Athumani afanyiwa operesheni
Mpiganaji Athumani Hamisi, Mhariri wa Picha wa magazeti ya habariLeo na Habarileo Jumapili ambaye yupo Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata ajali mwezi uliopita maeneo ya Kibiti akiwa njiani Kwenda Kilwa kushiriki futari ya Vodacom amefanyiwa operesheni leo.
Taarifa za kuaminika zinasema kwamba operesheni hiyo imefanikiwa.

Hata hivyo haikuzungumzwa mipango yake ya tiba.Athumani
Watu ambao wameiambia blogu hii wamesema kwamba madaktari hakuwaridhishwa na jinsi mgonjwa huyo alivyocheleweshwa kufikishwa hospitalini kwa matibabu.
Ilichukua siuku kadhaa kwa mgonjwa huyo kufanyiwa taratibu za kupelekwa kwa tiba Afrika Kusini kutokana na matatizo kibao yanayosonga hospitali ya taifa ya Muhimbili kitengo chake cha mifupa cha Moi na Wizara ya Afya ambapo kibali kilichukua 'karne' kupatikana huku uchunguzi wa awali ukichukua miaka 'dahari' kufanyika kutokana na kukosekana kwa mashine muhimu ya CT Scan.
Pamoja na hayo lukwangule inamuombe nafuu ya haraka na mafanikio mema.

2 Comments:
asante sana kwa hizi latest. nakupongeza pia kwa kufuatilia maendeleo ya stori unazotoa.
usisahau kutupa (kunipa???)latest kuhusu ujenzi wa barabara ya kilwa maeneo ya rangi tatu!!!
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
Links to this post:
Create a Link
<< Home