MWIMBAJI mahiri wa taarabu nchini Nasma Khamis 'Kidogo' amefariki dunia, Baba mdogo wa marehemu, Hamis Kaniki alithibitisha.
Imeelezwa kuwa Nasma alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na malaria.
baba mdogo huyo amesema hadi umauti unamkuta Nasma alikuwa akijishughulisha na masuala ya biashara pamoja na mifugo, ingawa pia usanii alikuwa akiendelea lakini akiwa anajitegemea.
Alisema marehemu alizaliwa miaka 57 iliyopita Kilwa Kivinje na alibahatika kupata watoto nane, ambapo sita wapo hai wakati wawili ni marehemu na kuwa maziko yatafanyika kesho makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Marehemu Nasma anakumbukwa kwa Kamba ya Mgomba, Koroboi, Ikwinini na Kidudu Mtu wakati kwiwa TOT na Kaona Mambo Iko Huku na Sanamu la Michelin alipokuwa Kundi la Muungano Cultural Troupe.
Marehemu ambaye pia alipata kuimbia kundi la Babloom Modern ingawa hakung'ara sana, atakumbukwa kutokana na upinzani uliokuwepo miaka ya 1990 kati yake na Khadija Omar Kopa, wakati huo Nasma akiwa Muungano na Khadija akiwa TOT.
Mungu amuweke Mahali Pema Peponi.Amin.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO