Wasomaji wa blogu Hebu tujikumbushe alichosema Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, katika kijitabu chake “Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania” a...
Wasomaji wa blogu
Hebu tujikumbushe alichosema Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, katika kijitabu chake “Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania” alichokitunga katika miaka ya 1990, katika ukurasa wa 15 hadi 16 kuhusu mfumo wa Serikali Mbili.
Msimamo huu wa Mwalimu pia unatoa mwanga kuhusu majibu ya swali katika mjadala uliokuwa ukiendelea hivi karibuni kuwa “Zanzibar ni Nchi au Siyo Nchi?”
“Nchi mbili zinapoungana na kuwa Nchi Moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili: Muungano wa Serikali Moja, au Shirikisho la Serikali Tatu. Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafutwa na Nchi mpya inayozaliwa itakuwa ni Nchi moja yenye Serikali Moja. Katika mfumo wa pili kila nchi itajivua madaraka Fulani ambayo yatashikwa na Serikali ya Shirikisho, na itakuwa na Serikali ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki.
Mambo yatakayoshikwa na Serikali ya Shirikisho ni yale ambayo yakibaki katika mamlaka ya nchi zilizoungamana, basi kwa kweli nchi hizo zitakuwa hazikuungana kuwa Nchi Moja, bali zitaendelea kuwa Nchi Mbili zenye ushirikino mkubwa katika mambo fulani fulani.
Nchi za Afrika Mashariki zilikuwa katika hali kama hiyo kabla ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zilikuwa Nchi Tatu zenye ushirikiano mkubwa, lakini hazikuwa Nchi Tatu zilizoungana kuwa Nchi Moja yenye muundo wa Shirikisho. Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni Nchi Moja yenye Serikali tatu, Serikali ya Shirikisho, na Serikali mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.
Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo ka sababu ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa ina watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000).
Mungano wa Serikali moja ungefanya ionekane kama Tangayika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tudhaniwe, hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya! Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha Serikali ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12,000,000 na pia ndiyo ingetoa sehemu, kubwa ya ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 12,300,000.
Ni watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo ingekuwa ndogo, hata bila ya mambo yasiyo ya Shirikisho. Na pia gharama zote hizo zingebebwa na Tanganyika.
Kwa hiyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? HIvi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila ya kuwa na Serikali yake, itaonekana kuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute muundo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila ya kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikali mbili zenye uzito unaolingana.
Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya ya muundo wa Serikali Mbili. Badala ya kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazama hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo utakaotufaa zaidi.”

COMMENTS