TGNP wazungumzia bajeti, Hii kali kuliko upinzani

MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NI BAJETI YA MFUMUKO!! Bajeti kitendawili Hapana shaka Watanzania wengi wali...

MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


NI BAJETI YA MFUMUKO!!

Bajeti kitendawili
Hapana shaka Watanzania wengi walitarajia kwamba Bajeti ya mwaka huu ingekuja na mikakati thabiti ya kukabili changamoto mbalimbali zinazoikabili serikali yetu na watanzania wote kwa ujumla., changamoto hizi ni pamoja na kuzidi kutanuka kwa tabaka la walalahoi na wenye vijisenti miongoni mwa jamii yetu, hasa eneo la kupatiwa huduma muhimu za jamii, na maisha bora, uporaji wa rasilimali adhimu unaofanywa na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa mgongo wa viongozi wa ngazi za juu serikalini, kukithiri kwa ubadhirifu wa fedha na mali ya umma, uchumi tegemezi wenye shinikizo na masharti toka kwa wafadhili, pamoja na kukithiri kwa ufisadi na ukiritimba katika ngazi zote za serikali.

swali ni je, ni kwa vipi Bajeti hii ya 2008/09 itatatua changamoto hizi na kukidhi matarajio ya Watanzania?Jibu ni hapana kama tunavyochanganua katika taarifa yetu ifuatayo:

Mapato na Utegemezi wa misaada ya nje.
Tunaipongeza serikali kwa kupunguza utegemezi wa misaada ya nje toka asilimia 42 mwaka jana hadi 34% katika bajeti ya mwaka huu, hata hivyo kiwango hiki bado ni zaidi ya theluthi moja ya Bajeti yote na kujiuliza punguzo hili la utegemezi lina mantiki gani Ikiwa 62% ya bajeti ya maendeleo hutegemea michango ya wafadhili na wahisani mbalimbali pamoja na changamoto na vipaumbele vinavyo ikabili?
Bajeti hii imeainisha kwamba 62% ya mapato yote yatatokana na na kodi, kiasi kikubwa ikiwa ni kodi itakayolipwa na wake kwa waume wanaofanya kazi katika sekta ya umma, wengi wao wakiwa ni wale wanatozwa kodi zaidi ya isivyostahiki. tunatoa mwito wa kupunguzwa kwa kiasi kikubwa cha kiwango cha kodi katika ngazi zote, mapendekezo yetu yakiwa ni kuanzia 10% kwa mapato ya kati ya shilingi 100,001 hadi 360,000: 20% kwa kati ya 720,000 hadi 3,000,000 : na mstari mpya wa 30-40% kwa wenye kipao cha zaidi ya shilingi 3,000,000
Tunaona kwamba rasilimali mbadala zingeweza kupatikana kama serikali ingeongeza lengo la toka 3% kutoka kwenye mapato yasiyo ya kodi hadi angalau 6% kukidhi madai ya wabunge pamoja na wanachi kwa ujumla.
hata hivyo tunaiona athari kubwa ya utegemezi wa misaada ya nje bado inaendelea kuwa ni shinikizo la wafadhili katika utungaji wa sera pamoja na ushirki wao katika mchakato mzima wa bajeti na jinsi wanavyoshinikiza sera ya uchumi mkubwa wa masoko huria kwa serikali yetu.

Upande wa matumizi.
Mapendekezo ya kutumia shilingi 7.1 trilioni ni kiasi kikubwa sana kwa maoni yetu, Serikali inatakiwa kwa dhati na makini kabisa kupunguza idadi ya wizara na mawaziri na kuhakikisha kwamba kila mtumishi wa umma anafanya kazi kwa ufanisi kuleta tija na kuthaminiwa kazi yake badala ya kuwa ni mzigo kwa mlipa kodi mlalahoi na Taifa kwa ujumla, tunazidi kusisitiza kwamba serikali iongeze rasilimali zaidi mbali ya watumishi walio katika sekta nyeti za huduma, wakiwemo waalimu, wauguzi,wataalamu wa maabara na maafisa kilimo hususan mabwana shamba.
kwamba asilimia 14 ya bajeti yetu imelenga kulipa madeni-huu ni upande mwingine wa utegemezi wa wafadhili na wahisani.
Kuongezeka kwa rasilimali kulikotaarifiwa kutahamishiwa kutoka kwenye sekta kuu ya wizara za serikali (52% katika bajeti) kwenda kwa mikoa (2%) na wilaya (19%) mamlaka za serikali-kimsingi kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii ni hatua nzuri lakini bado hatujaisahau Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa serikali iliyofichua ubadhirifu na ufujaji mkubwa wa fedha za serikali katika Halmashauri zetu, tunaona kwamba ufumbuzi ni kuwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kusimamia Matumizi ya Serikali kama ilivyo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lengo ikiwa ni kutokomeza ufisadi
swali moja la mwisho: 8% ya Bajeti kutengwa kwa "matumizi maalum"-tunajiuliza ni yapi? na kwa nini? Tunakemea vikali na hatutaki tena ufisadi!!
Tunapongeza uamuzi wa serikali kutenga karibu theluthi mbili ya bajeti yote (64%) kwa ajili ya sekta zenye kipaumbele ambazo ni elimu, miuondombinu, maji, afya kilimo na nishati.Hata hivyo tungependa kujua ni kwa jinsi gani mgawanyo wa rasilimali hizi adimu utakavyokwenda kwa kila sekta?, kwamba ni nani atakayefaidika?, ni nani hatahusishwa/husishwa na la muhimu zaidi hatua gani zitachukuliwa kuhakikisha kila sekta inarekebisha kutanuka kwa wigo wa tabaka na upendeleo katika utoaji wa huduma kwa bora kwa jamii?
katika hili mkazo wetu utakuwa ni kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na ufugaji, sekta inayoonyesha kuwa na mchango mkubwa kwenye changamoto ya ajira/kuwezesha wananchi kujikimu kimaisha na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi na pato la Taifa (soma makala yetu katika gazeti la The Citizen la Juni 11, 2008) Tunapigania sana ushirikishwaji wa wananchi unaozingatia na kulenga katika kuwakomboa kiuchumi hasa wakulima wadogowadogo (peasant farmers) ambapo wengi wao wakiwa ni wake kwa waume wamejiajiri/kuajiriwa, badala ya kusisitiza mkakati wa kuwekeza katika sekta kubwa ya kilimo. kama ilivyo sasa. Wakisha kujiundia ushirika wao, rasilimali kubwa itahitajika kuwekezwa katika kufanya tafiti, kutoa mikopo, kupanua wigo wa wataalamu, kutafuta na au kuimarisha masoko kutoa ruzuku na kuweka mfumo wa bei.
Hatua madhubuti zinahitajika ili kuthamini na kurasimisha kazi zisizo na malipo wanazofanya wanawake (free female labour) ambazo kimtazamo hazina malipo (unpaid work) na ambapo wanawake (kwa kiasi kikubwa) hubebeshwa mzigo huo na jamii, kazi hizo ni kama vile kupika, kuchota maji, kutafuta kuni na nishati nyingine za majumbani, kulea watoto, na kutunza wagonjwa na wazee majumbani. Tunaamini utatuzi wa suala hili utawezekana kwa kuwa na teknolojia mbadala na kuwa na mipango na mikakati ya utoaji wa huduma za jamii katika maeneo ya makazi ya watu.
Rasilimali zaidi zinaweza kuelekezwa katika kuboresha usafiri maeneo ya vijijini ili kupunguza ubebaji wa mizigo kichwani na pia kuunganisha na masoko ya mazao ilihali mkakati wa kuwa na viwanda vya Taifa vya kusindika mazao ya kilimo na upatikanaji wa nyenzo kuzalisha pembejeo za kilimo kwa upande mmoja, lakini piakupata malighafi na chakula kwa upande mwingine.

Sekta ya kilimo
Kumekuwepo na shinikizo toka kwa wafadhili na mashirika yaliyo katika sekta binafsi kwa mkakati wa kuwekeza mitaji kwenye mashamba makubwa na kuonekana kuungwa mkono na bajeti hii, (hitaji la mashamba makubwa ya umwagilaji) maoni yetu ni kwamba kwa kufanya hivi ni sawa na kukaribisha dhahama kwani wakulima binafsi wadogowadogo waliojiajiri wana hatari ya kukosa kukaribia ardhi kwa kuwa vibarua kwenye mashamba hayo, mfano tumeuona katika mashamba ya miwa ya Turiani Morogoro, ambapo watoto wao wengi huajiriwa katika miji ya jirani kama watumishi wa baa, wafanyabiashara ya ngono, watumishi wa ndani, wamachinga au mama lishe, hadi wanapotekwa kwenda mijini zaidi, je uu ndio mpango wa serikali kwa mustakabali wa wanachi wa vijijini? Je wataendelea kukubaliana na hali hii wataiga ya wajoli wao yanayojiri Kenya na Afrika Kusini?

Maji safi na maji taka!
nia ya serikali ya kupunguza bajei katika sekta ya maji kwa 40% kutoka 5% mwaka jana hadi 3% mwaka huu imetushtua sana! tunatoa mwito kwa kilio cha watu wote kudai zaidi na si rasiliumali pungufu katika sekta ya maji,. Tunapozungumza, wananchi wengi waishio vijijini wamesahaulika katika kupata huduma ya maji safi na salama na kuimarisha huduma ya maji machafu ukilinganisha na wqakazi wa mijini, kwa mujibu wa rioti ya umaskini na maendeleo ya Binadamu (PHDR 2007) ni moja ya tano tu ya kaya za vijijini zinazoweza kupata huduma ya maji ya bomba na hifadhi ya maji na nyingine 12% wakiwa na huduma ya hifadhi ya maji.
Zaidi ya yote chini ya nusu ya kaya za Watanzania wote (47%) wana hudima ilyoimarika ya maji taka, miaka 47 baada ya Uhuru. (PHDR 2007 UK. 46)! Maji ni miongoni mwa vipaumbele vikuu kwa wasichana/wanawake, si kwa sababu tu kwamba wao ndio wachotaji wakuu wa maji katika kaya, wakiwa wanalazimika kutembea umbali mrefu huku wakibeba maji vichwani mwao bali kwaa sababu ya majukumu yao kedekede katika kaya kama vile kupika, kuuguza, usafi pamoja na kazi nyingine za nyumbani kama matoke ya mgawanyo wa kazi kijinsia.

Masuala Mtambuka
kwa nini Bajeti imekua kimya juu ya masuala ya UKIMWI, wanawake, vijana, walemavu, mazingira na masuala mengine mtambuka ya kipaumbele? masuala haya yaanatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee ili yasije kuzamishwaa kwenye "muongo mpya wa fedha" wa misaada na mikopo ya bajeti (General Budget Support)

Mgawanyo wa kipato
Tunatoa mwito wa mkakati dhabit wa kuhakikisha mgawanyo sawa wa kipato mijini na vijijini. Ripoti ya hivi karibuni ya (PHDR 2007) imeonyesha kwamba 25% ya Watanzania wote walikuwa wanaishi katika hali ya umasikini mwaka 2007, kama ilivyotafitiwa kwenye matumizi ya kila kaya kwa kila mkazi (per capital household consumption)

Ajira na maisha Bora
bajeti hii haina mkakati wa jinsi ya kuwezesha ajira na uhakika wa maisha bora, kwa mujibu wa PHDR uk. 11 hali ya watu wasio na ajira ni mbaya sana maeneo ya mijini kwa kila mmoja lakini hasa kwa wanawake na vijana. 40% ya wanawake katika Jiji la Dar es salaam na 19% katika maeneo mengine ya mijini hawana ajira ukilinganisha na wanaume 23% kwa Dar es salaam na 14% kwa mikoani.
Nyanja nyingine ya ajira ni kiasi kikubwa cha wanawake wanaofanya kazi zisizo na malipo(unpaid work) zaidi kuliko wanaume majumbani, kama ilivyoainishwa katika utafiti wa hivi karibuni wa tathmini ya muda unaotumika kwa kazi hizo (time use study), kazi hizi zinahitaji kuthaminiwa hesabu za fedha na kujumuishwa katika pato la Taifa, ilihali sera/mikakati mahususi ikiundwa na kuendelezwa ili kutoa rasilimali zaidi kupunguza kiasi cha kazi zisizo na malipo kwenye huduma za msingi za matunzo kama vile malezi ya mtoto, kupika, kuchota maji na kukata kuni, kuuza wagonjwa/kutunza wazee na nyinginezo.

mfumo wa maamuzi
hotuba ya bajeti katika sehemu mbalimbali imgusia umuhimu wa sekta binafsi katika kufanikisha kufikia malengo ya bajeti, lakini kwa kiasi kidogo au kama vile hakuna mahali ambapo imeeleza mchango wa asasi za kiraia zikiwemo zile ndogondogo na zile zenye kampeni za kitaifa za ushawishi na utetezi, ukiachilia mbali mchango wa taasisi za kidini katika utoaji wa huduma. Hatua nzuri imechukuliwa katika kuzishirikisha asasi za kiraia kwenye mchakato mzima wa bajeti-matarajio yetu ni kuona muendelezo wa ushiriki katika mchakato wa kuandaa bajeti na ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya bajeti katika ngazi zote, ukihusisha Wananchi-nyenzo pia ya kuhakikisha kwamba hii kweli ni Bajeti ya Wananchi!!!!!

Imesainiwa na

..............................
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji
Mtandao wa Jinsia Tanzania

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4811,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: TGNP wazungumzia bajeti, Hii kali kuliko upinzani
TGNP wazungumzia bajeti, Hii kali kuliko upinzani
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/tgnp-wazungumzia-bajeti-hii-kali-kuliko.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2008/06/tgnp-wazungumzia-bajeti-hii-kali-kuliko.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy