Tamasha la kumi na moja la nchi za Jahazi ambalo litafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 11 hadi 20 Julai ya mwaka huu wa 2008 limepanga kuwapagawisha watu kwa kuleta makundi ya sanaa machachari kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika.

Tamasha la mwaka huu lenye ujumbe unaofahamika kama mikinzano ya utamaduni kwa jinsi ambavyo linachanganya utamaduni kutoka karibu ya kila pembe ya dunia.

Vikundi zaidi ya 30 kutoka Tanzania, Msumbiji, Malawi, Comoro, Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe na kutoka bara la Asia vitakuwepo.

Picha uzionazo ni za makundi kutoka Sunga Umukoshi kutoka Zambia, Afrikali kutoka Tanzania bara na kundi la Nfthe.Ni uhondo kwa kwenda mbele.

aksante Dedah kwa kutoupdate about Ziff

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO