Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha
mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Kiyovu Sport ya Rwanda
itakayochezwa jijini Kigali.
Waamuzi hao ni Thierry Nkurinziza atakayekuwa katikati wakati wasaidizi wake ni
Jean-Claude Birumushahu na Jean-Marie Hakizimana. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hudu
Munyemana kutoka Rwanda. Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka Uganda.
Mechi hiyo namba 13 itachezwa Februari 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Amahoro jijini
Kigali, na itaanza saa 9.30 kwa saa za Rwanda. Mechi ya marudiano itachezwa Machi 4
mwaka huu, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
CAF YAMTEUA LIUNDA KUSIMAMIA MECHI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa
Kamishna wa mechi namba 3 ya Ligi ya Mabingwa kati ya AS Vita Club ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Atletico Olympique ya Burundi itakayochezwa kati ya
Februari 17, 18 na 19 mwaka huu jijini Kinshasa.
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Gabon watakuwa Mbourou Roponat, Wilfred Nziengu
na David Obamba. Mwamuzi wa akiba kutoka DRC ni Mupemba Nkongolo.
Mechi ya marudiano kwa timu hizo itachezwa kati ya Machi 2, 3 na 4 jijini Bujumbura
ambapo Kamishna atakuwa Eugene Katamban kutoka Uganda.
0 comments:
Post a Comment