TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia hudum...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya
m-pesa hadi asilimia 20 ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala
yeyote wa m-pesa. Gharama hizi zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16
Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema wateja wa
Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote
nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia
zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma
ya Vodacom M-PESA .
"Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua
huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo
tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ", alisema
Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama
mpya za kutoa fedha. 'Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi"
alisisitiza Bw. Meza.
Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya Kampuni kupunguza
gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi
50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo 'tuma na
ushinde' ambapo shilingi milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote
cha promosheni.
Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na
wanajiwezesha kupitia huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa
na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili kuhakikisha umuhimu
kwa maisha ya kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.
Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya
bili kama vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA.
Vilevile inaweza kutumika kulipia tiketi, safari za ndani za ndege
za Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za
shule, kuweka na kutoa fedha kupitia Benki ya CRDB, Western Union na
huduma zingine nyingi.
Vodacom m-pesa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania
nzima, hakuna shaka kwamba Vodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika
ufumbuzi na umaarufu na matumizi ya kuongezeka siku hadi siku na
kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa masuala ya
fedha hapa nchini.
MWISHO
Imetolewa kwa niaba ya:
Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa wateja wakubwa
Vodacom Tanzania Limited
Tel: Tel: +255754704265
Maulizo kwa ajili ya vyombo vya habari:
Matina Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited
+255755484800

COMMENTS