Monday, September 29, 2008

Kesi ya Lundenga yasogezwa mbele

KESI ya madai inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania Hashim Lundenga imesogezwa mbele mpaka Oktoba 22 mwaka huu anaripoti Evance Ng’ingo .
Kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na inaendeshwa na Hakimu Nyigumalila Mwaseba.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mke wa Lundenga, Twigi Lundenga akidai talaka na haki nyingine muhimu kama mke.
Katika kesi hiyo mashahidi watano wanatarajia kutoa ushahidi kuhusiana na suala hilo.
Katika madai yake Twigi, anadai Lundenga amhakikishie malezi kwa watoto wao wawili wanaosoma ambao ni Harris Lundenga na Hamna Lundenga.
Pia mke huyo wa Lundenga ameitaka mahakama iamue alipwe fidia kulingana na uzito katika kesi hiyo iliyopo mahakamani hapo.

2 Comments:

At September 30, 2008 10:13 PM , Blogger Mswahilina said...

Jamani, Hashim Lundenga ni Muislam, anaruhusiwa kuona Wake 4 na kuwa na masuria kadhaa.

 
At October 2, 2008 6:38 AM , Anonymous Anonymous said...

UISLAMU GANI ALIONAO WAKATI KUTWA YUPO NA WANAWAKE WALIOVAA VICHUPI? KWANI UISLAM NI JINA?

VITENDO VYAKE HAVIASHIRII KUWA NI MUISLAM. KWANZA KUITESA FAMILIA YAKE PILI KUENDESHA BIASHARA ZA UCHI TATU KUWA MLEVI ANAPIGA LAGA HADHARANI SASA HUO UISLAMU UKO WAPI?

MWACHE MAMA ADAI TALAKA YAKE

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

Links to this post:

Create a Link

<< Home