Friday, October 31, 2008

SBL watoa udhamini kwa mshiriki wa Mr Universe







Mtunisha misuli hapa nchini David Nyombo amepata udhamini kamambe ambao utamuwezesha kushiriki katika mashindano ya watunisha misuli wa Dunia Mr. Universe yatakafanyika Bahrain kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 7,mwaka huu.
Udhamini huo umetolewa na kampuni ya bia ya Serengeti .
Udhamini huo umetangazwa wakati Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Teddy Mapunda alimkabidhi mwanamisuli huyo vifaa vyake katika hafla iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Dar es Salaam.
Pichani ni Teddy Mapunda akimkabidhi vifaa vya Michezo vyenye David Nyombo , picha nyingine akishindana kutunisha misuli na Bingwa wa Afrika mwaka 2008, David Nyombo,na tatu waandishi wa habari wakipata dawa baada ya kazi katika hafla hiyo ya kutoa udhamini kupitia kinywaji cha Vitamalt Plus .

Duu mabalozi wa Zain wakiwa kazini


Mabalozi wa Zain bwana Issa Michuzi na bi Lady Jay Dee wakiwa katika uzinduzi wa Kanga mpya ya Zain, Dar es Salaam,hivi karibuni.

Kufa si rahisi lakini cha moto....


Wakazi wa Mbagala kufa hawafi lakini cha moto wanakipata . Kwa muda sasa maji yanakuwa na mgogoro kutokana na ujenzi wa barabara ya Kilwa ambao umetafuna mabomba yaliyopo. Naam wataalamu walitakiwa kujua kwamba mabomba hayo yanazikwa pande hii na pande ile yakiwa na umbali wa kutosha kutoka barabarani. Lakini wataalamu wetu hawakufanya hivyo, wao walikuwa wanaona miaka miwili tu hawajui kwamba ipo siku kitu fulani kitahitajika. Tutajifunza lini mipango miji. Picha hii ni mali Albart Jackson.

Thursday, October 30, 2008

Wanajeshi waliokuwa Anjouan warejea wote

KUNDI la mwisho la Wanajeshi wa Tanzania waliobaki katika kisiwa cha Anjouan kuimarisha ulinzi na kusimamia uchaguzi limerejea nchini wiki hii.

Taarifa iliyosainiwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo imesema.

Akizungumza na Wanajeshi hao katika Kambi ya Jenerali Twalipo Mgulani jijini Dar es Salaam Kamanda huyo aliwapongeza wanajeshi wote walioshiriki kukikomboa kisiwa hicho.

Shimbo alisema operesheni hiyo pekee ya Umoja wa Mataifa (AU) ilifanyika kwa mafanikio na kuiletea sifa Tanzania ambayo iliongoza operesheni hiyo.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuiletea sifa nchi yetu kwa kumn’oa Muasi Kanali Mohamed Bacar,kuimarisha ulinzi baada ya operesheni na kusimamia vyema uchaguzi wa Rais wa kisiwa hicho”Alisema Mnadhimu Mkuu

Alisema operesheni hiyo imesaidia JWTZ kupata uzoefu katika mambo mbalimbali ya ulinzi wa amani ikiwemo kushirikiana na majeshi mengine likiwemo Jeshi la Polisi na kujifunza kuwa operesheni za pamoja zinahitaji umakini ,kujitolea na busara katika utendaji wakati wote wa kutekeleza jukumu.

Alisema Tanzaniakwa sasa imeandaa kundi la kwanza lililopo Msata Pwani kwa ajili ya kushiriki katika ulinzi wa amani katika jimbo la Darfur Sudan huku kunci jingine litakaloshiriki katika ulinzi wa amani linaandaliwa na Brigedia ya Kusini na kundi la tatu linaandaliwa na Brigedia ya Zanzibar.

Kamanda Shimbo alisema Brigedia ya Kaskazini yenye makao makuu mkoani Arusha inajiandaa kwa ajili ya kushiriki katika zoezi la jumuia ya Ushirikiano wa Nzchi za Kusini mwa Afrika (SADC) litakalofanyika mwakani nchini Afrika Kusini

Tanzania ilishiriki katika Operesheni Demokrasia nchini Comoro mwechi Machi ambapo JWTZ iliongoza majeshi ya Umoja wa Afrika kumng’oa Muasi Kanali Mohamed Bacar.

Ilivyokuwa siku wastaafu walipoipararaizi njia ya wakubwa
















Picha hizi ni mazingira yalivyokuwa siku ya mgomo wa staili yake wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ilivunjika mwaka 1977. picha hizi ni kwa hisani ya Jackson Albart wa kampuni ya Ladyband

Wednesday, October 29, 2008

mama Kikwete nchini Japan


WAMA Chairperson Mama Salma Kikwete look at pupils learn through computers when she visited Li Yuan primary school in Shenzhen city,China yesterday.Mama Kikwete is in China for a five days working visit to China at the invitation of Huawei Technologies company with its headquarters in Shenzhen City,China.photo by Freddy Maro.

salenda bridge wazee wazuia magari, Kigamboni kivuko chaparamia gati

Leo ni siku mbaya kabisa katika jiji la Dar es salaam lakini kwa jiji la watu zaidi ya milioni tano pengine hawajui kumetokea nini.Leo makubwa mawili ya asubuhi chapchap yametokea.
Moja ni wazee wastaafu ambao hawajalipwa fedha zao za kiinua mgongo sijui au malipo gani yalabi, manake hii shida wakati mwingine hata hujui malipo gani hayajalipwa manake yapo mengi, walijilaza pale Salenda bridge na kuzuia magari yote yanayotoka mjini na kuingia mjini katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.Mishe mishe hiyo ilianza saa 12 na nusu na wakaja kuondolewa kwa nguvu na polisi majira ya saa mbili, foleni ya magari ni mpaka
mwenge utajaza.
Tukio la pili ni la Mv Kigamboni kuparamia gati.
Kutokana na Mv Kigamboni kuparamia hilo gari majira ya asubuhi, maelfu ya wakazi wa
Kigamboni, Kibada,Mji mwema, Ungindoni, Kongowe na wanaotumia kivuko wakitokea maeneo ya Mbagala Kijichi, Mbagala Kiburugwa, MbagalaKuu MbagalaRangi Tatu ambao wanashindwa
kutumia barabara ya Kilwa kutokana na kuharibika kwa kipande cha barabara ya Kilwa
eneo la msikitini hadi katika Mto kizinga kwenye deviation ya daraja walijikuta wanapambana
kuwahi kazini kwa kutumia Mv Alina.
Haikuwezekana maofisa wanaokatisha tiketi kudhibiti watu ilibidi maa MP yaani wale polisi wa jeshi na Polisi wenyewe tena wenye ngazi za maofisa kuanza pilikapilika za kudhibiti wananchi hasa baada ya kujikuta wakilazimika kusaidia wakazi walitumbukia katika maji katika
patashika za kuwania kivuko.
Pamoja na crude way waliyotumia kuzuia watu, manake kila mtu anataka kuingia katika kivuko
bila mpangilio,kuwapo kwao kulisaidia kumantain aina fulani ya oda.
Muda mrefu niliokuwa pale hakuna mtu anayeeleza kwa ufasaha nini
hasa kimesibu MV Kigamboni.Kila mmoja naasema lake na nadhidha hakuwa tayari kuongea.
Pamoja na kutotaka kuzungumza mtu wa kawaida unajiuliza hivi inakuwaje hasa kivuko
kinapoparamia gati?
Juzi niliongea na mtu mmoja kumuuliza MV Kigamboni ina matatizo gani
hasa? Hii ilitokana na ukweli kuwa nilicheza rumba nayo saa tatu usiku. Tukiwa tunatokea
mjini kabla ya kupiga gati, tukaona tunapelkwea kwanza kaskazini kisha haoo tukarejea
kusini kama tunataka kwenza Zenj baadaye Magharibi na dakika 15 baadaye wuuuhh ndio tukapiga nanga.
kama mazingira hayol ya juzi hayakupewa jibu ndio leo najikuta lazima nitumie utaratibu wa
kujitumbukiza katikati ya watu nifanikiwe kuvuka.
Mke wangu wakati tupo katikati ya mamia ya watu alisema angalia jiwe, sasa utaonaje jiwe manake kivuko kimefika na wtau wote wanajisukuma kwa mbele , nikachana kiatu manake nilipiga teke jiwe katika harakati za kujizuia nisipelekwe baharini.
Naam, hayo ni baada ya kuangalia MV Kigamboni ambayo inaonekana kama muda si muda itaishiwa principle ya kuelea ya displacement manake ina matundu fulani ambayo sidhani kama ni ya meli ya makusudi halafu ukitazama ule ulaji wa kutu ahh yaani hata kama ndio meli lazima iwe na kutu hivi upana wa chuma bado upo kweli au ndio maana kinatembea pooooolepole, kuna mtu wa marine anaweza kuelezea mambo haya sijui.
Huku mvua zimeanza barabara ya Kilwa ikiwa tete ipo siku tutasikia kitu kibaya Kigamboni,
Mungu atunusuru na tuhurumie kwa kufikiria vibaya, lakini scientifically something bad is
about to happen, watch out!!! eti hivi vivuko vina miaka mingapi?
Halafu nashindwa kuamini hivi ni kweli lakini, nadhani unafahamu nashindwa kuamini nini.Bahati mbaya sikuwa na kamera manake misele ya asubuhi wakati mwingine
hata vya kuazima mtu unasahau.

Tuesday, October 28, 2008

Dar es Salaam kumezwa na bahari


JIJI la Dar es salaam ni kati ya miji mikuu 19 Barani Afrika ambayo imo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uongezeko la kina cha maji ya bahari kunakosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Hayo yamo katika ripoti ya mwaka 2008/09 ya hali ya miji mikuu duniani (State of the World’s Cities), taarifa ambayo imeziduliwa mbele ya waandishi wa habari, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, (UN- HABITAT) Bibi Anna Tibaijuka.

Ripoti hiyo ambayo hutolewa kila miaka miwili inaonya kuwa ni miji mikuu michache sana iliyoko katika ukanda wa bahari itakayonusurika na janga hilo.

Pamoja na Dar e s salaam, miji mikuu mingine ambayo imo katika hatari ya hiyo na hata kutoweka kabisa ni pamoja na Abijani, Accra, Alexandria, Algiers, Capetown, Casabalanca, Dakar, Djibout, Durban, Freetown, Lagos, Libreville, Lome, Luanda, Maputo, Mombasa, Port Louis na Tunis.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa UN-Habitat, Anna Tibaijuka, anatoa wito kwa serikali zote kutoa kipaumbele katika kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na tishio hilo lilodhahiri la mabadiliko ya yali ya hewa.

Anasema serikali za mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea yote yanakabiliwa na hatari hyo, hivyo zinatakiwa kuzingatia masuala ya mipango miji endelevu na inayoweka mbele maslahi ya watu maskini ambao ndio watakaoathirika zaidi kutokana na athati hizo za kuharibiwa kwa mazingira na ongezeko la joto duniani.

Taarifa hiyo inafafanua na kubainisha kwamba si muda muda dunia itaanza kushuhudia madhira ya mabadiliko ya hali ya hewa , na hasa katika wakati huu ambao zaidi ya asilimi 50 ya watu wanaishi katika miji.

Na kwamba hali itakuwa mbaya zaidi kwa afrika kwa kuwa haina mipango mkakati madhubuti ya kukabiliana na majanga ya kibinadamu na hasa yale yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa hii ambayo walengwa wake ni waandaaji wa sera na wahusika wa mipango miji, pamoja na mambo mengine inalenga kutoa tahathari kwa kuonyesha ni miji mikuu ipi ambayo katika hatari kubwa ya kuathirika na ongezeko la kina cha maji na ni jumuia zipi zinazoweza kutoweka kabisa katika uso wa dunia.

Kwa mujibu wa taarifsa hiyo, katika karne iliyopita ya 20, ilikadiriwa kuwa kina cha maji kiliongezeka kwa sentimeta 17, na kwamba inatarajiwa kuwa kati ya mwaka 1990 hadi 2080 kina cha maji kitaongezeka kati ya sentimeta 22 na 34.

Aidha taarifa hiyo , inaeleza zaidi kwamba kuna miji mikuu3,351 ulimwenguni ambayo aidha iko yako chini ya usawa wa bahari, au haiku mbali sana na usawa wa bahari, na kwamba asilimia 64 ya miji hiyo iko katika nchi zinazoendelea.

Huku Asia ikiwa na zaidi ya nusu ya miji mikuu hiyo na ambayo yako katika hatari kubwa, ikifuatiwa na Bara la Amerika na Caribbean lenye asilimia 27 ya Miji Mikuu, na Afrika ikiwa na silimia 15.

Aidha Bara la Ulaya lina robo tatu ya miji mikuu, huku moja ya tano ya miji yote katika America ya Magharibi iko chini ya usawa wa bahari.Pamoja na kuonesha ni miji mikuu ipi itakayoathiriwa na ongezeko hilo la kina cha maji, taarifa hiyo pia inaelezea hali halisi ya ukuaji wa miji mikuu, idadi ya watu inaoingia katika miji hiyo, hali ya huduma za jamii , lakini pia inaainisha utofauti wa makazi uliopo kati ya watu matajiri, wa kipato cha wastani na maskini kabisa.

Aidha ripoti hiyo inaonyesha kwamba katika kila watu watatu katika nchi zinazoendelea, mmoja anaishi katika makazi duni (slums) Taarifa hiyo pia inabainisha kwamba karibu watu milioni tatu kila siku wanaingika katika miji mikuu na miji hususani katika nchi zinazoendelea.

Inaonyesha taarifa hiyo kwamba ifikapo kati kati ya karne ya 21 idadi ya watu wanaoishi katika miji mikuu katika nchi zinazoendelea itaongezeka maradufu kutoka watu bilioni 2.3 mwaka 2005 hadi bilioni 5.3 ifikapo mwaka 2050 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bara la frika na kama hali hii ya watu kukimbili kuishi katika majiji na miji mikubwaitaendelea, basi ifikapo mwaka 2050 idadi ya kubwa ya watu wake itakuwa inaishi katika miji mikubwa, huku kukiwa na watu 1.2 bilioni watakaokuwa wakiishi katika majiji na miji hali itakyoifanya afrika kuwa na robo ya watu wote duniani wanaoishi katika miji mikuu.
Mwisho.


Na Maura Mwingira, NewYork,Marekani

HUAWEI TO SUPPORT WAMA'S EDUCATION PROGRAMMES


The Wanawake Na Maendeleo (WAMA) Foundation and the Chinese HUAWEI Technologies Company have signed a memorandum of understanding in which the company will support WAMA's education programs by providing Electronic learning, E-learning, in its model schools in Nyamisati ward, Rufiji district, and Coastal region.

The signing ceremony took place at HUAWEI Technologies Headquarters in Shenzhen city in China yesterday whereby the new WAMA executive Secretary Daudi Nassib and HUAWEI Tanzania Chief Executive officer, Evan Zou signed the MOU documents and exchanged the notes in the presence of WAMA chairperson Mama Salma Kikwete and HUAWEI Executive Vice President, Qu Wenchu.

The First Lady is China for a five days working visit at the invitation of the HUAWEI Technologies Company.

Speaking shortly after the signing ceremony, WAMA chairperson Mama Salma Kikwete said that her organization seeks to enhance educational opportunities for the girl child, vulnerable children and women and that the new technologies provided by HUAWEI has the best potential to help her foundation achieve this Endeavour.

"WAMA and HUAWEI have agreed in principal to collaborate in the area of education and communication. We believe that, based on your experience in communication, you will help WAMA realize its long term dream of providing E-Learning in WAMA model schools", she said.

Mama Salma said the Electronic learning technology will provide the girl child and other vulnerable children with the much needed platform to enjoy quality education and access development opportunities adding that in the long term, it will improve public related services and social welfare of the people of Tanzania.

On his part, the HUAWEI executive Vice president Qu Wenchu said that his company will collaborate closely with WAMA in supporting the education programs and is ready to work closely with the Tanzanian government on e-Government implementation to enhance quality delivery of public service in Tanzania.

Huawei is one of the Worlds leading Telecommunications Company focused on building long term partnerships with Telecommunications operators.The Company started its operations in Tanzania on March 2000 and has 450 employees presently 70 percent of whom were recruited locally.

Ends


In the Picture: New Wanawake na Maendeleo(WAMA) Executive Secretary Mr.Daudi Nassib(left) exchanged the documents with Huawei Technologies Company,Tanzania Executive Officer Mr.Evan Zou,shortly after the two signed a memorandum of understanding in which Hawei will support WAMA's educational programmes on E-learning.The signing ceremony took place at the company's headquarters in Shenzhen city in China and was witnessed by WAMA's chairperson Mama Salma Kikwete(second left) and HUAWEI's Executive Vice President Mr.Qu Wenchu(third left)(photo and stoy by Freddy Maro)

Monday, October 27, 2008

jamani mafuriko uwanja wa Taifa







Rafiki yangu Feruzi Maganga, mwananchi namba moja ameniletea picha hiizii kuelezea Rahaaa ya ushindiiii. Si unajua baada ya miaka mingapi takribani nane hivi, Yanga ndio inapumua. Simba inashangilia kandanda na Yanga inashangilia kuondoa uteja na ama hakika Maganga sina la kusema hiyo ndiyo raha yake, Thanks man Raha ya ushindi.

Sunday, October 26, 2008

Yanga yamaliza uteja kwa Simba


KELELE, nderemo na milio ya honi magari vilifunika anga la Dar es Salaam baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya watani wao wa jadi Simba baada ya ukame wa miaka kibao.
Bao la mapema la Mkenya, Benard Mwalala lililojazwa wavuni dakika ya 16 lilitokana na krosi safi ya mchezaji wa zamani wa Simba, Athumani Iddi. Mpira uliozaa bao hilo ulianzia kwa mfungaji hodari wa Yanga Boniface Ambani.
Mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Simba ni Agosti 5 mwaka 2000.
Pamoja na mchezo bomba, mchezo huo ambao ulishuhudia kadi tatu nyekundu zikitolewa na mwamuzi Victor Mwandike.
Mchezaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ alikuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 63 kutokana na kumpiga kiwiko mchezaji mmoja, wakati mfungaji wa bao pekee la Yanga Mwalala naye alionyesha kadi hiyo dakika 72 Wakati akiondoka uwanjani ili kumpisha Kigi Makasi lakini alijichelewesha na kumsababisha beki wa Simba Meshack Abel kumsukuma hivyo wote kutolewa kwa kadi nyekundu.
Hali hiyo ilisababisha Simba kumaliza mchezo wakibaki uwanjani wachezaji 8 na Yanga 10, pamoja na kubaki pungufu Simba bado walionekana kucheza na kusaka bao la kusawazisha lakini wachezaji wake Musa Hassan ‘Mgosi’ alipoteza nafasi kadhaa za wazi za kufunga pamoja na Nico .

Katika hatua nyingine mchezo huo wa watani hao wa jadi leo ulijaa vitendo ambavyo vilikuwa vinashiria imani za ushirikina na kupelekea mpira kusimama kwa dakika kadhaa pale mchezaji wa Simba Ulimboka Mwakingwe kwenda golini mwa Yanga na kutoa vitu na kuvitupa nje na kuibua mayowe kwa mashabiki wa Simba na kufanya wapiga picha kukimbilia kupiga picha vitu hivyo.
Na kabla ya mpira kuanza Simba ilingia kwa staili ya aina yake pale Mwenyekiti wa timu hiyo aliongoza na mchezaji Mgosi na kwenda moja kwa moja kwenye goli moja huku akipiga danadana.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema kuwa timu yake ameridhishwa na kiwango cha timu yake na ushindi wa bao 1-0 unatosha baada ya kuwa katika shinikizo kubwa la kutakiwa kushinda kutoka kwa viongozi na mashabiki wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikifungwa kwa muda mrefu na Simba.
Wakati kwa upande wa Simba , kocha Benzink alisema mchezo ulikuwa mzuri na kikosi chake kilicheza vizuri mno na kupata nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake walishindwa kuzitumia na wapinzani wao walitumia nafasi hiyo moja ya shambulizi la kushtukiza kupata bao ambalo limewafanya waibuke na ushindi.
Aidha kocha huyo alisema hakuwatumia wachezaji wa timu hiyo kutoka Nigeria Orji Obina na Emeh Izechukwu kutokana na wachezaji hao kutofanya mazoezi kwa sababu ambazo hazijui.

Pichani ni Ulimboka na George Owino wakichuana vikali. Habari kwa hisani ya Betram Lengama ambaye alikuwa uwanjani na picha ni ya Bongo Pix

JK atembelea New Tabora Textille na kuonya mishahara midogo ni chanzo cha migororo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya kuwa tabia ya baadhi ya waajiri nchini kuwalipa mishahara kidogo wafanyakazi wao itazua migogoro kati yao na wafanyakazi wao.
Amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuwa waajiri wanawakabidhi wafanyakazi mashine za mamilioni ya fedha, ili wazilinde na kuzitumia, lakini wakati huo wanawalipa mishahara “kiduchu”.
Rais Kikwete ametoa onyo hilo leo, Jumapili, Oktoba 26, 2008 wakati alipokagua kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha New Tabora Textille Mills cha mjini Tabora, na kuzungumza na wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho, katika siku ya nne ya ziara yake ya siku nane mkoani Tabora kukagua shughuli za maendeleo.
Rais Kikwete ameuambia uongozi wa kiwanda hicho: “Ni jambo gumu kidogo kueleweka hili. Mnawakabidhi wafanyakazi wenu mashine na mitambo ya mamilioni ya fedha, lakini bado mnawalipa mishahara kiduchu.”
Amesema Rais: “Msibane maslahi ya wafanyakazi. Mnaweza kuwalipa mishahara kidogo kwa muda, lakini hatimaye hili litawaingiza katika migogoro na wafanyakazi wenu wenyewe.”
Hata hivyo, Rais ameusifia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuonyesha mfano wa nini kinatakiwa kufanywa na viwanda vya nguo nchini.
“Nashukuru na kuwapongeza sana kwa sababu nyie mmeonyesha mfano. Tusiishie kwenye kuchambua pamba tu, tusiishie kwenye ginnery tu. Hatua inayofuata sasa ni kutengeneza nyuzi na hatimaye kutengeneza nguo hapa hapa nchini,” amesema Rais na kuongeza:
“Kwa sababu tunaposafirisha na kuuza pamba nje, tunachofanya ni kumpelekea malighafi mwenye kiwanda kama hiki hiki cha hapa.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Tusijisifie kwa uhodari wa kuwa na viwanda vingi vya nguo na kuuza pamba yetu nje ya nchi. Tuanze sasa safari ya kutengeneza nguo. Lazima tuongeze thamani kwenye malighafi yetu. Nyie mnajua kuwa kilo mbili tu za pamba zinatengeneza shati moja?
Uongozi wa kiwanda umesifia sera za ubinafsishaji na kusema kuwa bila sera hizo, kiwanda hicho kingeendelea kufungwa hata kama mpaka sasa kinazalisha kwa asilimia 50 tu ya uwezo wake.
Kiwanda hicho kilichojengwa mwaka 1981 kikiwa kiwanda cha umma, kilifungwa mwaka 1981 kutokana na matatizo ya menejimenti. Hakikufunguliwa tena hadi mwaka 2004, kiliponunuliwa na watu binafsi.
Tokea wakati huo zaidi ya dola za Marekani milioni tatu zimewekezwa katika kiwanda hicho ambacho kinaajiri watu 355 ambao wanafanya kazi kwa shifti tatu. Kiwanda hicho kinatumia kati ya marobota 900 na 1,000 ya pamba.
Mpaka sasa kiwanda hicho kinasafirisha nyuzi kwenda Italia, Ureno, Uturuki, Colombia na China. “Tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira mazuri yanayotuwezesha kuendelea na uzalishaji katika kiwanda chetu.
Baadaye leo, Rais amezidua mradi wa josho na lambo la maji kwa ajili ya binadamu na mifugo na hata kufungia samaki katika kijiji cha Imalamihayo, nje kidogo ya mji wa Tabora.

Pinda azindua wiki ya usalama barabarani



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akijiandaa kukunjua kalenda iliyochapishwa na Baraza la Usalama Barabarani ikiwa inaonyesha alama mbalimbali za usalama barabarani mara baada ya kuzindua maadhimishi ya wiki ya Usalama Barabarani inayofanyika kitaifa Mkoani Morogoro kuanzia leo na kufikia kilele Novemba mosi mwaka huu

Morogoro kizaazaa kitupu




KITUO cha kupokea umeme wa gridi ya Taifa cha Shirika la Umeme Tanesco kilichopo Morogoro, leo alfajiri kimenusurika kuteketea kwa moto baada ya kutokea hitilafu katika moja ya chombo muhimu kinachopokea umeme huo na kuusambaza katikati ya Manispaa ya Morogoro.
Mafundi wa zamu walilazimika kutumia mitungi ya kuzimia moto kuudhibiti moto huo.
Chombo hicho cha transfoma kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamu kama 33kv Incomer Circuit Breaker kiliteketea. Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Bengiel Msofe alisema kwamba moto huo ulitokea majira ya saa 10 ya alfajiri baada ya chombo hicho kuzidiwa na kulipuka.
"Tukio hili limetulazimisha kukata umeme baadhi ya maeneo na kuyaacha yale muhimu kama Hospitali na Ikulu ndogo na tunajaribu kurekebisha tatizo hili mara moja kwa kusaidiana na mafundi wenzetu kutoka Dodoma ambao walikuwa Mang'ula kwa kazi nyingine nimewaarifu," alisema Msofe na kuongeza.
"Tuna akiba moja ya kifaa hiki, wenzetu wakifika tutasaidiana nao kufunga na kurudisha huduma ya umeme katika Mji wa Morogoro", aliongeza Msofe.
Hata hivyo, alisema mbali na hitilafu ya chombo hicho, upepo mkali uliombatana na mvua uliotokea juzi jioni katika Wilaya ya Morogoro, imesababisha nguzo nyingi za umeme kuanguka na nyaya kuninginia hovyo.
Upepo huo ulioambatana na mvua nyingi uliezua si tu nyumba, bali pia na kumbi za starehe na kuangusha miti ambayo imeziba njia.
Upepo huo ambao uliambatana na mvua iliyochukua takribani dakika 10 hadi 15 iliyoleta madhara makubwa kwa nyumba nyingi kuezuliwa na upepo na kuwafanya baadhi yao kusitiriwa na majirani zao.


Picha ni meneja huyo wa Tanesco akiangalia chombo hicho na picha nyingine ni vurumai za upepo zilivyoshughulikia jengo la starehe la Vijana Social habari na picha na John Nditi wa HabariLeo Morogoro

Friday, October 24, 2008

Life is so short, so...











Balozi wa TSN wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HabariLeo, Sundaynews na HabariLeo Jumapili Nelly Kamwelu akisalimiana nami wakati alipoingia katika ofisi ninazofanyia kazi kwa mwajiri wangu TSN hapa Samora. Alikuwa amefika hapa Oktoba 21 kuangalia hivi tunafanyaje hasa kazi zetu ili akatuwakilishe vyema. Picha nyingine ni pozi tu za mwanadada huyo.Picha hizi ni za Bernard Rwebangira.

Wakati nipo mgeni katika mambo ya habari


Wakati fulani unawakumbuka watu haklafu hujui uwapate namna gani. Lakini ni kweli kuwa wapo waliohai na wapo waliosafiri. Picha hii ni moja ya picha za zamani ambazo nilipiga wakati nikimaliza kozi ya ndani ya utangazaji.

Nilikuwa ndio kwanza mweupe kiasi katika masuala ya uandishi. Picha hii tulikuwa Mkurugenzi wa Radio tanzania wakati huo David Wakati, unaweza kumtambua pia Mkurugenzi wa maelezo kwa sasa Kassim Mpenda ambaye wakati huo alikuwa Mhariri Chumba cha habari.

Wapo ambao bado wako Radio Tanzania na wengine wamechepuka na kuendelea katika maeneo mengine na wapo walioko katika taasisi zinazochampioni masuala ya wanawake kama Bi Nkya na wapo ambao walirejea kwa muumba wetu kama Idd Mchata (mtangazaji maarufu kipindi fulani hapa nchini). Wale waliohai nawapa Hi na wale waliotangulia mahali patulivu, Mungu awarehemu.

Americans are in trouble, look at this

Fayette County residents on the race issue"I'm not voting for Obama, he's black."
Charles is a registered Democrat in Uniontown, Pennsylvania.
"If it wasn't for Obama I would vote Democrat. Blacks just cause trouble, that's the taste I've got in my mouth."
Race is the question mark hanging over this election.
Barack Obama is ahead in the polls. There's a widespread feeling now that the election is his to lose.
But there is something that is worrying Democrats. How accurate are the polls? How many voters are saying they will vote for Mr Obama because they do not want to be perceived as racist?
Once they enter the polling booth will it be an entirely different story?
Simply put, how many people out there think like Charles but are not admitting it?
Charles said the vast majority of his friends felt the same way as him.
Uniontown is a rural town in south-west Pennsylvania. Its countryside is breathtaking, particularly now as the leaves change their colour from green to gold to burnt red.
But the area is poor and unemployment is high. Traditionally it is staunchly Democrat - but race is an election issue.
At a local restaurant a friendly waitress started chatting to us. The conversation turned to politics.
She shrugged, she was not even sure when the election was to be held, she could not pronounce Mr Obama's name.
"I like McCain because I can say his name, so I'll probably vote for McCain."
She was not well informed, but her views were clear.
"He's from Africa or something. I don't even know where he's from. I know he grew up here, but he's not from here. I think American presidents should be from America."
These are not isolated opinions - just not often voiced publicly.
In the primaries 12% of voters across the state said race was a factor - and that is close to Mr Obama's current lead in the polls here.
Recently, Congressman John Murtha had this to say about his home state: "There is no question that western Pennsylvania is a racist area".
He did, however, predict that Mr Obama would still win the state, and he later apologised for the remarks.
The polls show Mr Obama is ahead in Pennsylvania, which also has a Democratic governor and traditionally huge Democratic majorities in the major cities - Pittsburgh and Philadelphia.
In Uniontown, of course I met Democrats who are voting for Mr Obama, and I also met a couple of Republicans who said they were voting Obama.
This is not about a town being racist, but rather how much the race issue is reflected in the polls.

He tries to put a good show for the people, but I don't think he is American
Brandon Hafield At a local hunting shop there were a variety of opinions. Registered Democrat Tom Currens said he would vote for the Republican candidate John McCain, but not because he had a problem with Mr Obama's racial background.
Todd Hackley, a registered Republican said he would vote for Mr McCain and had this to say on the race question:
"Race is an issue, it has to be, not that we want it to be. My thoughts are that Obama will get as many votes from the blacks, as he will not get from the whites.
"I do believe there are a lot of whites who won't vote for him because of the colour of his skin, but I believe there are a lot of blacks who will vote for him because of his colour."
Todd has always voted Republican and when I asked him if colour was an issue for him he said it might have been years ago, but not now.
Brandon Hafield said said he was undecided who to vote for, but when I asked if Mr Obama was a patriot he said no.
When I asked if he was American, he said: "I think he tried to be, I don't think he is, he tries to put a good show for the people, but I don't think he is."
I hate to think we would have racial prejudice entering into a campaign here, but I think perhaps we do
Local radio presenter Bob Fultz, who hosts a regular talk show, says prejudice is definitely present, even though few callers are willing to discuss it openly.
"White voters aren't saying what they really think, whether that's here in Fayette County or nationally. I had one caller who said he thinks Obama is Osama with plastic surgery."
However, Mr Obama has gained points for his perceived ability to handle the credit crunch - and Uniontown has its own financial woes.
Russ Mechling is a retired engineer who used to be the president of the local company Fayette Engineering. He is a registered Democrat who will be voting for Mr Obama.
"There is a little bit of a racial backlash, but I think it's becoming less and less as the economic situation gets worse and worse.
"I think that will probably cost McCain more votes than any other single factor."

Thursday, October 23, 2008

bado nipo, ni muda tu unagomba

dear wananet, wanabloga

Nimekuwa nje tangu Jumatatu, si kwamba kuna kasoro za kiufundi la hasha. Pamoja na kuwa mtumishi wa blog hii pia nilipata tatizo la muda kwani mwajiri wangu amenipa 'go' kwenda kufukua kitabu huko Saut kampasi ya dar. Nataka kujikita katika utafiti na kumeneji . sasa basi muda umekuwa haujapangika vyema kati ya skuli, kibaruani na katika blogu hii. Kutokana na mazingira haya naona tutarekebisha mambo ili tuwe na ratiba ya kupeana taarifa na Mungu akipenda tutaendeleza libeneke letu kwa kasi ile ile, bado najifunza ratiba ya skuli na kasi yake katika umri wangu ni misele ya aina yake.

Monday, October 20, 2008

Ikulu yalalamikia coverage ya vyombo vya Habari Mbeya

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ziara ya Mheshimiwa Rais Mkoani Mbeya

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alihitimisha ziara yake ya siku 10 yenye mafanikio makubwa katika Mkoa wa Mbeya jana mchana, Jumamosi, Oktoba 18, 2008.

Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya vyombo vya habari nchini, na hasa magazeti, vimeandika baadhi ya matukio ya ziara hiyo, kwa namna ya wazi ya kuwapotosha wananchi kuhusu ziara hiyo ambako Rais alitembelea wilaya zote saba zenye halmashauri nane za Mkoa huo.

Taarifa hii inalenga kuweka bayana ukweli ulivyokuwa katika ziara hiyo ambako, kwa mara nyingine, Rais alipata nafasi nyingine nzuri kufanya kile ambacho hukifurahia sana kukifanya- yaani kukutana na wananchi, kusililiza kero zao, karaha zao, raha zao, mafanikio yao, na mahitaji yao ambayo wanaamini Rais wao anaweza kusaidia kuyatafutia majawabu.

(a) Rais akatisha ziara ya mkoa

Rais alipanga kukaa katika Mkoa wa Mbeya kwa siku 10. Amefanya hivyo. Hakukatisha ziara hiyo kama ilivyoandikwa katika baadhi ya magazeti. Aliingia Mbeya Oktoba 9, akaondoka Oktoba 13 jioni kwenda Tanga kuzima Mwenge, na akarejea jioni ya Oktoba 14 na kuondoka jana, Oktoba 18, jumla ya siku 10 kamili.

Ni vyema kujua kuwa kila Rais anapoweka mguu katika Mkoa wowote, iwe ni asubuhi, mchana ama jioni ni siku kamili ya kuwapo kwake katika Mkoa ama eneo hilo.

Kilichotokea ni kwamba kwa sababu ya ratiba kuwa na shughuli nyingi, ziko shughuli mbili ambazo hakuweza kuzifanya. Ameahidi atapata nafasi ya kwenda tena Mbeya kuzifanya shughuli hizo.


(b) Mkutano wa majumuisho ya ziara kwenye Uwanja wa Sokoine

Na wala Rais hakuahirisha kuhutubia wananchi wa Mbeya kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wakati wa majumuisho yake ya Mkoa huo kama inavyodaiwa.

Rais hakupangiwa kuhutubia mkutano kwenye uwanja huo kwa sababu alikwishakuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja huo Februari 19, 2006, alipokwenda kuwashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuongoza nchi yetu.

Na wala Rais hafanyi majumuisho ya ziara za mikoa kwenye mikutano ya hadhara. Huifanya kazi hiyo kwa kukutana na viongozi wa kisiasa, kijamii, kiuchumi, kidini, na kiusalama wa mikoa katika mkutano wa viongozi. Ndivyo alivyofanya jana katika Ukumbi wa Mkapa mjini Mbeya.

(c) Kutotembelea Mbeya Vijiji

Kama nilivyoeleza hapo juu, Rais alitembelea wilaya zote saba za mkoa huo zenye halmashauri nane kwa sababu Mbeya yenyewe ni wilaya moja lakini ina halmashauri mbili, moja ya mjini na nyingine ya vijijini.

Wakati mwingine uelewa wa waandishi wetu unapumbazisha kabisa. Jana, kabla ya kuingia kwenye mkutano wa majumuisho, Rais alitemebelea kiwanda cha kutotoa vifaranga vya kuku katika eneo la Songwe, ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa Songwe, pamoja na kuzindua hospitali teule ya wilaya ya Ifisi, vyote vikiwa katika eneo la Wilaya ya Mbeya lakini katika maeneo ya vijijini.



(d) JK akiri Mbeya ni pagumu

Huu pia ni upotoshaji mwingine. Kama kuna kitu Rais amekisema wakati wa majumuisho ya ziara yake jana ni kuumwagia sifa sana mkoa huo kwa jitihada za maendeleo ya wananchi – iwe katika elimu, iwe katika afya, iwe katika kilimo, iwe ni katika huduma za maji, iwe ni katika ufugaji, iwe katika umwagiliaji na maeneo mengine muhimu ya maendeleo.

Kile kinachoelezwa kuwa Mbeya ni pagumu, ni pale alipowasihi viongozi kujenga tabia na mwenendo wa uongozi wa pamoja akisizitiza kuwa viongozi hao wanajenga nyumba moja na hivyo hawana sababu ya kugombea fito kwa sababu ya tofauti zilizopo miongoni mwa baadhi ya viongozi wa Mkoa huo. Tofauti miongoni mwa viongozi wachache wa mkoa huo haziufanyi mkoa mzima wa Mbeya kuwa mgumu.

(e) Msafara wa Rais kupigwa mawe

Mwenendo mzima ambao uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaweza kujivunia ni kujitokeza kwa wingi mno kwa mamia kwa mamia ya wananchi wa mkoa huo kila alipopita Rais ama kwenda kwa shughuli za maendeleo wakati wa ziara hiyo.

Kila sehemu, wananchi walimtaka asimame, wamwone, awasalimie. Na kama ilivyo ada, hakusita, hata sehemu moja, kufanya hivyo.

Hamu ya wananchi wa Mbeya kumwona na kumsikiliza Rais wao ndiyo ilimfanya Mhe. Rais kusema kuwa alikuwa ameondoka Mkoa wa Mbeya akiwa na kumbukumbu nzuri za wema, ukarimu na upendo wa wananchi wa Mbeya.

Ilikuwa ni hamu hiyo hiyo ambayo wananchi wa kijiji cha Kanga walikuwa nayo wakati Rais anafanya ziara ya Wilaya ya Chunya ambako alipitia na kuhutubia mikutano mikubwa ya wananchi katika maeneo ya Chunya Mjini, Makongolosi na Mkwajuni.

Kwa bahati mbaya wakati anawasili katika kijiji cha Kanga tayari ilikuwa usiku kati ya saa moja na saa mbili kwa sababu ratiba ya maeneo mengine ilikuwa imecheleshwa mno na hamu ya wananchi wa maeneo hayo kumsimamisha na kumwona Rais wao. Hivyo, msafara wake ukapita bila kusimama katika kijiji hicho.

Kile kitendo cha kiongozi wao kutosimama katika kijiji hicho ambako wananchi walikuwa wamejitokeza kwa mamia, wakasimama barabarani kwa saa nyingi wakiwa na hamu kumwona Rais wao, kikachochea na kusisimua tahayari (frustration) kwa vijana ambao wakaanza kurusha mawe kwenye baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara.

(d) Magari ya Rais

Magari ya Rais, kwa maana ya magari yote yanayotengeneza sehemu kuu ya msafara wa Rais, hayakutupiwa hata jiwe moja. Na wala Rais mwenyewe hakupata habari za tukio hilo mpaka alipokuwa amewasili Ikulu ya Mbeya.

Na alipopata habari hizo alitoa maelekezo maalum kuwa zisije zikachukuliwa hatua za kipolisi kusumbua kijiji kizima na kutaka upelelezi wa suala hilo ufanyike kwa uangalifu mkubwa bila jabza.

Magari yaliyotupiwa mawe ni yale yaliyokuwa nyuma katika sehemu ya pili ya msafara, yaani nje ya sehemu kuu ya msafara. Na mpaka Rais anaondoka Mbeya jana, ni watu watano tu walikuwa wametiwa mbaroni, tofauti na habari za kubuni za magazeti kuwa wamekamatwa watu 60.

Rais anaamini kuwa tukio hilo la kijiji cha Kanga ni tukio la uharifu. Kamwe haiwezi kutokea Rais Kikwete asisumbuliwe na tukio lolote la uharifu katika nchi yetu. Hili ni tuko lililomkera, lakini kama alivyoeleza jana kazi hiyo waachie polisi waendelee nayo.

Muhimu kusisitiza hapa ni kwamba tukio hilo siyo tukio linalowakilisha taswira ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wameonyesha mapenzi makubwa kwa kiongozi wao mkuu. Ni makosa kwa kuuchukulia mkoa mzima wa Mbeya kama mkoa wa waharifu kwa sababu ya tendo lililotendwa na watu wachache katika kijiji kimoja tu.


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

19 Oktoba, 2008

Msanii akionyesha vibweka vyake Mbeya


Msanii chipukikizi kutoka kijiji cha Itaka,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya,Huruma William Mgalla mwenyewe umri wa miaka 20, akitembea juu ya kamba iliy kuubaurudisha umati wa watu uliohudhuria mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mbeya hivi karibuni.Picha hii ni ya Freddy Maro

Siku rais alipokutana na maalbino




CHAMA cha Maalbino Tanzania, jana kilitoa kilio chake cha ongezeko la mauaji ya albino nchini mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kumuomba aunde tume ya kukomesha mauaji hayo ambayo yameanza kuiondolea sifa ya amani Tanzania.

Akisoma risala kwa niaba ya maalbino wenzake jana mara baada ya maandamano ya kupinga vitendo vya mauaji ya albino, Mratibu wa maandamano hayo, Josephat Torner, alisema hali ya mauaji kwa sasa ni tishio kwa jamii ya albino kiasi cha wengine kufikia hatua ya kufikiria kukimbia nchi, kukimbilia mijini na wengine kuacha shule.

“Athari za mauaji haya kwa sasa ni kubwa. Watoto wetu wengi jamii ya albino wameacha kabisa shule na wengine wamekimbia kabisa vijijini kwenda mijini, wapo wanaolindwa na polisi kama madini ya tanzanite,” alisema Torner.

Alisema jamii hiyo inazidi kudharauliwa kwani kila maalbino wanapopita imekuwa kawaida kuitwa ‘dili’ hali ambayo inazidi kuwatia hofu.
Naye Rais Kikwete alisema pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia vyombo vyake vya dola na asasi zisizo za serikali katika kupambana na mauaji hayo, bado iko haja kwa elimu juu ya albino kusambazwa kwa jamii ili iweze kuachana na mila potofu na ushirikina. “Nimepokea mapendekezo yenu na ninawaahidi nitayapitia na kuyafanyia kazi, lakini ni muhimu wote kutambua kuwa chanzo kikubwa cha mauaji haya ni ushirikina na mila potofu walizonazo wananchi juu ya albino,” alisema Kikwete.
“Hata ukikata mikono ya albino wote nchini kama huwajibiki ipasavyo na kujituma huwezi kuwa tajiri, acheni ujinga hawa waganga wanawadanganya zindukeni sasa na mtambue kuwa wajinga ndio waliwao,” alisema.
Alisema serikali katika kutoa adhabu na kusimamia haki za wananchi wake haina ubaguzi na kwamba muuaji yeyote atakayekamatwa adhabu yake ni kifo awe ameua albino au la.
“Najua wanaharakati wanapinga adhabu hii ya kifo na wanataka ifutwe najua wananilaani lakini ndio sheria iliyopo kwa sasa,” alisema.
Alisema katika harakati za kupambana na mauaji hayo tayari watu 47 wamekamatwa wakihusishwa na mauaji ya maalbino, kati yao 17 wamekamatiwa Mwanza ambako ndiko kunakoongoza kwa mauaji hayo, sita Mara, wawili Kagera, mmoja Shinyanga na wawili Mbeya.


Pichani Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi,Maalbino ,wakati alipopokea maandamano ya kulaanani ukatili na mauaji ya maalbino,yaliyofanyika katika viwanja vya ukumbe wa Karimjee jijini Dar es salaam jana asubuhi.


picha nyingine ni Mbunge wa kuteuliwa anayewakilisha maalbino, Al Shaimaa John Kwegyir
akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuzindua nakuichangia taasisi ya Goodhope Star Foundation ambayo itatetea na kutoa huduma kwa maalbino nchini,iliyofanyika
katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam jana jioni.Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete zaidi ya shilingi 16.3/m zilikusanywa.Rais Kikwete alitoa
jumla ya shilingi milioni mbili na nusu 2.5/m kama mchango wake kwa taasisi
hiyo.


Picha ya mwisho baadhi ya wakereketwa wa kupigani haki za maalbinoo wakiandamana jijini
Dar es Salaam jana .Maandamano hayo yaliishia katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais Jakaya Kikwete.Picha zote na Freddy Maro.

Saturday, October 18, 2008

Rais ateta kuhusu kuvurumishiwa mawe


RAIS Jakaya Kikwete amesema kushambuliwa kwa msafara wake kwa kupigwa mawe wilayani Chunya mkoani Mbeya, hakumsumbui na kuvitaka vyombo vya habari kuacha kukuza mambo.
Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, kutofadhaika kutokana na shambulio hilo, kwa sababu tukio hilo haliwakilishi taswira njema ya mkoa huo wa Nyanda za Juu Kusini. Pichani rais akizungumza na wananchi wa Chuna na picha hii ni mali ya Freddy Maro.

Manispaa yamzika kimakosa mwanamke aliyekufa kwa uzazi





WATU saba wanahojiwa na Polisi kuhusu mtafaruku ulioibuka baada ya tukio la wafanyakazi wa Manispaa ya Singida kupewa kimakosa na kwenda kuuzika mwili wa marehemu uliokuwa umehifadhiwa katika hospitali ya Singida kwa muda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Celina Kaluba alisema tayari Polisi inawahoji watu saba kuhusu tukio hilo na watakaobainika kuhusika kwa uzembe huo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katika tukio hilo lisilokuwa la kawaida, Manispaa ya Singida iliuzika mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mwanahamisi Omari (39) mkazi wa kijiji cha Kinyagigi katika halmashauri ya wilaya ya Singida, ambaye alifariki Oktoba 16 katika hospitali ya Nkungi kwa matatizo ya uzazi anaripoti Hudson Kazonta wa habariLeo
Mwili wa Mwanahamisi ulipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa siku moja kabla ya kwenda kuzikwa siku inayofuata.
Akizungumzia suala hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Aubrey Mushi, alisema hali hiyo imesababishwa na uzembe wa muuguzi wa zamu pamoja na wafanyakazi kutoka Manispaa wenye majukumu ya kuzika miili ya watu iliyokosa ndugu.
Alisema katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo kulikuwa na maiti moja ya mahabusu mwanaume aliyejulikana kwa jina la Mwamanela Makumbi (32) ambaye alifariki Oktoba 16 mwaka huu.


Picha hizi za Hudson zinaonyesha pilika za ufukuaji wa kaburi na kurejeshwa mwili katika mortuary kwa hifadhi tena kabla ya kuendelea na safari.

Nilipokutana na nguli wa mafoto ya sinema



Nilipata kuzungumza na mmoja wa wapiga picha wa sinema wazuri waliopo nchini anaitwa Syllone siku ya Ijumaa.Unajua nilikutana naye kwa dharura katika eneo la karibu na mlango wa kuingilia katika ofisi ninazofanyia kazi za HabariLeo na sikujua kwamba kulikuwa na mtu anatutazama mpaka nilipoletewa picha hii kwa njia ya mtandao na jamaa yangu katika mambo haya Maganga Feruzi.

Katika picha hizi niseme tu mimi na Syllone tulijadiliana mambo mengi lakini kubwa hasa ni kuhusu hili tamasha la filamu la nchi za Ulaya ambalo linafanyika New World Cinema pale Mwenge nje kidogo kutoka hapa ninapofanyika kazi Posta.

Tukaonyeshana ratiba kuona picha ambazo zinafaa kuangaliwa kwa sababu za kitaalamu na nyingine ambazo zinatugusa akina siye tunaopenda kukosoa kazi za watu kwa lengo la kupata mambo bora zaidi.

Nikamkumbusha enzi zake ambazo hazina kompyuta na filamu yake ya Kibuyu na directors cut ndani ya filamu hiyo na pia Gubu la Wifi. Nikamuuliza haoni kwamba sinema hizo mbili wanaweza kufanya re make? By the way Maganga aksante kwa kunivizia.

Friday, October 17, 2008

Polisi wanauliza huu mchuma wa nani?





Askari doria tangu asubuhi waliliona gari hili limeegeshwa katika eneo lisilostahili katika makutano ya barabara za Morogoro na Ile ya Umoja wa Mataifa pale Fire, Dar es salaam. Inakuwa hasa? Walijiuliza.Watu wa Karibu wanasema wameliona hapo muda.Wakaendelea na safari.


Lakini gari hili la gharama aina ya Mercedes Benz T 139 AAD baada ya kuonwa kwanza na watu wa doria na kulimezea walirejea tena.Wakaliona halina hata dalili ya kuondoka.Wakarejea tena wakaona lipo palepale, Mhhh hili gari hili!!! Walishangaa.
Ilipofika mchana wakalishtukia na kuamua kulipiga kamba na kulivuta kulipeleka kituo Kikuu cha polisi, manake hii si kawaida.
Gari lililotumika kulivuta ni break down yenye namba ambayo mbele haijulikani (kibati kimekatika) lakini inaishia 522 AJP na juu yake imeandikwa Lukaga Motors.
Hivi ni kweli kuna mtu amelihifadhi pale?Je liliharibika, au kitu gani kimemsibu mwenye gari hili ambalo pia vielelevyo vyake kama bima na kadha wa kadha katika kioo mbele vinaonekana vimeisha wakati wake?
Au.... basi chochote kile unaweza kufikiria lakini kama unajua kitu kwanini usiwatonye polisi au mweleze jamaa kupitia lukwangule.
Picha hizi zote ni msaada wa Yusuf Badi thanks bud.

Kariakoo risasi zatumika kuzima vurugu


Maeneo ya Kariakoo leo yaligubikwa na kiwuingu cha vurugu kiasi cha kusababisha askari wa doria kutumia risasi za moto kusambaratisha makundi yaliyokuwa yakivaana katika maeneo hayo.
Ingawa haikuwa inajulikana kwa yakini kilichosababisha mtafaruku huo muungwana mmoja wa Kariakoo alisema kwamba ghasia hizo zilitokana na juhudi za Takukuru kukamata walamba rushwa miongoni mwa askari wa Jiji.
Inasadikiwa mtego wa kunasa walamba rushwa hao ulishtukiwa na katika jiokoe jikoe mambo yakaharibika na kuwa mtego w apanya kunasa waliomo na wasiokuwamo.
Mtu aliyetupasha habari amesema kwamba askari wa Doria walilazimika kutumia risasi za moto kwa kuzipiga hewani ili kuondoa ghasia ambazo inaonekana zilitaka kuharibu shughuli za kibiashara katika mitaa hiyo ya Msimbazi.
Watu kadhaa wanashikiliw ana polisi katika kituo cha Msimbazi kwa mida hii kuhojiwa.
Kwa muda mwingi askari wa jiji wameonekana kuwa balaa badala ya kuwa msaada kutokana na patashika wanazofanya kwa watu mbalimbali na wakati mwingine bila kutumia busara.

Thursday, October 16, 2008

John McCain abanwa mbavu



MGOMBEA Urais kupitia tiketi ya Democrats, Barack Obama amemning'iniza mgombea Urais kwa kupitia chama cha Republican John McCain katika mdahalo ulioonyeshwa moja kwa moja na televisheni.
Huu ulikuwa mdahalo wa mwisho mgumu kuelekea katika uchaguzi ambao utafanyika mwezi ujao.
Mambo yaliyojiri katika mdahalo huo ni uchumi na usalama wa ndani na juhudi za McCain kumpaka tope Obama zilionekana kugonga mwamba kutokana na mgombea huyo wa Democrats kutulia na kujibu hoja.
Aidha alimshutumu McCain kwa kutumia siasa za chuki badala ya kumwaga sera za nini atawafanyia wananchi wa Marekani.
McCain pia alimshutumu Obama kwa kutaka kupandisha kodi, kauli ambayo ilijibiwa vyema na Obama.
Televisheni za Marekani zilionyesha kwamba Obama amenyakua pointi nyingi katika mdahalo huo.
Kura za maoni za CNN zimeonyesha kuwa Obama alishinda kwa asilimia 58 kwa 31; wakati za CBS zinaonyesha kuwa Democrat ni washindi kwa asilimia 53 kwa asilimia 22 za McCain.
Pia wale ambao hawakuonyesha wazi wanamuunga mkono nao katika Mtandao wa Fox walionyesha kwamba Obama ndiye mshindi.


Pichani mzee baada ya kibano aking'amua kwamba anakwenda kusiko kwake kutoka jukwaani

The Goethe-Institut invites you to the photo exhibition

Goethe-Institut inakualika kwenye maonyesho ya picha Movement Frozen in Time. Exhibition of Dance Images In line with the Visa 2 Dance Festival .
Katika mkakato huo wa Visa 2 Dance Festival The exhibition presents dance photographers from Germany and their perspective on dance and movement.
Maonyesho haya ni maoni na mtazamo wa wapigapicha za dansi kutoka Ujerumani kuhusu dansi na mtazamo.
Opening on Tuesday, 21st October at 8 pm, Alliance Française, Free Entrance
The exhibition will run until 8th November 2008.
Monday to Saturday from 10 – 6 pm.
Ufunguzi utakuwa tarehe, 21 October, Alliance Française, saa mbili usiku Kiingilio bure Maonesho yataendelea mpaka tarehe 08 Novemba 2008.
Jumatatu mpaka jumamosi kuanzia saa 4 – 12 jioni.
Contact/Anuani:
Ulrike Schwerdtfeger
director@daressalaam.goethe.org
(022) 213 4800 0782 - 502 190

MAALBINO WAUNDA KLABU YA SOKA



HABARI NJEMA KWA WANAHARAKATI WA UNYAMA DHIDI YA MAALBINO
HUKU KUKIWA NA WAHAKA JUU YA MSTAKABALI WA USALAMA WAO KUTOKANA NA VITENDO VIOVU VYA KUWATOA ROHO KWA IMANI ZA KIHIRIKINA, WADAU AMBAO NI ALBINO WAMEANZISHA RASMI TIMU YA SOKA INAYOJULIKANA KAMA 'ALBINO MAGIC TEAM' YENYE MAKAO YAKE KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD DAR.
KWA MUJIBU WA MRATIBU WA TIMU HIYO, OSCAR HAULE, TIMU HIYO YENYE WACHEZAJI WA UMRI MBALIMBALI IMEANZA TIZI UWANJA WA OCEAN ROAD KILA SIKU JIONI, NA ENDAPO MAMBO YATAKUWA MSWANO WATACHEZA MECHI YAO YA KWANZA WIKI IJAYO NA TIMU AMBAYO ITATAJWA KARIBUNI.
PAMOJA NA KULA TIZI LA NGUVU KILA SIKU, TIMU HIYO HIVI SASA IKO KATIKA KUSAKA WAFADHILI AMBAO WATAWASAIDIA KUPATA VIFAA VYA MICHEZO PAMOJA NA MAHITAJI MUHIMU IKIWA NI PAMOJA NA MADAWA NA LISHE ILI KUJIWEKA FITI.
MDAU HAULE AMETOA WITO KWA ALBINO NCHI NZIMA KUJIUNGA PAMOJA NA KUANZISHA TIMU ZA MICHEZO MBALIMBALI IKIWA NI NJIA MOJAWAPO YA KUHAMASISHA UMMA KUWAONA KWAMBA WAO NI WANAJAMII KAMA WALIVYO WATU WENGINE.
AMETOA MWITO PIA KWA MAKAMPUNI NA WATU BINFASI KUISAIDIA ALBINO MAGIC TEAM KWA HALI NA MALI ILI HUKO MBELENI IKIWEZEKANA WAANZISHE LIGI YAO ILI KUENDELEZA LIBENEKE LA KUMALIZA DHANA POTOFU KWAMBA ALBINO HAWAWEZI KUFANYA JAMBO KATIKA JAMII NA PIA KUONDOA UNYANYAPAA WA KILA AINA UNAOWAKABILI.
MRATIBU HUYO AMESEMA WAKO TAYARI KUPOKEA MSAADA WA AINA YOYOTE ILI KUFANIKISHA AZAMA YAO YA KUJIKOMBOA WENYEWE KUTOKA KATIKA LINDI LA UNYANYASAJI NA UHARAMIA DHIDI YAO.
AMESEMA NAMBA YAO YA SIMU NI
+255 716 040 550
HAYA SHIME WADAU, NDUGU ZETU HAWA WAMEAMUA KUJIKOMBOA NA TUWASAIDIE KWA HALI NA MALI ILI NDOTO YAO ITIMIE...

Madonna na guy Ritchie wasema basi inatosha, wanatengana


Material Girl Madonna na mume wake Guy Ritchie wameamua kuachana baada ya miaka takribani minane ya ndoa.
Wawili hao wamesema kwamba wanadhani watakubaliana bila kwenda mahakamani, msemaji wa Madona Liz Rosenberg amesema.
Taarifa hiyo inahitimisha umbeya wa miezi kadhaa kwamba wana ndoa hao wawili walikuwa hawaelewani.
Watu hao ambao wameishi miaka saba na nusu wana watoto wawili wa kiume Rocco na David Banda, Mmalawi aliyeasiliwa Mei mwaka huu.
Gazeti la Sunday Times limeandika kuwa Madonna na Ritchie kwa pamoja wana mali yenye thamani ya paundi milioni 300, nyingi ya hizo zilitengenezwa na Madonna.
Madonna na Ritchie walioana Desemba 2000 katika kasri ya Skibo huko Scotland.
Madonna pia ana binti wa miaka 12 anayeitwa Lourdes, kutoka mahusiano yake ya kwanza.

Dona productions anakupa mchirizi wenye liwazo kubwa hebu mnyake

Vipi Msimbe
Here is an All exclusive Bongo Mix I did for African Hip Hop Radio. Ifyou could post it on u r blog(http://lukwangule.blogspot.com/) nitashukuru
"Its Oct and time to roll out the Sep/Oct Podcast that I did forAfrican Hip Hop Radio Bongo Flava edition. Make sure to check out theintro which features Dead Prez. Shouts out to Juma and all the Africanhip hop radio crew.
We will be showcasing the Bongo Flava Podcast onAfrican Hip Hop Radio every month. Make sure to check out the introwhich features Dead Prez."
Download Link: http://www.zshare.net/audio/18219980db4a4c2f/
Tracklisting
African Hip Hop Intro
MwanaFA - Bado Nipo Nipo
Wanaume TMK - Dar Mpaka Moro
Prof. Jay - Nang'atuka
MB Dog Feat. Madee - Latifa
Cloud Tissa Feat G-Solo - All Over
Inspector Harun - Shetani Hana Mwaka
Top Band Feat. Matonya - Beki Hazikabi
Queen Darleen Feat Ali Kiba- Najua Nakupenda
Joe Makini-Sitachoka
Ali Kiba - Zuu
AY - Usijaribu
Zanto Feat. Tilly One - Mpenzi Jini
Ay Feat Q Chirah - Binamu
MB Dogg - Naona Raha
Chidi Benz Feat K-Lynn - Naitwa Nani
Jay Moe- Maisha Ya Boarding
TID and WanaFA- Raisa
MH. Temba - Mwaka Wa Shetani
Mex B - Kukuku
Noorah Mwanafalsafa Feat Enika - Zai
Q Chilla feat Nyota Ndogo - Wivu
Professor Jay feat Jay Mo - Hapo Sawa (Remix)
Dataz and Squeezer - Wajua
Hafsa Feat Banana - Presha
Marlaw na Chidi Benz - Bado Nimenuna
Ali Kiba - Msela

--ISHIKE!!!!!
DJ DonaDj/Producer
www.djdona.comwww.myspace.com/donaproductions

Wednesday, October 15, 2008

Ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha saruji wazinduliwe


Rais Jakaya Kikwete akishuka kutoka katika tingatinga muda mfupi baada ya kuchimba udongo na tingatinga hilo ili kuzindua rasmi ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha saruji kinachomilikiwa na kampuni ya Athi River mining Company limited,huko maweni Tanga jana.Kiwanda hicho kitakuwa kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki.

Tuesday, October 14, 2008

Walimu wafanyaghasia kubwa mkutanoni

RISASI za moto zilitumika leo kutawanya walimu na kuokoa viongozi wao ambao walikuwa wakipigwa kwa mawe na chupa na walimu waliochukizwa na kauli yao kuhusu tamko la mahakama la kusitisha mgomo.
Viongozi hao wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakizungumza kuhusu tamko la Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kusitisha mgomo uliopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho walimu walibadili kibao, wakatusi wenzao na kuwafanyia varangati kubwa lililohitaji okoaji ya polisi.
Walimu hao baada ya patashika waligeukiana wenyewe na baadaye kujitoma nje ya ukumbi wa mkutano wa Diamond Jubilee hall na kuanza kuwafanyia jeuri waendesha magari huku wenye ngozi nyeupe wakipita wakiitwa mafisadi.
Kasheshe hiyo iliyoonyeshwa katika vyombo vya habari na televisheni ilitoa sura mbaya ya aina ya walimu tulionao pamoja na shida walizonazo walimu hao na watanzania kwa ujumla, ustaarabu wa kukubali maamuzi ya mahakama na kuyapinga kwa mtiririko wa kisheria ulitakiwa kuwapo.
Kwa maoni yangu Lukwangule, Sasa huwezi kushangaa wanafunzi nao wakileta dhahama za kuchoma shule na kupiga walimu wao, kumbe walimu wenyewe nao wako kama ilivyoonekana katika televisheni.Iam Sorry.

Vibration wakiwa kazini


Wanenguaji wa bendi ya vibration wakishambulia jukwaa katika ukumbi wa Mango Gardeni mwishoni mwawiki hii. Picha hii na mmoja wa wachangiaji wa blogu hii Albart Jackson

Suzy akiwa anawapeleka mbio mashabiki wake


Mnenguaji mahiri wa Bendi ya FM Academia Suzi Cyz akionyesha umahiri wake wa kunengua muziki katika moja ya maonyesho ya bendi hiyo jijini Dar. Suzy amekuwa kivutio kikubwa miongoni mwa wanenguaji wa bendi hiyo. Picha na albart Jackson.

mwenge wazimwa Tanga


Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Shanes Martin Nungu akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa michezo wa Mkwakwani Tanga leo wakati wa kilele cha sherehe za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.Sherehe za kuzima Mwenge zilifanyika leo katika viwanja hivyo ambapo rais alihutubia na kuzungumzia juhudi za serikali kukabiliana na msukosuko wa kifedha duniani. Pia alizungumza juu ya urejeshaji wa fedha za Tanzania zilizopo katika mabenki ya biashara.Aidha aliwataka wananchi wamuenzi mwalimu kwa kufanya matendo yanayolenga kuzalisha mali zaidi na hasa chakula.Picha hii ni Mali ya Freddy Maro

Treni ya Bara yapata ajali uwanja wa ndege


TRENI ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) iliyokuwa inatoka Bara ilikwama kwa saa nne karibu na maeneo ya uwanja wa ndege Dar es salaam baada ya behewa moja kupata hitilafu na kuchomoka katika njia ya reli .
Abiria wote walitoka salama pamoja na kwamba walikuwa na mshtuko kutokana na vumbi na mlio wa chuma kusagika.
“Baada ya hapo tulisikia kelele za chuma kusagana, kutokana na hali hiyo abiria tuliokuwapo tuliogopa na wengine walianza kukimbia huku wakipiga kelele, lakini tunashukuru Mungu Treni ilisimama salama,” alisema Damian Mbowe aliyekuwapo kwenye behewa hilo namba 2209, akitokea Mwanza.
Kwa mujibu wa shuhuda Maganga Feruzi alisema behewa linaonekana kuwa limeburuzwa na kusema mabehewa yanaonekana kuchoka kutokana na maizngira yanayoonmekana ya hitilafu hiyo ambayo ilifanyiwa kazi na mafundi wa TRL kwa zaidi ya saa nne.
Dereva wa injini namba 73 R 19 wa treni hiyo, aligoma kuzungumza na kudai kuwa habari kamili za tukio hilo zitatolewa na uongozi wa TRL na kwamba yeye si msemaji.
Pichani wananchi wakiwa wanashuka katika treni kujaribu kuona namna ya kuingia mji wa Dar. picha hii ni mali ya Yusuf Badi

Rais alipozuru kitovu cha kilimo, Uyole


Mkurugenzi wa Kituyo cha Utafiti wa Kilimo Uyole Mbeya , Dk. Catherine Madata akimwonyesha Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete mbegu mpya ya mahindi iliyo buniwa na kuzalishwa na kituo hicho wakati Rais lipotembelea kituo hicho hivi karibuni.Picha hii ni mali ya Freddy Maro.

Nyerere day, haya ni maoni ya gazeti linalomilikiwa na serikali HabariLeo


Wanafunzi wa Nyerere tumepotoka, tumemsahau!

LEO Watanzania tunatimiza miaka tisa tangu kuondokewa na kiongozi wetu mpendwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Tunasema kiongozi mpendwa kwa sababu tangu alipotangaza kung’atuka katika uongozi wa nchi na baadaye katika Chama Cha Mapinduzi alichokiasisi, bado aliendelea kuwa baba aliyekemea pale alipoona mambo hayaendi vizuri.

Ni kiongozi mwenye sifa nyingi, lakini kubwa ni ile sifa ya kutopenda makuu. Licha ya madaraka makubwa aliyokuwa nayo, lakini maisha yake yalionekana ya kawaida hivyo kumfanya afanane na wananchi aliowaongoza.

Ndio sifa inayofanya hadi leo Watanzania tuendelee bado kumkumbuka hasa katika kipindi hiki ambacho macho yetu yanashuhudia maadili katika jamii, wakiwamo viongozi wetu, yakiwa yamemong’onyoka.

Viongozi wetu wamepotoka na hata zile tambo za kuahidi kumuenzi mwasisi huyo wa taifa ambazo tulizitoa mbele ya jeneza lake na hata kando ya kaburi lake hazionekani na zimetoweka katika matendo yao.

Leo hii jamii imeshuhudia baadhi ya viongozi wetu na watumishi waandamizi wa umma wakijilimbikizia mali kwa tamaa zao na wengine wamediriki kuiingiza nchi katika mikataba mibovu kwa tamaa na uroho wao wa kutajirika haraka bila kujali athari ambazo taifa litapata.

Vitendo hivi vya kutia aibu enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere hatukuviona na hiyo inatokana na yeye kuipenda nchi yake kwa moyo wake wote na kufanya kila jambo alilofanya atangulize mbele zaidi maslahi ya taifa yake badala ya maslahi binafsi.

Tunapoadhimisha miaka tisa ya kuondokewa na kiongozi huyu ambaye ameendelea kuwa taa yetu katika kipindi hiki cha giza, tunawasihi viongozi wetu waiangalie taa hii iwaangaze na pale wanapoona hawaendani na mafundisho yake waweze kujirudi.

Tunaomba wajirudi ili taifa hili changa aliloliasisi miaka 47 iliyopita liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Tunataka kuona kwa vitendo wanafunzi hawa wa mwalimu wanavyoipigania nchi yao kama ilivyokuwa kwa mwasisi huyu wa taifa letu, ili ile ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuifanya Tanzania iwe moja ya nchi zinazokimbia katika kujiletea maendeleo yake yenyewe iweze kufikiwa.

Tutafikia hatua hii iwapo viongozi wetu, na sisi wengine wote, tutaacha tamaa na uroho wa kujilimbikizia mali na jamii kuichukia rushwa kama alivyoichukua Mwalimu Nyerere.

Viongozi waonyeshe njia na tuonekane kweli kuwa sisi ni wanafunzi wake watiifu tuliofundwa kuichukia rushwa na vitendo vingine vyote ambavyo vinachangia kurudisha nyuma maendeleo yetu.

ends


katuni hii ni ya Fadhili

Chadema yaiburuta CCM Tarime



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani wa Tarime uliofanyika juzi.

Mgombea ubunge wa chama hicho, Charles Mwera, alitangazwa kumrithi Chacha Wangwe aliyekufa ajalini Julai mwaka huu, baada ya kushinda kwa kupata kura 34,545 huku mgombea wa CCM Christopher Kangoye akipata kura 28,996.

Mgombea wa NCCR-Mageuzi, Haruni Marwa alipata kura 949 wakati mgombea wa DP Benson Makanya alipata kura 305.

Kwa ushindi huo wa ubunge na udiwani Chadema inaendelea kuongoza halmashauri ya wilaya ya Tarime huku CCM ikiendelea kubaki chama cha upinzani katika halmashauri hiyo.

Kwa upande wa udiwani mgombea wa udiwani wa Chadema, John Heche, alishinda kwa kupata kura 4,820 akifuatiwa na mgombea wa CCM, Peter Wambura, aliyepata kura 3,239.

Mdogo wake marehemu Wangwe, Gideon Wangwe wa NCCR- Mageuzi aliambulia kura 169, John Rotente wa CUF kura 79 na Johanes Sando wa DP alipata kupata kura 24.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa jana na msimamizi wa uchaguzi huo Trasias Kagenzi, mgombea huyo wa CCM Kangoye alisema hakuridhika na matokeo hayo kwa kile alichodai kuwa kulikuwa na hitililafu wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kampeni.

Kangoye ambaye alifika katika ofisi ya halmashauri muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo hayo huku akiwa amefuatana na Katibu wa CCM wa wilaya ya Tarime, Iddi Stambuli, alisema atapinga matokeo hayo kwa msimamizi wa uchaguzi na ikishindikana ataenda mahakamani.

Mgombea huyo pia alikataa kusaini matokeo hayo na kukinzana na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye awali alisema wagombea wote wamekubali na kusaini matokeo.

Licha ya msimamo huo wa Kangoye, msimamizi wa uchaguzi alimkabidhi Mwera hati ya kumtambua kuwa ni mbunge wa halali wa jimbo la Tarime.

Kangoye alisema msimamizi alitangaza matokeo huku akiwa bado anajumlisha kura za vituo alizopewa na mawakala wa CCM. Alianisha kasoro nyingine kuwa ni vitisho vya nguvu vilivyowafanya wapiga kura wasijitokeze kupiga kura.

Akizungumza kwa huzuni, Kangoye alisema vitisho vya mambo yatakuwa kama Kenya na makundi ya vijana ya kujaa katika vituo vya kupigia Kura, ndivyo vilivyofanya wapiga kura 78,186 ambao hawakujitokeza kutumia demokrasia yao kati ya 146, 919 ambao walijiandikisha katika Daftari la Kura.

Kangoye alipingana na kauli ya Katibu Mwenezi wa Chama hicho, John Chiligati, ambaye alisema mwishoni mwa wiki kuwa kama wagombea wao watashindwa watakubali matokeo kwa maelezo kuwa hiyo ndio demokrasia ya kweli.

Kwa upande wake, Mwera licha ya kutangazwa mshindi, alikiri kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi za vitisho vya polisi, watu kukatwa mapanga lakini wananchi wamekubali sera zao na wamemchagua awe mwakilishi wao bungeni na kuahidi kuwa ataanza kazi mara moja ya kuwatetea bila kubagua Itikadi za vyama,

Mwera alifafanua kuwa atavaa viatu cha marehemu Wangwe kwa kutetea haki za wanyonge.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema amepata mpiganaji mwenzake ambaye ataongeza nguvu ya upinzani ya kuwashughulikia mafisadi.

Zitto alikumbusha kuwa ni mara ya kwanza katika kuanzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 kwa Chadema kushinda uchaguzi mdogo.

Kabla ya kutangazwa matokeo wafuasi wa Chadema walianza kushangilia kutokana na matokeo ya awali kuonyesha ilikuwa inaongoza kwa kwenda ofisi za Halmashauri ya Wilaya zilizotumiwa na Tume ya Uchaguzi.

Wakiwa bado mita 400 kufika eneo ambako matokeo yalikuwa yatangazwe walikumbana na kigingi cha polisi na kushindwa kujizuia huku wakiimba nyimbo kuwa Chama cha wahuni chashinda, mende kaangusha kabati na kuanza kujibizana na polisi waliokuwa na silaha mbalimbali.

Baada ya majibizano hayo, polisi walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi huku nao wakiwapiga na kuwajeruhi polisi kadhaa kwa mawe na kuanza kutimua huku wakipiga yowe. Tukio hilo lilichukua saa nne na kufanya kazi za biashara mjini hapa kufungwa na shughuli za mahakama ya mwanzo kusitishwa.

Katika sakata hilo polisi ambao walikuwa wanaongozwa na Kamanda wa operesheni maalum nchini Venance Tossi iliwakamata zaidi ya watu 50.

Wananchi hao walikuwa wakipiga kelele kuwa kucheleweshwa kwa matokeo ni jaribio la kuwapokonya ushindi.

Polisi waliokuwa wamejipanga kila kona ya kuzunguka hizo za halmashauri walifikia hatua za kuwazuia hata watumishi mbalimbali wa Serikali akiwemo Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Tarime Mjini, Samweli Gimeno ashindwe kwenda katika eneo lake la kazi.

Mchakato wa kuwania kiti cha ubunge Tarime kilianza Septemba 14 kwa vyama vyote kunadi sera zake kwa wananchi na kufikia tamati juzi huku kampeni hizo zikigubikwa na mbwembwe na vurugu, fujo za kila namna na kufikia hatua za watu kumwaga damu kwa kukatwa mapanga.

Miongoni mwa watu ambao walionja chungu ya kampeni ni kiongozi wa DP taifa Mchungaji Christopher Mtikila ambaye alishambuliwa kwa mawe mawe hadi kumjeruhi kichwani. Pia baadhi ya watu wengine walijeruhiwa kwa mapango na wengine kuuana kwa ushabiki wa vyama.

Miongoni mwa mwembwe katika kampeni hiyo ni kurushwa kwa helkopita tatu. Chadema ndicho kilichoanza mbwembwe hizo kwa kupaua anga kwa kutumia Helkopta na CCM kujibu mapigo kwa kupeleka mbili kwa mpigo ambazo licha ya kuyafikia maeneo mengi vijijini lakini Helkopta ya mbowe imezitungua na kuibuka Mshindi wa Udiwani na Ubunge.

Nashon Kennedy anaripoti kutoka Mwanza kuwa Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba amesema CCM inakubaliana na ushindi huo na kukiri kuwa ingawa walijiandaa kwenda kumg'oa mtu lakini haikuwa bahati yao.

Aliipongeza Chadema kwa ushindi ilioupata lakini akawatahadharisha kuwa wakae mkao wa kuondoka ifikapo mwaka 2010 kwa maelezo kuwa CCM ni kama wamejikwaa tu.

"Unapoanguka usiulize umeangukia wapi, angalia ulipojikwaa, tunawapongeza Chadema kwa ushindi huu walioupata,” alisema.


Pichani Mbunge mpya wa Tarime

Sunday, October 12, 2008

Tarime ni mibomu, jamaa hawajatulia


POLISI wa Kutuliza Ghasia (FFU) leo mjini Tarime baada ya saa moja usiku walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Chadema ambao waliingia mtaani kushangilia ushindi kufuatia matokeo ya awali yaliyobandikwa vituoni, TBC! imeripoti katika taarifa yake ya saa mbili usiku.
Tarime leo ilifanya uchaguzi wa Ubunge na Udiwani baada ya nafasi hizo kuachwa wazi kufuatia kifo cha Chacha Wangwe kiasi cha miezi miwili iliyopita.
Ingawa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na utulivu, matokeo ya awali ya mjini Tarime yameonyesha kwamba wagombea wa Chadema walikuwa wamewaacha mbali wagombea wenzao wa CCM, NCCR-Mageuzi, DP na CUF.
Habari zinasema kwamba polisi walilazimika kuingilia kati kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema baada ya kuanza kurushiana mawe na CCM katika maeneo ya Sabasaba ambapo Chadema ilipata kura 120, CCM 40, DP1, NCCR Mageuzi 2 na CUF 2.
Habari zinasema kwamba ushindi wa Sabasaba ukiongezwa na habari kwamba Chadema pia inaongoza katika maeneo ambayo ni ngome yao ya Nyamongo,Kimokerere na Sirari ilifanya wafuasi hao wakiuke agizo la kutulia majumbani kwao hadi matokeo rasmi yatakapotolewa kesho.
Habari za awali zinasema kwamba wapigakura waliokuwa wametulia, walijipanga katika mistari mirefu nje ya vituo vya kupigia kura kabla ya saa 1.00 asubuhi, ambao ulikuwa muda rasmi wa kuanza kupiga kura.
Uchaguzi mdogo pia ulikuwa ukifanyika katika kata nyingine kadhaa nchini jana ambazo zimepoteza madiwani wao kwa sababu mbalimbali.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime, Traseas Kagenzi, alisema kwa taarifa alizokuwa nazo hadi mchana, muda mfupi kabla ya kufungwa kwa vituo saa 10 jioni, hakukuwa na matukio yo yote ya uvunjifu wa amani.Kagenzi alisema kama matokeo kutoka vituo ambako kura zinahesabiwa yangewasilishwa kwa muda mwafaka, washindi wangetangazwa baadaye leo usiku.
Pichani Baadhi ya wakazi wa jimbo la Uchaguzi la tarime waliojitokeza leo kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Mbunge na Diwani Tarime wakiwa katika mistari . Picha hii ni mali ya Bernard Rwebangira.

Rais akizungumza na watoto yatima


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa na taasisi ya The Mango Tree Orphan Support Programme Trust ya mjini Kyela,Mkoani Mbeya,muda mfupi baada ya Rais kufungua jengo la maktaba katika makao makuu ya taasisi hiyo mjini Kyela jana.Picha hii ni mali ya Freddy Maro.

Watoto wanapokosa mchungaji inakuwaje mitaani?.



Watoto zaidi ya 11 mwishoni mwa wiki wameonekana wakizurura katika mitaa mbalimbali, hapa wakiwa katikaMtaa wa soko Kuu la Manispaa ya Songea bila uangalizi. Walipoulizwa na mpiga picha hii walisema wanakwenda kuleeeee bila kutaja jina la mtaa wala uchochoro.Maafisa ustawi wa jamii wanalijua hili? Picha hii ni mali ya Mdau Juma Nyumayo wa Songea

GTV wazindua kadi mpya

GTV, kampuni kubwa ya televisheni ya kulipia barani Afrika inazindua kadi ya kukwangua ambayo itawawezesha wateja wake kulipia huduma za televisheni kila mwezi kwa kutuma namba iliyoko kwenye kadi. Kadi hiyo ijulikanayo kama G-UP.

Kadi hiyo inatarajiwa kurahisisha ulipiaji wa huduma kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyo kawaida.

Kadi hizo ambazo ni ya aina tatu tofauti maalumu kwa vifurushi vitatu vya GTV, itakuwa yenye thamani ya Sh. 46,100/- kwa G Plus, Sh. 23,100/- kwa G Choice na Sh. 13,200/- kwa G Home.

Mteja atahitajika kununua kadi inayoendana na kifurushi anacholipia kila mwezi kisha atakwangua sehemu iliyofunikwa ili kuipata namba atakayoitumia kwa malipo.

Kisha mteja ataandika neno “PAID” kwa SMS kwenye simu yake, kisha ataacha nafasi, halafu namba iliyo kwenye smartcard ya dikoda bila kuandika sifuri zilizo mwanzo wa namba hiyo, kisha ataacha nafasi, halafu namba yake ya akaunti ya GTV, nafasi tena, ndipo aandike namba iliyopo kwenye kadi aliyoikwangua.
Baada ya hapo mteja atatakiwa kutuma SMS hiyo kwenda namba 0787 064 679 na hapo atakuwa ameshalipia huduma yake.
Meneja Mkuu wa GTV Tanzania Ronald Mtawali alisema hatua hii imetokana na azma ya GTV ya kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa na pia hitaji la kuwepo kwa njia rahisi ya kulipia kwa wateja wao ambao wanaongezeka.
“Tulisikiliza yale wateja wetu waliyoyataka katika kuboresha huduma za malipo hasa kwa kuzingatia mfumo utakaoendana na taratibu za maisha yao ya kila siku,” alisema.
“Hii ni hatua kubwa katika historia ya huduma ya televisheni ya kulipia barani Afrika. Wateja wa GTV hawatahitaji tena kupanga foleni ndefu ili kufanya malipo yao. Unachohitaji kufanya ni kujipatia kadi yako ya G-UP kutoka kwa mawakala au kituo chochote cha kusambazia huduma zetu.”
Mtawali aliongeza, “Kadi ya G-UP tayari iko sokoni na mawakala wa GTV tayari wameanza kupata mwitikio mzuri toka kwa wateja.” Alisisitiza pia kuwa kadi hizo zitapatikana nchini kote.


Kwa maelezo zaidi
Karine Fouchet, GTV, PR Manager, +44(0)20 7072 8600, karine.fouchet@gtv.tv
Ash Myers, GTV, Corporate Marketing & PR Director, +44(0)20 70728608, ash.myers@gtv.tv
Mabhe Matinyi, Media Relations, Silver Bullet PR, +255 712785695 mabhe@ayr.co.tz

Saturday, October 11, 2008

Mugabe 'gives Zanu-PF key posts' ,deal sasa si dili tena

Zimbabwean President Robert Mugabe has allocated key ministries to his own party - in defiance of a power-sharing deal, reports say.
The opposition Movement for Democratic Change (MDC) said the move had put the deal "in jeopardy".
The MDC had signed the power-sharing agreement with Mr Mugabe's Zanu-PF party on 15 September.
But the parties have been deadlocked in allocating ministries and have called back South African mediators.
South Africa's former President Thabo Mbeki was invited back after a meeting on Friday between Mr Mugabe, MDC leader Morgan Tsvangirai and MDC splinter group head Arthur Mutambara.
'Nonsense'
On Saturday, Zanu-PF said a list of ministries had been agreed by all the parties.
Bright Matonga, Zanu-PF's deputy information minister in the previous cabinet, told the BBC the allocation was very fair.
Zanu-PF takes 14 ministries and 16 are allocated to the two factions of the MDC, he said.
Mr Matonga said the post of finance minister had yet to be decided.
But MDC spokesman Nelson Chamisa said: "This is Zanu-PF's arrogant wish list that puts the whole deal into jeopardy. It is unilateral, contemptuous and outrageous.
"Just yesterday we agreed to call in the facilitator Thabo Mbeki because there was a deadlock. The MDC totally and absolutely rejects this nonsense."
One of the MDC's key expectations was that it would get control of the police if Zanu-PF controlled the army.
Under the deal Mr Mugabe remains president while Mr Tsvangirai becomes prime minister.
But the deal has so far failed to ease the country's crippling economic crisis.
Some outlets have been licensed to sell goods in US dollars
On Thursday, it was announced that Zimbabwe's annual inflation rate had soared to 231,000,000%.
Meanwhile, the UN says it needs $140m for food aid over the next six months.
Critics of Mr Mugabe say he triggered the economic crisis when he began seizing white-owned farms for land redistribution ahead of parliamentary elections in 2000.
But Mr Mugabe blames Western sanctions which target him and his chief supporters for wrecking Zimbabwe's economy.
The crisis worsened after disputed elections earlier this year. Mr Tsvangirai gained more votes than Mr Mugabe in March's polls, but not enough for outright victory.
He pulled out of a run-off in June, accusing Zanu-PF militia and the army of organising attacks on its supporters which left some 200 people dead.

Palin abused power, probe finds


Hawa wamarekani huwa wanachekesha kwelikweli ona sasa. If kama kiongozi wa kawaida did this kutatiokea nini when she becomes Makamu wa Rais katika taifa la wababe?

this is the story !


The running mate of US Republican presidential candidate John McCain has been found guilty of an abuse of power, according to a state legislature probe.
Alaska's Governor Sarah Palin was accused of sacking a senior state official over a family feud.
But the McCain-Palin campaign team said that the report showed Mrs Palin acted within "proper and lawful authority".
The report could have an impact on Republican hopes of winning next month's US presidential election.
"I find that Governor Sarah Palin abused her power by violating Alaska Statute 39.52.110 (a) of the Alaska Executive Branch Ethics Act," investigator Steve Branchflower concluded in the panel's 263-page report.

Monegan's refusal to fire Wooten was not sole reason for his dismissal, but a contributing factor
Sarah Palin's acted within her rights as Governor of Alaska

Mrs Palin has always denied any wrongdoing, and her supporters say the charges were motivated by her political opponents.
"This was a partisan-led inquiry run by [Democratic candidate Barack] Obama supporters and the Palins were completely justified in their concern," a McCain campaign spokesperson said.
Mrs Palin was accused of dismissing Mr Monegan for refusing to sack a state trooper who was in a bitter custody battle with her sister.
The report concluded a family grudge was not the sole reason for the dismissal, but was a likely contributing factor.
However, the report said that the actual sacking of Mr Monegan was not beyond Mrs Palin's legal powers.
Speaking after a bipartisan investigating panel reached its decision on what has become known as Troopergate, Mr Monegan said he felt "vindicated".
"It sounds like they've validated my belief and opinions," he said. "And that tells me I'm not totally out in left field."
The panel found Mrs Palin in violation of a state ethics law prohibiting public officials from using their office for personal gain.
Legislators do not have the power to take formal legal action against the governor; that would be up to Alaska's Personnel Board.
If the Board decides Mrs Palin violated state law, the case will be referred to the president of the state Senate.
Mrs Palin's lawyer said that the report had not been conclusive.
"In order to violate the ethics law, there has to be some personal gain," said Thomas Van Flein.
"Mr Branchflower has failed to identify any financial gain."
And Alaskan state Senator Gary Stevens, a Republican, said there were "some problems" with the finding.
"I would encourage people to be very cautious, to look at this with a jaundiced eye," said Senator Stevens, after the report's release was announced.
Several Republican politicians had earlier attempted to have the investigation stopped on the grounds that it was politically motivated.
The investigation into the affair began before Mr McCain selected Mrs Palin as his running mate in August.
The US presidential race has now become so polarised both Republicans and Democrats will likely see the report's findings as vindication for their own trenchant views about Mrs Palin, says the BBC's Richard Lister in Washington.
Alaska's governor will either be seen as the victim of a Democratic party hatchet job, or a hypocrite.
Most voters, for now at least, seem more concerned about who will extract them from the current economic crisis, rather than any questions about political infighting in far-off Alaska, our correspondent adds.
Mrs Palin maintains she fired Mr Monegan in July over a budgetary dispute.
But Mr Monegan said he was dismissed for resisting pressure from Mrs Palin and her husband, Todd, to fire State Trooper Mike Wooten, Mrs Palin's former brother-in-law.
Mr Monegan said he simply wanted the truth to be made known.

"The governor did want me to fire [Mr Wooten], and I chose to not," he told the Associated Press news agency.
"He didn't do anything under my watch to result in termination."
Todd Palin has admitted he did publicise what he called the "injustice of a violent trooper keeping his badge".
But he said his wife, who did not give evidence to the enquiry, then told him to drop the matter.

Mbeya wapongeza sera za ubinafsishaji


UMOJA wa Wakulima Wadogo wa Chai wa Rungwe (RSTGA), Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya umeipongeza Serikali kwa kubuni sera sahihi ya ubinafsishaji, yenye maono (vision) na manufaa kwa wananchi wa kawaida.

Pongezi hizo zimetolewa jana Ijumaa, Oktoba 10, 2008 na Mwenyekiti wa RSTGA, Mchungaji Uswege Mwakalinga wakati anawasilisha shughuli za umoja wake kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufungua Kiwanda cha Chai cha Mwakaleli, Wilayani Rungwe kilichokarabatiwa upya.

Mchungaji Mwakalinga amemwambia Rais Kikwete kwenye eneo la kiwanda hicho katika eneo la Rungwe Mashariki kwenye siku yake ya pili ya ziara ya Mkoa wa Mbeya: "Tunaishukuru Serikali kwa kubuni sera yake sahihi ya ubinafsishaji, wenye maono ya mbali na wenye maslahi makubwa kwa wananchi wa kawaida. Huko nyuma, baadhi yetu, kama walivyo baadhi ya watu, tulikuwa na maoni kuwa ubinafsishaji ni sera ya ovyo," amesema Mchungaji huyo na kuongeza: "Kumbe tulikosea. Sisi katika RSTGA sasa tunajua fika faida za sera ya ubinafsishaji, sasa tunajua kuwa hii ni sera ya maana sana," amesema Mchungaji Mwakalinga.

Baada ya kuwa amesikia maneno hayo, Rais Kikwete aliingilia kati na kusema: "Ninakushukuru sana, kwa angalau kuisifia sera hii lakini pia kwa kukiri kuwa ni sera sahihi na yenye maono ya mbali."

Rais Kikwete alikuwa katika eneo hilo la Mwakaleli kufungua kiwanda cha chai cha Mwakaleli ambalo limekarabatiwa rasmi upya kufuatia sekta binafsi kuingia katika uendeshaji wa kiwanda hicho. RSTGA kinaendesha kiwanda hicho kwa ushirikiano wa ubia wa TATEPA, umoja huo wa wakulima ukiwa unamiliki asilimia 25 na TATEPA ikiwa inamiliki asilimia 75.

Kwa pamoja taasisi hizo mbili zimeunda kampuni ya Wakulima Tea Company Limited ambayo inaendesha kiwanda hicho na kingine cha chai wilayani Rungwe.

Kabla ya kuwasili kufungua kiwanda hicho, Rais Kikwete amepokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Rungwe katika eneo la Rufingo, ambako amefungua pia jengo la SACCOS la wanachama wa chama cha kukopa na kuweka katika eneo hilo, na pia kuzungumza na wananchi.

Kabla ya kufika Rufingo, Rais amesimama kwa muda katika eneo la Mwanjelwa, nje kidogo ya mji wa Mbeya, ambako amesikiliza kilio cha wananchi kuhusu ajira.

Pia amesimama katika kijiji cha Ntokela ambako ameelezwa shida ya maji na ukosefu wa matuta kwenye barabara inayopita katika kijiji hicho ili kupunguza ajali katika barabara hiyo kuu ya lami kutoka Mbeya mjini kwenda Tukuyu.

Rais pia amelazimika kusimama mara mbili mjini Kiwira kutokana na wingi wa watu, na ameahidi kuangalia upya bei za bati na saruji baada ya wananchi wa eneo hilo kuwa kumlalamikia kuhusu bei kubwa ya vifaa vya ujenzi.

Pia wamemlalamikia kuhusu pembejeo. Katika eneo la Kimo-Magereza, Rais Kikwete amesikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu shida ya maji, shida ambayo imekuwa inarudiwa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya tokea kuwasili katika mkoa huo juzi Alhamisi, Oktoba 9, 2008.


Pichani:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa Mwakaleli muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda cha Chai huko Mwakaleli wilayani Rungwe jana mchana.Picha hii ni mali ya Freddy Maro na habari na mwandishi maalum. Thanks wadau

Friday, October 10, 2008

MDAU MPYA HUYU ANAOMBA KUUNGWA MKONO WADAU

HABARI ZA KAZINAOMBA NIWEKEE TANGAZO HILI KWENYE BLOG YAKO. NDUGU WADAO WA BLOG NAOMBA MJUMUIKE NAMI KATIKA BLOG YANGU MPYA INAYOITWA http://ushaurinamsuya.ning.comHUMU NDANI UTAKUTANA NA MARAFIKI TUTASHAURIANA IKIWA NI PAMOJA NA MADA MBALI MBALI UTAKUTANA NA FUNNY VIDEO PICTURE PIA UNAWEZA KUCHATI NA NDUGU NA JAMAA KARIBUNI WOTE TUNDELEZE KIJIJI CHETU AMBACHO NI DUNIA KUPITIA MTANDAO MWALIKE NA MWENZIO ASANTENI
Mr,Elirehema G.Msuya
Hotspot Business Solution (T) Ltd
Branch Manager
P. O. Box 1122
Dodoma - Tanzania
Tel.+255 26 2322490/1
(Office) +255 26 2351175
(Home)Fax: +255 26 2322489
Cell: +255 786 359066 +255 713 552829
Website:www.hotspot-tz.com
www.ellymsuya.4t.com

Lizombi we acha utamu kolea maungoni!!!!


Oktoba Mosi huwa siku ya wazee na picha hii ya Juma Nyumayo wa Songea aliipiga siku hiyo wakati wazee walipokuwa wakitwangwa na burudani ya Kikundi cha ngoma ya Lizombi Shaba cha Manispaa ya Songea kwenye bustani ya Manispaa Songea. Thanks mdau

Watu kama sisimizi wampokea rais Mbeya


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbeya waliojitokeza kumlaki kwa shangwe wakati wa mwanzo ya ziara yake ya kikazi leo Mkoani humo.Akiwa hapa amezuia mashamba ya Mbarali waliyoepwa wekezaji kwa ajili ya kilimo cha mpunga kufanya shughuli za kulima mazao ya kutengenezea nishati mibono.

Pia akiwa njia kuelekea wiayala nyingine mwanjelwa alisimamishwa na vijana aambaow alikuwa wanalilia ajira. Amewataka waunde Tume ili akirejea katika wilaya hiyo kabla ya kumaliza ziara azungumze nao namna ya kurekebisha hali hiyo.

Unajisikie binti kwa leo...?


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mtoto aliyejiatambulisha kwa jina la Lulu Patti muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mbeya tayari kwa kuanza ziara ya siku kumi mkoani humo ambapo atazindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Picha hii ni mali ya Freddy Maro.

leo asubuhi nakuja ofisini






Kutokana na kuzidi kwa foleni kutoka makazi yangu mpakani mwa Mbagala Rangi Tatu na kongowe kuja Posta ninakofanyia kazi leo niliamua kupita njia ya Kongowe Kigamboni na kuibukia Posta. Njiani nilikuwa na kijikamera kidogo ambacho kilinipa nafasi ya kupiga picha mbili tatu pale Kigamboni, Kongowe mwisho na nikaona kumbe daraja la mto Mzinga pale Kongowe na Mbagala linajengewa njia za kwenda na miguu. Congla kwani yale magari yanayotumwa pande zote mbili yakikukuta darajani pale shughuli yake huwa pevu.

Thursday, October 9, 2008

Watatu na mganga wadakwa wakitaka nywele za albino

JESHI la polisi Mkoani Ruvuma limewatia mbaroni watu wanne kwa tuhuma za kutaka Nywele za Albino kwa ajili ya matibabu ya Mgongo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpandangindo Wilaya ya Songea vijijini, mkoani hapa, Expedito Luambano, alisema siku ya tukio mtu mmoja , John Mwangata alikwenda kwa Mama Msemwa Mkazi wa Kijijiji cha Mpandangindo, Songea Vijijini ambaye pia ni Albino na anaishi na watoto watatu ambao pia ni Albino kumuomba nywele za albino alizodai kuwa ni dawa ya mgongo.
Mama huyo alimjibu Mwangata kuwa arudi siku iliyofuatia saa tano Asubuhi ili aone jinsi ya kuwanyoa nywele hizo watoto hao Albino na kumpatia tayari kwa kupeleka kwa mganga wake kwa matibabu anayotaka.
Mama Msemwa alikwenda kwa Mwenyekiti wa Albino Mkoani Ruvuna, Amiri Msemwa ili apate ushauri. "alikwenda naye Mwenyekiti alikuja kwangu na tukawataarifu polisi na ambao kwa pamoja tulipanga mtego wa jinsi ya kuwanasa watu hao, " alisema Luambano.
Alisema majira ya saa tano walitokea watu watatu ambao walimpa Mama Msemwa shilingi 2000 ili wapewe nywele za Albino na kwa kuwa Polisi walisha panga mtego waliwakamata wote watatu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma Falhum Mshana amethibitisha tukio hilo na kuwataja watu hao kuwa ni, Joseph Mkinga Mkazi wa Mtyangimbole, Songea Vijijini, Mussa Zula, Mkazi wa Liwumbu Manispaa ya Songea na mmoja aliyejulikana kwa jina moja tu la Nyema Mkazi wa Liwumbu.
Ofisa Mtendaji huyo alisema watu hao walipoulizwa, walidai kuwa walitumwa na Mganga anayejulikana kwa jina la 'LinogaLyene' kwa tafsiri ya Kiswahili LinanogaLenyewe na kwamba pia amekamatwa . Kamanda alisema watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Habari hii imehisaniwa na Juma Nyumayo wa habariLeo ambaye ana makazi yake mkoani Ruvuma.

da subi ameleta hii ambayo nataka kushea nawe..

Umekisikia kibao cha Samba Mapangala (Orchestra Virunga) kwa jina "Obama Ubarikiwe"? 'That one'.... "my frienchs....." sikiliza: http://nukta77.com/matangazo.aspxSubi

Wednesday, October 8, 2008

Colombia tayari kutupa msaada wa kukabili mihadarati

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Nchi za Afrika zimeonywa kuwa macho na uwezekano wa kugeuzwa soko kubwa la madawa ya kulevya kutoka Marekani Kusini, hasa baada ya Marekani kuwa imedhibiti soko lake.

Onyo hilo limetolewa leo (Jumanne, Oktoba 7, 2008) na Balozi mpya wa Colombia katika Tanzania, Mama Maria Victoria Suarez wakati alipokutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu, Dar es Salaam.

Akizungumza na Rais Kikwete baada ya kuwa amewasilisha hati zake za utambulisho, Mama Suarez amesema kuwa upo uwezekano kuwa nchi za Afrika zikalengwa na wafanyabiashara wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya baada ya soko la Marekani kudhibitiwa.

“Kama unavyojua, Marekani iliyokuwa soko kuu la madawa ya kulewa sasa imedhibiti biashara hiyo kwa kiasi kikubwa, na hivyo inawezekana kuwa hawa wachuuzi wakaanza kutafuta soko jipya katika Afrika,” amesema mama huyo na kuongeza kuwa kwa sababu hiyo upo umuhimu mkubwa wa Afrika kushirikiana na Colombia katika udhibiti wa madawa ya kulevya.

“Utakuwa unajua Mheshimiwa Rais kuwa madawa ya kulevya yametusumbua sana katika Colombia, na hivyo tunao uzoefu kidogo ambao tunaweza kugawana na Afrika kwa jinsi Bara hili linavyoweza kupambana na madawa ya kulevya,” amesema mama huyo ambaye makazi yake yako Nairobi, Kenya.

Mama huyo amesema kuwa kwa sasa inaonekana kuwa sehemu ya Afrika iliyoathirika zaidi ni Afrika Magharibi, na kuwa bado eneo la Mashariki halijaguswa sana na biashara hiyo haramu.

Lakini Rais Kikwete amemwambia mama huyo kuwa hata Afrika Mashariki imeanza kuwa soko kubwa la madawa ya kulevya. “Hapa sisi tunalo tatizo kubwa. Hapa mjini, kwa mfano, vijana wengi wameharibiwa sana na madawa haya. Tunahitaji uzoefu na ushirikiano wa Colombia katika jambo hili.”

Rais pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Dk. Guido Cornelius Herz.

Katika mazungumzo kati yake na Rais Kikwete baada ya kuwa amewasilisha hati zake, Dk. Herz amemhakikishia Rais Kikwete kuwa Ujerumani haitapunguza misaada yake kwa Tanzania ama nchi nyingine za Afrika kutokana na misukosuko mikubwa inayoukumba mfumo wa fedha duniani.

“Napenda kukuhakishia Mheshimiwa Rais kuwa pamoja na misukosuko mikubwa inayoukumba mfumo wa fedha duniani, hasa katika nchi ya Marekani na Bara la Ulaya, bado Ujerumani itaendelea kuheshimu ahadi zake kwa wabia wake wa maendeleo, kama Tanzania na nchi nyingine za Afrika,” amesema Balozi huyo.

Dk. Herz ametoa uhakikisho huo baada ya Rais Kikwete kuwa amesema kuwa ingawa kwa sasa Tanzania haijakumbwa na athari za misukosuko hiyo ya mfumo wa fedha duniani, wasiwasi ulioko ni kwamba nchi tajiri zinazokumbwa na hali hiyo zinaweza kuamua kupunguza misaada yake kwa wabia wake wa maendeleo katika Afrika.

Rais pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya wa Austria na Thailand. Mabalozi hayo, Apichit Asatthawasi wa Ufalme wa Thailand na Roland Hauser wa Austria wana makazi yao Nairobi, Kenya.



Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

07 Oktoba, 2008

Walimu sasa wapitisha azimio la kugoma mpaka kieleweke

BARAZA Kuu la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo lilipitisha tamko la kuanza mgomo mfululizo wa walimu kuanzia Jumatano ijayo iwapo serikali itakuwa haijawalipa madai yao yote.
Kikao cha Baraza hilo lililohudhuriwa na wajumbe 81 kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania Bara kwa kauli moja kilipitisha azimio hilo la kuanza kwa mgomo huo.
Rais wa Chama hicho, Gratian Mukoba, akisoma maazimio na tamko hilo rasmi mbele ya wajumbe hao, alisema azimio la kwanza ni la walimu wote nchini kuingia katika mgomo rasmi katika muda huo uliopangwa kutokana na serikali kushindwa kutimiza madai ya walimu hadi ilipofika leo.
Kwa mujibu wa Rais huyo, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na serikali kushindwa kulipa madai mbalimbali ya walimu yakiwamo fedha za likizo, uhamisho na kupandishwa kwa madaraja.
“Walimu wote nchini wataingia katika mgomo kama ulivyopangwa kuanza Oktoba 15, mwaka huu…mgomo huo hautasimama hadi serikali itakapolipa madai yote,” alisema Rais huyo.
Hata hivyo alisema pamoja na kuanza na kuendelea kwa mgomo huo , walimu wanaosimamia mitihani ya kidato cha nne wa mwaka huu wao wataendelea kusimamia hadi siku ya mwisho ya mitihani hiyo na kujiunga na wenzao kuendelea na mgomo.

Ewura waminywa kiaina Morogoro, wenye mafuta wapeta





MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeshindwa leo imeshindwa kuvifunga vituo sita vya kuuza petroli mjini hapa vilivyobainika kuuza mafuta yaliyochanganywa, kutokana na amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa ya kuzuia kuvifunga.
kama wanaojua nini kitajiri wakuu wa vituo hivyo walikimbilia mahakamani ambapo walipata amri hiyo ya mahakama jana.
Vituo vinavyohusika ni Oilcom-Kihonda, Kobil-Msamvu, Camel Oil-Msamvu, Kobil-Barabara ya Dodoma, Petro-Sokoine na Oil Com-Nanenane.
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Titus Kaguo alisema hadi leo asubuhi wakati wa mchakato wa kufunga vituo hivyo, Ewura ilikuwa haijapata nakala ya amri ya mahakama. Kutokana na hali hiyo, Ewura inakusudia kufuata taratibu nyingine za kisheria kuhusiana na amri hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kwenda kutaka kufunga vituo hivyo sita, Mkurugenzi wa Petroli wa Ewura, Cyril Massay, alisema ukaguzi wa kushtukiza ulioanza kufanyika Mei, 2007 katika mikoa 14, Mkoa wa Morogoro umebainika kuwa na vituo vingi vinavyouza mafuta yaliyochanganywa.
Mikoa mingine iliyokaguliwa na Ewura kwa kipindi hicho ni Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Shinyanga, Pwani, Manyara, Dodoma, Iringa, Tabora, Kagera na Tanga.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo tatizo la mafuta kuchanganywa, hasa dizeli na mafuta ya taa limethibishishwa kuwapo kwa kiwango kikubwa hapa nchini.

Pichani ni Mkurugenzi wa Petroli wa EWURA, Sirili Massay ( katikati) akizungumza kwa kusisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ( hawapo pichani) juu ya masuala mbalimbali za taasisi hiyo na picha nyingine ni za baadhi ya vituo vilivyopata mwavuli wa Mahakama.Picha zote na John Nditi wa HabariLeo Morogoro

haya ndiyo niliyoyapata kuhusu Athumani Hamis

wapenzi wasomaji
Nilipata habari na hii habari yaliyo yangu nimeyanyaka na yanayofaa kuangaliwa na marafiki na wadau wa blogu hii nimewaachia...Nitaarifa ya kufikia jana Oktoba Saba,2008.
Lukwangule


Dear Beda,
Mambo hapo Dar?Nimeshukuru kwa kuwa umefanikiwa tena kunipata. Kazi uliyonituma nimeikamilisha lakini ina tofauti na ile ya mwanzo lakini ni vyema ukaelewa kwamba watu hapa wanafanyakazi more professsional.
Naam sasa turejee habari uliyoniomba nifuatie: Kwanza Athumani yuko bomba na huwezi kuamini kwamba anaumwa namna ile. Anazungumza na unaweza kumsikia na ukiwa nje huwezi kabisa kujua kwamba Athumani anaumwa.
Pili yule muuguzi amerejea nyumbani kati ya juzi au jana.Mnaweza kumtafuta kuzungumza naye.
Tatu ile operesheni haikufanyika. Niliuliza maswali mawili kwa mpigo na nilijibiwa standard.Nikajua imefanyika na hali inaendelea vyema. Watu niliozungumza nao pamoja na wanaomsimamia ni kuwa ile operesheni iliahirishwa baada ya madaktari kukubaliana kwamba ni lazima kwamba kidonda kitibiwe kipone ndio operesheni ifanyike.
Madaktari wamekuwa wakisita kufanya operesheni kwani ipo karibu na kidonda wanahofia wanaweza wakasababisha complications. Kuhusu mawasiliano ni wazi inategemea zaidi mafanikio ya operesheni hiyo ambayo itafanyika wakati wowote ule ambao madaktari watakubaliana.
La msingi kaka yangu Athumani yupo bomba na hospitali hii ni njema kabisa kwani alipofika tu alifanyiwa checking yote ndiyo ikazaa haja ya operesheni na damu kuongezwa.
Na pia scan ya kwetu ilikuwa si njema wao wakafanya yao na kila kitu wanakijua.Kumbuka nilikueleza pia kwamba madaktari waliudhika na kucheleweshwa kwake kwani angeliwahi walikuwa na uhakika wa mambo mazuri zaidi kwa Athumani.
Unaweza kupata mengi kwa huyo muuguzi aliyerejea kuona jinsi mambo yalivyo mazuri hapa Afrika Kusini kuhusu tiba.
Pengine busara na heri sana utaratibu wa hapo nyumbani wa kupeleka wagonjwa nje ukabadilika kwani unafanya baadhi ya wagonjwa kufikishwa maeneo ya tiba wakiwa wamechelewa au tatizo limeongezeka.
Basi nisalimie wote

MADAGASCAR: No welcome for sex tourism

Kwenye visiwa utalii hushamiri sana. lakini pamoja na utalii kuna mambo ambayo yanaambatana nayo, kumomong'onyoka kwa maadili na kuingia kwa utalii unajihusisha na ngono. Madagascar wameliona hilo na wamechukua hatua.Je Zanzibar inaweza kujifunza nini kutoka Madagascar? Yapo mengi hasa ikizingatiwa kuwa sasa hivi pamoja na ukimya wetu Unguja imegeuka kisiwa cha ngono, wanaokuja wanajua namna ya kupata ngono wanazohitaji.Hii ni taarifa ya IRIN.
Lukwangule

TOLIARA, 7 October 2008 (IRIN) - The warning posters start at the airport in the capital, Antananarivo, informing visitors that Madagascar says "NO to sex tourism" and "Malagasy women are not tourist souvenirs".
Large billboards notifying arrivals that the authorities will also prosecute those caught having sex with children line the route into the city, and at tourist hotels - along with a colourful "Welcome to Madagasikara - the land of the lemurs" - there is likely to be a sign saying the hotel has a right to check the age of anyone accompanying guests to their rooms.
Madagascar, the vast tropical island off the east coast of Africa, is trying to expunge itself from the sex tourism map, and especially to close its doors to paedophiles shopping for minors.
To underline its commitment, the government has adopted a new law against the sexual exploitation of children that includes punishment of the adult exploiters; several foreigners have been convicted as a result.
But a walk after dark through the streets of Toliara, a thriving tourist town in southern Madagascar, shows that much still needs to be done. Sex workers own the streets, blowing kisses and waving at foreigners, trying to cash in on the tourists who are not visiting this impoverished Indian Ocean island for its unique bio-diversity.
"It's a very cheap place, women are beautiful, there are few controls on sex tourism. Nobody says anything about this; you can come here and do whatever you want," said Jose Louis Guirao, who runs projects for Bel Avenir, a non-governmental organisation (NGO) promoting educational, social and health-related initiatives. "The women start when they are 10 to 12; they are very young."
A report by the US State Department this year said Madagascar was a "source country for women and children trafficked within the country for the purposes of sexual exploitation", but praised the government for trying to tackle the problem.
The reality
The reality is that children, mostly from rural areas, are highly vulnerable to exploitation: they are trafficked for domestic servitude, forced labour and sex work; children often enter the labour market with the approval of their mothers, for whom their income may be the only source of living. In Toliara Province, for example, 80 percent of people live in poverty.
Bruno Maes, the UN children's fund (UNICEF) representative for Madagascar and the Comoros, is unequivocal in his condemnation of the sexual exploitation of children. "A child who is a victim of sexual abuse may suffer serious and lifelong consequences; this is a crime that is totally unacceptable in all contexts. UNICEF is concerned about its spread in Madagascar," he told IRIN.
At Bel Avenir's offices, Aline, a sex worker, is attending a meeting with her colleagues, some of whom have brought their children, to find out more about their rights, future opportunities, and protection.
Aline makes jokes and plays with the condoms distributed by the NGO, but turns serious when she talks about her trade. "We take on every client that there is - we need money. I don't say no, but the girl who gets the blond client, a French or an American, is the lucky one," she told IRIN. "Many foreigners come to Toliara and get girls. They like Madagascar, they like the young girls very much."
The main source countries for child sex tourists are reportedly France, Italy, Spain, Germany and Switzerland, and the neighbouring islands of Mauritius and Reunion. Victims are usually girls, but reports of foreign male tourists seeking sex with underage boys are becoming more frequent.
Advocacy groups say progress is being made in tackling child sex tourism, but controlling it is very difficult because of corruption, and even protests from the children's parents - prostitution is often an inherited occupation passed down for generations.
Madagascar has so far been much less affected by AIDS than most other countries in continental Africa, but international organisations warn this could change quickly. "The total lack of knowledge about the disease, from what I see here, means that it could soon be much, much worse," said Bel Avenir's Guirao.
An economic boom linked to local mining projects has attracted sex workers from across the island to the flourishing new towns, and an outbreak of syphilis in the southeastern mining town of Fort Dauphin in 2007 rang alarm bells: it pointed to the lack of condom use, and sexually transmitted infections also heighten the risk of HIV transmission.
Asked if she used the condoms given out by Bel Avenir, Aline said: "Many clients don't want that, and they give dollars or euros and I agree no condom. That is my life in Madagascar."

Sauti za Busara 2009 mambo yekete, samba naye yumo


The sixth edition of the Sauti za Busara music festival will take place in Zanzibar, 12-17 February 2009; admission is free to all each day before sunset.Sauti za Busara (Sounds of Wisdom) is an international festival celebrating East African music taking place around the second weekend of February each year in Zanzibar.
Featuring top-quality musical performances by more than 400 established and upcoming artists (40 groups in total), Sauti za Busara has already established itself as one of Africa’s leading music festivals. It’s an event that unites people in celebration.We are proud to announce Samba Mapangala has just confirmed he will be performing with the legendary Orchestre Virunga. He is one of East Africa’s best-loved musicians, with a series of hits over the past 25 years, including Virunga, Ahmed Sabit, Vunja Mifupa, Sungura, Vidonge, Dunia Tuna Pita, and Nyama Choma.Samba Mapangala & Orchestre Virunga (DRC/Kenya/USA), Msondo Ngoma Band (Tanzania), Omar Pene & le Super Diamono (Senegal), Mangala Camara (Mali), Nawal (Comoros/France), King Ayisoba (Ghana), TY (UK), Meta and the Cornerstones (Senegal/USA).
Others are The Moreira Project (South Africa), Comrade Fatso and Chabvondoka (Zimbabwe), Jagwa Music (Tanzania), AY (Tanzania), Joh Makini (Tanzania), Elemotho (Namibia), Segere Original (Tanzania), Best of WaPi (Pan Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar), Bi Kidude (Zanzibar).
Others are Iddi Achien'g (Kenya), Khethi with Kibo Sounds (South Africa/Tanzania), Rachel Magoola (Uganda), Wahapahapa Band (Tanzania), Omega Bugembe Okello (Uganda/USA), Aron Nitunga (Burundi/Canada), Safar (Zanzibar), Kiumbizi (Pemba), Zinduka Ngoma (Zanzibar), Dj Side (Zanzibar), and more to be announced

Tuesday, October 7, 2008

Mhe. Marc Ravalomanana akiwa nchini Zanzibar


STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY


PRESS RELEASE



Zanzibar 7.10. 2008
MADAGASCAR imeahidi kuanzisha uhusiano na ushirikiano wake na Zanzibar katika sekta za uchumi na kuelezea kufurahishwa na mafanikio yaliopatika Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Amani Abeid Karume.

Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Madagascar Mhe. Marc Ravalomanana wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume Ikulu mjini Zanzibar.

Katika maelezo yake Rais Ravalomanana ambaye alifuatana na mkewe pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na ujumbe wake alimueleza Rais Karume kuwa Madagascar iko tayari kuanzisha ushiririkiano na uhusiano kati yake na Zanzibar katika sekta za uchumi ikiwemo utalii na biashara.

Ravalomanana alimueleza Dk. Karume kuwa juhudi zitaanza kufanywa kwa kukaa pamoja kati ya Mawaziri wa nchi mbili hizo kwa kuangalia taratibu za kuanzisha na kuendeleza ushirikiano huo wa kibiashara na utalii.

Alieleza kuwa kutokana na Madagascar na Zanzibar kuwa vyote ni visiwa ambavyo vinazalisha zao la karafuu itakuwa ni jambo la busara kushirikiana kwa pamoja katika kuangalia soko la pamoja hali ambayo itasaidia kuimarisha sekta ya biashara kwa pande zote mbili.

Rais huyo wa Madagacar alieleza kuwa ipo haja ya kukaa pamoja na kuzungumza pamoja kwa mustakabali wa kushirikiana katika kuendeleza na kukuza sekta hizo kwa lengo la kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

Aidha, Rais Ravalomanana na Rais Karume walitoa nafasi ya mazungumzo kati ya viongozi wa ujumbe huo na waziri wa Biashara, Utalii na Uwekezaji Mhe. Samia Suluhu Hassan ambao walijadili hapo hapo juu ya kuanza kwa taratibu hizo haraka iwezekanavyo.

Katika majadiliano yao mafupi yaliofanyika hapo hapo Ikulu viongzi hao walifikia makubaliano ya kukutana kati ya Waziri anayeshughulikia masuala hayo wa nchini Madagascar pamoja na Waziri Suluhu kukaa pamoja na kwa lengo la kushirikiana kwa karibu.

Hasa katika suala zima la zao la karafuu. Pia, viongozi hao walieleza namna ya kuanzisha usafiri wa ndege wa moja kwa moja kutoka Madagascar kuja Zanzibar hali ambnayo itazidi kupanua soko la biashara na utalii. Sambamba na hayo, katika mjadala huo kulikubalika kuanza taratibu hizo kabla ya mkutano wa Kimataifa wa Biashara.

Nae Rais Karume alitoa pongezi zake kwa Rais Ravalomanana kwa mashirikiano mazuri anayoyaendeleza ikiwa ni pamoja na azma yake hiyo ya kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi katika sekta za maendeleo. Dk. Karume alisifu mafanikio mbali mbali yaliopatikana katika sekta za maendeleo na uchumi nchini Madagascar na kueleza kuwa kufanikiwa huko kunatokana na juhudi za wananchi na viongozi wao.

Rais Karume alisema kuwa kuna njia nyingi za kushirikiana kati ya Zanzibar na Madagascar ikiwemo biashara, utalii na hata usafiri wa anga kwani usafiri huo wa ndege kutoka Madagascar hadi Zanzibar ulikuwemo mnamo miaka ya sabini.

Alisema kuwa katika sekta ya utalii ipo haja ya kushirikiana zaidi kwa pande mbili hizo kwani tayari Madagascar imeshapiga hatua kubwa katika sekta hiyo ambapo pia Zanzibar hivi sasa nayo inasonga mbele kwa kasi katika kuimarisha na kuendeleza sekta hiyo ambayo ni muhimu.

Sambamba na hayo, Rais Karume alisifu uhusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizo ambapo alisema unaweza kuimarika na kutoa mafanikio kwa pande zote mbili na Zanzibar itaendelea kuuthamini na kuutunza.

Rais Ravalomanana akiwa na mkewe walipokelewa na mwenyeji wao Dk. Karume akiwa na mkewe Mama Shadya Karume katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Viongozi mbali mbali wa Vyama vya siasa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walifika uwanja wa ndege kumpokea mgeni wao huyo, akiwemo Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. Ali Juma Shumuhuna.

Mara baada ya mapokezi hayo kiongozi huyo alifanyiwa taratibu zote za mapokezi wanayofanyiwa viongozi wa Kitaifa wanapofika nchini, Pia kiongozi huyo akiwa na ujumbe wake na pamoja na mkewe waliangalia ngoma za asili kutoka vikundi vya utamaduni vya Zanzibar. Mara baada ya mazungumzo na Dk. Karume, Ravalomanana aliendelea na ziara yake ya siku moja Zanzibar kwa kwa kwenda kuangalia sehemu za kihistoria likiwemo Kanisa la Mkunazini na kupata historia juu ya soko la utumwa na baadae kuelekea Kizimbani kuangalia shamba la viungo na baada ya hapo alirejea Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya chakula kilichotayarishwa kwa ajili yake na ujumbe aliofuatana nao, chakula kilichotayarishwa na mwenyeji wake ambae ni Rais Karume.

mwisho


Pichani Rais wa Madagascar Marc Ravalomanana akisalimiana na watoto baada ya kutembelea Kanisa la Mkunazini mjini Unguja leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini. Picha hii ni mali ya Mwanakombo Jumaa.

LEO ni siku ya kuzaliwa Rais Jakaya Kikwete


LEO ni siku ya kuzaliwa ya Rais Jakaya Kikwete ambaye anatimiza umri wa miaka 58.
Rais Kikwete alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika Kijiji cha Msoga, Kata ya Lugoba Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Ni mmoja wa watoto wa Khalfan Kikwete na Asha Binti Jumbe (wote ni marehemu).
Alizaliwa akiitwa Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete, na kukua katika familia ya viongozi. Babu yake alikuwa Chifu; baba yake alikuwa kiongozi wa serikali; yeye alianzia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baba yake mzazi alifariki dunia Agosti 8, 1998, Kinondoni Dar es Salaam; mama yake aliaga dunia Juni mosi, 1999. Mama mzazi wa Rais Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wake watano wa Mzee Khalfan aliyekuwa na watoto watatu.
Rais Kikwete ni mwanawe wa pili, akitanguliwa na dada yake yake mkubwa, Zena (marehemu), na mdogo wake, Mohamed Mrisho Kikwete.
Kabla ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Kikwete alikuwa Waziri kwa miaka 17 ikiwamo miaka 10 ya uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aligombea urais katika uchaguzi Mkuu uliopita akashinda, na Desemba 21, 2005 aliapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania.
Kwa mujibu wa kitabu cha ‘Kikwete, Safari ya Ikulu,’ Rais Kikwete ana watoto saba; wawili kati ya hao, Ridhiwani na Salama alizaa na mke wake wa kwanza, Aziza Sabuni (marehemu); watano amezaa na mkewe wa sasa, Salma ambao ni Miraji, Ally, Khalfan, Mwanaisha na Rashid ‘Chodo’.




Pichani Rais Jakaya Kikwete akikata keki wakati wa hafla fupi ya kusherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake ambapo ametimiza miaka 58 . Sherehe hizo ziliandaliwa na wafanyakazi wa Ikulu ya Dar es Salaam. Picha hii ni mali ya Freddy Maro wa Ikulu

Utamu kolea, weeeh


Wasanii wa Namibia wakicheza ngoma ya Kalahari wakati Mapokezi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako nchini humo jana. Waziri Mkuu yupo nchini Namibia kwa ziara ya kiserikali. Hii ni Picha ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Monday, October 6, 2008

Mitihani ya kidato cha nne yavuja


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo asubuhi lilifuta mtihani wa hisabati wa Kidato cha nne baada ya kumaizi kwamba jamaa walipata 'nondo' na kuzama nayo.

Mitihani ya Kidato cha nne ilianza nchini kote leo.

Kutokana na kuvuja kwa mtihani huo , hisabati nyingine sasa itafanyika Oktoba 27, mwaka huu kuanzia saa 2:00 hadi saa 5:00 asubuhi.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako alisema walipata taarifa za kuvuja kwa mtihani huo pamoja na ya Historia, Fizikia na Lugha ya Kiingereza na kulazimika kuchukua polisi kwenda sehemu waliyoelezwa na kuipata mitihani hiyo.
Dk. Ndalichako alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kabla ya mchana wa leo kuhusu tukio hilo, baadaye akafanya mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lakini hakutaja sehemu walipoipata mitihani kwa maelezo uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na uvujaji huo ili hatua stahili zichukuliwe.
Alisema ilipofika saa 6:00 usiku wa kuamkia leo, baada ya kuangalia kwenye data base yao walithibitisha mtihani uliokuwa wa kweli (umevuja) ulikuwa wa Hisabati pekee na hivyo mitihani mingine itaendelea kufanyika kama kawaida kwa kuzingatia ratiba iliyokwishasambazwa.
Dk. Ndalichako alionyesha shaka na wafanyakazi wa baraza hilo kuwa huenda wamehusika kikamilifu katika kuuza mitihani lakini akasema wazi kwamba hawezi kujiuzulu kwani haitasaidia kitu.
Hii si mara ya kwanza kwa nchi hii mitihani kuvuja ila safari hii imekuwa ni funga kazi.

Pichani baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kisutu wakiwa wamekaa kujisomea leo asubuhi baada ya kuelezwa kuwa mtihani wao wa kwanza umefutwa kutokana na kuvuja.

Msimbazi ' Simba' watimuana, kisa vipigo mfululizo


UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba imewafukuza na kuwasimamisha wachezaji na makocha wa timu hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali maarufu kama ‘Field Marshal’ alisema leo mbele ya wanachama wa klabu hiyo katika makao makuu ya Simba yaliyopo mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo ilifikiwa na kamati za utendaji, ufundi na mashindano baada ya kuwahoji wachezaji wote wa timu na benchi la ufundi mmoja baada ya mwingine juu ya tuhuma mbalimbali zilizopelekea timu kuwa na mwenendo mbovu kwenye ligi

Dalali alisema katika hicho kilichofanyika juzi kamati hizo zilifikia uamuzi wa kuwatimua kwenye klabu hiyo kiungo mkabaji kutoka nchini Kenya Edwin Mukenya na kipa wake namba moja Amani Simba pia katika mkumbo huo wa kufukuzwa yumo Kocha Msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo 'Julio' na kocha wa magolikipa Iddi Pazi ‘Father’.

Aidha Dalali alisema wachezaji Mussa Hassan Mgosi na Henry Joseph wamesimamishwa kwa muda.Wachezaji Ulimboka Mwakingwe ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Simba na kiungo mchezeshaji Mohamed Banka wamepewa karipio.

Kwa mujibu wa Dalali uamuzi huo pia umezingatia mapendekezo ya kocha mkuu Krasmiri Benzinki na kufuatia uamuzi huo benchi la ufundi la Simba litakuwa chini ya Benzinki ambaye sasa atasaidiwa na mlinzi wa zamani wa klabu hiyo Amri Said.


baadaye kidogo Mwenyekiti huyo wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali, alitangaza kujiuzulu wadhifa huosaa chache baada ya wanachama na wapenzi kuutaka uongozi wake ung’oke kutokana na kuchoshwa na mwenendo mbovu wa timu yao ya soka katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Dalali maarufu kama Field Marshall miongoni mwa mashabiki wake, alitangaza uamuzi huo saa tisa alasiri na kukaririwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika matangazo yake.

“Nimeamua kujiuzulu wadhifa wangu wa Mwenyekiti wa Simba kwa sababu watu wamekwenda nyumbani kwangu, wamevunja milango ya nyumba yangu, wamewapiga wanangu…siwezi kuendelea kuiongoza Simba. Mimi si Mwenyekiti tena wa Simba, waitishe uchaguzi mwingine,” alisema Dalali alipozungumza na radio ya TBC Taifa.


Picha hii ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali akizungumza na wanachama na wapenzi wa timu ya Simba waliofika makao makuu ya Klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam kupinga kusimamishwa kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya baadaye kuamua kusema haiwezekani kukaa na wanachama wahuni wanaenda kuwashikisha adabu watoto wake. Hivi kweli kuna uhusiano wa klabu na familia za watu.Picha hii ni ya Yusuf Badi.

Kwa staili hii siwezi kuucheza mpira wa miguu


Mchezaji wa timu ya soka ya kombaini ya Kibosho Mgiye Shebe (katikati) akichuana na Ladaki Benedict wa kombaini ya Tambarare katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Mbunge wa Moshi Vijijini Cyril Chambi yanayozishirikisha timu kutoka shule za sekondari katika jimbo hilo na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Tambarare ilichapwa 2-1. Picha hii ni mali ya TIGO waanzilishi wa Extreme

Hivi mdau kweli imekaa sawa kweli?


Ajali nyingi za magari hutokea kwa kusababishwa na madereva wazembe, pichani ni moja wa madereva hao wa basi la Fresh Coach akijaribu kuyapita malori mawili ya mizigo katika eneo lililo na kona pamoja na mlima bila kujua athari ambayo anaweza kuipata kwa kuhatarisha maisha ya abiria na mali. Hebu angalia ! Huoni juu, upo kwenye kona na unampita mtu na mtoto wake na lori jingine pia!Yaani kwa mpigo duh! Picha hii ni mali ya Father Kidevu aka Mroki Mroki.

Ngiri wanapojinafasi karibu na binadamu


Nguruwe pori aka ngiri ( sio ile ya binadamu) wakila majani kwa staili kama wanavyoonekana pichani .Hapa ni karibuni na eneo la vyoo vinavyotumiwa na wageni wanaotembelea Pori la Akiba la Wanyama la Selous eneo la Matambwe, Kata ya Kisaki, Wilayani Morogoro picha hii ni mdau John Nditi wa Morogoro.

Tunakula vya wenzetu sisi je?


Nani anajua maana ya bango hili?

Wapo watu wanaosema kwamba huu ni udhalilishaji, wapo wanaopata kigugumizi kulizungumza, lakini hawalipendi. Kwangu mimi naona ni opportunity nzuri za kutuambia Watanzania kwamba tunakula kodi za wenzetu je sisi tunakumbuka kutoa kodi hizo ili zifanye mambo ya maana kwetu na kwa wengine? Na kama tunatoa tunajua zinafanya nini? Na tunapojua zinafanya nini tunaelewa vipi somo hili la Uraia.?

Picha hii niliomba nipigiwe na muungwana Yusuf Badi baada ya kusikia malalamiko mengi katika mabasi yetu ya daladala Mbagala.. Mbagala hadi Posta. Yusuf ana makazi yake pale Mtongani alipochukua 'snap' hii kwenye barabara ya Kilwa ambayo inaendelea kujengwa. Kasi ya ujenzi inatia moyo ingawa mifereji bado mhuuu.... Na foleni wakazi wa Mbagala wanakoma, si asubuhi si jioni.

Saturday, October 4, 2008

Habari zaidi juu ya nini kilijiri Tabora kabla ya vifo

HABARI za kuudhi zinaendelea kumiminika kuhusiana na mkasa mzito wa kupoteza watoto 19 kwa mpigo wakati wa disko mjini Tabora kwenye sikuku ya Idd.
Baadhi ya watoto walionusurika kifo katika ukumbi wa Bubbles Night Club siku ya Idd mosi ambako wenzao 19 walipoteza maisha, wamesema wanaamini ulevi wa baadhi yao ulisababisha janga hilo.
Watoto hao walisema pia kwamba tathmini yao inaonyesha kwamba waliokuwamo ndani ya ukumbi siku hiyo walikuwa kati ya 1,000 hadi hata 1,500.
Uwezo wa ukumbi huo ambao ulijengwa kwa ajili ya mikutano ni kuhudumia watu wazima 150. Mmoja wa watoto hao akizungumza kwenye maziko ya rafiki yake ambaye walikuwa naye disko siku hiyo, Said Sudy (12) alisema siku hiyo ya tukio, mabaunsa wa ukumbi huo walikuwa wakimlazimisha kila mtoto aliyekuwa anaingia ukumbini kununua pombe aina ya Simba Gin. Polisi inaendelea kuwatafuta mabaunsa hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo .
Kwa habari zaidi ingia saiti ya HabariLeo http://www.habarileo.co.tz

Zain walipowapelekea wateja wao Acudo Impact


Rapa wa bendi ya Akudo Impact, Canal Top akighani huku mnenguaji wa bendi
hiyo akicheza wakati bendi hiyo ilipotumbuiza ukumbi wa Equator Grill, Temeke,
Dar es Slaaam juzi. Maonyesho yote ya sikukuu ya Idd ya Akudo yalidhaminiwa na
kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ambayo pia ilidhamini maonyesho ya
Vibration Sound na vikundi vya Hip-Hop Zanzibar

Hii sikuweza kuvumilia niliichukua


Hii ilikuwa kali sikuvumilia kuiacha. Hii ni sehemu tu ya mavituzi yaliyochanganya katika tamasha la Makuya huko Ntwara somo.

Inavyoonekana Ilikuwa ni makamuzi kwa kwenda mbele .... kama kaka michuzi alivyosema we acha bwana ngoma za asili ni mazoezi tosha kabisa. Unaweza kuyaona makamuzi haya ndani ya http://makuyafestival.blogspot.com/ picha hii imetoka kwa mdau kwame mchauru aliyeshuhudia tamasha hilo.

Mpunga wa nchi kavu ndani ya Ruvuma


Huenda siku moja Ruvuma wakafanikiwa vikali katika kuilimo cha mpunga kutokana na juhudi zao za kujifunza mambo mengi katika kufanikisha kilimo cha mpunga wa nchi kavu.


Pichani ni Wawikilishi wa Kata toka Halamashauri ya Songea vijijini wakiwa katika Shamba darasa la Seedfarm, Manispaa ya Songea, kujifunza kilimo cha mpunga wa nchi kavu. Wa kwanza kushoto ni mtaalamu wa kilimo cha mpunga toka Morogoro, Ramadhani Upole, aliyeletwa na Ofisi ya Vicoba kufundisha wakulima namna ya kustawishs kilimo cha zao hilo tamu kwa kulikuwa ili kupambana uhaba wa chakula kwa kuwa na aina mbalimbali ya nafaka. Ruvuma ni maarufu kwa mahindi na maharage. Picha hii ni ya mdau wa Ruvuma kaka Juma Nyumayo.

wawakilishi wa rwanda ndani ya east africa model search


Hawa ndio visura kutoka Rwanda wataliwakilisha taifa hilo katika mchuano wa east africa model search.Visura haow alipatikana baada ya mchuano mkali mjini kigali. Kutoka kushoto ni Ninnete Hezagira, Nadege Gasama, Noela Aushimiyamama na Nannnete Ausabe.Picha kutoka kwa kaka Michuzi Jr ndani ya blog yake

Friday, October 3, 2008

Wengine zaidi wadakwa kwa maafa ya Tabora

WATU wengine wawili wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio lililosababisha vifo vya watoto 19 waliokufa wakati wanacheza muziki siku ya Idd Mosi.

Polisi walisema leo kuwa waliokamatwa ni Meneja wa disko la One Ten Teck Jaffar Rashid na Meneja wa Bubbles Night Club, Vituko Salala. Kabla ya kukamatwa kwa mameneja hao, Polisi waliwakamata wamiliki wa madisko hayo ambao ni Projestus Fidelis na Shashikant Manji Patel.
Kwa mujibu wa vyombo vya dola watu hao ndio waliandaa disko la watoto katika siku hiyo ya Idd.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, alisema leo kuwa wakurugenzi hao na mameneja wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu chanzo cha tatizo lililosababisha watoto hao kupoteza maisha.
Alisema Polisi imempa taarifa rasmi ya kushikiliwa kwa watu hao, huku ikimuarifu kwamba walinzi wa milangoni katika madisko hayo mawili "Mabaunsa" nao wanasakwa ili waweze kuhojiwa kuhusu sakata hilo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema wakurugenzi hao, watahojiwa pia na Tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkasa huo, ambayo alisema ilianza kazi leo na kuwataka wananchi waipe ushirikiano ili iweze kupata taarifa za ukweli zitakazofanyiwa kazi na serikali.
Juzi watoto 19 walikufa dunia na wengine kulazwa hospitali ya Kitete baada ya kukosa hewa katika kumbi za disko wakatik wa sherehe ya idd.
Sherehe za Idd hufanyika kuadhimisha kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.

Damu yamwagika Tarime

WATU wawili wafuasi wa CCM na Chadema wamekufa kwa kukatana kwa panga na kisu baada ya kutofautiana kimtazamo kuhusu ushabiki kwa vyama vyao jana usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Liberatus Barlow, amewataja waliouana kuwa ni Mwita Marwa (25) na Manga Mesere (22), wote wakazi wa Kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu.
Barlow alisema kwamba tukio hilo lilitokea jana saa 12 jioni wakati marehemu hao walipokuwa wakinywa ulevini na kuanza kutoleana matusi yaliyosababisha Mesere kumjeruhi shingo Marwa ambaye kabla hajakata roho alimchoma Mesere kisu tumboni na kusababisha utumbo kumwagika.
Barlow aliongeza kuwa kutokana na vifo hivyo hakuna aliyekamatwa kwa sababu mahasimu hao waliuana baada ya kuchokozana wao wenyewe.
Alisema Polisi itafanya uchunguzi na kuweka jalada hilo katika kumbukumbu.
Hata hivyo, amewaonya wanasiasa waache siasa za mabishano na kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kufikia hatua ya kuuana.

Athumani afanyiwa operesheni


Mpiganaji Athumani Hamisi, Mhariri wa Picha wa magazeti ya habariLeo na Habarileo Jumapili ambaye yupo Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata ajali mwezi uliopita maeneo ya Kibiti akiwa njiani Kwenda Kilwa kushiriki futari ya Vodacom amefanyiwa operesheni leo.
Taarifa za kuaminika zinasema kwamba operesheni hiyo imefanikiwa.

Hata hivyo haikuzungumzwa mipango yake ya tiba.Athumani
Watu ambao wameiambia blogu hii wamesema kwamba madaktari hakuwaridhishwa na jinsi mgonjwa huyo alivyocheleweshwa kufikishwa hospitalini kwa matibabu.
Ilichukua siuku kadhaa kwa mgonjwa huyo kufanyiwa taratibu za kupelekwa kwa tiba Afrika Kusini kutokana na matatizo kibao yanayosonga hospitali ya taifa ya Muhimbili kitengo chake cha mifupa cha Moi na Wizara ya Afya ambapo kibali kilichukua 'karne' kupatikana huku uchunguzi wa awali ukichukua miaka 'dahari' kufanyika kutokana na kukosekana kwa mashine muhimu ya CT Scan.
Pamoja na hayo lukwangule inamuombe nafuu ya haraka na mafanikio mema.

Thursday, October 2, 2008

Idd yenye simanzi kubwa




RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Abed Mwinyimsa kuchunguza na kubaini chanzo cha vifo vya watoto 19 waliokuwa wakishiriki disko toto, tukio lililotokea jana jioni mjini humo.
Pamoja na watoto hao kufa wengine 16 wapo hospitalini Kitete kwa matibabu.
Watoto waliofariki ni Veronica Wanigu(7)Beatrice Makelele(14)Jacob Gerald (12)Salma Hamisi(12)Hadja Waziri(10) Rehema Moto (12)Seleman Idd (11) MrishoSeleman (10)Abdalah Rehan (14’)Agatha Manigu(12) Paulina Emanuel (11) Mohamed Kapaya (15) Ramla Yenga(15)Habiba Shaaban (14).Wengine ni Donald Kasela (12)Mwanahamisi Waziri (11) Ashura Jabal (12) na Yasin Rashid (11).
Waliolazwa hospitali hospitali hadi sasa baada ya wengine kumi kuruhusiwa ni Msimu Rehani (14) Naomi Joseph (13) Tatu Amani (15) Kulwa Idd(12) Sakina Ally (10) na Jumanne Abdallah(11)
Rais kwa kupitia Waziri Athuman Juma Kapuya amesema kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo na kutuma salamu zake za rambirambi kwa mkuu huyo wa Tabora na wafiwa.
Kutokana na agizo hilo serikali mkoani hapa imeunda tume maalumu itakayoshirikisha wadau mbalimbali ili kubaini chanzo cha tatizo hilo na kuhakikisha halijirudii tena.
Kutokana na msiba huo, Rais Kikwete ametoa ubani wa shilingi laki tano kwa kila marehemu ambapo shirika la hifadhi ya jamii(NSSF) ambalo jengo lake ndilo lina kumbi hizo limetoa shilingi tano kwa kila marehemu na shilingi laki moja kama pole kwamajeruhi, na serikali ya mkoa wa Tabora imetoa shilingi elfu hamsini kwa kila marehemu.
Mitaa mingi ya mji huu imebaki kuwa na watu katika makundi makundi wakijadili tukio hilo na wengine wakilia kwa kupoteza watoto au ndugu zao.
Mkuu wa Mkoa ameagiza kufungwa kwa kumbi zote za disko na dansi mpaka atakavyotangaza vinginevyo.
Naye Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba wamiliki wa kumbi mbili za disko Bubbles Night Club, Shashikanti Patel na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Projestus ambaye anamiliki Top Five disco sound wanashikiliwa na polisimjini hapa kufuatia tukio hilo.
Watu hao wanatakiwa kuisaidia polisi katika uchunguzi wake.
Msanifu wa majengo aliyesanifu jengo hilo la NSSF ambako tukio hilo lilitokea John Mlundwa alisema kuwa kumbi hizo zilijaza watoto kinyume na uwezo wake nakuongeza kuwa kumbi hizo zilijengwa kwa matumizi ya mikutano na matumizi ya ofisi na siyo matumizi ya sherhe za watoto kwani watoto wanatakiwa kustarehekatika maeneo ya wazi.
Picha hizi japo hazipendezi kwa namna yoyote ile ni jengo la NSSF Tabora ambalo lilikuwa na kumbi hizo za disko,chumba cha maiti cha hospitali ya kitete ambapo miili ya watoto hao ilikuwa inahifadhiwa na mamia ya wananchi wakiwa katika hospitali.Picha na mdau wa Tabora

Wednesday, October 1, 2008

Karume ataka Wazanzibari wadumishe amani


RAIS Amani Abeid Karume amewataka waislamu kushikilia msingi wa amani uliokuwapo katika kipindi chote cha mfungo wa Ramadhan kwa kujali zaidi utulivu, amani na usalama wa nchi badala ya shari na vurugu.
Akihutubia Baraza la Idd katika sherehe za Idd el Fitr visiwani hapa leo Rais Karume alisema Waislamu wana wajibu mkubwa wa kuendeleza mema yanayozingatia amani na maadili yaliyopatikana katika mfungo mwezi Mtukufu wa Ramadhan .
Aidha Rais alionya dhidi ya tabia ya waumini wachache kutumia sherehe za Idd kama nafasi ya kurudia maovu na kusisitiza kuwa matendo hayo ni kuudhalilisha Uislamu na pia Mtume Muhamad pamoja na taifa lote.
“Tuendeleze kustahamiliana na kuvumiliana, kukuza upendo kati yetu katika jamii moja, kuheshimu tabia na taratibu za sheria za dini na nchi; na zaidi ya yote kuendelea kusaidiana katika shughuli zetu za maisha,” alisema.


Pichani ni Waziri kiongozi mstaafu wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamadi (katikati) akibadilishana mawazo na Wastaafu wenzake DK Moh'd Gharib Bilali (kushoto) na Ramadhani Haji Faki Kwenye Baraza la Idd lililofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar leo.Picha hii ni Martin kabemba.

Rais ajumuika na wengine katika swala ya Idd



Rais Jakaya Kikwete akiwa katika swala ya Idd msikiti uliopo Kinondoni Muslimu. Rais alijiunga na waumini wengine kusherehekea kumalizika wka mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Alipotoka nje ya msikiti alipata nafasi ya kusalimiana na waumini wengine waliopenda pia kupata mkono wa Idd kutoka kwa rais. Picha kwa hisani ya Fredy Maro wa Ikulu

Buffalo yatekwa na majambazi Pori la Kasindaga, kagera

BASI la Buffalo ambalo lilikuwa safarini kutoka Bukoba kagera kuja Dar es salaam leo asubuhi lilitekwa na majambazi kwa dakika kadhaa na katika majibizano ya risasi kati ya askari polisi wanaosindikiza gari hilo na majambazi hao raia mmoja wa Madagascar amepoteza uhai wake.

Utekaji nyara huo umefanyika katika pori la Kasindaga mkoani Kagera

Habari kutoka Bukoba zinasema raia huyo wa Madagascar ni Halvilo Karishina (48) na katika tukio hilo abiria wanne walijeruhiwa kwa risasi sehemu mbalimbali za mwili .

Karishina alikufa papo hapo baada ya majambazi waliokuwa katika pori la Kasindaga mkoani Kagera kurusha risasi hewani na kumpata Karishina na abiria wenzake wanne waliokuwa wamekaa sehemu za madirishani.

Kwa mujibu wa Polisi, basi hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T802 AEV likiendeshwa na dereva Suleiman Mfaume, liliondoka Bukoba jana saa 12:00 asubuhi likiwa na abiria 43.

Walioshuhudia walisema basi hilo lilipofika katika pori la Kasindaga majira ya saa 3:15 asubuhi lilisimamishwa na majambazi wapatao wanane ambao walikuwa na bunduki tatu aina ya SMG na mabomu ya kutupa kwa mkono ambayo idadi yake haikujulikana.
Askari aliyekuwa anasindikiza basi hilo alijibizana nao kwa risasi kabla ya kupata msaada wa doria ambao waliweza kuzima jaribio la kuteka basi hilo.
Majambazi hao walikimbilia porini na askari wameongeza nguvu kuyasaka porini.