Simulizi la Jumatatu..Mimi! Mi mtamu wewe...!-2

Mwenda alikuwa na kazi kubwa ya kutambua kwamba baba yake ana ugonjwa gani na hali hiyo haikumpendeza hata kidogo. Kitu cha kwanza ambacho a...

Mwenda alikuwa na kazi kubwa ya kutambua kwamba baba yake ana ugonjwa gani na hali hiyo haikumpendeza hata kidogo. Kitu cha kwanza ambacho alifikiria usiku huo ni kuhakikisha kwamba anapata majibu ya maswali yote madogo madogo ambayo yangelimsaidia kutambua hali halisi ya baba yake. Maswali hayo angeliyajua kupitia mazungumzo na mama yake na pia kupitia vipimo vidogo ambavyo angelipendelea kujua kabla ya kupeleka vipimo Morogoro.

Hakuwa na shaka kuwa baba yake alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu ambacho kimeachwa kumtafuna kwa muda mrefu. Lakini matatizo mengi katika watu ambao wamepita umri kidogo huambatana sana na shida ambayo inaweza kuwa nayo katika mzunguko wa hewa hasa katika nyumba za msonge ambazo uwapo wa madirisha huwa ni wa aina yake na wakati mwingine hakuna kabisa.

Ilikuwa shida tupu, lakini ni wazi kuwa hakuwa na muda wa kujadiliana kuhusu suala hilo ni mazoea tu yamewaweka watu katika nyumba hizo ambazo mzunguko wa hewa kwa mgonjwa huwa taabu. Kutokana na baridi watu wengi wamekuwa wakiishi katika hali ya kujifungia zaidi.
Haikuwa rahisi kuondokana na dhana ya zamani kwamba madirisha yanaruhusu wanga kupita na kwamba kuwa na madirisha makubwa ni kuwakaribisha wachawi kukuroga.Zilikuwa imani za kijinga lakini zenye mwelekeo ambao si wa kawaida hata kidogo.

Utamaduni ambao umejijenga kuhusiana na maisha ya kawaida ya wanadamu wa maeneo haya ya mlimani, hofu ya maisha ya kurogana na pia hali ya kutokuaminiana imefanya mazingira ya maisha kuwa na aina fulani ya mfuatano na hata ujenzi kufanana. Baada ya kukamilisha kila kitu pamoja na mawazo, kula chakula na kuoga Mwenda alirejea katika chumba chake na kisha akaenda kumwangalia mama yake jinsi anavyohangaika kumsaidia baba yake kula chakula.
"Baba Mwenda kidogo tu angalau uonyeshe kwamba unakula kwa mtoto" alisema mama Mwenda. Kweli baba alijitahidi lakini mwishoni hakuweza aliashiria kunawishwa na kuachwa kupumzika.
"Nitakula baadaye" alisema kwa sauti ya chini kabisa ambayo ilisikiwa na Mama Mwenda pekee.
Mwenda alimtazama baba yake alivyokuwa akihangaika akabaki anajiuliza kama maisha mwishoni ni hivyo hivyo kwa kila mtu. Kuwa mzima na kijana kuhangaika na mwishoni kuwa mzee na kujikuta huna nguvu hata ya kuhimili magonjwa. Katika maisha yake hakuwahi hata mara moja kumuona baba yake katika hali hiyo ya kudhoofu. Alikuwa baba ambaye siku zote anajituma.
"Mama ilikuwa siku zote hali hiyo au.."
"Siku hizi afadhali mzee Mkalindi anamsaidia kwa dawa zake. Baba yako karogwa halafu mtesi wake ndiye yule yule. Mzee Malinyingi sijui tumemkosea nini"
"Mama nawe unaamini hayo?"
"Nisiamini hayo unadhani sisi wewe kwenda Ulaya tuna heri hapa? Hata ndugu za baba yako wanatuonea"
"Sipendi kuamini."
"Amini mwanangu manake haya ni mambo ambayo hayaeleweki, ulimwengu wa kiza."
"Ingawa nimefika namuona baba mgonjwa mpaka nitakapoondoka baba yangu atakuwa shwari we ngoja uangalie.Hamkupeleka bure Mwenda, mmempeleka awasaidie na sasa ndio wakati wangu" alisema huku akitoka nje kwani mama yake alimfanyia ishara kuwa anataka kumsafisha baba yake.

Akiwa nje akawa anafikri sana. Fikira zake zilikuwa katika dunia nyingine dunia ya watu kutofahamu vyanzo vya magonjwa na kuishiwa kudanganywa na waganga wa kienyeji.Dunia ya kuoanisha ilikuwa ngumu kwani yapo mambo yanafanyika ambayo hayakuwa na msimamo hata kidogo wala kuwa na uhusiano na mgonjwa.Mama alikuwa na nafasi yake ya woga na japokama alikuwa anaamini kwamba Mungu yu pamoja nao amekuwa na mashaka na jinsi ndugu wa mume wake walivyomtenga yeye na mume wake wakimwacha ahangaike.

Haikuwa inaswihi kwa namna yoyote ile lakini ni wazi haikuwa sawasawa pia.
Mungu hata hivyo amewakumbuka kwani wakati anamuomba amsaidie binti yake arejee kuona sura ya mwisho ya baba yake amerejea kweli kweli na amerejea huku akiwa hajui kama ni kwa muda au kwa kuendelea.
Alimuosha mume wake pale akampa dawa zake za kuchemsha na baada ya kuona jasho linamtoka akamfunika na blanketi akapunguza taa na kumfuata mwanawe ukumbini, alijua muda wa kuwa macho bado.
Alifika na kuketi akiwa amechoka sana.
"Nakuona mama huna hata hamu ya kuzungumza."
"Nina hamu kubwa mwanangu lakini sina furaha hata chembe."
"Unataka furaha gani mama zaidi ya mwanao kurejea" alimuuliza kwa mzaha alikuwa anajua nini maana yake.
"kweli mwanangu umerejea lazima niwe na furaha lakini umekua wewe kuna zaidi ya hili la wewe kurejea. Nimeishi na baba yako tangu ubikira wangu mpaka nazeeka, sijui mume mwingine mimi na huyu sasa ni zaidi ya mume ni rafiki kipenzi mwaminifu na ambaye kumkosa siwezi hata kidogo."alisema na kushusha pumzi.

Ni kweli baba Mwenda alikuwa rafiki mwema na mwaminifu na hata wakati alipokuwa akihangaika kupata mtoto huku watoto wake akizika mmoja baada ya mwingine mara tu baada ya kujifungua , baba Mwenda alibaki kuwa mume anayejali. Hakusikiliza kauli za ndugu zake wala maneno ya kuzusha na kuudhi kutoka kwa mawifi zake yeye alibaki akiwakodolea macho wala hawajibu. Walipomkera akasema hovyo wakataka kumtenga.
"Mwanamke gani anazaa panya wanaokufia mshimoni" walisikika wazi wakisema na hiyo ilimuuma sana lakini aliendelea hivyo, wakahangaika kwa waganga ndipo alipompata Mwenda ambaye alitulia na kuendele akupumua hakuamini miezi iliyofanya miaka mpaka anaondoka kwenda shule na anaondoka kwenda ulaya na sasa anarejea ilikuwa tamu mno kwake yeye ambaye alionekana kama mwanamke mwenye laana kubwa.
Alijua kwanini alikuwa akihesabika na laana alikuwa ni mwanamke ambaye hakuwa chaguo la kijiji kile ,alikuwa chaguo la baba Mwenda ambaye alikutana naye katika ngoma kijiji cha nne ambacho walifika kupeleka pombe.Kwa ufupi yeye pale alikuwa anaonekana kama mtoka mbali aliyekuja kupora mali. hakuwa na haja na mali zao yeye alikuwa mwanake ambaye anajua dasturi za kiluguru na hakuwa na sababu za kuhangaika na mali ambazo si zake.
"Mama nakuona una mawazo mengi sana?"
"Umesema mambo ambayo yamefanya moyo wangu ulipuke ukumbuke mambo mengi sana, mengi si mazuri na hivyo baba yako akiondoka namie nitaondoka nitakuacha katika mji wa watu ambao si wema hata kidogo" alisema na baadaye kuendelea kumkumbusha mtoto wake jinsi walivyomlea kwa shida lakini walivyotukanwa sana mpaka yeye anaondoka anaenda shule anamaliza na kwenda zake Ulaya.
"Mhh nambie mwanangu sasa wewe ni daktari?"
"Sana mama . Mimi daktari ninaelimu sawa na madaktari wengine japokama nimejifunza Urusi" alisema kwa tabasamu kubwa huku akimkumbatia mama yake.Ilikuwa ni kumbatio zuri ambalo lilikuwa na kila aina ya upendo.
"sasa mwanangu ni kama unavyoona nilikuwa nasali kila siku kwa mizimu yetu ikurudishe salama ili angalau umuone baba yako manake nimekuwa nikiishi katika dunia ya woga muda wote huu."
"Kweli mama nimemuona baba na hali yake hairidhishi hata kidogo. Pamoja na kuona kama nimechelewa lakini nataka kujaribu kurejesha afya ya baba"
"Sidhani kama unaweza mwanangu. Sumu imesambaa kila mahali ndivyo mganga alivyosema"
"Mama waganga nao ni watu kama sisi si miungu. Mimi naamini baba kama ameweza kufika muda huu ni lazima atapona. Nitahakikisha atapona. Naona ameanza kukohoa nenda kamsaidie lakini ninataka kukuambia mama hakuna kurogwa wala nini hii hali ya kawaida na hospitali watatuambia nini. Kesho asubuhi nataka kutwaa vipimo vyote vya baba nivipeleke hospitalini Morogoro nitarejea na majibu."
"Haya sasa utachukuaje vipimo hivyo?"
"Mungu akituamsha asubuhi sana basi nataka makohozi yake, na nitamtoa damu kidogo kuondoka nayo vifaa ninavyo"
"Damu mwanangu umekuwa chinjachinja?"
"Wala mama nataka kujua kitu kilichopo ndani ya damu ya baba niweze kumsaidia baba yangu."
"Mama huyo baba yako ni mume wangu mimi lazima umsaidie.Una moyo wa kujituma kama baba yako akupe na moyo wa kusamehe pia kama hali haitakuwa sawasawa" alisema mama yake.Mama aliondoka pale na mtoto alisema wazi kwamba atashinda gemu ile japo inaonekana kuwa ngumu kidogo.
Asubuhi ilipofika ilikuwa taabu kubwa kwani haikuwa rahisi kwa Mwenda kuondoka baba yake alikuwa amebanwa sana. Lakini kwa ishara alimruhu kuondoka naye akaondoka haraka zaidi.
Alifika madukani kabla ya kucha na kupata lifti ya landrover iliyokuwa inampeleka hospitali ya mkoa wa Morogoro mgonjwa mmoja.
Alifika Morogoro moja kwa moja na kama ameandikiwa bahati alikutana na mtu ambaye alimwacha Urusi miaka mitatu iliyopita Dk Madelaine ambaye alimkumbuka moja kwa moja.
"Hee Mwenda umeingia lini" walisemezana kwa Kirusi baada ya kufahamiana.
"Ndugu yangu nimerejea jana nimepandisha mlimani nimekuta baba yangu hoi nimechukua sampuli nije hapa nione ana nini."
"Hilo tu dogo mimi nipo hukohuko maabara".Waliondoka na kuelekea maabara ambako walihangaika pamoja na baada ya saa nne waliweza kubainisha kwamba baba yake ana kifua kikuu, ana tatizo la ini , ana malaria na pia alikuwa na tatizo la figo.
"hili la malaria na kifua kikuu hakuna shida hebu chukua za kumwanzishia dozi kama wiki mbili hivi akipanda vyema mlete tuone hilo ini na figo lina matatizo gani" alisema Medeline ambaye baadaye aliondoka na kumsindikiza rafiki yake mpaka soko kuu la Morogoro ambako alipanda lori kurejea nyumbani kwao Mgeta.

Itaendelea Jumatatu ijayo

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Simulizi la Jumatatu..Mimi! Mi mtamu wewe...!-2
Simulizi la Jumatatu..Mimi! Mi mtamu wewe...!-2
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2011/03/simulizi-la-jumatatumimi-mi-mtamu-wewe_28.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2011/03/simulizi-la-jumatatumimi-mi-mtamu-wewe_28.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy