Na Mwandishi Maalum, Gairo, Kilosa, Morogoro Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa Serikali itachukua hatua za kufidia moja kwa moja be...
Na Mwandishi Maalum, Gairo, Kilosa, Morogoro
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa Serikali itachukua hatua za kufidia moja kwa moja bei ya wakulima wa zao la pamba, ili kuwalinda wakulima hao dhidi ya athari kubwa za kushuka kwa bei ya zao hilo kutokana na mtikisiko wa uchumi wa dunia.
Rais amesema kuwa hatua kamili za Serikali kuhusu kuwalinda wakulima hao ambao bei ya pamba yao imeshuka sana kutokana na mtikisiko wa uchumiwa dunia zitatangazwa karibuni.Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali haitaweza kufidia bei hiyo kwa kiasi kikubwa kutokana na uwezo mdogo, lakini angalau itachukua hatua kiasi cha kupunguza makali ya bei kwa wakulima.
Rais ametangaza habari hiyo njema jana, Ijumaa, Juni 26, 2009 wakati a alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa mji wa Gairo, Wilaya ya Kilosa, kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Morogoro.
Rais aliwasili wilayani Kilosa jana asubuhi kwa gari akitokea mjini Dodoma ambako alifanya ziara ya siku mbili kikazi.
Rais Kikwete yuko Kilosa kukamilisha ziara ya Mkoa wa Morogoro aliyoifanya Novemba, mwaka jana, lakini akaacha kiporo jimbo la uchaguzi la Gairo.
Mkoa wa Morogoro ulikuwa wa 21 na wa mwisho wa Tanzania Bara kutembelewa na Rais Kikwete katika miaka mitatu ya kwanza ya uongozi wake. Rais Kikwete alikamilisha ziara ya mikoa yote ya Tanzania wakati alipotembelea mikoa ya Zanzibar na Pemba Januari, mwaka huu.
Rais Kikwete amewaambia wananchi kwenye mkutano huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Mji Mdogo wa Gairo: “Tutajaribu kuchukua hatua za moja kwa moja za kufidia bei ya wakulima wa zao la pamba. Hatua kamili zitatangazwa baadaye baada ya wataalamu kukamilisha tathmini yao ya jinsi wakulima wa zao hilo wanavyoweza kusaidia.”
Amesema Rais: “Hatuwezi kufanya mambo makubwa sana kwa sababu bei ikishuka huko kwenye masoko ya kimataifa ni vigumu sana kuipandisha bei hiyo kwenye soko la ndani.”
Bei ya pamba kwenye soko la kimataifa imeshuka kutoka senti 82 za dola mwaka jana hadi kufikia senti 40 tu.
Ameongeza Rais Kikwete: “Nia ya Serikali ni kupunguza makali ya wakulima wa pamba. Hatutamaliza tatizo, lakini tutapunguza makali. Hii ni Serikali inayosikia kilio na matatizo ya wananchi. Hii ni Serikali inayojali.”
Kauli hiyo ya Rais Kikwete inakuja siku chacha tu baada ya kiongozi huyo kuwa ametangaza hatua kamili za kulinda na kunusuru uchumi wa Tanzania dhidi ya athari kubwa za mtikisiko mkubwa wa uchumi wa dunia.
Rais Kikwete alitangaza hatua hizo Juni 10, mwaka huu, 2009 wakati alipolihutubia taifa alipozungumza na wazee wa Mkoa wa Dodoma na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Kilimani, Dodoma.
Mpango huo wa kunusuru uchumi utaigharimu Serikali kiasi cha sh trilioni 1.7 na hatua za mpango huo zitanufaisha sekta mbali mbali zilizoathiriwa na mtikisiko huo wa uchumi. Moja ya malengo makuu ya Mpangu huo ni kuongeza kasi ya kuzalisha chakula.

Pichani: Rais Jakaya Kiwete, akimsikiliza mzee wa kimila wa kabila la wakaguru, Anock Malali ‘ Chamkaya’ mwenye kushika kinasa sauti baada ya kumsimika kuwa mzee wa Kimila wa Kabila hilo Juni 26 kabla ya Rais kuwahutubia mamia ya wananchi wa Mji Mdogo wa Gairo, Wilayani Kilosa , Mkoani Morogoro.Picha hii kwa hisani ya mwandishi wa habariLeo Morogoro John Nditi
COMMENTS