MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeanza kutoa posho ya Sh 100,000 kila mwezi kwa watumishi wake 111 wa kada mbalimbali wanaoishi na virusi vya Ukim...
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeanza kutoa posho ya Sh 100,000 kila mwezi kwa watumishi wake 111 wa kada mbalimbali wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wenye Ukimwi.
Posho hiyo inayolenga kuwawezesha kununua chakula cha lishe kwa ajili ya kuboresha afya za miili yao inatolewa na mahakama hiyo ikiwa ni utekelezaji wa waraka wa watumishi wa umma namba 2 wa mwaka 2006 kuhusu huduma kwa watumishi wa umma wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wenye Ukimwi
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Kmati ya Ukimwi ya mahakama hiyo, Jaji Bernard Luanda kwenye semina ya Ukimwi kwa watumishi wa mahakama kuu kanda ya Iringa iliyofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Mahakam Kuu Iringa ikihusisha wilaya za Iringa, Kilolo na Mufindi.
Alisema wengi wa watumishi hao ni wale waliojitokeza kupima Ukimwi kwa hiari kati ya mwaka 2006 na mwaka huu, mahakama hiyo ilipoanza jitihada za kuutekeleza kwa vitendo waraka huo.
“Nchini kote watumishi 365 wa mahakama wamekwishajitokeza kupima hali ya afya zao na kati yao 111 waliobainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo na kutoficha hali ya afya zao wameanza kupata kiasi hicho cha fedha, nje ya mishahara yao ili kisaidie kuwawezesha kupata lishe muhimu zinazohitajika kwa ajili ya kuboresha afya zao,” Jaji Luanda alisema.
Kwa kupitia mafunzo hayo, Mratibu wa Ukimwi wa mahakama hiyo, Wanyenda Kutta aliyataja madhumuni ya semina hayo kuwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi wa mahakama kupitia vipengele muhimu vilivyoko katika waraka huo, kujua hali ya Ukimwi mkoani Iringa, huduma zinazotolewa, wajibu wa mahakama katika udhibiti wa Ukimwi kwa kutumia fedha za serikali, ukweli kuhusu Ukimwi, na kinga, tiba na lishe.
“Kwa watumishi wanaoendelea kuficha hali ya afya zao, tuanomba wajitokeze kwa wakuu wao wa vituo vyao vya kazi ili waingizwe kwenye orodha ya watumishi wa mahakama wanaotakiwa kupata msaada huo wa fedha uliotajwa na Jaji Luanda kwa ajili ya lishe,” alisema.
Katika mada yake kuhusu hali ya Ukimwi mkoani Iringa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Ezekiel Mpuya alisema kuwepo kwa mipango hafifu ya kukabiliana na janga hilo mahali pa kazi kumechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizi ya Ukimwi mkoani Iringa.
Hata hivyo alisema kwa kushirikiana na wadau wote muhimu na kwa kuutekeleza waraka huo wa serikali, mpango mkakati wa miaka minne wa mkoa wa Iringa unalenga kupunguza kasi ya sasa ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 50.
“Takwimu za kitaifa zinaonesha mkoa wa Iringa unaoongoza nchini kwa kuwa na asilimia 15.7 ya maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa kupitia mkakati tuliojiwekea tunataka ifikapo mwaka 2012 maambukizi hayo yawe yamepungua kwa asilimia 50,” alisema.
Source Frank leonard wa Habarileo

COMMENTS