Temporary Shelter

CHATROOM

Thursday, November 27, 2008

Sorry bloggers

samahani sana kwa kutokuwa nanyi kuanzia Jumamosi tena bila taarifa. Inaudhi lakini ni ukweli I had to get out from dar es salaam kwenda Up country for a specific reason. My mwajiri alitaka nifanyekazi yake na sikuwa na muda hata wa kusema kwaheri na mbaya zaidi safari yenyewe ilikuwa ngumu kiasi ya kwamba hapakuwapo na mawasiliano hata kama unataka kuwasiliana na bloggers katika kijiji chetu inakuachukua nguvu zote kisha unakata tamaa. Ninachotaka kusema kwamba nipo Bara na almost nipo incomunicado. But nikishaingia kijijini nitawaambieni nilikuwa wapi nafanya nini na nini kimenikera Iam Sorry again. But if God loves it and that is what i Think namuomba To meet again.
Lukwangule

Saturday, November 22, 2008

Kaka magnus akiwa na tabasamu la Nondozzz


Leo kulikuwa na mahafali pia ya CBE kama hufahamu chuo cha biashara.Katika mahafali haya mwandishi wa habari wa HabariLeo Magnus Mahenge naye alikuwapo.Pichani bwana mahenge (wa tatu kutoka kushoto) akitabasamu pamoja na wengine katika mada ambayo nadra sana kusikika, watu wamelamba nondoz bwana, lazima utabasamu.Picha hii ni mali ya Yusuf Badi.

Ajali mbaya yatokea Mbeya na kuua 10

Watu 10 wamekufa papo hapo na wengine nane kujeruhiwa vibaya baada ya lori walilokuwa wakisafira kutoka Kamsamba kueleka Mlowo wilayani Mbozi likiwa limebeba shehena ya Mahindi na Samaki kuacha njia na kupinduka katika eneo la Nambizo wilayani humo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema hadi kufikia jana jioni majina ya watu waliokufa katika ajali hiyo yalikuwa hayajatambulika na kwamba dereva wa gari walilokuwa wanasafiria hajatambulika jina wala umri wake kutokana na kukimbia mara baada ya ajali hiyo.
Alisema abiria hao walikuwa wanasafiri katika gari lenye namba za usajili T 140 AWQ aina ya Mitsubishi, ambapo gari hilo lilikuwa limebeba shehena ya mahindi na samaki likisafiri kutokea Kamsamba kuelekea wilayani Mlowo wilayani Mbozi.
Alisema licha ya kubeba mizigo, pia gari hilo lilikuwa limebeba abiria 18 waliokuwa wamekaa juu ya mizigo hiyo.

Polisi Zambia wadaiwa kuua madereva wa Tanzania

Yapo madai kuwa madereva wawili wa kampuni usafirishaji ya Dhandho wameuawa nchini Zambia katika mahabusu za polisi.
Kauli hiyo imetolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kityuo cha Mbeya ambao waliamua kugoma kutaka kujua kulikoni.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao walidakwa na polisi kwa tuhuma za kuuza madini ya shaba waliyokuwa wakisafirisha namwingine mafuta na tairi.
Madereva wanaodaiwa kuuawa na polisi wa nchini Zambia ni Miki Mwalunu (33),
Mkazi wa eneo la Simike Jijini Mbeya aliyekuwa anaendesha gari lenye namba za
usajili T. 892 ARD aina ya Scania lenye tela no. T.465 806 ARF na mwenzake
Zacharia Sikafunje dereva wa gari no. T.643 AJT aina ya Scania likiwa na tela no.
T.665 AJT.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stpehen alipotafutwa kwa ajili
kuzungumzia tukio hilo hakupatikana, Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John
Mwakipesile alisema hana taarifa za kuuawa kwa Watanzania hao na kwamba
Jumatatu atawasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia ili kupata
taarifa kamili.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Baadhi ya madereva wa Kampuni
hiyo, walisema kuwa hawapo tayari kuendelea na kazi hadi Mkurugenzi wa
kampuni hiyo tawi la Mbeya, Karimu Dhandho awape maelezo ya kina kuhusiana
na vifo vya madereva wenzao.
"Tumeazimia kugoma hadi uongozi utakapotueleza kilichotokea na namna
miili ya wenzetu itakavyorudishwa nchini” walisema.
Naye Meneja wa Meneja Utawala wa Kampuni ya Dhandho, Kapteni mstaafu
Joseph Mwasege, akizungumza na waandishi wa habari, alikiri kupata taarifa za
kifo cha dereva mmoja, Mwalumu tu.
Alisema uongozi wa kampuni hiyo umemtuma mwakilishi wao, Soud Kalamazi ili
kwenda kupata ukweli kamili juu ya vifo vya madereva hao, ambapo alisema kuwa
walipata taarifa za kukamatwa kwa dereva Mwalunu .

Hotuba ya rais kuadhimisha miaka 10 ya Sauti,rais akerwa na ubabe wa wanafunzi


HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGOSTINO TANZANIA (SAUT) MWANZA,
TAREHE 22 NOVEMBA, 2008


Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu
wa JimboKuu la Dar es Salaam;
Mhashamu Askofu Jude Ruwaichi, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania;
Mhashamu Askofu Mkuu Joseph Chennoth, Mwakilishi wa Vatican;
Mhashamu Askofu Anthony Mayala, Askofu Mkuu wa Mwanza;
Wahashamu Maaskofu wote mlioko hapa;
Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa;
Waheshimiwa Wabunge;
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Bwana Sandy Weill wa TOUCH FOUNDATION;
Dkt. Antonio Gotto, Mwakilishi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Weill Cornell cha New York, Marekani;
Bwana Angus O’Shea, Mkurugenzi Mtendaji wa TOUCH FOUNDATION;
Profesa Joseph Shija;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana:
Naomba nianze kwa kukushukuru wewe Muhashamu Kardinali, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino Tanzania kwa heshima hii kubwa mliyonipa ya kujumuika nanyi katika siku hii muhimu na ya kihistroria. Kama tulivyoelezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, leo tunaua ndege wawili kwa jiwe moja. Mbali na mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino na mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Weill Bugando, leo pia tunaadhimisha miaka 50 ya uhai wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).
Kwa hakika leo ni siku ya aina yake. Mimi na mke wangu, Salma tumefarijika sana kuwa miongoni mwa watu waliopata bahati ya kuishuhudia siku hii. Sote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uhai na afya njema na kutuwezesha kuwepo na kushiriki katika sherehe hii adhimu.
Shukrani kwa Waliosaidia
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu, Wageni Waalikwa;
Napenda pia kuitumia nafasi hii kuungana na wasemaji walionitangulia kuwakaribisha wageni wetu waliotoka nje ya Tanzania. Tunawakaribisha kwa mikono miwili nchini mwetu na hasa hapa jijini Mwanza. Kuwepo kwao miongoni mwetu siku ya leo ni jambo la faraja kubwa. Tunatambua wanayo majukumu mengi lakini uamuzi wao wa kuwa nasi hapa Bugando ni kielelezo tosha cha mapenzi yao kwetu Watanzania.
Namshukuru kwa namna ya kipekee Bw. Sandy Weill kwa msaada mkubwa alioutoa na anaoendelea kuutoa katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando. Chuo hiki kipo katika hali hii hivi sasa kutokana na mchango wake mkubwa. Na, kwa msaada wake na ushirikiano wake, nina imani kuwa Chuo chetu kitakuwa bora zaidi siku za usoni. Naomba kwa niaba yenu nyote nimshukuru sana kwa msaada wake na moyo wake wa huruma na upendo kwa nchi yetu na watu wake.
Namshukuru pia Dkt. Antonio Gotto, Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha New York, Marekani. Chuo hicho kimekuwa na ushirikiano wa karibu na Chuo Kikuu cha Bugando na kupitia ushirikiano huo, Chuo chetu kimeweza kupata misaada ya fedha, wakufunzi na vifaa mbalimbali vya mafunzo. Ni ushirikiano huo ndiyo uliwezesha kumvuta Bw. Sandy Weill kutusaidia kama anavyofanya sasa.
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama sitamtaja Bw. Angus O’Shea, Mkurugenzi Mtendaji wa Touch Foundation ya Marekani ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia masuala ya uendeshaji na kutafuta wafadhali wa ujenzi wa Chuo hiki.
Let me take this opportunity to extend a warm welcome to all our guests from abroad. We welcome you to Tanzania and to Mwanza in particular. We feel greatly honoured to have you here with us today. I hope that all of you will have an enjoyable and memorable stay in our country. To Mr. Sandy Weill, I express my sincere thanks to you, I can’t find suitable word to express our immense appreciation for the generous support you extended to Weill Bugando University. The University is what it is today because of your support. On the same vein I thank Dr. Antonio Gotto, the Dean of the Weill Cornell Medical College of the University of Cornell from New York for coming and the cooperation and support of Weill Cornell Medical college to Bugando. To Mr. Oshea and to Touch Foundation we thank you for the invaluable contribution you have made towards the management and raising requisite resources. We are deeply touched

Pongezi
Muadhama Kardinali na Wahashamu Maaskofu;
Nakupongeza sana wewe binafsi na Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki nchini kwa kutimiza miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Ilikuwa ni miaka 50 ya mafanikio mengi ya kujivunia na kutolewa mfano. Sisi sote ni mashuhuda wa mafanikio yaliyopatikana kwani yanajieleza yenyewe na yanaonekana katika nyanja mbalimbali za maisha ya Watanzania. Mafanikio haya ni matokeo ya uongozi wenu mahiri na uliotukuka, kufanya kazi kwa bidii na maarifa, moyo wa uvumilivu na upendo kwa waumini wenu na wananchi wote wa nchi yetu. Mambo ni mengi na orodha ni ndefu sana nachelea kuyataja yote kwani tutakesha na hatutayamaliza.
Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi, natoa pongezi na shukrani nyingi kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kwa Kanisa Katoliki kwa jumla kwa mchango wake mkubwa na adhimu iliyoutoa na inayoendelea kutoa kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Tanawatakia mafanikio maradufu katika miaka hamsini ijayo.
Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali inatambua na kuthamini sana mchango wenu. Naahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika juhudi zenu za kuwahudumia na kuwatumikia Watanzania katika harakati zao za kujiletea maendeleo na maisha yaliyo bora zaidi.
Mheshimiwa Kardinali na Wahashamu Maaskofu;
Nawapongeza na kuwashukuru sana kwa uamuzi wenu wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino na Vyuo Vikuu Vishiriki vitatu kikiwemo hiki cha cha Tiba hapa Bugando. Mahafali haya ya leo ni kielelezo dhahiri cha usahihi wa uamuzi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Aidha, ni ushahidi wa ninyi kuwa watu makini mnaotekeleza kwa vitendo maamuzi yenu. Uamuzi wenu huo umesaidia sana katika kuimarisha jitihada zetu kitaifa za kupata wataalamu zaidi wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Leo tunashuhudia mahafali ya kumi ya SAUT na mahafali ya kwanza ya Vyuo Vikuu Vishiriki yakilipatia taifa wataalamu wapatao 900 wa fani mbalimbali. Nimepungukiwa maneno bora zaidi ya kuelezea furaha yangu na shukrani zangu kwenu. Naomba mridhike nikisema Asanteni sana, tena sana.
Pia napenda kuitumia nafasi hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa Chuo cha Mtakatifu Agostino na ule wa Vyuo Vikuu Vishiriki vyote vitatu pamoja na wahadhiri na wafanyakazi wote kwa kazi nzuri waifanyayo na mafanikio yanayoendelea kupatikana. Ni ukweli ulio wazi kuwa bila ya juhudi zao, mafanikio yote haya yasingepatikana na wala tusingekuwa na mahafali haya hapa leo. Kwenu nyote nasema asanteni sana kwa kazi nzuri. Nawaomba muendelee na moyo huo. Nawahakikishieni ushirikiano na msaada wangu na wa wenzangu Serikalini kwenu. Mimi na wenzangu tunatambua fika kwamba mafanikio yenu ndiyo mafanikio yetu. Hivyo, tunao wajibu wa kusaidiana.


Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu na Wageni Waalikwa;
Mwisho katika pongezi, ingawaje siyo mwisho kwa umuhimu, napenda kuwapongeza wahitimu wote ambao wanatunukiwa vyeti na shahada zao siku ya leo. Huu ni mwanzo wa safari yenu ndefu ya kujenga maisha yenu na ya familia zenu, wakati huo huo mkiwahudumia Watanzania wenzenu na wanadamu kwa jumla. Kama alivyosema Mkuu wa Chuo sote tunawatarajia kufanya kazi kwa bidii na maarifa mkitumia elimu yenu huku mkizingatia maadili na miiko ya kazi na taaluma zenu. Kwa maneno mengine tunawategemea mtoe utumishi uliotukuka kwa Watanzania na wanaadamu wenzenu wote wakati mtakaopata fursa ya kuwahudumia. Naungana nae na wote tuliokuja kushuhudia mahafali yenu, kuwatakia kila la heri. Inshalla, Mwenyezi Mungu atawaongoza ila msimsahau kumuomba na kumtanguliza kwa kila hatua muipigayo.
Naomba mtambue sasa kuwa mambo ya uanafunzi sasa yameshafika mwisho na yale ya mwalimu dunia ndiyo yanaanza. Tena ni vyema mkajua kuwa mambo ya mwalimu dunia wakati mwingine huwa magumu. Lakini ni mambo yanayowezekana. Wapo wenzenu wengi wengine wameweza, kwa nini wewe usiweze? Kinachohitajika ni wepesi wa utambuzi wa mambo, ubunifu, moyo wa kujituma, uvumilivu nidhamu uwapo kazini na nje ya kazi.
Natambua kuwa baadhi yenu mtaajiriwa Serikalini na kwingineko. Kwa hakika walimu na madaktari tutawaajiri wote labda mtu akatae mwenyewe kuwa mtumishi wa Serikali. Najua wengine wataajiriwa na wadau wengine ikiwemo sekta binafsi. Lakini wapo wengine ambao hawataajiriwa na Serikali au kupata ajira kwingineko, naomba msikate tamaa. Tafuteni fursa ya kujiajiri wenyewe. Mimi niko tayari kuwasaidia kadri iwezekanavyo pale mtakapohitaji msaada wangu wa uwezeshaji kwa mipango yenu.
Elimu ya Juu
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu na
Wageni Waalikwa;
Naomba nirudie tena kutoa shukrani zangu kwa Kanisa Katoliki kwa mchango mkubwa inaoendelea kuutoa katika kuendeleza elimu nchini. Natambua kwamba kasi yenu ya uwekezaji katika elimu ilipungua baada ya uhuru, pale Serikali ilipotaifisha shule mlizokuwa mnamiliki na kuendesha nchini. Sera ile na hatua zile zilikuwa ni za muhimu kuchukua kwa wakati ule. Zimesaidia katika kujenga msingi wa utangamano, umoja na utaifa tulionao sasa katika nchi yetu.
Wahenga wanasema kila zama na mambo yake. Baadae katika nusu ya mwisho ya miaka ya 1980 na miaka ya 1990 kumekuwepo na mageuzi makubwa ya sera za kiuchumi na kisiasa nchini. Sera ile kuhusu shule zinazomilikuwa na madhehebu ya dini ikaguswa nayo. Kwa sababu hiyo, baadhi ya shule zilizokuwa zinamilikiwa na madhehebu ya dini zilirejeshwa. Nasema baadhi ya shule kwa sababu ulegezaji uliofanywa katika sera haukulenga kurejesha shule zote. Ilionekana haingekuwa jambo la busara kwa serikali kufanya hivyo.
Lakini, jambo kubwa na la msingi lililoletwa na mageuzi hayo ni kule kuruhusu madhehebu ya dini na mashirika ya kidini na watu binafsi kuanzisha vyuo vya elimu ya juu nchini. Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino ambacho leo tunasherehekea mahafali yake ya 10, ndiyo matunda ya sera hiyo mpya ya Serikali.
Hakika sera hiyo imekuwa na manufaa kwa nchi yetu na watu wake. Hivi sasa, pamoja na SAUT, tunavyo vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki binafsi 20 vyenye wanafunzi 18,286. Idadi hii tunapoichanganya na ile ya vyuo vikuu vya umma 11 vyenye wanafunzi 64,666, ndiyo inayotufikisha kwa uwiano wa asilimia 2 wa vijana wa umri wa kupata elimu ya chuo kikuu kuwa vyuoni. Kiasi hicho bado ni chini ukilinganisha na majirani zetu wa Kenya na Uganda au hata na wenzetu wengi wa nchi za Kusini mwa Afrika katika SADC.
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu na
Wageni Waalikwa;
Hatuna budi sisi katika Serikali, mashirika ya dini na wadau wengine wa elimu tuendelee kushirikiana katika kukuza na kuendeleza elimu ya juu nchini. Mahitaji bado ni makubwa kwani vijana wengi wenye sifa ya kujiunga na vyuo vikuu bado wanakosa fursa hiyo. Kwa mfano, kwa mafunzo ya udaktari mwaka wa jana asilimia 76 ya vijana wenye sifa hawakuchukuliwa katika vyuo vyetu vikuu. Wakati huo huo nchi ina upungufu mkubwa wa madakatari. Hapa nchini daktari mmoja anahudumia watu 28,000. Hali ni hivyo hivyo kwa fani nyingine muhimu. Mimi naamini tukiendelea kushirikiana kama tufanyavyo tutalikabili ipasavyo tatizo hili.
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu;
Nawaahidi mambo mawili kutoka Serikalini. Kwanza kwamba sera ya kuruhusu wadau wengine zaidi ya Serikali kujenga, kumiliki na kuendesha vyuo vya elimu ya juu nchini, na vyuo vikuu, yaani pamoja tutaidumisha na kuiendeleza. Katu hatutageuka nyuma na kuwakatalia wengine washiriki au kutaifisha vyuo vyao na taasisi zao.
Na, pili tutaendelea kushirikiana na kusaidiana katika uendeshaji wa vyuo vyetu hivi kadri inavyowezekana. Kwa ajili hiyo, Serikali itaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya serikali na visivyokuwa vya Serikali kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa au zitakazowekwa na Serikali.
Mikopo ya Wanafunzi
Natambua kuwa suala la mikopo ya wanafunzi limekuwa chanzo cha misuguano kati ya wanafunzi na serikali. Misuguano hiyo imekuwa inachukua sura mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Kuna wakati misuguano ilihusu utaratibu wa utoaji na ulipaji wa mikopo kwenye Bodi ya Mikopo. Kuna wakati kulikuwa na misuguano kuhusu uchangiaji kwa uwiano wa asilimia 60 kwa 40. Baada ya kulalamikiwa kuwa utaratibu huo haukujali na kutofautisha watoto wa mwenye uwezo na wasiokuwa na uwezo, Serikali ikautazama upya. Ukaanzishwa utaratibu mpya wa kutoa mikopo kulingana na uwezo wa mwanafunzi au wazazi au walezi wake kuchangia ukaanzishwa. Yaani “means testing” ambao unatumika katika nchi kadhaa katika ukanda wetu. Kwa ajili hiyo, wapo wanafunzi wanaopata mkopo kwa asilimia 100 kwa kukosa uwezo na wapo wanaojigharamia wenyewe kwa asilimia 100 kwa sababu wanao uwezo. Pia wapo wanaopata mikopo pungufu kwa viwango mbalimbali kutegemea na uwezo wao.
Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa kati ya jumla ya wanafunzi 41,396 walioingizwa kwenye utaratibu wa mikopo, wanafunzi 5,835 au asilimia 14 wanapata mkopo asilimia 100, wanafunzi 23,936 au asilimia 57.8 wanapata mkopo asilimia 80, wanafunzi 10,278 au asilimia 24.8 wapata mkopo wa asilimia 60, wanafunzi 1,288 au asilimia 3.1 wanapata mkopo asilimia 40, na ni wanafunzi 59 tu wanapata mkopo asilimia 20.
Tulipofanya marekebisho hayo, tulidhani tumetoa jibu. Bahati mbaya haikuwa hivyo. Tena, sasa kukaja madai mapya kwamba utaratibu huu wa kutoa mikopo kwa mujibu wa uwezo wa kila mtu kulipia usiwepo kabisa, bali kila mmoja apewe mkopo kwa asilimia 100. Jazba zikapanda au kupandishwa na kwingineko migomo ikachochewa na hata ghasia, hivyo kusababisha baadhi ya vyuo kufungwa.
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu;
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu;
Sera ya wananchi kuchangia sehemu ya gharama kwa huduma za maji, elimu na afya zitolewazo na Serikali iliyoanza kwenye miaka ya 1990, ilibuniwa kwa sababu za msingi kabisa na kwa nia njema. Ni sera ambayo ilibuniwa na kutekelezwa kwa sababu ya manufaa yake. Haikubuniwa kwa roho mbaya au kwa nia ya kutesa au kukomoa wananchi. Hivyo sivyo hata kidogo na, hiyo kamwe haiwezi kuwa dhamira ya Serikali.
Hali kadhalika, katika uchangiaji kwa huduma zote, suala la uwezo wa mtu kulipia lilizingatiwa. Wakati wote wale wasiokuwa na uwezo walihurumiwa na wale wenye uwezo waliachwa kulipia kwa uwezo wao. Ni ukweli usiopingika kuwa wapo miongoni mwetu wenye uwezo wa kulipa.
Kama tujuavyo au tukumbukavyo, kabla ya mabadiliko hayo ya kisera huduma hizo zilikuwa zinatolewa bila ya wananchi kuchangia. Lakini, kwa sababu ya mahitaji ya huduma hizo na shughuli nyingine za Serikali kuendelea kukua kwa sababu ya idadi ya watu kuongezeka na nyakati kubadilika, uwezo wa Serikali wa kubeba mzigo wa kugharamia huduma hizo kwa kiasi na ubora ule ule ukazidi kupungua.
Mwaka hadi mwaka hali ya upatikanaji wa huduma hizo ukaanza kushuka na kuwa wa kiwango cha chini kwa maana ya kutokidhi mahitaji ya watu na ubora wake kuwa chini. Kwa kutambua ukweli huo, na kwa nia ya kutaka kuona wananchi walio wengi wanapata huduma hizo na zinapatikana kwa ubora wa kuridhisha, ndipo sera ya uchangiaji na ushirikishaji wa wadau wengine ikabuniwa na kuanza kutekelezwa.
Serikali ilikuwa mkweli kwa wananchi inaowaongoza kuhusu hali halisi ilivyokuwa na uwezo wake wa kuwahudumia. Nia ilikuwa njema, lakini uwezo ulikuwa mdogo na ulizidi kupungua kadri watu walivyoongezeka.
Ni ukweli ulio wazi kuwa sera hiyo mpya ya uchangiaji imekuwa na manufaa kwa taifa letu na watu wake. Watu wengi zaidi wakawa wanapata huduma za maji, elimu na afya kuliko ilivyokuwa zamani. Aidha, hata ubora wa huduma hizo sasa ni wa juu zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Hata hivyo, bado wako watu wengi nchini ambao hawapati huduma hizo na ubora bado si wa kiwango cha juu vya kutosha ingawaje umepanda kiasi. Maana yake ni kwamba bado tunayo kazi kubwa ya kufanya mbele yetu ili watu wengi zaidi wapate huduma za maji, elimu na afya na kukuza zaidi ubora wa huduma hizo.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Kwa hali yetu ya sasa ya uchumi, wingi wa watu na uwezo wa kifedha wa Serikali, hatuwezi kurudi kule tulikokuwa wa huduma hizo kutolewa asilimia 100 kwa gharama za Serikali. Tukifanya hivyo matokeo yake yatakuwa ni yale yale yaliyowafanya viongozi wetu walionitangulia wa Awamu ya Pili na Tatu wafanye mageuzi tunayoendelea kuyatekeleza sasa. Tutawahudumia watu wachache zaidi na hata ubora wa huduma utaathirika.
Muadhama Kardinali na Wahashamu Maaskofu;
Kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu, tukirudia mfumo wa zamani, tutachukua wanafunzi kidogo zaidi wa kujiunga na vyuo hivyo. Hatari nyingine ninayoiona hapa, pia ni ule uwezekano wa Serikali kuanza kuwa mbinafsi kwa kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa vyuo vyake tu tofauti na ilivyo sasa inagharamia hata wanafunzi wa vyuo binafsi kama SAUT na vinginevyo. Isitoshe, hata kama Serikali ingeamua kugharamia wanafunzi watakaosoma katika vyuo vyake pekee, naamini bado hatutamudu kuwahudumia wanafunzi wote ipasavyo. Hata huko itabidi wahudumiwe baadhi tu. Kwa sababu hizo na nyinginezo, naamini mfumo wa sasa wa kila mwenye uwezo kuchangia kwa uwezo wake unawawezesha vijana wetu wengi zaidi kupata fursa ya kusoma katika Vyuo Vikuu. Kinyume chake wachache watapata fursa hiyo. Wenye uwezo wanapochangia nguvu na Serikali inawawezesha wasiokuwa na uwezo kusaidiwa.
Napenda kuwahakikishia vijana na Watanzania wenzangu wote kuwa ningependa sana kila Mtanzania apate elimu bure, maji bure, na matibabu bure. Lakini, natambua kuwa uwezo wa Serikali yetu kufanya hivyo kwa sasa ni mdogo. Ni kutokana na ukweli huo ndiyo maana ikaamuliwa tufanye kinachowezekana. Kufanya hivyo ni kwa manufaa yetu sote. Ni kwa maslahi ya taifa letu. Kufanya vinginevyo ni hasara kwetu sote.
Kuhusu manung’uniko yahusuyo taratibu za utoaji wa mikopo katika Bodi ya Mikopo napenda kusema kuwa tumeyasikia na tunayafanyia kazi. Tunafikiria mambo kadhaa ya kufanya. Miongoni mwake tunafikiria kuangalia uwezekano wa kuvifanya vyuo kuwa wakala wa Bodi ya Mikopo. Maana yangu ni kwamba tunatazama kama shughuli ya utoaji wa mikopo ya mwanafunzi iwe pale chuoni anaposoma. Yapo pia mawazo mengine ambayo yanaendelea kutazamwa kwa nia ya kurahisisha utaratibu wa upatikanaji wa mikopo na kuondoa usumbufu uliopo sasa.



Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofiu;
Ndugu Wananchi,
Napenda kuitumia fursa hii, tena kwa moyo mzito sana, kuelezea masikitiko yangu kuhusu tabia wanayoinyesha baadhi ya wanafunzi wa baadhi ya vyuo vikuu. Kwanza ni matumizi ya migomo. Ndugu zangu mimi sina tatizo na wanafunzi kudai haki zao pale inapostahili. Mimi mwenyewe niliwahi kuwa kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi pale Mlimani na nilifanya kazi hiyo. Tatizo langu ni pale wanafunzi wanapoonyesha ubabe, wanapofanya fujo, wanapoharibu mali na wanapopiga wenzao wasiotaka kushiriki migomo. Hii siyo sawa. Unaweza kudai haki bila kugoma na pale inapokuwa hapana budi kugoma, kufanya vurugu siyo lazima. Kingine kinachonisikitisha pia ni lugha inayotumika na kuelekezwa kwa walimu wao, viongozi wao wa Chuo, viongozi wa serikali na hata watu wengine wa umri kuzidi wa kwao.
Ukiisikiliza ile lugha wanayotumia baadhi ya wanafunzi, unajiuliza maswali mengi kuhusu jamii yetu: tulipo na mbele tuendako kuhusu malezi na maadili ya mtoto wa Kitanzania tunayoyajua sisi sote. Narudia kusema kuwa mimi naamini kabisa kwamba wanafunzi wanaweza kudai kile wanachoona wanakistahili bila kufanya fujo, bila matusi, bila ubabe, bila kudharau, kutukana na kukejeli walimu na viongozi wao, na bila kupiga wenzao walioamua kufanya kile kilichowapeleka Chuoni kwa kutoshiriki kwenye migomo na kuingia madarasani. Hili la malezi, nawasihi wazazi wenzangu tuendelee kulipa uzito unaostahili kwani ndiyo taswira yetu na jamii yetu itakayoonekana mbele yetu na wenzetu.
Lakini kwa upande wa Serikali, tutaendelea kuchukua hatua madhubuti kabisa kuhakikisha kwamba sheria za nchi zinafuatwa na zinaheshimiwa. Na pale fujo au uchochezi wa kuvunja amani utakapotokea basi sheria itafuata mkondo wake. Si busara kuwafumbia macho wachache wanaochochea migomo na kusababisha vurugu.
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu;
Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Bugando;
Kwa upande wa Hospitali ya Bugando napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo na Kanisa Katoliki kama ulivyoainishwa kwenye makubaliano yetu ya mwaka 1971. Katika makubaliano hayo Serikali iliomba Hospitali ya Bugando kutoa huduma za afya za rufaa kwa Kanda ya Ziwa. Tulikubaliana kuwa ili kufanikisha hayo Serikali inalo jukumu la kutoa fedha zinazohitajika kuendesha hospitali. Fedha hizo ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi, dawa, vifaa-tiba na matumizi mengine ya maendeleo ya hospitali.
Nafurahi kusema kuwa Serikali imekuwa inatimiza wajibu wake huo. Katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2004/2005, Serikali imetoa shilingi 17,772,915,763 kwa ajili ya uendeshaji wa hospitali ya Bugando. Napenda kuwahakikishia kuwa tutaendelea kutimiza wajibu wetu huo ili kuiwezesha hospitali yetu hii kutoa huduma bora zaidi za matibabu kwa wakazi wa Ukanda huu wa Ziwa.
Hitimisho
Muadhama Kardinali, Wahashamu Maaskofu na Wageni Waalikwa;
Naomba nimalize hotuba yangu kama nilivyoanza. Nawashukuru tena kwa kunialika na kuniwezesha kushiriki katika tukio hili la kihistoria. Nawashukuru pia kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kufundisha wataalamu katika nchi yetu. Leo hapa tumeshuhudia wahitimu wa fani mbalimbali zikiwemo za Udaktari, Ualimu, Uhasibu, Uanasheria, Uchumi na Mawasiliano ya Umma. Kada zote hizi ni chachu muhimu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.
Aidha, tunawashukuru tena wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakichangia katika jitihada zetu za kuimarisha na kupanua elimu ya juu. Mchango wao bado unahitajika kwani safari yetu bado ni ndefu. Hivyo tunawaomba wasichoke bali waendelee kutusaidia.
Kwa upande wa Vyuo vyetu Vikuu, napenda kurudia wito wangu kwenu kuhusu umuhimu wa kutoa wahitimu waliobobea katika fani walizosomea. Vyuo vyetu viwe ni tanuru la kuoka na kuivisha wataalamu watakaokuwa na uwezo wa kuwahudumia vizuri wananchi na kuleta mabadiliko katika jamii yetu. Aidha, wataalamu tunaowafundisha pia wawe na uwezo wa kukubalika nchini na popote duniani.
Na mwisho kabisa napenda kuwahakikishia tena nia ya Serikali ya kuendelea kufanya kazi pamoja na Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya dini pamoja na wadau wengine katika kuimarisha na kupanua elimu ya juu na elimu kwa jumla hapa nchini. Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake wa msingi wa kuweka mazingira mazuri yatakayowawezesha watu binafsi na madhehebu ya dini kushiriki kwa ukamilifu katika kuendeleza elimu ya Chuo Kikuu hapa nchini.
Hivyo msichoke kutukumbusha wajibu wetu kama ambavyo na sisi hatutachoka kuomba ushirikiano na msaada wenu pale inapostahili. Ni ukweli kwamba sote tuna lengo moja la kuwahudumia Watanzania ili wawe na maisha yaliyo bora zaidi. Nina hakika kuwa tukiendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kama ambavyo tunafanya hivi sasa tutatimiza malengo yetu.
Mungu ibariki Tanzania.
Nawatakia maadhimisho mema.
Nawashukuruni sana kwa kunisilikiza.
Pichani: Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Sista Alicia Masenga aliyehitimu Shahada ya udaktari wa Magonjwa ya binadamu Wakati wa Mahafali iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino mkoani Mwanza leo . Wapili kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Thadeus Ruwaichi na watatu kushoto ni makamu Mkuu wa Chuo Padre Joseph Kitima. Picha hii ni mali ya Freddy Maro.

Friday, November 21, 2008

SAUTI waadhimisha miaka 10 na maneno yenye maana

BARAZA la Maaskofu Tanzania(TEC) limewaomba wasomi wa vyuo vikuu nchini kuhakikisha kuwa wanaitumikia nchi yao kwa uzalendo na ukweli.
Rai hiyo ilitolewa leo Jijini hapa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Askofu Norbet Mtega wakati wa Ibada maalum ya kuwaombea wanachuo wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Weill Bugando kwenye sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Bugando(Bugando day) na miaka
kumi ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (Saut) yaliyofanyika kwenye hospitalini hapo.
"Ni matarajio yetu,Sisi baraza la Maaskofu Tanzania kuwaona wasomi wetu na madaktari wetu mnakuwa na moyo wa huruma katika kuwahudumia wagonjwa mkitanguliza uzalendo wa nchi yenu,"alisema Askofu Mtega.
Akizungumzia ufisadi aliwatahadharisha wasomi wote nchini kumrudia Mungu kwa maelezo
kuwa hiyo ndiyo silaha pekee ya kujikinga dhidi ya ufisadi.
Naye Jacob Kambili, anandika kutoka mwanza kuwa Utawala wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha mjini Mwanza umesema kamwe taasisi hiyo ya elimu ya juu haiungi mkono migomo ya wanachuo wa vyuo vya serikali inayoendelea nchini kote, wakipinga sera ya sasa ya uchangiaji elimu.
Makamu Mkuu wa SAUT, Padre Dk. Charles Kitima alisisitiza msimamo huo hapa Alhamisi wiki hii wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kiasisiwe, ambayo mgeni wake rasmi alikuwa Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.
"Kweli wanachuo wengi, hususani wale wanaotoka kwenye familia maskini, wanahitaji sana fedha ili waweze kukidhi mahitaji yao ya msingi ya elimu. Lakini bado sisi tunaamini kwamba tatizo hilo nyeti linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa amani kwa njia ya mazungumzo ya kujenga pekee". alisitiza Dk Kitima.
Makamu Mkuu wa SAUT alitumia fursa hiyo ya sherehe za maadhimisho ili kuwasilisha taarifa fupi ya maendeleo ya Chuo hicho, kilchoanzishwa mwaka 1998 kutoka iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Taasisi ya Mafunzo ya Jamii Nyegezi (NSTI).
Akizungumzia mipango mkakati ya chuo chake hicho, Dk Kitima alisema baadhi ya malengo waliojiwekea yamefikiwa ikiwa ni pamoja na ongezeko la wanachuo kutoka 294 katika mwaka wa masomo wa 1998/1999 hadi kufikia wanachuo8,790 hivi sasa.
Kati ya wanachuo hao, kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo, wanachuo 6,206 wanasomea sehemu ya Malimbe (main campus), 781 ni wanachuo wa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Bugando (BUCHS), 1,202 walioko katika Chuo Kikuu kishiriki cha Ruaha, mkoani Iringa ili hali wanachuo 600 wanasoma katika chuo kikuu kishiriki cha Mwenge, mjini Moshi.
Kuhusu mipango ya baadaye, alisema SAUT ambayo sasa inajivunia kwa kuwa na jumla ya wahadhiri 140, inakadiria kuwapoea wanachuo 15,000 katika kipindi cha miaka sita kijacho, ikizingatiwa kwamba tayari Chuo kimewapeleka nje wahadhiri 50 kwa ajili ya masomo ya ngazi ya PhD.
"Endapo mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, tunadhamiria kuanzisha vyuo vikuu vinne zaidi vishiriki katika mikoa ya Dar es Salaam, Tabora, Mtwara na Ruvuma" alidokeza.
Mapema, akiuhubiria umati huo ambao ulikusanyika hapo kama waumini wa kanisa Katoliki waliojukuika ili kutoa shukrani zao kwa Mungu kwa kuijalia SAUT kutimiza miaka kumi ya uhai wake, Mwadhama Kadinali Pengo alikemea vikali kila dalili za mmomonyoko wa maadili zilizoanza kujidhihirisha katika jamii.

Thursday, November 20, 2008

Jaji Warioba na hasira zake kwa walafi


Leo jaji warioba kakumbushia maadili na azimio la Arusha akasema jamanai eee viongozi wamezidi tama za mali ... kwa maneno mengine viongozi wengi ni walafi wa mali.Pichani Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza jambo na Viongozi wa vyama vya siasa, Emmanuel Makaidi wa NLD (kushoto) na Prof Ibrahim Lipumba wa CUF baada ya kufungua semina ya maadili ya viongozi Dar es Salaam leo. Picha hii ni ya Mroki Mroki

Walimu wavamia maofisi ya Madc na Maded wauliza kulikoni?




OFISI za madc na Maded wa Temeke na Kinondoni leo zilipata matatizo kidogo wakati walimu walipovamia kutaka kujua kulikoni baada ya majina yao kutokuonekana katika karatasi za malipo kwenye mbao.
Pichani ni walimu wakiangalia majina yao.
Imeelezwa kuwa wilaya ya Kinondoni zaidi ya walimu 200 walijiandikisha kuuliza kulikoni kwingine wakafanya maandamano.

Oni
Something is wrong somewhere kwanini taarifa sahihi zisitolewe kuhusu nini kinafanyika mbona watu wanafanya vitu vionekane kama matusi? Na nilipowatafuta jamaa kujazia stori kila mtu akawa anaruka kimanga. Kuna shida kwelikweli na ofisi hizi za umma, utafiti vile wanalinda magunia ya bangi.

Lukwangule

Meli ya kivita ya Uholanzi yatia nanga Dar




MELI ya kivita ya Uholanzi MV De Ruyter imetia nanga katika bandari ya dar es salaam ikijiandaa kwenda Mombasa kusindikiza meli ya Shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa(WFP) kuingia katika maji hatari ya Somalia.
Meli hiyo ya WFP inapeleka msaada wa chakula kwa wananchi wa Somali ambao wamekumbwa na madhila ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Meli hiyo ya Uholanzi ipo chini ya Kamanda Peter Reesink.
Waandishi wa habari wa Kitanzania walipata nafasi ya kutembelea meli hiyo ambayo itakuwapo dar kwa siku kadhaa kabla ya kuendelea na safari yake.
Maji ya Somalia yamekuwa hatari kutokana na uharamia unaoendeshwa katika maji hayo na watu ambao wana asuili ya Somali wakiwa na vifaa vya kisasa kabisa vya kufanyia ghasia hizo katika maji.
Pwani ya somali ambayo mwendo mfupi kuna njia kuu ya meli duniani kwa sasa inaonekana haiwezi kuwa salama mpaka vikosi vya wanamaji kutoka nchi mbalimbali vidhibiti uharamia huo.
kwa sasa katika pwani hiyo kuna meli ya mafuta ya Saudia ambayo wataiachia kama saudia italipa dola za Marekani milioni 25.
Pichani ni meli yenyewe ikiwa imetia nanga na nyingine waandishi wa habari wakipewa maelezo katika meli hiyo.

maziko ya Mzee Ngozoma yalivyokuwa huko kasoro bahari

MAMIA ya wananchi wa Tarafa ya Mkuyuni, na Matombo wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Rashid Ngozoma Matunda yaliyofanyika juzi ( Nov 19) kijijini kwao Lungala Tarafa ya Mkuyuni Wilayani Morogoro.
Mazishi ya kiuongozi huyo mwandamizi wa Yanga yaliyofanyika kijijini hapoNovemba 19, mwaka huu majira ya saa 12 :30 jioni na yalihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Morogoro (MRFA) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Athuman Kambi.
Kwa upande wa msafara wa Yanga uliongozwa Mwenyekiti wake , Iman Madega, Katibu Mkuu Lucas Kisasa na viongozi wengine waandamizi wa timu hiyo.
Akizungumza na Habari leo mjini hapa jana ( Nov 20) baada ya mazishi ya kiongozi huyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Morogoro, ( MRFA) Aristos Niktas, alisema mamia ya wananchi kutoka vijiji vya Tarafa Mkuyuni na baadhi ya Matombo walishiriki kikamilifu katika mazishi ya marehemu Matunda.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa MRFA, uongozi wa Chama hicho na wapenzi wa soka wa Mkoa wa Morogoro kuwa wamempoteza kiongozi aliyekuwa mtetezi wa haki katika kuendeleza michezo nchini.
Alisema kwa kutambua mchango wa kiongozi huyo, MRFA imetoa ubani wa kiasi cha sh: 50,000 ikiwa ni ishara ya kuungana na familia ya marehemu na viongozi wa timu ya Yanga wakati wa kipindi cha majozi ya kumpoteza kiongozi shupavu wa michezo hapa nchini.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa MRFA alisema familia ya marehemu imeushukuru uongozi wa soka wa Mkoa wa Morogoro kwa kujitokeza kushiriki mazishi hayo kwa kuonyesha kwamba Marehemu alikuwa ni kipenzi cha wanamichezo.
Kwa upande wa uongozi wa Yanga ulioongozwa na Mwenyekiti wake Madega ulimwelezea Marehemu alikuwa ni kiongozi mwenye kuopenda mshikamano na viongozi wezake na busara zake zilitumika katika kuleta maendeleo ndani ya Yanga.
“ viongozi wa Yanya katika mazishi hayo walimzungumzia marehemu kuwa akiluwa ni kiungo kikubwa kati ya wanachama na viongozi katika kudumisha umoja na mshikamano “ alinukuu maneno ya viongozi wa Yanga
Naye Katibu Mwenezi wa Tawi la Yanga la Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, Leonard Masawe, alityeongozana na viongozi wa Matawi ya Yanga ya Morogoro, amewataka wanachamana viongozi wenzake kumwezi Marehemu kwa kusimamia mshikamano na utulivu ndani ya Yanga.
“ binafsi yangu nina fikiri ni wakati mzuri kumwezi mzee matunda kwa kusimamia mshikamano na amani katika timu zetu iwe Yanga ama watani zetu Simba “ alisema Masawe na kuongeza.
“ Matunda alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wasiopenda malumbano na siku zote hadi kifo chake amekuwa ni mtetezi wa misingi ya haki ya kila mwanachama…na ameiwezesha Yanga kuwa moja na tulivu hivyo ni wakati wa kuyaendeleza hayo” alisema Masawe
Akimzungumzia Marehemu, alisema alikuwa mhimili katika soka ndani ya Yanga na kwa timu nyingine katika kupenda maendeleo ya timu na wachezaji wake na jambo hilo ndilo lililomletea heshima kubwa katika jamii.
Katibu Mwenezi huyo alisema pamoja na kuwa muhimili katika soka, Marehemu Matunda katika kijiji alichozaliwa alikuwa ni mmoja wa wazee wanaoheshimika na wananchi wenzake wakiwemo wazee , vijana na akina mama.
Alisema wao kama viongozi wa matawi walimua kwenda katika kijiji hicho kuungana na viongozi wengine wa Yanga na MRFA na kuungana na wananchi wengine kuupokea mwili wa Marehemu majira ya saa 11 na dakika 45 ulipotokea jijini Dar es Salam na kushiriki kikamilifu mazishi hayo. Hata hivyo alisema wapenzi wa Yanga na Simba wa Tarafa hizo walijitokeza kwa wingi kuweza kumzika Mzee Matunda ambapo utani wa jadi wa timu hizo wa hapa na pale wakufurahisha zilijitokeza wakati wa shughuli za mazishi zikiwazinafanyika.
“ sijawahi kuona mazishi makubwa kama haya ya Mzee Matunda ..watu wengi walijitokeza kumzika na utani wa Simba na Yanga pia ulijitokeza wa kufurahuisha kati ya wanachama wa Simba na viongizi wa Yanga waliohuhdhuria mazishi hayo” alisema Masawe
Rashid Ngozoma Matunda alifariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Mwananyamala , Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla na mwili wake kusafirishwa juzi hadi kijijini kwake Lungala, Tarafa ya Mkuyuni Wilayani Morogoro na kuzikwa jioni ya siku hiyo.

habari hii imeletwa na mdau John nditi

Msiba wa mpiganaji Mike Sikawa

Nilikuwa naongea na John Mhala wa Arusha mwandishi wa HabariLeo alinitaarifu kuwa huenda mwandishi Mike Sikawa akazikwa Jumatatu ijayo mkoani Arusha habari zaidi nitawapatia kwa jinsi Mhala atakavyokuwa anawasiliana nami.

Wednesday, November 19, 2008

Mike Sikawa wa BBC afariki dunia

MTANGAZAJI wa idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mike Sikawa (55) ,amefariki dunia jana mchana baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari.
Sikawa, ambaye pia aliwahi kufanya kazi katika Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News na HabariLeo, alifariki dunia juzi majira ya saa 8.47 mchana nyumbani kwake Njiro, nje kidogo ya mji wa Arusha.
Kwa mujibu wa mdogo wake marehemu, Mchungaji Charles Sikawa, ndugu yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu na kutokewa na kidonda mguuni.
Mchungaji huyo alisema ndugu yake alipata matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini ikiwamo AICC, KCMC, St. Thomas na Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili iliyoko Dar es Salaam lakini hakupata nafuu yoyote.
Alisema ilifika wakati nusura akatwe mguu uliokuwa na kidonda lakini madaktari walifanikiwa kukwangua nyama ya mguu wa kidonda lakini haikuweza kusaidia.
Mchungaji huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kuhangaika kwa muda mrefu katika hospitali mbalimbali hapa nchini na kushindwa kupata nafuu, Sikawa alikuwa akipata matibabu akiwa nyumbani kwake hadi alipofikwa na mauti.
Alizaliwa King’ori wilayani Arumeru mkoani Arusha na kusoma elimu ya msingi katika eneo hilo kabla ya kufaulu na kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Ilboru na Mzumbe ya mkoani Morogoro.
Katika miaka ya 1970, aliajiriwa katika kampuni ya TSN kama mwandishi wa kawaida na baadaye kujiunga na idhaa ya Kiswahili ya BBC kama mtangazaji. Ameacha mjane na watoto wawili ambao wako Amerika ya Kusini.
Mipango ya maziko inasubiri ndugu, jamaa na marafiki walioko nje ya mkoa wa Arusha na sehemu zote alizofanyia kazi.
Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ametuma salamu za rambimbi kutokana na kifo cha mwandishi huyo na kuelezea jinsi alivyoguswa na msiba huo.
Dk. Migiro alisema alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika UN, Sikawa alikuwa mwandishi wa kwanza kumtafuta kwa ajili ya kumhoji juu ya uteuzi huo.

KCB Tanzania watoa milioni 25 kwa ajili ya ZAYADESA


Mama Shadya Karume, the chairperson of Zanzibar Youth Advancement forDevelopment, Education, Sanitation (ZAYADESA) is welcomed by DorisParsons, Head of Corporate Affairs and Communications, KCB Tanzania at a ceremony in Zanzibar where KCB Tanzania donated25m/- to ZAYADESA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi katika ikulu ya Tripoli jana jioni.Rais Kikwete alifanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Libya.Picha hii ni ya Fredddy Maro wa Ikulu

Tuesday, November 18, 2008

Inakuwaje kama mafisadi wa EPA wapo kila mahali katika uchumi?

kaka Beda
KAMA Watanzania wanalia na EPA hivi wanajua kwamba watuhumiwa wengi wa EPA wana mtandao mkubwa wa biashara? Wanajua kwamba wanahisa kubwa kubwa na nzito nzito katika mabenki na taasisi nyingine za kifedha? Hivi wanapokuwa rumande nini hasa kinatokea. Kuna maswali mengi hapa ya kujiuliza kama matajiri hawa wanasumbua sana mtaani kwetu hapa kama sio wakiondoka na baadhi ya taasisi za kifedha zinaondoka? Hebu angalia jinsi walivyo na mahisa kila mahali na nyie waandishi hamna cha kufanya.

Oni

Hii ni kazi ya polisi na waandishi wakitia mguu jasho litawatoka.Kazi iliyobaki ni ya DPP na sheria za mahakama
Lukwangule

Mbunge anapolalama na barabara


Mbunge wa jimbo la Temeke,Abasi Mtemvu, wa pili kutoka kushoto) akimuonyesha mkandarasi,Gaston Nsemwa wa Kampuni ya Lukolo ambayo imepewa kazi ya kujenga barabara ya Jeti kipande cha kilometa moja na nusu inayounganisha eneo hilo na Tandika Devis corna kwa kiwango cha lami.Mtenvu katika ziara yake karibuni alimlalamika mkandarasi huyo juu ya kiwango cha lami ambapo alisema uhandisi upo kwa kiwango cha chini sana na wala kazi hiyo hailingani na fedha walizotoa na kuitaka kampuni hiyo kufanya marekebisho haraka.Picha na habari na mdau Yusuf Badi.

Pinda awakomalia wanaopenda makongamano

SERIKALI imezitaka wizara zote zinazotaka kuandaa semina au makongamano kuomba kibali kwa Waziri Mkuu kabla ya kufanya hivyo.
Agizo hilo limetolewa kutokana na kile kilichobainika kuwa semina na makongamano yanayofanywa na Wizara mbalimbali yanagharimu fedha nyingi, jambo ambalo limeonekana ni ufujaji.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema jana mjini Dodoma kuwa kibali cha semina au kongamano kitatolewa kwa Wizara husika kama lina tija na si vinginevyo.
Pinda alisema kumekuwa na utaratibu mbaya wa matumizi ya fedha katika wizara mbalimbali nchini ambapo kila idara imekuwa ikifanya semina, kongamano, warsha na motisha, jambo ambalo limekuwa likigharimu fedha nyingi.
“Siku hizi kila idara wanafanya semina, kongamano halafu eti kuna kitu kinaitwa motisha katika idara, mambo haya yanagharimu fedha nyingi halafu wakati huohuo tunasema serikali yetu masikini hivi ni kweli jamani?” alihoji Waziri Pinda.
Pinda alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa na ili kisitumike katika warsha au makongamano, ni afadhali fedha hizo zikatumika katika kununua matrekta yaweze kugawiwa na kuwasaidia wakulima.
“Siku moja niliziagiza kila wizara iniletee bajeti yake ya mwaka kuhusu makongamano na warsha, wizara moja tu ndiyo iliyoniletea na bajeti yake ilikuwa Sh bilioni 4, jamani hii ni wizara moja na wizara ziko nyingi je, zikileta wizara kumi ni Sh bilioni 40 hizi fedha ni bora zitumike kununulia matrekta lakini si kwa ajili ya semina,” alisema Pinda.
Aidha alizitaka halmashauri zote nchini kupunguza matumizi katika semina na makongamano na badala yake fedha za maendeleo zitumike katika maendeleo.

Dar washauriwa barabara za juu, kukwepa msongamano

SHIRIKA la Maendeleo la Kimataifa la Japan, JICA, limewasilisha ripoti ya Sera na Mpango Kabambe wa Uendelezaji Mfumo wa Usafirishaji katika Jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kutumia sh trilioni 5 katika kipindi cha miaka 20 kuanzia mwakani.
Katika ripoti hiyo iliyofanyiwa kazi kwa takriban mwaka mmoja baada ya serikali kuiomba JICA mwaka 2005, imelenga katika kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuweka njia na madaraja ya juu, mabasi yaendayo kasi, njia za reli ili kuondoa msongamano katika Jiji hilo.
Akielezea kuhusu ripoti hiyo Mhandisi Mshauri wa JICA, Junji Shibata alisema mradi wa kuboresha sera za usafirishaji kwa Dar es Salaam inawezekana endapo taasisi zote zinazohusika katika usafirishaji zikiungana na kutafuta namna ya kutekeleza yaliyopendekezwa katika ripoti hiyo.
Alisema nguvu ya serikali kuu pekee katika kuboresha usafiri Dar es Salaam haiwezi kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo iwe ni kwa ufadhili au mapato ya ndani bali nguvu ya pamoja inahitajika hata kama mpango umelenga kipindi cha miaka 20.
“Tatizo la msongamano hapa Dar es Salaam ni kubwa sana ikilinganishwa na umuhimu wa Jiji hili kuongeza pato la Tanzania, hivyo ni wajibu kwa serikali na asasi za usafirishaji kupanga namna ya kutekeleza mradi huu maana sisi kama JICA kazi yetu ilikuwa ni kuonyesha mpango uweje na tumekamilisha,” alisema Shibata.
Shibata alifafanua kuwa mpango huo hauingiliani na mipango mingine iliyokwishawekwa na serikali ukiwamo wa mabasi yaendayo kasi, Dart, bali unaboresha na kwamba tofauti na Dart kuhusisha barabara kuu wenyewe wamependekeza kuwepo na mabasi ya kasi yatakayotumia barabara za juu katika jiji zima.

Ngozoma Matunda afariki dunia


MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Rashid Ngozoma Matunda amefariki dunia leo Dar es Salaam kutokana na shinikizo la damu.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lucas Kisasa aliliambia gazeti la HabariLeo kuwa Mzee Matunda ambaye pia aliwahi kushika nafasi ya uenyekiti na umakamu kwenye vipindi tofauti vya uongozi, alikutwa na mauti leo kati ya saa saba na nane mchana baada ya kuugua ghafla.
Kisasa alisema kwa mujibu wa maelezo aliyopatiwa na wana familia ya marehemu, Matunda aliamka vizuri tu asubuhi hiyo lakini kufikia saa nne asubuhi hali yake ilibadilika na kuwafanya wamkimbize hospitali ya Mwananyamala kupata matibabu, lakini alifariki kabla ya matibabu.
“Wanafamilia wanahisi kuwa Matunda amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu ingawa haijathibitika hivyo kitaalamu.”
Kisasa aliongeza kuwa msiba wa kiongozi huyo upo nyumbani kwa marehemu Manzese Uzuri na mwili wa kiongozi huyo unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda mkoani Morogoro kwa maziko.
Matunda atakumbukwa na wapenzi na wanachama wa Yanga kwa juhudi zake katika kuleta maendeleo ndani ya klabu hiyo, kwani akiwa Mwenyekiti mwaka 1998 aliiongoza Yanga mpaka hatua ya robo fainali ya michuano Ligi ya Mabingwa Afrika na kuzawadiwa Sh milioni 90.
Kutokana na klabu hiyo kupewa kiasi hicho cha fedha baada ya kufikia hatua ya robo fainali chini ya kocha Tito Mwaluvanda (sasa marehemu), ulizuka mgogoro ambao ulimfanya Matunda kupinduliwa na Abbas Tarimba Juni 20 mwaka 1999.

Wafaransa wamenisahihisha ndani Eastern Africa Producers Union

Dear

Thank you very much for your press release !
Kindly note that the French Embassy in Kenya (and not Alliance Francaise) supported the Forum, organized by the Kenya International Film Festival.
Best regards
Antoine Antoine
YvernaultAttaché audiovisuel régional Afrique de l'est
Regional Audiovisual Attache for Eastern Africa
Ambassade de France - Nairobi+254 20 277 87 30

Ngoma Africa band na baba wa kambo!


The Ngoma Africa Band,bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake nchini ujerumani, baada ya kutingisha na "Apache wacha Pombe" sasa wanafunga mwaka kwa kuachia wimbo wao mpya "Baba wa Kambo" ambao unaweza kuhusikia katika http://www.bongocelebrity.com/.
Wimbo huo ni ni utunzi wake kiongozi na mwimbaji wabendi Ebrahim Makunja aka Ras Ebby Makunja alimaarufu bwana kichwa Ngumu.
Katika wimbo huo Ngoma Africa wamefungua kesi ya kumshtaki "Baba wa Kambo" kwa jamii kutokana na udikteta wake ndani ya familia! isitoshe bendi imemteua mwanahabari maarufu Bw.MUHIDIN ISSA MICHUZI kuwa hakimu wa kuamua kesi hiyo!hakimu bado anapitia jarida la kesi hiyo!

Monday, November 17, 2008

Bwana shamba ashikishwa mkwanja kwa kazi njema


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Bwana Shamba wa Kata ya Mpunguzi, Athumani Mpanda baada ya kutoa maelezo mazuri na yakitalaamu ya jinsi anavyowasaidia wakulima wa kijiji hicho kulima kwa tija hasa zao la zabibu . Pinda alimzawadia Bwana Shamba huyo shilingi laki tano (500,000/= katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Mpunguzi wilayani Dodoma Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Dodoma jana. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Breaking news.. waliobaki rumande EPA sasa saba

Jeetu patel na mfanyakazi mmoja wa BOT wametoka nje kwa dhamana na kufanya idadi ya watu ambao bado wapo lupango kwa tuhuma za EPA kubaki saba.
Habari zaidi tunaweza kuzileta baadaye.

lilian internet kimwana kisichochuja jukwaani


Mnenguaji mkongwe nchini ambaye bado kuchuja ni Lilian Internet . Kimwana huyu bado yupo juu na haoneshi kwamba atashuka hivi karibuni. Yeye ni mmoja wa wanenguaji waandamizi nchini, akitamba tangia enzi za Diamond Sound wakati wa miondoko ya 'ikibinda nkoi' kule silent inn .Sasa yupo na twanga, akitwanga na kupepeta. Picha hii mali ya Issa Michuzi

Pinda na mwembe uliozaa vyema Dodoma


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (wapili kulia) wakitazama mwembe uliozaa matunda vizuri katika shamba la Mbunge wa Bahi na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma, William Kusila lililoko kwenye kijiji cha Intitaa katika jimbo la Bahi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi. Waziri Mkuu yupo mkoani Dodoma kuhimiza maendeleo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mgodi Bulyanhulu wabainika kutoa taarifa zisizosahihi

KITENGO cha Ukaguzi wa Dhahabu (GAP), kimebaini upungufu mkubwa katika mikataba ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika migodi ya Bulyanhulu, Geita ambayo imekuwa ikiipatia serikali hasara.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala cha Ukaguzi wa Dhahabu katika migodi mikubwa nchini, Bruno Mteta akizungumza na viongozi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu kwenye Kijiji cha Kakola wilayani hapa alisema timu yake imebainika kuwa yapo matumizi mengine ya uendeshaji wa mgodi ambayo yamekuwa yakisomeka isivyo na baada ya GAP kukagua vitabu vya mwekezaji huyo ambaye ni Barrick Gold Corporation, walikiri kuwapo kwa makosa na wameanza kuyarekebisha .
Mkuu huyo yupo katika kutekeleza programu ya uelimishaji wa umma mkoani Shinyanga juu ya migodi mikubwa ya dhahabu.
Mteta alisema hayo akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi hao waliowawakilisha wananchi wao walipohoji mikataba na upungufu uliokwishabainika kupitia ukaguzi wa kitengo hicho kilichoanzishwa Agosti mwaka jana.
Alisema baada ya kitengo hicho kuanza ukaguzi katika mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick Gold Corporation na Geita Gold Mine mali ya Anglo Gold Ashanti, imebainika kumekuwapo na taarifa zisizo sahihi huku wawekezaji hao wakidai kuwa wanapata hasara, jambo alilosema si la kweli.
Alisema pamoja na kuwa ujenzi wa mgodi hauhitaji fedha nyingi na huchelewa kupata faida, lakini baadhi ya maeneo yamekuwa yakitolewa taarifa zisizo sahihi.
Akitoa mfano katika mgodi wa Geita, alisema GAP imebaini kuwapo kwa taarifa za uongo juu ya matumizi ya uendeshaji wa mgodi, hali iliyosababisha mwekezaji huyo kukiri upungufu na kuahidi kulipa Sh bilioni 30 zilizokuwa zisilipwe serikalini kwa madai tu ya kugharamia shughuli za uendeshaji wa mgodi, jambo ambalo baada ya ukaguzi, iligundulika siyo kweli kwa vile haliingiliani na mkataba.
Aidha, katika ukaguzi huo imebainika kuwa wawekezaji hao wamekuwa wakijiamulia kujinunulia vitu ovyo kutoka nje ya nchi licha ya kuwa baadhi ya vitu hivyo vinapatikana nchini.
Kitengo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Nishati na Madini, kina kazi ya kuhakiki wingi na ubora wa dhahabu inayozalishwa na kusafirishwa nje na migodi mikubwa ili kujua thamani yake halisi na kiwango cha mrabaha kinachostahili kuingia serikalini.

Saturday, November 15, 2008

So natural, Pinda and the wife


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifurahia mavazi ya kimila waliyovalishwa na wazee wa kijiji cha Babayu wilayani Bahi wakiwa katika ziara ya mkoa wa Dodoma, Novemba 14,2008. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mama Kikwete ndani ya Charity Bazaar


First Lady Mama Salma Kikwete negotiates with Tsitsi Shitela for items on sale at Zimbabwe stall during the Diplomatic Spouses Group Annual Charity Bazaar in Dar es Salaam yesterday. (Photo by Bernard Rwebangira)

Profesa Jay akipagawisha ndani ya Fanta Flava Teens Parties


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Joseph Haule (Profesa Jay),akitoa burudani kwa wakazi wa Manzese Midizini katika nusu fainali ya Fanta Flava Teens Parties Dar es Salaam leo iliyoandaliwa na Kampuni ya vinywaji ya Cocacola

Hivi tunahitaji Kikwete kuja kutengeneza nyumba hizi?




Wakati mwingine kuishutumu serikali ni kupoteza wakati. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa bomba si kwa wizi lakini kwa kutumia maarifa na akili. Hainijii akilini kama kweli wanakijiji wa Mvuha Morogoro Vijijini wamefikia hatua hii.Yaani udongo upo tena unaofaa kutengeneza tofali na miti ipo lakini wao wanajilaza katika nyumba kama hii. Mimi hainijii akilini kwa sababu kwetu mlimani tuna nyumba za tofali za kuchoma za kuezekwa na nyasi halafu sisi ndio watu wa mwisho kabisa duniani, tunalima kabichi zinazoozea shambani.

Yaani kokoriko kweli hafikirii hatima ya Zimbabwe.. ona sasa MDC wamejitoa




Zimbabwe's political crisis deepened on 14 November with the withdrawal of the opposition Movement for Democratic Change (MDC), led by Morgan Tsvangirai, from the moribund power-sharing deal with President Robert Mugabe's ZANU-PF.
An MDC communiqué at the end of a national council meeting said it would peacefully campaign against any unilateral government appointed by Mugabe, and called for fresh elections under international supervision.
The party defended its decision on the grounds that, since the signing of the power-sharing agreement on 12 September, Mugabe had pursued an "obstructionist approach" and an "entrenched power-retention agenda" for the ZANU-PF party.
The MDC alleged that this included the "crafting of an assassination plot, codenamed Operation Ngatipedzenavo, intended to eliminate the MDC leadership", amid a wider campaign of violence and intimidation aimed at the party "and the people of Zimbabwe".
The communiqué rejected a resolution passed by leaders of the Southern African Development Community (SADC) on 9 November, urging the formation of an all-inclusive government to save the faltering agreement.
The MDC accused the SADC of mistakenly narrowing the sticking points to only control of the home affairs ministry and police, ignoring the unresolved logjams over the distribution of other portfolios, the appointment of provincial governors, permanent secretaries and ambassadors. IRIN was unable to get comment from ZANU-PF.
The power-sharing deal, brokered by South African President Thabo Mbeki, appointed as mediator by the SADC, was meant to fairly apportion ministries between ZANU-PF, Tsvangirai's MDC, and a breakaway faction of the MDC led by Arthur Mutambara.
Mugabe was to retain the presidency, while Tsvangirai was to become prime minister and have a say in the running of the government until new elections in 2012. But no constitutional amendment was passed to create the post of premier, and the deal was quickly overcome by bickering over posts and powers.
Mugabe is now expected to form a government without Tsvangirai - which many fear signals a return to the extreme levels of violence that racked the country during this year's election, when over 80 MDC supporters were killed.
Everybody knows that ZANU-PF has no solution to the country's problems, and everyone was hoping that Tsvangirai will agree to come into the government and solve our problems The MDC won the 29 March legislative poll and Tsvangirai beat Mugabe into second place in the presidential vote, but fell short of the 50 percent plus one ballot required for a first-round victory.
Tsvangirai withdrew from the presidential run-off, citing the political violence, which left Mugabe as the sole candidate. However, the election was condemned regionally and internationally as unfree and unfair.
Disappointment
Zimbabweans in Zimbabwe's second city, Bulawayo, received the news of the MDC's withdrawal from the unity deal with mixed feelings.
Martha Moyo, 28, said she was disappointed. "Everybody knows that ZANU-PF has no solution to the country's problems, and everyone was hoping that Tsvangirai will agree to come into the government and solve our problems."
Jabulani Sithole, 36, said the MDC was justified in refusing to take part. "It is clear that Mugabe did not want the MDC in government, because he should have negotiated in all earnestness, but giving them useless ministries was an indicator that the talks are dead, and what is left now is for the talks to collapse."
The MDC was condemned as "unpatriotic" by Nhamo Tsunga, 40. "These people [MDC] just want power, and they do not care how much we are suffering. The MDC should have just agreed to join government, and then sort out the other issues when they are in government. All this shows that they are selfish, and they are doing these things for themselves and not for the people."
Zimbabweans have been battered for years by shortages, lack of social services, and an inflation rate estimated at 231 million percent in July.
A trio of elders - former UN secretary-general Kofi Annan, former US president Jimmy Carter, and rights activist Graca Machel - are due to visit Zimbabwe next week to try and focus global attention on the humanitarian crisis.

Friday, November 14, 2008

Barabara mpya inapoumuka, mhh hii Mbagala hiii!!!


Waziri wa Miundo mbinu Dk shukuru Kawambwa akipewa maelezo na mhandisi mkazi wa Kajima Keish juu ya maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kilwa.

Naam sina uhakika kama mhandisi mjenzi huyu amemweleza waziri wetu kwamba lami wanayotumia ina matatizo.

Manake barabara katika mizunguko ya Bendera tatu, Jitegemee, Kambi ya Twalipo yote lami yake imeumuka. Halafu katika tuta linalozuia walevi wasigongwe pale Tanesco napo lami imeumuka. Kitu kinachomuka hupigwa hamira ndani yake sina hakika hamira gani imesababisha lami hii kuumuka.

Ujenzi unaonekana kuwa dhaifu kuanzia mitaro iliyopo ambayo inaonyesha utata mpaka katika ushindiriaji. Barabara kabla haijaisha inaumuka inakuwaje? Kuna maelezo ya kina kweli mtu anaweza kusema. Tunataka barabara ya Mbagala ikamilike ikae na itulie kwa viwango manake tunaambiwa mpaka katika matangazo yao ni Kodi za Wananchi wa Japan na ama hakika lazima tuwe na adabu zitumike vyema na sisi tulipe vyema. lakini ukiangalia huu ujenzi hapa utulivu si rahisi mtu mmoja atuambie inakuwaje vile mimi si mhandisi bwana. Hata zile nondo zinazotumika katika daraja lamto Kizinga labda zina hesabu zake za kuweka mzigo vyema, lakini kuna ghorofa hapa lilianguka ile misuko ya nondo na aina za nondo mhhhh! Mimi bwana si injinia lakini napozi swali Dk kawambwa ndio anajua.....

Serikali yazindua matangazo mapya ya utalii Uingereza




Na Mwandishi Maalum


SERIKALI ya Tanzania imezindua kampeni kubwa ya matangazo ya utalii kwenye vituo vya treni ya chini ya ardhi na London tax nchini Uingereza yaligharimu Sh.milioni 800, yatatakayodumu kwa miezi sita.Katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwanguga, katikati ya jiji la London katika sehemu ya maarufu ya watalii ya "London Eye" iliyopo karibu na ukumbi wa bunge la Ungereza.


Waziri Mwangunga alikata utepe kwenye tax mbili zenye matangazo hayo zilizokuwa katika eneo hilo, kuashilia kuzinduliwa rasmi kwa tangaz hilo na baada ya hapo na ujumbe wake walikwenda katika kituo kikubwa cha treni cha Victoria kuangalia moja ya matangazo ya vituo vya treni.


Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Publications, Bw.Juma Pinto iliyoratibu matangazo hayo alisema Serikali imelipia matangazo 25 tu kwenye vituo vya treni, lakini imepata matangazo ya ziada kwenye vituo vitano zaidi na kufanya matangazo hayo makubwa kufikia 30.


Bw. Pinto alisema kampuni ya CBS inayoratibu matangazo hayo ya vituo vya treni imetoa matangazo mengine 15 kwenye vituo vya treni ya DLR na matangazo 1,000 ndani ya treni.Matangazo hayo yote yatadumu kwa miezi mitatu.


Mkurugenzi huyo wa Jambo alisema matangazo mengine yaliyopo kwenye mkataba huo ni London Tax 100 "Black Cab" na matangazo 200 yatakakuwa ndani ya hizo tax yametolewa bure.Matangazo hayo ya London Tax yatadumu kwa miezi sita na yanatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani.


Awali mwaka mwaka huu mwezi Machi, Tanzania iliweka matangazo 100 kwenye mabasi ya London na matangazo sita katika uwanja wa ndege wa Heathrow, lakini baadhi ya watu wakidai kuwa hakuna matangazo yoyote yaliwekwa London.


"Mimi nadhani wanasiasa walikuwa wanataka kucheza mchezo wao mchafu kwenye haya matangazo, jambo ambalo haliingi akilini kusema kuwa hakuna matangazo wakati hadi leo kuna matangazo yetu pale Heathrow," alisema


Bw. Pinto.Alisema mwezi mMachi mwaka huu Serikali ililipia matangazo manne na tukaongezewe mawili na kuwa sita pale sehemu ya kuchukulia mizigo termian 4, matangazo yale yalikuwa yaishe mwezi Julai mwaka huu, hadi leo matangazo yapo na ndio yaliyoghalimu pesa nyingi."Haya matangazo ya Tanzania tunayafanya kwa umakini mkubwa kama daktari anaemfanyia mgonjwa operasheni, lakini kila siku panapokuwa na ukweli uongo unajitenga, sisi tunaendelea na kazi na watafute lingine," alisema Bw. Pinto.


Akizungumza katika uzinduzi kampeni hiyo, Waziri shamsa alisema Serikali ilishaweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji.


Wazir shamsa alisema awali Serikali ilizindua kampeni kama hii kule Marekani mapema mwezi uliopita kwenye televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingereza.matunda ya matangazo hayo yameanza kuonekana baada ya Marekani sasa kuongoza kupeleka watalii badala ya uingereza.


Alisema hivi sasa Tanzania imeamua kujitangaza na kuvitangaza vivutio vyake katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi ili tuweze kuongeza pato la Taifa na pia matangazo kama haya yanatumika kuitangaza nchi pia.


"Kweli tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publications kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyotaka na tuna imani hata huko siku za baadae tutaendelea kufanya nao kazi na hata kama kulikuwa na matatizo kidogo basi ya kibinadamu tu, alisema Waziri Shamsa.


Alisema Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa duniani kwa sababu imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la Taifa kutokana na watalii wengi sasa wanaongia nchini, hali inayofanya idadi yao kuongezeka mwaka hadi mwaka.


Alitoa tathmini ya watalii wa Uingereza wanaotembelea Tanzania alisema mwaka 1997 walifika watalii 25,000 hadi 2006 walifika 69,160 na mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka na kuamini idadi hiyo itaongeza mwaka huu."Tutashilikiana na balozi zetu kuhakikisha tunafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tunafanikiwa katika kuutangaza utalii na kuna mikakati mingi tumeifanya na sasa ni utekelezaji wake unaendelea," alisema Blandina Nyoni.


Alisema sasa wanaelekeza nguvu kwa nchi za Ulaya na hapa Uingereza ndiyo sehemu muhimu hapa Ulaya, kwani ndiyo nchi ambayo inapokea wageni wengi kuliko nchi nyingine yoyote hapa Ulaya, hivyo kujitangaza hapa ni sawa na kujitangaza duniani.


Awali Balozi wa Tanzania Uingereza, Mwanaidi Senare Maajar alisema tayari ubalozi wake umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na wizara ya utalii tangu mwaka jana.Balozi Maajar alisema Uingereza ni ufunguo muhimu katika sekta ya utalii wa Tanzania, hivyo wameweka mikakati mikubwa ya kufanyia kazi soko la utalii ili kuongeza idadi ya watalii na pia lengo la pili ni kuitangaza Tanzania.


"Tanzania tuna vivutio vingi sana ambavyo vinahitajika kutangazwa,na haya yaliyotangazwa katika matangazo ya sasa ni vichache tu kati ya vivutio vingi,serikali yetu inafuata misingi ya demokrasia na hata hali ya kisiasa ni nzuri na wananchi wake wana upendo mkubwa sana," alisema Balozi Maajar.


