TANGAZA NASI LEO

Thursday, January 26, 2012

Côte d'Ivoire yaachana na huduma za afya bure


Famasi ya Abobo-Baoulé iliyopo Abidjan.

Côte d'Ivoire inaachana na mtindo wa kutoa huduma za afya bure kwa sababu za kgharama kuwa kubwa.
Uamuzi huo umetwaliwa baada ya kufanya mradi wa majaribio wa huduma za afya bure.
Serikali imesema kwamba katika kipindi cha miezi tisa serikali ililazimika kulipa jula ya faranga za Kifaransa bilioni 30 sawa na dola za Marekani milioni 60 katika mazingira magumu, anasema waziri wa afya Yoman N'dri .
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Abidjan Januari 24 mwaka huu alisema kwamba kuanzia mwezi ujao serikali haitalipa fedha kwa huduma za matibabu na kwamba huduma za bure zitakuwa kwa ajili ya wanawake na watoto wao.
Watoto hao ni wale walio chini ya miaka sita.
Aidha wamesema wkamba gharama za kumuona daktari zitapunguzwa hadi faranga 650 swa na dola 2.
Imeelezwa kuwa wizi, udhaifu katika menejimentgi na kupanda gharama za matibabu kumefanya huduma za afya za bure zilizoanzishwa na na Rais Alassane Ouattara mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kupunguz amakali ya matibabu kushindikana.
Waziri wa Afya N’dri alisema utekelezaji wa mpango huo wa huduma bure za afya kwa wananchi ulmeshindikana kutokana na kubuniwa vibaya na ghala la serikali la dawa kushindw akuifikia nchi nzima huku likiwa na asilimia 30 tu ya dawa zinazohitajika.
Amesema nyingi ya dawa hizo zimekuwa zikivushwa na watendaji.

"Kuanzia mwanzo baadhi ya wauguzi na madaktari wamekuwa wakitumia mwanya uliopo kuchukua dawa majumbani kwao kasha kuziuza” anasema Florantin Yao, muuguzi katika hospitali kuu ya serikali ya Port-Bouët iliyopo Kusini mwa Abidjan.

Wizara hiyo imesema kwamba imeewachukua hatua kali wauguzi na madaktari 20 kwa kuvuruga utaratibu huo na mmoja ametupw ajela miaka miwili.
SOURCE:IRIN

0 comments: