Hii ni habari ambayo imeandikwa na Habarileo Mafisadi wazidi kulizwa .Watatu zaidi wafikishwa kortini .walioshitakiwa walichota Sh bilioni ...
Hii ni habari ambayo imeandikwa na Habarileo
Mafisadi wazidi kulizwa
.Watatu zaidi wafikishwa kortini
.walioshitakiwa walichota Sh bilioni 44
.Jeetu na wenzake waendelea kusota rumande
.Masharti ya dhamana yawa mwiba
Na Shadrack Sagati na Mariam Mogella
WAMILIKI wengine wa kampuni tano ambazo zilihusika kuchota mabilioni ya fedha Benki Kuu (BoT) jana walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kughushi nyaraka na kuiba.
Washitakiwa hao ni Falijala Hussein, Rajab Maranda ambao ni wamiliki wa kampuni za Mbale Farm, Lashashi Tanzania Ltd, Money Planners Consultant na Kaloloma & Brothers. Mwingine ni mkazi wa Arusha, Japhet Lema anayemiliki kampuni ya Njake Enterprises ya Arusha ambayo nayo ilijichotea mabilioni kutoka katika akaunti hiyo ya EPA.
Kufikishwa kwa washitakiwa kunafanya idadi ya washitakiwa ambao tayari wamefikishwa mahakamani kuwa 13 baada ya washitakiwa wengine 10 kufikishwa mahakamani juzi.
Idadi ya kampuni wanazowakilisha ni 11 ambazo idadi ya fedha walichota ni Sh bilioni 42 kati ya Sh bilioni 133 zilizochotwa na kampuni 22 kutoka katika akaunti ya EPA iliyoko BoT mwaka 2005.
Kesi ya kwanza inayowakabili Falijala Hussein na Rajab Maranda wanadaiwa kughushi na kuiba Sh bilioni 3.9 mali za BoT kwa kutumia kampuni ya Mbale Farm wakisingizia kupewa deni na kampuni ya Lakshimi Textile Mills Ltd ya Japan.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Warialwande Lema. Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na watasomewa maelezo ya awali Novemba 14 mwezi huu.
Katika kesi hiyo washitakiwa wanatetewa na Wakili Mabere Marando. Dhamana yao iko wazi lakini wanatakiwa waweke nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba, wawe na wadhamini wawili, kuwasilisha hati za kusafiria ofisi ya mwendesha mashitaka na kutotoka nje ya Dar es Salaam. Katika kesi nyingine Maranda alipandishwa kizimbani peke yake mbele ya hakimu Hezron Mwakenja akidaiwa kuiba Sh milioni 207.3 kutoka BoT. Ilidaiwa alifanya wizi huo baada ya kughushi nyaraka akionyesha kuwa kampuni yake ya Lashashi Tanzania Ltd ilikabidhiwa deni na kampuni ya General Marketing ya India.
Hakimu Mkazi Hezron Mwakenja ndiye anayesikiliza kesi hiyo ambayo pia upelelezi wake umekamilika. Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo moja ya sharti anatakiwa aweke Sh milioni 103.6 ili aweze kupata dhamana.
Wakili wake Hashimu Rungwe alichelewa kutetea mteja wake awasilishe hati ya mali inayolingana na thamani ya fedha hizo, hali iliyomfanya hakimu asisitize kuwa mahakama hairudi nyuma katika kutoa masharti kwani tayari alishaandika masharti hayo.
Baadaye Maranda alipandishwa tena kizimbani pamoja na Falijala wote wakituhumiwa kughushi nyaraka katika ofisi ya msajili wa makampuni (Brela) na kisha kuiba Sh bilioni 2.3 kwa kutumia kampuni ya Money Planners Consultant.
Katika kesi hiyo washitakiwa hao walipandishwa mbele ya hakimu Mkazi Anyimilile Mwaseba na wote wakituhumiwa kudanganya kuwa wamepewa deni hilo na kampuni ya B Glancel Ltd ya Ujerumani.
Hakimu Mwaseba katika masharti ya dhamana pia aliwataka washitakiwa walipe nusu ya fedha zinazodaiwa kuiba au wawasilishe nyaraka ambazo zimeshafanyiwa uhakiki na mamlaka husika kuthibitisha kama zina thamani hiyo. Sharti hilo lilikuwa gumu kutimizwa kwa siku ya jana na walirudi rumande hadi Jumatatu kesi hiyo itakapoenda kwa ajili ya kufanya mchakato wa upatikanaji wa dhamana.
Maranda na Falijala baadaye tena walifikishwa mbele ya hakimu mkazi Hadija Msongo wakichota Sh bilioni 1.8 kutoka BoT. Ilidaiwa walifanikisha wizi huo kwa kutumia kampuni ya Kiloloma & Brothers baada ya kuwasilisha hati za kughushi kutoka Brela wakidai kuwa wamepewa walipwe fedha hizo na kampuni ya D.C Export Ltd ya Mumbai, India.
Mawakili wa washitakiwa hao Joseph Tadayo na Mbaya kamala licha ya kujitahidi wapatiwe dhamana, lakini bado mambo yaliendelea kuwa magumu kutokana na masharti yake kufanana na yale kwenye kesi zingine.
Hakimu Hadija alisisitiza kuwa washitakiwa wanatakiwa wawasilishe hati ambazo zimehakikiwa na mamlaka husika kuonyesha kuwa zina thamani ya nusu ya fedha zinazodaiwa kuibwa.
Mtuhumiwa mwingine aliyepandishwa jana ni Japhet Lema ambaye yeye alijichotea Sh bilioni 2.6 kwa kutumia kampuni yake ya Njake Enterprises ya mjini Arusha. Alijipatia kiasi hicho baada ya kudanganya kwa nyaraka za kughushi kuwa kampuni yake imepewa deni hilo na kampuni ya C. Itoh ya Japan.
Naye alipelekwa rumande hadi Novemba 17 pale kesi yake itakapoenda kwa ajili ya kusomewa masharti ya awali na kuendelea na mchakato wa kupatiwa dhamana ambayo ina masharti kama washitakiwa wengine katika kesi hiyo.
Katika kesi zingine ambazo zilifikishwa mahakamani hapo jana, masharti ya dhamana yameendelea kuwa machungu kwa washitakiwa akiwamo kinara Jeetu Patel na wenzake ambaye anaendelea kusota rumande.
Mahakimu kadhaa ambako kesi ya Jeetu na wenzake zinasikilizwa wameonyesha kuwa wakali kwa kusisitiza hati wanazowasilisha mahakamani hapo ziwe zimefanyiwa tathmini na mkaguzi wa serikali.
Lengo la mahakimu hao Eva Nkya na Neema Chusi ni kutaka kujiridhisha katika kuthibitisha kuwa thamani ya mali hizo inalingana na nusu ya fedha wanazotakiwa waweke mahakamani ili wapate dhamana.
Katika kesi iliyoko mbele ya hakimu Nkya, Jeetu anashitakiwa Devendra Vinodbhai Patel na Amit Nandy ambako wanadaiwa kuiba Sh bilioni 3.3 kwa kutumia kampuni Navy Cut Tobacco Ltd. Kesi hiyo itaenda tena leo kutolewa maamuzi ya dhamana.
Mbele ya kesi iliyoko mbel eya Hakimu Chusi Jeetu anashitakiwa kwa pamoja na Devendra, Nandy na Ketan Chohan na wote wanadaiwa kuiba Sh bilioni 3.9 kwa kutumia kampuni yao ya Bina Resorts Ltd.
Kinara huyo pia anadaiwa kutumia kampuni ya Bencon kwa kuchota Sh 2.6 na pia alitumia kampuni ya Malta Mining na akaiba Sh bilioni 4.9.
Washitakiwa waliotumia kampuni ya Changanyikeni ambao ni Bahati Mahenge, Davis Kamungu, Godfrey Mosha, Manase Mwakale na Edina Mwakale ambao wanatuhumiwa kuiba Sh bilioni 2 nao hawakutimiza masharti ya dhamana. Mshitakiwa mwingine ambaye alifikishwa juzi ni Johnson Lukaza ambaye alichota Sh bilioni 6.3 kwa kutumia kampuni yake ya Kernel.

COMMENTS