SERIKALI imeshawalipa wastaafu 31,444 wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa tamko kuwa haitatoa malipo mengine nje ya hati ya ma...

SERIKALI imeshawalipa wastaafu 31,444 wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa tamko kuwa haitatoa malipo mengine nje ya hati ya makubaliano kati yake na wastaafu hao.
Kwa mujibu wa hati ya makubaliano ya Septemba mwaka 2005 iliyofikishwa Mahakama Kuu na kupewa hadhi ya hukumu na kuhitimisha madai ya wastaafu, inabainisha kuwa serikali itawalipa wote waliofanya kazi katika jumuiya kabla ya Juni 30, 1977 na baada ya hapo serikali haitadaiwa tena.
Katika hati hiyo, serikali ilikubali kuwalipa wadai 31,831 Sh bilioni 117 kwa misingi ya stahili ya kila mmoja kulingana na taarifa ya kila mtu kwenye jalada na nyaraka nyingine zilizothibitishwa na serikali ilikubali kuchukua gharama za mawakili ili wastaafu hao wasidaiwe chochote.
Akitoa tamko la serikali kuhusu madai ya wastaafu hao kama alivyoahidi Rais Jakaya Kikwete wakati wa hotuba yake ya mwezi uliopita, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema Wizara yake itaendelea kupokea maombi kutoka kwa wastaafu halali na kuyashughulikia ipasavyo.
“Kwa mfano, wastaafu 10 kati ya 21 waliodhihirika kuwa wanastahili kulipwa, hundi zao ziko tayari na wanaweza kuzichukua wakati wowote Hazina,” alisema Mkulo.
Katika maelezo ya serikali, Mkulo alisema hadi Septemba mwaka huu, serikali imetumia Sh bilioni 114.2 kwa ajili ya kuwalipa wastaafu hao 31,444.
“Waliopunjwa mafao yao katika ukokotoaji, ikithibitika watalipwa. Ili kuepuka udanganyifu, tunashughulikia wadai mmoja mmoja na sio makundi,” alisema.
Alisema katika kutekeleza jukumu la kuwalipa wastaafu hao yalijitokeza matatizo mengi, ikiwamo upungufu wa nyaraka ambao umechelewesha utaratibu huo kukamilika mapema na madai yasiyo na ushahidi au kuwapo ushahidi wa maneno.
Pia madai ya wafanyakazi wasiostahili kulipwa kama walioajiriwa baada ya Juni 30, 1977, waliostaafu kabla jumuiya kuvunjika, waliokuwa vibarua wa Cargo, wafanyakazi wa iliyokuwa Bora Shoes, waliokuwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia cha Afrika Mashariki na wafanyakazi wa iliyokuwa UDA/DMT.
Wengine ni wafanyakazi wa Taasisi zilizoondolewa kwenye Jumuiya kabla ya kuvunjika kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Sokoine na Idara ya Kodi ya Mapato.
Tatizo jingine ni kuibuka makundi kutaka kulipwa mafao, wakidai yapo malipo ya Serikali ya Awamu ya Nne na kuongeza, “tatizo hili linatokana na uelewa wao kuwa fedha walizolipwa zilikuwa kwa ajili ya ahadi ya serikali ya awamu ya tatu na wakiamini yapo mabilioni ya fedha kutoka Serikali ya Uingereza.”
Harakati za kudai mafao kwa wastaafu hao zilianza mwaka 1999 wakati serikali ilipoanza kulipa mafao kwa kujumuisha riba ya asilimia saba, ambapo wastaafu walilalamika walipunjwa na mwaka 2003 walifungua kesi Mahakama Kuu kudai walipwe mafao waliostahili kulipwa.
Mwaka 2004, serikali iliteua kamati ya mwafaka iliyowahusisha serikali na wastaafu kuangalia upya madai hayo na baadaye yalizaa hati ya makubaliano iliyofikishwa Mahakama Kuu na kupewa hadhi ya hukumu iliyotolewa na Jaji Oriyo.
Hata hivyo, wastaafu hao walijitokeza tena wakidai mafao yao na kwenda kukaa Ikulu na siku chache zilizopita walifunga barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi eneo la Selander, huku wengine wakivua nguo.

COMMENTS