TIMU ya Soka ya Taifa, Taifa Stars inaondoka nchini Juni20,2008 saa moja asubuhi kuelekea mjini Yaounde, Cameroon tayari kwa mechi ya marudi...
TIMU ya Soka ya Taifa, Taifa Stars inaondoka nchini Juni20,2008 saa moja asubuhi kuelekea mjini Yaounde, Cameroon tayari kwa mechi ya marudiano.
Mechi hiyo ni moja ya zile za awali kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika na zile za Kombe la Dunia zitakazofanyika Angola na Afrika Kusini mwaka 2010.
Hata hivyo, kiungo wa Stars, Athumani Iddi ambaye aling’ara kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita katika Uwanja Mpya Dar es Salaam na kutoka sare ya bila kufungana, huenda akakosa safari hiyo kutokana na kuugua malaria.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalabela amesema hata hivyo wamemuomba kocha waende na Iddi kwani hali yake si mbaya sana na endapo atapata nafuu akiwa huko na kukatokea mchezaji mwingine akawa hayuko fiti jambo ambalo hatuombei litokee anaweza kuchezeshwa.
Mwakalebela aliongeza kuwa mbali ya Iddi, mshambuliaji wa Stars Daniel Mrwanda pia ni mgonjwa ingawa imeanza kutengemaa lakini mchezaji Abdi Kassim ndiye atakayebaki kutokana na kuwa majeruhi.
Katika hatua nyingine Mwakalebela alisema TFF imetoa Sh milioni 34 kwa kikosi cha Stars kama sehemu ya Shirikisho hilo kuwapatia motisha wachezaji na kuwapa ari katika mchezo huo wa marudiano wa kesho.
Mwakalebela alisema kwa kiasi hicho kila mchezaji aliyemo kwenye kikosi cha Stars chenye wachezaji 27 atapatiwa Sh milioni moja na zitakazosalia zitagawanywa kwa benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo.
Wakati huohuo mmoja wa wadhamini wa Taifa Stars, Benki ya NMB nayo imetoa Sh milioni 6.2 kwa kikosi cha Stars kutokana na mchezo safi walioonyesha dhidi ya Cameroon.
Ofisa Biashara Mkuu katika benki hiyo Bas Nierop amewapongeza wachezaji wa Stars kwa kuonyesha mchezo wa hali ya juu na wana matumaini kwamba timu hiyo itapata matokeo mazuri katika mchezo huo wa marudiano wa kesho na kusema kuwa fedha hizo zilizotolewa kama asante kwa mchezo huo mzuri zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti za wachezaji hao na viongozi wao kwenye benki hiyo.
NMB Leo iliwaandalia chakula cha mchana kikosi cha Stars katika Hoteli ya Movenpick ambako pia kulifanyika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa iliyofanywa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo, Iddi Kipingu ambaye alikabidhi kwa Nahodha wa Stars , Henry Joseph na Kocha Maximo na Mkuu wa Msafara Samuel Nyala.
Kipingu aliyefanya kazi hiyo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo , George Mkuchika aliyewapongeza wachezaji kwa kuonyesha mchezo mzuri na kuwataka kufanya hivyo maradufu na hakuna cha kuwazuia kutokana na kile walichofanya Jumamosi.
Kikosi cha Taifa Stars pamoja na mashabiki ambao wataambatana na timu hiyo kilitarajiwa kuondoka leo saa moja asubuhi na ndege ya kukodi ya Shirika la Tanzania (ATCL).

Pichani Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Idd Kipingu (kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa mjumbe wa Kamati ya TFF, Samuel Nyala(katikati) wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Benki ya NMB. Wengine pichani toka kushoto ni nahodha wa Timu ya Taifa, Henry Joseph, Afisa Biashara Mkuu wa NMB, Bas Nierop na Kocha Mkuu wa timu hiyo Marcio Maximo. Timu hiyo inaondoka leo kwenda nchini Cameron. Picha hii ni ya Father Kidevu
COMMENTS