Wednesday, October 1, 2008

Buffalo yatekwa na majambazi Pori la Kasindaga, kagera

BASI la Buffalo ambalo lilikuwa safarini kutoka Bukoba kagera kuja Dar es salaam leo asubuhi lilitekwa na majambazi kwa dakika kadhaa na katika majibizano ya risasi kati ya askari polisi wanaosindikiza gari hilo na majambazi hao raia mmoja wa Madagascar amepoteza uhai wake.

Utekaji nyara huo umefanyika katika pori la Kasindaga mkoani Kagera

Habari kutoka Bukoba zinasema raia huyo wa Madagascar ni Halvilo Karishina (48) na katika tukio hilo abiria wanne walijeruhiwa kwa risasi sehemu mbalimbali za mwili .

Karishina alikufa papo hapo baada ya majambazi waliokuwa katika pori la Kasindaga mkoani Kagera kurusha risasi hewani na kumpata Karishina na abiria wenzake wanne waliokuwa wamekaa sehemu za madirishani.

Kwa mujibu wa Polisi, basi hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T802 AEV likiendeshwa na dereva Suleiman Mfaume, liliondoka Bukoba jana saa 12:00 asubuhi likiwa na abiria 43.

Walioshuhudia walisema basi hilo lilipofika katika pori la Kasindaga majira ya saa 3:15 asubuhi lilisimamishwa na majambazi wapatao wanane ambao walikuwa na bunduki tatu aina ya SMG na mabomu ya kutupa kwa mkono ambayo idadi yake haikujulikana.
Askari aliyekuwa anasindikiza basi hilo alijibizana nao kwa risasi kabla ya kupata msaada wa doria ambao waliweza kuzima jaribio la kuteka basi hilo.
Majambazi hao walikimbilia porini na askari wameongeza nguvu kuyasaka porini.

1 Comments:

At October 1, 2008 11:09 PM , Anonymous Anonymous said...

tatizo la ujambazi maeneo hayo ni la muda mrefu sasa. kinachoonekana ni kama vile serikali imeshakubali yaishe! kama serikali ilikuwa msitari wa mbele kupeleka jeshi letu comoro ili kurudisha amani na usalama huko kwa nini inashindwa kufanya operesheni ya jeshi 'inch by inch' kusafisha eneo hilo? charity begins at home!

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

Links to this post:

Create a Link

<< Home