Suala la wanenguaji wanaovaa nusu uchi linakera mara mbili. kwanza linataka kuonekana kama ni kitu cha kawaida, huu ni ujuha tena ni ujuha ...
Suala la wanenguaji wanaovaa nusu uchi linakera mara mbili. kwanza linataka kuonekana kama ni kitu cha kawaida, huu ni ujuha tena ni ujuha kalulu. Lakini pili ni aina ya hatua zinazochukuliwa katika kulikemea suala hili, bado, linahitaji sauti na kemeo kwa kila mwenye mapenzi mema na nchi hii.
Tatizo inaonekena wajibu wa kufanya hivyo ni wa watu wachache. Katika Bunge lililomaliza kikao chake hivi karibuni suala hili lilijitokeza na Mheshimiwa Naibu wa Habari, Utamduni na Michezo Waziri Joel Bendera alikiri kuwa kunegua nusu uchi sio kitu kizuri kimaadili.
Waziri akaeleza hatua ambazo Wizara yake na Baraza la Sanaa wanazochukua kulikemea suala hili. Sisi tunampongeza Mheshimiwa Bendera kwa hatua yake hiyo lakini kwa kinywa chetu kipana tunamtaka aende hatua moja zaidi.
Hawa Watanzania wameshazoea kukaripiwa na tena kama kukaripiwa kwenyewe ni kwa maneno matupu.
Watanzania, tena bahati mbaya sasa hivi kuna hata raia wa nchi jirani wanaochombeza haya mambo wana kitu kimoja. Kama wakijua kuwa hakuna kitu zaidi ya karipio ukiwakaripia watajifanya kukunyenyekea na kukusikiliza, lakini wakitoka hapo wanaendelea na tabia yao hiyo hiyo.
Wizara na Baraza nendeni hatua moja zaidi ya kukemea, jambo hili sasa ni kama donda ndugu. Vipindi vya televisheni vina nyimbo ambazo mavazi yao hayafai. Hata pale kunapokuwa na mavazi mazuri kuna picha katika fulana ambazo hazifai. Watu wanapiga muziki wakiwa wanafulana zenye alama ya majani.
Bangi! Kweli ina maana hadi mimi Maganga kutoka ushirombo niliekuja na tongo tongo nimeona kuwa fulana zile zina picha ya Bangi ina maana watu wa mji huu hawajaona na kukemea? Haya mambo ya kunengua nusu uchi mwanzoni yalikuwa zaidi katika kumbi za starehe tena zile zinazoitwa Casino, taratibu linaingia katika klabu za usiku na baadaye kuenda mbali zaidi ya hapo.
Sasa hata kwenye kumbi za uchochoroni. Haya makubwa huu ni muziki au biashara ya kuonyesha maungo? Taratibu vituo vyetu vya Televisheni navyo vikaaanza kulichua na kutoa picha katika vipindi vyao vya michezo.
Wizara isikemee tu ipige marufuku.
Leo imetokea kwa wanenguaji kesho itatokea kwenye filamu. Kesho kutwa kwenye magazeti na mtondogoo kwenye intaneti. Hivi ndio tunataka? Mimi Maganga mshamba kutoka huko swekeni hili siliafiki. Kama kuna watu wanaoniunga mkono naomba kutoa hoja. Magangaferuzi@gmail.com.
unaweza kukipata kipande hiki kwa undani wake katika gazeti la The Football, hapa nimeazima tu si unajua mambo ya entertainment!

COMMENTS