Saturday, August 30, 2008

Nachomoka Dar kuingia vijijini

Wapenzi wa lukwangule nataka kusema kwamba kesho Mungu akinijalia nachomoka mjini na kwenda safari. Sina hakika na mzunguko wangu lakini Mungu akipenda tutakuwa tunaonana jioni nikitoka katika kusaka nyoka.

This is the way forward says Rais Kikwete na Bush



Rais George Bush wa Marekani akimwonyesha Rais Jakaya Kikwete madhari ya ikulu ya Marekani,White House, wakati Rais Kikwete alipomtembelea Rais Bush katika ikulu ya Marekani ya Washington D.C. kabla ya kufanya mazungumzo.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Bush.Picha na Freddy Maro.

Friday, August 29, 2008

Hizi dawa za kichocho na minyoo vipi vile...?






ZAIDI ya wanafunzi 363 wa shule za msingi mkoani Rukwa na Morogoro leo walikimbizwa katika hospitali mbalimbali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kupewa dawa za kinga ya kichocho na minyoo katika mikoa hiyo.


Kutokana na hali hiyo utoaji wa chanjo katika mikoa hiyo ulilazimika kusimamishwa kwa muda.

Tafarani kubwa ilizuka baada ya watoto hao kupoteza fahamu mara tu baada ya kunywa dawa hizo.


Habari kutoka Rukwa zinasema kuwa utoaji chanjo hiyo ulisimamishwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kutoa povu mdomoni huku baadhi yao wakitapika na kupoteza fahamu.


Kutokana na hali hiyo wazazi wa wanafunzi hao walivamia shule hizo katika Manispaa ya Sumbawanga hususan shule za msingi Chemchem, Katandala, Mwenge, Malangali na Jangwani wakitishia kuwapiga walimu kwa kile walichodai kuwa wamesababisha hali hiyo.


Hali ilizidi kuwa mbaya wakati wazazi wa wanafunzi hao walipofika hatika hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na kukataliwa kuingia wodini wakiwa na lengo la kuwaona watoto wao waliokuwa wamefikishwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Wazazi wa watoto hao waliwapiga mawe madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo huku wakilia kitendo kilichosababisha polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wapelekwe hospitalini kuwatawanya wananchi zaidi ya 600 kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mabomu hayo yalipigwa kwa zaidi ya saa tatu na kuweza kuwatawanya wananchi hao waliokaa umbali wa mita 500 ingawa baadhi yao wakiendelea kulia wakidhani watoto wao wamekufa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Saduni Kabuma alisema wanafunzi wote waliofikishwa katika hospitali hiyo wamepatiwa matibabu na wengi wao wameruhusiwa.
Alisema hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyefariki dunia kwa tukio hilo au aliyekuwa mahututi baada ya kumeza dawa hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel Ole Njoolay aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kutokuwa na uamuzi wa kukurupuka katika kukabiliana na matatizo badala yake wawe wasikivu kwani serikali kamwe haiwezi ikawapa sumu raia wake.
Njoolay amewataka wazazi mkoani Rukwa kuwapeleka watoto wao kesho kuendelea na chanjo ya surua na polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwani ni salama na wala hakuna madhara yatakayotokea.
Nako Morogoro anaripoti kuwa chanjo ya kichocho na minyoo imekwama kutolewa mkoani hapa baada ya kuzuka vurugu katika shule mbili ulipoenea uvumi wa kufariki dunia kwa mwanafunzi baada ya kupewa chanjo hiyo.
Katika utoaji wa chanjo hiyo wanafunzi 63 walizirai na kufikishwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Vurugu zilizozuka zilisababisha polisi kutumia mabomu ya kutokwa na machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika maeneo ambako chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa huku wakiwarushia mawe wahudumu na walimu kuwalazimisha wawaachie watoto wao warudi majumbani.
Polisi inawashikilia watu 25 wakiwamo wanawake wawili kutokana na vurugu hizo.
Vurugu hizo zilianza jana saa tano na saa sita mchana katika shule za msingi Mafisa A na B, katika Kata ya Mwembesongo hali iliyowalazimu walimu kupiga simu Kituo cha Polisi kuomba msaada wa ulinzi.
Katika vurugu hizo polisi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Clemence Bazo, alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe chini ya jicho lake moja na kupelekwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa matibabu ambako alishonwa nyuzi sita.
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Thobias Andengenye alisema jeshi hilo lilikuwa halijapokea taarifa ya mtoto aliyekufa kufuatia chanjo hiyo.
Wakati huohuo, Mganga Mkuu wa mkoani Morogoro, Frida Mokiti amesimamisha utoaji wa chanjo hiyo ya kichocho na minyoo hadi itakapotangazwa tena kwa mkoa huu.

Picha hizi za matukio mbalimbali mkoani Morogoro ni kwa hisani ya John Nditi wa Morogoro na habari ni kutoka kwa Gurian Adolf na John nditi wote watendaji wa habari Leo

HOTUBA YA WAZIRI MKUU YA KUFUNGA BUNGE



HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), WAZIRI MKUU, WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA KUMI NA MBILI WA BUNGE – DODOMA TAREHE 29 AGOSTI 2008
UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, leo ni takriban siku ya 81 tangu Bunge lako Tukufu lilipoanza Mkutano wa Kumi na Mbili, tarehe 10 Juni 2008 hapa Dodoma. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuongoza, kutusimamia, kutulinda na kutuweka salama hadi siku ya leo, tarehe 29 Agosti 2008 tunapohitimisha Mkutano huu wa Kumi na Mbili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri muda tuliokaa hapa Dodoma ni kipindi kirefu kwa maisha ya binadamu. Mambo mengi yametokea. Msomi wa siku nyingi Bwana Terry Flanagan aliandika: “A lot of Water has passed under the Bridge”. Nakubaliana naye kwamba ni kweli maji mengi yamepita chini ya daraja. Yapo matukio ambayo yametokea katika kipindi hicho yakiwepo ya furaha na mengine ya huzuni. Nitumie nafasi hii ya mwanzo kabisa kukupongeza wewe Mheshimiwa Spika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kwa kipindi hiki hadi mwaka 2009 utakapofanyika Mkutano wa 55 wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Mjini Arusha, Tanzania. Kuchaguliwa kwako, ni heshima kwako binafsi, kwa Bunge letu na kwa Taifa kwa ujumla, na ni uthibitisho wa Tanzania kukubalika Kimataifa. Nakupongeza Sana.

3. ` `Niungane nanyi tena Waheshimiwa Wabunge, pamoja na Watanzania wote kutoa pole kwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari wakati akisafiri kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Vilevile, nampa pole Mheshimiwa Severina Mwijage, Mbunge wa Viti Maalum – CUF, kwa kufiwa na binti yake, mjukuu wake pamoja na dereva wake katika ajali ya gari mwezi Julai 2008. Nitumie fursa hii pia kutoa salaam za pole kwa Wabunge wenzetu na Watanzania wote waliopata majeraha, kwa kupoteza ndugu, jamaa, marafiki na mali kutokana na ajali, maradhi na sababu nyingine mbalimbali. Ni dhahiri kuwa, kwa wenzetu waliopoteza maisha tuliwahitaji sana katika maisha yetu na ujenzi wa Taifa kwa ujumla, lakini Mwenyezi Mungu amekubali watutangulie mbele ya haki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke Roho za marehemu wote mahala pema peponi. Amina.

4. Mheshimiwa Spika, kwa huzuni kubwa na kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kuungana na wananchi na jirani zetu wa Zambia katika wakati huu mgumu wa kumpoteza Rais wao, Hayati Dkt. Levy Patrick Mwanawasa ambaye alifariki dunia tarehe 19 Agosti 2008, mjini Paris, Ufaransa. Marehemu atakumbukwa sana kwa uhodari wake katika kusimamia uchumi, kujenga Demokrasia na Utawala Bora katika nchi yake. Kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika, atakumbukwa kwa juhudi zake zisizo na kikomo katika kujaribu kumaliza migogoro ya kisiasa katika Bara la Afrika. Nawapa Pole sana Jirani na Ndugu zetu wa Zambia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina.

5. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina Miswada ifuatayo:

i) Muswada wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma wa Mwaka 2008
[The Public Audit Bill, 2008];

ii) Muswada wa Sheria Mpya ya Utawala wa Bunge wa Mwaka 2008 [The National Assembly (Administration) Bill, 2008].

iii) Muswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa Mwaka 2008 [Appropriation Bill, 2008]; na

iv) Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2008 [Finance Bill, 2008].

6. Vilevile, Miswada ifuatayo ilisomwa kwa mara ya kwanza:
(i) Muswada wa Sheria ya Wanyamapori wa Mwaka 2008 [The Wildlife Bill, 2008] ;

(ii) Muswada wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama wa Mwaka 2008 [The Animal Welfare Bill, 2008] ;

(iii) Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Bodi ya Usajili wa Makandarasi wa Mwaka 2008 [The Contractors Registration (Amendment) Bill, 2008]; na

(iv) Muswada wa Vyama vya Siasa (Marekebisho) wa Mwaka 2008 [The political Parties (amendment) Bill, 2008];
Katika Mkutano huu Bunge lako Tukufu pia lilipitisha Azimio la Bunge la Kuridhia Kufuta na Kusamehe Madai ya Kodi pamoja na Riba na Hasara itokanayo na Upotevu wa Fedha na Vifaa vya Serikali na Maduhuli yaliyoshindikana kukusanywa kwa kipindi kinachoanzia Mwaka wa Fedha 1990/1991 hadi tarehe 30 Juni, 2007.

Nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kazi nzuri mliyoifanya katika kujadili na hatimaye kupitisha Miswada na Maazimio yote yaliyowasilishwa mbele ya Bunge lako Tukufu katika kipindi cha Mkutano huu. Vilevile, nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kupokea Taarifa ya Kamati ya kuishauri Serikali kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini, Taarifa ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge linalohusu Uuzwaji wa Nyumba za Serikali na Taarifa ya Serikali kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC niliyoiwasilisha kama Bunge lako Tukufu lilivyoelekeza.

7. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata nafasi ya kuuliza Maswali 500 ya Msingi pamoja na mengine mengi ya nyongeza. Nitumie fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge kwa Maswali yao mazuri ambayo yameisaidia Serikali kutoa ufafanuzi wa Shughuli za Maendeleo kwa ajili ya Taifa letu. Vilevile, nawapongeza Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao walijibu kwa ufasaha Maswali yote yaliyoulizwa na Waheshimiwa Wabunge. Pamoja na mambo mengine, changamoto iliyoko mbele yetu ni kuwahimiza Wataalam wetu kuendelea kupata majibu mafupi na sahihi kwa wakati, na yenye kulenga katika kutumia muda wa Maswali kikamilifu na kwa ufanisi zaidi. Kwa kufanya hivyo, Bunge letu Tukufu litaweza kujibu Maswali mengi zaidi na hivyo kuwapatia Wananchi picha halisi kuhusu maendeleo ya Nchi yetu na kutatua kero zao kwa kasi zaidi.

8. Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu, pia Bunge lako Tukufu lilipokea Kauli Nne (4) za Serikali zilizotoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kutoka Serikalini. Nawapongeza Waheshimiwa Mawaziri waliotoa Kauli za Serikali kwa ufafanuzi mzuri na Waheshimiwa Wabunge waliowasilisha Hoja Binafsi ili kupata ufafanuzi na ufahamu zaidi wa masuala mbalimbali.


MASWALI KWA WAZIRI MKUU

9. Mheshimiwa Spika, kipindi cha kila Alhamisi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu ambacho kilianza mwezi Aprili 2008, katika Mkutano wa Kumi na Moja kimeleta msisimko wa kipekee. Kwa upande mmoja, Wabunge wamepata fursa nyingine ya kuuliza Maswali ya Kisera na kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa Waziri Mkuu. Kwa upande mwingine, Serikali imetumia Maswali ya kipindi hicho kujua hisia za Wabunge ambao ndio Wawakilishi wa Wananchi. Tumeweza kujua ni maeneo gani makubwa ambayo Serikali inahitaji kuweka mkazo katika utendaji kazi wake wa kila siku.

10. Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwa kipindi hicho, Waheshimiwa Wabunge wameuliza jumla ya Maswali 85 ya Msingi na Maswali 31 ya Nyongeza. Ili kubaini maeneo yenye kuhitaji mkazo, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya tathmini na uchambuzi wa Maswali yote yaliyoulizwa na kuyaweka kwenye makundi matatu ya MKUKUTA. Makundi hayo ni Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato, Huduma za Jamii, na Utawala Bora. Katika uchambuzi huo, imeonekana kuwa kati ya maswali yote yaliyoulizwa, Maswali 40 yanahusu Ukuaji Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato, Maswali 17 Huduma za Jamii na Maswali 53 Utawala Bora. Vilevile, kuna Maswali 6 yaliyoulizwa na Waheshimiwa Wabunge ambayo hayaangukii moja kwa moja katika makundi haya matatu ya MKUKUTA. Maswali haya ni yale yanayohusu masuala ya Kimataifa ambayo pia ni muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Takwimu hizi zinaonyesha kwamba eneo la Utawala Bora lina maswali mengi kulinganisha na makundi mengine. Kwetu sisi Serikalini, hii ni changamoto kubwa na ni ujumbe kwamba kunahitajika jitihada za ziada kuimarisha Taasisi zetu za Utawala Bora. Sote tunatambua umuhimu wa Utawala Bora katika kuweka mazingira mazuri ya Ukuaji Uchumi na Ufanisi katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.

11. Ni ukweli usiopingika kwamba, Taasisi zenye misingi mizuri ya Utawala Bora, zinazojenga mazingira ya Utawala Bora unaozingatia Sheria, Taasisi zinazohakikisha kwamba mali za watu zinakuwa na usalama, Taasisi zinazodhibiti Rushwa ili isiathiri utendaji kazi ni misingi muhimu ya Ukuaji Uchumi. Hivyo, nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge na Wananchi wote kwamba, Serikali imechukua wingi wa Maswali katika eneo la Utawala Bora kama ujumbe wa eneo linalohitaji kuwekewa mkazo zaidi katika ngazi zote za utendaji wa Serikali. Vilevile, Serikali itaendelea kuweka mkazo katika Kukuza Uchumi ambao ndio msingi wa kuongeza Mapato yatakayoiwezesha kutoa huduma bora za jamii na kuimarisha Taasisi za Utawala Bora. Nichukue tena fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa Maswali yenu. Changamoto iliyo mbele yetu ni kutumia fursa hii ya Maswali ya Papo kwa Papo kujikita katika Masuala ya Sera zaidi kama Kanuni zetu zinavyoelekeza. Kwa kufanya hivyo tutaweza kuboresha zaidi muda huu adimu ambao tumejipangia kukubaliana.

12. Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu lilipata bahati ya kutembelewa na Wananchi wengi kutoka sehemu mbalimbali Nchini, ikiwa ni pamoja na Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Waheshimiwa Madiwani na kadhalika. Vilevile, katika Mkutano huu, wapo Wageni kutoka nje ya Nchi ambao walitembelea Bunge hili wakiwemo Wageni kutoka Mabunge ya Denmark, Kenya, Msumbiji, Namibia na kutoka Jimbo la Gauteng – Afrika Kusini. Walikuwepo pia Wageni kutoka Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola-CPA, Uingereza, akiwemo Dkt. William Shija, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Tulitembelewa na kuhutubiwa hapa Bungeni na Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York na mwisho Rais wa Jamhuri ya Visiwa vya Comoro, Mheshimiwa Ahmed Mohamed Sambi, ambaye pia alihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tunawashukuru Wageni wote waliotutembelea, kuongea nasi na hata wale waliokuja kujionea jinsi tunavyoendesha shughuli zetu hapa Bungeni.

13. Mheshimiwa Spika, kutembelewa na Wageni hawa ni ishara tosha kwamba Bunge lako Tukufu, lina uhusiano mzuri na Wananchi pamoja na Mabunge mengine Duniani. Nina imani Wageni wetu wamejifunza mengi mazuri ya Bunge hili, nasi tumepata uzoefu wa yale wanayofanya katika Mabunge yao kule walikotoka.

14. Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati kabisa na kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwanza, kwa uamuzi wake wa kuja kulihutubia Bunge na Pili, kwa Hotuba yake nzuri sana aliyoitoa ndani ya Bunge hili tarehe 21 Agosti 2008. Kama alivyosema mwenyewe Mheshimiwa Rais na kama ilivyodhihirishwa na Hotuba yenyewe, Watanzania kwa ujumla wamepata Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Nne kwa kutambua na kuelewa Serikali yao imetoka wapi, iko wapi na inaelekea wapi.

15. Wengi wetu tunaamini kwamba siku zote Sala ni Chakula cha Roho. Vivyo hivyo, sichelei kusema kwamba Hotuba ya Mheshimiwa Rais imekuwa Chakula cha Amani, Utulivu na Mshikamano uliodumu katika Nchi yetu kwa muda mrefu. Hotuba hii hakika imekuwa chakula cha kutupa nguvu ya kusukuma kwa Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya utekelezaji wa Mipango mbalimbali ya Maendeleo ya Taifa ikiwemo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2005, MKUKUTA, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, na Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa.

16. Mheshimiwa Spika, vilevile tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake wa kuelekeza kwenye Sekta ya Kilimo fedha za EPA. Uamuzi wake ni wa Kijasiri, Kishujaa na unastahili kupongezwa na Watanzania wote. Mheshimiwa Rais Hongera Sana kwa uamuzi huu wa Kihistoria. Wakati tukifurahia uamuzi huu, Viongozi na Wananchi wote tunao wajibu mzito na changamoto kubwa ya kuhakikisha kwamba Wakopaji wa fedha hizo zitakazoelekezwa katika shughuli za Kilimo watazielekeza na kuzitumia kwa kuwekeza, kuinua na kuendeleza Sekta ya Kilimo. Taratibu za kuziingiza fedha hizo katika Bajeti ya Mwaka 2008/2009 zitazingatiwaa kama Sheria na Kanuni za Matumizi ya Fedha zinavyotaka.

17. Mheshimiwa Spika, Mkutano huu ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwasilisha, kujadili na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali pamoja na Makadirio ya Fedha kwa Wizara, Mikoa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka 2008/2009. Waheshimiwa Wabunge wote mtakubaliana nami kwamba, Hoja zote zilijadiliwa na Waheshimiwa Wabunge kwa umahiri mkubwa. Vilevile, naamini mtaungana na mimi kukubali kwamba mjadala ulikuwa wenye msisimko na wakati mwingine wenye hisia kali. Mkutano huu wa Kumi na Mbili utakumbukwa sana hasa kwa mjadala mkali wakati wa kujadili Wizara ya Katiba na Sheria; na Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano). Mimi ninaamini kabisa kwamba, Waheshimiwa Wabunge waliochangia kwa hisia zao walikuwa na hoja ambazo zililenga katika kujenga Nchi yetu. Mwanafalsafa Karl Max alisema kwamba Jamii isiyokuwa na msukumo wa mawazo haiwezi kuendelea. Kwa hiyo, mambo tunayojadiliana kwa mtizamo tofauti ni dalili njema ya kujaribu kutafuta mwelekeo wa kufikia mwafaka mzuri wa Hoja. Na pengine tukubali kwamba kusikiliza mawazo ya wengine hata kama ni tofauti na unavyowaza ni ustaarabu wa kutosha na kuna wakati tutafika na kukubaliana kwa kiasi kikubwa. Kwa misingi hiyo, ninaamini kabisa kwamba majadiliano haya yanayoonekana yenye hisia kali yatakuwa ni kichocheo na changamoto kwetu kurekebisha yale ambayo yataonekana ni busara kuyarekebisha kwa maslahi ya Taifa letu.

18. Napenda nitumie nafasi hii tena kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia Mijadala kwa Maandishi na kwa Kauli wakati wa Kupitisha Makadirio ya Mipango na Matumizi ya Fedha ya Wizara mbalimbali. Michango yenu ni chachu katika kuongeza kasi ya kuwatafutia Wananchi wetu Maisha Bora pamoja na kuipa Serikali changamoto ya kuboresha utendaji na Mipango yake. Ni matumaini yangu kwamba tutaendelea kuhimiza yale yote yaliyopendekezwa na ushauri uliotolewa kutimiza malengo tuliyojiwekea. Tuendelee na juhudi hizo, kwani zinatoa mchango mkubwa katika kusukuma Maendeleo ya Wananchi wetu na Taifa kwa jumla.

19. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Mwaka huu wa Fedha 2008/2009, imelenga kukusanya Mapato ya ndani Shilingi Trilioni 4.7. Hili ni ongezeko la asilimia 31 ikilinganishwa na Makusanyo ya Mapato katika mwaka 2007/2008. Ili kufikia lengo hili, hatua kadhaa zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na:
(i) Kupanua wigo wa Mapato ya Serikali kwa kusajili Walipa Kodi wapya na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika Sekta zote za Uchumi;

(ii) Kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa Ushuru na Kodi katika Forodha pamoja na kuziba mianya ya ukwepaji kodi;

(iii) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kwa nia ya kuongeza uwajibikaji miongoni mwa Walipa Kodi na Watoza Kodi kadhalika;

(iv) Kurekebisha Sera na Sheria zinazotoa misamaha ya kodi kwa Sekta ya Madini. Serikali inatafakari na kuainisha marekebisho ya Sheria mbalimbali ambayo yatahitajika yafanywe ili kupunguza misamaha ya kodi na kuokoa mapato ya Serikali; na

(v) Kuendelea kutoa Elimu ya Biashara na namna ya ukokotoaji kodi kwa Wafanyabiashara.

20. Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kueleza matumaini yetu na ya Wananchi kwa ujumla kwamba wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na katika ngazi zote katika ukusanyaji wa Mapato, watatimiza wajibu wao ili fedha zinazokusudiwa zikusanywe. Hii itatuwezesha kutekeleza kikamilifu mipango mbalimbali iliyopangwa katika Bajeti hii.

21. Kuhusu matumizi, napenda kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma. Aidha, tutaimarisha uwezo wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa kazi mbalimbali za Serikali zilizopangwa ikiwemo Miradi ya Maendeleo ili kuhakikisha kuwepo kwa nidhamu katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali. Napenda kuzipongeza Kamati zote za Kudumu za Bunge lako Tukufu zinazohusika na masuala ya matumizi ya mali na fedha za Umma. Tunathamini mchango wao na ushauri wao kila mara umekuwa changamoto kwetu ya kuongeza ufanisi zaidi.

Bei ya Mafuta

22. Mheshimiwa Spika, kasi ya upandaji wa Bei ya Mafuta katika Soko la Dunia inaendelea kuyumbisha uchumi wa Nchi zote Duniani na hasa zile masikini sana kama yetu. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba, upo uwezekano mkubwa kuwa Bei hizi za mafuta zikaendelea kupanda tena katika siku za usoni. Hata hivyo, katika siku za karibuni tumepata faraja baada ya kuona bei zikishuka badala ya kupanda. Sababu mojawapo ya ongezeko la Bei hizi ni Umoja wa Nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC) kutumia mwanya wa kupanda kwa Bei za Mafuta kuongeza matumizi yao ya Kibajeti na hivyo kutotaka kushusha viwango vya matumizi hayo. Vilevile, Benki Kuu za Nchi hizi za OPEC zimelazimika kujiwekea fedha nyingi za tahadhari ili kujikinga na mabadiliko yoyote mabaya ya kiuchumi yanayoweza kutokea siku za usoni na kuathiri Uchumi wa Nchi zao. Nchi hizi pia zimeamua kutumia fursa hii ya mapato yatokanayo na Mafuta ili kuwekeza zaidi kwa ajili ya maendeleo ya vizazi vijavyo. Hii ni kwa sababu upo wasiwasi kuwa miaka ijayo rasilimali hii inaweza kwisha au Bei kushuka kutokana na mabadiliko makubwa ya Teknolojia ambayo yanaelekea kutumia nishati mbadala. Kwa vyovyote vile, Bei hizi kubwa zinaziwezesha Nchi hizi kujiweka vizuri hasa ikizingatiwa kwamba wana uwezo wa kukaa pamoja na kupanga Bei.

23. Pamoja na kwamba kuna mwelekeo wa kushuka kwa Bei za mafuta, bado kushuka huko kunaweza kusitusaidie sana katika kipindi cha muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya Mafuta Duniani kunakosababishwa na ukuaji mkubwa wa uchumi hasa kwa Nchi za China na India. Kwa Nchi zinazozalisha Mafuta, kupanda kwa Bei za Mafuta ni mavuno ya kwelikweli ambayo hawana budi kuyatumia ili kufanikisha mipango yao ya sasa na kwa vizazi vijavyo. Lakini kwa Nchi maskini kulazimika kulipia matumizi makubwa ya Nchi hizo ni mzigo mkubwa ambao utaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa sana.

24. Mheshimiwa Spika, tafsiri ya upandaji huu wa Bei za Mafuta na kutokuwepo utayari wa Nchi za OPEC kushusha Bei hizo ni kwamba tutalazimika kutumia fedha zetu za kigeni zaidi ili kuendelea kutumia mafuta ambayo ni muhimu katika kuendesha uchumi wetu. Kwa vile mafuta yanatumika kwa usafirishaji na uzalishaji, gharama za usafiri na usafirishaji wa bidhaa nyingi zitaendelea kupanda. Pili, tutahitaji fedha nyingi zaidi za kigeni kuagiza mafuta kwa ajili ya Viwanda na Usafirishaji.

25. Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji itaendelea kuhakikisha kwamba Bei za Mafuta hapa Nchini hazipandishwi kiholela ili kumlinda mlaji asiathirike sana. Kwa kuwa hatuna uwezo wa kudhibiti upandaji Bei katika Soko la Dunia, tunaangalia yale tunayoweza kuyafanya ndani ya Nchi yetu ikiwa ni pamoja na kukamilisha Kanuni zitakazotumiwa na Waagizaji Mafuta, ikiwemo TPDC ili waweze kuanza kuingiza mafuta kwa wingi na kwa bei nafuu inayotokana na ushindani wa Waagizaji Mafuta. Wizara ya Nishati na Madini ikishirikiana na EWURA ifuatilie kwa karibu mwenendo wa Bei za Mafuta katika Soko la Dunia ili kuhakikisha kwamba Wafanyabiashara hawatumii mwanya huu kuwaumiza Wananchi. Vilevile, kadri matumizi ya Gesi katika Viwanda na vyombo vya usafiri yatakayokuwa yanaongezeka tutapunguza uagizaji wa mafuta kutoka nje. Serikali yetu inaelekeza nguvu katika utafiti wa Gesi zaidi ili itumike kama nishati mbadala.

KILIMO

26. Mheshimiwa Spika, Tanzania tukifananishwa na Nchi nyingine tumebarikiwa kuwa na ardhi kubwa yenye rutuba nzuri, maji ya kutosha (Maziwa na Mito) pamoja na hali ya hewa nzuri ya kutuwezesha kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo. Kuanzia mwaka jana, 2007 kumekuwepo na upungufu mkubwa wa Chakula pamoja na kuendelea kupanda kwa bei za chakula Duniani kote. Hali hii inaweza kuwa ni neema kwa Wakulima kama tutatumia fursa hiyo vizuri. Kama Nchi za OPEC zinavyonufaika kutokana na ongezeko la Bei ya Mafuta, na sisi tunaweza kufaidika vya kutosha na ongezeko la Bei ya Vyakula kama tutajipanga vizuri. Watanzania tunayo fursa kubwa ya kuleta Mapinduzi ya Kilimo, lakini Mapinduzi haya hayawezi kuja bila ya kuwa na mabadiliko makubwa ya namna tunavyowekeza rasilimali zetu na mtizamo wetu kwenye Sekta ya Kilimo.

27. Mheshimiwa Spika, tunalo eneo la Hekta Milioni 44 linalofaa kwa Kilimo, lakini eneo linalolimwa ni Hekta Milioni 10.8, sawa na asilimia 24 tu. Vilevile, tunazo takriban Hekta Milioni 30 zinazofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji, lakini ni jumla ya Hekta 29,000, sawa na asilimia 0.1 tu zinazotumika. Takwimu hizi zinadhihirisha kwamba tunahitaji kubadilisha mwelekeo wa matumizi ya maeneo yanayofaa kwa Kilimo ili tuweze kuyatumia kikamilifu. Ili kuweza kuongeza eneo la Kilimo, ni wakati muafaka wa kuanza Kilimo cha Mashamba makubwa yanayotumia Teknolojia ya Kisasa, yaani “Kilimo cha Kibiashara” (Commercial Farming). Mimi ninaamini wapo watu wanaoweza kujitosa katika Kilimo hicho cha Biashara hapa Nchini. Tatizo ni woga wa kuanza. Mimi nasema Tusiogope! Tuanze sasa.

28. Mheshimiwa Spika, ninaelewa kwamba chini ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo – ASDP kupitia Mpango wa Kilimo wa Wilaya - DADPS, Wananchi wanaweza kupata Matrekta makubwa na madogo, Majembe ya kukokotwa na Ng’ombe na Maksai. Ziko Pikipiki na Baiskeli kwa Maafisa Ugani. Vilevile, uko Mpango wa kuwajengea nyumba Maafisa Kilimo wa Tarafa, n.k. Kinachotakiwa ni kuwashirikisha Wananchi ili miradi hiyo iibuliwe na Wananchi wenyewe na kupitishwa na Wilaya. Nilijaribu kupata Taarifa jinsi Wananchi wanavyoshirikishwa katika kuibua miradi yao kwa maendeleo yao nikabaini kwamba hili halijafanyika. Hivi najiuliza tatizo ni nini? Inaelekea Halmashauri hazijawahamasisha Wananchi kufanya hivyo chini ya DADPS, hivyo hawajui. Naziagiza Halmashauri zote kuchukua jukumu la kuwahamasisha Wananchi kushiriki katika kuibua miradi ya Kilimo inayolenga katika Kilimo cha Kibiashara.

29. Mheshimiwa Spika, katika Karne hii ya mabadiliko ya Hali ya Hewa na Mazingira kwa ujumla, Kilimo kinatakiwa kubadilishwa na kwenda na wakati kulingana na mabadiliko hayo na kuwa na Kilimo cha Kisasa na cha Kibiashara kinachoangalia mwelekeo wa mahitaji ya Soko na Ushindani wa Uzalishaji wa Kimataifa. Jambo hili ni muhimu, hasa tukizingatia kuimarishwa kwa Soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla.

30. Kilimo hapa Nchini bado hakijawa Kilimo chenye Tija kutokana na kuendeleza Kilimo cha Kujikimu (Subsistance Farming), badala ya Kilimo cha Biashara. Hii ndiyo sababu kubwa ya Wakulima wengi kuendelea kuwa maskini. Kilimo chetu bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uwekezaji Mdogo, Vishamba Vidogo Vidogo, Matumizi ya Teknolojia Duni, Uhaba wa Miundombinu, na Uhaba wa Masoko ya Mazao tunayolima. Vilevile, Kilimo chetu kinategemea zaidi Mvua kuliko Umwagiliaji Maji; Wakulima wengi kulima bila kutekeleza Kanuni za Kilimo Bora; na tatizo la upatikanaji mdogo wa Pembejeo za Kilimo, kama madawa, mbolea na mbegu bora. Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2007/2008, tumelima Hekta Milioni 2.88 za Mahindi kati ya Hekta Milioni 44.0 za Ardhi inayofaa kwa Kilimo na kuvuna Tani Milioni 3.6 kwa wastani wa Tani 1.2 kwa Hekta. Hata kwa eneo hilo hilo la Hekta Milioni 2.88 kwa Kilimo cha Mahindi kama tungetumia Teknolojia Sahihi na Zana Bora za Kilimo, tungezalisha wastani wa Tani 5 kwa Hekta na tungeweza kupata Mahindi tani Milioni 14.4 na kuongeza Usalama wa Chakula Nchini. Tunahitaji kuboresha Kilimo chetu ili kuongeza uzalishaji kwa Hekta, hivyo kuongeza kipato.

31. Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu wa Chakula na Upandaji wa bei za Vyakula Nchini, ambao umesababishwa na Teknolojia duni zinazotumika, ikiwa ni pamoja na uduni wa matumizi ya Zana za Kilimo, inabidi sasa tuongeze uzalishaji wa Chakula kwa kutumia Teknolojia ya Matrekta Madogo aina ya Power Tillers. Trekta la Power Tiller, linafanya kazi baada ya mtu kulisukuma na linaweza kufanya kazi zote ambazo zinafanywa na matrekta makubwa. Matrekta haya husukumwa na mtu wakati wa kulima, na gharama zake ni kidogo sana na linabana matumizi ya mafuta.

32. Mheshimiwa Spika, takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa Trekta hizi ndogo za kusukumwa – Power Tillers, hutumia Lita 2 za mafuta kwa kulima ekari moja, ikilinganishwa na Lita 8 kwa ekari kwa kutumia trekta kubwa. Kwa Dar es Salaam, Trekta hizi zinauzwa kati ya Shilingi Milioni 4.0 na Milioni 8.4 kwa mfano, Trekta la Kichina Shilingi Milioni 4.25, Trekta la Kijapani – Kubota Shilingi Milioni 6.1. Bei hizi ni pamoja na vifaa vyake mbalimbali, kama vile Jembe, Haro, Tela, Gurudumu za Mpira na Gurudumu za Chuma.

CHANGAMOTO KWA HALMASHAURI

33. Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa iliyopo ni kwa Halmashauri za Wilaya kuwawezesha Wakulima kupata pembejeo kwa urahisi. Kwa mfano, kama bei ya Power Tiller moja ni takriban Shilingi Milioni 6.1 pamoja na zana zake muhimu, na kama Halmashauri itatenga hata Shilingi Milioni 50 tu kwa mwaka, itaweza kuanza kununua na kusambaza zana hizi kwa Vikundi vya Wakulima au Mkulima mmoja mmoja. Trekta hizi ni nzuri na zitatusaidia sana katika kuongeza uzalishaji wa mazao, hasa kwa Wakulima wadogo wenye mashamba kati ya ekari 5 hadi 20. Uongozi wa Halmashauri uhamasishe Wakulima katika kuendeleza matumizi ya Matrekta haya katika maeneo yao. Vilevile, Halmashauri ziwawezeshe Wakulima kuyanunua au kukopeshwa Matrekta haya ili kuongeza uzalishaji. Hii ni pamoja na kuhamasisha uundaji wa Vikundi Vidogo Vidogo, ambavyo vinaweza kukopeshwa na vikaanzisha Vituo vya Kukodisha Matrekta ili kurahisisha Kilimo cha Mazao ya Chakula na Biashara. Kwa kuanzia nimeziagiza kila Halmashauri kuweka kwenye Ajenda zake wazo hili na nimezitaka kunipatia taarifa kuhusu maamuzi yao na hatua wanazozichukua kueneza zana hizi. Hili ni jambo linalowezekana kwa kutumia Bajeti zetu.

34. Vilevile, ili kuwapa Wakulima huduma za Ugani, Halmashauri ziwawezeshe Mabwana na Mabibi Kilimo na Mifugo kuwafikia Wakulima. Kwa mfano, bei ya pikipiki moja ni takriban Shilingi Milioni 3. Kwa bei hizo, hivi kweli Halmashauri zetu haziwezi kutenga fedha kwenye Bajeti zao kununua pikipiki kwa Mabwana na Mabibi Shamba. Nitapenda vilevile kupata taarifa jinsi kila Halmashauri Nchini ilivyoweka mikakati katika kutekeleza jambo hili. Wakuu wa Mikoa watoe taarifa za Halmashauri zao ifikapo tarehe 30 Septemba 2008.

35. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa mafunzo juu ya matumizi ya Zana Bora za Kilimo ili kuongeza uelewa wa Wakulima wa zana mpya. Zana zitakazohusika ni pamoja na Matrekta Madogo ya Mikono na vifungashi vyake, mashine za kupandikiza mpunga, majembe ya palizi yanayokokotwa na Wanyamakazi na mashine ndogo za kusindika muhogo, korosho na mtama. Serikali pia itafanya tathmini ya kina juu ya mahitaji ya mashine na Zana mbalimbali za Kilimo kulingana na uwezo na mahitaji Nchini na kuanzisha mfumo wa ukusanyaji, utunzaji na usambazaji wa takwimu za Zana za Kilimo ili kurahisisha uandaaji wa Mipango ya Maendeleo. Mwongozo wa kutumia Zana za Kilimo kibiashara utaandaliwa na Wizara itaendelea kutoa ushauri wa kiufundi na utaalam katika Halmashauri za Wilaya ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya Zana za Kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji na tija katika Kilimo.

36. Mheshimiwa Spika, Mwandishi, Mshairi na Mchekeshaji wa Uingereza Bwana Paul Chatfield aliandika:
“Kilimo ndicho Mkemia Bora kuliko wote, hugeuza Ardhi, na hata Mbolea, kuwa Dhahabu, humlipa na kumzawadia Mkulima afya bora”.

Nakubaliana na Mwandishi huyu kwamba tunaweza kubadili Ardhi yetu kuwa Dhahabu kama tukizingatia Kilimo Bora kwa kutumia Zana Bora za Kilimo na Pembejeo nyingine kwa usahihi. Nichukue fursa hii kwa mara nyingine tena kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake wa kuongeza fedha za Akaunti ya EPA kwa ajili ya Kilimo. Nina imani kuongezeka kwa fedha hizi kutatia hamasa Kilimo na uzalishaji kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Nisisitize tena hizi siyo fedha za Warsha za Kilimo kwa Watendaji Maofisini, ni fedha za kununulia Pembejeo na ihakikishwe kwamba yule anayestahili kupata, anapata na kutumia.

MASOMO YA HISABATI

37. Mheshimiwa Spika, katika Hotuba yangu ya kufunga Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge lako Tukufu niliyoitoa tarehe 25 Aprili 2008, nilizungumzia kwa kirefu kuhusu maboresho ya Sekta ya Elimu, hususan umuhimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi. Pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi, nilitoa tahadhari ya kukosa Wana-Sayansi ambao ni Watu muhimu sana katika maendeleo ya Taifa letu kwenye Karne hii na nyingine zijazo. Nililinganisha ufaulu wa Masomo ya Sayansi na Sanaa katika Shule za Msingi na Sekondari ambako ilithibitika kwamba ufaulu wa Masomo ya Sayansi katika Shule hizi kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2003 hadi 2007 ulikuwa umeshuka sana.

38. Vilevile, tarehe 26 Julai 2008, nilipata fursa ya kuwatunukia zawadi Wanafunzi wa Darasa la Saba wa Mkoa wa Dodoma na Walimu ambao walifanya vizuri zaidi kwenye Mtihani Maalum wa kupima uwezo wao wa Somo la Hisabati. Katika hafla hiyo, Wanafunzi 20 walipewa zawadi na “Benki ya CRDB” kwa kufanya vizuri. Kati ya Wanafunzi 20, Wasichana walikuwa 10 na Wavulana ni 10. Aidha, ilibainika kwamba Washindi wawili wa mwanzo ni Wasichana. Nawapongeza sana Wanafunzi wote 20 na hasa Wasichana Wawili walioshika namba moja na mbili kwa kuonyesha mfano wa kufanya vizuri katika Hisabati. Hii inadhihirisha kuwa kufanya vizuri inawezekana kwa kila Mwanafunzi.

39. Mheshimiwa Spika, natoa changamoto kwa Halmashauri zote na Mikoa yote Tanzania kuiga mfano huu wa Dodoma wa kuwapima na kuwashindanisha Wanafunzi kwenye Somo la Hisabati na Sayansi. Itakuwa vizuri pia kuwatambua Walimu wa Hisabati na Sayansi ambao Wanafunzi wao watafanya vizuri katika kuwashindanisha. Tuwabainishe na wote wapewe zawadi kama walivyofanya katika Mkoa wa Dodoma. Nayaomba Makampuni mbalimbali na Watu binafsi kujitokeza katika kutoa zawadi kama walivyofanya wenzao wa CRDB kwa Mkoa wa Dodoma. Lengo liwe ni kuwaongezea ari na juhudi Walimu katika kufundisha Masomo ya Hisabati na Sayansi na Wanafunzi kupenda na kuongeza juhudi katika Masomo haya na kuwapa motisha Wanafunzi wanaofanya vizuri.

HALI YA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA HISABATI NCHINI ILIVYO SASA

40. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa nilizungumzia kwa kina kuhusu Masomo ya Hisabati na Sayansi katika Mkutano wa Kumi na Moja, leo napenda nitumie muda kidogo kuelezea kuhusu hali ya ufundishaji na ufaulu wa Somo la Hisabati peke yake hapa Nchini. Imedhihirishwa kwamba Somo la Hisabati ndilo Somo ambalo ufaulu wake ni wa kiwango cha chini sana kuliko Masomo mengine yote. Taarifa za Ukaguzi wa Shule zinaonyesha kwamba, hali ni mbaya zaidi katika Shule za Msingi. Kwa mfano, mwaka 2001, katika Mtihani wa kumaliza Darasa la Saba, asilimia 62 ya Watahiniwa katika Wilaya ya Morogoro Vijijini walipata Sifuri katika Mtihani wa Hisabati. Hali hii inamaanisha asilimia 62 ya Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Wilaya hii walimaliza shule bila kujua Hisabati rahisi za kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya. Katika Mtihani wa Kidato cha Nne, mwaka 2007, matokeo yanaonyesha kwamba asilimia 69 ya Watahiniwa Walishindwa katika Mtihani wa Hisabati. Katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia hali kama hii inatisha na haiwezi kuruhusiwa kuendelea kutokea.

41. Mheshimiwa Spika, sababu nyingi zimetolewa kuhusu kushindwa kwa Wanafunzi katika Masomo, hususan Hisabati. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na zifuatazo:
i) Msingi Mbaya kuanzia Elimu ya Awali: Imekuwa ni kawaida watoto kuwekewa msisitizo katika Somo la Kiingereza katika Elimu ya Awali. Hali hii imesababisha Wanafunzi wengi kukifahamu Kiingereza kwa sababu ya msingi mzuri, imara na bora. Inasikitisha hali sivyo ilivyo katika ufundishaji wa Hisabati. Wakati sasa umefika wa kuanza kuweka msisitizo katika ufundishaji wa Hisabati kuanzia Elimu ya Awali. Wanafunzi wajengewe msingi mzuri ili wapende na kujua umuhimu wa Hisabati;

ii) Upungufu wa Walimu: Shule nyingi hazina Walimu wa Hisabati;

iii) Woga wa Somo la Hisabati: Wanafunzi wengi wamekuwa waoga kwa jinsi Hisabati zilivyo. Wako wanaojiandaa kabisa kujihami na wengine wanachukia kabisa kusoma Somo la Hisabati;

iv) Uhaba wa Vitabu na Vifaa vingine vya Kufundishia: Kwa hali hiyo, Walimu wanakuwa ndio Waandikaji Wakuu kwa kutumia Ubao na Chaki. Aidha, Wanafunzi hawawezi kupata nafasi ya kujisomea wala kufanya mazoezi ya kutosha;

v) Ukosefu wa Motisha: Walimu na Wanafunzi wanakosa motisha ya kufanya Somo la Hisabati. Baadhi ya Walimu wamekata tamaa katika ufundishaji wa Somo la Hisabati;

vi) Kushindwa kuanza kufundisha mapema Somo la Hisabati Ziada “Additional Mathematics” kuanzia Kidato cha Kwanza: Pamoja na kwamba utaratibu huu ulikwishaanza takriban miaka miwili iliyopita, baadhi ya Shule hazijaanza kufundisha Somo hilo; na

vii) Ukosefu wa Walimu wenye uwezo wa Kufundisha Somo la Hisabati: Baadhi ya Walimu hawajawahi kuhudhuria Mafunzo Maalumu ya Somo la Hisabati. Wapo Walimu waliosoma Uhasibu ambao ndio wanaoutumiwa kufundisha Hisabati. Inakuwa vigumu kwa Mwalimu huyu aliyesoma Uhasibu kuweza kufundisha Hisabati katika Vidato vya juu zaidi, k.m. Kidato cha Tatu na cha Nne. Aidha, kuna baadhi ya Walimu ambao hawakufaulu vizuri Hesabu au hawafahamu vizuri Hesabu.

Haya ni baadhi tu ya matatizo yaliyobainishwa ambayo yamesababisha kushuka kwa ufaulu wa Somo la Hisabati. Lakini Mwandishi mmoja wa Vitabu, Bwana Henri – Marie Beyle akielezea hisia zake kuhusu Somo la Hisabati alisema: “I used to love Mathematics for its own sake, and still I do, because it allows for no hypocrisy and no vagueness….”. Anachosema Bwana Henri ni kwamba kwa Somo la Hisabati halina unafiki wala utata. Ni somo la wazi ambalo ni dhahiri. Unaposema: mbili zidisha mbili ni nne na sio vinginevyo. Kwa maana hiyo, ni muhimu tuchukue hatua za maksudi kuliendeleza.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA

42. Mheshimiwa Spika, pamoja na sababu zilizoorodheshwa hapo juu, zipo hatua za maksudi ambazo zimeanza kuchukuliwa. Baadhi ya hatua hizo ni:
i) Kuundwa kwa Chama imara cha Somo la Hisabati Nchini, kinachojulikana kama Chama cha Hisabati Tanzania (CHAHITA) ambacho kimekuwa mstari wa mbele kukuza na kuendeleza Somo la Hisabati Nchini. Chama hiki kimekuwa kikiwaunganisha Walimu wa Hisabati Nchini kwa kufanya Warsha mbalimbali na kuandaa Mikutano ya Mwaka yenye lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kufundisha somo hilo muhimu. Wito wangu kwa Walimu wote wa Hisabati Nchini ni kujiunga na Chama hiki ili kuweka mawazo yao pamoja ya jinsi ya kuendeleza Somo hili la Hisabati;

ii) Kuinua na kukuza Rasilimali Watu, hususan wale ambao tayari wana Elimu ya Hisabati kwa kuwapatia mafunzo zaidi ya mbinu mbalimbali za Hisabati. Kupanua upeo na uwezo wao wa kujua Hisabati ili waendane na mahitaji ya maendeleo ya sasa. Wale ambao wamekuwa wakijenga tabia ya kupenda Hisabati wamepata maendeleo na kurahisisha kazi zao;

iii) Kujenga dhana ya kujiamini kwa Watu wanaojua Hisabati na kujenga falsafa ya mambo kwa mpangilio wenye mantiki (Logic Thinking) kwa kuwapatia mazoezi ya mara kwa mara; na

iv) Kuwekeza katika Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia msingi wake ni ujuzi na uwezo katika Somo la Hisabati. Kwa maneno mengine ni vigumu kukawa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia bila kutegemea Hisabati.

43. Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba Somo la Hisabati linaonekana kuwa gumu, mwenendo wa sasa wa Wanafunzi wengi kushindwa katika Mitihani ya Somo hili ni suala ambalo linahitaji hatua za haraka ili kuinua ubora na kiwango cha ufaulu wa Somo hili. Hivyo, pamoja na hatua zilizotajwa hapo juu zinazochukuliwa hivi sasa, hatua zifuatazo pia zitachukuliwa:
i) Kufundisha Walimu wengi zaidi wa Hisabati wenye mbinu mpya na za kisasa za ufundishaji wa Somo la Hisabati;

ii) Kuandaa vifaa vya kufundishia ambavyo vinaendana na mabadiliko yanayotokea ya Somo la Hisabati ili Somo hili liweze kuvutia;

iii) Kutunga na kuwa na vitabu vya kutosha vya Somo la Hisabati Mashuleni na vyenye mifano halisi inayozingatia Mazingira ya Nchi yetu;

iv) Kubadilisha mbinu za ufundishaji kutoka katika mbinu za mhadhara (lectures) kwenda katika mbinu shirikishi (participatory oriented teaching);

v) Kuboresha mbinu za kupima uwezo wa Mwalimu akiwa Darasani na uwezo wa Mwanafunzi kuelewa;

vi) Kuwekeza zaidi katika Somo la Hisabati kwa kutenga Bajeti ya kutosha katika Somo hili;

vii) Kuimarisha Ukaguzi wa Somo la Hisabati ili kubaini mapungufu mapema na kuyaondoa; na

viii) Kuanzisha Somo la “Additional Mathematics” kuanzia Kidato cha Kwanza kila Shule ya Sekondari.

44. Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba Somo la Hisabati ni Somo linalojenga dhana ya kujiamini na kujenga falsafa ya mambo kwa mpangilio wenye mantiki. Hii inanikumbusha kisa cha Mwalimu mmoja ambaye alitoa zoezi la Hisabati Darasani, akawa anamwuliza Mwanafunzi wake kama ifuatavyo:
“Kama nikikupatia Panya wawili na wawili tena na wengine wawili, Panya wangapi utakuwa nao?”

Mwanafunzi yule akajibu: Saba!

Mwalimu akasema: Hapana, hebu sikiliza vizuri swali langu.
“Kama nikikupatia Panya wawili na wawili tena na wengine wawili, Panya wangapi utakuwa nao?”
Mwanafunzi yule akajibu: Saba!

Mwalimu akasema: Aah! Hebu niulize kwa njia nyingine.
“Kama nikikupatia Maembe mawili na mawili tena, na mengine mawili, utakuwa na Maembe mangapi?”
Mwanafunzi yule akajibu: Sita!

Mwalimu akasema: “Safi sana. Sasa nirejee kwenye swali
langu. Kama nikikupatia Panya wawili na wawili tena na wengine wawili, Panya wangapi utakuwa nao?”
Mwanafunzi akajibu: Saba!

Mwalimu kwa hasira akamwambia Mwanafunzi yule:
“Inakuwaje kwa akili zako timamu unasema mafungu matatu ya Panya wawili wawili ni Saba?”

Mwanafunzi akajibu tena kwa upole : “Kwa vile tayari ninaye
Panya mmoja nyumbani!!”

Mfano huu unaonyesha umuhimu wa Mwalimu wa Hisabati kutumia muda mrefu kwa Mwanafunzi mmoja mmoja ili somo hilo lieleweke vizuri pamoja na mpangilio mzuri wa kuuliza kile unachotaka na Mwanafunzi kukielewa. Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, Somo la Hisabati ni muhimu sana kwa kujenga uwezo wa awali wa Mwanafunzi. Napenda kurudia wito wangu kwa Mashirika, Taasisi na Watu Binafsi kutoa motisha kwa Wanafunzi, Walimu na Shule ili kukuza Vipaji vya Somo la Hisabati. Ninaamini tukiamua tunaweza. Tulifanya vizuri kuwatambua na kuwaenzi wenye Vipaji katika Mchezo wa Mpira wa Miguu hapa Bungeni, tufanye hivyo hivyo pia kwa wenye Vipaji kwa masomo ya Hisabati ili kuendeleza fani hii. Tuwaenzi Wanafunzi na Tuwaenzi Walimu wao.

45. Mheshimiwa Spika, ziko taarifa kwamba mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu Somo la Hisabati hayajaungwa mkono na utafiti wa uhakika kubaini chanzo cha Wanafunzi kushindwa vibaya katika Somo hili. Nimeambiwa kwamba Chama cha Hisabati Tanzania (Mathematics Association of Tanzania) wamependekeza kufanya utafiti wa uhakika wa kubaini chanzo cha Wanafunzi kushindwa vibaya. Nitumie nafasi hii pia kuiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufuatilia kwa karibu pamoja na mambo mengine mapendekezo yatakayotolewa na CHAHITA na Taasisi zingine zilizopo kama vile, Idara ya Hisabati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ili kubainisha matatizo na nini kifanyike.

46. Mheshimiwa Spika, leo nimeongelea sana kuhusu Somo la Hisabati. Hata hivyo, ziko changamoto nyingi zinazoikabili Sekta ya Elimu kwa ujumla. Changamoto kubwa ni kuinua kiwango cha Ubora wa Elimu kinachotolewa, kuboresha utoaji wa Elimu, utekelezaji wa lengo la Pili na la tatu la Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Elimu; na Utekelezaji wa Malengo tuliyojiwekea kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2005. Katika Ilani ya CCM kwa mfano, tumejiwekea Malengo ya kujenga angalau Shule moja ya Sekondari katika kila Kata. Vilevile, tumejiwekea Malengo ya kuboresha mazingira ya Shule, ikiwemo upatikanaji wa Vifaa na Ujenzi wa Maabara na kukabiliana na upungufu wa Walimu. Ni dhahiri kwamba, changamoto hizi ni kubwa na zinahitaji kiasi kikubwa cha fedha ili kukabiliana nazo.

47. Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto hizo katika Sekta ya Elimu, ndio maana mwaka 2001, Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheria ya Bunge Na. 8 iliyoanzisha Mfuko wa Elimu hapa Nchini. Madhumuni yakiwa ni kuongezea nguvu zaidi juu ya zile za Serikali katika kugharamia Sekta ya Elimu katika kuinua kiwango cha Ubora wa Elimu. Vilevile, tunayo Mamlaka ya Elimu Tanzania ambayo imeanzishwa Sambamba na Sheria hii ili kusimamia upatikanaji wa Mapato na Shughuli za Mfuko huu. Jukumu kubwa la Mamlaka hii ni kuelimisha na kuhamasisha Wadau wa Elimu wakiwemo ninyi Waheshimiwa Wabunge na Umma kwa jumla juu ya umuhimu wa kuchangia Maendeleo ya Elimu Nchini, hususan kupitia Mfuko wa Elimu. Pamoja na kuwa na Mfuko wa Elimu kwa Nchi nzima, napenda kuziagiza kila Halmashauri katika ngazi ya Wilaya na kila Mkoa kuwahamasisha Wananchi kuanzisha Mifuko ya Elimu kwa ajili ya Maendeleo ya Elimu katika Wilaya na Mikoa. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuboresha kiwango cha Elimu kilichopo sasa kwa kasi zaidi bila ya kusubiri Serikali kufanya kila kinachohitajika.

48. Mheshimiwa Spika, tarehe 19 Agosti, 2008 nilipata nafasi ya kufungua Warsha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Mifuko ya Elimu iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa hapa Dodoma. Bila shaka yapo mengi mazuri tuliyojifunza katika Warsha ile, hususan kutoka kwa wenzetu wa Ghana na Nigeria ambao walialikwa kutoa Mada kuhusu uzoefu wao katika Uendeshaji na Usimamizi wa Mifuko ya Elimu. Naitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kusambaza Azimio lililokubalika kwenye Warsha hiyo pamoja na uzoefu uliopatikana kwa Mikoa na Wilaya zote ili kuipa ufahamu wa Mifuko hiyo hapa Nchini. Azimio hilo liandaliwe kwa lugha nyepesi ambayo itaeleweka na Wadau wa ngazi zote.

Utekelezaji wa Mpango wa Afya ya Msingi (MMAM)

49. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na TAMISEMI, imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) wa mwaka 2007/2008. Mpango huu una lengo la kusogeza huduma za afya karibu na Wananchi. Mpango huu utatekelezwa katika Awamu Mbili za miaka mitano mitano. Katika Awamu ya Kwanza kipaumbele kimewekwa kwenye upatikanaji wa Watumishi watakaotoa huduma katika vituo vilivyopo ambavyo havina Wataalam. Vituo hivyo vinajumuisha Zahanati 652 zilizojengwa na Wananchi kwa msaada wa TASAF.

50. Mheshimiwa Spika, tangu Mpango huu kuanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2007/2008, mafanikio yaliyopatikana ni katika maeneo yafuatayo:
i) Watumishi na Ajira:
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika mwaka 2007/2008, iliajiri jumla ya Watumishi 200 wa Kada mbalimbali kwa ajili ya Hospitali za Rufaa za Kibong’oto, Mbeya na Mirembe. Vilevile, Serikali ilitoa kibali cha Ajira kwa Wataalam 6,437 wa Kada za Afya katika Halmashauri, Sekretarieti za Mikoa na Wizara mbalimbali. Kutokana na kutokuwepo kwa Wataalam wa kutosha katika Soko la Ajira Serikali iliwapangia vituo Wataalam 4,812 tu. Wataalamu 3,645 kati ya hao walipangiwa kutoa huduma katika Vituo na Zahanati mbalimbali zikiwemo 253 kati ya 652 zilizojengwa na Halmashauri kwa kushirikiana na Wananchi na TASAF. Zahanati hizo tayari zimefunguliwa na zinafanya kazi.

ii) Mafunzo ya Watumishi wa Afya:
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweza kuvifanyia ukarabati na kubadilisha matumizi ya Vyuo mbalimbali. Mpango huu wa ukarabati na upanuzi wa Vyuo utaendelea mwaka hadi mwaka kadri fedha zitakavyopatikana ili kuongeza idadi ya Wanafunzi wanaodahiliwa na kufikia lengo la Watumishi wanaohitajika.

Vilevile, Serikali imebadili matumizi ya Vyuo 16 (Vyuo 10 vya Uuguzi na 6 vya Sayansi Shiriki) vilivyokuwa vya mafunzo ya kujiendeleza kuwa vya Wataalam wa Afya. Hii imewezesha Wizara kudahili jumla ya Wanafunzi Watarajali 827 katika Vyuo hivyo. Kati ya hao 519 ni wa Vyuo vya Uuguzi. Chuo cha Uuguzi Mirembe kimeongezewa Programu ya Stashahada kwa Wanafunzi, Wataalam wa Afya watarajiwa. Vyuo vya Sayansi Shiriki 6 vilidahili jumla ya Wanafunzi 308.

Utekelezaji wa Mpango wa Afya ya Msingi unaendelea na inatarajiwa utapata kasi zaidi.

51. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha hoja yangu, napenda kusisitiza maeneo machache yafuatayo:-
Moja: Tunayo changamoto ya kupanda kwa Bei ya Mafuta ambayo inaathiri uchumi wetu kwa kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Tusitumie kupanda kwa bei ya Mafuta kuwa kisingizio cha kuwaumiza Wananchi hata pale ambapo hapastahili kupandisha bei za bidhaa. Vyombo vinavyohusika vifuatilie kwa karibu mwelekeo wa Bei ya Mafuta na bei za bidhaa kuhakikisha kwamba Wafanyabiashara hawatumii mwanya huu kuwaumiza Wananchi;

Pili: Bado ipo nafasi ya kutumia Kilimo katika kubadili maisha ya Mtanzania. Viongozi wote wakiwemo Waheshimiwa Wabunge tuonyeshe mifano katika kuendeleza Sekta ya Kilimo. Tuwahimize Wananchi waongeze juhudi, tuwape moyo na kuwahamasisha kutumia Zana Bora za Kilimo ili kuongeza tija. Maisha Bora yanapatikana kama tukitumia utaalam kwenye Kilimo;

Tatu: Suala la Watoto wetu kupenda kusoma Somo la Hisabati linahitaji msukumo wa pekee. Tuliseme, tuliongee, na tulizungumze bila kuchoka kuanzia Majumbani, Chekechea na kuendelea. Tuwape moyo Watoto wetu wajue umuhimu wa kusoma na kufanya vizuri katika Somo la Hisabati; na

Nne: Tuwahimize Wananchi wapende kuanzisha na kuchangia katika Mifuko ya Elimu kwenye maeneo yetu. Tunayo mifano kwamba katika ngazi ya Familia tunaweza kuchangia vizuri sana katika kufanya Sherehe mbalimbali. Tutumie dhamira hiyo hiyo kuchangia Mifuko ya Elimu kuwasomesha Watoto wetu. Tubadilike kifikra. Tujiunge na jamii zenye kupenda maendeleo ya Elimu. Tunaweza! Kilichobaki ni kuamua na tufanye hivyo sasa!

Hitimisho

52. Mheshimiwa Spika, mwisho nikushukuru wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kutuongoza vizuri, kwa busara na kwa kuzingatia Kanuni za Bunge wakati wote wa Mkutano huu. Tumejifunza mengi kuhusu Taratibu na Kanuni za Bunge. Mmetuvumilia, mmetuongoza na tumekubaliana. Ninawashukuru tena Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yenu ya dhati kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu. Niwashukuru Watumishi na Wataalam wote wa Serikali waliosaidia kujibu Maswali na Hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge zilizojitokeza hapa wakati wa Mkutano huu. Aidha, nawashukuru Waandishi na Vyombo vya Habari kwa kuwapatia Wananchi habari kuhusu Majadiliano yaliyokuwa yanaendelea hapa Bungeni.

53. Kwa namna ya pekee niruhusu niwashukuru Madereva wote wa Viongozi, Madereva wa Waheshimiwa Wabunge, Madereva wote wa Watendaji Wakuu wa Serikali na Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi ambao katika kipindi chote cha Mkutano huu wamehusika kuwaendesha Viongozi wote wakiwemo Waheshimiwa Wabunge pamoja na Wataalam kutoka sehemu mbalimbali Nchini kufika hapa Dodoma kuhudhuria Mkutano huu wa Kumi na Mbili. Wamefanya kazi nzuri. Nawasihi waendelee kuwa Makini katika kazi yao hii muhimu. Nasi tunawahakikishia kwamba tunathamini mchango wao katika maendeleo ya Nchi yetu. Mwisho kabisa namshukuru Kaimu Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah na Watumishi wote wa Ofisi ya Bunge kwa huduma nzuri zilizowezesha kukamilisha shughuli zilizopangwa katika Mkutano huu bila matatizo.

54. Mheshimiwa Spika, kazi kubwa ambayo bado iko mbele yetu hususan baada ya kukaa Bungeni kwa kipindi chote hiki ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika kutekeleza yote tuliyoyapitisha kwenye Mkutano huu. Bwana Albert Einstein Mwanafizikia aliandika: “The World is a dangerous place. Not because of the People who are evil; but because of the People who don’t do anything about it”. Nchi yetu ni nzuri na ina Amani tele. Tukitimiza wajibu wetu sote nina hakika tutafanikiwa katika azma yetu ya kujiletea maisha bora. Twendeni tukawajibike. Twendeni tukafanye kazi. Twendeni tukatumie rasilimali zilizopo katika Nchi yetu kuinua uchumi wetu. Tutumie fedha tulizoziidhinisha hapa kwa uangalifu na nidhamu kubwa. Tumekuwa hapa kwa siku 81 tukijadili na kuidhinisha Bajeti za kila Wizara. Kazi iliyofanyika ya kuidhinisha fedha hizi ni kubwa. Itakuwa haina maana kama tutaacha fedha hizo zilizoidhinishwa zitumike bila mpangilio! Wananchi wetu hawatatuelewa. Umaskini utaisha na maisha bora yatapatikana kama tutatumia vizuri rasilimali zilizopo kwa maendeleo yetu. Sote tushirikiane kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu.

55. Mheshimiwa Spika, nitumie muda huu kumwomba Mwenyezi Mungu awatangulie, awalinde na awaongoze katika safari ya kurejea nyumbani na Majimboni mwenu.

56. Mheshimiwa Spika, Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Mwezi Septemba 2008. Napenda niwatakie Waislamu wote Mfungo mwema na wenye mafanikio ili kila atakayeamua kufanya Ibada hiyo aifanye kikamilifu na kama inavyoagizwa katika Kitabu cha Quran Tukufu.

57. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo napenda kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liahirishwe hadi tarehe 28 Oktoba 2008, Siku ya Jumanne, Saa 3:00 Asubuhi litakapokutana katika Ukumbi huu hapa Dodoma.

58. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.





Irene K. Bwire,
Cell:+255-784-365-214,
Email: irenekaki@yahoo.com

Will Smith akutana na Karume




Rais wa Zanzibar na DK Amani Abeid Karume alimpata mgeni Ikulu ambaye ni muigizaji kutoka Marekani Will Smith.

Walipata nafasi ya mazungumo na baadayue kupiga picha ya pamoja wakiwa na wake zao kama picha hizi za Ikulu ya Zanzibar zinavyoonyesha.


Ziara inayolipa ya Marekani, mihela mitupu


The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation.Mr.Bernard Membe and The US Trade and Development agency(USTDA) Deputy DirectorMs. Leocadia Zak sign an agreement in which USTDA will award a $600,000 grant toward establishing operational ptotocols in the implementation and enforcement of electicity,petroleum and natural gas regulations based on international practices.The Signing ceremony took place at USAID Headquarters,in Washington D.C. this morning in the presence of President Jakaya Mrisho Kikwete and the Deputy USAID administrator James Kunder.The First Lady Mama Salma Kikwete who is accompanying the President, attended the ceremony.

Ziara ya kikwete yavuna vitabu vya sayansi


The USAID Chief Education division,Africa Bureau Dr.Sarah Moten welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete at her office in Washington DC yesterday.During a meeting with the President,Dr.Moten announced a new assistance in which USAID will procure $1.5 million worth of much needed-science books for secondary school students in Tanzania. Picha hii ni mali ya Freddy Maro wa State House.

da Chemi yupo ndani ya Edge of darkness na wakali wa mamuvu


Nilifurahishwa na habari hii ya da Chemi kuingia katika muvu jingine tena katika kipindi kifupi. Ninavyojua wakali waliomo ndani ya Edge of Darkness utaona kwanini nimefurahi.

Hapa chini nakupa taarifa yake mwenyewe kwa wale wanaopenda burudani za aina hii, wapenzi wa mambo ya filamu.


Go... go... go...da Chemi! all the baraka.

kutoka Lukwangule



Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba. Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room. Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.Haya nitawapa updates.Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

Thursday, August 28, 2008

happy besdei michuzi


Happy birth day michuzi

and God bless you


Hii ni kutoka kwa lukwangule

Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu Richmond aliyoitoa leo Bungeni


Wasomaji hii ndiyo taarifa ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameiwakilisha bungeni. Imechapwa kwa mkono sikuwa na muda wa kuhakiki taipografiki eras. lakini nimetekeleza ahadi yangu ya kwamba tutaleta kinachowezekana. Hatuna nyongeza.

Msimbe lukwangule




TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MH. MIZENGO P PINDA,(MB),
KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE
YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA RICHMOND
DEVELOPMENT COMPANY LLC
28 AGOSTI 2008

UTANGULIZI:

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 37 cha kanuni za kudumu za Bunge(Toleo la 2007), naomba kuwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya Mkataba baina ya Tanesco na kampuni ya Richmond Development Company LLC.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Kumi wa Bunge tarehe 15 Februari 2008, Bunge lako tukufu lilipitisha Maazimio 23 baada ya mjuadala wa taarifa ya kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwezi Novemba 2007 ili kuchunguza mchakato wa Zabuni ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa kuzalisha umeme wa dharura nchini mwaka 2006. Kwa kuzingatia uzito wa suala hili, wakati nilipotoa hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi wa Bunge nilieleza kuwa serikali itaunda timu ndogo ya wataalamu ili kuchambua kwa makini na kupendekeza namna ya kutekeleza maazimio hayo 23 yaliyopitishwa na Bunge. Vilevile niliahidi kuwa kamati hiyo itazingatia mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Taarifa ya kamati Teule ya Bunge na Taarifa za majadiliano zilizoingizwa kwenye kumbukumbu za Bunge(HANSARD).

Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Aprili 2008 wakati nikitoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa kumi na moja wa Bunge lako tukufu , niliwasilisha taarifa ya Awali ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika utekelezaji wa maazimio hayo.

Aidha , niliahidi pia kuwa serikali itajitahidi kuharakisha utekelezaji wa Maazimio hayo kwa kadri itakavyowezekana na Taarifa rasmi itawasilishwa katika Mkutano huu wa Kumi na mbili wa Bunge jambo ambalo linafanyika leo.

4. Mheshimiwa Spika, mwezi februari 2008 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikubali kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa(Mb). Aidh , Mawaziri wawili, Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha(Mb), na Mheshimiwa Nazir Karamagi(Mb), nao kwa wakati mmoja walijiuzulu kw akuwajibika kwao kisiasa kwa maslahi ya Taifa. Kutokana na uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu, kikatiba kulisababisha Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa, jambo ambalo lilikuwa ni uamuzi mkubwa kwa serikali. Hatua hii inaonyesha kiwango kikubwa cha usikivu wa serikali yetu hasa kwa kuzingatia kwamba hatua hii ilichukuliwa mapema mara tu baada ya Taarifa ya Kamati Teule kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu.


Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hiyo, napenda kueleza hatua nyingine muhimu zilizochukuliwa na serikali hadi hivi sasa:-

Kwanza, Serikali imekwishapeleka maelekezo kwa kila Wizara na Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Maazimio haya na hatua za utekelezaji zinaendelea kuchukuliwa na vyombo hivyo.

Pili, Kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya Tanesco na Richmond development Company LLC uliorithiwa na Dowans S.A , Serikali imechukua hatua ya kusitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

Tatu, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba baina ya Tanesco na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Kampuni ya Dowans S.A.

Nne, Watumishi wote wa Umma waliohusika katika mchakato wa kuandaa na kutoa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND wameandikiwa barua za kujieleza kama hatua za awali za kinidhamu kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma, Aidha kwa wale watakaoonekana kuwa wamefanya makosa ya jinai hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo sasa ningependa kueleza kipengele kwa kipengele kuhusu hatua za utekelezaji wa Maazimio yote kama yalivyorekebishwa tarehe 15 Februari 2008 na mtoa Hoja wakati akihitimisha hoja yake.

AZIMIO NAMBA 1.

“Sheria ya manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004(Public procurement Act, 2004) haina nguvu ya kutosha. Sheria ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale Sheria na Kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Wizara ya Fedha na Uchumi ikishirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa manunuzi ya Umma(PPRA), wamekwishaainisha maeneo yote yenye mapungufu na yanayohitaji marekebisho kwenye Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

Baada ya zoezi hilo kufanyika , Serikali itawasilisha katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu, mapendekezo ya kufanya Marekebisho katika Sheria hiyo, maeneo yatakayozingatiwa ni yafuatayo:

(i) Kuipa uwezo PPRA kusitisha Zabuni yoyote pale itakapobainika kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Manunuzi ya Umma.
(ii) Kuipa nguvu PPRA kutoa maelekezo kwa Mamlaka zinazohusika na ununuzi(yaani Procuring Entities)kuchukua hatua kwa watakaokiuka Sheria ya manunuzi ya Umma.
(iii) Kuifanya PPRA kuwa Taasisi Huru inayojitegemea ikiwa na Muundo sawa na ule wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali(CAG).
(iv) Kufanya marekebisho yatakayowezesha Sheria kutoa adhabu kali kwa Viongozi na Watumishi wa Umma watakaobainika kujihusisha na ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.
(v) KUfanya marekebisho ya kuzitaka Mamlaka zenye dhamana zitakazopokea hoja za ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka PPRA, kutoa taarifa kuhusu hoja hizo katika kipindi maalum na ikibidi kuchukua hatua zaidi kwa Taasisi au Mtu atakayekiuka Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.
(vi) Kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kushughulikia masuala ya Ununuzi wa Dharura yanapotokea.
(vii) Kuweka utaratibu wa kuwezesha kufanyika uchunguzi wa kina(due diligence) kwa wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia mikataba na Serikali.
(viii) Kuweka utaratibu wa kutumia kamati Huru ya wataalamu itakayofanya uchunguzi wa kina pale itakapobidi.


AZIMIO NAMBA 2:

“Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma(PPRA) isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayp ni Taassi ya Ununuzi(procuring Entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika ofisi ya Rais na Taarifa zake kuwasilishwa Bungeni.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

(i) Kulingana na Sheria ilivyo hivi sasa, PPRA ni Taasisi Huru inayojitegemea nje ya Muundo wa Wizara ya Fedha na uchumi, Aidha PPRA ina Bajeti yake inayojitegemea na pia ina chombo chake maalum cha usimamizi yaani Bodi ya wakurugenzi. Hata hivyo, katika Marekebisho ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika. Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kufanya PPRA iwe na Muundo sawa nma ule wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo utatoa uhuru kwa Chombo hicho kutoa maamuzi ya kila siku bila kuingiliwa na Chombo chochote, ingawa kisera itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa HAZINA kama ilivyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(ii) Kuhusu Taarifa za mwaka za PPRA kuwasilishwa Bungeni, suala hili limezingatiwa katika Kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, inayotumika hivi sasa. Chini ya sheria hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi huwasilisha bungeni taarifa ya kila mwaka ya utendaji wa PPRA.

AZIMIO NAMBA 3:

“Mikataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa Dowans Holdings S.A) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya serikali ya maisha bora kw akila Mtanzania.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Pamoja na kutoa taarifa ya utekelezaji wa Azimio hili, napenda kueleza kuhusu hali ilivyo sasa kwa Mikataba baina ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Power Rental.

(i) Mkataba baina ya TANESCO na IPTL

Mgogoro uliopo sas akati ya TANESCO na IPTL unatokana na kutokubaliana kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha capacity charge kinachotozwa na IPTL.

Kwa mujibu wa Mkataba wa kuuziana umeme kati ya IPTL na TANESCO, capacity charge inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji (eguity) wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31 uliopaswa kuwa umewekezwa (ambao ni US $ 36.54 milioni) wakati IPTL wanaanza kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO tarehe 15 Januari, 2002. hata hivyo kufuatia uchunguzi uliofanywa na TANESCO imegundulika kwamba mtaji halisi wakati IPTL inaanza kuzalisha umeme ulikuwa shilingi hamsini elfu tu (50,000/=). Hivyo, mtaji huu ndiyo unaostahili kutumika kukokotoa capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

Kwa mantiki hiyo, madai ya TANESCO na Serikali katika mradi huu ni kuwa capacity charge inayotozwa na IPTL izingatie kiwango halisi cha mtaji (equity) uliowekezwa na IPTL na si zaidi ya hapo. Aidha serikali na TANESCO inadai kutoka IPTL kiasi chote cha malipo kilichofanywa kimakosa kama capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

Kutokana na Serikali kutoridhika na kiwango cha malipo ya capacity charge chini ya mradi huu wa IPTL, ilisitisha malipo kwa IPTL; jambo ambalo lilipelekea IPTL kufungua Sauri la Madai dhidi ya TANESCO kwenye Mahakama ya New Cork Nchini Marekani mwezi Novemba 2007. mnamo mwezi Aprili 2008 Serikali ilishinda Sauri hilo baada ya Mahakama hiyo kutupilia Mbale Sauri hilo na kuelekeza kwamba mgogoro huo uwasilishwe kwenye Baraza la Usuluhishi (Arbitration) kama Mkataba baina ya pande mbili unavyoelekeza.

Tarehe 9 Julai, 2008 IPTL iliwasilisha mgogoro huu kwenye Internacional Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Kwa sasa shauri hili bado halijatolewa uamuzi.

Hata hivyo, serikali imejiandaa ipasavyo kutetea na kulinda haki zake chini ya Kamati Maalum ya Serikali iliyoundwa kushughulikia mgogoro huu. Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo maalum ni Wakili wa Kujitegemea, Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Hivyo, Mkakaba huu tayari umekwishapitiwa na Kamati husika na mapungufu yake yaliyobainika ndiyo yamepelekea kuwepo kwa shauri hili.

(ii) Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND (ulioridhiwa na DOWANS)

Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006, Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya Mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Wanasheria waliobobea katika masuala ya Mikataba ya Kimataifa wa Kampuni ya REX ATTORNEYS. Uchunguzi wa REX ATTORNEYS ulibaini pamoja na mambo mengine kwamba;

(a) Utaratibu mzima wa manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia Mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2004;

(b) Kutokana na ukiukwaji huo, Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC, haukuwa halali na hauna nguvu kisheria; na,

(c) Vilevile, hata kama Mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji (assignment) wa mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya Richmond Development Company LLC kwenda DOWANS HOLDINGS S.A. na hatimaye Dowans Tanzania Limited haukuwa halali.

Kwa kuzingatia mapungufu hayo yaliobainishwa katika Mkataba huo serikali iliamua kusitisha huduma za Dowans Tanznaia Limited kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

(iii) Mkataba baina ya Tanesco na Aistom Power Rentals (APR)

Kama nilivyoelezwa na WAziri wa Nishati na Madini William Ngeleja wakati akiwaslisha hotuba yake hapa bungeni tarehe 8 Julai 2008, katika mkutano huu wa Bunge lako tukufu alifafanua kuwa mitambo ya Alstom Power Rentals ilikodishwa na Tanesco kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe 20 Machi 2007 hadi tarehe 19 machi 2008. baada ya ya muda wa mkataba huo kumalizika serikali haikuhuisha mkataba huo licha ya jitihada za wahusika kutaka uhuishwe.


iv) Mkataba baina ya Tanesco ya AGGREKO

Mkataba baina ya Tanesco na Aggreko ulianza kutekelezwa mwezi Desemba 2006 na unatarajiwa kumalizika mwezi Novemba 2008. Kamati ya Serikali ya Wataalam inapitia mkataba huu ili kujiridhisha kama upo kwa maslahi ya taifa na kuchukua hatua kadri itakavyoonekana inafaa.

v)Mkataba baina ya Tanesco na SONGAS

Kwa sasa mkataba mkubwa wa Sekta ya Nishati ambao unapawa kupitiwa upya ni baina ya Tanesco na Songas. Mkataba wa Songas unahusisha wadau wengi na unajumuisha mikaaba midogo mbalibmali ipatayo ishirini na moja inayohusu masuala ya utafutaji, usambazaji, ununuzi na mikopo ya uendelezaji wa gesi asilia na hivyo kuwa na uzito wa aina yake (Complex). Ili kuwa na tija katika mapitio ya mikataba hiyo na kupata ushauri mzuri, serikali inaendelea kushauriana na wataaalam washauri waliobobea katika sekta hiyo ya gaesi asilia wakiwemo wanasheria ambao wataweza kushauri ipasavyo iwapo kuna mapungufu yoyote yanayostahili kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya taifa.

AZIMIO NAMBA 4:
“Serikali itathmini uya uhalali wa kuwepo Mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLC (Sasa Dowans Holdings S.A) kwa lengo la kusitisha mlipo kwa Dowans Holdings S.A na kuvunja mkataba huo haraka iwezekanavyo.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Kama nilivyoeleza awali kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa mkataba baina ya Tanesco na Richmond uliorithiwa na Dowans , Serikali imesitisha mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008. vile vile Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na mkataba huo.

AZIMIO NAMB 5:
“Kwa kuwa mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLS (Sasa Dowans Holding S.A) umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalam katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali; Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakili wa serikali Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, wawajibishwe na mamlaka juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.”


HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
I) Kikatiba Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mshauri mkuu wa Serikali katika masuala yote ya sheria za nchi. Hivyo ana wajibu mkubwa wa kuishauri serikali katika maeneo ambayo anaona yanakiuka Sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Kutokana na nafasi yake kikatiba, mamlaka yake ya nidhamu ni mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo mwanasheria mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba hao linashughulikiwa na ofisi ya Rais Ikulu

Kuhusu Wakili wa Serikali Donald Chidowu ambaye aliukwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya majadiliano (GNT) akimwakilisha mwanasheria mkuu wa Serikali, amepelekwa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia misingi ya kanuni asilia ya haki ya kusikilizwa kwanza (natural justice) na kuzingatia Sheria za Utumishi wa umma.

Mtumishi huyu amewasilisha utetezi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria ya sheria na katiba ambaye ndiye Mamlaka yake ya nidhamu katika muda wa siku 14 zilizotakiwa. Hivi sasa maelezo ya utetezi wake yanafanyiwa uchambuzi wa mamlaka yake ya nidhamu ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

AZIMIO NAMBA 6:

“Katika kushughulikia mikataba yote na makampuni ya nje, Serikali ihakikishe kuwa wakala wa usajili wa biashara na Leseni (Brela) inatumika kikamilifu kupat aaarifa kamili za makampuni haya. Aidha ofisi zetu za ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi na vile vile katika kuyachunguza makampuni hayo kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya Serikali, kabla ya kuingia mikataba husika.”


HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Serikali imetafakari na kuzingatia kwa makini pendekezo hili. Hatua zilizoanza kuchukuliwa ni pamoja na zifuatazo:

i) Kuanzia sasa balozi zetu zote za nje zitakuwa zinashirikishwa kikamilifu katika kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kwa makampuni ya nje ambayo Serikali inatarajia kuingai nayo mikataba katika manunuzi ai katika miradi mikubwa. Serikali imeshato amaelekzo haya kwenye wizara zote. Aidha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataif anayo imetoa maelekezo kwa balozi zetu zote ili zizingatie uamuzi huu.

ii) kama ilivyoelezwa katika Azimio namba moja, serikali itawasilisha mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ili kuongeza kifungu kinachohusu kufanya uchunguzi wa kina wa wazabuni wa ndani na nje ya nchi wanaoomba kuingia mikataba na Serikali. Miongoni mwa mapendekezo haya ni pamoja na kuwa na kamati huru ya awataalam itakayofanya uchunguzi huu wa kina pale itakapobidi.

iii) katika kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inatumika ipasavyo katika masual ya manunuzi ya umma PPRA tayari imeanzisha mfumo wa habari na mawasiliano katika manunuzi ya umma ujulikanao kama procurement information system. Ni matumaini ya Serikali kuwa mfumo huu utatumika kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za manunuzi kati ya mamala yaani PPRA na taasisi za ununuzi.


AZIMIO NAMBA 7;

Wajumbe wote wa kamati ya Serikali ya majadiliano (Government Negotiation Team-GNT) ambao ni maafisa waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya umma kwa kulitia hasara taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika kushughulikia suala hili (yaani katika mchakato mzima wa zabuni pamoja na majadiliano ya mkataba baina ya Tanesco na Richmond kulikuwa na kamati za aina tatu.

Kwanza ni kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Johnson Mwanyika (mb) katibu Mkuu wa wizara ya nishati na madini Arthur Mwakapugi pamoja na akatibu mkuu wizara ya fedha na uchumi Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla

Kamati ya pili ilikuwa ni timu ya wataalamu (expert team) iliyokuwa na wajumbe na Taasisi zifuatazo:

1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)
2. Dk Lutengano Mwakahesya- Nishati na Madini (Mjumbe)
3. Theophilo Bwakea –Nishati na madini (mjumbe)
4. Stephen Mabada –Tanesco (mjumbe)
5. Athanas Mbawala –tanesco (mjumbe)
6. James Mwalilimo –Tanesco (Mjumbe)
7. Julius Sarota –Nishati na Madini (mjumbe)

Kamati hii ilikuwa na jukumu ya kutathmini wazabuni wote waliokuwa wameomba zabuni za mitambo ya kukodi ya dharura ya kufua umeme wa megawati 105.6.

Kamati ya tatu ni ile ya majadiliano ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development Company LLC. Wajumbe wa kamati hii ni:

1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)
2. Theophilo Bwakea –Nishati na madini(mjumbe)
3. Stephen Mabada –Tanesco (Mjumbe)
4. Godson Makia –Tanesco(Mjumbe)
5. Donald Chidowu –Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (Mjumbe)
6. Dick Tewa –Benki Kuu (Mjumbe)
7. Gideon Nassari –CTI (Mjumbe)
8. Julius Sarota –Nishati na Madini (Sekretarieti)
9. Mwita Wangwe –Tanesco (Sekretariet)

Kamati mbili za wataalam (yaani kamati ya pili na ya tatu) zote zilikuwa zinaripoti na kutoa ushauri kwa kamati ya makatibu wakuu wawili wa Hazina, na Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Azimio hili, wajumbe wote wa kamati hizi tatu wamepelekewa barua za kutakiwa watoe maelezo kwa mujibu wa Sheria zinazohusu nidhamu katika utumishi wao.

Hatua hii inazingatia Misingi ya Kanuni Asili ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuingiza Serikali katika mkataba unaonekana kutokuwa na maslahi kwa Taifa.

Maeneo hayo ni pamoja na:

(i) Kutotumia utaalamu na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalamu, kifedha na kuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya zabuni.
(ii) Kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa zabuni.
(iii) Wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development LLC uchunguzi wa awali (Due Diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya zabuni (post qualification)
(iv) Kutokuwa makini na hivyo kushinddwa kutambua udanganyifu wa ubia/ uhusiano wa kibiashara kati ya Richmond Development Company LLC na Pratty & Whitney
Watumishi wote wameshawasilisha utetezi wao katkka muda wa siku 14 zilizopangwa. Aidha, hivi sasa utetezi wao unafanyiwa uchambuzi wa kina na Mamlaka zao za nidhamu ili hatua muafaka zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala Utumishi wao.

Kwa upande wa watumishi wa Tanesco ambao ni Stephen Mabada, Athanas Mbawala James Mwalilimo, Godson Makia na Mwita Wangwe, Kamati Ndogo ya Nidhamu ya Bodi ya Tanesco tayari imekwisha pitia maelezo ya watumishi wao wote na mapendekezo ya kamati hiyo yamewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco ambayo itatoa maamuzi yake na kuishauri Serikali.

AZIMIA NAMBA 8:

“Waziri wa Nishati na Madini Mh. Nazir Karamagi (MB), aliyeshabikia sana uhaulishaji wa Mkataba kutoka kwa Richmond Development Company LLC kwenda kwa Dowans Holdings S.A awajibishwe,”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Nazir Karamagi (MB) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini alijiuzulu Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hatahivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kwa lengo la kutaka kujua kama kuna rushwa yeyote ambayo ilijitokeza katika mchakato huu inayomhusisha Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb), katika suala hili.

Taarifa ya uchunguzi huo itawezesha Serikali kuamua juu ya hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa dhidi yake.

AZIMIO NAMBA 9

“Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru awajibishwe kwa manufaa ya Umma na Maofisa wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya Umma”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Zoezi la kufanya uchunguzi lililofanywa na Takukuru lilihusisha watumishi wafuatao:

(i) Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea akiwa ndiyo msimamizi mkuu wa Takukuru, iliyohusika na uchunguzi wa mchakato wa mzima wa zabuni ya umeme wa dharura, ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC.
(ii) Mkurugenzi wa Upelelezi, Alex Mfungo ambaye ndiye alisimamia zoezi zima la uchunguzi na kuandaa ripoti ya uchunguzi ya Takukuru kuhusu suala hili.
(iii) Maofisa wanane wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa taarifa katika maeneo yao ya utaalamu katika mchakato mzima wa Zabuni ya ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC
Ili kutekeleza azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi. Vilevile wasaidizi walio chini yake walioshiriki katika zoezi hilo nao wametakiwa kutoa maelezo yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru ambaye ndiye mamlaka yao ya Nidhamu. Hii ni kuzingatia Misingi ileile ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice).

Hatahivyo kwa kuzingatia mazingira ya shauri hili, Katibu Mkuu Kiongozi ataamua juu ya utaratibu mzuri wa hatua za nidhamu dhidi ya wasaidizi wote wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru waliohusika katika suala hili.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi Mkuu na Wasaidizi wake wamepelekewa barua wajieleze ni yafuatayo:

(i) Kushindwa kuona kuwa taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Wataalamu wa Taasisi yake haikubainisha kuwepo kwa kasoro nyingi zilizokuwepo katika zabuni hiyo kama zilivyoainishwa katika Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge.

Badala yake Takukuru iliona kwamba: Mchakato mzima ulizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali.



*Hayakuwepo mapungufu makubwa katika zabuni
*Hakukuwa na hasara kwa taifa kutokana na zabuni hii.

(ii)Kushindwa kuona kuwa ushauri uliotolewa na PPRA kwa TANESCO kuhusu muda wa kutangaza zabuni kimataifa ulipuuzwa na hivyo kuvunjwa kwa taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 na hivyo kutia shaka.

Hivi sasa watumishi wote tisa wameshawasilisha utetezi wao katika muda uliopangwa. Aidha kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma, Mamlaka yao na nidhamu inapitia utetezi wao ili kutoa uamuzi unaostahili.

AZIMIO NAMBA10

“Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada)US$4,865,000) yaliyofanywa kwa Dowans Holdings A.S iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Wizara ya Fedha na Uchumi na Benki Kuu ya Tanzania wamechunguza na kuona kuwa malipo ya US$4,865,000 yaliyolipwa kwa kampuni ya Dowans Holdings S.A iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC ni halali. Malipo hayo yalilipwa tarehe 2Februari 2007 ikiwa ni gharama za ndege za usfairishaji wa mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura baada ya kupokea invoice Na.EFD786675.Uchunguzi unaonyesha kuwa, taratibu zote za malipo zilifuatwa na malipo yalifanywa baada ya kuhakikiwa na TANESCO, wizara ya Nishati na MAdini na HAZINA baada ya kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kwamba yanawiana na mkataba husika.

UK. 17

AZIMIO NAMBA 11

“Shetia ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995(The Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakan, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya BUnge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

(i)Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Jakaya Mrishi Kikwete katika Hotuba yake tarehe 21 Agosti 2008 wakati akilihutubia Bunge lako Tukufu kwamba, serikali inayo dhamira ya dhati ya kuangalia namna ya kutenganisha shughuli za biashara na uongozi katika Utumishi wa Umma katika ngazi za juu za viongozi na watendaji waandamizi. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imeanza mchakato wa kushughulikia suala hili na tayari wamewasilisha mapendekezo yao ya awali serikalini.

(ii)Hivi sasa serikali imeunda Timu inayojumuisha wajumbe kutoka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchunguzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na TAKUKURU ili kufanya uchambuzi zaidi wa mapendekezo hayo. Aidha, Timu hiyo itafanya uchambuzi wa Sheria za Nchi zilizofanikiwa kuweka utaratibu wa viongozi wa Umma kuweza kutenganisha shughuli za biashara zao na uongozi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi.

(iii)Katika zoezi hili, wananchi na wadau mbalimbali watashirikishwa kikamilifu ili kupata maoni yao.

(IV) Baada ya hatua hizo serikali inatarajia kuwasilisha hapa bungeni marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma mwezi Aprili 2009.

UK18.

AZIMIO NAMBA 12
“Serikali ijiepushe kadri inavyowezekana na uataratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa Umma na kuhakikisha kuwa Wizara zote zina taarifa za bei halisi za mahitaji yao kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Katika utekelezaji wa Azimio hili, wizara zote, wakala na idara za serikali zinazojitegemea. Mikoa pamoja na mashirika ya umma zimeagizwa kuzingatia kikamilifu taratibu za manunuzi na ugavi kama zilivyoanishwa katika Sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Pamoja na maelekezo hayo hatua zifuatzo zitachukuliwa:

(i)Serikali imeamua kuwa kila inapowezekana taasisi za ununuzi zinunue vifaa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa hizo, ikibidi kununua kutoka kwa wakala walioidhinishwa ni lazima taratibu za manunuzi ya umma zizingatiwe kikamilifu.

(ii)Katika hatua za awali, Wizara ya Fedha na Uchumi inaandaa utaratibu wa kufanya ununuzi wa pamoja wa bidhaa zinazoweza kutumika na taasisi zaidi ya moja(common use items). Utaratibu huo utakapokamilika utawezesha bidhaa hizo kuagizwa kwa pamoja kupitia wakala wa serikali wa huduma za ununuzi na endapo itabidi kununua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji kwa lengo la kupata unafuu wa bei.

(iii)Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma tangu mwezi Juni 2008, imempata mtaalamu mwelekezi wa kuandaa mfumo wa ununuzi wa pamoja na kupata takwimu za bei. Dira za bidhaa mbalimbali(indicative Price) kutoka kwa wazalishaji wa bidhaa na huduma. Kazi hiyo itakamilika mwezi Septemba 2008. takwimu hizo zitawekwa katika mtandao wa Mamlaka na kwenye matoleo ya Jarida la Masuala ya Ununuzi Tanzania ili ziweze kutumiwa na taasisi za ununuzi pamoja na Wazabuni. Bei hizo zitafanyiwa mapitio ya mara kwa mara na PPRA.

UK 19

AZIMIO NAMBA 13:
“Serikali izihusihe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba mikataba ya kibiashara ni siri, hata kwa walipa kodi wenyewe. Aidha, serikali ihakikishe kuwa Kamati zote za bunge zinapitia mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu chini ya sekta zao ili kuliondolea taifa mizigo isiyo na lazima.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Tarehe 24 Aprili 2008, Ofisi ya Waziri Mkuu ilimwandikia narua Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumfahamisha kuhusu utekelezaji wa awali wa baadhi ya maazimio ya Kamati Teule yaliyopitishwa na Bunge katika narua hiyo, utekelezaji wa maazimio Namba13, 15, 16, 21 na 23 yaliyotolewa taarifa. Hata hivyo, kwa madhumuni ya taariga hii ninapenda kurejea kwa muhtasari maelezo kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo.

Kuhusu Azimio Na.13, serikali imechambua Azimio hili kwa kina na imekubali kimsingi kwamba, mikataba yote muhimu ya serikali itakuwa inawekwa kwenye maktaba maalum ya bunge ili kamati za Bunge lako Tukufu ziweze kupata nafasi ya kupitia mikataba mikubwa ya kibiashara nay a kuda mrefu chini ya sekta zao na kushauriana ipasavy.

Kuhusu kuzihusisha Kamati za kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maanalizi ya mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu, serikali imeanza kufanya tafiti katika mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ili kupata uzoefu zaidi utakaosaidia katika utekelezaji wa suala hili.


“Waziri wa Nishati na Madini Dkt Ibrahimu Msabaha(MB) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kw amakusudi kwenye mkataba wa Kampuni ya Mfukoni.

Aidha Kamishna wa Nishati nNdugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri katibu mikuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company (LLC) ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye mradi wa bomba la mafuta.

Ndugu Mrindoko ndie aliyeandika barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA.

(a)Mheshimiwa Dkt Ibrahimu Msabaha(Mb) aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alijuzulu mwezi Februali 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili.

Hata hivyo kwa lengo la serikali kujidharisha zaidi kuhusu ushiriki na ushauri wake katika msual ahili, Vyombo vya dola vinaendelea kkuendesha uchunguzi wa kina.

Lengo ni kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote inayomhusisha Mheshimiwa Dkt Ibrahim Msabaha(Mb) ambayo ilijitokeza katika mmachakato huu ili hatimae uamuzi stahiki dhidi yake uweze kuchukuliwa.

(b) Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw Arhtur Mwakapugi ambae alikuwa miongoni mwa wajumbe watatu wa kamatio iliyoundwa na Katibu Mkuu Fedha na Uchumi, Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye amepewa barua ya kutakiw akujieleza katika maeneo ambayo kamati ya bunge ilibaini kuwa hakuyazingatia kwa maslahi ya taifa.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa sheria na ikanuni za nidhamu katika utumishi wa ummaa na misingi ya kanuni Asilia ya haki ya kusikilizwa kwanza (Natural Justice)
Kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Badahi ya maeneo ambayo katibu mkuu ametakiwa kujieleza ni kama yafuatayo: (1) Kutozingatia maagizo ya baraza la Mawaziri kuhusian ana suala la ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura.

(11) Kutozingatia ushauri wa kitaalam ukliotolewa na PPRA kuhusu kufuata sheria ya manunizi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005.

(111) Kutoishauri Serikali ipasavyo kuhusu umuhimu kuifanyia uchunguzi zaidi kampuni ya Richmond Development Company (LLC) ili kujidhihirisha na uwezo wake kifedha kiutendaji, kiutaalamu na kiuzoefu ili kulinda maslahi ya Taifa.

Hivi sasa Mamlaka yake ya nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi inafanya uchambuzi wa maelezo yake aliyoyawisilisha ili hatiame maamuzi yatolewe kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi.

Azimio Namba 15.
“Utaratibu wa kuteua Wakurugenzi wa Makamisha katika Wiazarta kuwa Wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa Mashirika yaliyo chini ya Waizara zao unazua mgongano wa kimaslahi na kudhoofisha usimamzi pamoja na uwajibikaji, hivyo serikali iupige marufuku mara moja”

Hatua zilizochokuliwa.

Ni ukweli Kuwa huenda katika baadhi ya maeneo mfumo huu wa uteuzi wa Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe wa Bodi za Mashirika ya umma unaweza kuwa na matatizo.

Hata hivyo baada ya seriklai kuzingatia Azimio hili imeona pia kwamba zipo pia faida za baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe wa bodi hasa katika kusaidia kutoa msimamo na ufafanuzi wa sera na mipango mbalimbali ya serikali.

Kwa kuzingatia umuhimu huo seriklai ianona ni vyema utaratibu huo uendelee lakini kila bodi itaangaliwa kipekee pale itakapodhihirika kuwa ni maslahi ya taifa kuwateua baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe katika baadhi ya bodi serikali itafanya hivyo kwa maslahi ya taifa letu.

AZIMIO NAMBA 16.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na uongozui wa Nchi kw aujumla, ni wajibu wake yey mwenyewe kupima uzito wa amtoeko ya uchunguiz huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge, vilevile ni wajibu Ibara ya 51 ya katiba kuangalia kama matokeo ya uchunguzi huu hayataathiri hadhi na uzito wakle nadni ya Bunge”

HATUA ZILZIOCHUKULIWA.

Serikali imefanya uchunguzi juu ya usajili wa Kampuni ya Richmond Development Company(LLC) pamoja na Richmond development Company Tanzania (LLCT) ili kubaini uhalali wake na kutaka kujidhihirisha kama usajili wake uliofanywa na BRELA ulikuwa kinyume cha sheria za Nchi Uchunguzi huo umebaini yafuatayo.

(1) Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited ili kubaini uhaklali wake na kutaka kujidhihirisha kama usajili wake uliofanyw ana BRELA ulikuwa kinyume cha Sheria za nchi uchunguzi huo umebaini yafuatayo.
(2) Kampuni ya Richmond Development Company(T) Limited ni kampuni iliyosajiliwa na BRELA hapa Tanzania terehe 12 Julai 2006 na kupewa Certificate of Incorporation Namba 57014 ili kuiwezesha kupatiwa leseni ya biashara ya uzalishaji wa umeme na Masoko unaonyesha kuwa Richomond Debvelopemnt Company (LLC) haikuwa imesajiliwa na BRELA.


(ii) Hakuna taarifa ndani ya BRELA zinazoonyesha kuwa Richmond
Development Company LLC iliyoshinda zabuni husika, ilikasimu
jukumu lake la kuzalisha umeme wadharura kwa Richmond Development
Company (T) Limited ambayo ndiyo ilisajiliwa Nchini kwa kusudio hilo.

(iii) Kutokana na utata huo uliojitokeza , Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ametoa ushauri juu ya Mamlaka ya BRELA Limited kwa kuzingatia
Sheria ya Makampuni (Sura ya 212) ,Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha
215 cha Sheria hiyo, BRELA imekwishatoa motisi ya siku thelathini
kwa Kmapuni ya Richmond Development Company (T) Limited
kuwasilisha utetezi wake kabla ya hatua za kuifuta kampuni hiyo
kuchukuliwa .Taarifa hiyo ya notisi iliyotolewa na BRELA haijajibiwa.

AZIMIO NAMBA 18.
“Wamiliki wa Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd wafunguliwe kesi ya jinai mara moja kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia Serikali”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Awali, Serikali ilimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa makini Taarifa za Kamati Teule ya Bunge pamoja na kumbukumbu zote za Mjadala wa suala hili Bungeni ,ili kubaini maeneo yenye Makosa ya Jinai ambayo yangewezesha Serikali kuwafungulia mashtaka Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richomond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao.

Baadhi ya maeneo ambayo yaliangaliwa ni pamoja na

(a) Kampuni ya Richmond Development Company LLC kuwasilisha taarifa za udanganyifu Serikalini kwamba wanauwezo wa kifedha,kiutendaji na utaalam katika kuzalisha umeme jambo ambalo halikuwa kweli.

(b) Kuwasilisha Hati na Vielelezo vya udanganyifu kwa Kamati ya Serikali na Mjadiliano kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ina Mkataba wa Ubia (Consortium Agreement )baina yake na Kampuni ya Pratt& whitney ambayo inajulikana kuwa na uwezo mkubwa Kimataifa

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishauri kuwa pamoja na mambo mengine ipo haja kwa Serikali

(i) Kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kuwa Kampuni ya Richmond
Development Company LLc haina uhai wa kikampuni (Corporate
Peronality ) na hivyo kujiridhisha kuwa mambo yote yaliyofanywa kwa
jina la Kmapuni hii, yalikuwa batili.Hii ni kwa kuzingatia fungu la 320 la
sheria ya Makampuni (Sura ya 212).

(ii) Kufanya uchunguzu wa kina katika makosa yanayoonekana kuwa ya jinai kwa watu waliohusika katika uwasilishaji wa baadhi ya nyaraka na vielelezo vingine vya udanganyifu vilivyowezesha Kampuni ya RICHMOND kupata ushindi wa Zabuni hii.

(iii) Kwakuwa Makosa ya Jinai hupelelezwa na Polisi ,TAKUKURU , Mamlaka ya Mapato na Vyombo vingine ambavyo vimepewa Mamlaka hayo kisheria , serikali iagize Vyombo hivyo vya Dola vilivyopewa Mamlaka ya kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi vifanye kazi hiyo.Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai (The Criminal Procedure Act Cap.20.R.E 2002).

Lengo la zoezi hili ni kijiridhisha na kupata umweli na ushahidi wa kurtosha unaoweza kupokelewa na kukubalika Mahakamani kwa kuzingatia masharti ya sheria ya ushahidi (The Evidence Act cap 6.R.E.2002)

Hivyo hivi sasa Vyombo vya Dola ikiwemo Idara ya Polisi vimepewa kazi hiyo na vinaendelea kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina wa nyaraka na hati mbalimbali zilizowasilishwa na wahusika kabla ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni na Taratibu zilizopo.

AZIMIO NAMBA 19:
“Serikali ichukue hatua za kuvinoresha na kuvitumia ipasavyo Vitengo vya Utabiri wa Hali ya Hewa na Kitengo cha Maji –TANESCO ili kuepusha Nchi na Maamuzi ya zimamoto, ambayo uzoefu unaonyesha yanaiingiza Nchi kwenye hasara kubwa”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hatua zifuatazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kama mkakati wa utekelezaji wa Azimio hili:
(i) Serikali imeanza kuimarisha Wakala wa hali ya Hewa Nchini kwa kutoa mafunzo na kuwapatia vifaa vya kisasa kama kompyuta, vifaa vya kupimia mvua na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya mawasiliano nay a kuchambua takwimu za hali ya hewa.mfano, hadi sasa Serikali imekwishanunua mitambo ya mawasiliano ya kisasa iitwayo Retin 4 na Snergie kwaajili ya kuimarisha Utabiri wa hali ya Hewa Nchini.

(ii) Kuhusu ushirikiano baina ya Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na TANESCO pamoja na Mabonde ya Maji ni mzuri, kwani kila siku TANESCO inapokea Taarifa za utabiri wa hali ya mvua na kuziingiza katika Takwimu za Msingi9( Data base) zinazoonyesha Mfumo wa uzalishaji umeme wa kila siku.

(iii) Vilevile ,serikali kupitia Mradi wa Maendeleo sekta ya Maji (Water sector Development program) itaimarisha Ofisi za mabonde ya maji ili kuwezesha upatikana wa taarifa muhimu kwa Vitengo vya mai vya TANESCO>Hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Watumishi na kukunua zana za kufanyia kazi kama vile magari na vifaa vya kupima kina cha maji, na wingi wa maji kwenye mito na mabwawa. Vifaa vingine ni vya kupimia mvua, maji nchini ya ardhu ,kupima ardhi na kuanzisha Mtandao wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta

AZIMIO NAMBA 20:
“Serikali iendeshe uchunguzi maalumu ili kubaini ukweli kama Taarifa rasmi ya TAKUKURU iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond lilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine na kama jalada halisi linalohusu Kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa lingine kwa lengo la kuficha ukweli”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwakushirikiana na Vyombo vingine vya dola wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu suala hili.

AZIMIO NAMBA 21:
“Ofisi ya Bunge ianzishe Mktaba Maalum itakayohusika na utunzaji wa Mikataba yote uinayoingiwa na Serikali”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali inakubali utaratibu huo na itatoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa Azimio hili kama nilivyoeleza katika Azimio Na.13.

AZIMIO NAMBA 22
“Miswada yote inayowasilishwa Bungeni hasa Miswada ya umeme na Mafuta, (The electricity Bill, 2007 na Petroleum Supply Bill, 2007) izingatie changamoto zilizoonekana wakati wa mjadala wa taarifa ya kamati Teule”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Miswada ya Sheria ya Umeme na ule wa Sheria ya mafuta ilijadiliwa bungeni mwezi Aprili 2008 na kupitishwa. Wakati wa Mjadala huo, ushauri uliopo katika Azimio hili ulizingatiwa kikamilifu.

AZIMIO NAMBA 23:

“Serikali iyafanyie kazi mapendekezo ya kamati teule na kuliarifu Bunge kuhusu utekelezaji wake ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15/2?2008.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Hali halisi inaonyesha kuwa, jitihada zimefanywa na Serikali kuhakikisha Maazimio ya Bunge yanatekelezwa ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15 februari 2008. Muda huo uliisha tarehe 14 Mei 2008. Hata hivyo, katika utekelezaji, imedhihirika kuwa baadhi ya Maazimio yanayohitaji muda mrefu kukamilisha mchakato wake wa utekelezaji hasa yale yanayohusu marekebisho ya Sheria na mifumo mbalimbali ndani ya serikali na pia yale yanayohitaji kufungua mashtaka ya jinai au mashtaka ya makosa ya nidhamu.

HATUA ZA NIDHAMU KWA WATUMISHI:

7. Mheshimiwa Spika, kabla ya kumalizia naomba kutoa angalizo kwamba , katika kushughulikia suala hili, kamati Teule ya Bunge katika baadhi ya Maazimio yake yanayohusiana na kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya watumishi wa Umma waliohusika katika mchakato mzima wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, imetumia maneno mbalimbali kama ifuatavyo:

AZIMIO NAMBA 5:

“…Wawawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu.”

AZIMIO NAMBA 7:

“…Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma…”.

AZIMIO NAMBA 9:

“… wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.”

AZIMIO NAMBA 14:

“…Wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni,”

8. Mheshimiwa Spika, katika kutafsiri maana ya maelekezo haya, Serikali imeona kwamba yanaweza kuwa na maana ya kushtakiwa Mahakamani kwa Makosa ya Jinai; ama kutumia Mamlaka ya Rais ya kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma; ama kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa Umma na kanuni zake.

Serikali baada ya kutafakari kwa kina suala hili, imeona kuwa katika mazingira ya suala hili, ni busara kutumia utaratibu wa hatua za mashtaka ya nidhamu chini ya sheria ya Utumishi wa Umma. Utaratibu hu ni mwepesi na unaweza kusimamiwa kwa haraka zaidi lakini bila ya kuathiri misingi ya Haki Asilia(Natural Justice) ya mtu kupewa haki ya kusikilizwa kwanza. Hii ni hatua muhimu sana kwani hata chini ya Mamlaka ya Rais ya kumstaafisha Mtumishi kwa manufaa ya umma, taratibu zinataka mtumishi apewe fursa ya kutoa maelezo ya kutetea kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Hii inatuondolea hatari ya serikali kushtakiwa kwa kutofuata sheria, Kanuni na taratibu kama ilivyowahi kutokea huko nyuma ambapo baadhi ya viongozi na watendaji walistaafishwa kwa manufaa ya umma kimakosa, na baadaye serikali ikalazimika kuingia gharama kubwa ya kuwalipa fidia. Vilevile, hatua hii inaipa nafasi serikali kupitia utetezi utakaotolewa kuona ni watumishi gani wanaoweza kustahili kushtakiwa kwa makosa ya jinai kwa mujibu wa Sheria za Nchi.

HITIMISHO:

9. Mheshimiwa Spika, napenda kusema kuwa yapo mambo mengi ambayo sisi kama taifa tumejifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mchakato wa zabuni ya mkataba baina ya Tanesco na Richmond, lakini pia na mikataba mingine. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha mfumo wa uwezo wetu wa ndani wa majadiliano ya mikataba hasa ile mikubwa ya kibiashara na kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ofisi yangu tayari imepata maoni ya wanasheria mbalimbali wakiwemo Mheshimiwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali staafu; Mheshimiwa Johnson Mwanyika-Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mheshimiwa Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini. Maoni yao yatatusaidia sana katika kuimarisha mfumo wa wetu wa majadiliano ya mikataba. Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru waheshimiwa wabunge hawa kwa maoni na ushauri wao mzuri sana.

Vilevile, nimepata nafasi ya kuzungumza na Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela, ambaye pia alinipa ushauri mzuri kuhusu namna mbalimbali za kui8marisha majadiliano katika mikataba baina serikali na vyombo vingine vya uwekezaji. Naomba kutumia fursa hii naye kumshukuru sana kwa mawazo yake.

Aidha, Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), tunaendelea kulifanyia kazi jambo hili. Serikali inatarajia kwamba jitihada hizi zitatuwezesha kubaini kwa kina mapungufu yaliyopo na kushauri njia bora zaidi za kuimarisha majadiliano yanayohusu mikataba.

10. Mheshimiwa Spika, mwisho natoa wito kwa watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa uadilifu, bidii, uzalendo na kuwa makini katika kila kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali. Kwa upande wake Serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa viongozi na watendaji wote katika ngazi zote za Utumishi wa umma wanafanya kazi kwa umakini na kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu.

11. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

(tamati).

Naambiwa huu ni wimbo mpya wa taifa, si mimi

WIMBO MPYA WA TAIFAThat is why we have a song to celebrate this....
Tanzaniaaa Tanzaniaaaa!
Nakupenda kwa moyo woooteee
Nchi yangu Tanzaniaaaa
Stori zako ni tamuu saanaaa!!
Nilalapo namwaza Vijisentiiii
Hujui kesho utakula nini weweeeeee
Tanzania Tanzania
Wakubwa Vijisenti wanabebana weweeeeeeeeeee
Tanzania Tanzania
Niamkapo Mkapa baba weee!
Tanzania Tanzaniaaaa
Nakupenda na EPA zakoooooo
Nakupenda kwa moyo woteeeeeee
TANZANIA !!! TANZANIA
The only country which its footballers play BUT do not win!!
The only country which Mzungu comes with one dollar and leaves with millions of them!!
The only country which its engineers build but the houses prematurely fall down!!
The only country with Politicians who believe in voo doo!!!
Attorney General!!
The only country where ufisadi is a Prestige!!!
The only country with many toothless TUMEz!!
The only country which its development is in Figures!!
But invisible!!
The only country where politicians are richest men!!
The only country where both English and Kiswahili Languagez iz a problem!!
AND THE ONLY COUNTRY which its PRESIDENT keeps on SMILING despite of national difficulties! !!
THE ONLY COUNTRY WITH HANDSOME PREZZIDAAA!! ! I REALLY LUV THIS COUNTRY!!

Miss Tanzania apata gari lake



Leo asubuhi kampuni ya simu ya mikononi iliyodhamini shindano la miss Tanzania 2008,Vodacom imekabidhi rasmi zawadi ya gari kwa mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreem Kalim.
Gari hilo jipya aina ya Suzuki Garnd Vitara lenye thamani ya sh Millioni 42 limekabidhiwa kwa mrembo huyo na meneja na meneja udhamini wa Vodacom Tanzania,Emillian Rwejuna.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi katika ofisi za Vodashop zilizopo mtaa wa samora jijini Dar na kushuhudiwa na maofisa wa Baraza la sanaaa,Kampuni ya LINO ambao ndio wanaadaaji wa shindano hilo,wadau wa sanaa na waandishi wa habari.
Akizungumza muda mfupi baada ya makabidhiano hayo,Rwejuna alisema Vodacom Tanzania,itaendelea kuboresha zawadi kila mwaka kwa washindi na washiriki,amesema kuwa ni matumaini ya Vodacom Tanzania kwamba zawadi hiyo ya gari ambayo amekabidhiwa itasaidia kurahisisha utendaji na shughuli mbalimbali za kijamii za mrembo huyo.
Rwejuna amesema kuwa sehemu wajibu wa Vodacom Miss Tanzania ni kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,shughuli ambazo kwa kiwango kikubwa zina mlazimu kusafiri,hivyo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba Vodacom Miss Tanzania anakuwa na usafiri wa kuaminika

Filamu ya Maisha ya bi kidude yapata tuzo




AS OLD AS MY TONGUE, THE MYTH & LIFE OF BI KIDUDE wins international award at Festival du Film Insulaire .


Each year since 2000, the French Island of Groix in Brittany has hosted the ‘Festival du Film Insulaire’, a competitive documentary event showcasing films from islands around the world.


The Lucien Kimité prize is awarded each year to the “most human” documentary in competition.


We are very proud to announce that our début feature documentary As Old As My Tongue won this year’s award.


With members of the production team currently scattered far and wide from Japan to Zanzibar and Cumbria to Cork, we invited our Zanzibari translation expert, Said el Gheithy of the Centre for Africa Language Learning to attend the festival.


As Old As My Tongue has now screened in more than 50 venues in 22 countries, winning 4 main awards and 4 further ‘best of the festival’ selections from juries and audiences.

ScreenStation [UK] is currently putting the finishing touches to a limited edition DVD of the film to be released in the UK on October 27th.


The UK release will be followed by a US and North America launch at the New York African Diaspora Film Festival in December. European launch is set for Cannes in January and last but not least, we return to Zanzibar for an African version at Sauti za Busara music festival in February 2009.

Ripoti ya Richmond, Hosea yuko katika matata


Waziri Mkuu ametekeleza ahadi yake na ametoa ripoti ya Richmond na wengi wetu tunaisubiri. Inaelekea watu wameshughulikiwa inavyostahili zinasubiriwa hatua za juu zaidi.Hosea anatakiwa kujieleza yeye na wasaidizi wake.
mwanasheria mkuu naye yumo.
Waliohusika katika mchakato wa ununuzi wamo.
Utaratibu wa prokuamenti umebadilika.
Tukipata ripoti kamili tutaitandaza hatuna maoni sisi ila nyie muone. Pichani Waziri Mkuu akihutubia bungeni kuwasilisha utekelezaji wa ripoti.
Lukwangule msimbe

TATHMINI YA MIAKA 10 YA BEIJING

TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME
P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286 Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244, Email info@tgnp.org, web www.tgnp.org


UZINDUZI WA MACHAPISHO: TATHMINI YA MIAKA 10 YA BEIJING: Mapendekezo kwa ajili ya Ushawishi, Utetezi na Mjadala wa Umma, NA HALI HALISI YA KIJINSIA TANZANIA:Kuimarisha Usawa wa Kijinsia,

TAARIFA KWA UMMA
Leo tunakutana katika mfululizo wa Semina za Kila Jumatano kuzindua rasmi chapisho la Hali Halisi na tathmini ya madai ya Miaka 10 ya Beijing.Huu ni uchambuzi mbadala wa hali ya mahusiano ya kijinsia Tanzania na mabadiliko muhimu yanayotakiwa katika kufanikisha ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia.

Kwanini taarifa hii ni muhimu?
Watanzania wamekanganyikiwa sana juu ya taarifa tofauti kuhusu hali ya kiuchumi na hali ya maisha ya watu, nyingi ya taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na serikali yenyewe, wafadhili vyama vya kiraia na watu binafsi..Ni hivi karibuni tu ambapo serikali imeelezea hali yake ilivyo kiuchumi, uchambuzi uliotolewa kupitia Bunge kuwafikia wananchi wa Tanzania. Taarifa hii ilidondoa vipengele vya mafanikoio kama vile kukua kwa uchumi katika eneo la uuzaji bidhaa nje ya nchi na kuongezeka kwa ajira. Kwa mujibu wa serikali na makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii yetu, kadhalika imeetaarifiwa kuwepo kwa hatua na mikakati madhubuti kuzingatia suala la jinsia katika sekta zote za serikali.

Hata hivyo tunaamini kwamba ni muhimu kwa wanaharakati wa masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kufanya tathmini yao juu ya hali halisi katika ngazi zote kwa kutumia mtazamo wa wanawake na wasichana kadhalika na makundi mengine yaliyo pembezoni/yaliyosahaulika. Pamoja na kufanya tathmini hii pia ni muhimu wanaharakati kufuatilia jinsi serikali inavyotekeza mikakati na sera zake. Hatma ya maazimio na mapendekezo ya semina hii itasaidia katika tafakari ya vipaumbele ambavyo ni tofauti na vile vilivyopo vya sasa vya uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika sera, utekelezaji na tathmini, kukosoa mfumo kiritimba uliopo, na kuweka mkakati wa kushinikiza hatua za utetezi na ushawishi.

Mnamo mwaka 2003, TGNP ilifanya uchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa mikakati ya maazimio ya kongamano la Dunia la Wanawake lililofanyika Beijing China mwaka 1995. Uchambuzi huu ulifanywa kwa niaba ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Tanzania. TGNP ilishirikisha pia wadau wengine miaka ya 2005 na 2006, na kupeleka madai na mapendekezo 15 madhubuti, ambayo yanazinduliwa leo hii a yakijulikana kama, Tathmini ya Miaka 10 ya Beijing: Mapendekezo kwa ajili ya Ushawishi, Utetezi na Mjadala wa umma. Madai haya yanagusia maeneo kama vile masuala ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia, elimu, afya, uchumi, siasa na haki za wanawake.

Wakati huo huo, Mtandao wa Jinsia(TGNP) mnamo mwaka 2006 ilitoa chapisho la kiingereza lilijulikana kama Gender Profile of Tanzania 2006: Enhancing Gender Equity kwa msaada wa SIDA (Sweden), lililozinduliwa mwaka 2007 hapa katika semina hizi za jinsia na maendeleo (GDSS). Toleo la Kiswahili la Gender Profile sasa liko tayari, likiitwa, Hali Halisi Ya Kijinsia Tanzania:Kuimarisha Usawa wa Kijinsia. Chapisho hili linadondoa hitaji la kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi, katika suala zima la mahusiano ya jamii, masuala ya kisiasa na sheria kwa ujumla ili kufanikisha ukombozi wa wanawake na usawa na haki kijinsia. Katika chapisho hili chambuzi yakinifu umefanyika katika sera na mifumo ya uchumi mkuu; muundo wa mageuzi kiuchumi; ubinafsishaji; na mifumo ya soko huria; ajira, mila na utamaduni; sheria; siasa; vyombo vya habari; huduma za jamii na hatimae kuangalia hali ya mtoto wa kike. Taarifa hii inahitimishwa kwa muhtasari wa mafanikio, changamoto na fursa zilizopo ili kufikia lengo la ukombozi wa wanawake na usawa wa jinsia katika ngazi zote.

Leo tunakutana hapa kuzindua machapisho haya mawili, na la muhimu zaidi, kuungana pamoja katika kupanga jinsi gani tunavyoweza kufanikisha aina ya mabadiliko tunayodai-katika maisha yetu ya kila siku kadhalika katika mashirika yetu na jamii nzima kwa ujumla. Masuala yaliyoibuliwa na madai yaliyomo si mageni, mengi yao yalijadiliwa katika mijadala wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) kila wiki, na hususan ile iliyojadili matarijio ya Bajeti ya 2008/09 tarehe 14 mwezi Juni 2008 na ile iliyofanyika baada ya hotuba ya Bajeti tarehe 18 Juni 2008. Wanaharakati wa ukombozi wa wanawake na usawa wa jinsia wanatoa mwito na wanadai hatua za utekelezaji sasa!

Semina jinsia na maendeleo ya leo tarehe 27 Augusti 2008 itatoa fursa kwa wana GDSS, wanaFemAct, wadau wa mitandao na makundi yote, na wadau wengine kwa ujumla kupanga mikakati ya utekelezaji kwa pamoja kwa ajili ya kujenga uwezo na ushawishi, ili kuhakikisha kwamba madai na mapendekezo yaha yanazaa matunda.

Kila mshiriki atapata nakala ya chapisho na fomu ya mrejesho, na tunawakaribisha katika hatua ya baadae kutusadia na taarifa ya jinsi ambavyo chapisho hili limetumika na jinsi mnavyojiwekea mikakati ya ya kusonga mbele na katika harakati za ushawishi (na jinsi gani mtazitumia nakala za ziada za machapisho haya) Nakala za ziada zitapatikana baada ya kuwa tumepokea fomu za mrejesho kutoka kwenu.

Imetolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)

………………………..
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji
Tarehe 27 Agusti 2008.

Wamasai wataka mapato zaidi ya utalii


Wajumbe wa Baraza la wafugaji wa jamii ya kimasai wanaoishi katika mamlaka ya hifadhia Ngorongoro (NCA) wametaka mapato yanayotokana na utalii yaelekezwe kuwanufaisha wenyeji wanaoishi katika mamlaka hiyo, taarifa ya Maelezo Arusha imesema.
Wametaka asilimia kubwa ya mapato hayo lazima yatengwe kuwanufaisha na kuwaendeleza wenyeji wanaoishi katika mamlaka hiyo ya Ngorogoro.
Wakijadili mapendekezo ya kuifanyia marekebisho sheria iliyoanzisha mamlaka hiyo mwaka 1959 wakati wa semina ya siku tatu liyoanza jana mjini Karatu wamesema sheria hiyo haijaweka wazi namna wenyeji hao wanaovyoweza kunufaika na mapato hayo.
Wajumbe wa baraza hilo la wafugaji wamesisitiza kuwa wenyeji jamii ya kimasai kwa zaidi ya miaka 48 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo wenyeji wa kimasai wanaoishi katika mamlaka hiyo bado wameendelea kuishi katika umaskini wa hali ya juu licha ya kuwepo na mapato makubwa yanayotokana na utalii.
Wajumbe hao wa baraza la wafugaji wameunga mkono hatua ya kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili iweze kuwa na tija na kuwanufaisha zaidi wenyeji wa kimasai wanaoishi katika mamlaka hiyo.
Wamesema imedhihirisha wazi kwa jinsi wenyeji wa kimasai wanaoishi katika mamlaka hiyo kuwa katika umaskini mkubwa kutokana na raslimali kidogo kuelezwa katika kuwaendeleza wenyeji hao.
Aidha wajumbe hao wamesema ushiriki mdogo katika maamuzi yanayohusu shughuli za hifadhi pia ni kikwazo kikubwa katika kuwaendeleza wenyeji hao.
Mkutano huo unafanyika chini ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi bwana Pius Msekwa na kuhudhuriwa na wajumbe wa baraza la wafugaji, wajumbe wa baraza la wafanyakazi pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi

Jakaya akiwa na rais wa ICCF


The President for International Conservation Caucus Foundation(ICCF) David Barron welcomes President Jakaya Mrisho Kikwete to a meeting held at the Rayburn building in Washingto DC this morning.During the Meeting Mr.Baron announced plans to build an International Conservation College in Arusha.President Kikwete is in the US for a working visit at the invitation of president George Bush. Picha ni mali yake Freddy Maro wa ikulu

Kikwete afagilia utekelezaji wa mpango wa malaria Zenj


Rais jakaya Kikwete amesema Zanzibar imefanikiwa kupambana na ugonjwa hatari wa malaria ambao unaoongoza kwa kuua watu hasa watoto chini ya miaka mitano nchini.

Rais aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wake na viongozi wa Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa (CGD) jijini hapa.

Alisema changamoto kubwa iliyopo mbele ya wananchi wa Tanzania Bara kutokana na mafanikio hayo ni kuhakikisha kuwa malaria inatokomea na kuacha kuwa muuaji kiongozi wa watu nchini.

Akipongeza hatua iliyofikiwa na Zanzibar katika mapambano hayo, Rais ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza ya kikazi nchini Marekani, alisema njia pekee ni ya kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa, unyunyiziaji sumu ya mbu katika mazalia na dawa za kupambana na malaria.

"Ni kweli kuwa Zanzibar ikilinganishwa na Tanzania Bara ni ndogo na yenye idadi ndogo ya watu na hivyo kuwa rahisi kufikia mafanikio hayo, lakini tunaweza kwa upande wa Bara tukaanza na wilaya 26 hadi mafanikio yapatikane," alisema Rais.

Alisema Serikali yake imepanga kutangaza hatua madhubuti za kupambana na malaria ifikapo Oktoba mwaka huu, huku akiitaka Zanzibar kuhakikisha inalinda mafanikio hayo, kwa kutoruhusu wadudu wa malaria kuingia kisiwani humo.

Aliipongeza Serikali ya Marekani kwa mchango wake mkubwa uliowezesha Zanzibar kufikia hatua hiyo ya mafanikio hayo ambapo mwaka 2005 iliweza kupambana na malaria na kubakiwa na maambukizi kwa asilimia 25 na mwaka huu maambukizi ni asilimia moja tu.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Mark Green, alisema ili mapambano hayo yafikiwe katika nchi yoyote inayotishiwa na ugonjwa huo, kinachotakiwa ni dhamira ya dhati na raslimali pamoja na watu kubadilisha tabia ikiwemo kudhubiti mazingira yanosababisha mazalia ya mbu..

"Kinachotakiwa ni wanawake na watoto kutumia vyandarua vyenye dawa, nyumba zinyunyiziwe sumu ya mbu, wajawazito watibiwe na huduma ya afya iwe ya kuridhisha kwa jamii," alisema Bw. Green ambaye anafuatana na Rais Kikwete katika ziara hiyo ya siku tatu.

Wengine katika ziara hiyo, ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Elimu, Ufundi na Mafunzo ya Amali za Taifa, Bw. Haroun Ali Suleiman.


habari hii imeandikwa na ;

Na Suzan Mshakangoto Maelezo, Washington, DC

Picha na Freddy Maro wa Ikulu

Wednesday, August 27, 2008

Polisi wapoteza maisha katika ajali

ASKARI polisi wawili wa kituo kidogo cha Himo, wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyotokea Agosti 26 mwaka huu iliyohusisha pikipiki yao na gari dogo.

Askari hao wakiwa katika pikikpiki waligongana na gari aina ya Toyota Mark II yenye namba za usajili T 443 AVX likiendeshwa na mfanyakazi wa kituo cha forodha Holili (TRA) .

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agusti 26 majira ya saa 4 usiku katika daraja la Kilacha barabara ya Holili-Moshi.

Akielezea zaidi tukio hilo kamanda Ng’hoboko alisema kuwa askari hao Saidi Mainda(36) na Koplo Musa Fadhili(41) walikuwa wakitokea Holili na katika safari za kawaida za matembezi; pikipiki hiyo mali ya Said wakati gari iliyokuwa ikiendeshwa na mfanyakazi wa TRA ilikuwa ikitokea Mjini Moshi.

Alisema kuwa askari hao walikuwa wakitokea katika matembezi yao ya kawaida na walipofika katika daraja la Kilacha walitaka kulipita gari lililokuwa mbele yao bila kuangalia kwa makini na walipotokea kwa mbele ndipo wakakutana na gari hiyo na kugongana nayo.

Ni mawe ya msingi


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akiweka jiwe la msingi Soko la Mazao ya kilimo kwa wananchi wa kijiji cha Buhingwe na Mlela wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua na kuangalia miradi ya maendeleo katika mkoa wa kigoma leo. Picha hii ni ya Amour Nassor wa Vice President Office.

Njaa yawanyemelea askari wa jiji,wakichukua mali za machinga kushtakiwa


SERIKALI imesema ni kosa la kisheria kwa mgambo au askari kumkamata mtuhumiwa na kuchukua mali zake na kuwataka watuhumiwa wanaofanyiwa hivyo hasa wamachinga kuwashtaki watu wanaowafanyia vitendo hivyo.
Kauli hiyo ameitoa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Aggrey Mwanri wakatik akijibu swali la Mbunge wa Mfenesini, Mossy Suleiman Mussa (CCM), aliyetaka kufahamu iwapo ni halali kwa mgambo wa Jiji la Dar es Salaam kuchukua mali za Wamachinga wanapofanya biashara sehemu zisizoruhusiwa.
Naibu Waziri wa Tamisemi, alisema ni kosa kwa mgambo au askari wa jiji kuchukua mali za watuhumiwa hasa Wamachinga wanapowakamata na kuwataka kuwashtaki watu hao kwani ni kinyume cha sheria.
Alitoa ombi kwa Wamachinga ili kuepuka kuchukuliwa mali zao kama inavyosemekana, kuwahi katika Kituo cha Polisi mara wanapokamatwa huku akiwasihi kufanya biashara katika maeneo waliyotengewa.
Awali, Mbunge huyo alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali kutafuta ufumbuzi wa mzozo kati ya wafanyabiashara ndogondogo na mgambo wa jiji na hasara iliyopatikana kutokana na mzozo uliotokea katika maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mwanri alikiri kutokea kwa mzozo huo baada ya wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa na Manispaa ya Kinondoni na kukaidi kufanya biashara katika maeneo waliyotengewa ya Tandale, Magomeni Sokoni, Manzese Urafiki, Kinondoni na Mabibo.
Alisema hasara zilizotokana na vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni ni askari mgambo tisa na wafanyabiashara watano kujeruhiwa kwa mawe na kuvunjwa kwa vioo vya Ofisi ya Ulinzi ya Halmashauri na vioo vya gari moja la halmashauri na mawili ya wananchi vilivunjwa.
Pichani baadhi ya wachuuzi ambao wamekuwa wakikumbana na rungu la mgambo au askari wa jiji.Hata zamani wachuuzi walikuwapo.They make life comfortable na kisha hatuna masupamaketi kama Ulaya. lakini mbaya ni uporaji wa askari.Wananchi mnasikia hoja ya serikali washughulikieni wakiwanyang'anya vitu vyenu.

Serikali kuu yaamua kuibeba Dar


SERIKALI kuanzia mwaka ujao itatenga fedha kwa ajili ya Jiji la Dar es Salaam.
Hiyo itakuwa ni bajeti maalumu tofauti na mikoa mingine kuanzia mwaka ujao wa fedha, anasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani wakati akijibu swali bungeni.
Amesema fedha hizo zilizoagizwa na waziri Mkuu Mizengo Pinda zimelenga kuondoa kero mbalimbali kwa lengo la kulifanya jiji hilo kuwa kioo kwa nchi nzima.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani, alithibitisha hilo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), aliyeitaka serikali kuwa na mpango maalumu wa kukabiliana na kero nyingi zilizopo Jiji la Dar es Salaam.
Alisema Waziri Mkuu aliagiza kuanzia mwaka ujao, jiji hilo kutengewa fedha maalumu ili kupunguza kero katika jiji hilo hivyo kulifanya liwe kioo cha nchi.



Maoni ya Lukwangule


kama hawawezi kutumia fedha zetu kurekebisha mambo ya msingi kama mitaro ya maana katikati ya jiji?Hawa jamaa hizi fedha za serikali kuu si zitakuwa ni kicheko kwa kwenda mbele katika kuzifakamia?Kweli tunahitaji fedha za serikali kuu kutengeneza mitaro madhubuti kuepusha uwezekano wa kuagiza gari zinazohitaji injini za boti wakati wa mvua kama picha inayoonekana.

Ukiangalia makusanyo ya masuala ya maegesho tangu wameanza kukusanya wamekuwa na ratiba gani na fedha hizo mbona maegesho mapya yenyewe hayajengwi , angalau hayo au hizo fedha ndio za kulipana madiwani?

haya angalia adha ya usafiri.Jiji wala hawajaamka kuona wkamba UDA ni mali yao na inafaa kuiwezesha kusaidia usafiri wa uhakika dar. Kubuni mradi wa ysafiri wa baharini, tumebaki talakaka tu.

Hizi fedha za serikali kuu hazitakuwa na maana yoyote wka Jiji.

Waingereza watoa vitabu kwa sekondari za pembezoni

READ International, supported by the Ministry of Education and partnering with the British Council, are celebrating the arrival of nine 20ft containers, filled with books, sports equipment and stationery. These educational resources are bound for 190 remote and needy secondary schools across Tanzania free of charge.

The containers are destined for Kagera Lindi, Mara, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Singida, Shinyanga and Tabora. On the 10th August, 60 UK student volunteers arrived in Tanzania to distribute the books directly to these secondary schools. These volunteers will spend time with the Tanzanian teachers and students to support the donations.

The books are for academic level ‘Form 1-6’ - Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, English and Geography as well as library reading books. READ International is also distributing several tons of sports equipment and footballs across Tanzania.

READ International has no political or religious agenda; they send only the best quality, most relevant and up to date resources from the UK to Tanzania. READ International have been operating in Tanzania since 2005, when 5 UK volunteers visited the Singida Region with 25,000 books followed by another 25,000 books to the Lindi region in 2006. In 2007 they brought 98,000 books to 90 Tanzanian schools. This year is the most successful yet for READ International.

Quotes:

Robert Wilson, Founder and Director of READ International said:
“We are proud to be supporting Tanzanian Schools on a national scale. Our innovative project can supply good quality, up-to-date, relevant but disused UK textbooks to hundreds of thousands of Tanzanian school children at a zero cost to Tanzanian schools. We hope that our actions will support a bi-lateral relationship between young Tanzanians and young British students, both empowered through education.”

Tony Brennan, Acting British High Commissioner of Tanzania said:
"READ International have shown great energy and resourcefulness in the three years that they have been working in Tanzania. Their idea - of taking second-hand but still useable and relevant textbooks from British schools and delivering them to Tanzanian ones - is a simple but effective way of improving the lives of thousands of Tanzanian children."

Mama Sitta, Former Tanzanian Minister of Education said:
“These resources are extremely valuable to our schools; providing this kind of educational support is one of the best ways to alleviate poverty in Africa”

Tuesday, August 26, 2008

Will Smith na mkewe Jada wako TZ


Majira ya jioni sana kama saa moja na dakika 52 niliingia katika blogu ya michuzi, kile kijiji cha wanajamii wote nikakutana na taarifa hii ambayo nilipenda tu wanaburudani na makini kuona hii ya maana, mwenye mifedha kaja kutumbua Tanzania na wapi anaelekea?... Unguja na unajua zari lote hili limeanzia kwa nani kuliibua? Si mwingine bali ni yule yule mzee wa kujiachia, michuzi jr.


haya yalikuwa maneno niliyoyakuta katika picha hiyo:


Mwigizaji mchekeshaji na mwanamuziki will smith na mai waifu wake jada pinckett smith wametua dar kinyemela na mchana huu wameelekea kula vekesheni huko zenji. michuzijr.blogspot.com alikuwepo hoteli ya kempinski kilimanjaro na kuwabamba wakielekea kupanda gari lililowapeleka uwanja wa ndege wa eapoti ya julius nyerere.


habari zinasema will smith alimuulizia lady jd na baada ya kumkosa kwa kuwa alikuwa studio akirekodi albamu yake mpya, akaacha maagizo kuwa bibie huyo afanye juu chini waonane akirejea toka zenj...


kwa sasa Will anatamba katika anga za filamu na I am legend na kuna ngoma nyingine inatamba sasa wakati mdada alifanya kweli katika filamu zilizoingiza mamilioni Matrix.

Unapokata tamaaa.. au unapofikiri inakuwaje vile!?


Mimi sina hakika nani kachoka kati ya huyu mama na huyu mzee halafu nani anauza na nani ana nunua lakini najua kitu kimoja hili ni soko la kila wiki ambapo wakulima hujaribu kuuza mazao yao.Pichani Wakulima wa Mlali, Wilayani ya Mvomero, Mkoani Morogoro katika njia inayopandisha kwenda lukwangule(Mgeta) wakiwa na mbaazi huku watu wa kazi wakishindilia kwenye viroba tayari kusafirisha au kuwauiz awafanyabiashara.Hapa Jumamosi iliyopita kiroba kilicheza kati ya shilingi 6000 na 7,000. Picha hii na mdau John Nditi kutoka mji kasoro bahari.

Barabara ya Mbagala inaendelea kuchongwa

Ujenzi wa daraja kubwa katika mto Kizinga linalounganisha wakazi wa Mbagala na Mtoni katika barabara ya Kilwa umeanza jana na taarifa za wajenzi, daraja hilo litachukua miezi mitatu kukamilika.
Ili kuwezesha magari kuendelea na safari katika barabara hiyo muhimu na ya pekee kuingia Mbagala zote na kuelekea Kusini njia ya pembeni imetengenezwa ikiwa na kalvati moja tu tena dogo kama unavyoliona.
Watumiaji wa barabara hiyo wenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi wameelezea hofu yao ya kutengwa na mji iwapo mvua za vuli zitanyesha kutokana na wajenzi kuacha njia ndogo ya kutolea maji kama inavyoonekana pichani.Wanasema wakati wa mvua eneo hili la Mto Kizinga na bonde lake hufurika kuanzia upande wa msikitini hadi eneo ambalo linatumiwa na watu wa kijiwe kuoshea magari makubwa.
Wenyewe walipohojiwa walisema hali ya hewa kwa sasa itawawezesha kujenga daraja husika na kulimaliza kabla ya mvua za mwishoni mwa mwaka.
Picha hii ya Badi Yusufu inaonyesha tundu pekee lililobaki kutolea maji upande wa pili katika njia ya mchepuko kuelekea Mbagala, huo weusi wa maji ni kemikali kutoka kiwanda cha jirani. Hufikiria kwamba wana mazingira hawapo wangelikuwepo tungeliendelea kula kambale kutoka katika bonde hili ambalo ni mkondo wa bahari.

Spika Sitta asawazisha mambo Dodoma, Rais anayo haki... hajavunja sheria

SPIKA wa Bunge Samuel Sitta leo amesawazisha mambo ambayo yamewatia kigugumizi wabunge waliochengua akili za watu juu ya hatua ya Rais Jakaya Kikwete ya kuagiz amatumizi ya fedha za EPA.
Spika Sitta amesema kwamba Rais hakukiuka sheria wala taratibu zo zote za fedha, kwa kuamuru baadhi ya fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) zitumike kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na mikopo ya kilimo katika Benki ya TIB.
Kwa mujibu wa Spika, taarifa kuhusu kupatikana na kutumika kwa fedha hizo inaweza kuletwa bungeni.
“Ni utaratibu sahihi kabisa,” alisema Spika Sitta. Alitoa ufafanuzi huo baada ya Suzan Lyimo (Viti Maalumu - Chadema) kutaka ufafanuzi huo kutoka kwa Spika kama ilikuwa sahihi kwa Rais kugawa fedha hizo.
Kauli kama hiyo pia iliwahi kutolewa katika vyombo vya habari na wabunge wengine wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa (Karatu) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), ambao walijenga hoja kwamba Bunge ndilo lenye jukumu la kugawa fedha za matumizi kwa serikali.

Mugabe azomewa bungeni

WABUNGE wa chama cha upinzani cha MDC katika Zimbabwe wamemzomea Rais Robert Mugabe alipolihutubia Bunge leo mchana, ikiwa ni miezi mitano baada ya uchaguzi uliogubikwa na mgogoro kufanyika.
Habari zinasema wabunge hao walikuwa wakiimba nyimbo za kukisifu chama chao cha MDC na kupiga kelele za chini chini wakati Mugabe alipokuwa akizungumzia mafanikio ya serikali yake.
Mwanzoni mwa hotuba yake hiyo, Mugabe alisema “kuna matarajio makubwa” kwamba makubaliano ya kugawana madaraka yatafikiwa.
Wapinzani wamesema bunge halikupaswa kufunguliwa hadi mazungumzo hayo yakamilike.
Awali chama hicho cha Movement for Democratic Change (MDC) kilisema kingesusa hotuba ya Mugabe, kikisema hakimtambui kama rais.
Jana Mwenyekiti wa MDC, Lovemore Moyo alichaguliwa kuwa spika wa bunge la Zimbabwe.
Chama kinachotawala cha Zanu-PF kilipata viti vichache katika uchaguzi wa Machi, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1980.
Edna Madzongwe wa Zanu-PF juzi alishinda urais wa baraza la seneti ambako chama hicho kina viti vingi.

CUF waandaa kongamano la ukosefu wa uongozi na hatma ya Tanzania

Chama Cha Wananchi
Office of The Secretary General
P.O. Box 10979
Dar Es Salaam, Tanzania
www.cuftz.info
www.hakinaumma.wordpress.blog

TAREHE: 26/08/2008

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU: KONGAMANO LA KITAIFA KUJADILI
UKOSEFU WA UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA

Imetolewa na Mbaralah Maharagande,
Mkurugenzi Haki za Binadamu na Mahusiano ya Umma.

Nchi yetu inapita katika moja ya kipindi kigumu katika historia yake tokea ilipopata Uhuru mwaka 1961. Hali ya uchumi ni ngumu sana huku gharama za maisha zikipanda kwa kasi ya ajabu chini ya falsafa ya ari, nguvu, na kasi mpya. Tofauti za kipato na kiwango cha maisha kati ya matajiri wachache na walalahoi walio wengi inazidi kuongezeka. Migomo ya wafanyakazi na wanafunzi imekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa.
Nyufa katika Muungano wetu zinazidi kukua na hata kutishia uhai wa Muungano wenyewe. Migawanyiko ya kidini inaonekana kuzidi kujikita. Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar umeshindwa kupatiwa jibu huku uchaguzi mkuu wa 2010 ukiwa unakaribia. Serikali inaonekana kuzidiwa nguvu katika mapambano dhidi ya ufisadi na sasa mafisadi wanaonekana kutamba. Taifa linakwenda bila ya Dira wala Mwelekeo unaoeleweka. Wananchi wanaonekana kukata tamaa.
Matatizo haya kwa kiasi kikubwa yanaonekana kusababishwa na ukosefu wa uongozi thabiti, makini na adilifu. Hii si hali nzuri na tusipokuwa makini Taifa litayumba sana. Wazalendo wakweli wa Tanzania hawapaswi kukaa kimya na kusubiri matokeo ambayo kwa vyovyote vile hayawezi kuwa mazuri.
The Civic United Front (Chama Cha Wananchi-CUF) kikiwa chama makini kikuu cha upinzani nchini, kinachotegemewa na Watanzania walio wengi, kimeandaa kongamano maalum kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu hali hii ya ukosefu wa uongozi na athari zake kwa hatima ya Tanzania. Kongamano hilo litafanyika siku ya Alhamis, tarehe 28 Agosti, 2008, kuanzia saa 3.30 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, mjini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba, atawasilisha mada kuhusu UKOSEFU WA UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA na baadaye washiriki watapata nafasi ya kuichambua mada hiyo na kutoa maoni na mtazamo wao.
CUF imewaalika watu mbali mbali kushiriki katika kongamano hilo wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, wahariri na waandishi wa vyombo vya habari, taasisi za kiraia na kijamii, viongozi wa kidini, wasomi na wataalamu, maofisa wa kibalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

HAKI SAWA KWA WOTE

Mbaralah Maharagande,
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mahusiano ya Umma.

0773 062 577

Maisha ya Obama mashakani?


Kuna habari kwamba maisha ya Barack Obama yametishiwa kwa kiasi cha kufanya wapelelezi wa FBI kuingilia kati.
FBI wamesema ni mapema kwao kusema chochote kile lakini wanaangalia hali halisi ilivyo.
Habari kutoka Denver zinadai kwamba mtu mmoja amekamatwa akiwa na bunduki, risasi na mihadarati katika gari lake.
Mji huu ndiko ambako mkutano wa chama cha Democrats unafanyika ili kuwapitisha wagombea wake wa Urais na makamu wa Rais.Uchaguzi mkuu wa Urais nchini Marekani utafanyika Novemba mwaka huu.
Imeelezwa kuwa watu wengine wawili wamekamatwa kuhusiana na kadhia hiyo.
“ Ni mapema mno kusema kwamba lilikuwa tishio halisi kwa maisha ya Obama au kama watu hao wangelikuwa na uwezo wa kutekeleza tishio hilo,” amesema afisa mmoja wa serikali ya Marekani ambaye anaelewa nini kinachofanyika. Ofisa huyo alizungumza hayo kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Obama anatarajiwa kuwasili mjini Denver baadaye wiki hii kukubali kuteuliwa kwake kuwania Urais wa Marekani. Msemaji wa FBI, Kathy Wright, amethibitisha kwamba taasisi yake inachunguza habari hizo lakini alikataa kufafanua zaidi.
Polisi wa Denver nao wamesema kwamba hawana cha kuzungumza kwa sasa.
Tharin Gartrell, 28,(mtuhumiwa) alikamatwa Jumapili asubuhi mashariki mwa Denver katika viunga vya Aurora.
Ndani ya gari lake kulikuwa na bunduki mbili aina ya rifles, moja ikiwa na kirekebisha mwelekeo(scope), fulana ya kuzuia kupenya risasi na boksi la risasi.Pia kulikuwa na simu za upepo (walkie-talkies) na mihadarati.
Mtu mwingine Nathan Johnson, 32, alikamatwa katika hoteli ya Denver wakati mtu wa tatu Shawn Robert Adolf, 33, alikamatwa katika hoteli ya Glendale .
Adolf alijaribu kutoroka kwa kuruka kutoka ghorofa ya sita na anashikiliwa akiwa hospitali.

Tamasha la tatu la sinema Ethiopia





Ethipian Intl. Film Festival


Dear all.

The 3rd Ethiopian Intl. Film Festival will be held from 17-24 Oct.2008 throughout Addis Ababa.If there is any film maker who is interested to participate please let me know by return mail.

Best regards,
festival director,
yirga

Hili ni tamasha la tatu la filamu la Ethiopia.Ni sehemu ya kuonyesha uwezo na ubingwa. Kila mara tunakimbia kupeleka kazi zetu kimataifa lakini hapa kuna kitu chya maana sasa Kwa watanzania wanaopenda kushiriki Tamasha hilo tafadhali muwasiliane na yirgashewa teshome katika e mail:


Monday, August 25, 2008

Usafiri wa kuaminika chini ya lukwangule




Huu ni usafiri ambao haujali mtoto wa kike, mwanamke, mvulana au mwanaume.

Katika picha hizi unaona watu wanavyoshindana na maisha. Na kama huwezi kukaa kwenye kitako basi unaweza kutumbukiza miguu kati ya farasi ukambeba na mdogo wako na mzigo. Mzigo ukizidi wala huombi msaada unakokota kama mabinti hao wanavyofanya.

