REFLECTION YA SAFARI KUSINI MWA TANZANIA

HAJA YA KUTAMBUA ‘MKUFU’ WA MAENDELEO UTANGULIZI Niliandika mradi wa kwenda Kusini mwa Tanzania kuandika habari baada ya uchaguzi. Nilie...


HAJA YA KUTAMBUA ‘MKUFU’ WA MAENDELEO


UTANGULIZI

Niliandika mradi wa kwenda Kusini mwa Tanzania kuandika habari baada ya uchaguzi.
Nilieleza nia yangu na baada ya nenda rudi ya majibu na maswali nilienda Safari hii ambayo hakika ilinifunza mambo mengi kuanzia ukweli wa mambo miongoni mwa wananchi,viongozi, matumaini na balaa linalokabili upungufu wa mkufu katika kutekeleza mradi mkubwa ambao unaunganisha mikoa mitatu na nchi jirani tatu.
Mradi huu ambao niliamua kufuatilia ni wa mabilioni ya shilingi ni ufunguo wa maisha ya watanzania na huenda ndio mradi pekee unaosuasua ambao hauna muunganiko na kueleweka vyema kwa watendaji wa serikali na wanasiasa sembuse wananchi.
Hoja ya msingi katika hili ni uchumi na kauli za chama tawala za kuinua mazingira ya Tanzania.
MRADI WENYEWE
Niliandika kuomba nafasi ya kuangalia mambo mawili ambayo ama hakika ni miradi miwili ambayo mimi niliona inafanana: nayo ni korido la Mtwara na makaa ya mawe na chuma.
Katika miaka 20 ijayo mwenendo wa Tanzania katika uchumi unategemea sana ufanisi wa miradi hiyo ambayo ukiigawa ni mitatu na yote ipo Kusini mwa Tanzania. Yaani korido, mawe na chuma.
Huwezi kuamini kabisa kwamba eneo ambalo limebaki kuwa maskini sana kwa kipato ndilo hasa lenye ufunguo wa maisha bora nchini Tanzania.
Ili kuwa na viwanda mama kama ilivyonadiwa na vyama vingi kikiwemo chama tawala cha CCM, chuma cha Liganga lazima kitoke kuwezesha utengenezaji wa nondo na bidhaa mbalimbali za chuma na uyeyushaji wa chuma wenye uhakika unahitaji umeme wa uhakika ndipo makaa ya mawe yanapotakiwa kutoka.
Chuma na makaa hayo yanahitaji miundombinu inayofaa kwa namna yoyote ile na hapa ndipo unapoangalia korido la Mtwara ambalo limelenga kujenga miundombinu na pia kuweka viwanda karibuni mwa Bandari.
Nilitarajia kuperemba sana mambo yanayohusu miradi hiyo kwa kuzingatia ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwa na msingi wa kutengeneza uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda mama na umeme wa uhakika.
SAFARI ILIKUWAJE
HOJA iliandikwa na kuwasilisha katika kitengo husika Desemba 31 mwaka 2010 ikapitishwa Januari 11 na tarehe 15 /1/2011 nilianza safari ambayo ilimalizika Januari 29,2011.Nililazimika kupanga namna ya kuanza kazi hiyo na haikuwa rahisi.
Nilianzia safari yangu Mtwara mahali ambapo kinadharia nilidhani ni kichwa cha miradi yote.
Nilifika huko lakini kutokana na mazingira halisi badala ya kutumia barabara ya Kusini Mtwara, Nachingwea, Masasi kuelekea Ruvuma katika katika legi ya pili ya safari nililazimika kurejea tena Dar es salaam na kuchukua safari ya kwenda Ruvuma kabla ya kurejea Iringa na kuingia Ludewa kupitia Njombe katika legi ya tatu.
Mvua upande wa Kusini zilikuwa zinanyesha kipindi hicho na hilo ndilo hasa lililonifanya nisipitie njia ya kusini kutokana na ukweli kuwa siku zilikuwa chache na kutoka eneo moja la kazi hadi jingine ni siku nzima kutokana na miundo mbinu dhaifu, nilikwama siku moja kufika katika eneo la biashara la boda Mtwara, nilikwama siku mbili Songea na nililazimika kulala siku mbili zaidi Njombe kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha njia nzima kuelekea Ludewa.
NILICHOJIFUNZA
Wilaya ya Ludewa ambapo wakati mvua pamoja na barabara yake kuhudumiwa kila mara inakuchukua siku mbili kutoka Njombe wa basi kufika huko ni eneo tajiri sana kijiolojia. Na Mtwara yenye bandari bomba kabisa inafaa kabisa kuwa gateway ya Tanzania na majirani zake.
Eneo la Ludewa linahifadhi mamilioni ya tani ya makaa ya mawe na chuma vitu muhimu vinavyoweza kufanya taifa lotelote lile duniani kujiamini kwamba linaweza kufanya kitu Fulani.
Mwaka 2004 wakati Rais Jakaya Kikwete akiomba kura alikuwa anaelewa thamani halisi ya eneo hili kwa taifa la Tanzania miaka 100 ijayo kwa kutengeneza thamani halisi ya utajiri wake wa kijiolojia ambapo makaa ya mawe na chuma yapo nje nje; ni hapa alipowaambia wananchi kwamba kazi ya kuyathamanisha (kuyafanyiakazi) madini hayo ilikuwa ianze katika awamu yake ya kwanza.
Imechukua miaka mingine mitano tangu ahadi itolewe kuanza kuona dalili ya kupambazuka hata baada ya miaka 40 ya kujua ukweli na kutoutekeleza. Hapa si madini ya mawe na chuma pekee, eneo hili la kusini lina miamba mingi yenye madini ya aina anuai.
Ingawa mwelekeo wa sasa ni kufua umeme kwa kutumia makaa ya mawe yaliyopo Mchuchuma kuwapo kwa hisani ya Mungu ya kuweka chuma karibu na makaa kunatoa taswira ya wazi kwamba ni sisi wenye matatizo na si Mungu na inawezekana kabisa kuwa moja ya mataifa yenye viwanda vikubwa vya chuma kama tukianza kukiyeshusha chuma kwa wastani unaostahiki.
Kuwapo kwa shughuli za uchimbaji mawe na chuma kunatakiwa kusaidiwe kutengenezwa kwa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe na pia chuma na katika hili barabara na treni ni muhimu.Kuna mazungumzo ya miaka nenda rudi,hakuna ufumbuzi unaonekana karibu.
Ingawa taarifa ya awali ilikuwa kujengwa kwa njia ya reli kuelekea bandari ya Mtwara ambapo kiuchumi ni sawasawa ikiwa ni pamoja na kutumbukiza mradi huo kama sehemu ya mradi mkubwa wa korido la Mtwara , utengenezaji wa miundombinu hii ya kusafirisha madini kunaweza kununufaisha pia wananchi wa wa kawaida wa eneo hilo ambao kwa sasa wanakuwa na dhiki kubwa mvua inapochanganya, kwa kuwaandaa tayari kutumia nyenzo husika kwa maendeleo.
Pamoja na kuonekana kwamba safari hii serikali ya Chama cha mapinduzi imedhamiria kupiga hatua moja kubwa mbele hasa ya kurekebisha upatikanaji wa umeme kwa kufungua maeneo ya Kusini ili pia kuvuna mali asili nyingine ambazo zinapatikana kama madini ya atomiki bado kunashida kubwa ya maunganiko kisekta na hasa uelewa wa Wananchi viongozi walio na Wananchi na katika safari hii nimebaini Wananchi hawajui kitu na viongozi wao sawia, wataalamu yao yamo katika makabrasha na katika mikutano ya kuomba fedha na mbaya zaidi yamo katika mioyo yao wakisubiri wanasiasa.
Miradi katika mikoa inayoandaliwa haina uhusiano wa karibu wa kubebana na miradi mikubwa iliyopo sasa na huenda itakapoanza kutekelezwa basi wananchi wataiona si sehemu yao.
JE SAFARI HII INA MANUFAA?
Ni dhahiri kwa makala nilizoandika katika hili wenye akili na wanazuoni wanaweza kuelewa nini hoja za wananchi na nini nilichokuwa nakifikiri baada ya mazungumzo marefu na umma.
Pengine kama si mradi huu nisingejua kwamba wananchi hawajui kuwa mradi wa korido la Mtwara upo rasmi toka miaka ya 2004 ilipotiwa saini na Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa huko Malawi, na mbaya zaidi hatutumii nafasi ya kibiashara kati yetu na majirani zetu huku itifaki ya forodha ikiwa kikwazo kikubwa.
Pia kwa mradi huu nimejenga maarifa mapya ya kiuandishi na kuweka taarifa mpya za mradi huu ambao unaweza kuwa na maana kama utakuwa kama mkufu kwa Wananchi na kutekelezwa kwa namna hiyo.
Nimeweza kujua kwamba makaa ya mawe yalijulikana toka ukoloni yakafanyiwa hesabu tukashindwa kujipanga wenyewe tukabaki ombaomba wa kimataifa wakati katani ingeliweza kututoa kwa kuweka msingi wa uchimbaji wa madini haya kwa kutumia nyenzo zilizopo na hasa umma.
MATATIZO
Pamoja na kujidai kuwa nimekuwa na muda wa kuona mambo, nilikacha kuenda maeneo mengine ya mbali kwani kukodisha pikipiki bei kubwa na magari hayafiki.Njia ya kwenda Ludewa kupitia Mbambay ina vitu vingi lakini sikuweza kwasababu lojisiki kuwa mbaya ingawa kijiolojia ni njia bora zaidi kuifuatilia.
Viongozi na wataalamu wamekuwa na msaada mdogo kutokana na woga na kutokuwa tayari kuwa wazi katika fikira, utoaji takwimu kutokana na kile wanachokiona na wanachoshughulika nacho katika viongozi wote aliyekuwa mkweli ni mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstafu Anatory Tarimo.
Mtwara wana shida ya biashara na Msumbiji hawana cha kuzungumza zaidi ya kulalamika, Ruvuma hivyo hivyo na Iringa vivyo hivyo.
Maeneo mengi hayafikiki kirahisi na wale wenyeji wanataka kulipwa kama watu wa skauti.
Lakini pia muda uliopangwa kwa kuzingatia fedha zilizopo si kitu sahihi sana kwani muda mwingi unatumika katika kusafiri kutokana na ubaya wa miundombinu na muda mdogo wa field hasa unapolazimika kutaka kusahihisha au kuwa na takwimu halisi.
Wanasiasa wamebaki kusema siasa, wataalamu nao wanakatisha tamaa na Wananchi wamebaki mbumbumbu na kufikiria kwamba wanageuzwa watumwa katika nchi yao:kuona wanasiasa wanazungumza tu wajapoambiwa wasukume kupatikane uwezo wa kukabiliana na mambo mapya.

COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: REFLECTION YA SAFARI KUSINI MWA TANZANIA
REFLECTION YA SAFARI KUSINI MWA TANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhj0KGP_a8XrJ4mrGMYOz4jhdcUqvjaA8V47SRx90NxcRTEVLOhiB6fV8elSTxrvWljPa9tqk9xWssuRcJb6wNwxdDmg5IjaruUMO-joDt-C0mlBirhQ856SA9LLQ6fnDWjRTDXhdEiF5AH/s320/mtwara+7.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhj0KGP_a8XrJ4mrGMYOz4jhdcUqvjaA8V47SRx90NxcRTEVLOhiB6fV8elSTxrvWljPa9tqk9xWssuRcJb6wNwxdDmg5IjaruUMO-joDt-C0mlBirhQ856SA9LLQ6fnDWjRTDXhdEiF5AH/s72-c/mtwara+7.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2011/05/reflection-ya-safari-kusini-mwa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2011/05/reflection-ya-safari-kusini-mwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy