MBUNGE wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla( CCM), ameanza kutekeleza majukumu yake kwa wananchi waliomchangua kwa kutoa msaada wa sh: milioni ...
MBUNGE wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla( CCM), ameanza kutekeleza majukumu yake kwa wananchi waliomchangua kwa kutoa msaada wa sh: milioni mbili kwa kamati ya maafa ya Wilaya ya Mvomero mara baada ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko ya mvua yaliyotokea mwanzzoni mwa mwezi katika Kata tano za Tarafa ya Mgeta.
Mvua hizo zilizoambatana na upepo zilitokea Novemba 11, mwaka huu ambapo zilisababisha vifo vya watu wa tatu kutoka Kata ta Bunduki kufariki dunia baada ya kusombwa na maji sambamba na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, vyanzo vya maji, mashamba na makazi ya watu.
Mbunge huyo alifanya ziara juzi ( Nov 19) siku moja baada ya kuhairishwa kwa kikao cha kwanza cha Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Katika hatua ya Mbunge huyo aliwatemebelea wananachi walioathirika katika Kata tano ya Bunduki, Langali, Mgeta, Tchenzema na Nyandira ambazo zinaunda Tarafa hiyo
Akiwa Kata ya Bunduki, Mbunge huyo aliwapta pole wananchi waliopoteza ndugu zao watatu kutokana na kusombwa na mafuriko ya maji ya mvua hizo ambazo ziliambatana na upepo mkali.
“ nikiwa Dodoma kwenye shughuli za Bunge ilipata taarifa ya mafuriko yaaliyosababaisha madhara makubwa pamoja na kupoteza maisha ya watu watatu …hivyo moja kazi ya mbunge ni kuwa mwakilishi wa wananchi na kuwasemea matatizo yao” alisema Mbunge huyo
Hivyo alisema kuwa baada ya kupata tathimini ya mahitaji halisi kutoka kwa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Mvomero chini ya Katibu wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji , Sarah Linuma, aliwalisiana na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda na kumjulisha maafa hayo.
“ hili suala ni la maafa na lipo chini ya Kamati ya Maafa ya Wilaya…lakini kama mbunge mwakilishi wa wananchi baada ya kuletewa taarifa kamili na mahitaji na Mkurugenzi wetu wa Wilaya ambaye ni Katibu wa Kamati hii” alisema Mbunge huyo
Hata hivyo aliongeza kusema “ nimechukua hatua za mwanzo kwa kumemwona binafsi mheshimiwa Waziri Mkuu na kumjulisha hali halisi naye amesikitishwa na kutoa pole kwa waathirika , pia kutoa agizo kwa Kitengo cha Maafa cha Ofisi yake kifike hapa Tarafa ya Mgeta kutoa misaada zaidi ya akibinadamu na kimiundombinu” alisema Makalla
Pamoja na kuwapa pole wananchi wa Kata hizo, Mbunge huyo waliwataka watendaji hasa wenyeviti wa Serikali za vitongoji, Vijiji na Kata kuendesha zoezi la kuhakiki wananchi walioathiriwa kwa usahihi bila kutoa upedeleo ili wahusika wawezekupata misaada itakayowalenga wahusika na si wengine nje ya hao.
“ nawaombeni tuwe waaminifu katika hili la kuorodhesha watu waliokubwa na maaafa haya…waliobomokewa nyumba zao na kuharibiwa mashamba yao…ili takwimu zinazoikifia Kamati ya Mafa ya Wilaya ziwe kamilifu na usahihi bila kutofautiana ili kila mmoja wao wenye kuguswa apatiwe msaada amaostahiki kwa nia ya kuondoa manung’uniko na lawama ziku za usoni” alisisitiza Makalla
Awali akitoa taarifa ya maafa yaaliyotokea Kata ya Bunduki, mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo, Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Salum Msonge, alisema kuwa mvua hizo zilizoambatana na upepo mkali ilitokea jioni ya Novemba 11, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine wawili kutojukukana walipo.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, kuwa Kaya nyingi katika Vijiji vitano vya Kata hiyo nyumba zao zimeharibiwa na mvua hizo zimeharibu ekeri 270 za mazao ya aina mbalimbali na kuhatarisha kujitokeza upungufu wa chakula , kuharibu vyumba vinne vya madarasa ya shule ya Msingi Kibigiri.
Pamoja na hayo alisema kuwa mvua hizo zimeharibu kabisa daraja kubwa Msofe linalinganisha kati ya Kata ya Mgeta na Bunduki sambamba na daraja jingine la Msituni , hivyo kusababisha wanafunzi wa shule ya msingi na Sekondari kupata atha ya kuvuka kwenda shuleni pamoja na wananchi wengine.
Nayo wananchi wa Kata ya Langali, Mgeta , Tchenzema na Nyandira , kwa nyakati tofauti walimshukuru Mbunge huyo kwa kuwajari kwa wakati mara baada ya kutokea kwa janga hilo lilolosababisha madhara makubwa wa wananchi wa Kata hicho.
“ tunakushukuru Mbunge wetu kwa kutujari kwa haraka na matumaini uliyotupatia kuwa Serikali kuu ipo mapoja nasi kwa kutusaidia kwa hali na mali pamoja na kuboresha miundombinu ya Barabara” alisema mmoja wa mkazi wa Kata ya Tchenzema
Hata hivyo kwa mujibu wa tathimini ya Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Mvomero chini ka Katibu wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sarah Linuma, katika barua yake kwenda kwa Mbunge huyo imeainisha kuwa mahitaji ya waathirika wote katika Tarafa hiyo kuwa bati ni 1,378, saruji mifuko 706 na mbao ni 813 sambamaba na vifaa vingine.
NB Kwetu sisi Nyandira sijui kibanda changu kama kipo hai manake nasikia ilikuwa mshike mshike kwelikweli na kutoka huku mbali lazima niende tutaambiana nikifika

COMMENTS