TANGAZA NASI LEO

Thursday, January 26, 2012

BREAKING NEWS ! Innocent na Buti Jiwe wafiwa na baba yao mzee Galinoma


Aliyekuwa mbunge wa Kalenga,Iringa amefariki dunia mapema leo asubuhi mjini Iringa ndani ya gari akiwa anakimbizwa hospitalini kutoka kalanga,ambako alikuwa anaishi.

Mheshimiwa Galinoma ,alikuwa mtumishi wa serikali mstaafu aliyeshika
nafasi mbali mbali katika uhai wake zikiwemo za Katibu mkuu idara ya ulinzi na
jeshi la kujenga taifa,mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mbuga za wanyama
pori,mwenyekiti wa bodi ya mashirika ya Umma(SCOPO),Katibu wa tume ya uchunguzi
wa viongozi,pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga ,Iringa.

Marehemu Galinoma alikuwa anaugua kwa muda mrefu pia aliwahi kuenda India
kwa matibabu na alikuwa huko wiki 6 na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu kwa kiasi fulani lakini baadae alizidiwa tena.

Marehemu ameacha wajukuu na watoto ,miongoni mwa watoto wake ni wanamuziki
Innocent na Buti Jiwe aka Enry Galinoma.

Taaritibu za mazishi zitatolewa si muda mrefu.

Mungu amlaze mahala pema peponi.


Kwa habari zaidi za msiba wasiliana na Joseph Galinoma kwa namba hii 00255716492048
au Denis Galinoma namba hii 00255784769945
Source:msemakweli2007@yahoo.com

0 comments: