ishinde na kwenda Afrika ya Kusini, akienda TFF hawatamfungia mlango. Michango yetu ya hali na mali inahitajika zaidi wakati huu kuliko wakati wote na pengine kipindi hiki ndio bahati yetu kuliko muda wote tuliowahi kuwa nao.
Kitu ambacho nakipinga kwa kinywa kipana ni baadhi ya vijitabia vyetu vya kulaumu, tumekuwa watu wa lawama mno. Nalisema hili mapema, tena Mungu bariki atuisaidie tushinde, lakini tukishindwa (Mungu apishie mbali) utasikia, miongoni mwetu watu wataanza ooh mimi nilijua tu hatufiki mbali kwa sababu moja mbili tatu hayakutekelezwa.
Tunataka kujenga vijitabia vya kutoa lawama au sababu za utetezi baada ya kisa. Yaani tumekuwa watu wa mikasa. Tunaposhindwa tunakuwa wachambuzi wazuri wa postmoterm ya kutoa sababu za kwanini tulishindwa au hatukufanikiwa kwa sababu hatukutekeleza baadhi ya mambo.
Bahati mbaya zaidi wapo miongoni mwetu hadi leo hii wanasubiri kadi ya mualiko wa kuchangia timu ya Taifa. Utasikia ooh sisi hatukuitwa kutoa maoni yetu. Tungetoa maoni yetu yangewasaidia sana wale vijana. Muda wa kutoa maoni hayo ni sasa. Mimi sidhani kama TFF wanakataa watu au kikundi cha watu iwe ni wataalamu, makocha au wachezaji wa zamani kutoa maoni yao. Cha msingi ni kufuata taratibu. Nitawashangaa sana TFF kama wakifunga milango na kuziba masikio ya kutopokea maoni kwa sababu timu hii si ya TFF ni timu ya Watanzania wote.
Kama kuna wachezaji wa zamani wanaotaka kuongea na wachezaji wa sasa wa Timu ya Taifa ili kuwapa mbinu za medani ambazo pengine hata makocha huwa hawawezi kuzitoa zote kwa sababu nyingine ni vipaji vya mtu mmoja mmoa, wakati wa kutoa mambo hayo ilikuwa jana na wakati muafaka ni leo. Ni sasa. Tuache lawama shughuli ndio hii iko mlangoni mtu asisubiri mpaka aje aombwe. Tuwape TFF halafu tubaki kuwalaumu kama hawatazingati ushauri wetu.
Kama kweli watanzani tunataka timu yetu iende Afrika Kusini. Timu hii itakwenda!! Mimi nina uhakika wa asilimia mia kwa mia. Lakini kama tuna mashaka ya aah lakini kuna Camerron au ooh kuna Cape verde kwa kweli hatufika popote. Kwenye dhamira ya kweli mende anaweza kuangusha kabati. Kama tutakuwa radhi kuishangalia timu yetu kwa nguvu na ari, Mungu wao na mungu wa manyani, ni mungu wetu sisi nina imani kabisa atatusaidia. Tuachane na uwakala wa kushangilia timu nyingine kama aibu iliyotyupata wakati tulipokuwa tunacheza na msumbiji ambapo watu walipopewa fulana tu wakabadilika!
Inawezekana TFF ambao ndio waratibu wa timu ya Taifa wakawa na mambo lukiki lakini ni wajibu wetu wadau wa soka kukkumbusha chama hiki kuhusu mambo ya msingi kwa ajili ya timu yetu ya taifa badala ya kusubiri tujeruhiwe ndio tuanze aah tulijua tu yatatokea hayo.
Tunakwenda Afrika ya Kusini au hatuendi? Kila mmoja ajiulize nafsi yake na aone nini amekifanya kufanikisha safari hiyo. Tuyaone mafanikio mbele yatu kwanza ndipo tutaweza kuyafikia. Katika hili watu wasibiri kadi za mualiko ili baadae tutoe lawama kwamba hatukualikwa. Timu hii si ya TFF ni Timu ya Taifa hili. Shughuli ipo mlangoni anayesubiri kadi ya mualiko anaisubiri kutoka kwa nani? Siwaagi nawauliza!

COMMENTS