Asubuhi hii ya leo nilienda kulpiga kura katika kituo changu kule Mbagala Mianzini. Yalikuwa majira ya saa mbili asubuhi na mambo yalikuwa s...
Asubuhi hii ya leo nilienda kulpiga kura katika kituo changu kule Mbagala Mianzini. Yalikuwa majira ya saa mbili asubuhi na mambo yalikuwa shwari sana.
Nilipiga kura yangu katika kituo cha Community ambacho kimehamishiwa katika ofisi ya kata ya Mianzini.msimamizi Aziz Idd alisema kwamba mpaka majira hayo ya saa nne mambo yalikuwa ni mazuri na hapakuwa na shida.
Baada ya kumaliza kazi ya kupiga kura nilitafuta maoni ya watu katika kituo kile,ambaow alisema wamefurahishwa na kasi ya wasimamizi na pia mpangilio wa majina kwani kama hayaonekanai wapo watu waliokuwa wanasaidia kujua ni kituo namba ngapi walipo.
Nilipomaliza nikaenda kituo chenye watu wengi, Mbagara Rangi tatu, kisha nikaenda Kongowe Mzinga na kumalizia na Mbagala Kizuiani .
Kwa ujumla mambo ni shwari mpaka saa sita mchana japo kulikuwa na kasoro za hapa na pale hasa katika kituo cha Rangi tatu na na Kizuiani.
Mbagala Kizuiani nilikutana na binti akiwa na mtoto wake. Nilijitambulisha kwake naye akajitambulisha. Anaitwa Tatu Swaum anasema tangu saa kumi na mbili yupo pale anahangaika kutafuta jina lake.
"Hii mara yangu ya kwanza katika maisha yangu kupiga kura nataka kupiga kura jina langu silioni" alisema Tatu. Nilipomdodosa zaidi alisema kwamba yeye alijiandikisha katika ofisi hiyo ya Kata ambapo ndipo anapostahili kupiga kura.
Askari polisi mmoja D 8541 aliamua kumsaidia baada ya kugundua kwamba amekuwa akizunguka na mtoto muda wote hata kabla kituo hakijafunguliwa.
Alichukua simu yake na kupeleka namba ya kitambulisho chake NEC, sikuwa na nafasi ya kuendelea kubaki pale niliondoka.Mbagala Rangi tatu, Rajabu, mpiga kura mmoja alisema kwam,ba jina lake halikuwa katika makaratasi nje lakini mtendaji alimsaidia kupiga kura baada ya kugundua kwamba jamaa amepeleka sms mara saba NEC na zote hazikujibiwa.
Mwanahawa Waziri ambaye alikuwa msimamizi msaidizi pale Rangi tatu alisema mambo ya eneo lile ni shwari.Rajab alisema amefurahi kupiga kura hata kama jina lake halipo lakini anataka siku za usoni NEC kuwa na utaratibu bora zaidi na wananchi waambie ukweli.
Hapa pia nilikutana na mzee mmoja Ayoub Yusuf Nassoro ambaye alishapiga kura lakini alikuwa akimsaidia mzee mwenzie ambaye jina lake lilikuwa halionekani popote pale.
Mzee Nassoro alisema mgawanyiko wa kata huenda ndio uliozua rabsha.
Naam kituo kingine ambacho nilifika ni cha kongowe mzinga ambapo makundi yalikuwa hapa na pale. Inaaminika eneo lile ni la CCM na CUF wanakamiana sana.
Ofisa mmoja wa polisi Pallangyo aliniambia mambo shega na kwa kipindi hicho watu wanatoka kanisa hakuna taabu hata kidogo.

COMMENTS