Picha hizi zimeletwa na mdau John nditi wa Morogoro wakati alipozuru tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro kuona gulio lao la kila wiki.Hii ilikuwa mwishoni mwa wiki

Rais Kikwete aelekea Marekani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo (Jumatatu, Agosti 25, 2008) mchana kwenda Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais George W. Bush.
Ziara hiyo inalenga kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa karibu zaidi kati ya Tanzania na Marekani, na shughuli zote za Rais Kikwete wakati wa ziara hiyo zinalenga kufanikisha jambo hilo.
Malengo makuu ya ziara hiyo yatakuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasa katika nyanja za elimu, afya na uchumi.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake keshokutwa, Rais Kikwete atahudhuria hafla ya mfuko wa kwanza katika Marekani kujishughulisha na masula ya elimu miongoni mwa Wamarekani wenye asili ya Afrika na Waafrika wa The Phleps Stokes Fund.
Kwenye hafla hiyo, Rais atazungumzia hali ya elimu ya Tanzania, mafanikio yake na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili sekta hiyo.
Baada ya hapo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano kuhusu sekta ya afya na hasa jinsi ya kupambana na kuufuta ugonjwa wa malaria nchini kwenye kituo cha maendeleo cha Center for Global Development.
Wakati wa mkutano huo pia zitataganzwa juhudi mpya na misaada mingine ya Marekani katika kupambana na malaria katika Tanzania.
Baadaye siku hiyo hiyo, Rais atakwenda kwenye Bunge la Marekani, ambako itatangazwa rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha wanyamapori cha International Conservation College kitajengwa Arusha.
Kwenye siku yake ya pili ya ziara hiyo, Rais Kikwete atakwenda Makao Makuu ya Shirika la Misaada la Marekani la USAID, ambako itatangazwa rasmi kuwa Marekani itatoa msaada wa kiasi cha dola za Marekani milioni 20 kusaidia maendeleo ya kilimo na usalama wa chakula nchini.
Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa atatia saini makubaliano ambako Marekani itasaidia usimamizi katika sekta za maji na nishati kupitia EWURA.
Rais pia atashiriki katika majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya elimu, na baadaye kushuhudia tangazo ambako Marekani itaipa Tanzania msaada katika sekta hiyo ya elimu.
Msaada huo utakuwa wa vitabu vya kufundishia masomo ya sayansi wa kiasi cha dola za Marekani milioni 1.5, na kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya kufundishia walimu na ujenzi wa maabara tatu za kufundishia lugha ya Kiingereza.
Rais anatarajiwa kukutana na wawezekaji maarufu katika Marekani.
Kwenye siku ya tatu ya ziara yake, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais George W. Bush katika Ikulu ya nchi hiyo ya White House.
Baada ya shughuli hiyo ya White House, Rais Kikwete atakwenda kwenye kituo maarufu cha waandishi wa habari katika Marekani cha National Press Center ambako Marekani itatangaza misaada zaidi kwa Tanzania katika nyanja ya afya, na hasa katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi na magonjwa ya mlipuko.
Chini ya msaada huo wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi, Marekani itasaidia ujenzi wa vituo viwili vya kisasa kabisa vya watoto, na pia itasaidia kuongeza uwezo wa Tanzania katika kupambana na magonjwa ya mlipuko.
Jioni ya siku hiyo ya tatu ya ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mchezo wa kikapu wa WNBA kati ya timu za Washington Mystics na Chicago Sky kwenye uwanja wa Veriton Center.
Wakati wa mechi hiyo, itatangazwa rasmi kuanzishwa kwa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” ambayo itaanza kufanya kazi rasmi mwezi ujao (Septemba) wakati ujumbe wa wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani utakapotembelea Tanzania.

Haya ndiyo kimsingi aliyasema rais wa Comoro


RAIS Ahmed Sambi wa Comoro leo amehutubia bunge la Tanzania na kimsingi ametoa shukurani na kualika Watanzania kufanya biashara na visiwa hivyo.
Rais huyo ameishukuru Tanzania na hasa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa ujasiri uliowezesha kukikomboa kisiwa cha Anjouan kilichokuwa kinashikiliwa na waasi bila kumwaga damu.
Akiwa ni mgeni wa kihistoria katika bunge la Tanzania kwani ni mara ya kwanza kwa Rais wa Comoro kupewa heshima hiyo, alisema Watanzania wanapaswa kujivunia askari wake.
Tanzania ilipeleka wanajeshi wake Comoro Machi mwaka huu kuitikia mwito wa Umoja wa Afrika (AU) ambao ulilazimika kutumia nguvu kumwondoa madarakani Kanali Mohammed Bacar ambaye alikuwa amekataa kustaafu baada ya kipindi chake kumalizika.
Baadaye aliandaa uchaguzi ambao alijitangaza ameshinda kwa kura nyingi, lakini Serikali ya Shirikisho la Comoro, AU na Jumuiya ya Kimataifa ilikataa kuutambua.
Alisema nchi hizi zina nafasi kubw aya kushirikiana kutokana na historia yake na aina ya watu ambao kimsingi wanashabihiana katika utamaduni.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alimwakilisha Rais alisema kitendo cha kushukuru ni cha kiungwana kwa kuzingatia kwamba ni hulka ya binadamu kusahau msaada anaopewa pale anapokuwa ametatua tatizo lililokuwa linamkabili.
Pichani rais wa Comoro akihutubia bunge.

Richmond kuanuliwa Alhamisi


SPIKA wa Bunge Samuel Sitta amesema kwamba Alhamisi wiki hii Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu maazimio 23 yaliyopendekezwa na kamati iliyoundwa kwa ajili ya kupitia mkataba wa Richmond.
Spika Sitta alisema Waziri Mkuu atawasilisha maazimio hayo siku moja kabla ya kutoa hotuba ya kuahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge la Bajeti ulioanza Juni 10, mwaka huu.
Bunge linatarajiwa kuahirishwa Ijumaa wiki hii majira ya saa saba mchana.
Machi 26, mwaka huu, Waziri Mkuu alikabidhiwa ripoti ya timu iliyoundwa na serikali kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya kampuni ya Richmond Development Company (RCC).
Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo. Picha hii ni mali ya Athumani Hamisi.

MDC washika nafasi ya Uspika Bunge la Zimbabwe


Habari toka Zimbabwe zinasema kwamba chama cha upinzani cha MDC kimeshika nafasi ya Uspika wa bunge la Zimbabwe.
Spika huyo ni Mwenyekiti wa MDC, Lovemore Moyo na anakuwa spika wa kwanza wa upinzani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980.
Chama kinachotawala cha Zanu-PF hakikuwa na mgombea katika nafasi hiyo ya spika.
Habari za awali zilisema wabunge wawili wa upinzani walikamatwa, walipokuwa wanakaribia kuapishwa, msemaji wa upinzani Nelson Chamisa, alisema.
Alisema polisi walikuwa wamepanga kuwakamata wabunge 15 wa upinzani, kuhakikisha chama tawala kinapata ushindi wakati wa uchaguzi wa spika.
Chama tawala cha Zanu-PF kilipata ushindi mdogo wa viti vya ubunge kwenye uchaguzi wa Machi mwaka huu, ikiwa ni mara ya kwanza tangu nchi hiyo ipate uhuru. Mazungumzo ya kugawana madaraka hivi sasa yamekwama.
Kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai ameonya kuwa ufunguzi rasmi wa Bunge kesho unaweza kuvuruga mazungumzo hayo.
Baada ya kuapishwa wabunge wa upinzani walikataa upande wa serikali, kwa mujibu wa habari kutoka bungeni.
“Nyinyi mnakaa upande ule. Hivi sasa nyie mko upande wa upinzani,” wabunge wa upinzani waliwapigia kelele wabunge wa Zanu-PF

Rama mla kichwa atinga kortini na pama

KIJANA aliyepatikana na kichwa cha mtu hospitali ya Muhimbili na kukitafuna wakati anataka kukamatwa Ramadhani Mussa (18) leo aliingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiwa amevaa kofia kubwa aina ya pama na kuficha uso wake ili asipigwe picha.
Hata hivyo kesi yake imeahirishwa na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Euphania Mingi hadi Septemba 8.
Upande wa Mashitaka uliokuwa ukiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Charles Kenyella ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba Mahakama kumpangia tarehe nyingine.
Awali ilidaiwa kwamba Ramadhani alimuua mtoto Salome Yohana wa miaka mitatu hapo Aprili 25 mwaka huu na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili eneo la Tabata Segerea kwa Bibi.
msomaji aliyenijuza habari hii hakufanikiwa kupata snap hata hiyo ya pama.

Mama watatu na mshikemshike wa kulisha watoto


Mdau Albart Jackson amenipatia picha hii kukumbusha watu kwamba mama huyu bado ana matatizo ya kuweza kulea watoto wake watatu. Pamoja na kupigwa jeki na wasamaria wema lakini mshike mshike bado mkubwa. Hivi wadau sheria ya ustawi wa jamii inasemaje? hana cha kuwapa zaidi ya maziwa yake. Hawa ni watoto mapacha watatu wakazi wa Tandale Uzuri, ambao ni Yohana, Paulo na Yohane wenye umri wa miezi 11 wakinyonya kwa zamu kwa anayeweza kusaidia anaweza kuwasiliana na mhariri wa gazeti la changamoto jamillah Abdallah au tembelea http://www.changamoto.com.

Mtanzania na Muangola huyu watafika walipofika wenzao?



Name: Ricardo David Ferreira Venancio

Age: 21

City of Residence: Luanda
Energetic Ricco Venancio has lived in four countries, on two continents and is always on the go! Born in Angola, he moved with his family to Lisbon in Portugal where he spent 15 years before heading to Manchester in the UK for two years. After that he headed to Johannesburg for a year before returning to Angola last year where he is currently living and working as a bank employee. Passionate about his family, Ricco says that they are his heroes and that if he wins Big Brother Africa, his prize money would go to his mom’s project.
The Angolan believes that ‘what goes around comes around’ and that people have got to ‘fight for their dreams.’ He’d like to live in a world without violence, and encourages audiences watching Big Brother Africa to show the world that in Africa respect, education and wisdom ‘play a huge part of our culture.’ He says viewers should remember that ‘this is only a game’ and says, ‘let’s keep our values a top priority regardless of the winner’s nationality.’
Asked how he relaxes, Ricco says, ‘I was born relaxed!’ But he does confess that he’s a bit disorganized and can be lazy. A huge football fan, he supports Sport Lisboa e Benfica, Atletico Sport Aviacao and Manchester United. In addition, he’d love to travel round the world and enjoys the music of Eminem, Justin Timberlake and Keima Roupa.

=====
Name: Latoya Lyakurwa

Age: 21

City of Residence: Arusha
21-year-old secretary Latoya from Tanzania describes herself as an extrovert because she likes people and loves to have fun. She says that she thinks she was chosen for Big Brother Africa because she has what it takes and says that she is the ‘right ingredient to spice up the house.’
The bubbly Latoya loves to shop, and enjoys dancing. Her favourite actors are Chris Tucker and Owen Wilson, and her favourite movie is the blockbuster DreamGirls. She enjoys tuning for The Tyra Banks Show and currently her favourite tune is Upgrade You by Beyonce and Jay-Z. Other performers she listens to include Linkin Park and Ludacris. Latoya would like to visit Jerusalem.
Asked about her favourite memory, Latoya says that it was time spent with her first love. Close to her family, she says that if she wins USD 100 000 she’ll use it on them. Commenting on her country, she says that Tanzanians are nice and humble and that the best place to visit in Tanzania is the Ngorongoro Crater.

wake za mandela ndani ya besdei



Mke wa sasa Nelson Mandela, Mama Graca Machel (kushoto) akimpiga busu mke wa zamani wa Mandela, Winnie Mandela (kulia), kwenye sherehe za kusherekea birthday ya 90 ya mume wao. Naona wanapatana vizuri tu. Je, wana-share siri za kumfurahisha mzee?Hili swali hakuuliza lukwangule ameuliza da chemi ndani ya swahili Time!

BBA yaanza Afrika Kusini, mwakilishi wetu anapendeza



MTU 12 sita kike na sita kiume zimeingia ndani ya jumba kubwa la BIG Brother Africa kuanza kile kinachopjulikana kama Biug Brother Africa III.
Zitakuwa ni siku 91 za mapenzi, husuda, chuki, hasira, matatizo ya kisaikolojia na hasira za watazamaji kwa watu wasiowapenda na wale ambao wanaamini kwamba jumba hilo linatengeneza uanaharamu wa aina fulani.
Siku 91 za watu kuwania dola 100,000.
Jana Agosti watu waliiona BBAIII laivu kupitia chaneli zao wakawaona washiriki wakijitoma ndani ya jumba hilo.
Mshiriki kutoka Bostwana, Tawana Lebani alikuwa wa kwanza kuingia kwenye jumba hilo ambapo mshiriki kutoka Zimbabwe, Chidzonga alikuwa wa mwisho, ambapo mshiriki kutoka Tanzania alikuwa wa sita, kuingia kwenye jumba hilo .
Na kwa kuanzia tu mshiriki wetu alikuwa na kitu, nikakumbuka mwaka jana kati ya tanzania na Angola, pasi shaka mshiriki wetu alikuwa anajua nini anachotaka, wauu!!! Waangola na watanzania tena nini?
Mshiriki wa Tanzania ni Latoya Lyakurwa(21) ambaye anatoka Arusha, na Muangola ni Ricardo Venanchio.
Washiriki wengine ni Thamsanqa Prusent kutoka Afrika Kusini, Tawana Lebani kutoka Botswana, Wilhelmina Abu-Andani kutoka Ghana, Sheila Kwamboka kutoka Kenya,Hazel Warren kutoka Malawi, Lucille Naobes kutoka Namibia, Uti Nwachakwu kutoka Nigeria, Morris Mugisha kutoka Uganda, Takondwa Nkonjera kutoka Zambia, na Munyaradzi Chidzonga kutoka Zimbabwe.
Kuanzia sasa hadi kumalizika kwa burudani hiyo DSTV kupitia chaneli yake namba 198, itakuwa ikiionyesha moja kwa moja kutoka ndani ya jumba hilo.
BBA ya pili ilifanyika mwaka jana ambapo Mtanzania Richard aliibuka kuwa mshindi na akaondoka na kitita cha dola 100,000.
BBA ya kwanza ilifanyika mwaka 2003 ambapo Mtanzania Mwisho Mwampamba alikuwa wa pili na wa kwanza alikuwa kutoka nchini Zambia.

rais wa Comoro anahutubia

Rais Ahmed Sambi wa Comoro ameshaanza kuhutubia, mimi kifaransa kimenipiga kombo kwa hiyo mpaka nitafsiriwe kwa kiingereza au kiswahili ndio niwapashe.
TBC 1 wanajaribu kutafsiri lakini naona ni kama ghasia huwezi kufuatilia nitawajuza baadaye.

Maganga Feruzi wa The Football anasemaje?

TFF mmekumbushwa simba ...fungeni mlango, au bado mpo mpo kwanza?

Kauli ya Mheshimiwa Rais Juzi kwamba takrima ya Serikali kumlipia kocha wa timu ya taifa sio ya milele imeeleweka na ujumbe wake kwa TFF uko wazi na wala hauhitaji kushereheshwa.

Kauli hiyo ni ya muhimu kwa sababu TFF imehadharishwa mapema na wala huduma hazikusitishwa ghafla. Nionavyo, TFF inahitaji msaada wa mawazo na ushauri sasa hivi pengine kuliko wakati wowote uliopita, lakini TFF na yenyewe pia ione haja ya ninachokisema vinginevyo hesabu itakuja kujulikana wakati huo tutakuwa tayari tumeshachelewa.

Ningekuwa na uhakika wa Rais ajae katika awamu ya tano, walau nisingekuna kichwa kuifiria hoja hii ya leo ya TFF
kumuajiri kocha wa timu ya taifa kwa upana huu, lakini inaniwia ugumu kwa sababu mimi si mtabiri na hatima ya jambo hili naona iko mlangoni linakuja hata kama kesho hiyo ni 2015.

Kwa sasa pengine si muhimu sana kuyakariri mambo ambayo tumekuwa tukiyasema katika safu hii kuhusu haja na umuhimu wa shirikisho hili na vilabu hasa vya Simba na Yanga kijijengea uwezo. Tumezungumza sana na kilichotufanya tufanye vile na hata sasa ni kuwa viongozi hawa ni wa kupita hivyo wakivurunda tutabaki kuwalaumu tu kwa kutoweka misingi imara lakini ndio tutakuwa tumeumia kama taifa na wakati tutakapokuwa tunalaumu tutakuwa tayari tumeshachelewa. zitabaki stori.!

Kinachonipa wasiwasi ni utayari wa viongozi hawa kubadilika. hofu yangu si ya leo. Kuna wakati mmoja wa viongozi wake aliwahi kuulizwa wanawatumiaje wachezaji wa zamani kuwashauri wachezaji wa sasa katika timu ya Taifa? Alichojibu ndicho kilichinichosha. Alisema mchezaji wa zamani anayetaka kutoa ushauri aende TFF na wao watampangia kuzungumza. Ni sawa lakini hii kauli ya anayetaka? Mimi nilifikiri utartibu mzuri ungekuwa kuwaomba na hata kuwaalika badala ya kusema "anayetaka". anayevukwa nguo ndio huchutama. Kwa hili la TFF kuajiri kocha sia ajabu wakasema mwenye ushauri aje badala ya kuwaomba watu wachangie au kuwaalika kwenye mijadala. wote tunakumbuka jinsi King Kibadeni alivyotahadharisha kuhusu suala la kufix mechi na mambo ya rushwa. badala ya kumuuliza taratibu awape nondo wakaibuka na kauli. THIBITISHA. Jamani! hata huyo IGP mwenyewe na watu wake huwa hawaendi hivyo. matokeo yake wale wote wenye fununu na mambo ya rushwa katika michezo wamefunga midomo.


Bahati hii tuliyonayo ya kuwa na viongozi wanaopenda michezo na utamaduni ni muhimu tuitumie sasa. Juzi wakati mheshimiwa Rais analipotembelea Jengo la wamachinga na kusitisha kwa muda jukumu lile ili aone mazoezi ya timu ya Taifa walau kiduchu kwa wanaomfahamu Mheshimiwa Rais ni kitendo kile walikitegemea na wala hawakushangaa.

Yupo rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa angeshangaa sana kama Rais asingeangalia angalau kwa sekunde mazoezi yale. Huyu ni Rais mwanamichezo aliyecheza na anayependa michezo. Waliokuwepo hapa jijini wakati Yanga inatoka kampala mwaka 1993 wanakumbuka. Ule uwanja wa ndani na basketball na kadhalika na kadhalika. Lakini ni lazima tukiri kuwa huyu ni Rais mpenda michezo yote na ndio maana imefika wakati sasa aangalie kusaidia michezo mingine. Wale wa riadha na wenyewe wajiandae wasiwe kama TFF ambao mbali ya kupewa ofa ya kumtafuta Kocha iliwachukua miezi kupeleka mapendekezo.

Wakati TFF inaangalia suala hili ni vyema pia itatumia fursa ilizonazo. Kwa kipindi kirefu ambacho Maximo anakuwa hayuko timu ya Taifa sijui wanamtumiaje. Kama hana cha kufanya au hajaambiwa kitu cha kufanya sia ajabu akatumia muda huo kuogelea kule ufukwe wa kigamboni. Mimi nilikuwa nafikiri kwa kuwa tumeletewa kocha kwa kweli tungemtumia kwelikweli. Atufundishie hata makocha wetu. Atoe mihadhara. Yawepo makongamano ya watu kujadili soka. Vyombo vya habari vikiombwa na kwa jinsi walivyo wanamichezo watakubali. Mbona watu walisaidia kampeni za Serengeti Boys inagwa baaadaye ikawa ndio zetu....! TFF ianze kujenga uwezo wa makocha wetu wa ndani kwa kutumia hawa kina Tonoko waliopo. Huyu Bushiri peke yake hawezi kuchukua ujuzi wote unahitajika mpango mkakati.


Lipo suala la viiingilio. Hili linasemwa kila kukicha. Vile viti vya kijani huwa havijai lakini watu wanashindwa kwenda kule kwa sababu ya bei. Lakini ni watu wanaokaa kwenye viti vile ndio wanaoshangilia timu muda wote. Waliokuwepo siku ya mechi na Black Stars ya Ghana waliona jinsi wale Waghana wachache waliokuwa pale viti vya bluu- VIP C walivyonyamazisha umati wa mashabiki. Kidoogo mzee Magoma moto ndio alikuwa anaenda nao sanjari. Sasa kama upangaji wa viingilio utakuwa haungalii siku ya mechi, muda wala tarehe katika mwezi ipo hatari kila siku shirikisho hili litasema linakula hasara.

Wakati huu TFF ni vyema waanze kujipanga pamoja na vyama vyao vya mikoa ili kuona ni jinsi gani watakuwa na udhamini wa maana au kuwa na mradi wa kudumu ambao utakuwa endelevu. Hii habari ya kutegemea makusanyo ya fedha za milangoni na malumbano haya mnayoendelea nayo na baadhi ya vilabu si ajabu wenye timu zao wakasusa kuja uwanjani hata kama uamuzi wao hautakuwa sahihi lakini watakuwa wamejeruhi mapato.

Wapo wanaonufaika na uuzwaji wa bidhaa za nembo ya Taifa na timu ya Taifa. Suala hili inaonekana kama halina mwenyewe au inaonekana kama ni biashara ya uchuuzi isiyo na tijara. Si kweli wati wananunua fulana na kofia kwa elfu kumi mpaka ishirini. Sisi tunasema TFF itoe zabuni za watu kutengeneza iuze hapa na mikoani. Pengine huu ni mradi usio na malipo lakini nenda pale jiji la Torino au tembelea Venice uona jinsi jezi za timu za Taifa zilivyo na bei ghali. Sisi hapa hiyo hatuna pengine tunaona huo ni umachinga.


Tulishawahi kusema kuhusu uwanja wa Karume lakini wapi. Kwa sasa wafadhili wa maana wameanza kujitokeza na pengine huu ndio wakati muafaka. Waambieni wawafundishe kuvua samaki badala ya kuwapa changu au vibua mnaposikia njaa. Jengeni basi uwanja wa maana mkubwa ambao mtakuwa na kitega uchumi chenu cha muda mrefu. Pengine hili nalo ni la muda mrefu sio dili kwa sababu uongozi wenyewe wa chama ni wa muda mfupi.

Basi alikeni timu za nje ziwe zinakuja hapa. Mbona kaka yangu Kadata alikuwa anazileta hapa timu za Zambia. Hili na lenyewe pengine lina usumbufu na kuogopa kula hasara.

Kama TFF inataka kuwa imara kimapato na kama alivyosema Mheshimiwa Rais mkiwa na uwezo mnaziepusha kuingiliwa katika maamuzi. TFF inapaswa kufikiria mara mbilmbui kuhusu mustakibara wake. TFF inahitaji viongozi watakaokuwa wanfikiria hatima ya nchi na sio hatima yao. Kina marehemu mzee Mangara wanakumbukwa leo kwa sababu waliifirikia zaidi Yanga kuliko walivyojifikiria wenyewe. Leo hii tunawakumbuka kwa hayo.

Kuna wakati niliwahi kuongea na kiongozi mmoja wa mpira nikamuambia mbona Dar inabaki kavu wikiendi zote hamna mechi mpaka au mpaka ligi ianze akaniambia aah maganga kama umeingia vichwani mwetu. Kuanzia mwezi ujao mechi itakuwa kila wiki. Leo hii nikimuona nitamshika masikio yake ni mwaka sasa. Wakati mwingine wala haihitaji kuapia ili ujue kama yapo mabadiliko ya dhati au changa la macho. Ni kwa matendo. Sijui kama TFF ipo tayari kwa hili. Huu ndio mtazamo wangu finyu. Siku njema.

Fadhili amezungtumzaje michezo Jumamosi?


haya ni mambo ya fadhili kwa jumamosi iliyopita

Provaida noma lakini tupo hewani...

Duu hizi intaneti jamani soo. Nilikuwa katika mapumziko mafupi kushughgulikia masuala ya kifamilia lakini nchi hii ilivyo na matatizo na watu wanaojiita maprovaida usiseme.Kutwa nzima ya Jumamosi na Jumapili mwishoe nikasema ahh ngoja komyuta nayo ipumzike. Wakatio neti inastablaizi umeme ukaondoka. lakini leo tumeingi tena manake tupo mjini tutakuw apamoja na hapa namuona rais wa Comoro anapigiwa wimbo wa taifa baada ya kukagua gwaride la heshima la Fanya Fujo Uone (FFU) Field Force Unit wazee wa kazi a.k.a hiyop fanya Fujo uone au kikosi maalum cha kuzuia ghasia na huyoo anaingia Bungeni.

Friday, August 22, 2008

Wabunge walalamikia VIP ya Julius Nyerere


WABUNGE leo walielekeza mashambulio kwa wanaosimamia chumba cha watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Wabunge wakiwa hawaridhishwi na hali ilivyo katika chumba hicho wamesema kwamba wamesababisha kishuke hadhi na kuwa kama daladala kutokana na kuruhusu wasio na hadhi kuingia humo holela hasa wazungu.
“Sisi tumekuwa wakarimu mno, tunawapa hadhi ya VIP, kwao hawatupi,” alisema Ramadhani Maneno (Chalinze-CCM), ambaye alilidokeza Bunge kwamba kuna wakati wageni wanaostahili husimama mle kama wako kwenye daladala.
Mwenzake, Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mashariki-CCM), alisema hali ilivyo kwenye chumba hicho cha VIP ni “vurugu tupu.” Alisema wakati fulani alikerwa wakati akitoka safarini Ulaya aliposhuhudia wafanyakazi wa Kampuni ya Saskatel inayojihusisha na TTCL, wakiingia mle huku wakiwa wamevaa kaptula.
“Ati nao wakapita VIP. Wazungu wamefanya pale kuwa ni mahali pa kuvutia sigara, fanyeni ili pale pawe na heshima,” alisema Nsanzugwanko.
Kabla ya hoja hiyo kujibiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye hotuba yake ya bajeti ilikuwa ikijadiliwa, Spika aliingilia kati baada ya Nsanzugwanko kuzungumza na kusema kuwa chumba kile hakistahili kuwa VIP, bali kilijengwa ili kiwe Ofisi ya Meneja wa Uwanja.
“Mimi nilikuwa Waziri wa Ujenzi wakati uwanja ule unajengwa (miaka ya mwanzo ya 1980). Ile ilipaswa kuwa Ofisi ya Meneja wa Kiwanja. Cha muhimu kwa serikali kutoa fedha ili ijengwe (VIP) nyingine,” alisema Spika.

Ridhwani Kikwete Mtoto wa Rais Aoa Dar es Salaam .


Rais Jakaya Kikwete akimuaga mkwewe Bi.Arafa Mohamed pamoja na mtoto wake Ridhwani Kikwete muda mfupi baada ya mtoto wake kufunga ndoa na Bi Arafa katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo majira ya alasiri kuelekea Magharibi.Picha hii ni ya Freddy Maro wa Ikulu

Mfalme Mswati alirejea nyumbani


Mfalme wa Swaziland, Mfalme Mswati wa Tatu ameondoka nchini leo Ijumaa, Agosti 22, 2008 kurejea nyumbani baada ya ziara binafsi ya siku tano nchini Tanzania.
Mfalme Mswati ambaye aliwasili nchini Jumatatu, wiki hii, kwa mapumziko ametembelea mbunga za wanyama za Tanzania ambazo zimekuwa maarufu duniani.
Taarifa ya Ikulu imesema kabla ya kuondoka, Mfalme Mswati aliagwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana leo mchana kwenye Hoteli ya Kempiski-Kilimanjaro mjini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili nchini mwanzoni mwa wiki hii, Rais Kikwete alimwandalia mgeni huyo dhifa kabla ya kuanza mapumziko yake kwenye mbuga za wanyama.

Diamond na ubani wa pwani leo usiku


LEO kunfanyika tamasha tamasha kubwa katika ukumbi wa diamond jubilee,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa buku kumi tu kwa kila kichwa,katika tamasha hilo linaloitwa ubani wa pwani litahusisha makundi kadhaa ya taarabu likiwemo kundi la East Africa melody,New Zanzibar Stars,kundi la Enomizizi kutoka Mombasa,Baikoko toka Tanga pamoja na Tot taarabu,na bila kumsahau mkongwe wao Bi kidude na muhogo wa jang'ombe Pichani B 12 na msanii wa muziki wa kizazi kipya Noora wakiwa wamepozi na mkongwe wa muziki wa taarabu hapa nchini Bi Kidude katika studio za Clouds.

dili la chap chap

Temporary Vacancy
Administration Assistant
Save the Children (Dar es Salaam office)
NEEDED URGENTLY
interviews will be conducted on Monday
25th August, 2008.
Henry Lyimo
Press and Information Assistant
EC Delegation in Tanzania
Umoja House
P.O.Box 9514
Dar es Salaam
Tanzania
E-mail:
henry.lyimo@ec.europa.eu
Delegation
www.deltza.ec.europa.eu

Ali kiba atua marekani kwa kishindo



Yule mwimbaji wa maarufu wa bongo flava Ali Kiba hatimae atua Marekani kwa maonyesho mbali mbali.amekuja kumaliza kiu ya muda mrefu kwa washabiki wake Afrika mashariki na kati.


Onyesho lake la kwanza litafanyika jumapili aug 31 kwenye ukumbi wa Mirage,address ni 4401 university blvd,Hyattsville,Md 20783 onyesho litaanza saa 4 usiku.
Kiba maarufu kwa nyimbo zake cinderella na makumuga ambazo kutwa haziishwi kuombwa na kurudiwa mara kadhaa,hususani wimbo wa cinderella umempatia umaarufu na sifa nyingi hapa Marekani.
Usipo wapigia Wakenya cinderella basi wewe dj hujui ku-ofcoz muziki.Ali Kiba atashirikiana na the mix master dj Luke, dj Joe Cat dady(WKYS 93.9) bila kumsahau dj young Kay blood yote ni kuwasha moto Labor day weekend Washington Dc.
Ali Kiba kwa mara ya kwanza Marekani,kwa onyesho la kwanza D.M.V., mara ya kwanza ndani ya mirage hall,4401 university blvd,Hyattsville Md 20783.na kwa mara ya kwanza kwenye BASHI LA UBWETE LA WATANZANIA LABOR DAY WEEKEND WASHINGTON DC.
watu pipo karibuni DC tucheze cInDeReLlA

BIG BROTHER AFRICA 3 STARTS THIS WEEKEND!


Twelve new housemates will begin an incredible 91 day adventure as M-Net’s blockbuster hit reality TV series BIG BROTHER AFRICA returns to DStv screens continent-wide on Sunday August 24 at 19:00 CAT!
With USD 100 000 up for grabs once again, live 24/7 coverage and a brand new house ready to open its doors, season 3 is set to mirror the runaway success of the first two seasons.
And whilst the identity of the housemates remains secret until the show goes live on air to over 40 African countries, M-Net has confirmed that Kabelo “KB” Ngakane will return as series presenter in a role he reprises from last season. The much-loved Channel O VJ and radio DJ, whose recently released single How Low Can You Go has seen him make the leap from TV personality to performer, will continue to be the primary link between the housemates and series fans.
In addition, M-Net has offered fans of the show a sneak peek at the all new Big Brother house, which underwent a total transformation in preparation for day one.
Comprising two bedrooms, one bathroom, a large lounge, an open plan dining area, a kitchen, diary room and a garden, complete with a striking new pool, it’s in the décor that the house marks it’s most dramatic differences. Colorful, bold and with a style that can only be described as an eclectic mix of energetic, youthful and fairytale, the BIG BROTHER AFRICA house is a character all on its own!
Living up to the new series tagline of Wild, Wicked and Wacky, the house includes unique features such as a “clock-themed bathroom” that are destined to capture fan attention and keep housemates entertained. In a house built for the express purposes of isolating housemates from the outside world, in a space where dates and times are excluded, it’s definitely worth tuning in to see what the housemates reactions will be to a bathroom jam-packed with clocks that don’t tell time!
In addition, the new house is equipped with 24 cameras and 52 microphones to provide audiences with a birds-eye view of the show all day, every day on DStv channel 198. Fans who tune in for the launch show will get the first complete look at the house, from top to bottom!
But the house isn’t the only element of the show that has evolved. The Brother Africa team has innovated once more and the popular ‘Shower Hour’ will now move from its morning slot to a late-night slot, giving housemates a new twist to life in the BB house!
Now, with the series just days away from launch, anticipation around the series is growing fast as fans wait for the big moment. Also gearing up for the launch is the M-Net website, which last year saw record-breaking traffic as fans of the show voted for evictions, downloaded videos, posted forum messaging and caught up with the latest breaking Big Brother news. The official website of the show is www.mnetafrica.com/bigbrother and it’s here that audiences will once more be able to interact with the series.
Given the popularity of Big Brother, several other official ‘fansites’ have also sprung up and fans who want to visit these can access them through the official Big Brother Africa website at www.mnetafrica.com/bigbrother
In addition to the Big Brother Africa website, fans can also interact with the series by SMS’ing the Big Brother Africa strapline, which is available on screen on DStv channel 198. For details of SMS numbers to use in each country, for detailed information on the Big Brother Africa housemates and for breaking news from the house, DStv audiences need only press the OK button on their DStv remote to access the series. This ‘OK’ function, plus the Big Brother Africa website go live at 21:00 CAT on Sunday August 24. Plus every Tuesday to Friday, fans who’ve missed any of the Big Brother Africa action can tune in to M-Net for daily edited highlights shows, along with a Monday night nomination show.
For now though, all attention is focused on Big Brother Africa 3 and the all-important launch. So diarize Sunday August 24 at 19:00 CAT, BIG BROTHER AFRICA 3, on M-Net and DStv channel 198. The launch show is set to feature special performances by Nigerian stars Naeto C and Ikechukwu, PLUS the big announcement of the twelve new BIG BROTHER AFRICA 3 housemates!
So get ready, it’s WILD, WICKED and WACKY!
Ends.

Thursday, August 21, 2008

Miss Utalii 2008


Nilitoa gari hili niliambiwa na mtu mmoja ni grafiki. Nikatembelea michuzijr nawakuta warembo hawa wakiwa wamelizunguka gari hili. hawa ni wanaosaka taji la Miss Utalii 2008 wakiwa wamelizunguka gari dogo ambayo mmoja wao atayeibuka mshindi atajinyakulia.

Gumzo la lukwangule:Nilichovuna saa 4 za kumsikiliza rais


JANA nilisema kwamba kutakuwa na makubwa leo. Naamini saa nne za kumsikiliza JK hazikuzaa hasara kama mtuma habari.Lakini kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi yapo makubwa yaliyoainishwa na kutolewa ufumbuzi ambao unaweza usiwe bora leo lakini miaka kadhaa ijayo.
jambo la msingi ambalo mimi nimeliona ni kuwa masulaa niliyodhani atayagusa aliyagusa, sikutarajia mengi makubwa katika EPA kwa kuzingatia mfumo wa sheria wa nchi yetu, lakini kwa sasa wabunge waliokuwa hawaelewi nini EPA sasa watakuwa wameelewa.
Nilichotoa hai katika EPA ni kufilisiwa kwa watu, kunyimwa nafasi ya kusafiri na fedha hizo zinazorejeshwa kusaidia wakulima kwa kuanzisha ruzuku katika mbolea na pia katika kusaidia TIB yaani Tanzania Investment Bank kuwa na uwezo wa kukopesha wakulima kwa muda nrefu na riba nafuu.
Swali linalobaki je hawa wahuni waliotwaa fedha ambazo si za serikali lakini serikali inaweza kudaiwa watafanywa nini? Matajiri azimio la Arusha walishughulikiwa kwa kurejesha mali zao kwa umma je hawa hawastahili kweli kushtakiwa, wanasheria wanajua lakini la maana zaidi utawala wa sheria hauna maana ya kuachia wakwivi kutokomea hivi hivi tu lakini pia si kwa kuwafanya waingie mahakamani bila kigezo,hawa ni wevi au wajanja hilo ni swali kwanza kisha... waswahili wanasema habari ndio hiyo... lakini amesema kwamba Novemba Mosi kitaeleweka mahakamani.
Nilisema shauri la zanzibar lakini kidiplomasia kabisa kasema watu wasikoroge mambo na kwamba ukiwa nje ni tanzania ukirejea hapa unazungumza zanzibar, alitumia akili sana kuhusu hili hasa aliposema wimbi hili nalo litapita walio watu wazima wasiwe wapuuzi, nadhani kimeeleweka.
Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge hilo kwa mara ya pili tangu ashike madaraka mwishoni mwa mwaka 2005 nilichoona kama alivyowahi kusema katika hotuba yake ya kwanza alitumai tena fursa hiyo kuelezea mwelekeo wa uchumi wa taifa na masuala mbalimbali ambayo serikali yake imekuwa ikiyapa kipaumbele.
Na shida zote alisema tusigombee fito, tunajenga nyumba moja na hili siwezi kulikataa, lakini inakuwaje unapokuwa na watu ambao hawaelewi hasa nini wanatakiwa kukifanya, na watu hao wakiwa viongozi? Lipo tatizo la ufinyu wa sheria na utawala pengine Sitta yuko sahihi sheria zetu zinaruhusu mambo kuenenda kigoigoi zaidi.
Huu muungano nao aliuzungumzia vyema, alisema wazi ubaya wa uropokaji, alisema matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi yanaweza kuchangia kuwavuruga kama siyo kuwachochea wananchi. Ilivyo ni kwamba kama ni kujadili suala la Muungano basi hapana budi mjadala ufanyike kwa hekima na busara na siyo jazba kama ambavyo imejitokeza katika siku za karibuni, hili siliendelezi sana.
Na huu mpasuko wa Zenj kumbe ulishafikia hatua nzuri lakini jamaa hawa wa Unguja kama wanavyosema katika suala la U nchi na Usio nchi amesema wanashindwa kuaminiana.
Kitu ambacho nilikiona kuwa kidogo cha mgomo, kumbe sivyo, rais alizungumzia haki ya watu kugoma, lakini ndani ya sheria, ndani ya uelekezi wa kawaida uliokubalika, kama kweli ni mgomo unaostahiki.
Hapa alifafanua vyema kuhusu mgomo unaokuja, hakuugusia wa walimu lakini huu wa TUCTA alisema mpaka kwa Kiingereza haukubaliki.Alikuwa na vigezo vyake.
Alisema kwamba mfuko wa hazina baada ya makubaliano sio ATM ni lazima kuweka sawa baadaya bajeti na walizungumzia Agosti sasa watu watazame kama serikali haitalipa.
Kweli kabisa serikali kwa mgao wa kota si ATM lakini nini maana ya maneno yote hayo ambayo serikali inazungumza. Inamaananisha kwamba haipo tayari kuyumbishwa, makubaliano ni muhimu watu wa TUCTA wanajua wamevumilia kiasi gani lakini wachambuzi wa mambo wa naweza pia kuelewa kwa kina nini maana ya kauli ya serikali kuhusiana na njia zilizotumika kutangaza mgomo.
Shauri la mwisho ambalo mimi nilisema ni la kawaida ni matumizi mabaya ya uhuru wa kunadika na kusema, maandamano,kupiga domo, kupinga serikali,kushughulikia hasira na kutuliza munkari.
kwa haraka haraka unaona kwamba alikuwa anachimba mkwara, lakini kama yeye aliwezesha upana wa mambo katika kucheua sumu mwilini alitaka watu wawe wastaarabu wasitapike bila mpangilio wakawavushia matapishi wenzao wakabaki wananuka bila sababu. Hili halina ubishi kucheua sum,u muhimu lakini utspike kwa mipangilio na uwe na sababu sio uachie tu mradi mdomo wa kutapikia unao
Kimsingi mimi nasema rais saa zake nne hazikuwa mbaya sana ingawa haya mengine ni elekezi za kawaida za nini amefanikisha katika miaka miwili na miezi saba ya utawala wake, kilichobaki ni kuangalia ushauri wa spika kwamba kunahitajika kasi zaidi kushughulikia wanaohujumu uchumi kwa mtindo wa EPA.
Naam, kweli tunahitaji mabadiliko kwani hii ni salamu, kazi yenyewe bado iko kwa wananchi wenyewe, ni hotuba inayotakiwa kuchambuliwa, kuna mengi sana ambayo sikuyatia hapa kwani huenda yakasaidia miaka mitatu ijayo wakati wa uchaguzi: ni ukweli kuwa wanaobungua nchi hii ni viongozi wafanyabiashara kwa hiyo tunahitaji waamue ama kuwa na biashara au kuwa wanasiasa na viongozi, hata ughaibuni linajulikana.

Kikosi cha JWTZ kushiriki ulinzi darfur

SAFARI ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania (JWTZ) kwenda kulinda amani huko Darfur imeiva na sasa wanatarajiwa kwenda huko katika kipindi cha wiki moja ijayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe alisema Bungeni.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 208/09, Muda mfupi kabla ya rais kuhutubia bunge, Waziri Membe alisema askari wa Tanzania wanakwenda huko kwa kutekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuunda jeshi lapamoja lijulikanalo kama Unamis 26 ili kusimamia amani huko Darfur.
“Tanzania kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika imekubali kupeleka askari wa kulinda amani huko Darfur ifikapo Septemba mosi mwaka huu,alisema.
Ingawa hakutaja idadi ya askari wanaotarajiwa kwenda huko, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Hussein Ali Mwinyi alisema wiki hii bungeni kwambakikosi kimoja kilikuwa kimeandaliwa kwa shughuli hiyo.

Muziki wa dansi wazidi kufunika ulaya! The Ngoma Africa Band Tena!!!!!!!!



Ni juzi tu siku ya jumamosi ya tarehe 09/08/2008 katika viwanja vya Robstock Park,katikati ya mji wenye maghorofa marefu FRANKFURT City,Ujerumani,
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band inayoongozwa
na mwanamziki nyota mahiri Ebrahim Makunja alimaarufu Ras Makunja na mdundo wao
wa dansi la Tanzania ambao umekuwa maarufu kwa jina la bongo dansi ulifanikiwa tena kwa mara nyingine kuyatingisha maghorofa marefu za mji huo na kuwatia kiwewe maelfu ya washabiki walio udhuria katika maonyesho hayo!
Kabla ya bendi ya Ngoma Africa kupanda jukwaani onyesho lilikuwa limetulia (cool) huku bendi nyingine kutoka Oteng Band (Ghana) hilikuwa ikitumbuiza,baada ya moja ya watayarishaji kuwatangazia washabiki kuwa sasa inapanda jukwaani bendi maarafu ya
The Ngoma Africa band(Tanzania) hapo tena kukawa hakuna mshabiki alieyakaa chini,
si wazungu ! wala si weusi,watoto kwa wakubwa palikuwa kama vile uwanja uliovamiwa na
siafu!
Ras Makunja mwenyewe akikiongoya jukwaani kikosi hiko chenye utajili wa wanamziki
wenze kujua kuporomosha mziki unao chezeka na kudatisha washabiki hakili
kwa mdundo wao wa nzimbo ya kiswahili!
Mlindimo wa mdundo huo haukumuacha mtu uliwachanganya hakili washabiki na kujisahau kabisa kuwa ni raia wa nchi,dini,rangi mbali mbali!
Ni Mziki pekee wa dansi wa Tanzania unaofanikiwa kuzoa mashabiki kwa kasi kubwa barani ulaya !na kuziacha hoi baadhi ya bendi yingine wakiwa na halama ya mshangao!
kwa jinsi gani!? washabiki wanatiwa kiwewe na mdundo huo wa Ngoma Africa Band,
Mpiga solo Gitaa wa bendi hiyo Christian Bakotessa a.k.a ChrisB ,aliwachengua washabiki na mlio wa gitaa la solo! mara tu pale aliporushwa hewani kwa kuitwa jina lake !na Ras makunja basi mlio wa gitaa hilo ni kazi moja tu!
Katika onyesho hilo pia kulikuwako wanahabari kutoka RADIO DEUTCHE WELLE wakiongozwa na mtangazaji mashuhuri wa Idhaa ya Kiswahili Bi.Swaum Mwasimba !
The Ngoma Africa Band itapanda tena jukwaani katika onyesho lingine kubwa la
AFRIKA FESTIVAL siku ya 29/08/2008 katikati mji wa Hamburg,katika jukwaa la wazi
la Hamburg-Altona ambako nako washabiki wanawasubiri kwa hamu.
Siku ya 30/08/2008 Ngoma Africa wamehalikwa kutumbuiza katika maonyesho ya Utamaduni wa Afrika (AFRIKA FEST) yatakayo fanyika katika mji wa Krefeld nako huko
kutakuwa na vunja jungu la PATA SHIKA ! za NGUO KUCHANIKA

Taarifa hii imeletwa na msemakweli

Nimepata mgeni ofisini


leo nilipata nafasi adimu ya kukutana na mdada wa nukta 77, da subi. duhh nilikutwa off guard lakini nilifurahi kuonana naye na pamoja na kufurahi kwa kunipa big up pia nilimshukuru kwa jinsi anavyotuwezesha wanablogu kukutana katika trafiki yake na kutuelekeza. Bado yupo vakasheni Dar ingawa anasema anataka kwenda kumkagua bi mkubwa kule Moshi. Kutokana na kufurahi sana kukutana na da Subi niliomba kula naye picha ya kupozi aliyotutungua bloga mwingine bongo pix mheshimiwa bernard rwebangira . Da Subi thanks for the call, I appreciate.

rais kamaliza hotuba zake na Spika amesema vote of thanks

Saa nne Rais amezungumza na kutoa ujumbe mzito katika masuala muhimu yanayohusu taifa kwa sasa. masuala hayo ni ya siasa, uchumi na jamii katika hili akagusia soka na haja ya TFF kuanza kujiandaa kuwa na mwalimu wao mwenyewe. mambo yakiwa bomba tutawaletea hotuba nzima ya mheshimiwa rais.
Amezungumzia kazi zilizofanyika na kutoa mwelekeo wa baadaye na kusisitiza kuwa tunajenga nyumba tusigombee fito.
Mambo matatu Spika amesema katika Vote of Thanks:
la kwanza maboresho si mazuri serikalini, utekelezaji. Kuimarisha uwajibikaji kwa watendaji kwa ngazi zote kuanzia mitaa hadi serikali kuu
La pili utawala bora na unazidi kuimarika. Utawala bora unaelemea kutazama haki ya mtu mmoja mmoja kuliko maslahi ya taifa. Mambo ya hovyo yanatokana na taratibu na sheria zilizopo ambazo zinafanya utaratibu mgumu.
la tatu suala la zanzibar, mpasuko kumalizika mapema na migogoo midogo kushughulikiwa mapema.

rais anamaliza taarifa yake

Migomo haikufuata utaratibu, haistahili kuwapo na haikubaliki michezo inaangaliwa sana.

Jamani Dodoma Rais anaendelea take three

Fedha za EPA kwenda katika mfuko wa ruzuku ya mbolea na fedha nyingine kwa mikopo ya TIB kushughulikia kilimo. Window imeshaanzishwa mikopo ya muda mrefu na riba ndogo.Shabaha ni kuanzisha benki ya kilimo.

bado tunaendelea na Dodoma

Jambo jingine ambalo nimelisikia sasa ni kushughulikiwa jamaa wa EPA kwa kupokonywa hati za kusafiria, kukamatwa mali zao na kikomo cha wanaolipa ni Oktoba 31 tarehe Mosi ambao bado basi wakione cha moto Novemba Mosi.
Fedha zinazotumika kwa maendeleo na Token money zitakuwepo kwa ajili ya watu ambao watafika kudai.

Rais anazungumza Dodoma

Mpaka sasa Rais amesema mengi kuhusu utawala bora, nidhamu na maisha lakini muungano tu ndicho ambacho nakiona amekiongelea kwa kutumia diplomasia sana na kusema watu wasikoroge mambo zaidi waache taasisi husika ziangalie kama kweli kuna kero katika muungano. Jambo jingine nishani za Comoro kwa askari na washiriki wengine.
Jambo jingine anataka uhuru wa sasa utumike unavyostahili, tuzoee kitu cha kusema watu na kuandamana lakini si kwa kuvuruga nchi.
Uchochezi na habari za kuleta machafuko hazikubaliki. Ametoa fursa ya utamaduni wa kutoa maoni tusiutumie vibaya uhuru huo.
Wananchi wanatakiwa kutumia vyema haki na fursa hiyo.
Haki isiyokuwa na wajibu ni upuuzi mtupu.

*** Hotuba inaonekana ni ndefu alishuka asubuhi hii, sita kasoro kama sita na kukwagua gwaride kabla ya kuenda kutia saini na kuingia jengo la bunge na hotuba ambayo ilionekana kama kitabu sijui atamaliza vipi lakini mazito ya kuua mtu hayapo mpaka sasa.

Wednesday, August 20, 2008

KIPA WA GHANA AZIMA RAHA YA WATANZANIA



BAO la kipa Richard Kingston wa Ghana ndilo lililozima furaha ya Watanzania waliofika kwenye uwanja mpya Dar es Salaam leo jioni kuishuhudia timu ya taifa, Taifa Stars, ikimenyana na Ghana ambapo matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.
Kingston aliyeidakia timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006 Ujerumani, alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika saba mpira kumalizikia, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na nduguye Larea Kingston.
Bao hilo ambalo limetokana na wachezaji wa Taifa Stars kutokuwa makini kwani kipa huyo alifika katika eneo la kupigia adhabu na kuzungumza na Larea kabla ya kwenda kuunganisha kwa kichwa.
Stars ambayo ilionekana kuelewana kwa dakika nyingi za mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 34 kupitia kwa nahodha wake Henry Joseph aliyefunga kwa kichwa baada ya kuunasa mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Jabu.
Katika mchezo huo, wachezaji wa Stars walionekana kuelewana kipindi cha kwanza ingawa dakika 20 za mwisho baadhi ya wachezaji walionekana kuchoka na kumlazimisha kocha Marcio Maximo kufanya mabadiliko.
Ghana ilishuka dimbani bila wachezaji wake nyota wanaocheza soka la kulipwa isipokuwa Amamoo William anayecheza soka Misri, lakini akiwa benchi.
Taifa Stars: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Salum Swed, Nadir Haroub, Geofrey Bonny, Mrisho Ngasa, Joseph/Kigi Makasi, Tegete/ Mgosi, Athuman Idd/Shaban Nditi, Nizar Khalfan/Adam King’wande.
Ghana: Richard Kingston, Boye John, Yeboah Godfred, Quartey Jonathan, Issah Gabriel, Apimah Barusso, Larea Kingston, King Osei Gyan/Kumordji Benard, Dickson Christoper, Tiero Kwabena/Ayew Yeboha na Moussa Narry/Kojo Poku.
Pichani mpira ulipompita Ivo. Picha hii ni kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com

Gumzo la lukwangule



Kesho kuna kitu kinataka kutokea nchini hapa, natumaini si kuvunjwa tena kwa baraza la mawaziri, manake hii sasa itakuwa taabu kubwa, lakini ni wazi Rais Jakaya Kikwete
kesho ataleta taabu kidogo mpaka hotuba yake imalizike na kila mtu ajuwe nini kimetokea.
Si kawaida kwa rais katikati ya safari yake akahutubia Bunge moja kwa moja labda kuna daawa inatafutwa kwa tatizo kubwa au anavunja bunge, natumaini tena si kuvunjwa kwa bunge manake itakuwa sooo.
Bungeni kesho asubuhi kila mtu atakuwa tisti, hii ni kutokana na rais kuifanya ziara yake hiyo bungeni kuwa ni siri yake mwenyewe hata wasaidizi wake hawajui wanahisi tu Rais ataenda kufanya nini. Masikhara hayo!!!
Ni baada ya maswali na majibu mishale ya saa nne Rais atakuwa yu katika mimbari ya pale bungeni akizungumza kinachomkera na kumfurahisha lakini akipeleka ujumbe mkataa kwa umma na kwa watunga sheria.
Naam yapo mengi ambayo watu tunahisi..labda rais atazungumzia haya yafuatayo ni labda:

EPA-- MANAKE AMEIPOKEA RIPOTI YA TUME ALIYOIAGIZA NA NDANI HUMO WAPAMBE WANASEMA CCM INATAJWA LAKINI KWA KUZUNGUKA SANA lakini unajua hii inapingana na nini hasa? Ni kuwa aliomba kuhutubia bunge kabla ya kupokea ripoti sasa sijui ni coincidence au alishaelewa vitu vinavyokwenda akasema njia ni hii hii.. wape salamu zao bungeni
SUALA ZA ZENJ-- WABUNGE WA ZANZIBAR WAMECHACHAMALIA HAKI YA KUWA TAIFA LISILO TAIFA NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO, NA MOTO UMESHIKA KASI KWELIKWELI.
MIGOMO YA WAFANYAKAZI-- HILI SASA LINATIBUA ZAIDI, MIGOMO SI DALILI NJEMA PAMOJA NA WALIMU KUSHIKISHWA KITU KIDOGO INAONEKANA KUWA MAMBO SI SHWARI
MPASUKA WA KISIASA ZENJ--HILI NDILO SUALA AMBALO ALIAZIMIA KABISA KULIFANYA AKIWA IKULU LABDA ANA YA KUSEMA KUHUSU HILI.
LAKINI PENGINE ANAKUJA KUTUPA TATHMINI YAKE YA KAZI KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI
Vyovyote itakavyokuwa Rais kesho atakuwa na mambo mazito ya kuzungumza kwani pamoja na ziara zake za nje hizi na za ndani kuna maeneo alikuwa anaonekana kuwa mkali kigodo kutokana na watu kushindwa kujituma na viongozi kubweteka.Isije ikawa kesho ni kiama cha mambo wakati rais anajiandaa kuelekea ughaibuni kutekeleza majukumu yake ya kimataifa katika kijiji Dunia.

Malori yakamatwa mpakani na magunia 240 ya mahindi

POLISI mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),leo walikamata malori mawili yakiwa na magunia zaidi ya 240 ya mahindi mpakani mwa Tanzania na Kenya, Namanga, taarifa ya Idara ya Maelezo imesema.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Elias Wawalali alisema kukamatwa kwa malori hayo kunatokana na kuwapo na taarifa za mfanyabiashara mzoefu za kutaka kuvusha mahindi kwenda Kenya bila kibali.
Wawalali alisema mfanyabiashara huyo mbali na kupewa onyo siku chache za nyuma na Idara ya Ushuru wa Forodha, lakini amekuwa akikaidi agizo hilo.
Alisema mahindi hayo kwa sasa yamechukuliwa na Kitengo cha Hifadhi ya Taifa ya Nafaka (SGR) Kanda ya Kaskazini Arusha ambacho kitanunua mahindi hayo na baadaye kuwauzia wananchi.
Mbali na hatua hiyo, pia TRA inafanya uchunguzi kuhusu mwenendo wa mfanyabiashara huyo iwapo katika biashara zake hizo amekuwa akilipa kodi ya serikali siku zote za nyuma.
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa malori hayo mawili yakiwa na shehena za mahindi kwa ajili ya kupelekwa nchini Kenya kinyemela.
Boaz aliyataja malori hayo kuwa ni yenye namba za usajili T324 AJK na T103 AJK kila moja likiwa limebeba magunia 120 yakipelekwa Kenya bila kulipia ushuru wa serikali na magari hayo kwa sasa yanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha wakati uchunguzi unaendelea kufanywa na TRA.
Hivi karibuni, serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, ilipiga marufuku usafirishaji wa nafaka kwenda nje ili kukabiliana na hali ya upungufu wa chakula nchini, hatua ambayo imekuwa ikikiukwa na baadhi ya wafanyabiashara.

Wabunge wanapotuliza akili baada ya mishemishe za bungeni



Jamani sitaki hata kuzungumza hii kitu imetokea Dodoma na hapa naiweka kwa sababu hii ni entatainimenti ya kwenda juu kwa mbele sana.Si mnamjua mheshimiwa huyu na wale... naona inafaa kwa burudani au vipi? Kwanza mheshimiwa Komba na Lupembe na pili mheshimiwa Komba akipepeta na..... jaza basi kama si kumalizia, inanoga kwelikweli.

Mnenguaji Rukia Bruno afariki dunia


MNENGUAJI maarufu wa Bendi ya FM Academia, Rukia Bruno amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam .
Lukwangule imehabarishwa na mdau Emmanuel Mrema wa habariLeo kuwa taarifa ya kifo ameipata kupitia balozi Credo aliyejitambulisha kama kaka wa Mwanamuziki Nyoshi el Saadat ambaye mkewe amefariki.
Katika mazungumzo ya simu alisema shemeji yake alikuwa Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kujifungua mtoto aliyefariki wiki moja iliyopita na kuzikwa hospitalini hapo.
“Habari za msiba za Bruno ni kweli na upo Sinza nyumbani kwa Nyoshi ambako familia ya marehemu ipo katika kikao cha kupanga siku ya maziko ya marehemu yatakayofanyika siku yoyote kuanzia sasa,” alisema Credo.
Aidha, Bruno alisema hafahamu chanzo umauti wa Rukia ambaye ameacha mume na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Staloni.
Kabla ya kuwa bendi ya FM Academia mnenguaji huyo alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, Bendi ya Tamutamu ambazo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuwapa burudani mashabiki.

Labor holiday weekend bash laja


Lile BASH la kila mwaka lifanyikalo kwenye LABOR HOLIDAY WEEKEND hapa Washington DC Metro linazidi kukaribia na maandalizi yanazidi kuiva.

Bash hilo ambalo mwaka huu lategemea kuwa bora zaidi ya yale yaliyopita, linaendelea kuboreshwa kwa kuhakikiwa pande zote za Michezo, Burudani, Vyakula na mjumuiko wa pamoja wa kifamilia kwa wanajamii wote wa ki-Afrika waishio maeneo ya karibu na wale wa mbali watakaoweza kujumuika.

Ijumaa ya tarehe 29 mwezi huu (Aug. 29) katika ukumbi wa Mirage Hall uliopo Hyattsville Maryland. Siku ya Jumamosi ( Aug. 30) itakuwa ni JusteLounge iliyopo Bethesda Maryland na kisha siku ya Jumapili (Aug.31) tutarejesha shughuli Mirage Hall kufunga week end.
Jioni za Jumamosi na Jumapili (Aug 30 & 31) kutakuwa na michezo ya soka na nyama choma katika viwanja vya michezo na mapumziko vya Middlebrooke Maryland.

Moja kati ya ahadi za uhakika kwa upande wa burudani ni muziki wa "kufa mtu" toka kwa mkali wa mixing wa clubs mbalimbali hapa Washington DC na pia 93.9 FM (WKYS Radio) Dj Joe. Joe ambaye ameshathibitisha ushiriki wake, amesema amejiandaa vema kutoa burudani ya aina yake kwa wale wote watakaohudhuria.Nyote mnakaribishwa

Tuesday, August 19, 2008

Wanaokwenda kanisani mambo mswano


Wataalamu wa sayansi, si mimi , wamesema kwamba kitendo cha kumpeleka mtoto wako kanisani kinakufanya mtoto atulie na kuongeza uwezo wake wa kuchakarika darasani na kupata matokeo bomba.
Kutokana na utafiti huo wanasayansi wameshawishi haja ya watoto kuhudhuria kanisani ambako pia wanatengeneza aina wigo wa kutoachana na masomo na kufanya vyema zaidi.
Utafiti huo umesema kwa kiingereza kuwa:If you want to boost your teenager's grade point average, take the kid to church. Watafiti wamesema kwamba kitendo cha kwenda kanisani au katika hafla inayofanana nayo inachochea uwezo wa kusoma na kuelewa mambo. Researchers found that church attendance has as much effect on a teen's GPA as whether the parents earned a college degree. Students in grades 7 to 12 who went to church weekly also had lower dropout rates and felt more a part of their schools.
Pamoja na utafiti kutoonyesha kama Mungu anafanikisha maksi za watoto hao na kuchaji ubongo lakini ni dhahiri kuwa watoto wanaokwenda kanisani mambo yao kichwani ni mswano sana.
On average, students whose parents received a four-year college degree average a GPA .12 higher than those whose parents completed high school only. Students who attend religious services weekly average a GPA .144 higher than those who never attend services, said Jennifer Glanville, a sociologist at the University of Iowa.
Jamaa aliyenadika kuhusu utafiti huo anabainisha kuwa watoto hao wanapoenda kanisani wanakutana na mambo haya ambayo yanawaongezea hamu na pia kuwapa utaratibu mtamu wa maisha:
Ndio kusema ukiachia Mungu wanafanikiwa kwa sababu:They have regular contact with adults from various generations who serve as role models. Their parents are more likely to communicate with their friends' parents. They develop friendships with peers who have similar norms and values. They're more likely to participate in extracurricular activities.
Those factors account for only half the predicted effect, Glanville and colleagues say.
"There are two directions you can go with this research," she said. "Some might say this suggests that parents should have their kids attend places of worship. Or, if we use it to help explain why religious participation has a positive effect on academics, parents who aren't interested in attending church can consider how to structure their kids' time to allow access to the same beneficial social networks and opportunities religious institutions provide."
Jamani Mungu ni mkubwa tutambue uwezo wake anachofanya kwa watoto wetu so...Other studies have shown that regular church-goers breathe easier and live longer. And kids whose parents go to church are better behaved and more well-adjusted. In each of these studies, the researchers cite the social-network and psychological benefits of churches.
Glanville and colleagues David Sikkink and Edwin Hernandez of the University of Notre Dame analyzed data from the National Longitudinal Study of Adolescent Health, a nationally representative sample of 7th- through 12th-graders that began in 1994. Students from 132 schools in 80 communities participated.
Kids who attended church were also more likely to have friends with higher GPAs who skipped school less often, Glanville said.
The study also showed whether the teens said religion was important to them.
"Surprisingly, the importance of religion to teens had very little impact on their educational outcomes," Glanville said. "That suggests that the act of attending church -- the structure and the social aspects associated with it -- could be more important to educational outcomes than the actual religion."
Religious-service attendance had the same effect across all major denominations, the researchers found. The results are detailed in the winter 2008 issue of the Sociological Quarterly.

Phil Collins Trumps Paul McCartney in Mega-Divorce ;Duhh talaka hii noma kabisa


Phil Collins' ex-wife may no longer be in his heart, but she'll definitely always have a place in his bank account.
The easy-rocking star has waved good-bye to marriage No. 3 and hello to a reported $46.68 million divorce settlement which, if accurate, shapes up to be the biggest ever celeb payout in British legal history, trumping even the astronomical amount Heather Mills received—said to be $45.37 million—from Paul McCartney earlier this year.
Collins, 57, and Orianne Cevey, 35, were married for seven years before separating in 2006. They have two children together, sons Nicolas, 8, and Matthew, 4.
It isn't the first time relationship woes have caused a dip in the Genesis frontman's fortunes, with Britain's Daily Telegraph even claiming that divorce settlements have eaten into as much as one-third of his estimated $280 million net worth, nearly $84 million going to his ex-wives.
After taking advantage of technological advances and infamously dumping wife No. 2, Jill Tavelman, by fax back in 1994, he was forced to pay $34 million.

Mkandala asema demokrasia imekua...


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala,amesema demokrasia nchini imekua kutokana na watanzania wengi vikiwamo vyama vya siasa kuwa huru kuchangia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo, utawala pamoja na siasa tofauti na zamani.
Mkandala alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 16 wa Hali ya Siasa nchini unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.
Mada kuu ni changamoto za siasa huria na mustakabali wake.
Alisema kutokana na kukua kwa demokrasia chama tawala CCM kimejikuta kikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa katika miaka miwili iliyopita kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania.
“Japokuwa CCM imeendelea kufurahia nafasi yake ya kuwa chama tawala hasa bungeni, ni wazi kuwa kuwapo kwa makundi ndani ya chama hicho hasa katika uchaguzi wa Rais mwaka 2005 pamoja na kuongezeka kwa uhuru kwa wanachama wa chama hicho kumeleta manufaa kwa wapinzani wa vyama vingine,” alisema Mkandala.
Alisema wabunge wa CCM Bungeni wameungana na wabunge wa vyama vya upinzani kuzungumzia hoja zinazogusa maslahi ya taifa kuhusu masuala ya ufisadi na rushwa.
Alisema katika hilo pia vyama vya upinzani navyo vimeonyesha uwezo wake tofauti na mwaka 2005 ambapo vimeweza kutengeneza na kuwasilisha bajeti ambazo zimeifanya serikali kuchukua tahadhari zaidi katika kutengeneza bajeti yake kwa kuweka kipaumbele katika mahitaji ya wananchi.
Kuhusu masuala ya jamii Mkandala alisema pamoja na kukua kwa demokrasia yapo masuala mengine ambayo yanakabili siasa za Tanzania kama suala la dini kati ya waislamu na wakristo hasa suala zima Mahakama ya Kadhi, masuala ya ardhi, suala la ufisadi katika Akaunti ya fedha za Nje (EPA) ubinafsishaji wa mali za umma na mikataba hasa ya madini.
Mkutano huo unaokutanisha mabalozi, viongozi wa siasa pamoja na wadau mbalimbali wa siasa unaendelea kesho ambapo mada nane zitawasilishwa na wataalamu wa siasa nchini.

Pichani:Mwenyekiti wa THE UDSM Mwalimu Julius Nyerere Research Chair in Pan-African Studies Professa Issa Shivji akiongea na mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe wakati wa mkutano wa 16 wa hali ya siasa nchini uliofanyika leo chuo kikuu cha UDSM .Picha hii imetolewa http:// issamichuzi.blogspot.com

Wama wapewa milioni 159/- na Wamarekani


TAASISI ya wanawake na maendeleo (WAMA) leo ilikabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 159 kutoka kwa wananchi wa Marekani kupitia Shirika lao misaada la USAID.
Akipokea hundi hiyo Mwenyekiti wa taasisi hiyo Salma Kikwete alisema kuwa msaada huo watautumia kuwasaidia watoto yatima na wale wanaotoka katika mazingira magumu kupata fursa ya kusoma .
Naye Mkurugenzi wa Shirika la misaada la Marekani hapa nchini Pamela White alisema kuwa Shirika lake liatendelea kusaidia taasisi na Mashirika yanayofanya juhudi mbalimbali kusaidia maendeleo katika jamii.

Pichani ni Mwenyekiti wa Taasisi wa Wanawake na Maendeleo (WAMA) Salma Kikwete na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Pamela White, wakiwa wameshika mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Milioni 159 iliyokabidhiwa kwa WAMA kuchangia mfuko wa kusomesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu. Wengine ni wajumbe wa Picha hii ni mali ya Mroki Mroki aka father Kidevu

wanajeshi kutolipa nauli...! Hii imekaaje washikaji...


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wamiliki wa daladala wasiwatoze nauli askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati mazungumzo ya kutafuta mwafaka juu ya suala hilo yakifanyika.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa majumuisho ya mjadala wa makadirio ya matumizi ya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa.
Kwa mujibu wa Dk. Mwinyi, hivi sasa yanafanyika mazungumzo kati ya wizara yake, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na wamiliki wa daladala kuhusu suala hilo la ulipaji nauli na baadaye itatolewa kauli rasmi.
“Kwa kuwa wamiliki walishawachukua (askari) kwa miaka mingi tunaomba waendelee kwa utaratibu huo wa zamani hadi hapo utaratibu mpya utakapotangazwa,” alisema Dk. Mwinyi bila kufafanua.
Julai 31, mwaka huu, gazeti la HabariLeo iliripoti ikimnukuu Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Alfred Mbowe akisema waraka ulikuwa umesambazwa ukiwataka wanajeshi wote wanaotumia usafiri wa daladala kulipa nauli kuanzia Agosti mosi hata kama watakuwa wamevaa sare.

Ze Comedy, EATV waambiwa wasubiri kesi ya msingi

MAHAKAMA Kuu, Kitengo cha Biashara, imetupilia mbali maombi ya kikundi cha wachekeshaji maarufu kama Ze Comedy ya kutaka the East African Television (EATV) na walalamikiwa wengine wazuiliwe kuwabughudhi kwenye maonyesho yao kwa kutumia jina la Ze-Comedy.
Akisoma uamuzi katika mahakama hiyo leo , Jaji Mfawidhi Katharine Orio alisema kuwa baada ya kuangalia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa hakuona miongoni mwa pande zote mbili mwenye haki ya kumiliki jina la Ze Comedy.
“Mahakama imetazama nyaraka zilizopo na imeona kwanza, hakuna mtu yoyote anayelimiliki jina la Ze Comedy linalogombewa kati ya waombaji (Ze Comedy) na mlalamikiwa wa kwanza (EATV) haki ya kulitumia jina hilo,” alisema Urio.
Jaji Orio alisema kuwa nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa EATV walishawasilisha maombi ya kuruhusiwa kutumia jina hilo, ambapo ofisi ya msajiri haijatoa maamuzi juu ya maombi hayo.
Kwa upande mwingine, waombaji nao walipewa kibali cha kutumia jina hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai 1, mwaka jana hadi Juni 31, mwaka huu.
“Kibali hicho kimeshakwisha na hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa kuna maombi ya wao kuendelea kutumia jina hilo. Kama kuna maombi ya aina hiyo, basi mahakama haina taarifa,” alisema Orio.
Aidha Jaji alisema pia kuwa kinachoombwa kwenye kesi ya msingi vinafanana na maombi ya muda yaliyowasilishwa ambayo yanahitajika kutolewa uamuzi hivi sasa.
Alisema kuwa kuruhusu maombi ya waombaji yaliyopo ni sawa na kuamua kesi ya msingi iliyopo bila kupata ushahidi kutoka pande zote mbili, ambayo kisheria haikubaliki.
Alisema kutokana na kesi za namna hiyo kutokuwa nyingi hapa nchini mahakama imeona si wakati muafaka wa kutoa zuio kwa sasa na akaelekeza kesi ya msingi isikilizwe haraka ili mwenye haki aweze kupatikana.
“Mahakama imeona mpaka ilipofikia hakuna mtu yoyote mdai na mdaiwa atakayewajibika kulipa gharama zozote za kesi zilizojitokeza mpaka kesi ya msingi itakapotolewa hukumu, ” alisema Urio
Baada ya kutoa uamuzi huo, jaji aliwaamuru mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao mahakamani hapo juu ya pingamizi zilizowasilishwa na walalamikiwa wakitaka kesi ya msingi itupiliwe mbali.
Aliwaamuru walalamikiwa kuwasilisha hoja zao tarehe 2, mwezi Ujao, ambapo walalamikaji watatakiwa kuwasilisha majibu yao tarehe 18, mwezi Septemba. Jaji amesema atatoa uamuzi Octoba 21 juu ya pingamizi hizo.
Wasanii hao walikuwepo kusikiliza kesi yao ni Lucas Muhuvile ‘Joti’ Sekioni David ‘Seki’, Mujuni Sylivery ‘Mpoki’ , Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’ Alex Chalamila ‘Mc Regan’ na Joseph Shamba ‘Vengu’
Kundi hilo lilikuwa likifanya maigizo katika Kituo cha EATV, lakini baada ya kumaliza mkataba wake, limeingia katika matatizo baada ya kituo hicho kudai kuwa wao ndiyo wenye hakimiliki ya Ze Comedy.
Kundi hilo ambalo karibuni lilitangaza kudhaminiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia channel ya TBC1, lilifungua kesi katika mahakama kuu ya kitengo cha biashara, ikiishitaki EATV, ikidai Sh milioni 200 na kituo hicho kiwaache huru.
habari hii ni ya mdau Na Emmanuel Mrema wa habarileo aliyekuwa mahakamani.

Rais wa Zambia afariki dunia,zatangazwa siku 7 za maombolezo



Rais wa zambia Levy Mwanawasa, 59, amekufa mjini Paris kutokana na ugonjwa wa moyo, taarifa ya BBC imesema.
Kiongozi huyo alipatwa na shinikizo la Moyo Juni mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Zambia Rupiah Banda, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi yake,alitangaza kifo cha rais huyo kwa njia ya televisheni.
Serikali imetangaza siku saba za maomboleozo kuanzia leo.Mwanawasa ameacha mjane na watoto sita.
Hapa chini ni Safari nzima ya Mwanawasa duniani kwa kizungu

Levy Patrick Mwanawasa (born September 3, 1948 in Mufulira,
Zambia — died August 19, 2008 in Paris, France) was a
Zambian politician. He was the President of Zambia from
January 2002 to his death.
Mwanawasa was the second of 10 children.
He holds a law degree from the University of Zambia. He
worked in private law firms from 1974 until 1978 when he
formed his own firm Mwanawasa & Company. In 1985 Mwanawasa
served as Solicitor General in the Zambian government but he
went back to private practice in 1986. After Frederick
Chiluba was elected as President, he appointed Mwanawasa as
Vice-President in December 1991. Mwanawasa left his firm in
March 1992.
Accident
It has been argued that due to his high profile as a lawyer,
he would have been the obvious choice to succeed President
Kenneth Kaunda. Before his party convention in 1990 he was
widely tipped to become the President of the Movement for
Multiparty Democracy (MMD), but he declined the overture,
citing his young age and inexperience, however he opted to
stand as a Member of Parliament and won with an overwhelming
majority of the popular vote.
Political opponents within his
party have been suspected of orchestrating an assassination
on his life. On December 8, 1991 Mwanawasa was involved in a
serious traffic accident in which his aide died on the spot.
He suffered multiple body injuries and was flown to
Johannesburg, South Africa for medical treatment. He
remained hospitalized for three months. A lasting effect of
the accident is his noticeably slurred speech.
The accident involved a government driver. A commission of
inquiry was set up to investigate who was responsible for
the assassination attempt. Visiting investigators from
Scotland Yard concluded that there had been, in fact, no
plot to speak of.
Politics
Mwanawasa served as Vice-President until he resigned in
1994, citing gross abuse of office and corruption by some
leaders and insubordination to him by some colleagues. In
1996 he unsuccessfully contested Chiluba for the presidency
of the Movement for Multiparty Democracy. He lost. He
retired from active politics again.
2001 election
In August 2000 the National Executive Committee of MMD
elected Mwanawasa as its presidential candidate for the 2001
election. He won the election, held on December 27, 2001,
with only 29% due to Zambia's first past the post system,
beating 10 other candidates including two other former vice
presidents (Godfrey Miyanda and Gen. Christon Tembo);
Anderson Mazoka came in a close second with 27%, according
to official results. Mwanawasa took office on January 2,
2002. However, the results of the elections were disputed by
main opposition parties, including Mazoka's United Party for
National Development, which many observers claim had
actually won the elections.
Both domestic and international election monitors cited
serious irregularities with the campaign and election,
including vote rigging, flawed voter registration, unequal
and biased media coverage, and the MMD's improper use of
state resources. In January 2002, three opposition
candidates petitioned the Supreme Court to overturn
Mwanawasa's victory. While the court agreed that the poll
was flawed, it ruled in February 2005 that the
irregularities did not affect the results and declined the
petition.
In January 2005, Mwanawasa apologized to the nation for
failing to tackle Zambian poverty. About 75% of the
country's population live on less than $1 a day, the United
Nations' indicator of absolute poverty.
He was elected as President of the MMD for a five-year term
in 2005.
2006 election
Mwanawasa ran for a second term in the presidential election
held on September 28, 2006; Michael Sata was considered his
main challenger. His re-election was confirmed on October 2;
according to official results, he received 43% of the vote.
He was sworn in for another term on October 3. A few days
later, he named a new cabinet and appointed Rupiah Banda as
Vice-President.
Foreign policy Mwanawasa has criticized President Robert Mugabe of
neighboring Zimbabwe. Mwanawasa was one of first African
leaders to publicly do so.
Health
In 2006, Mwanawasa experienced a mild stroke.
While in Sharm el-Sheikh, Egypt, for an African Union
summit, Mwanawasa was hospitalized due to a stroke on June
29, 2008.
On July 1, he was flown to France for further treatment. The
head of the Egyptian hospital to which Mwanawasa was taken
said that the doctors there had stopped the brain hemorrhage
and that he was in a semi-comatose state. Vice-President
Banda said that his condition was stable, and Minister of
Information Mike Mulongoti noted that Mwanawasa had
previously suffered from hypertension; Mulongoti also
stressed that Mwanawasa was a "very hard working man" and
said that this may have been a factor.
Due to Mwanawasa's incapacitation, Banda became acting
President.
Death reports
On July 3, 2008 news outlets began reporting that Mwanawasa
had died in a Paris hospital due to his stroke. The story
originated at the Johannesburg-based 702 Talk Radio, which
cited Malone Zaza, who claimed to be the head of protocol at
Zambia's High Commission in Pretoria, South Africa; however,
the commission denied having someone employed at the embassy
with that name. Mulongoti, speaking for the government, said
the news of Mwanawasa's death was "false," and he urged the
South African media to show more restraint in its reporting.
As the reports were spreading, South African President Thabo
Mbeki called for a moment of silence in Mwanawasa's memory;
the South African government quickly expressed regret over
this misunderstanding and expressed Mbeki's hopes for
Mwanawasa's recovery.
Treatment in France
Mwanawasa was hospitalized at the Percy Military Hospital in
Paris. In a statement on July 7, 2008, Banda said that
Mwanawasa "remain[ed] in a stable condition" but had to
undergo surgery, which Banda described as minor, to correct
a breathing problem. Banda said on July 8 that this
operation was successful. On July 11, Banda said that that
Mwanawasa's condition was stable and that his doctors were
"satisfied with his current status".
Benny Tetamashimba, the MMD's Chairman for Information and
Publicity, subsequently said that the MMD "should begin
looking for a successor" to Mwanawasa as President of the
MMD. Mulongoti, speaking on state radio on July 14, said
that Tetamashimba's suggestion did not represent the
government's views.
United Party for National Development leader Hakainde
Hichilema said that Mwanawasa's incapacitation had paralyzed
the functioning of the government. On July 15, Patriotic
Front leader Michael Sata questioned the official claims
about Mwanawasa's health, and he called for a team of
doctors to be sent by the Cabinet to examine Mwanawasa; this
team would then disclose Mwanawasa's actual condition. On
July 17, the MMD announced that Tetamashimba was facing
potential disciplinary action, including the possibility of
expulsion from the party. Tetamashimba argued that he had
been misunderstood. He also said that Mwanawasa's condition
was improving and that he was "responding to treatment",
while asserting that the government was functioning smoothly
and criticizing the opposition call for a team of doctors to
report on Mwanawasa's health.
Banda gave another update of Mwanawasa's condition on July
24, saying that he was making "steady progress ... in his
recovery". Skepticism regarding Banda's optimistic updates
was reportedly widespread. Minister of Health Brian Chituwo,
speaking before the National Assembly on August 8, said that
Mwanawasa's "healing process will indeed be long" due to the
"serious nature of [his] illness".
Banda said on August 18 that Mwanawasa's condition had
suddenly deteriorated and urgent medical intervention was
necessary. The intervention was successful, according to
Banda, but Mwanawasa remained in serious condition. However,
on 19th August 2008, a family member who wished to remain
anonymous confirmed that Mwanawasa had passed away early
that morning.
Personal life
Mwanawasa was married to Maureen Mwanawasa until his death,
and had four children with her: Chipokota, Matolo, Lubona
and Ntembe. He also had two other children (Miriam and
Patrick) from his first marriage. His wife was a baptized
member of the Jehovah's Witnesses but has since been
disfellowshiped, because of her active role in politics. It
is against the faith of Jehovah's Witnesses to take part or
sides in politics.
In March 2005, Mwanawasa was baptised by Southern Baptist
missionaries. Pichani mwanawasa na mkewe.
So God rest him in peace

Tamasha la Muziki la Positive Vibes

Taarifa inatolewa kwa Umma kwamba Jumamosi tarehe 23 Agosti 2008 katika ukumbi wa New Msasani Club kutafanyika Tamasha la Muziki la Positive Vibes. Kauli mbiu ni “Pambana na Ufisadi, Linda Rasilimali”.
Burudani yenye ujumbe mahususi katika tamasha hilo itatolewa na Bendi ya MS Yes, na Vibration Sound pamoja na wanamuziki wa Bongo Fleva na Hip Hop akiwemo Profesa Jay na Wagosi wa Kaya wanatarajiwa kushiriki kawenye onyesho hilo.
Wabunge vijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamealikwa kuwa wageni rasmi katika tamasha hilo wakiongozwa na Zitto Zuberi Kabwe.
Tamasha hilo ni sehemu ya harakati za vijana katika kutetea rasilimali ya Taifa. Kiingilio katika tamasha hilo ni Shilingi 3,000 kwa Kawaida, Viti Maalum za kati ni 5,000 na Viti Maalumu ni 10,000.
Asilimia kumi ya faida ya Tamasha hilo itatatolewa kwa vituo vinavyoshugulikia walioathirika na madawa ya kulevya, asilimia kumi ya mapato ya Tamasha hilo itawezesha wanamuziki kwenda Mikoa mingine kutoka burudani na kufikisha ujumbe wa kutetea rasilimali za Taifa.
Waratibu wa Tamasha wanaomba watu mbalimbali, Makampuni, vyama na vikundi mbalimbali kujitokeza kudhamini tamasha hilo. Kamati ya maandalizi ya Tamasha imeundwa ikihusisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Imetolewa na Mratibu wa Tamasha.
Fulgence Mapunda (Mwana – Cotide)

* Mpaka sasa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limejitokeza kudhamini sehemu ya Tamasha hilo.

It takes two to tango, ni msemo tu... tamasha linaendelea argentina





Tamasha la kumi la miondoko ya dansi ya tango linaendelea katika jiji la Buenos Aires, Argentina . Tamasha hili ambalo lilianzia Agosti 15 mwaka huu linatarajiwa kumalizika Agosti 24.Ni msimu mzuri kwa wasaka noti kwani hata wanasesere ambao wanaonyesha kucheza tango huuzwa kwa wingi.

Global travel management company signs Winglink Travel Limited as partner in Tanzania

Winglink Travel Limited, one of the leading independent travel management companies in Tanzania, today announced that it has joined BCD Travel, one of the largest global travel management companies, as its exclusive representative and official Partner.
Winglink Travel Limited was established in 1998 and has grown to be one of the leading travel agencies based in Tanzania dealing with travel services for various corporates, NGOs and Ministries. An IATA and TASOTA accredited travel company delivering a comprehensive suite of solutions for business and leisure travellers. With 20 employees operating from two locations in Dar Es Salaam and Arusha, the company services both national and multinational corporations from across the industry spectrum.
BCD Travel simplifies and streamlines the corporate travel process, helping companies manage and control the movement of their people, information and resources. The company focuses on implementing an integrated, seamless technology platform throughout all global locations to provide full access to, and analysis of, travel data for these clients. Clients can take advantage of BCD Travel’s presence and technology infrastructure to track every trip, every traveler, and the costs incurred throughout every journey.
“To speak of the increasing globalization of today’s marketplace is to repeat what has become commonplace. But the ability to provide real, workable solutions to the companies operating in that marketplace is far less common – and that is precisely what BCD Travel does,” said Greg O’Neil, BCD Travel’s managing director & senior vice president of Growth & Emerging Markets. “Our expansion into Tanzania means we are now better positioned than ever before to deliver our travel solutions to national and multinational customers around the globe.”
Faiza Punja, Wing Link’s managing partner, said, "I am confident that being with the BCD Travel network is the best move for us, because we believe that our understanding of the local market together with BCD Travel's strong global reach and credibility will provide major benefits for us both. BCD Travel shares our philosophy for growth and success in the region, and we are excited by the decision to forge a strategic partnership with BCD Travel for corporate travel management solutions in Tanzania. We will continue to service our existing clients with every attention to detail and will work together to foster new business development growth and enhance our overall service offering.”
At the end of 2007 BCD Travel took the strategic decision to develop Africa within its hub strategy, followed in March this year with the appointment of a strategic development manager (SDM) for the region, tasked with driving expansion and business development, introducing new technology and operational processes and raising awareness of the BCD Travel brand.
With the signing of Winglink and new Partners in another four markets (Gabon, Madagascar, Mauritius, Senegal), BCD Travel announced last week that it has more than doubled its presence in sub-Saharan Africa. This growth will continue with another five markets being launched in the coming months. This expansion builds on the existing presence in eight other countries, and means that BCD Travel can deliver its unique travel management solutions to national, regional and global corporations located across the African continent.

DC wa Tegeta apokea wageni ateta na wadau


DC wa Tegeta mheshimiwa nanihii jana alibahatika kutembelewa na ugeni mzito katibu wa ccm tawi la kwa mama huko London, mh. suzan mzee (kulia), ambaye yupo bongo kwa vekesheni fupi. shoto ni mdogo wake .

Wakati wa ziara hiyo DC wa Tegeta alitoa ufafanuzi na kuomba radhi wadau wote kwa kwikwi iliyomuandama juma zima.
ni kwamba, katika juhudi za kufanya globu ya jamii iwe bora zaidi, amepata server ambayo ina nafasi kubwa hata za kuanzisha libeneke la video kama alivyoahidi awali. tatizo linakuja kwamba mitambo ya host imekuwa ikiteleza mara kwa mara kudaka link ya globu ya jamii na kusababisha kwikwi ya mara kwa mara.
na ili kukomesha kwikwi hiyo ameona bora aendeleze libeneke kwenye anuani ya issamichuzi.blogspot.com kama ilivyokuwa zamani wakati akisubiri wahandisi wa host warekebishe mambo.
Mheshimiwa alitoa kunradhi kwa usumbufu uliowapata wadau na kushukuru kwa jinsi maelfu ya wadau wanavyolifuatilia suala hilo na kumpa moyo kuwa asikate tamaa. naye aliahidi kuendeleza libeneke bila kusita pamoja na kukumbwa na changamoto za kiufundi ambazo ziko nje ya uwezo wetu.
anatumaini wanakijiji mtaendelea kumuelewa na kumvumilia

Monday, August 18, 2008

Taarifa ya Ikulu kuhusu EPA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatatu, Agosti 18, 2008) amepokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payments Accounts - EPA) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amekabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson P.M. Mwanyika.

Mwanasheria Mkuu huyo alifuatana na wajumbe wengine wa Timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hosea.

Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.

Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.

Timu hiyo iliundwa na Rais Kikwete Januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

Wakati anaunda Timu hiyo, Rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

Rais aliunda Timu hiyo baada ya kuwa amepitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2005/06 za EPA katika Benki Kuu Tanzania (BOT), uliofanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Kampuni hiyo ya Ernst and Young iliombwa na Serikali kuifanya kazi hiyo. Iliianza Septemba, 2007 na kumalizika Desemba, mwaka huo huo, 2007.

Rais Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo Januari 7, mwaka huu, 2008 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, Rais aliitolea maamuzi Taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda Timu ya Mwanyika.


Imetolewa na

Kurugenzi ya Mawasilia ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

18 Agosti, 2008

Rais akabidhiwa ripoti ya EPA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo majira ya saa tano hivi Ikulu ya Dar es salaam alikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account-EPA) .

Waandishi awali walialikwa, kisha kukatokea shughuli Ikulu, wakaagizwa ahirisho baadaye mzee mzima alikabidhiwa ripoti.

Kabla ya Bunge kwisha rais atalihutubia, Sijui atakuja kumwaga watu au atakuja kutuambia EPA si kitu si chochote.Walahi ni yeye na wachunguzi ndio wanajua nini kimo ndani ya ripoti hiyo na nini wameshauriana. Lakini rais anapoomba kulihutubia Bunge basi ujuwe mambo makubwa yaja kwani kawaida yeye ni mtoa uelekezi na mvunjaji wa hilo bunge. Mengineyo lazima yawe makubwa.

Pichani rais akipitia lijitabu la ripoti hiyo muda mfupi baada ya kukabidhiwa na mwenyekiti wa timu iliyoongoza uchunguzi huo Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Johnson Mwanyika.(Picha nyingine)Wengine katika timu hiyo ni Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea.

Mabweni ya Sekondari ya Masista Bingwa yateketea


MABWENI mawili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bigwa, inayomilikiwa na Masista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro yameteketea kwa moto mapema leo alfajiri na kusababisha hasara kubwa kwa mali ya shule na wanafunzi zaidi ya 100.
Pamoja na kusababisha hasara hizo, wanafunzi wanne wa kidato cha nne, Jesca Mgaga, Rose Nyambo, Havenlight Lazaro na Sarah Jaka ambao walibakia mabwenini kutokana na kuwa wagonjwa, walizirai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo, Makamu wa Mkuu wa Shule, Sista Mgimwa Luigina, alisema moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika, ulitokea majira ya saa 12:20 alfajiri wakati wanafunzi walipokuwa katika ibada ya misa kanisani kabla ya kuanza kwa vipindi vya masomo.
Alisema moto huo umesababisha hasara kubwa ambayo haijafahamika rasmi ya mali ya shule na ya wanafunzi hasa wa kidato cha tatu na nne waliokuwa wakiyatumia mabweni hayo mawili kwa kulala.
“Shule hii ina wanafunzi 371 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita…moto umeteketeza mabweni mawili ya wanafunzi wa kidato cha tatu na nne …na kila bweni lina vyumba 10 kwa maana hiyo wanafunzi walioathiriwa na moto huu ni zaidi ya 100,” alisema Sista Luigina na kuongeza kuwa hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa na moto huo kwa kuwa wote walikuwa nje ya mabweni yao.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu alisema kutokana na tukio hilo, ameunda Kamati ya watu watano itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Raphael Ndunguru, kwa ajili ya kusaidia kutafuta chanzo sahihi cha moto huo.
Alisema Kamati hiyo imepewa siku sita kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwake kwa ajili ya kubaini tatizo na kuchukua hatua za kukabiliana na majanga ya moto siku za usoni.

Pichani ni sehemu ya bweni lililoungua na wanafunzi wakijaribu kurekebisha mambo.Stori na picha na John Nditi, mdau wa Mlogolo

Waziri mkuu aelekeza utatuzi wa mgogoro wa msitu wa Sakare


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa mapendekezo ya kutatua mgogoro wa msitu wa Sakare Wilayani Korogwe kati ya wananchi wa eneo la Dindira na Kiwanda cha Chai cha Mponde Wilayani Lushoto.
Katika mapendekezo hayo, Waziri Mkuu aliwashauri wananchi wa Dindira wakiruhusu Kiwanda cha Chai cha Mponde kivune kuni kutoka Sakare kwa muda tu ili kiwanda kisisimame na kitafute chanzo kingine cha kuni.
Vile vile alisema atamshauri Rais afute miliki ya msitu huo kutoka kwa mgeni mmoja Mzungu ambaye aliutelekeza miaka mingi iliyopita na baadaye umilikishwe vijijiji kadhaa vinavyouzunguka msitu huo.
Waziri Mkuu alikuwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tanga kwenye hoteli ya Mkonge leo (Jumatatu Agosti 18, 2008) asubuhi mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili ya mkoa huo iliyomwezesha kupata maelezo kuhusu mgogoro wa msitu huo.
Jana mara baada ya kuwasili alitembelea Kiwanda cha Chai cha Mponde na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na baadaye akazungumza na wananchi wa Dindira.
Waziri Mkuu alisema ili kutatua mgogoro huo, ni vema kiwanda cha chai kikaruhusiwa kuvuna kiasi cha kuni kutoka katika msitu huo kwa muda na baadaye kitafute eneo jingine la kupata kuni.
Vile vile, Waziri Mkuu alisema, msitu huo siyo wa Kiwanda cha Chai cha Mponde wala wa wakazi wa Dindira au vijiji vingine vichache vinavyozunguka msitu huo wala, ila Rais atashauriwe afute hati iliyopo na baadaye umilikishwe upya.
Alisema kwa vile kijiji cha Dindira na vingine vichache vinavyozunguka msitu huo viliomba
kumilikishwa msitu huo, mara baada ya hati kufutwa vinaweza vikafikiriwa kumilikishwa.
Akizungumza kumshukuru Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Musa Shekimweri alisema viongozi wa mkoa huo na wa Wilaya, watafuatilia mapendekezo hayo ya Waziri Mkuu ili yatekelezwe kutatua mgogoro huo.
Pichani waziri Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Dindila wilayani Korogwe alipofanya ziara wilayani hapo mwishoni mwa wiki. Habari na Picha kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 980
DODOMA

Vodacom wakabidhi madarasa Bukoba


Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Kanali mstaafu Ernos Mfuru akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyumba vitatu vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 50 vilivyojengwa kwa ufadhili wa Vodacom Foundation.Kulia ni afisa habari wa Vodacom Foundation Bw Yessaya Mwakifulefule.Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika sekondari ya Bugene Wilayani Karagwe. Picha na Vodacom .I am Sorry awali iliandikwa mkoa wa Bukoba na mdau aliyeileta na ikapitiliza. Lukwangule

Serikali yazindua ununuzi wa hisa zake NMB

SERIKALI asubuhi ya leo imezindua rasmi mauzo kwa wananchi na makampuni ya asilimia 21 kati ya 51 ya hisa zake ndani ya benki ya NMB .
Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mauzo ya hisa hizo hoteli ya Kilimanjaro Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na uchumi Jeremia Sumari alisema kuwa serikali imetenga asilimia tano ya hisa hizo kwa ajili ya kuwauzia wafanyakazi wa NMB.
Sumari alisema kuwa asilimia 80 ya hisa zitauzwa kwa wanunuzi binafsi na asilimia 20 zitauzwa kwa makampuni binafsi ili kuwawezesha wananchi kunufaika zaidi.
Sumari alisema kuwa ununuzi huo ulioanza rasmi leo utadumu kwa wiki tatu ambapo utamalizika Septemba 8 mwaka huu, ispokuwa wafanyakazi wa NMB watakaendelea kununua hisa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Sumari alisema kuwa bei ya hisa ni shilingi 600 ambapo mtu anaruhusiwa kununua hisa 100 ambazo ni sawa shilingi 60,000 ambapo hisa zitanunuliwa kwa mafungu ya mia mia kulingana na uwezo wa mnunuzi.

Jay dee na Profesa Jay wapata tuzo za Pam




Mkurugenzi Mtendaji wa Jarida la Pam Awards (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kizazi kipya Judith Wambura (Lady Jay Dee) na Joseph Haule (Profesa J) baada ya kuwatunukia tuzo ya wanamuziki hao bora wa jarida hilo mwaka 2007 kwa nchi ya Tanzania pia kila mmoja alijinyakulia dola 500.Picha nyingine ni mwanadada jayDee akionyesha mkwanja alioupata.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya New Afrika.Picha na Albart Jackson wa Changamoto

Sunday, August 17, 2008

zanzibar ni nchi au si nchi wamshukia Dk.mwakyembe


Inaonekana kama malumbano ya zanzibar ni nchi au si nchi inachukua muda mwingi wa wanasiasa wa Unguja na magazeti ya Dar es salaam. Iwe kuna ukweli au la lakini mtu akiwa privileges na anajua kuchambua si lazima aseme manake inaonekana wanaozungumza na wengine na anayetakiwa kusema kala kobisi. Hii sasa noma. Hebu angalieni baadhi aya magazeti ya asubuhi ya leo.

Moto wateketeza hoteli Zanzibar


HOTELI za Paje Beach Bungalow (pichani-kutoka katika mtandao) na Kitete Beach Bungalow za eneo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, zimeteketea kwa moto leo, taarifa ya habari ya TBC imesema.
Watu walioshuhudia moto huo ambao ulizuka majira ya saa 5 asubuhi, umesababisha uharibu mkubwa wa mali zenye thamani ya mamilioni ya fedha.
Taarifa hiyo ya habari ya TBC Taifa imesema kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo kwa kuwa wakati moto unaanza, wageni waliopanga hoteli hiyo walikuwa nje ya vyumba vyao.
Habari zinasema wananchi wa karibu wakishirikiana na wafanyakazi wa hoteli hiyo pamoja na msaada wa gari la zimamoto, walifanikiwa kuuzima moto huo majira ya saa 7:15.
Chanzo cha moto huo hakikufahamika maramoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja hakuweza kupatikana maramoja kuelezea tukio hilo.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa moto kuteketeza hoteli mbili za kitalii kwa wakati mmoja .

Chacha wangwe na mzimu wake unaotesa


Juzi kuna kitu kiliibuka kwa Tarishi hauawi (tarishi.wordpress.com) nikasema jamani nendeni mkasome. leo magazeti ya asubuhi dar es Salaam yameibuka na kauli ambazo zinazidi kuleta hofu na mashaka kuhusu nini kilijiri wakati Bosi wa Chadema aliposikia kifo cha Chacha wangwe mbunge wa Tarime kupitia chama hicho. Mtanzania walisema: Mbowe asherehekea kifo cha Wangwe, Mzalendo Kigogo Chadema alishangilia wangwe ... na Mbowe alikataa ubani wa wangwe Habari Leo. Nini hasa kinaendelea katika siasa za Tanzania? Hivyo vichwa vya habari vinajionyesha vyenyewe na huyo Tarishi hauawi anatuweka mahali pagumu zaidi katika fikira zetu.

jamani dawa hizi nyingine hazifai ona sasa, toto saba kwa mpigo


MWANAMKE wa Misri, Ghazala Khamis (27) amejifungua mapacha saba mwishoni mwa wiki na watoto wote pamoja na yeye wapo salama, madaktari wamethibitisha.
Emad Darwish, Mkurugenzi wa Hospitali ya El-Shatbi ambayo ipo mji wa Alexandria amesema kati ya watoto hao, wanne ni wa kiume na watatu wa kike na walikuwa na uzito wa kati ya pauni 3.2 na 6.17 .

Darwish alisema watoto hao wamewekwa kwenye vyumba maalumu vya kutunzia watoto katika hospitali (kama unavyoona pichani).
Taarifa zinasema Ghazala kabla ya watoto hao saba alikuwa tayari ana watoto wa kike watatu na alitumia dawa za uzazi ili apate mtoto wa kiume.
“Hii ni mara yangu ya kwanza katika miaka yangu 33 katika kazi hii kuona mtu akijifungua watoto saba kwa mpigo,” Darwish aliliambia shirika la habari la Associated Press lililonunukuliwa na mtandao wa Yahoo.
Darwish alisema aliamua kumfanyia upasuaji mwanamke huyo mwishoni mwa miezi minane ya ujauzito wake baada ya figo yake kuwa na matatizo.
Darwish alisema Ghazala, mke wa mkulima wa jimbo la kaskazini mwa Misri la Beheira, alilazwa hospitalini hapo miezi miwili kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Kwa vipimo vya awali naweza kusema hakuna mtoto aliyeonekana na matatizo yoyote, wote wapo safi na wanaviungo vyote,” alisema mkurugenzi huyo.
Khamis alisema Wizara ya Afya ya nchi hiyo imeahidi kutoa kutoa maziwa na nepi za bure kwa miaka miwili ijayo ili kumsaidia dada yake.

Burudani ya Kitange ya Wakaguru


Sehemu kubwa ya burudani ambazo zilikuwa zinafanywa na makabila yetu zinaanza kuwa ni kwa ajili ya matukio makubwa tu kama kupokea viongozi au labda jambo kuuuuubwa. Mtu asiye na kwao ni mtumwa na sisi je mbona tunaachia alama zote za usisi kutoweka. Unayo ni ngoma ya Kitange ya Kabila la Wakaguru , wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, tazama inavyopendeza. Picha na mdau wa Morogoro John nditi ambaye ilitokea alikuwa huko Kilosa.

Kachumbari ya Helsink


Hii ni kachumbari aliyoandaliwa Majjid Mjengwa huko Helsink na wenyeji wake. kama unabisha nenda kaone katika blog Mifugo http://mjengwa.blogspot.com/ yake jinsi alivyokirimiwa na wenyeji wake.Wazungu wakarimu kama nini.

Morgan Tsvangirai akubali Uwaziri Mkuu?



ZIPO habari kwamba kiongozi wa upande wa upinzani Morgan Tsvangirai atakubali nafasi ya Uwaziri Mkuu katika serikali mpya itakayoundwa nchini Zimbabwe inayozingatia maslahi ya kitaifa.
Tetesi hizo zimebainishwa wazi na Shirika la Utangazaji la Uingereza ,BBC, katika taarifa yake kuhusu mazungumzo yanayoendelea nchini Afrika Kusini za viongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.
Katika mazungumzo hayo ambayo Botswana imekataa kuyahudhuria, viongozi chini ya Uenyekjiti wa Thabo Mbeki wamekuwa wakizungumza kukwama kwa mazungumzo
ya kutafuta mwafaka wa Zimbabwe.
Imedaiwa kwamba katika hotuba yake Tsvangirai alionyesha dalili ya kukubali nafasi hiyo.
BBC imesema imepata msimamo wa Tsvangirai kutokana na kuvuja kwa hotuba yake kulikoifikia Shirika la habari la The Associated Press la Marekani.
Imeelezwa kuwa Tsvangirai atakubali kuwa waziri Mkuu na kuacha madaraka ya Urais na amiri jeshi mkuu kwa Bwana Mugabe.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kuthibitishwa na pande zozote zinazohusika na mazungumzo hayo.Akifungua mkutano wa siku mbili Mbeki alisema ana matumaini kwamba pande zinazosigana nchini Zimbabwe zitafikia maafikiano mjini Johannesburg.
Mbeki ndiye anayertatibu mazungumzo ya kuondoa mgogoro ulioibuliwa na uchaguzi mkuu duru ya pili ambapo Morgan Tsvangirai alikataa kushiriki.

Endesha Ndoto Yako 2 yakabidhi RAV 4 Korogwe


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania imemkabidhi gari jipya aina ya Toyota RAV 4, mshindi wa tano wa promosheni kubwa ya magari ya Endesha Ndoto Yako 2, Kihiyo Nassoro, katika hafla iliyofanyika mjini Korogwe mkoani Tanga jana Jumamosi Agosti 16, 2008.

Kihiyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni mkazi wa eneo la Ngombezi mjini Korogwe, alikabidhiwa gari hilo na Meneja Mauzo wa Zain Kanda ya Kaskazini, Kizito Milambo.

Kihiyo, ambaye kazi yake ni kubangua korosho, ndiye aliibuka mshindi katika droo ya tano Juni 30, mwaka huu. Promosheni hiyo inahusisha magari 11 yanayotolewa na Zain Tanzania kwa kipindi cha mwaka mzima.

Akiwa na uso uliojaa tabasamu na bashasha, Kihiyo alikabidhiwa gari hilo lenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 40, mbele ya umati wa watu waliojitokeza katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi, nyuma ya kituo cha mabasi mjini Korogwe.

Makabidhiano hayo pia yalihudhuriwa na Ofisa Masoko wa Zain Tanzania, Caroline Kakwezi. Akizungumza baada ya kukabidhiwa ufunguo na kadi ya gari hilo lililovuta umati mkubwa wa watu kulishuhudia, Kihiyo alisema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kutimiza ndoto yake ya kumiliki gari lake binafsi kutokana na kushinda bahati nasibu hiyo ya Zain.

Promosheni ya Endesha Ndoto ni sehemu ya programu endelevu ya Zain Tanzania. "Lengo letu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwafanya waishi kwa raha zaidi kwa kuzingatia kauli mbiu yetu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa)," alisema Milambo.

Mpaka sasa droo ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain imekwishawawezesha watu watano kuibuka washindi wa magari aina ya RAV 4. Mshindi wa kwanza alitoka Dar es Salaam, wa pili alitoka mkoani Mbeya, wa tatu Iringa, wa nne Pwani na wa tano Tanga.

Ili kushiriki katika promosheni ya Endesha Ndaoto 2, mteja anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda nambari 100 na utakuwa ameingia rasmi kwenye promosheni hiyo.

Mbali ya zawadi ya magari, Zain pia inatoa zawadi nyingine anuwai kupitia Ndoto Pointi. Kila mara mteja wa Zain anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto Pointi. Kwa kila Tsh 500 anayozungumza anajipatia ndoto pointi moja.

"Mteja akifika kati ya Ndoto Pointi 1,000 hadi 3,000 anajishindia kufurishi cha zawadi kutoka Zain, akifika Ndoto Pointi 3,001 hadi 5,000, anajishindia simu mpya aina ya Nokia 1110i. Mteja akifika pointi 5,001 hadi 7,001 anajishindia simu aina ya Nokia 1650 wakati pointi 7,001 hadi 9,000 anajinyakulia Nokia 53100 au Ipod. Pointi 9,001 na kuendelea mteja anajishindia simu ya kisasa ya Blackberry bure," alisema Magavilla.

Pichani Meneja Mauzo wa Zain Kanda ya Kaskazini, Kizito Milambo (kushoto) akikabidhi ufunguo na kadi ya gari aina ya Toyota RAV 4 kwa mshindi wa tano wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Kihiyo Nassoro, mjini Korogwe mkoani Tanga jana. Droo ya sita inatarajiwa kufanyika leo (Jumatatu) Dar es Salaam.

Kilimanjaro kuingia mkataba na Young Africa SC

Bia ya Kilimanjaro inatarajia leo kuingia mkataba na timu ya wananchi Yanga kuipa udhamini wa shilingi milioni 350.
Ingawa haijaelezwa kinagaubaga thamani halisi ya mkataba na muda utakaotumika, mkataba huo unaipatia Yanga chanzo kingine cha mapato ukiacha mfadhili wake mkubwa Yussuf Manji na pasi shaka vyanzo vingine.
Mwenyekiti wa Yanga katika taarifa yake hakutaka kuzungumza zaidi mpaka hapo saini zitakapowekwa na mambo kuwa hadharani.Bia ya Kilimanjaro ni mali ya Tanzania Breweries
Limited(TBL).

Saturday, August 16, 2008

Elizabeth Kawogo's story, madhila aliyokumbana nayo msaidizi wa ndani Mtanzania huko Ulaya


Story by Freddy Macha, photos by Ayoub Mzee of Ben TV


When the door is opened, Mariam Kilumanga flashes a broad smile. So does one of her teenage children; but then she yells out for the chief guest in her house.
I hear footsteps treading down the stairs; in trepidation. I have read all the court papers, and perused all the claims and counter claims. I have even spoken to the woman herself on the phone and heard the stories.
I have listened to one of my editors and chatted with London's Ben TV presenter and blogger Ayoub Mzee. Yes, the story has all the details: but it does not tally with the person standing before me with tearful eyes and in a green yellow kanga.
I had expected a young and robust 25-year-old. At that age, a woman is ripe, ready and full of zest. I'm in shock that I dare not show. This is not the way Africans look in London. This is Ulaya, a place of dreams for many back home. Or is something wrong with my vision?
Yes, here is someone who has been to hell and back. Elizabeth Kawogo was born in Njombe, Tanzania, 25 years ago. Having dropped out of school because her parents could not afford fees she went to Dar es Salaam in 1997, aged 15, to try her luck in the city.
"I wanted a better life," she says timidly.
Shy, humble, forlorn; I have to strain my ears to hear what she is saying. After having spoken for a while, she refuses to allow me to take her picture. Even when Mariam Kilumanga, her guide and defender, has reassured that her story will help other people in similar (or worse) circumstances; she is still suspicious. Her face should not be shown in the media, she says. I realise this is a frightened woman.
Even though a London labour tribunal declared that her employers, Mr and Mrs Ramzan Dhanji, had discriminated against her and ordered them to pay 58,585 sterling pounds in compensation, she is still not comfortable. Not comfortable to even talk about her future plans.
And the sad thing, according to the grapevine in the Tanzanian community in London, there are many others like her. She is neither the first nor the last, someone whispers, as soon as I mention the case.
The court was told that Elizabeth had been working as a cleaner for Mrs Zainab Alibhai in Dar es Salaam since June 2004.
She then agreed with Mrs Alibhai to go with her to the UK to serve her as a domestic helper and assist her during the period she was to undergo medical treatment in London.
Between June 2006 and May, last year, Elizabeth was turned into a domestic animal, working up to 105 hours a week and sleeping in the most appalling of conditions. The judge reprimanded her employers, saying they should not treat domestic workers the way they do back in Tanzania.
Their defence was that she was a guest of the family and had agreed to work voluntarily. Is that why they did not pay her a single cent? Is that why she had to use toilet paper during her monthly periods, when women require extra sanitation?
Is that why she had no warm clothes during the cold winters? Is that why she was not permitted to eat the good food she cooked for her bosses but instead was given stale bread and leftovers?
No wonder, Elizabeth is so traumatised that she is scared to even have her photograph taken. There is a big lesson here.
It's a lesson for our poor ill-educated people - individuals from remote villages and shantytowns who are often taken for a ride by crafty and powerful people.
Luckily, Elizabeth met people who lent her a hand and liberated this dismayed Njombe woman.
Fortunately, when Elisabeth went to church, she found sympathy in Bertha, who introduced her to Patricia Mzena of TAWA (London's Tanzanian Women Association).
Then with Mariam Kilumanga and with assistance from Mrs Radhia Msuya (then at Tanzania High Commission), she was removed from her tormentors.
Luckily, for Elizabeth, she is now free. But what about the many others still suffering similar ordeals?
Who will hear and bail them out?
The British High Commission in Dar es Salaam?
Who?Freddy Macha is writer and musician working in the media and entertainment business since 1976.
Email: kilimanjaro1967@hotmail.com
Blog: www. freddymacha. blogspot.com
Watch the full interview with Elizabeth Kawogo on THE DIALOGUE program presented by Ayoub mzee on Monday the 18th august 2008 FROM 10AM- 12 noon on BEN TV SKY 194
OR LIVE ON :
http://www.bentelevision.com/
Remeber THE DIALOGUE is every monday from 10- 12 noon LIVE or Click the link below for more
http://ayoubmzee.blogspot.com/2008/08/tz.html

Blog nyingine, yaani mambo yaenda yakiongezeka


Huyu ni BARAKA MAHENGE from RUAHA UNIVERSITY COLLEGE(SAUT) akiwa ofisi moja hapo town kwa ajili ya FIELD.He is taking bachelor of science in computer science!!. All the best kwa washkaji wote mlio PT ofisi mbalimbali....I expect to get your pictures too.
Soma Ujumbe chini
hi ,
i hope unaendelea vizuri na shughuli zako ...we thank you for keeping us informed most of the time... Sasa nilikua naomba unisaidie kuipromote blogg yetu na sisi inayoitwa:
http://www.vyuotz.blogspot.com/
inahusu wanafunzi wa vyuoni na wengine wote ... mainly ni kwa ajili ya kuexchange ideaz na kujua kinachoendelea katika campus zetu...yaani vyuoni!!
i hope utanisaidia kwa kuongeza pale kwenye list ya blogg zako!!
hata kama unaweza kufanya njia nyingine ya kuiadvertise zaidi....
i hope utanisaidia
thanx in advance!!
Mdau Willy
--------------------------------------------------
Ujumbe kwa wanafunzi

HALLOW COLLEGE STUDENTS ALL OVER TANZANIA.
This is for welcoming you all and letting you know that now as students we have got our new blog........
This blog will be helping us to air our views on the ongoing things in our country and the world at large and chatting and letting others know what is going on around all our campuses...also it is designed for all of us to share our views about entertainments,education,sports,lifestyles,rumours and a little bit of politics and otha important things.....
So i take this opportunity to welcome you all and starting from this year of 2008 we will be having our blogg and you are all welcome to post your comments on this...
we will be using both languages ENGLISH and our mama KISWAHILI..
WELCOME YOU ALL
Mdau Willy

kwikwi mtandao wa globa publishers

Kuna matatizo ya kiufundi yamejitokeza kwenye mtandao wa globalpublisherstz.com kuanzia asubuhi ya leo ambayo yamesababisha kutokufunguka kwa mtandao huo na pia web master kushindwa ku fanya up dates za leo.
Tunawaomba radhi wasomaji wetu kwa tatizo hilo ambalo linashughulikiwa ipasavyo na HOST wetu na ameahidi litakwisha baada ya saa kadhaa zijazo.Kiufundi yalikuwepo mabadilko ya kuhama kutoka server moja kwenda nyingine ambayo yamesababisha hali hii.
Hatua ya kuhama ilikuwa ni muhimu kwa sababu za kiusalama na tunawaahidi kuwa tatizo kama hili halitajirudia siku zijazo.Asanteni kwa uvumilivu wenu na tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote mtakaoupata.
Web Master
Global Publishers Ltd
Dar es salaam
Tanzania
EA.

Mfalme Mswati aja kuwinda Selous


MFALME Mswati III wa Swaziland anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu kwa ziara ya siku tatu ya uwindaji, Idara ya Habari (Maelezo) imeeleza.
Kwa mujibu wa Maelezo, Mswati anatarajiwa kupokewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar Es Salaam.
Maelezo imeikariri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo imesema kuwa mara baada ya kuwasili nchini Mfalme Mswati atakwenda Hifadhi ya Taifa ya Selous ili kuwinda.

Rais Kikwete katika picha ya pamoja wenzake Sandton


Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto) akiwa pamoja na baadhi Marais wa chi za SADC.Kutoka kushoto Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe,Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi,Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao,Mwenyekiti mpya wa SADC Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini na Mfalme Mswati III wa SWAziland.Mkutano huo wa 28 wa jumuiya ya maendeleo ya uchumi Kusini mwa Afrika SADC unafanyika katika mji wa Sandton,Johannesburg Afrika ya Kusini.Picha hii ni ya Freddy Maro wa Ikulu

katuni ya Fadhili


Huu ni mchoro wa Fadhili kuhusu anavyoona michezo kwa wiki hii. Just Enjoy and have funny kama si kutoa comment zako

jamani shija na Blandina wametoka mbali hawa wacha wameremete


Leo majira ya saa nne father Kidevu katika pitapita yake alichomokea kanisa la Mtakatifu Joseph na kukutana na washikaji niliofanya nao kazi kwa miaka 10 pale Guardian, Bw Robert Shija Mipawa na Bi. Blandina Leticia Buluda wakiwa wanameremeta. congraaa wawili nyie kwani hakika mmetoka mbali. Bwana shija ni mkali wa masuala ya komyuta wakati bibie ni katibu mhutasi.

Ajali haina Kinga




Mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alipata ajali mbaya ya pikipiki iliyosababisha kupoteza unyayo wa mguu wake jana majira ya saa moja na nusu Barabara ya Nyerere maeneo ya kiwanda cha mabati cha Kiboko (pichani ni Pikipiki T 574 ARS kama ambayo inavyoonekana baada ya kuzimwa na walinzi wa kampuni moja ya ulinzi.)
Mtu huyo hata hivyo alifanikiwa kwa msaada wa wasamaria wema kuwaataarifu ndugu zake wanaoishi maeneo ya Banana.Moja ya picha inaoonyesha unyayo (fuatilia kaduara ka kishikaji)hata hivyo picha hizi hazikuweza kuonekana vizuri kwa sababu ya hali ilivyokuwa katika tukio hilo kuwa ni huzuni na kusikitisha na pia ukosefu wa mwanga wa kutosha. Picha hizi zimepigwa na kamera ya kwenye simu. nakushukuru msamaria mwema kwa picha hii na pole kwa mwendesha pikipiki aliyepata ajali.

Ajali iliyomtoa roho mchungaji wa Assemblies




Hii ni ajali iliyotokea agosti 14 huko Doma, Morogoro. Siku madereva watakapotambua kwamba wanatakiwa kutunza mali na watu wataacha ghasia hii ya kuweka mali na roho za watu pamoja na zao kuwa rehani.
Basi la aina ya Scania T 820 AGE , Mali ya Simba Mtoto, likiwa limegongwa sehmu ya Dereva na kusababisha Dereva , Amri Masimba na Abiria Mary Chatahika , ambaye ni mchungaji wa kanisa la Asembles of God kufariki dunia papo hapo, Basi hilo lilogongwa na Lori T 680 AAB aina ya Scania lenye tella T 626 AAB ambapo Dereva wake , Aboud Hassan naye alifariki dunia, ajali ilitokea eneo la Doma, Wilayani Mvomero, katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro.Basi hilo lilikuwa linatokea Lilongwe Malawi kwenda Nairobi Kenya na Lori lilikuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Zambia. Picha na habari hii ni imefikishwa humu na John nditi wa Morogoro

Friday, August 15, 2008

JK atoa dawa ya msongamano dar es salaam


RAIS Jakaya Kikwete ameagiza huduma za kijamii zipelekwe nje ya Jiji, ili kuepusha msongamano.
Rais alisema hayo leo asubuhi wakati akiweka jiwe la msingi katika Machinga Complex Ilala dar es Salaam.Jengo hilo linaendelea kujengwa.
Machinga Complex inayojengwa na uongozi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ni wazo la Kikwete alilolitoa mwaka 2005 mjini Dodoma.
Rais alisema kutokana na msongamano uliopo jijini, haina maana tena kufikiria kujenga jengo kubwa kama hilo tena mjini. Jengo hilo lililopo Mtaa wa Lindi, Ilala Dar es Salaam. “Mkilazimika kubomoa nyumba, bomoeni tu, mradi utaratibu unafuatwa wa kisheria na kijamii, lakini lazima tukubali kwamba mji unakua na katika maendeleo yoyote ni lazima upande mmoja upate msukosuko, kusemwa, lakini matunda ndiyo kama haya,” alisema.
Aliwataka watendaji wasiogope maneno yanayoandikwa ama yatakayoandikwa magazetini kutokana na hatua mbalimbali watakazochukua kwa ajili ya upanuzi wa mji, lakini akawaonya tabia ya kuwahamisha watu kwenda nje ya miji bila kuwapatia huduma siyo sawa.
“Mnawapeleka watu Bunju, Tuangoma, lakini hamfikirii hao watu watatibiwa wapi, maji yako vipi, umeme hampeleki halafu mnawalazimisha waondoke waende huko, hii si sawa, pelekeni huduma za kijamii nje, lakini ziambatane na miundombinu bora,” alisisitiza Rais. Aliuagiza uongozi wa Jiji chini ya Meya wake Adam Kimbisa, kuhakikisha kuwa majengo mengine madogo kuliko hilo lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 10,000 yanajengwa katika Manispaa ya Temeke na Kinondoni, pia kutaka uwazi ufanyike wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara.
Picha hii ya Athumani hamisi wa HabariLeo inaonyesha rais alipokuwa akiweka jiwe la msingi

Mkutano wa Misa-Tan kesho

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa afrika,tawi la Tanzania (MISA-TAN) kesho watafanya mkutano wao wa mwaka na kuchagua viongozi wapya wa Bodi ya Uongozi ya Taifa .
Mkutano huo wa mwaka utafanyika jijini Dar es Salaam na kuchagua Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Mweka Hazina na wajumbe sita wa bodi watakaochaguliwa kutoka kanda sita nchini.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Rose Haji inasema suala la jinsia litapewa kipaumbele katika uchaguzi huo ambao ni wa kwanza kufanyika chini ya katiba mpya iliyopitishwa katika mkutano mkuu wa mwaka jana.
Alisema katiba hiyo ni kubalifu kwa sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs Act 2002) pamoja na Katiba ya MISA ya kanda ambapo kwa mara ya kwanza wajumbe wa Baraza la Uongozi wa taasisi hiyi watachaguliwa kulingana na kanda.
Alisema bodi itakuwa na wajumbe tisa badala ya 12 waliopo katika bodi ya sasa na pia Bodi ya wadhamini ya MISA –Tanzania itakuwa imefutwa kulingana na katiba mpya ambapo pia marekebisho ya katiba yatajadiliwa.

Balozi Misri tayari kusaidia kilimo asilia Tanzania


Balozi wa Misri nchini Wael Nasr amehimiza watanzania kutumia kilimo endelevu ili kukwepa matumizi ya mbegu zenye vinasaba ambazo ni hatari. Amesema taifa lake liko tayari kuisaidia Tanzania katika hilo.
Asema kinachoongelewa leo katika nchi zinazoendelea kuhusu mazao yatokanayo na vinasaba, ni maafa kwani mazao mengi yatokanayo na vinasaba ni hatari kwa afya za watumiaji na mazingira kwa ujumla. Balozi Nasr aliyasema hayo alipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian ofisini kwake Dar es Salaam.
Alisema Tanzania imejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba ya kutosha, na mkulima anaweza kunufaika kwa kilimo endelevu akizingatia matumizi bora ya ardhi na mbolea asilia na kupata mazao bora.
Alisema Misri ipo tayari kuchangia katika lolote litakalohitajika kwa Tanzania, akitolea mfano ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kuhusu masuala mbali mbali yakiwamo ya matumizi bora ya maji na mazingira.

Katika picha hii ya Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais anaonekana Balozi wa Misri nchini, Wael Nasr (kushoto), akijadili jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, alimpotembelea waziri huyo ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu Dar es Salaam jana.

Hatima ya Ze Comedy J’nne


HATIMA ya kesi ya kundi la wachekeshaji maarufu kama Ze Comedy itajulikana Jumanne Mahakama itakapotoa uamuzi kama wasanii hao waendelee na shughuli zao au la.
Uamuzi huo ulikuwa utolewe leo kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, haukutolewa kutokana na Jaji Catherine Urio anayesikiliza kesi ya msingi kuwa katika safari ya kikazi.
Kundi hilo liliiomba Mahakama kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao wakati kesi ya msingi inasikilizwa.
Kesi iliyofunguliwa na kundi hili ni dhidi ya Televisheni ya EATV, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) pamoja na Msajili wa Nembo za Biashara, likiomba Mahakama iwazuie kuingilia biashara zao na kuruhusu kutumia jina lao.
Pia waliitaka Mahakama kutoa tamko kuwa walalamikaji ni wamiliki wa jina la Ze Comedy kabla na baada ya kuingia makubaliano na kulipwa fidia ya Sh milioni 200 na walalamikaji kutokana na usumbufu.

Rais aruka kwenda Afrika Kusini


RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo (Ijumaa, Agosti 15, 2008) kwenda Afrika Kusini kushiriki katika Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo wa siku mbili unaanza kesho (Jumamosi, Agosti 16, 2008) katika Ukumbi wa Sandton Convetion Centre, mjini Johannesburg.
Lakini hata kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wenyewe, Rais Kikwete leo jioni alitarajiwa kushiriki katika kikao cha Asasi ya Ushirikiano wa Siasa na Ulinzi ya SADC, ambayo wajumbe wake ni Tanzania, Swaziland na Angola.
Rais Kikwete pia alitarajiwa kuhudhuriwa chakula cha jioni cha kazi kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi huo huo wa Sandton Convention Centre.
Mbali na mkutano wenyewe, Rais Kikwete na wakuu wengine wa SADC kesho watahudhuria sherehe za kutangazwa kwa washindi wa Zawadi za SADC katika maeneo mbali mbali, na kutolewa zawadi kwa washindi hao.
Zawadi hizo ni SADC Media Awards, SADC Water Awards, SADC Secondary Schools Essay Competition.
Kesho pia Rais Kikwete na wakuu wengine wa SADC watashuhudia uenyekiti wa Jumuia hiyo ukibadilishana mikono kutoka Zambia kwenda Afrika Kusini, ambao ndio wenyeji wa Mkutano wa mwaka huu.
Baadaye mchana kesho, wakuu hao wa SADC watafanya kikao cha faragha na keshokutwa wakuu hao watashiriki katika uzinduzi wa Eneo la Biashara Huru la SADC (SADC Free Trade Area).
Rais Kikwete na ujumbe wake unatarajiwa kurejea nyumbani Jumatatu, Agosti 18, mwaka huu.


Pichani Rais Jakaya Kikweteakiagana na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam leo, alipokuwa akielekea Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC unaotarajiwa kuanza kesho. Picha na Amour Nassor (VPO)

Wanaotaka kujua sinema kuna blogu nyingine

Dear all,
Please find attached a list of some regional film festivals.
Please feel free to add any missing information. And if there are some so small film events I've forgotten please add them.
Yours in cinema
Or
Audiovisually yours

www.daddyruhorahoza.blogspot.com

Chacha wangwe aibuka kutoka kuzimu?


Jamani habari ndiyo hiyo.Kuna maswali yanaendelea na wana bloga inaelekea wanapata kile ambacho labda wengine hawajui. Sina hakika kama nitakuwa nimekukosea kwa kukuelekeza katika blogu ya tarishi hauwawi upate kuona mkasa mzima unaozunguka katika shauri hili la marehemu chacha wangwe aliyekuwa mbunge wa tarime kupitia chama cha chadema.

Naomba nenda tarishi.wordpress.com ujionee habari ambazo huenda zikakushtua kama sio kukuliza au kukufanya utafakari upya mambo mengi.

Thursday, August 14, 2008

Hatimaye tume ya Muhimbili imeundwa leo

SERIKALI imeunda Tume maalumu ya wataalamu watano kuchunguza tukio la mauaji lililofanywa na mgonjwa wa akili Jumatatu wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam.
Agosti 11, mwaka huu, mgonjwa wa akili David Denge (21), aliyekuwa amelazwa Muhimbili akitokea Hospitali ya Mwananyamala, Kinondoni, aliwaua wagonjwa wenzake wawili wa akili na kuwajeruhi wengine watano kwa chuma kinachotumika kutundika chupa ya kuongezea maji mwilini.
Tume hiyo inayoanza kazi Jumatatu ijayo, imepewa wiki mbili kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na itafanya kazi chini ya Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara hiyo ambaye atahakikisha Tume inapata msaada unaohitajika.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa alisema Wizara imeunda tume hiyo ili kubaini mazingira yaliyochangia kutokea kwa tukio hilo na kisha kutoa taarifa kwa umma na mapendekezo ya kuzuia tukio hilo lisirudiwe
Alisema tume hiyo itakuwa na wajumbe watano ambao wawili watatoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao ni Dk. Joseph Mbatia na Jovin Lyimo, Nassoro Mnambila kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Joviter Katabaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe mwingine kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye jina lake litapatikana baadaye.

kama bunge vile huku je, Mahakama ya Kadhi

Shauri la uwapo au kutakuwapo kwa Mahakama ya Kadhi limesumbua Bunge wakati wa mjadala wa Wizara ya Katiba na Sheria .
Muda mwingi ulitumika kuonyesha hisia kuhusu mahakama hiyo huku upande mmoja ukidai haki ya kikatiba katika kukamilisha ibada huku upande mwingine ukisema suala la ibada lisitumbukizwe kuwa maalum na lichangiwe na kila mtu.
Katika utoaji maoni hayo, wabunge ambao ni Wakristo walipinga kuundwa kwa mahakama hiyo wakisema inaweza kuwa chanzo cha vurugu nchini.
Wabunge Waislamu nao walitetea kwa nguvu uundwaaji wa mahakama hiyo wakisema wananchi hawana haja ya kuwa na wasiwasi kwa vile itakuwa inashughulikia masuala yanayowahusu Waislamu tu.
Awali, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alipowasilisha makadirio ya Wizara yake, alisema Tume ya Kurekebisha Sheria imekamilisha utafiti kuhusu uundwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini na imekwisha kuwakilisha taarifa ya mapendekezo yake serikali kwa mujibu wa sheria.
“Hivi sasa serikali inaitafakari kabla ya kufanya maamuzi. Bunge litafahamishwa uamuzi wa serikali mara tu utakapotolewa,” alisema.

michango bado inahitajika kusafirisha mwili wa marehemu Jacob Castory Mpogole

Tafadhali ili tuweze kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania.Tafadhali pitieni habari kwa kufuata link au kusoma hapo chini, web-masters naomba muipandishe hii stori tafadhali.http://www.tzuk.com/index.php?option=com_content&task=view&id=2495&Itemid=105 Ndugu WATANZANIA mwili wa marehemu Jacob Castory Mpogole sasa upo tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Tanzania na mipango imeshafanywa ya kuusafirisha mwili mwisho wa Juma hili.Familia ya marehemu inashukuru kwa michango ambayo imetolewa hadi sasa ambayo kwa tathmini za mpaka jana usiku zilikuwa zimefikia £1300, lakini bado tunahitaji michango zaidi ili kuweza kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu katika muda uliopangwa, hivyo Watanzania wote na marafiki wa Tanzania mnaombwa kusaidi kuchangia chochote kile ili kufanikisha zoezi hili la kupeleka mwili wa marehemu katika sehemu yake ya mapumziko.Kikao cha mwisho kitafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 Agosti 2008.
Bank: LLOYDS TSB
Account Name: Mrs. Ummy H. Shella
Account Sort Code:77-91-09
Account Number:13923068
Kassim-07985488194
Ummy-07962338257
Abubakar Faraji
Swift Freights Uk Ltd.
Unit 62-8 Fountayne Road
London N15 4QL
United Kingdom
Tel:0208-801-9800
Mobile -07852260024

Salamu kutoka Cuba


Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Cuba wakati wa ziara yake nchini humo.Dk Shein aliwataka wanafunzi hao kuzitumia vyema nafasi hizo za masomo na baada ya kuhitimu warudi kulitumiakia Taifa lao.Nakushukuru mdau uliyeleta picha hii kwa sababu umenifanya kujua kwamba mpwa wangu bado anachakarika kuusaka udaktari wake mjini Havana. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

mwanamke mrefu kupita wote afariki dunia


Mwanamke mrefu ambaye alifikia futi saba na inchi saba amefariki akiwa na umri wa miaka 53.
Mwanamke huyo alifariki Indianapolisi Jumatano asubuhi.
Mwanamke huyo Sandy Allen, ambaye alitumia urefu wake kuwaelezea wanafunzi kwamba si vibaya kuwa tofauti na wengine amekufa akiwa katika nyumba ya wazee huko Shelbyville, Ind., mmoja wa marafiki wa mwanamke huyo,Rita Rose alisema.
Sababu ya kifo chake bado kujulikana ingawa Allen alishafikishwa hospitalini mara kadhaa akiwa na tatizo la sumu katika damu yake.Pia alikuwa na tatizo la kisukari, matatizo katika uvutaji pumzi na kushindwa kufanyakazi kwa figo zake.
Mjini London, msemaji wa Guinness World Records, Damian Field alithibitisha kwamba hadi Jumatano mwanamke huyo ndiye aliyekuwa anatambulika kama mwanamke mrefu zaidi duniani ingawa baadhi ya webu zimekuwa zikimzungumzia mwanamke wa Kichina ambaye ana urefu wa futi saba na inchi 9.
Imeelezwa tatizo la kansa lilifanya homoni za urefu kuzalishwa zaidi na hivyo alikuwa akiendelea kukua hadi pale alipofanyiwa operesheni ya kuzuia ukuaji wake mwaka 1977.
Allen ambaye alizaliwa Juni 1955 akiwa na uzito wa paundi 6-1/2 akiwa na miaka 10 alishakua kufikia futi 6 na inchi tatu na akiwa na miaka 16 alikuwa na urefu wa futi 7 na inchi 1.
Pichani Sandy Allen akiwa na Will Denk, katika picha iliyopigwa Septemba 2,1995 katika maktaba iliyopo Shelbyville, Ind.,

Wednesday, August 13, 2008

Dk Shein awasili nchini baada ya ziara ndefu ughaibuni


Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akitoka nje ya chumba cha kupumzikia wageni (V.I.P) kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mara baada yakuwasili nchini leo akitokea katika ziara za kikazi nchini Mexico na Cuba. Picha hii ni ya Amour Nassor wa Ofisi ya Makamu wa Rais. Welcome back sir

Wahadhiri sasa kuketi hosteli za wanafunzi Mlimani

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), umebadilisha matumizi ya hosteli walizokuwa wakiishi wanafunzi eneo la Ubungo na sasa zitakuwa zinakaliwa na wahadhiri wa chuo hicho.
Habari zilizothibitishwa na uongozi wa chuo hicho, zinaeleza kuwa wanafunzi takriban 220 wanaokaa katika hosteli hizo Julai mwaka huu, walipewa taarifa za kuhama katika hosteli hizo ifikapo Septemba mosi kupisha walimu wao.
Majengo matatu ya hosteli hizo yana vyumba 36 kwa kila jengo na uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 220. Hosteli hizo hutumiwa zaidi na wanafunzi wanaosomea Shahada ya Uzamili.

Tsvangirai ataka muda kutafakari

Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai amesema kwamba anahitaji muda kufikiri, hali ambayo imesababisha kuahirishwa kwa mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Zimbabwe.
Mazungumzo yaliyoanza Jumamosi iliyopita yanaonekana bado ni mazito.
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amesema kwamba Morgan Tsvangirai ameomba muda ili kuweza kutafakari.
Thabo Mbeki amesema hayo huku kukiwa na tetesi kwamba Rais Robert Mugabe alikuwa amefikia mwafaka na kundi jingine la MDC ambalo lilijiondoa katika MDC ya Morgan Tsvangirai.
Mbeki jana alitarajiwa kuondoka nchini Zimbabwe kuelekea Angola baada ya kuwapo nchini humo kwa siku tatu za mazungumzo.
Rais huyo wa Afrika Kusini amesema kwamba amepania kuhakikisha kwamba anasaidia kuondoa matatizo ya wananchi wa Zimbabwe.
Mazungumzo hayo ambayo yamelenga kuzaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yanamshirikisha Rais Robert Mugabe, Morgan Tsvangirai na Arthur Mutambara.

Wakenya wameishtukia ishu ya tuisheni

SERIKALI ya Kenya imepiga marufuku wanafunzi kupelekwa katika masomo ya ziada (tuisheni) wakati wa likizo, shirika la Utangazaji la BBC limetangaza.
Kauli hiyo imetolewa dhidi ya shule zote ziwe za binafsi au za umma.
Serikali imesema kwamba inakuwa na mashaka makubwa ya afya ya akili ya wanafunzi kwa jinsi wanavyorundikiwa kazi hata wakati wanapostahili kupumzika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Karega amesema kwamba wanafunzi hao wanastahili kupumzika wakati wa likizo zao na si kufanyakazi ya ziada .
Mashaka hayo yameelezwa baada ya wanafunzi katika sekondari zipatazo 300 kufanya ghasia.
Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sababu za ghasia hizo wamesema kwamba wanafunzi wengi wamekuwa wakilalamikia mzigo mkubwa wa masomo na kipindi kirefu cha kujifunza.
wanafunzi 200 wameelezwa kukamatwa kufuatia ghasia hizo katika miezi michache iliyopita ambayo imesababisha hasara ya mamilioni kwa mali na majengo ya shule.
Uamuzi huo wa serikali umeungwa mkono na chama cha wazazi ambao wamesema kwamba hali hiyo itasaidia wanafunzi kupumzika baada ya mitihani.
Aidha wazazi wamekuwa wakilalamika kwamba ada ya tuisheni ilikuwa kubwa mno na inayosumbua.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu cha Kenya (KNUT) amepongeza hatua hiyo.
"Hali ya muda wote kusoma na hakuna kupumzika na kucheza kunamfanya mwanafunzi kuwa mjinga," anasema Mwenyekiti huyo wa KNUT , David Wesonga.
"Wazazi pia wanahitaji muda wa kucheza na watoto wao baada ya masomo," anasema Cleophas Tirop, Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wakuu wa Sekondari nchini Kenya (KSSHA).
Hata hivyo serikali imesema kwamba kwa wanafunzi ambao ni dhaifu wataandaliwa mpango maalumu utakaokuwa unasimamiwa na serikali yenyewe.

Mwakyusa asema anaunda tume Muhimbili



Kinara wa Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii Profesa Mwandosya amesema kwamba ataunda tume kujua kulikuwa na tatizo gani mpaka maafa yakaikumba Muhimbili kwa mgonjwa wa akili, David Donge kushambulia wagonjwa wenzake na kuua wawili.

Mgonjwa huo aliyelazwa na wenzake leo alifikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji.

Tangazo la kuunda tume amelitoa baada ya kuwatembelea wagonjwa wanaotibiwa majeraha wadi ya Kibasila namba 13 . Wagonjwa hao ni Maurice Oyana (20) na Peter Milanzi (20); wagonjwa wengine Hamis Mohammed (41) na Athuman Abdallah (23) walilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI) katika hospitali hiyo na hali zao si nzuri.
Akizungumza baada ya kutembelea wagonjwa hao, Waziri Mwakyusa alisema amezungumza na uongozi wa hospitali hiyo katika vitengo vyote na kupata maelezo kuhusiana na tukio hilo, lakini kutokana na uzito wa tukio lenyewe, imemlazimu kuunda tume.

habari mbaya kwa wanaokwenda Msumbiji kupitia Ruvuma

KIVUKO cha Kilambo kinachovusha abiria na mizigo kutoka Tanzania kwenda nchi jirani ya Msumbiji katika Mto Ruvuma wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara kimezama baada ya kupata hitilafu.
Habari kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa kivuko hicho kilizama alfajiri ya Jumamosi ya wiki iliyopita, kikiwa katika maandalizi kuvusha abiria na mizigo kutoka upande wa Msumbiji kwenda Tanzania.
Habari hizo zilieleza kuwa wakati tukio hilo linatokea hakukuwa na abiria, wala mizigo ndani ya kivuko na kuzama kwake kulibainika baada ya wasimamizi kufanya ukaguzi wa awali kabla ya kuanza safari.
Fundi Msanifu Mwandamizi ambaye ni Msimamizi wa kivuko hicho, Janson Mbawala ambacho kinamilikiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), alikili kuzama kwa kivuko na kuongeza kuwa kulisababishwa na matangi matatu ya hewa kuzibuka na kuingiza maji.
“Baada ya kufanya ukaguzi wa awali kabla ya kuanza safari tukagundua upande mmoja wa kivuko umetitia……tulipochunguza zaidi tukagundua kuwa matangi matatu ya hewa yamezibuka na kusababisha maji kuingia ndani….tulikifunga kamba kuzuia kisizame chote hivyo tayari kuna mafundi kutoka makao makuu tunashirikiana kutengeneza,” alisema.
Alisema matengenezo ya kivuko hicho yatadumu kwa zaidi ya wiki moja na nusu, na kwamba hakukua na kitu wala mtu ye yote aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Pascal Mayalla akiwa hospitalini Muhimbili


Mwandishi wa habari na Mtangazaji Pascal Mayalla anaendelea vyema kwa mujibu wa mazungumzo ya Athuman Hamisi wa Habari leo na mimi kuhusiana hali ya mpiganaji huyu baada ya kupata ajali kule Dodoma. Athumani alipata nafasi ya kumuona mpiganaji huyu na kuzungumza naye na kuchukua foto hii kuwataarifu watu kwamba mambo yanaendelea vizuri kwa wastani tumuombee tu atoke salama.

Sasa Issa Michuzi anapanda kotekote

Wadau kwa taarifa yenu tu ni kuwa Issa Michuzi mwanakiji mzee sasa anapanda kote kote katika blogspot na katika www hayo ndiyo mambo ya mtandao. Ndio kusema unaweza kumpata katika www.michuzi-blog.com na pia ndani ya http://issamichuzi.blogspot.com nawatakia usomaji mwema na pia mambo mswano kwenye libeneke.

Leo ni besdei ya Mhariri wa habari wa HabariLeo


Wasaka nyoka na wafanyakazi wa HabariLeo leo walipiga hepibesdei kwa mkuu wa engine room ya Habarileo leo Mgaya Kingoba kama mnavyoona wanavyotoosi na mdau alikuwemo pia kusema long live Mgaya Kingoba na besdei njema

Hizi ni salamu rasmi kutoka kwa Issa muhidin Michuzi dc wa nanihii

WADAU WATUKUFU!

TAKRIBANA SIKU TATU ZIMEPITA NA www.michuzi-blog.com HAIKO HEWANI KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZA KIUFUNDI ZA HOST WETU BLOGGER-GOOGLE AMBAYE ANA MATATIZO YA KUUNGANISHA FTP SERVER YAKE NA GLOBU KIBAO IKIWEMO HII YA JAMII. HIVYO WAKATI TUKISUBURI MAMBO YAKAE SAWA MUDA SI MREFU UJAO, LIBENEKE LINAENDELEA KULE KWA ZAMANI AMBAKO NI www.issamichuzi.blogspot.com.

NAOMBA RADHI KWA CHANGAMOTO HII AMBAYO IKO NJE YA UWEZO WETU NA WAHANDISI WA GOOGLE WAMENIHAKIKISHIA KWAMBA MAMBO YATAKUWA MSWANO PUNDE TU NA WAMEOMBA UVUMILIVU WAKATI HUU AMBAPO WANATAFUTA SULUHISHO LA KUDUMU ILI KWIKIWI ISITOKEE TENA HUKO MBELENI.

SAMAHANI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOPATIKANA

MUHIDIN ISSA MICHUZI

BBC Idhaa ya Kiswahili na ulimwengu wa soka


BBC Idhaa ya Kiswahili, kama kawaida inaendelea kutoa burudani ya soka isiyo na kifani kwa mashabiki waliopo Afrika Mashariki na Kati kupitia kipindi chake maarufu, BBC Ulimwengu wa Soka.
Kikosi kizima cha BBC Ulimwengu wa Soka - Alex Mureithi, Charles Hilary, Idd Seif, Hassan Mhelela, Peter Musembi and Salim Kikeke, kitakuletea maelezo na matokeo ya mechi zote za ligi kuu ya soka ya England msimu huu, inayoanza Jumamosi Agosti 16.
Katika kuanza msimu, BBC Ulimwengu wa Soka itakutangazia moja kwa moja mchezo kati ya Hull itakayocheza na Fulham, kwenye uwanja wa KC. Matangazo ya mchezo huo yataanza saa kumi na nusu Afrika Mashariki.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Solomon Mugera anasema: " Tulianza matangazo ya moja kwa moja ya ligi kuu ya England mwaka 2006. Wasikilizaji wetu wanatuambia kipindi cha BBC Ulimwengu wa Soka kimewanufaisha kupindukia, kuwaburudisha na kufuatilia vilivyo mechi za soka, na kwa lugha wanayoielewa vyema ya Kiswahili. Tutatangaza tena msimu huu wote, na nina hakika wasikilizaji wetu watafurahia sana".
Jinsi ya kupata matangazo ya BBC Ulimwengu wa Soka:
Nchini Burundi, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Bujumbura kupitia 90.2 FM, na katika 105.2 FM kwa maeneo mengine.
Nchini Kenya, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana kupitia redio washirika - Radio Simba mjini Nairobi katika 102.7 FM, Sheki FM mjini Mombasa katika 106.6 FM na kupitia West FM mjini Bungoma katika 94.9 FM.
Nchini Rwanda, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Kigali katika 93.9 FM, mjini Butare katika 106.1 FM, na mjini Kibuye katika 93.3 FM.
Nchini Tanzania, BBC Ulimwengu wa Soka inapatikana mjini Zanzibar katika 94.1 FM na Pemba katika 93.5 FM. Vilevile unaweza kupata matangazo haya kupitia radio washirika: Radio Free Africa mjini Dar Es Salaam katika 98.6FM, Mwanza katika 89.8FM, Shinyanga katika 88.2FM, Kagera katika 94.1FM, Arusha katika 89.0FM, Mbeya katika 88.8FM, Dodoma katika 89.0FM, Rukwa katika 89.1FM, Ruvuma katika 89.6FM, Mtwara na Lindi katika 89.0FM, Singida katika 88.3FM, Iringa katika 93.5FM, Tanga katika 99.3FM, Tabora katika 90.0FM, Kigoma katika 90.0FM, Morogoro katika 93.8FM, Kilimanjaro katika 88.2FM, Mara katika 93.5FM na katika 1377 AM/MW kwenye maeneo yote Tanzania.
Pia kupitia Radio One mjini Dar Es Salaam katika 89.5 FM, Arusha katika 95.3 FM, Dodoma katika 100.8 FM, Mwanza katika 102.5 FM, Moshi katika 1323 AM na katika 1440AM kwenye maeneo mengine yote. Radio 5 mjini Arusha katika 105.7 FM, na Sky FM katika 101.4 mjini Dar es Salaam.
BBC Ulimwengu wa Soka pia inapatikana kote Afrika Mashariki na Kati kwenye masafa Mafupi katika 11705 kHz,
na vilevile kwenye tovuti:
http://www.bbcswahili.com/
BBC Idhaa ya Kiswahili pia itakuletea matangazo ya mechi zifuatazo:
Jumamosi, Agosti16, 2008 Hull v Fulham
Jumamosi, Agosti 23, 2008 Liverpool v Middlesbrough
Jumamosi, Agosti 30, 2008 Everton v Portsmouth
Jumamosi, Septemba 13, 2008 Blackburn v Arsenal
Jumamosi, Septemba 20, 2008 Liverpool v Stoke
Jumamosi, Septemba 27, 2008 Man Utd v Bolton
Jumamosi, Oktoba 04, 2008 Chelsea v Aston Villa
Jumamosi, Oktoba 18, 2008 Liverpool v Wigan
Jumamosi, Oktoba 25, 2008 Tottenham v Bolton
Jumamosi, Novemba 01, 2008 Chelsea v Sunderland
Jumamosi, Novemba 08, 2008 Man City v Tottenham
Jumamosi, Novemba 15, 2008 Arsenal v Aston Villa
Jumamosi, Novemba 22, 2008 Chelsea v Newcastle
Jumamosi, Novemba 29, 2008 Tottenham v Everton
Jumamosi, Disemba 06, 2008 Bolton v Chelsea
Jumamosi, Disemba 13, 2008 Tottenham v Man Utd
Jumamosi, Disemba 20, 2008 Arsenal v Liverpool
Ratiba hii inaweza kubadilishwa wakati wowote na mamlaka husika. BBC haihusiki na mabadiliko hayo.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na: Solomon Mugera,
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC
solomon.mugera@bbc.co.uk
Christine George,
Assistant International Publicist,
BBC World Service
+44(0)207557 1142;
christine.george@bbc.co.uk

Tuesday, August 12, 2008

Mdau