Mbali na Waziri Shamsa,Balozi Maajr, wengine waliohudhulia uzinduzi huo ni Katika Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Blandina Nyoni, Mkurugnezi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Bw. Peter Mwenguo, Balozi Msaidizi,Bw.Chabaka Kilumanga,Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Bw.Gerald Bigurube wa Tanzania na kundi zima la kundio la utamaduni la sisi Tambala.


Baada ya shughuli hiyo ya uzinduzi, Bazozi Maajar aliandaa tafrija fupi ya chakura cha mchana ubalozini na baadae kutoa utambulisho kwa Waziri kwa wafanyakazi wa ubalozi na wale kampuni ya Jambo Publications na baadae Katibu mkuu, Blandina Nyoni kutoa utambulisho kwa msafara wa wizara hiyo.


Mwisho


Caption


Pichani ni


Waziri Shamsa Mwangunga akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa London Tax 100 zinataokuwa na matangazo ya Tanzania kwa miezi sita.Wa Kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Utalii, Bi Blandina NyoniKatika sherehe hizo zilifanyika katika sehemu ya watalii ya London Eye juzi.(Picha kwa hisani ya Jambo).




Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Peter Mwenguo kulia akiwa na Mkurugenzi wa masoko, Bw. Mcha katika picha ya pamoja huku nyuma likionekana tangazo la Tanzania lilolokuwa katika kituo hca treni cha Victoria juzi.

Mbagala ni big town bwana!

Asante sana Beda.
Wenye kusaidia watusaidie. Mbagala ni potential 'big town' in the future!Nadhani wawekezaji wanakosea, population ya mbagala ni kubwa na huenda ukawa mji mkubwa sana hivi karibuni, ngoja barabara iishe utaona!
M., England

Shukurani la libeneke

Ndio kaka.
Natumai waendelea vema sana. Napenda kukupongeza kwa taarifa na habari ambazo mnatupatia sisi tulio nje ya nchi.
Tunanufaika saana na habari zenu na tunashukuru kwa hilo.
Kazi njema sana Kaka.
www.changamotoyetu.blogspot.com

Mtoto hujambo?


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsabahi mtoto mwenye umri wa miaka minne Catherine Paul aliyelazwa katika taasisi ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hii.Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo kupokea vifaa vya upasuaji mishipa na Ubongo vilivyo tolewa msaada na Kampuni ya Synthes Spine yenye makao yake makuu nchini Uswisi, kupitia hospitali ya Chuo Kikuu cha Weill Cornell kilichopo New York nchini Marekani.Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji Mishipa na Ubongo Dr.Roger Hartl.

Thursday, November 13, 2008

NDOVU SPECIAL MALT KWA WANATAALUMA


TUKIO JINGINE KUBWA LA NDOVU SPECIAL MALT KWA WANATAALUMA
Bia yadhamini mkutano wa wafanyabiashara na wanataaluma kwa Sh. milioni 5
Ndovu Special Malt yaendelea kuunga mkono wafanyabiashara
Udhamini ni katika mfululizo wa kuhusika kwa bia hiyo na matukio ya wanataaluma

Dar es Salaam: Ndovu Special Malt, moja ya bia maarufu nchini kwa mara nyingine tena inaendeleza ushirikiano wake na jumuiya ya wafanyabiashara nchini kwa kudhamini mkutano wa pili wa wafanyabiashara ujulikanao kama The 2nd Grand Networking After Dinner Talk 2008 ambao umeandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Baraza la Wahutubu la Afrika Mashariki (ESB).
Katika udhamini wake kwa mkutano wa mwaka huu, Ndovu Special Malt imetoa jumla ya Sh. milioni 5, fedha ambazo zitatumika katika maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo pamoja na mipango mingine ya kuuendeleza.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya udhamini huo kwa CTI, Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt Mpeli Nsekela alisema, “Sisi Ndovu Special Malt tunajivunia sana kuhusika na jumuiya ya wafanyabiashara hapa nchini. Tunafahamu fika mchango wa jumuiya hii kwa uchumi wetu na nchi nzima kwa ujumla ndiyo maana tumeamua kushirikiana na CTI na ESB katika tukio hili kubwa. Udhamini huu unasimika rekodi ya Ndovu Special Malt ya kushiriki katika matukio ya kibiashara ambapo wanataaluma mbalimbali wanakutana kubadilishana mawazo na kujenga mikakati.”
Ndovu Special Malt, ambayo kwa kawaida inapendelewa na watu wenye mtazamo wa kitaaluma, tayari imefanikisha matukio kadhaa yaliyowakutanisha wafanyabiashara na wanataaluma wengine yakiwemo udhamini wa miezi 9 wa Mkutano wa British Council wa Wakurugenzi, Warsha ya CTI ya Wanawake na Ujasiriamali, Chakula cha Jioni cha Taasisi ya Wahandisi, mikutano ya Mtandao wa Wanataaluma wa Tanzania na Usiku wa Wanamasoko ambao hufanyika mara nne kwa mwaka.
Mkutano huo utakaofanyika kwenye hoteli ya Movenpick Royal Palm jijini Dar es Salaam Ijumaa Novemba 21 utawakutanisha pamoja wafanyabiashara wakubwa, wakurugenzi watendaji, maofisa wa Serikali, wanadiplomasia, mameneja, wajasiriamali, wanataaluma mbalimbali na wadau wengineo. Mkutano huo utahutubiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Balozi Juma Mwapachu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) Felix G. N. Mosha.
Ndovu Special Malt inatengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pichani:CTI Business Development Services Dir. Cecilia Chambaka (r) speaks to the media during Ndovu Special Malt's presentation of the sponsorship cheque to CTI. Left is Ndovu Special Malt Brand Manager Mpeli Nsekela

Sasa walimu ruksa kugoma

THE Court of Appeal yesterday reversed the decision given by the High Court’s Labour Division, barring teachers to go on strike to press their payments.

Justices Edward Rutakangwa, Nathalia Kimaro and Bernard Luanda quashed the orders given by Judge William Mandia dated October 13, 2008 against Tanzania Teachers Union and set aside all High Court proceedings.

They ruled that the proceedings conducted by the High Court on the matter were a nullity and the judge erred in entertaining the application that was lodged by the Attorney General (AG) to oppose the teachers’ strike slated for October 15.
The Appeal Court’s decision appears to allow the teachers to proceed with their strike to press the government to pay them their demands.

Biashara hii jamani hebu ichangamkieni GTV na TTCL

beda naona upo mtandaoni, nilikuuliza sometime jinsi ya kuunganisha gtv maeneo yetu huko mbagala. pia jinsi ya kuunganisha mtandao wa simu za pre-pay (TTCL) nyumbani huko mbagala kwa dumba.
msomaji wako from England

Msomaji wangu nilipeleka shauri lako kwa wahusika lakini inaelekea inawapa taabu sana kuzungumza kwa hiyo naitandaza tena kuwakumbusha kuwa wanakosa soko Mbagala kwani kuna watu wanataka kuwafanyia mambo ndugu zao.
Lukwangule

NBC YAWANIA TUZO YA BENKI BORA AFRIKA


Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), moja ya benki zinazoongoza nchini imechaguliwa kuwa miongoni mwa benki 7 zitakazoshindania Tuzo za Benki Bora Afrika.

Tuzo za Benki Bora Afrika zinatoa heshima kwa juhudi za mageuzi ya kiutendaji, mifumo ya kisasa ya ufanisi na utendaji pamoja na ukuaji wa sekta ya kibenki barani Afrika. Tuzo hizi zinakusudia kusimika uwezo wa taasisi za kibenki zinazoongoza barani Afrika na watendaji wake ambao wanazidi kupanua uwezo wao katika sekta ya mabenki ulimwenguni.

Akizungumzia tukio hilo la kihistoria kwa benki hiyo na wadau wake, Mkurugenzi Mkuu wa NBC Christo de Vries alisema, “Haya ni mafanikio ya hali ya juu kwa NBC na utamaduni wetu wa ufanyaji kazi. Tuzo za Benki Bora Afrika zinawatunuku watendaji waliofanikiwa zaidi katika nyanja ya mabenki barani Afrika na kwetu sisi hii ni hatua kubwa katika njia tuliyoanza kuipitia tangu tulipoanza shughuli zetu hapa nchini.”
Tuzo za Benki Bora Afrika zinatambua mchango wa watu na taasisi za fedha zinazofanya juhudi za kuleta maendeleo barani Afrika na kusherehekea mafanikio ya mageuzi ya sekta hii nyeti. Tuzo zitatolewa kwa washindani waliochangia ufanisi mzuri katika sekta hiyo barani humu kwa mwaka 2007 katika makundi mbalimbali 17.
Uteuzi huu unaiweka NBC kwenye kundi moja na benki nyingine kubwa 6 Afrika nzima ambazo ni Attijariwafa Bank, Banco International de Mozambique, Intercontinental Bank, Oceanic Bank, Standard Bank na Zenith. Utaratibu wa kumchagua mshindi utafanyika mjini Washington DC, Marekani.
“Sote tunatambua kuwa kuchaguliwa huku kusingewezekana bila ya mchango mkubwa toka kwa jamii nzima ya NBC. Hatua hii imekuja wakati ambapo benki hii inapata changamoto tele toka kwa benki zingine mbalimbali na mazingira yanayobadilika kila wakati. Itakubalika kuwa kuchaguliwa huku kutatoa msukumo mkubwa kwetu sote kama wafanyakazi na benki yetu kwa ujumla,” aliongeza de Vries, akigusia nafasi NBC iliyomo katika soko la mabenki nchini Tanzania ambapo benki hiyo imekuwa ikiendelea kiutendaji.

kennedy alitabiri mweusi kuukwaa upresidee USA

Marehemu Robert Kennedy, mdogo wake John F. Kennedy ambaye aliuawawa mwaka 1963 akiwa rais wa Marekani, alitabiri mwaka 1968 kuwa huenda baada ya miaka 40 mtu mweusi ataweza kuwa rais.

Just for common knowledge:


Negro was the politically correct term for identifying black people in the 1960?s, instead of the other word, so Bobby Kennedy was being quite respectful to Black (African Americans) in that aspect when he gave this quote at that time.
But aside from that, his words were prophetic. Kennedy said this in 1968, here it is 2008? Exactly FORTY YEARS LATER!!! One of those things that make you say hmmm.
Hii nimeibua kwa dada Chemi Che-Mponda ndani ya swahilitime

Mchezo wa Korogonza jukwaani kesho



Dar Mchezo wa kuigiza wa Korogonza ulioandaliwa na kituo cha Sanaa za maonyesho Tanzania (TzTC) utanyeshwa kesho katika ukumbi wa Balozi Arts Center zamani Nyumba ya Sanaa jijini Dar es Salaam.

Meneja wa onyesho hilo Aloyce Makonde alisema leo kuwa tayari mchezo huo unaoshirikisha wasanii 10 kutoka vikundi mbalimbali umeshaonyeshwa katika miji ya Dodoma na Morogoro, na kwamba onyesho la kesho litaanza saa 1:00 jioni ambapo kiingilio kimepangwa kuwa shilingi 3000 na 1000 kwa wanafunzi.

“Ni mchezo ambao unazungumzia harakati za mwanamke mjasiliamali katika kukabiliana na maisha na kupamba na rushwa na umeandalia maalum kwa ajili ya kuonyesha kwenye tamasha la tano la Taasisi ya Sanaa za maonyesho mashariki mwa Afrika (EATI) litakalofanyika nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu,” alisema.

Amesema mchezo huo umetungwa na mtunzi mahiri hapa nchini Edwin Semzaba kutokana na warsha ya utunzi wa michezo iliyoendeshwa na taasisi ya PACSEA na kwamba onyesho la mchezo huo linatumia lugha ya kiingereza na Kiswahili.

“Onyesho limetumia lugha zote mbili ili kutoa nafasi kwa hadhira ya tamasha kuuelewa, limechanganya pia masuala ya ngoma ili kulipa onyesho uhalisia wa masuala ya utamaduni wa Mtanzania,” alisema Aloyce.

Mchezo huo unaongozwa na Godfrey Mngereza na kushirikisha wasanii mahiri akiwemo mwanamuziki Irine Sanga, washiriki wengine ni Asha Salim, Deosonga Njelekela, Ian Mwaisunga na Habiba Issa, wengine ni Aclay Mwalusamba ambaye ni mbunifu wa Mwanga, Zakaria Ngulunda Meneja wa Jukwaa na Halifa Sabuni ambaye ni Mbunifu wa Maleba. Mwisho.

Video kali ya Eric yaingia mtaani


ERIC WAINAINA

DAIMA

THE MUSIC VIDEOS


A collection of Eric Wainaina Videos Loaded with indepth interviews, never before seen footage and much more FEATURING THE OFFICIAL DAIMA (Kenya Only) VIDEO IN STORES NOVEMBER 20th

Beat the Christmas rush and get this collectors item now!

For more information or your advance copy Call Raninmaker on 020 44 54 182

TOT Plus taarabu kumsindikiza Dogo Mfaume Bagamoyo


KUNDI zima la Tanzania One Theatre (TOT PLus Taarab) watamsindikiza msanii chipukizi anayekuja kwa kasi Dogo Mfaume ambaye atazindua albamu yake ya 'Kazi ya Dukani' mjini Bagamoyo siku ya jumamosi hii katika ukumbi wa Saadan Club.

Akizungumza katibu mipango wa TOT, Gasper Tumaini amesema kuwa wamekubali kumsapoti Dogo Mfaume kutokana na kazi yake nzuri ambayo ipo katika albamu yake mpya ya Kazi ya Dukani ambayo inakuja kwa kasi ya ajabu.

Amesema kuwa katika onyesho hilo ambalo watashirikiana naye kwa upande wa muziki wa taarabu chini ya malkia wa mipasho Afrika ya mashariki na kati Khadija Kapa ambaye naye atatambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya za zamani.

"Unajua onyesho hilo litakuwa ni zuri na la aina yake kwani Dogo Mfaume ataitambulisha albamu yake ya Kazi ya Dukani na Khadija Kopa naye atambulisha nyimbo zake mbili mpya kwa wakazi wa Bagamoyo" amesema Tumaini ambaye hakupenda kutaja nyimbo za Kopa.

Amesema kuwa onyesho hilo ambalo litafanyika katika ukumbi wao wa nyumbani wa Saadan Club litaanza saa 2 usiku na wapenzi wao 20 wa kwanza wataingia bure na kuweza kuondoka na albamu ya Dogo Mfaume.

Mratibu wa onyesho hilo, Kuruthum Hadji amesema kuwa onyesho hilo litapambwa na maonyesho mengine ya utangulizi ya ngoma za kiasili kutoka katika vikundi vingi vya mjini Bagamoyo ili kuweza kumsapoti Dogo Mfaume ambaye sasa anatikisa na albamu yake mpya ya Kazi ya Dukani.

Sisi Tambala funika bovu London




Photos and story By Ayoub Mzee
Today at the excel exhibition centre in London , the Story of Tanzania has been laid bare as a land of ready smiles and incredible contrasts that beckons the visitor with a rich diversity of experiences.
It has also been laid bare as a fascinating and charming land of warm and friendly people. I sat there listening to the great men from Tanzania who were sent to sell their Country.
The story started from Tanzania being a country with the world’s most diverse ecosystem, squirrels, snakes that can glide through the air, pitcher plants and the countless species of flora and fauna yet to be discovered, to the story of underwater marine life and the untouched coral reefs to rich heritage and wilderness to modern city land scape .
Then Entered the Tanzania performing artists and dancers renown for their artistically intricicate beadwork around their bodies like the masai accompanied by Sisi Tambala band of fine musicians who sang in Swahili and some English . This set the whole house on fire.
I looked at the faces of the Tanzania team which had the expressions that reminded me of the words written by the great peot Simon Murray
"It was the first time I scored a goal.The only time I scored a goal in FactI was never a striker but like all little boys ,I dreamed of getting the winner in a big game.Yet because I was tall and lanky I always seemed to be putIn defence ..I was first and quite Strong but I just didn’t looklike a footballer at that young gangly age.So there I was , it was a corner , I think ,or id just wanderedInto the box. There were lots of players in front of me :a crowd.And I was towards the back. This was before I had been diagnosedwith severe short sightedness .I saw a blur of white approaching and I remember kind of falling ,stumbling forward s. The ball came all the way through the crowd.I poked out my leg. The solid leather ricochet off my shin andthe ball trickled into the back of the net.No one else seemed to know what happened apart from ….it was a goal!My one and only goal"
At the end of the day , as I was walking home , I could not stop thinking thatWho ever is in charge of the Tanzania Tourist board , he /she is doing a great job .
Well done this time .
You made us proud

Maziwa yenye sumu toka China yapo Dar... watch out!

Samples of the Chinese milk impounded in Dar es Salaam and sent to South Africa in October
for tests have been found to be contaminated with the killer chemica, melamine, The Citizen
can reveal.
A confidential report seen by The Citizen indicates that the chemical was found in three of
the nine samples the Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA) provided during the
investigation.
The authority had seized 34 tonnes in its crackdown on milk imports following the Chinese
scare, but the sample tested and found to contain melamine, was taken from seven tonnes, which a single trader had imported.
The news confirms the fears that Tanzania might have narrowly escaped disaster, with traders
having imported contaminated milk from China, where baby milk laced with melamine caused the deaths of four children last July, and had by September infected 94,000
other people across several continents.
Yesterday, the TFDA Director-General, Dr Singonda Ndomondo, confirmed receiving a
report from South Africa, indicating that the Chinese milk was contaminated.
The news will shock many consumers and might jolt the market, considering that about 70
per cent of the milk and milk products consumed in Tanzania are imported. With a population of
more than 4 million, Dar es Salaam needs at least a million litres of milk a day, but the
local processors are able to supply less than 60,000 litres a day.
?Yes, it is true that some of the samples we sent to South Africa have tested positive with
melamine chemicals, but everything will be made public on Thursday (tomorrow),? Dr Ndomondo said by telephone, when contacted for comment.
She said the authority, whose responsibility is to ensure the safety of drugs and food sold to
millions of consumers every day, would issue the full report on the Chinese milk saga at a press
briefing in Dar es Salaam.
Dr Ndomondo declined to discuss what steps TFDA was taking to mitigate the consequences of the findings until the full report was tabled before the authorities.
However, The Citizen independently established that the TFDA planned to destroy the
seven tonnes of the contaminated Chinese milk impounded.
A total of 34 tonnes of imported powdered milk was seized from several traders in September,
after the board banned imports of Chinese milk.
Local tests didn?t yield anything, hence the decision to send the samples to South Africa,
which has more sophisticated laboratories. A source told The Citizen that
the Dar es Salaam trader who brought in the contaminated milk cargo had been informed about the findings.
He said: ?A condemnation certificate has been issued to him. Among other things, he will
be required to pay for the cost of destruction of the tainted milk.? However, The Citizen
couldn?t establish when this will be done.
Tanzania reacted quickly to an alert issued by the World Health Organisation (WHO) at the height of the Chinese milk saga.
TFDA also suspended the issuing of import licences for milk products until the investigation
is concluded.
Senegal, Liberia, Benin, Burkina Faso, Burundi, the Democratic Republic of Congo, Gabon, Ivory
Coast, and Togo also slapped bans on Chinese milk imports after investigations in China found in
milk traces of melamine, a chemical used to make plastics.
The Chinese milk scandal involved milk and infant formula, and other food materials and
components, which had been adulterated.
The scandal broke on July 16, after 16 babies who had been fed on milk powder produced by
Shijiazhuang-based Sanlu Group were diagnosed with kidney stones.
With China's wide range of export food products, the scandal has affected countries on all the
continents.
According to scientific journals, melamine is a hard synthetic substance better known for its
flame retardant properties.
The nitrogen-rich molecule is sometimes illegally added to food products in order to increase
their apparent protein content.
It has also been employed as a non-protein nitrogen, appearing in soy meal, corn gluten meal and cottonseed meal used in cattle feed.
Melamine is known to cause renal and urinary problems in humans and animals when it reacts with cyanuric acid inside the body, sometimes present in drinking water and in animal feed, so its use in food production is universally banned.
Melamine adulteration of food products made headlines when pet food was recalled in Europe and the United States in 2007.
A number of arrests were made following the scandal in China.
The head of Sanlu, seven local government officials, as well as the director of the
administration of quality supervision, inspection and quarantine were sacked or forced
to resign over the scandal.
The WHO described Chinese milk saga as one of the largest food safety concerns it has had to
deal with in recent years. In late October, it was discovered that the problem had
spread to eggs and possibly other food categories.

habari hii ipo katika gazeti la Citizen na serikali bado imepoa haitoa taarifa watu wakaelewa nini kinaweza kuwasibu na wapi wakimbilie kikiwapata. Haki ya mlaji ipo wapi?

Wednesday, November 12, 2008

Chuo kikuu chasimamisha masomo kimtindo



Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimewasimamisha masomo wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kwa muda usiojulikana.
Uamuzi huo unaelekea kulenga kuleta amani chuoni hapo ambapo migomo ya wanafunzi imekuwa ikitibua mazingira ya usomi.
Wanafunzi wamekuwa wakishinikiza serikali kukubali kugharamia elimu moja kwa moja.
Wanafunzi wamekuwa katika mgomo kwa siku tatu mfululizo.
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo leo asubuhi, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (DVC) Profesa Yunus Mgaya alisema maamuzi hayo yamefanywa katika kikao cha dharura cha 184 cha baraza la chuo.

Tuesday, November 11, 2008

Zain yaipiga tafu THT kukabili ukimwi kwa sanaa




KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania imekipatia kikundi cha burudani cha Tanzania House of Talent (THT) pesa kwa ajili ya kutoa elimu kupitia sanaa na maigizo katika programu maalum ya elimu ikiwa ni kampeni ya mapambano dhidi ya maradhi ya UKIMWI katika shule za msingi na sekondari nchini, na kupanua wigo wa maarifa ya maradhi hayo kwa wanafunzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe alisema Zain imetoa sh. milioni 35 katika mradi huo wa THT ili kusaidia kuelimisha wanafunzi na kizazi kipya kwa ujumla katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujikinga na maambukizo ya maradhi ya UKIMWI.
"Zain inafurahia kufanya kazi na THT kwa lengo la kuwalinda vijana wa Tanzania. Vijana ndio taifa la kesho, na tunaamini mchango wetu kwa THT katika programu hii ya elimu itakayotumia sanaa kuelimisha wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kuhusu kujikinga na maambukizi ya UKIMWI, utasaidia kizazi kipya kujikinga na maradhi hayo," alisema Tunu.
Rebecca Young, Meneja wa THT alisema: "Tunaona fahari kwa Zain kujikita kusaidia programu yetu na kutupatia pesa za kuendeleza programu yetu. Sanaa imedhihirisha ni njia bora ya kufikisha ujumbe kwa jamii, na THT ina uwezo wa kutumia njia hiyo kufikisha ujumbe kuhusu mada mbalimbali kwa njia ya sanaa jukwaani," alisema.
Pesa hizo zitaisaidia THT kupata mwamko wa kutoa elimu kuhusu maambukizi ya maradhi ya UKIMWI na mengine kwa ujumla. THT pia itaandaa semina zitakazoelimisha kuhusu mambo mbalimbali ya msingi kwa jamii ikilenga hasa kupambana na maradhi ya UKIMWI.
Vijana wa THT watatoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa ikiwa ni pamoja na ujumbe kupitia muziki, dansi na ngoma. Vijana hao watafanya maonyesho katika shule 20 za Dar es Salaam, kwa lengo la kuwaelimisha wanafunzi hao.
Mbali na pesa hizo, Zain pia imetoa mchango wa basi kwa THT litakalowezesha vijana wanaounda kundi la THT kutumia kusafiri katika shule 20 za Dar es Salaam kwa lengo la kutoa elimu kupitia sanaa.
Kikundi cha THT kilianzishwa mwaka 2005 na kinaundwa na vijana wapatao 45 wenye umri kati ya miaka 14 na 24. Kundi hilo la vijana limekuwa likitoa burudani maridhawa katika matukio mbalimbali nchini.
"THT inaamini kwamba vijana wana jukumu la kutoa elimu kwa vijana wenzao na jamii kwa ujumla. Zain inawapa vijana wa THT nafasi ya kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya muziki, dansi na ngoma," alisema Rebecca. THT inaamini itafikisha ujumbe kwa haraka zaidi kwenye jamii kupitia burudani katika karne hii ya 21.
TANGAZA NASI LEO

xx