Kwa heri Kanumba, umefumba wakati unachanua

"POLE sana kwa Kanumba, Hongera kwa Simba" huo ulikuwa ujumbe wa SMS katika simu yangu, ujumbe kutoka kwa mkuu wangu wa kazi, Jos...


"POLE sana kwa Kanumba, Hongera kwa Simba" huo ulikuwa ujumbe wa SMS katika simu yangu, ujumbe kutoka kwa mkuu wangu wa kazi, Joseph Kulangwa ambaye ndiye Mhariri wa Gazeti la HabariLeo, moja ya magazeti yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya TSN. Sikuelewa Pole ya Kanumba, niliweza kuelewa Hongera ya Simba.

Kabla sijaamua kumpigia simu kujua kulikoni, kwani sikuwa najua kilichotokea, ujumbe mwingine kutoka kwa rafiki yangu mmoja kutoka Dodoma uliingia "Steven Kanumba amekufa".

Sasa usingizi ukanitoka, Duhh. Kutoka hapo nikawa na mfululizo wa salamu na nilipofungua kompyuta asubuhi nikakutana na maneno haya: Beda, Kama ujuavyo Kanumba alikuwa mdau na shabiki mkubwa wa ZIFF. Sisi hata huku tumehuzunika sana kwa kifo chake. Langu ni shairi tu kwa rafiki yangu aliyenitangulia Steven Kanumba. Martin

*ULALE PEMA PEPONI STEVEN KANUMBA* Ulikuwa mtu mbele ya watu, ukajivika tabasamu cheko na bashasha, ulikuwa wa mwanzo na jemadari, kuona mbele na safari kuongoza, Ulikuwa wa mwisho kununa, uliposimangwa kwa kero na ujuvi, Wewe ulishika panga, ukaingia mwituni na njia kutupasulia!

Eh jiti kuu la mwituni, ndege wema na wabaya watamiapo, Eh mzizi ulotambaa, ukagusa nyika na bahari kwa pamoja, Eh mbuyu wa thamani, dawa poa na sumu kali zote zipo, Eh wimbo wa pozeo, jua la kuchea na mwezi wa kuchwea.

Nikwambe nini jabali, ulobeba tasnia, Nikusifuje kwa hili, mbinguni wakasikia, Leo dunia hulali, Pepo yakutazamia, Ugone mpheho Steven, Umbudo nakukumbuka.

Naam Kumbe ni kweli Steven Kanumba amekufa, na shairi katungiwa na Profesa Martin Mhando, Mwalimu wa mambo ya filamu aliyeko Chuo Kikuu cha Murdoch nchini Australia. Profesa Mhando ni mtu niliyetokea kumfahamu sana si kwa sababu ya U profesa bali alivyosimamia Tamasha la Filamu la Zanzibar kwa miaka kadhaa akituunganisha wapenzi na wadau wa masuala ya filamu na aliondokea kumpenda sana Kanumba kwa kuonesha njia kwenye tasnia ya filamu.

Je, mimi namjua Kanumba, kijana wa Kisukuma kutoka Shinyanga? Inawezekana kabisa simjui lakini nimefanya naye kazi kadhaa kama mwandishi na mara ya mwisho nilizungumza naye katika Red Carpet ya Ziff pale New Maisha Club na akaniambia kazi zikipungua tukutane tuzungumze.

Pamoja na hayo napenda kukiri kwamba nilivoti kwake katika masuala kadhaa niliyoletewa mezani kwangu kama mhakiki wa filamu na mara kadha nimepigia vyema sinema zake na nne kati yake zilipata nafasi mbalimbali ikiwamo ya The Devils Kingdom na This Is It.

Nilifanya naye mahojiano mara kadhaa, lakini nayakumbuka majibu yake matatu manne hivi yanayoweza kukupa kiwi:“Hakuna dhambi mpya” alisema haya wakati anajibu swali la kwa nini sinema za Bongo zinafanana na sinema za Nigeria, huu ulikuwa mwaka 2010.

“Kwani wewe unanionaje?” Ni swali alilouliza Kanumba kwa mwanafunzi mmoja wa Zanzibar kutoka Shule ya Sekondari ya Forodhani alipoenda kutoa salamu kama mgeni wa ZIFF. Swali hilo lilitokana na maelezo ya wajihi wake Kanumba wakati akiigiza katika sinema zake na kama Kanumba anajisikiaje na anaonekana vipi kwa wananchi wengine kwa kuigiza katika sinema kama mchawi.

"Hapana, Msimbe ni lazima kuangalia kwamba kazi hii inakuwa bora kwa jinsi inavyostahili. Unapoigiza na watu wa kimataifa kama hawa," alisema nilipomuuliza mbona anachukua muda mrefu kutoa filamu yake ya Devil’s Kingdom.

Pia hakuwa na dhiki kueleza changamoto, furaha na mafanikio yake na haya unaweza kuyaona katika mahojiano na Mwandishi wa HabariLeo Jumapili Angela Semaya (nilikuwapo):Alisema hivi:"Mimi Steven Kanumba nikiwa kama producer (projuza)na director (muongozaji) niliyevumbua kipaji cha Jennifer, nikiwa Mkurugenzi wa KANUMBA THE GREAT FILMS (kampuni inayoshughulika na masuala yote ya sanaa ya Jeniffer) nachukua nafasi hii kumpongeza Jennifer kwa hatua aliyofikia akiwa bado na umri mdogo hakika najivunia hili." alisema Kanumba.

Pamoja na kwamba mbunifu, mtundu, mcheshi alikuwa anapenda kuzungumza ukweli na asiyependa bifu kwa waigizaji wenye umri mdogo aliona umuhimu wa kuwalinda. Aliwalinda sana watoto anaoigiza nao kwa kuwa alisema wasipolindwa watalemewa na umaarufu na kushindwa kutekeleza wajibu wao. Mara kadhaa gazeti la HabariLeo liliwahi kumuomba kuwafanyia mahojiano watoto hao na ilipendeza alivyotupa ruksa tulimjua kwamba ni mwangalifu na ni mweledi katika fani yake.

Maneno ya Angela Semaya ( katika face book):Yaani mbali na kuwa msanii mzuri lakini nitamkumbuka Kanumba kwa kunipa kibali cha kufanya mahojiano na watoto wawili maarufu alioigiza nao, Jenniffer wa This Is It na Sophia wa Big Daddy kwa ajili ya makala ya nyota, yanadhihirisha ukweli ninaouzungumza kumhusu Kanumba katika ulinzi na weledi kama muongozaji na mlezi. Kanumba alishawahi kumwambia: “Wewe ni mama nakuamini nakuruhusu kufanya mahojiano na watoto hawa. Alisema sitaki watoto wa watu wahojiwe na kuandikwa vibaya,” Kimsingi unaona alipenda watoto. Katika kazi yangu ya uandishi sijawahi kukutana na mtu ambaye yuko radhi kwa mahojiano, anayekubali kushindwa na anayejenga hoja miongoni mwa wasanii kama Kanumba. Kanumba ni miongoni mwa wasanii ambao wameitambulisha sana Tanzania nje kwa sasa katika tasnia ya filamu, ametumia sana ujuu wa Nigeria katika filamu barani Afrika kutengeneza jina lake na pia kufanya nao kazi. Kutokana na yeye pasi shaka ndio akina Monalisa nao wanaangalia soko la Magharibi kwa kuingilia milango ya Ghana kwa lengo lile lile kupanda chati katika tasnia hii. Kwa kazi alikuwa mahiri mno hata kama projekti ambayo si yake. Unaweza kuiona katika kazi ya Pilipili ya Black Sunday (hii filamu nilishawahi kusema mwandishi wake amekopi "Butterfly on a Wheel" ya Liongate), Komedi hii inavyokuwa ya aksheni na kuwaacha washiriki wake wakiwa katika patashika kubwa ya kuonesha uasili wake katika mchezo ambao ama hakika kama ni stori ya Tanzania thamani yake ni kubwa.

Katika filamu hii ambayo washiriki wake ni Steven Kanumba, Yvonne Cheryl 'Monalisa', na Yusuf Mlela mambo yanayofanyika yamefanana sana na sinema ya mwaka 2007 ya Marekani iliyotolewa na Lionsgate ya "Butterfly on a Wheel".

This Is It ni moja ya filamu bomba ya kwake mwenyewe kuanzia wazo hadi kuitengeneza. Filamu hii imempeleka kwenye Tamasha la Filamu la Afrika (Fespaco) pamoja na kwamba ni ya Kiswahili . Filamu hiyo pia ilinikutanisha tena na Kanumba katika mahojiano yaliyofanywa na Angela Semaya wa HabariLeo Jumapili.

Mahojiano hayo ndio yaliyozaa nyota wetu binti mdogo wa miaka 11 Khanifa Daudi (Jennifer) ambaye pamoja na mambo mengine Jennifer alielezea anavyomjua Kanumba na jinsi alivyofanikisha uigizaji wake.

This Is It ni sinema ya ulozi ambayo imeondokea kupendwa sana pia nchini Kongo na Rwanda kiasi ya kwamba wakati wanaenda kuitambulisha wananchi wa Kongo na Rwanda walimshangilia sana Jennifer.

Nilikutana naye tena Kanumba katika RED CARPET katika ukumbi wa New Maisha Club siku ya Jumapili tarehe 22 Januari 2012. Hapa nilimuuliza kaka vipi akasema mambo yako taiti ana programu ndefu lakini yenye tija, tukimaliza miezi mitatu hii tuonane kuna project za kufa mtu (akimaanisha atakonga nyoyo za wapenzi wake). Ndoa Yangu akiwa na Wolper ilitarajiwa mwezi huu.

Pamoja na kusema ukweli ninavyomfahamu mimi, kwa kumuona katika kikundi cha Kaole, nimeanza kumfuatia katika habari zake kikamilifu mwaka 2007 baada ya kuona kwamba kuna kitu kipo kwa msanii huyu ambaye ni mbunifu na matata katika kazi zake.

Kanumba, ambaye amekufa akiwa na umri wa miaka 28, naweza kuthubutu kusema kwamba ni miongoni mwa waigizaji bora hapa nchini ambao walikuwa wanasafisha njia kwa staili ambayo ni nadra kuonekana katika historia za ukuaji wa sinema duniani.

Kwa miaka kumi aliyokuwapo katika anga za sanaa katika televisheni na video (filamu) kasi ya kijana huyu ilionesha kwamba tupo (kama taifa) karibu sana na matumizi ya kamera ya mm35 na grafiki zilizotulia, baada ya kupotea kwenye miaka ya 1970 tulipomaliza Fimbo ya Mnyonge. Akiwa amezaliwa kama Steven Charles Kanumba kutoka kwa bwana na bibi Charles Meshark Kanumba Januari 8, 1984, alikua katika familia ya Kikristo na dada wawili.

Akiwa anatokea Shinyanga na Msukuma kwa kabila ( si ajabu lafudhi yake inakuwa nzito) amepitia Shule ya Msingi Bugoyi kisha akaingia Mwadui Seminari iliyopo Shinyanga na kukamilisha masomo yake ya O-Level Shule ya Dar es Salaam Christian Seminary. Masomo ya kidato cha tano na sita alichukulia Jitegemee .

Alijiunga na Kaole Sanaa Group ya Dar es Salaam kama muigizaji na kuanza kutokea katika vipindi vya kuigiza vya televisheni za TBC na ITV ikiwemo ‘Jahazi’, ‘Dira’, ‘Zizimo’, ‘Tufani’, ‘Sayari’, ‘Taswira’, ‘Gharika’ na ‘Baragumu’. Mwaka 2009, Kanumba alialikwa katika Big Brother Africa House na akaleta zogo kubwa nchini kwamba hajui Kiingereza. Lakini kama msanii yeyote yule alikuwa na namna ya kulizungumzia hilo na tuliobaki tulicheka.

Sijaona kazi zote za Kanumba lakini nusu yake zilionesha wazi kwamba alikuwa na safari fupi ya uhakika kuingia katika mambo ya Hollywood kule kwenye kitita chenye uhakika.
Buriani Steven Kanumba umefumba wakati unachanua.
Imeandikwa na Beda Msimbe
ilitoka kwa mara ya Kwanza Habarileo Jumapili 8/4/2012

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Kwa heri Kanumba, umefumba wakati unachanua
Kwa heri Kanumba, umefumba wakati unachanua
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbGr7YLnKG6gvPWlyHmpnqMGmGXtJ5W4FER-QfAMBrLV9EPFA2PHE4hy53I7TmXdEsnKdYmKhJ7ZWRk-CAo4zFtwh3H62oD9vEO2Zar9W0rynCRxcbazJVftjyCLNTwrc0d-PLmww_7ppJ/s320/kanumba6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbGr7YLnKG6gvPWlyHmpnqMGmGXtJ5W4FER-QfAMBrLV9EPFA2PHE4hy53I7TmXdEsnKdYmKhJ7ZWRk-CAo4zFtwh3H62oD9vEO2Zar9W0rynCRxcbazJVftjyCLNTwrc0d-PLmww_7ppJ/s72-c/kanumba6.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/04/kwa-heri-kanumba-umefumba-wakati.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/04/kwa-heri-kanumba-umefumba-wakati.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy