F .status-msg-wrap { display: none; }
Thursday, December 30, 2010
Lady Jay Dee amaliza mwaka na matawi ya juu

Lady Jay Dee amaliza mwaka na matawi ya juuLady Jay Dee amekuwa msanii wa kwanza kupata endorsement katika maji ya kunywa ambayo yana jina lake yanayotolewa na Mohamed Enterprises Limited.Pamoja na kuonesha maji hayo kwa waandishi wa habari leo katika hoteli ya Paradise City jijini Dar, pia alizungumzia mkataba huo na mipango yake.
Jay Dee alisema kwa mwaka 2011 pamoja na megine atafungua mgahawa uitwao 'Nyumbani Lounge' karibu na Best Bite Restaurant maeneo ya Ada Estate pamoja na kutoa albamu yake ya tano.
Aidha amesema kwamba amepunguza maonesho yake hapa nyumbani baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Sonny ya kuandaliwa matamasha ya kimataifa.
Pichani Jay Dee akionesha maji na nyingine akizungumza na waandishi wa habari.
Source:
Ankal Michuzi
Celebrating Bongo Films, Bongo Sounds, Music and Performances!

Celebrating Bongo Films, Bongo Sounds, Music and Performances!


From Friday 31st Dec 2010 to 2nd January 2011

Friday 31st Dec. Shows:

Films on the Big Screen:
This is it –Star: Steven Kanumba,
Hanifa Daudi, Othman Njaidi,
Huba – Star: Ahmed Olutu,
Natasha & Hashim Kambi,

Saturday 1st Jan Show:

Films on the Big Screen:
Don’t Cry – Star: Haji Adam
Divorce–Star:Vincent Kigosi,

Sunday 2nd Jan Show:

Films on the Big Screen:
Awards Night-Winning Film

Followed by:
Performances by: Tanzania House of Talents (THT)
Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amini, Barnabas, Ditto, Lina, THT Band and Dancers

Ticket Price:

Tsh 5000/- Local & Tsh 10,000/- Foreigner

In the Old Fort (Ngome Kongwe) from 7pm to 1am
kutoka www.filamucentral.co.tz na wasanii bora

kutoka www.filamucentral.co.tz na wasanii bora


HAWA NDIO BORA KWA 2010
Kwa kutambua mchango unaotolewa na wasanii wetu katika tasnia ya filamu mtandao huu umeguswa na kazi za wasanii hawa na kuwatambua kwa kuwatangaza kulingana zoezi tulilokuwa tunaliendesha la BORA ZA 2010, wadau hawa wamechaguliwa na wapenzi wa filamu hapa nchini ambao pia ni wapenzi filamucentral ambao kila siku wanatembelea mtandao huu kwa habari za filamu za Swahiliwood. Gonga HAPA kuona matokeo

Tunawapongeza wale wote walioshinda na kuibuka washindi katika nafasi walizoshiriki, kila aliyeingia katika mtanange huu alikuwa ni bora lakini siku ya siku tuliitaji mshindi mmoja ambaye ndiye tunamtngaza leo hii, tumefarijika sana kwa ushirikiano mlioonyesha wadau wa tasnia hii toka mwazo wa zoezi hili hadi mwisho, tunapenda kuwatambua waliotikisa mwaka 2010 na kusema Hongera.
BORA ZA 2010

1. Msanii chipukizi bora za 2010 – HANIFA DAUDI (Jenifer)
2. Muigizaji bora wa kike — YVONNE CHERRYL (Monalisa)
3. Muigizaji bora wa kiume — STEVEN KANUMBA (Kanumba The Great)
4. Mwandishi bora wa mswaada – ALI YAKUTI
5. Mchekeshaji bora – ATHUMAN MUSSA ( KING MWALUBADU)
6. Filamu yenye kava bora – DANGER ZONE
7. Mtayarishaji bora wa filamu – STEVEN KANUMBA
8. Kampuni bora ya utengenezaji filamu – RJ Company
9. Msambazaji bora – Game 1st Quality
10. Muongozaji bora – VICENT KIGOSI (Ray The Greatest)

Matokeo haya ni kwa mujibu wa watembeleaji wa mtandao

wa

http://www.filamucentral.co.tz
Wednesday, December 29, 2010
WAZIRI NAHODHA AIKUNA BASATA

WAZIRI NAHODHA AIKUNA BASATA


BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limegushwa na kauli ya Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mheshiwa Shamsi Vuai Nahodha ya kuzitaka idara za Serikali kutumia sanaa katika kutoa elimu kwa Umma.

Akizungumza Ofisini kwake Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego alisema, kauli hiyo inaonyesha wazi kwamba Waziri Nahodha anatambua umuhimu wa sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii na kwamba BASATA inamuunga mkono na kumpongeza sana kwa kuwa na mtazamo huo chanya kuhusu sanaa.

Waziri Nahodha hivi karibuni, alitoa agizo kwa idara za serikali kutumia sanaa kama njia ya kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi ili ujumbe uweze kuwafiki wananchi wengi hasa kwa kuwa wananchi wanapenda sana kuangalia vipindi vya sanaa kuliko vipindi vingine.

Kwa kauli hiyo ya Nahodha Ghonche amesema ni kauli inayofaa kuungwa mkono si kwa sababu amezungumzia masuala ya sanaa bali ni kwa sababu ameona umuhimu wa kutumia mbinu inayokubalika na kuaminiwa katika katika kufikisha ujumbe.

"Sanaa ni chombo chenye nguvu katika kufikisha ujumbe na inafahamika hivyo, sisi kama wadau wa masuala ya sanaa tunamshukuru sana Waziri Nahodha kwa kuliona hilo na kutoa wito kwa idara za Wizara yake kutumia sanaa katika kuwaelimisha wananchi juu ya masuala mbalimbali, kwa kweli tumefarijika sana kuona mtu ambaye si mwana sanaa anatambua hilo na kulisema hadharani," alisema Ghonche.

Amesema pamoja na kauli hiyo ya Waziri Nahodha ni vyema idara na asasi zingine zinazotaka kutumia sanaa katika kuelimisha jamii zikawatumia wasanii waliosajiliwa na BASATA na wenye vibali badala ya kutumia tu wasanii wasiotambuliwa.

"Katika kutekeleza hili ni vyema wakatumika wasanii ambao wamesajiliwa na wanatumbuliwa na BASATA ili kuepusha ubabaishaji," alisema Ghonche.
SOURCE:CAJA
Polisi wapewa baiskeli Dar

Polisi wapewa baiskeli Dar


Askari Polisi wakijaribu kuendesha sehemu ya baiskeli 100 zilizokabidhiwa na Kampuni ya Home Shopping Centre kwa Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu kwa ajili ya kusaidia doria Dar es Salaam leo.
Katika makabidhiano hayo, pia Askari waliofanya vizuri katika kazi pamoja na raia waliolisaidia jeshi hilo kwa misaada mbalimbali walitunukiwa sifa na zawadi mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, shamsi Vuai Nahodha.
SOURCE:POLISI
CHENGE ACHAGUA KULIPA FAINI KUKWEPA JELA

CHENGE ACHAGUA KULIPA FAINI KUKWEPA JELA


Andrew Chenge ambaye alishawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali na mara ya mwisho waziri wa miundo mbinu leo alipata nafasi ya kuchagua kati ya faini ya laki saba au jela miaka mitatu katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.
Hukumu hiyo ilikatwa na Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.
Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.
P-Square bado wapowapo tu

P-Square bado wapowapo tu


P-Square ni Mapacha wawili wa jimbo la Anambra nchini Nigeria wanaofanya vyema sana katika muziki wote wakiwa na digrii ya mawasiliano na biashara kutoka chuo kikuu cha Abuja.
Watu hawa wamekuwa na umaarufu mkubwa hasa baada ya kutoa albamu yao ya Get Squared.
Albamu hiyo imejikita Afrika na duniani na inafanya vyema sana.
Peter na nduguye Paul wamekuwa wakifanya vyema na hivi karibuni walishinda dola milioni 1 za Marekani katika tamasha la muziki la Kora la mwaka 2010.pamoja na umaarufu wao vijana hawa bado wanataka kuwa peke yao.
Genevieve Genevieve Nnaji

Genevieve Genevieve Nnaji


kama humjui ni Mdada mwenye mtoto mmoja. Pamoja na mafanikio makubwa ambayo wengi wa wasanii hawajayafikia, mdada huyu bado yuko singo.
Mtoto wake huyu alimpata akiwa sekondari lakini akabadilisha mfumo wa maisha na kuendelea na maisha katika tasnia ya sanaa na anafanya vyema.
Mwaka 2005, alipata tuzo ya African Movie Academy ya uigizaji bora katika nafasi ya kinara.
Alianza kuigiza akiwa na umri mdogo katika tamthilia Ripples wa miaka minane na kuingia Nollywood akiwa na miaka 19.
Ameshaigiza sinema zaidi ya 80 huko Nollywood na mmoja wa waigizaji wanaolipwa fedha nyingi sana.
Binti huyu pia ni mwimbaji na ameshatoa albamu ya Logologo mwaka 2004 na ameshafanya matangazo mengi ya kibiashara.
Mwaka 2004, alikuwa balozi wa Face of Lux ya Nigeria. Mwaka 2008,alianzisha laini yake ya mavazi kwa jina la St. Genevieve na akachaguliwa kuwakilisha vipodozi vya Face of MUD mwaka 2010.
Katika kipindi cha Oprah Winfrey Show, alitamkwa kama muigizaji bora wa kike kutoka bara la Afrika.
Pamoja na mambo mengi binti huyu anaonekana kukwepa kuwa na mwanamme .
Mapacha walioungana kusoma Jangwani

Mapacha walioungana kusoma Jangwani


WANAFUNZI wawili wakazi wa wilaya ya Makete ambao wameungana kiwiliwili watajiunga na shule ya sekondari ya Jangwani ya jijini Dar es Salaam baada ya kufaulu vizuri mtihani wakitaifa wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa hivi karibuni.
Wanafunzi hao Maria Mwakikuti na Consolata Mwakikuti wenye umri wa mika 13 kwa pamoja wamesema ndoto yao ni kuona wanakuwa wataalamu wa kompyuta waliobobea
Pichani Mapacha wawili walioungana kiwiliwili, Maria Mwakikuti (kushoto) na Consolata Mwakikuti (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Getrude Mpaka na wadau wengine katika hafla ya kuwapongeza kwa kufaulu mtihani wa darasa la saba.
SOURCE:Frank Leonard mwandishi wa Habarileo
Tuesday, December 28, 2010
Kikao cha kazi cha NHIF Morogoro

Kikao cha kazi cha NHIF MorogoroBaadhi ya Maofisa wa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , watatu kutoka kulia sambamba na watendaji wakuu wa Mfuko huo , mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kazi kwa maofisa hao Desemba 28, mwaka huu mjini hapa.
Katika mkutano huo zilivuja habari kwamba jamaa zangu wa mologolo wameamua wka makusudi mazima kuacha kuchukua fedha za tele kwa tele zinazotolewa na serikali kujazia mifuko ya afya ya jamii CHF.
Kutochukua kwao kumetokana na kutopelkeka taarifa za michango na maombi ya kujaziwa kwa fedha kutoka serikali kuu kupitia NHIF licha ya kuombw akufanya hivyo mara kwa mara. Wilaya yah morogoro iliyofanya hivyo ni Ulanga pekee.Sijui kama mkuu wa mkoa analijua hili hasa ukizingatia kwamba zahanati nyingi za morogoro mambo yake ndivyo sivyo.
Source: Mdau Morogoro
ENZI HIZO... katika juhudi za kuburudisha watoto maalumu

ENZI HIZO... katika juhudi za kuburudisha watoto maalumu‘…Unashangaa nini, ni hisia za kijana mwenye ulemavu wa mtindio wa ubongo , aliyetambuliwa kwa jina la Omari Sijali ( 18) wakiwatizama wenzake walikuwa wakisililiza na kufurahishwa na vijana ambao ni wazee wa siku hizi wakiigiza kupiga muziki na kuimba nyimbo za mwanamuziki mashuhuri Hayati Mbaraka Mwishehe zilizowika katika miaka ya sabini hadi sabini na tano , huku wakiwawamevalia suti za bulagoo na viatu vya raizoni ngazi nne, wakati wa hafla ya chakula kilichoandaliwa na Askofu Telesphory Mkude, wa Jimbo la Morogoro la Kanisa katoliki leo, iliyofanyika Uaskofuni, Kilakala (prokura)
Source: John nditi wa habarileo
Monday, December 27, 2010
Askofu Mkude asifu utulivu baada ya uchaguzi

Askofu Mkude asifu utulivu baada ya uchaguzi


KANISA Katoliki Jimbo la Morogoro, limewasifu Watanzania kwa kuonesha ukomavu wa kudumisha amani , umoja pamoja na utulivu mara baada ya kumalizika kwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu , mbali na kutolewa kwa madai mbalimbali ya kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa juu ya ‘uchakachiaji’ wa matokeo ya kura za urais, wabunge na madiwani.
Pamoja na kuwasifu Watanzania katika kudumia amani, umoja na utulivu, limewashauri viongozi wenye mamlaka Serikalini kuangalia kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu na pamoja na kuweka msukumo wa suala la mchakato wa kuudwa kwa katiba mpya.
Pongezi na rai hiyo zimetolewa na Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphory Mkude,(pichani) juzi Des 25 , wakati wa mahubiri yake kwenye misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrice , ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristu takribani miaka 2000 iliyopita.
Hivyo alisema Watanzania wameonesha ukomavu wa kisiasa baada ya kufanikwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu licha ya kasoro mbalimbali zilizojitokeza , ambapo baadhi ya viongozi wa vyama zilivyoshiriki uchaguzi huo kutoa madai mazito, kuwa kura zao zimechakachuliwa kitendo kilicholeta hofu kwa wananchi.

“ tumepita salama katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010…tunahaki ya kumshukuru mungu , taifa limebakia salama , amani, umoja na utulivu tofauti na nchi nyingine zilizofanya uchaguzi na zikajikuta zikingia kwenye migogoro kama tunavyoiona kwa wenzetu wa nchi ya Ivory Coast “ alisema Askofu Mkude
Hata hivyo pamoja na kusifu hali hiyo, Askofu Mkude, amewaomba viongozi wenye dhamana ya kudumisha umoja wa watanzania kutolifumbia suala la Katiba ambayo imeonekana kulalamikiwa na kada mbalimbali ili matakwa ya waliowengi yawezekupatiwa ufumbuzi wa kina.
“ Suala la Katiba inagaliwe upya , iangaliwe kwa msingi ya kuiwezesha Tanzania kuendelea kuwa nchi ya amani na utulivu na hayo yanafaa kuandaliwa mapema ili uchaguzi mkuu wa 2015 ufanyike ndani ya Katiba hiyo ili nchi iigie katika vurugu” alisema Askofu wa Jimbo hilo la Morogoro.

Kwa upande wa choko choko za Udini, Askofu Mkude amewashauri viongozi wanaolizungunzia jambo hilo ni vyema wakaliweka wazi ni maeno gani yenye udini badala ya kulizunguza ki ujumla bila kuyaainisha maeneo hayo moja kwa moja kama yanavyotamkwa.
“ hili naomba la udini viongozi wetu walitamke wazi bila uficho …kwa kuwa tunaona siku zote watanzania bila kubaguana dini zao wanapanda mabasi kwa pamoja …wanashirikiana kwa mengi …sasa tuambiwe udini upo wapi , uoneshwe kwa mifano badala ya ujumla wake “ alisisitiza Askofu huyo
Hata hivyo amewataka watanzania kuendelea kudumia umoja na utaifa wa nchi yao kwa lengo la kufanikisha maendeleo yao sambamba na kujenga upendo wa kuwasidia kwa kila hali watoto yatima wanaoishi maeneo mbalimbali kwenye jamii yetu.
Mdau Morogoro
Werema asema watu wasizungumze kibatabata kuhusu katiba

Werema asema watu wasizungumze kibatabata kuhusu katiba


Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Weremaame asema Katiba ni sheria mama na inapaswa kuheshimiwa kwa ajili ya maslahi ya umma.
Alisema mabadiliko yanayotakiwa lazima yazingatie matakwa ya umma lakini si kufanya matakwa ya mtu fulani na kuongeza kuwa hoja za katiba zinafaa kufikishwa katika meza na kuzungumzwa kwa pamoja.
“Kila mtu anazungumza kama bata, watu wanazungumza kibatabata, lazima tujiulize Watanzania wanataka nini? Wakati fulani iliwekwa vifungu vya haki za binadamu kuanzia kifungu cha 12 hadi 29 kwa kuwa vilihitajika, tuzungumze si kutishana,” alisisitiza Jaji Werema huku akitolea mfano Katiba ya India ya mwaka 1948 iliyofanyiwa marekebisho mara 50.
Hayo aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya Chande Othman Ikulu.
Alipoulizwa kutoa maoni yake kuhusu baadhi ya vyama vya siasa ‘kushikia bango’ suala hilo, Jaji Werema alisema vyama hivyo vina haki na vipo sahihi kufanya hivyo, lakini si kila kitu kilicho sahihi ni sawa au kinafaa kwa wakati husika, hivyo kilicho cha muhimu ni wananchi kuulizwa wanataka nini.
Pichani Jaji Werema(kushoto) akizungumza na waziri wa mambo ya ndani nahodha leo Ikulu.
jaji mkuu mpya aapishwa,mwingine alonga

jaji mkuu mpya aapishwa,mwingine alongaJaji Mkuu Chande Othman (58) ameapishwa leo na kusema kwamba atatoa kipaumbele katika kuleta hadhi ya mahakama za mwanzo na kuhakikisha kwamba mahakama inatekeleza wajibu wake ipasavyo kama sehemu ya mhimili wa dola.
Mahakama hizi ndizo zile ambazo akina yahe tunaenda huko na zinanuka rushwa kwelikweli kutokana ama mazingira mabaya ya kazi, jingo na hata wataalamu wenyewe katika mambo ya sheria.
Pamoja na kumshukuru jaji Mkuu mstaafu Agustino Ramadhani alisema kwamba anajua ana changamoto kubwa ya kuhakikisha kwamba mhimili huo wa dola unafanyakazi yake inavyotakiwa kwa kushirikiana na mihimili mingine.
“ Namshukuru mwenyezi Mungu kwa wema wake kwangu lakini pia Rais kwa kuniheshimu, namshukuru Jaji Mkuu Mstaafu (Augustino Ramadhani), amefanya mengi lakini pia watanzania kwa ujumla, nina kazi kubwa mbele…..
….kuongoza mahakama katika dira tuliyoiweka ya kwamba haki kwa wote na kesi kusikiliwa kwa wakati, ni wajibu wangu kufikia lengo hilo, kutatua migogoro inayoletwa mahakani tena kwa wakati,” alisema Jaji Othaman.
Jaji Othman ambaye ni Jaji wa tano mzalendo kushika wadhifa huo kati ya saba waliowahi kuwa Majaji Wakuu wa Tanzania alisema kuwa changamoto zipo nyingi na hawezi kusema atazimaliza lakini hadhi ya Mahakama hasa za Mwanzo ni jambo la msingi kwani hubeba sura ya mahakama kitaifa.
Kwa upande wake Jaji Mkuu Mstaafu, Ramadhani alisema amefurahia uteuzi huo kwani anahakika mafanikio yaliyofikiwa atayaendeleza ingawa hakusita kukiri kuwa changamoto bado ni nyingi kwa mhimili huo wa dola.
“ Mafanikio ni mengi na bila shaka atayaendeleza, miongoni mwayo ni kuimarisha uhusiano wa mihimili ya dola (Bunge, Serikali na Mahakama), ongezeko la majaji, kusimamia na kusambaza teknolojia ya kompyuta kwa haraka na kusimamia maslahi ya watumishi wa mahakama,” alisema Jaji Mkuu Mstaafu, Ramadhani.
Alipoulizwa ni changamoto gani kubwa anayoona mrithi wake atakabiliwa nayo, alisema zipo nyingi ila atamwambia yeye mwenyewe kwa kuwa zinamuhusu yeye na si vyombo vya habari ila alisisitiza wananchi kutojichukulia sheria mkononi bali kuiamini mahakama.
Jaji Othman alizaliwa mwaka 1952 na mbali na kushika wadhifa mbalimbali nje na ndani ya nchi, amekuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kwa miaka saba.
Picha ya kwanza ni kuapishwa kwa jaji na ya pili jaji mstaafu akizungumza na waandishi wa habari.
Saturday, December 25, 2010
Nakutakieni wanalibeneke christmass njema

Nakutakieni wanalibeneke christmass njemaLeo Ni Krismasi, siku ambayo binadamu wanakumbuka kuzaliwa kwa mwokozi miaka takribani zaidi ya elfu 2000 iliyopita. Alizaliwa kuwa daraja kati ya dunia na mbingu, alizaliwa kutupatanisha.Alizaliwa bethlehemu ya Uyahudi katika juma ambalo kaisari alikuwa anataka hesabu ya idadi ya watu.
Kwa wakatoliki leo ilikuwa Isaya, Waebrania na Luka naam ni raha iliyoje kuwa katika amani ya mwokozi na kuwa na uhakika na wokovu ni karaha iliyoje kugundua huna amani tena kwa sababu za kijinga.
Nawatakia wote Krismasi njema na yenye amani kubwa katika mioyo yenu na kuweni na kiasi katika sikukuu. Picha hizi ni ukumbusho tu wa amani na hiyo nyingine watu wakijipanga kuingia katika groto kanisa la Nativity huko Palestina.
no image

Mwanamuziki mkongwe wa Tabora Jazz afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe Rehani Juma amefariki dunia usiku wa kuamkia jana
alfajiri akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya mkoa ya Kitete, Tabora.
Taarifa kutoka jamaa wa karibu wa marehemu, Athumani Rehani zinasema
kuwa mwanamuziki huyo ambaye aliwika enzi za miaka ya 70 hadi 90
alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Athumani alisema kwamba mwanamuziki huyo alikufa katika hospitali ya
Kitete Tabora ambako alikimbizwa kwa matibabu siku tatu zilizopita.
Sababu za kifo bado kutolewa na madaktari waliomhudumia.
Kwa mujibu wa taarifa hizo mwanamuziki huyo ambaye alitamba sana na
kibao cha Jullie kilichopigwa na bendi ya watunjatanjata (washirika)
alizikwa jana hiyo kwao Tabora katika maeneo ya Chemchem, karibu na
shule ya sekondari ya Milambo.
Rehani ambaye anatoka katika familia ya wanamuziki kabla ya umauti
wake alikuwa akiendelea na shughuli za muziki mjini Tabora akipiga
rythimu na solo katika bendi ya Tabora Sound wanasensema Malunde.
Rehani ambaye ni mdogo wa marehemu Khalfan Juma aliyekuwa anapiga
gitaa la besi katika bendi ya western kwa muda mrefu kabla hajajiunga
na Tabora jazz ,pia alishawahi kupigia Paselepa na akina Marehemu
Msafiri Haroub ambao wote wametoka Tabora.
Tabora Sound sensema malunde inaundwa na wanamuziki wengi waliofanyia
kazi katika bendi ya Tabora Jazz na kwa sasa inaongozwa na Madaraka
Moris maarufu kama baba kiwembe ambaye pia alikuwa Munisa Ndesa, na
watunjatanjata.
Tabora Sound inamilikiwa na mwanamuziki mkongwe aliyekuwa Tabora jazz
iliyotamba katika miaka 1970 Salum Ruzira ambaye alikuwa anapiga besi
kama anapiga ngoma, kama utafuatilia kwa karibu wimbo wa dada remmy.
Makaribisho kwa utamaduni wa kwetu

Makaribisho kwa utamaduni wa kwetu


Malawi’s Foreign Minister Etta Banda(on her knees, right) welcomes in style, President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived in Blantyre for one day working visit yesterday. On the left is Malawi’s Minister of transport and public infrastructure. President Kikwete later held talks with President Bingu wa Mutharika of Malawi who is also the current chairman of African Union AU. The President returned to Dar es Salaam yesterday evening.
Thursday, December 23, 2010
ARusha poa.. UN yaanzisha mfumo wa kimataifa wa umaliziaji ICTR

ARusha poa.. UN yaanzisha mfumo wa kimataifa wa umaliziaji ICTR


Katika kutunza na kudumisha hadhi ya mahakama za kimataifa za mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR) na mauaji ya halaiki ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani ( ICTY), Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, limepitisha Azimio la kuanzisha Mfumo wa Kimataifa wa kushughulikia umaliziaji wa mashauri ya masalia ya Mahakama hizo mbili.
Wajumbe wa Baraza hilo wamepitisha azimio hilo lililopewa namba 1966 linaloeleza kwamba, mfumo huo wa kimataifa(International Residual Mechanism), utakuwa na matawi mawili yaani tawi la ICTR ambalo makao(seating) yake yatakuwa Arusha na tawi la ICTY ambalo makao yake yatakuwa The Hague, Uholanzi.
Azimio hilo limepitishwa siku ya jumatano kwa kupigiwa kura na wajumbe 15 wa Baraza la Usalama. Katika kura hiyo wajumbe 14 wameunga mkono na mjumbe mmoja hakufungamana na upande wowote.
Kwa tawi la ICTR Mfumo huo utaanza kazi Julai Mosi 2012 na kwa Tawi la ICTY Mfumo huo utaanza kazi Julai Mosi 2013. Mfumo huo wa Kimataifa wa kushughulikia mashauri ya masalia utakuwa na haki, stahili na wajibu kama ilivyo kwa mahakama hizo ambazo zinatarajiwa kukamilisha kazi zake zote si zaidi ya desemba 31 2014.
Kupitishwa kwa azimio hilo na kuanzishwa kwa mfumo huo, licha ya kwamba kunaziongezea muda mahakama hizo kukamilisha kazi zake, lakini pia kunahusisha suala zima la uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu zote muhimu zinazohusiana na shughuli zote za mahakama hizo za kimataifa.
Baraza Kuu la Usalama wa kupitia azimio hilo, limezitaka Mahakama hizo mbili kuweka mazingira mazuri ya kipindi cha mpito kuelekea kuanzishwa kwa mfumo huo wa kimataifa. Na pia kuhakikisha kwamba zinakamilisha kazi zake zote ifikapo desemba 31. 2014, ili kuruhusu mfumo huo kushughulikia mashauri ya masalia na kesi ambazo watuhumiwa kwake bado hawajapatikana.
Vile vile Baraza la limetoa wito kwa nchi zote kuhakikisha kwamba zinatoa ushirikiano madhubuti kwa Mahakama hizo katika kipindi chote cha kuelekea uhitimishaji wa kazi zake.
Ushirikiano huo ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa na wahalifu wote wanaosadikiwa kujificha katika nchi zao ili waweze kufikishwa mbele ya sheria.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza mara baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, wameeleza kuwa kupitishwa kwa azimio hilo ni moja yahatua muhimu sana si tu katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa wahutuhumiwa kufikishwa mbele ya sharia, lakini ni kielelezo tosha kwamba hakuna mhalifu ambaye yuko juu ya sheria.
Kukamilisha na hatimaye kupitishwa wa Azimio hilo kuna hitimisha mchakato na majadiliano ya muda mrefu, ndani ya Baraza Kuu la Usalama na Jumuia ya Kimataifa, kuhusu hatima ya Mahakama hizo za Kimataifa pamoja na uhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu zake baada ya kukamilisha kazi zake.
Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali ukiwamo Ubalozi wake katika Umoja wa Mataifa, na kama nchi ambayo ndiyo mweyeji wa Mahakama ya Rwanda iliendesha kampeni na kujenga hoja za nguvu za kutaka ifikiriwe kupewa stahili ya si tu kuhifadhi nyaraka na kumbumbuku za mahakama ya Rwanda bali pia kuwa tawi la kushughulikia ukamilishaji wa mashauri ya masalia ya Mahakama hiyo.
Source:Ubalozi wa Tanzania UN
Wednesday, December 22, 2010
ZIFF watengeneza dirisha dogo la hamasa

ZIFF watengeneza dirisha dogo la hamasa


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tamasha la filamu la kimataifa la Zanzibar (ZIFF) wameandaa tamasha dogo la filamu la siku tatu litakaloanza Desemba 31 mpaka Januari 2 mwakani katika mji Mkongwe nchini Zanzibar.
Tamasha hilo pamoja na kutengeneza hamu ya watu kutaka kuona sinema pia lina lengo la kutoa muamko wa Tamasha kubwa litakalofanyika Julai 2 mpaka 20, 2011. Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Mkurugenzi wa ZIFF Martin Mhando alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha filamu za Kitanzania pekee.
Mhando alisema kuwa katika onesho hilo filamu sita za Kitanzania zitaoneshwa ambapo mbili bora zitakazochaguliwa zitaoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika liitwalo FESPACO litakalofanyika nchini Burkina Faso.
Filamu hizo ni Divorce,This is it, Briefcase, Best wife,Nani,Huba, Black Sunday na Don’t Cry. Filamu hizo ni kutoka kwa wasambazaji Steps na Pilipili.
Alisema kuwa katika tamasha hilo litakalofanyika Ngome Kongwe litasindikizwa na burudani kabambe ya muziki kutoka kwa kundi la Tanzania House of Talent (THT) litakalofanya maonesho kwa siku zote tatu. Wengine wanaochanja mbuga katika medani ya muziki watakaoshiriki nmwasiti, Marlaw, mataluma, Amin, barnaba, Pipi na wengine.
Alisema kuwa ZIFF imepata mafanikio katika anga za kimataifa ambapo Desemba 3 mpaka 5 ilionesha filamu zake mjini Potsdam nchini Ujerumani ambapo mtengeneza filamu Sajani Srivastava alionesha filamu yake ya Nani. Pia ZIFF ilionesha filamu zake katika tamasha la Trinidad and Tobago na pia linatarajia kuonesha filamu zake jijini New York nchini Marekani katika African Art Museum. Wakali wengi wa sinema akiwamo Mlela na Baby madaha walikuwapo katika mkutano huo na waandishi wa habari.Pichani niZIFF Direkta Dk Martin Mhando akizungumza maelezo leo asubuhi.
TID kuizindua Sifai Desemba 28

TID kuizindua Sifai Desemba 28


KHALID MOHAMED al maarufu kama Top In Dar (TID) akishirikiana na bendi yake ya TOPBAND wanatarajia kufunika Club Bilicanas wakati watakapofanya uzinduzi wa albamu yao ya Sifai Desemba 28 mwaka huu.

Katika uzinduzi huo ambao atasindikizwa na Lady Jay dee, sam wa ukweli, magwair, Jay More na wengi wengine uchakavu utakuwa sh 7000 tu na shughuli itaanza saa tatu usiku hadi majogoo.
Msiba kwa akina Ras Makunja huko Rufiji

Msiba kwa akina Ras Makunja huko Rufiji


Marehem Hassan Jumanne Makunja
Amezaliwa 4-03-1964 amefariki 19-Dec-2010

Marehem Hassan Jumanne Makunja ni mdogo wake Ras makunja.
Late Hassan Makunja amefariki dunia uko Utete,Rufiji,mkoani Pwani
siku ya 19.December 2010 na kuzikwa 20.12.2010.
Marehem Hassan Makunja alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo,
alikwenda mjini utete,Rufiji kwa mapuziko na kumtembela mama yake mzazi,
Ndipo umauti ukamkuta .
Familia ya marehem inasikitika kuwajulisha jamaa na marafiki taarifa hii ya msiba wa Ndugu Hassan Jumanne Makunja,kuwa hatunaye tena.
Rambi rambi wasiliana namba hii 0787532929 au 0718893419, Bi.Ummy Makunja
Tuesday, December 21, 2010
Kumbe inawezekana kutoichezea serikali ha Mhh

Kumbe inawezekana kutoichezea serikali ha MhhTingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam, leo usiku lilivunja maeneo ambayo yamejengwa kinyume cha utaratibu katika maeneo ambayo inaaminika kuwa ni ya wazi au hayaruhusiwi kujengwa.Hapa ni kiwanja kilichopo karibu na Hoteli ya Palm Beach.
Ukuta mwingine uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan katika Barabara ya Ocean Road, ulivunjwa pia na askari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Source:Mohamed Musa
no image

BAE pays fine to settle Tanzania corruption probe

KAMPUNI kubwa ya ulinzi ya Ulaya,BAE Systems, inandaa namna ya kuilipa serikali ya Tanzania fidia ya shilingi bilioni 67.29 (paundi milioni 30) baada ya kesi yake kumalizika leo.
Malipo hayo yanatokana na sharti la kwanza la makubaliano kati ya kampuni hiyo n a Taasisi ya Kuchunguza Makosa makubwa ya jinai ya Uingereza, SFO.
Kauli hiyo imetolewa baada ya kampuni hiyo kuhukumiwa kulipa faini ya Paundi 500,000 au Dola za Marekani 775,000, sawa na shilingi bilioni 1.12 baada ya kukiri kosa la ‘kushindwa kuweka kwa usahihi kumbukumbu za manunuzi.’
Mpango wa ununuzi wa rada kwa ajili ya Tanzania ulikuwa na thamani ya dola milioni 40 sawa na paundi milioni 28.
Mahakama ilitoa hukumu hiyo kwa kuzingatia shauri la kutoweka taarifa vyema. Suala la kutoa mlungula halikufikishwa ambalo awali lilitawala uchunguzi wa SFO halikufikishwa mahakamani.
Jaji David Bean alisema itakuwa ni kuukataa ukweli kufikiri kuwa wakala wa BAE nchini Tanzania, Shailesh Vithlani, alilipwa mamilioni ya dola eti kwa sababu tu anajua kuunganisha vyema masuala ya biashara.
BAE ilikubali kwamba inawezekana kwamba sehemu ya dola milioni 12.4 (waliyomlipa Vithlani) ilitumika kwa ajili kuisaidia kupata zabuni hiyo.
Hata hivyo waendesha mashtaka wamesema kwamba ni vigumu sana kuweza kujua Vithlani alifanya nini na fedha hizo na wala hawakuiwakilisha kwamba sehemu ya fedha hizo zilitumika vibaya.

Kampuni ya BAE imesema kwamba imefurahishwa na shauri hilo kumalizwa na kwamba inaandaa utaratibu wa kuilipa Tanzania fedha zake.

endelea na chiinglish


The fine brings to end a proces started in February, when BAE agreed to plead guilty to "breaching its duty to keep accounting records" for the radar deal in Tanzania.
BAE also agreed at the time to pay a $400m fine to the US, after admitting to "defrauding the US" over the sale of fighter planes to Saudi Arabia and Eastern Europe."
As a result, the SFO and US Department of Justice ended their investigations into bribery and corruption by BAE.
Yesterday, the High Court judge presiding over the the settlement questioned the evidence and terms of the SFO's plea bargain with BAE.
Mr Justice Bean threatened to call a halt to the sentencing of BAE, questioning whether he could continue on the basis of the facts before him. Although he continued with the sentencing it was not before tearing into the evidence presented by the prosecution.
"My overriding feeling is that you cannot sentence with this evidence," Mr Justice Bean said. "The proposition that the Crown cannot prove to criminal standard that corrupt payments were made is one thing. To say that those payments were not properly used is another.
"There is a big gap."
The SFO's deal with BAE involved the company paying a £30m fine after pleading guilty to failing to keep proper accounting records. The accounting records relate to $12.4m paid to a "marketing agent" in Tanzania, Shailesh Vithlani, to facilitate an air traffic control deal with the country.
Fedha hizo zililipwa kwa makampuni ya Vithlani ya British Virgin Islands na kampuni ya Merlin iliyosajiliwa Tanzania.
The court heard covert agents were hired by BAE in a number of circumstances; when it was illegal to employ them overtly; because of tax implications arising from the agent making undeclared payments to third parties; or to avoid "embarrassment and press interest" due to large fees being paid.
The normal limit on payments to covert agents was 20pc of the price of a contract. Because Mr Vithlani's fee was 30pc it was personally authorised by BAE's then chairman Sir Richard Evans.
Mr Justice Bean also questioned the terms of a widespread indemnity agreed between BAE and the SFO to preclude certain further prosecutions relating to the case.
Through cases such as BAE and earlier this year, Innospec and Robert Dougall, the SFO has tried to establish a precedent for plea bargaining in UK law.
In the Dougall corruption case, Judge Bean, the same judge sitting in the BAE case, turned an agreed suspended sentence into a prison term.
A £12.7m fine agreed with chemical company Innospec was branded "inadequate".
no image

Katiba mpya?polepole Jamani

ANGALIZO:

Katika gazeti la leo la Habarileo ambalo ndilo ninalofanyia kazi niliandika wazo langu. Limesomwa na watu si haba. Kuna vitu watu hukasirika wakisoma mawazo mengine. Lakini pia kuna watu wanaokasirika wakiulizwa maswali. Kuna hoja nyingi ambazo zingine zilitumwa katika simu yangu binafsi.Si mbaya nikasema haya yafuatayo baada ya wewe kuisoma habari yenyewe.
LukwanguleKatiba Mpya polepole jamani

UKIFUNGUA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 katika utangulizi wake unaona misingi ya Katiba na katika misingi hiyo unakutana na sababu kwanini tuna Katiba.

Pamoja na sababu hiyo pia inaelezwa kuwa Katiba iliandikwa na watu ikapitishwa katika Bunge na kisha kuanza kutumika kwa manufaa ya watu wa taifa hili na nchi kwa ujumla wake.

Nchi bila Katiba itakuwa nchi yenye ufisadi wa aina yake na hii inaweza kuleta mushkeri mkubwa kwa binadamu.

Kwa sasa kuna maneno, kelele na mazungumzo yanayoendelea miongoni mwa watu waliobahatika kujua maana ya Katiba na hatima ya mazungumzo yao mara zote wanataka
Katiba mpya na wanatushawishi wengine kwamba bila Katiba mpya hakutakuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Naam, kwa Katiba hii hii tumepata uongozi wa kisiasa, kwa Katiba hii hii tuna mhimili wa Bunge na Mahakama na uongozi na kwa Katiba hii hii inayochanwa na kusimangwa
tunakuwa na demokrasia mpya.

Unapofungua Katiba na kukutana na maneno yafuatayo (nanukuu): KWAKUWASISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani: Tuendelee.

Katika mijadala inayoendelea hakuna hata mtu mmoja anayesema katika maelfu ya maneno
yaliyomo katika Katiba wapi pana tatizo na panahitaji kubadilishwa, mazungumzo na kelele ni kwamba Katiba hiyo imepigwa viraka 14 inastahili kufumuliwa na kuundwa upya.

Pia inazungumzia ujamaa ambao hatuufuati. Hili lahitaji majadiliano zaidi. Sina sababu ya kusoma alama za nyakati, kwani huona hizi alama zinapoteza watu mawazo ya kusonga
mbele na ukweli huo unazingatia mabishano ya sasa kwamba mwisho wa kuinjilisha ni mwaka
wa kesho na mwaka wa kesho kutwa Mei 21 Mungu anamaliza hesabu zake.

Mimi ni Mkatoliki nakumbuka ipo sehemu alipoulizwa Yesu mwisho wa dunia alisema ni baba
pekee anayejua siri hiyo lakini makubwa yatapita duniani kabla ya neno hilo kutimia.

Na kutokana na hilo wazo la kusoma alama za nyakati kuhusiana na Katiba huwa naliona kama ni jepesi sana.

Watu wanaozungumza suala la Katiba iliyoundwa na wachache wanaojua namna ya kuendesha nchi wakaipitisha katika Bunge, nalo ni wachache wenye dhamana ya kutunga sheria na kisha kufanyiwa kazi, lakini sasa wanataka Katiba mpya ya kuuliza kila mtu.

Naam, inawezekana kabisa. Lakini swali langu la msingi ambalo nataka kila mtu alifikirie ni hii
Katiba inayotoa nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu haja ya kuwa na Katiba mpya inajulikana kweli kwa watu?

Nauliza hivi kwa sababu itakapokuja hiyo drafti mpya tunaweza kujua tatizo lilikuwa wapi hasa katika kazi iliyopita? Mimi naona watu ni wa binafsi mno na wanataka kuendesha nchi katika
umri wa binadamu , hili haliwezekani, twendeni polepole ni mustakabali wa taifa na lazima kila mtu ajue nini kipo katika Katiba ya zamani, kasoro zake na kwanini ni lazima kuwa na Katiba mpya.

Kwa sababu nchi ni zaidi ya miaka 70 na ishirini ya kuazimwa na Mungu aliyonayo binadamu, inahitaji kwenda kwa mtindo kama wa jeshi kubwa katika kuwania kipito kidogo.

Katiba inaweka michoro muhimu ya maisha na kanuni na huwezi kudharau hilo kwani linaweza likatafsiriwa vibaya. Kama hali ni hiyo kama tunajadili juu juu tu ni sawa na kuona
kaburi zuri nje ndani kuna uvundo.

Pengine huo ni msimamo mbaya lakini kiukweli niseme kinachobaki katika Katiba ni muonekano unaoweza ama kukozwa au kuchushwa kwa kuzingatia mawazo ya kundi linalotaka mamlaka au linalotawala kwa wakati huo, na bila shaka tunaotaka Katiba mpya tu wapi na tuna sababu gani nje ya hii niliyoigusia.

Manake sehemu kubwa ya Katiba haifundishwi na wala vipengele vyake havijulikani vyema nini kanuni si ya msingi na itifaki za kimataifa tulizoridhia.

Kutokana na hoja yangu hapo juu napenda kuwauliza watu wanaotaka katiba , hivi ni kweli wanataka kuandikwa upya kwa Katiba au wana lao jambo? Nasema hivi kwa sababu nyingine kubwa kama hatujaaminiana.

Narejea tena hivi ni kweli tunataka katiba, nani anajua katiba ya zamani atatoa na mfano na kusema kutokana na ubaya wa Katiba hii hapa na pale na huko ni lazima kudai Katiba mpya, sivyo mimi naona kama Watanzania tunahemea juu juu kama mpira baharini, tumepigwa pampu.

Naam kwenye Biblia Waisrael walitaka kuwa kama wengine, wakataka watawala, Mungu akawapa kilichofuata nadhani walijuta, lakini wamekuwa kama wengine.

Huo ndio ukweli wa dunia ulio mchachu. Pamoja na ukweli kuwa tunahitaji katiba bado nadhani si sahihi kutuvurumisha Watanzania katika wimbo tusiouelewa; tueleweshane kwanza,
manake hiki ni kitu kikubwa na hakika tusipoeleweshana tunaweza kwenda msobemsobe halafu ikawa kiama hapa, bila taarifa ya haraka.
mwisho

HOJA ZA WATU

mwenye namba+255683019370 aliandika hivi...: Niseme moja kwa moja. kwanini uandike jambo ambalo hulifahamu na kutusumbua wapenzi wa habarileo?Soma mwenyewe wazo hableo ya tarehe 21/12 kuhusu katiba... unataka tufahamu au unaelewesha jamii kitu gani? nakuomba uiandike upya.Habarileo nalipenda... mwisho wa kunukuu.

mwingine aliandika hivi:

Katiba mpya?... Polepole jamani!
Name: DATUS MAHENDEKA
Email: datusmahendeka@yahoo.com
Date sent: 21st December 2010 @ 07:20
Comment: Una mawazo mazuri lakini Katiba Mpya inahitajika ndio maana viongozi waliopita na Mh. Pinda ameliona hilo.na huyu naye

Katiba mpya?... Polepole jamani!
Name: joseph mwita
Email: terrell_bibbs@yahoo.com
Date sent: 21st December 2010 @ 04:05
Comment: Katiba mpya ni lazima,mwandishi sio kwa sababu unaandikia gazeti la siri kali ndio unataka kujikomba kwake. Wananchi tunataka katiba ambayo itapunguza mamlaka ya raisi,tume ya uchaguzi huru na mwananchi wa kawaida awe na uwezo wakuwachagua kwa kura viongozi wengi kuanzia watu kama wakuu wa mikoa. Wananchi wakitaka kitu hakuna kitu cha kuwazuia na wakati ni huu.

Hoja yangu:

Sikuandika ili kuma mtu yoyote pozi. nawakumbusha haja ya wananchi kuelewa ili kuwa na mchango mkubwa katika katiba na suala si haraka kwa sababu wewe unalifahamu. Asilimia 80 ya watu wa nchi hii wanategemea kilimo kujilisha na kusomesha watoto wao, ukilifahamu hilo, kifalsafa tu manake tuna watu wengi wasiojua mambo fulani yanayohusu maisha yao ndani ya jamii.wako katika jembe la mkono na dhiki yao kubwa ni chakula na wapi pa kupata vijisenti wanavyoporwa na wajanja kwa kuwapoa kima ksiichohalali kwa nguvu zao.
sasa ukiwa na watu wa aina hiyo ambayo hata maana na msingi wa katiba hawajui ni vyema kwanza ukafanya kazi ya kuwaelimisha. Zipo NGO nyingi zinazosema kwamba kazi yao ni kuelimisha jamii kuhusu mustakabali wao, lakini hawafanyi.
Mimi nataka mtu anieleze kwa kuanzia kwake mwenyewe, kama si baba yake, mkewe au mume wake kama si mjomba na shangazi yake mtoto wake wa kiume au wa kike kama kweli wanafahamu katiba tuanzie na hiyo iliyopigwa misele ya mwaka 1977.
Tuangalie katiba ya mwaka 1965 na tuangalie katiba ya mwanzo kabisa tuseme ya tanganyika ambayo ilikomba mpaka sheria ya kutozwa sh 100 kama unakutwa karibu na nyumba ya kulala wageni, sheria ambayo mpaka leo haijaondolewa wala kufanyiwa marekebisho.
Mimi si kwa sababu nafanyakazi serikalini ninajikomba, au mtu anadhani kwamba sifikiri, unatembea nchi hii unawauliza watuj maswali ya msingi kabisa kuhusu maisha yao hawajui cha kujibu, wanadhani kwamba serikali ndio mama na ndio baba yao na chama wanachokiamini hakifanyi makosa na viongozi wanawaamini hawafanyi makosa ndio wakombozi wao.
Kazi kubwa ya waandishi ni kuelimisha na kuwakumbusha watu, nimefanyakazi yangu si ya kupinga katiba bali binadamu lazima watengeneze subira katika kila hatua kubwa katika maisha ya nchi yao, itafika wakati suala linarejea kwa wananchi kwa usahihi, watasema nini kuhusu ukweli wa katiba kama wao wenyewe hawajui?
Madaraka ya Rais lazima yapunguzwe sawa tukiyapunguza tunayapeleka wapi na kiasi gani tumbakishie. Tunataka kuchagua viongozi wetu wa mikoa sisi wenyewe, kanuni zipi na aina gani ya demokrasia tunaifanya.
Tunataka haki za binadamu kwa kiwango gani na wapi mipaka . kama mimi nataka kutembea uchi kwanini unikataze , si unakataza haki yangu ya msingi.
Kuna mambo mengi yanayotakiwa kuangaliwa katika katiba si suala la kukurupuka na ili watu wawe na upeo mpana wa kuchangia ni lazima kwanza wajue nini maana ya katiba, kuangalia wenzao wamefanya nini, kuna marekebisho gani yanatakiwa na wapi ni mipaka na kwanini mashoga wasiwe sehemu ya katiba na kila mtu akafanya lake. Nini utamaduni wetu katika hili kwa sababu sisi si kisiwa lakini pia si wapuuzi.
Hilo ndilo hasa nililotaka kuwakumbusha watu. Ukiwa na hasira huwezi kuliona hili na kama hujawahi kukaa na kuongoza watu katika misukosuko hakika huwezi kuwa na busara kwa sababu wewe unataka leo kumbe unatakiwa kuangalia kasi ya mabadiliko ya mambo duniani, kuhami yale mazuri na kuhakikisha kwamba watu hawapotoki kwa kuwa na tafsiri finyu ya uhuru wao ndani ya katiba.
Labda hili linaweza kueleweka.
Tumeenda shule kwa sababu hizi hizi kuangalia wka kina masuala mazito yanayohusu jamii kwa kuishirikisha vyema lakini si kuwaburuza.
naitwa Beda Msimbe kutoka juu ya milima ya Uluguru, upande wa Magharibi wa Lukwangule.
Monday, December 20, 2010
Friday, December 17, 2010
Waziri Mkuu Pinda akubali katiba mpya

Waziri Mkuu Pinda akubali katiba mpya


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda leo amesema serikali haina kigugumizi wala kuona ugumu katika mjadala unaoendelea sasa nchini kuhusu Katiba mpya na atamshauri Rais Jakaya Kikwete namna ya kushughulikia madai hayo.
Aidha, amesema mchakato wa kuwapatia Waislamu Mahakama ya Kadhi, lakini kwa kuzingatia utaratibu utakaofaa bila kuathiri sheria zilizopo, unaendelea na siyo kwamba suala hilo limeshapatiwa ufumbuzi.
Amesema atamshauri Rais Kikwete kuhusu namna bora ya kushughulikia madai ya Katiba mpya, huku msimamo wake ukiwa ni kuundwa kwa jopo la watalaamu kutoka kada zote za maisha au kuwashirikisha wananchi wenyewe katika kueleza nini kifanyike kuhusu Katiba mpya.
Mbele ya wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake Magogoni, Dar es Salaam Waziri Mkuu alikiri kuwapo kwa mjadala mkali unaoendelea kuhusu Katiba mpya, lakini akasema si vyema kuona kuwa madai hayo si ya msingi, hivyo ni vyema kuheshimu mawazo ya watu wanayoyatoa.
Pichani Waziri mkuu akizungumza na wahariri ofisini kwake.
Source:Habarileo
Toleo jipya la noti ni kiboko kwa usalama

Toleo jipya la noti ni kiboko kwa usalama


Benki Kuu ya Tanzania leo imetangaza kutoa toleo jipya la noti ya sh 500,1000,2000, 5000 na 10000. Noti hizo zitaingia katika mzunguko Januari Mosi mwakani na zitaenda sambamba na noti zilizopo sasa.
Gavana wa Benki hiyo Prof.Benno Ndullu amesema wakati akizindua noti hizo kwamba noti za zamani zitaendelea kutumika mpaka zitakapomalizika zenyewe katika mzunguko na
wananchi wazipokee na kuzitumia.
Amesema pia hakutakuwapo na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa noti mpya.Katika maelezo yake amesema kwamba toleo hilo jipya lina taswira inayozingatia maendeleo ya uchumi na Jamii ya Tanzania.
Alisema kuna ambadiliko kidogo katika toleo jipya ambapo waasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani karume wamewekwa katika toleo jipya.Nyerere anaonekana katika noti ya shilingi elfu moja na Karume katika noti ya sh 500. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, tano na kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama.
Hata hivyo kutokana na kupungua kwa ukubwa wa noti wameweka vichwa wanyama badala ya wanyama wazima kama ilivyo katika noti za zamani.
katika kupambana na wale wanaotengeneza noti bandia na kuongeza uhai wa fedha hizi katika mzunguko kabla ya kuchakaa toleo jipya limeongezwa ubora kw akuwekwa alama maalumu mpya za usalama na kutumia taaluma mpya kuziimarisha.
kwa mara ya kwanza kumewekwa pia alama nyingine ya usalama alama ya motion ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho.
gavana amewataka wananchi kufuata maelekezo ya alama z ausalama za noti hizo na kwamba wataendelea kutoa elimu na pia watuw anaweza kufuatia taarifa hizo katika mtandao wa komyuta:www.bot-tz.org
Pichani gavana wa bot akionesha sampuli za noti hizo katika bango
Thursday, December 16, 2010
Maelfu wamsindikiza Dk Remmy katika safari yake ya mwisho

Maelfu wamsindikiza Dk Remmy katika safari yake ya mwisho

MMOJA wa wanamuziki ambaye alikuwa na mashairi na maudhui ambayo hayababaishi katika muziki wake Ongala Mungamba Ramazani Mtoro maarufu kama Dk Remmy Ongala amezikwa leo katika makaburi ya Sinza karibu kabisa na makazi yake.
Kwa umati ulioshiriki katika maziko ni wazi ilikuwa lazima kuaga kufanyikia viwanja vya Biafra kutokana na Makazi yake hayo ambayo ndiyo yametoa jina la kituo cha Sinza kwa Remmy kutokidhi haja.
Dk Remmy aliyezaliwa Februari 1947 alikufa kutokana Jumapili iliyopita kutokana na matatizo ya kisukari na kiharusi.
Watu mbalimbali wa kada anuia walifika kumuaga na kumzika mwanamuziki huyo ambaye miziki yake katika kuhimiza kujikinga na ukimwi na maisha ya watu maskini ilikuwa inasisimua mwili na maungo.
Baadhi ya watu mashuhuri waliokuwapo ukiachia wanamuziki maswaiba na wasanii wenhine ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi, Mbunge wa Ubungo John Mnyika, Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan.
Akitoa salamu za serikali Waziri Nchimbi alisema kuwa mchango wa Remmy hautosahaulika kwa kutokana na aina ya ujumbe aliokuwa akiimba.
Alisema kuwa ujumbe wa Remmy uliendana na wakati na masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijitokeza serikalini.
Alisema kuwa Remmy atakumbukwa kwa mchango wake katika masuala mbalimbali muhimu kama vile kuhamasisha vita dhidi ya umaskini, magonjwa na kuzungumzia masuala ya kijamii.
Hoja hizo pia ziliungwa mkono na mwanamuziki Cosmas Chidumule ambae pia aliwataka wanamuziki kuiga mfano wa Remmy katika kutunga nyimbo zenye ujumbe.
Alisema kuwa Remmy hakuwa na majivuno kama wasanii wengine wa sasa ambao hujisahau majukumu yao katika jamii na kuanza kuimba nyimbo zisizofaa.
“ Sio wanamuziki wa nyimbo za kisasa au za dansi tu ila hata wanamuziki wa Injili nao wanatakuwa kujifunza kitu kutoka kwa Remmy, Remmy hakuwa na majivuno hakuwa na muda wa kupoteza kazini aliheshimu wapenzi wa muziki wake” alisema Chidumule.
Naye askofu wa kanisa la Pentekoste David Mwasoko alimwagia sifa marehemu Remmy kuwa alikuwa mwanamuziki mwenye wito na kipaji cha ajabu katika muziki aliyekitumia kipaji chake kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Alisema kuwa Remmy aliamua kukata rasta zake ili kutumia muda wake kumtukuza Mungu kitendo ambacho ni baraka kubwa kwa msanii huyo.
Wanamuziki wa Injili walikuwapo katika viwanja hivyo na waliimba nyimbo kadhaa za dini ya kikristo za kumtukuza Mungu huku wengine wakiimba nyimbo za zamani za Remmy.
Bwana alitoa zawadi, bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe RIP Ramazani Ongala
MAKATIBU TAWALA WAAPISHWA IKULU

MAKATIBU TAWALA WAAPISHWA IKULU


Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha makatibu tawala wapya wa mikoa sita katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Makatibu Tawala hao wapya walioapa leo mbele ya Rais ni pamoja na Bi.Evelyne Philbert Itanisa wa mkoa wa Arusha, Benedict Ole Kuyan wa Mkoa wa Tanga,Mgeni Sufiani Baruani wa Mkoa wa Morogoro na Liana Ayoub Hassan wa Singida.
Wengine ni Nassor Mohamed Mnambila wa Kagera na Kudra Juma Mwinyimvua wa Tabora.Pichani Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Arusha Bi.Evelyne Philbert Itanisa akikabidhiwa nyenzo baada ya kula kiapo mbele ya Rais Dr.Jakaya Kikwete
SOURCE: Freddy Maro.
Chuo cha muziki cha DCMA na Urithi Concert

Chuo cha muziki cha DCMA na Urithi Concert


Chuo cha Muziki cha Zanzibar, Dhow Countries Music Academy (DCMA), kitafanya onesho la muziki Ijumaa tarehe 17 Disemba 2010 kusherehekea mafanikio ya mwaka wa mazomo.

Chuo kitashirikiana na wahisani wa makampuni ya Vodacom, Mnarani Beach Cottages na Zanair, kufanikisha onesho la muziki la aina yake kwa ajili ya kusherekea mafanikio ya Chuo katika mwaka 2010.

Onesho hilo, ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka na kujulikana kwa jina la URITHI CONCERT litafanyika katika kiwanja cha Muembe Kisonge, Michenzani mjini Zanzibar.

Mratibu wa onesho hilo, Mahsin Basalama, amewaahidi wapenzi wa muziki mjini hapa burdani mwanana kutoka kwa makundi mbali mbali ya Chuo ikiwemo Taarab, Ngoma za kiasili, Kidumbaki, Muziki wa Dansi pamoja na Jazz.

Katika wasanii mashuhuri watakaotumbuiza ni pamoja na mpigaji Kidumbaki maarufu Makame Faki pamoja na wengine wengi. Onesho hilo litaanza saa mbili usiku na kutegemewa kufurika kwa wapenzi wa muziki kutoka sehemu mbali mbali za kisiwa cha Unguja.

Chuo cha DCMA kimekuwa kikiandaa Onesho la Urithi kila mwaka kwa dhamira ya kuyawasilisha mafanikio ya Chuo kwa jamii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwavutia vijana kufanya maamuzi ya kujifunza muziki kupitia kozi zinazotolewa hapo Chuoni.

DCMA ni taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) inayoendesha mafunzo ya muziki yenye kuweka msisitizo katika ufundishaji wa muziki wa ala za muziki wa kimatuduni.

Source:Kheri A. Yussuf
Development, Marketing & PR Manager
Dhow Countries Music Academy, Zanzibar
Mobile: 077.362 0202
no image

The gentlemen keeps on nagging

Tired of getting low amounts of useless traffic to your website? Well i wish to tell you about a new underground tactic that makes me personally $900 each day on 100% AUTOPILOT.
I could truthfully be here all day and going into detail but why dont you merely check their website out? There is a great video that explains everything. So if your serious about making hassle-free money this is the website for you. Auto Traffic Avalanche
Wednesday, December 15, 2010
KUNA MAMBO MAKUBWA LUSAKA

KUNA MAMBO MAKUBWA LUSAKA


PRESIDENT Jakaya Kikwete has led Tanzanian delegation in deliberation and consequent adoption of Lusaka Declaration in fighting illegal exploitation of natural resources in the Great Lakes Region.
The president arrived at Lusaka Internal Airport (LIA) on Tuesday evening to attend the special summit on the Fight against illegal exploitation of natural resources, organized by the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR).
Mr. Kikwete was among six heads of states that attended the summit and approved six tools developed with a view to curbing illegal exploitation of natural resources. Such tools are regional certification mechanism, harmonization of national legislation, regional database on mineral flaws, formalization of the artisanal mining sector, promotion of the extractive industry transparency initiative and whistle blowing mechanism.
The summit was preceded by a secretariat and a committee of ministers meeting, of which Tanzania was represented by Deputy Minister for Energy and Natural Resources and his counterpart in Foreign Affairs and International Relations docket, Mr Mahadhi J. Maalim.
The summit was officially opened today at the Intercontinental Hotel by Zambian President, Rupiah Banda, who among other things, paid tribute to the outgoing Executive Secretary of ICGLR, Ambassador Liberata Mulamula for her exemplary leadership.

Pichani Some Heads of State and delegates attending a Special Summit on The Fight of Illegal Exploitation of Natural Resources in Lusaka Zambia, front row, from left to Right Deputy Chairperson of African Union Commission(AUC) Erastus Mwencha, UN Deputy Executive Secretary Dr.Asha Rose Migiro, Namibia’s President Hifikepunye Pohamba, President Dr.Jakaya Kikwete, the host Zambia’s President Rupiah Banda, DRC President Joseph Kabila, Angolan Prime Minister, Republic of Congo’s President Denis Sassou Nguesso and Burundi’s President Pierre Nkurunzinza
SOURCE photo by Freddy Maro.
NEW XMAS TREAT MAIL

NEW XMAS TREAT MAIL


Uongozi na WAfanyakazi wa Paradise All suites hotel kwa kushirikiana na Angella Bondo Show (kipindi kilichopewa msukumo na kipindi cha Oprah Winfrey) wanawakaribisha katika “Christmas brunch” (mlo unaojumuisho wa asubuhi na mchana) itakayofanyika Jumamosi tarehe 18,Desema 2010.

Restaurant Manager wa hoteli hiyo Bw. Anold Lema amesema kuwa siku hiyo itakuwa mahsusi ya kuwafurahisha tuwapendao hivyo ni siku itakayokuwa na mambo mbalimbali ikiwemo michezo kati ya kina mama, kina dada, marafiki na binti zao. Michezo hii itawasaidia kina mama hawa kutumia muda huo kukaa na kufurahi na wale wawapendao katika msimu huu wa sikukuu.

Tiketi za kiingilio tayari zimeanza kuuzwa sehemu mbali mbali jijini, hoteli ya Paradise iliyopo katika jingo la Benjamin Mkapa katikati ya jiji na Chicken Hut Mlimani City. Tunawakaribisha wote kujumuika nasi katika sherehe hii.

Ticketi zinauzwa Tsh 30,000 kwa mtu mmoja.
Kenya mambo yameiva...Uhuru Kenyatta mtuhumiwa  namba moja ICC

Kenya mambo yameiva...Uhuru Kenyatta mtuhumiwa namba moja ICC


MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) leo imemtaja Waziri wa Fedha wa Kenya,Uhuru Kenyatta kama mmoja wa watuhumiwa sita wanaotakiwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za kuchochea ghasia zilizosababisha mauaji baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2007.
Wengine ni waziri wa viwanda Henry Kosgey, Waziri wa zamani wa elimu, William Ruto na Mkuu wa polisi mstaafu Mohammed Hussein Ali.
Watu hao wanatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo zilizosababisha mauaji ya watu 1,300 na kuwakosesha makazi watu wengine 650,000.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mwendesha mashtaka mkuu wa ICC , Louis Moreno Ocampo aliwataja wahusika wengine kuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na katibu wa
baraza la mawaziri Francis Muthaura na mtangazaji Joshua Arap Sang.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo watu hao watapelekewa hati za kuitwa mahakamani na kama wakikataa ataomba hati za kuwakamata wakamatwe.
Kwa mujibu wa Ocampo,watu hao sita wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kuchochea ghasia,kutesa, kudhalilisha na kuua raia.
Ocampo alisema mkuu wa polisi wa zamani, Ali, anatuhumiwa kuamuru askari polisi kuwapiga risasi na kuwaua waandamanaji ambao hawakuwa na silaha.
Ocampo amewataka watuhumiwa hao kujisalimisha wenyewe na pia kuacha kutisha mashahidi.
SOURCE: XINHUA
Kikwete Lusaka kwa mkutano muhimu

Kikwete Lusaka kwa mkutano muhimuRais Jakaya kikwete leo asubuhi wakisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi huku mwenyeji wao Rais Rupiah Banda(katikati) akishuhudia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa maziwa makuu .Viongozi hao wapo lusaka kwa special summit on illegal exploitation of natural resources .
Picha nyingine ni rais akikaribishwa mjini Lusaka kwa maua jana.
Source:Freddy Maro
Copyright © 2012 lukwangule entertainment All Right Reserved
Designed by UjenziOnline