Drive Angry ya Nicolas cage ni babu kubwa..angalia trela

KATIKA waigizaji ninaowahusudu sana ambao hunipa raha kwa jinsi wanavyoendesha mambo yao ni Nicolas Cage, mtu ambaye sinema zake zimejaa u...


KATIKA waigizaji ninaowahusudu sana ambao hunipa raha kwa jinsi wanavyoendesha mambo yao ni Nicolas Cage, mtu ambaye sinema zake zimejaa ubabe na wakati mwingine kasi isiyokuwa na mazungumzo.

Kama umeshawahi kuona vitu kama “Moonstruck,” “Raising Arizona,” “Vampire’s Kiss” na “Leaving Las Vegas,” unaweza kumwangalia Cage katika umahiri wa aina yake kwenye dunia ya sinema na hasa anapoigiza dunia nyingine ndani ya dunia halisi.

Hakika ninasema unaweza kabisa kutambua kwamba hawa ni baadhi ya watu wachache katika wakati wao, ambaye amefanyakazi inayotamanisha macho, inayoamsha hisia za mwili na kukufanya ukae katika tafakari kubwa.

Cage ana safari ndefu katika mambo ya filamu lakini kwa uhakika kuanzia mwaka 1996, Cage amejibadili sana na kuwa katika staili ya Sylvester Stallone na kujiingizia fedha nyingi.

Mabadiliko haya unaweza kuyaona katika filamu nyingine zenye utamu mkubwa “The Rock,” “Con Air,” “Face/Off,” “Snake Eyes,” “Gone in Sixty Seconds,” “National Treasure,” “Ghost Rider” na filamu nyingi ambazo hadhi yake ni babu kubwa.

Pamoja na kumuona muigizaji wetu huyo katika namna hiyo katika karne hii ya 21 kwa mara nyingine tena anazuka na kitu kikali “Drive Angry,” inayoumbwa vyema na Patrick Lussier na mtata mwingine wa picha za mauaji zenye maneno kidogo Roger Corman.

Mpango mzima wa “Drive Angry” hauna tofauti na sinema hizo za genre ya mauaji ya kutisha na mauzauza ya ushetani.

Ndani ya picha hii Cage akicheza kama Milton anatoka maeneo yasiyopenyeka wala mtu aliyemo kutoka huko kuja kurejea duniani (jehenamu) kuhakikisha kwamba anazuia washenzi fulani kumtoa mjukuu wake kichanga kafara kw ahila baada ya kumrubuni binti yake na kumuua.

Kundi hili la waabudu ushetani lilikuwa linaongozwa na Billy Burke wakiwa na William Fichtner mtunza hazina wa ushetani huo ambaye amekuwa akifuatilia roho za watu zilizotibuka au ambazo zinaweza kutibuka.

Katika patashika hizo yaani stori, mtu mmoja mrembo Piper ( Amber Heard) anakuwa rafiki wa Milton na ndiyo huyu anakula naye kizaazaa mpaka mwisho.

Lussier na Todd Farmer, ambao pia waliandika “My Bloody Valentine” ndio waliochezesha skrini ya filamu hii na kuifanya kuwa moja ya filamu bora kabisa za Cage.

Simulizi lake limedakwa katika mpangilio ambao huwezi kuuachanisha na masimulizi ya hadithi ya kusisimua ya Richard Kadrey ya 2009 yenye jarida linalosomeka “Sandman Slim,”.

Lussier anaitumia vyema teknolojia ya 3-D na kuifanya sinema hii kuwa na utamu ambao ni nadra kuupata na vigumu sana kuusimulia.Filamu hii ina mbio za magari, bunduki kibwene na risasi kama mvua huku ukifurahishwa na gari anayoiendesha Milton ya ’69 Charger ambayo kama kawaida inakuwa mwanzo na mwisho wa matatizo.

Lussier amefanya kazi ya kutosha kuweka mambo mengi ya siri na ya faraghani wazi kwa kuzingatia muondoko wa filamu yenyewe; na hata ukijaribu kutotaka kuizungumzia “Drive Angry” ukiiangalia itakufanya uwe na uhakika, mimi nimeiona katika trela.

Filamu hii ina mambo mengi yanayohusu ubinadamu na utupu, vurumai zisizokuwa na mantiki kichwani na kama huna akili tazama usiache ubongo wako nje ya nyumba.

Ni simulizi kali ambalo linaonesha kuwa Cage ni fasta na mwisho wa matatizo.

Utamu wa picha hii upo unapoelewa kuwa John Milton (Nicolas Cage) ni mhalifu ambaye ametoka eneo wasiloweza watu kutoka kwa lengo moja tu, nalo ni la kumuua Jonah King (Billy Burke), kiongozi wa kundi linaloabudu mashetani hapa duniani.

Jamaa huyu ndiye aliyemshawishi kwa mitego mikubwa mtoto wa kike wa Milton kujiunga na kundi lake katika siku ambayo baba yake (Milton) amekufa.

Lakini alipoingia alichofanya ni kumuua binti huyo wa Milton na mumewe na kisha kumnyakua mjukuu kwa lengo la kwenda la kumtoa kafara binti huyo katika dini ya kuabudu mashetani.

Baada ya kuwahoji wafuasi kadhaa wa King, Milton anagundua kwamba kafara hilo litatolewa katika eneo linaloitwa Stillwater, gereza lililopo Louisiana.

Milton anasimama eneo fulani kupata mlo ambako anakutana na binti mrembo Piper (Amber Heard), ambaye hataki kumpa penzi rafiki yake wa kiume, Frank (Todd Farmer), ili aweze kumuoa kwanza.

Milton anaiharibu gari ya Piper kwa lengo la kumfanya afike kwake. Wanaenda nyumbani kwa Piper na pale binti huyo anamuona Frank akifanya mapenzi na mwanamke mwingine na balaa kubwa linazuka.

Milton anamsaidia kumnyuka kisawasawa Frank kisha anamchukua Piper na kwenda naye hadi mji wa Smithfalls. Huko nako matata mapya yanaanza.

Wakati huo huo mtumishi wa shetani, The Accountant (William Fichtner) anawasili duniani kumfuata Milton kumrudisha jehenamu. Baada ya kumhoji Frank, anagundua kwamba Milton na Piper wanaelekea Louisiana na anajitumbukiza ndani ya polisi na kujifanya ajenti wa FBI ili awe na kasi ya kumfikia Milton.

Na kuanzia hapo ni bunduki na mauzauza ya shetani , magari hewani magari baranarani , milipuko, anatekwa huyu anazidiwa huyu mpaka mtoto anaokolewa na anapewa Piper na baadaye yule mtumishi wa shetani anapatana na Milton wanarejea pamoja.

Kuna mengi mno ya kusimulia ambayo yamo katika hadithi lakini kwa leo ninapenda kukushawishi kuisaka filamu hii kama wewe ni mmoja wa mashabiki wa mzee huyu wa kazi kama katika Ghost Rider kama Drive Angry.

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Drive Angry ya Nicolas cage ni babu kubwa..angalia trela
Drive Angry ya Nicolas cage ni babu kubwa..angalia trela
https://i.ytimg.com/vi/RXCApQDv6-o/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/RXCApQDv6-o/default.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2011/03/drive-angry-ya-nicolas-cage-ni-babu.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2011/03/drive-angry-ya-nicolas-cage-ni-babu.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy