MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAMUAGA MIGIRO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki Moon akiwa na Msaidizi wake wa Karibu, Dkt. Asha-Rose Migiro wakati wa tafrika ya kumshuk...


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban  Ki Moon akiwa na  Msaidizi wake wa
Karibu, Dkt. Asha-Rose Migiro wakati wa tafrika ya kumshukuru na kumuaga
iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa  UNFPA, UNAIDS na Roll Back Malaria, kwa kutambua
mchango wake katika suala zima la Afya ya Jamii, namna alivyofanya kazi kwa karibu
na Mashirika hayo. katika tafrija hiyo Ban Ki Moon alielezea sababu zilizomfanya
akaamua kumchagua Migiro kuwa msaidizi wake wa  karibu. miongozi mwa sifa  hizo ni
uelewa wa mambo, ukaribu wake na watu maskini na walio katika mazingira magumu.Na
kwamba si mtu wa makuu wala kujikweza.

·         Ya mshukuru kwa mchango wake katika kutetea afya ya wanyonge
·         Yasema alikuwa na mchago mkubwa sana katika vita dhidi ya malaria, ukimwi, kifua kikuu na afya ya wanawake na watoto
·         Ban ki Moon asema alikuwa si mtu wa makuu na mtu wa watu

Na  Mwandishi Maalum

Mashirika ya  Umoja wa Mataifa yanayohusika na  masuala ya  Idadi ya Watu ( UNFPA),Ugonjwa wa Ukimwi ( UNAIDS) na   Mpango wa  kupambana na Ugonjwa wa Malaria ( RBM) jana jumanne yaliandaa tafrija kamambe ya kumshukuru  na kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha- Rose Migiro.
 Tafrija hiyo ya aina yake  na ambayo  mgeni  rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa, Ban Ki Moon,  akiambatana na mke wake na kuhudhuriwa pia na  wadau  mbalimbali  akiwamo Mtendaji  Mkuu wa UNDP Bi Helen Clark, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika UM,  sekta binafis na taasisi za kiraia imefanyika hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Akizungumza wakati wa  tafrija hiyo, Katibu Mkuu Ban ki Moom ameleezea baadhi ya  sababu  zilizomsukuma  kumteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa msaidizi wake wa karibu.
 “ Nilianza kumfahamu Asha- Rose Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri wa mambo ya nje  katika nchi zote. Uwezo wake na uelewa wake wa mambo ulinivutia sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba aliwahi kuwa waziri anayehusika na masuala ya wanawake na watoto. Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye alikuwa ananifaa kuwa msaidizi wangu wa karibu” akasema Ban Ki Moon na kuufanya umati ulihohudhiria tafrija hiyo kushangilia kwa nguvu.
 Kama hiyo haitoshi, Ban Ki Moon amemuelezea Dkt. Asha- Rose Migiro kama msaidizi wake wa karibu ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa lakini ni mtu ambaye alikuwa hana makuu na wala hata siku moja hakujikweza.
“ Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa msaidi wangu wa karibu, amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu muadilifu sana, ni mtu aliyekaribu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu watu waliokuwa katika mazingira magumu.  Daima amekuwa mstari  wa mbele kunisaidia  na hakuna hata siku moja alipojikwenza. Na kwa sababu hii  anastahili tafrija hii” akasisitiza Ban Ki Moon.
Aidha Ban Ki Moon akamuelezea  Asha- Rose Migiro kama kiongozi ambaye daima alitoa kipaumbele  cha aina yake katika masuala ya afya ya jamii  eneo alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake yote kama naibu katibu mkuu kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote walio katika mazingira magumu
Kwa upande wao waandaaji  wa tafria hiyo na wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemuelezea  Naibu Katibu Mkuu, kama kiongozi ambaye mchango  wake umesaidia sana katika  kuihamasisha jumuiya kimataifa kuweka mkazo wa aina yake katika kushughulika afya ya jamii.
Bw. Michel Sidibe, Mkurugenzi mtendaji wa  UNAIDS yeyé alimuelezea Asha- Rose Migiro kama dada yake ambaye sifa zake zinaazia mbali.
“ Asha- Rose Migiro ni dada yangu, ni dada ambaye anasifa za kipekee, ni mwanamke wa kwanza  aliyefaulu  kwa daraja la kwanza katika sheria kutoka chuo kikuu cha dar es Salaam,  ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje nchini Tanzania,  na ni mwanamke wa kwanza kutoka afrika kuwa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa” akasema Bw. Sidibe kauli iliyoamsha tena makofi kutoka kwa wageni waalikwa.
Hakuishia hapo, Michel Sidibe akamuelezea Migiro kama kiongozi aliyefanya kazi  kwa karibu na  Shirika lake katika kuhakikisha kwamba  maambukizi ya  virusi vya ukimwi yalikuwa yakipungua ikiwa   ni pamoja na kupatika kwa tiba ya uhakika kwa waathirika.
“ Tunakila sababu leo hii kumshukuru kwa namna alivyoshirikiana nasi, na ingawa  unaondoka lakini tambua kwamba mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuenziwa” akasisitiza  Bw. Michel Sidibe.
Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Umoja wa Maifa la  Idadi ya Watu, Dr. Babatunde Osotimehin amesema  juhudi kubwa zilizoonyeshwa na  Naibu Katibu Mkuu  katika  kushughulikia masuala ya afya ya jamii, kumefanikisha kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi  hali kadhalika vifo vya watoto wachanga chini ya miaka mitano.
“Katika kipindi  cha uongozi wako, umefanikisha sana katika kuhamasisha  jumuia ya kimataifa kuongeza  misaada yao na kutoa kupaumbele katika afya ya mama na mtoto, tunakushukuru sana kwa hili, na   Mungu aendelee kukubariki” akasema Dr. Babatunde Osotimehin.
Kwa upande wake,  Bw. Herve Verhoosel,  Mwakilishi wa  Mapango wa kupunguza Malaria, yeyé alimuelezea  Dkt. Asha-Rose Migiro kwamba chini ya  uongozi wa Ban Ki Moon, ameweza kujenga misingi bora ya  ushirikiano   na muamko   miongoni mwa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kwamba  kunakuwapo na uhusiano kati ya sekta za umma za zile za binafasi katika kutimiza malengo ya afya ya jamii ikiwa ni pamoja na kasi ya kupunguza malaria
 Akiwashukuru waandaji wa tafrija hiyo, Naibu Katibu Mkuu amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki Moon kwa kumuamini kuwa msaidizi wake wa karibu katika kipindi cha miaka mitano na nusu.
Akasema   ingawa yeyé amejituma  na kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, lakini amefanya hivyo kwa kuwa Ban Ki Moon alimuamini kwamba anaweza. Na kwamba daima ataendelea kuienzi heshima hiyo.
Akatumia fursa hiyo kumueelezea Ban Ki Moon kama kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba kila mtoto angalau alikuwa analala kwenye chandarua, akina mama wajawazito walikuwa hawapotezi maisha kutoka  na uzazi.
Aidha  Migiro amewashukuru kwa moyo wa dhati wasaidizi wake wa karibu  aliofanya nao kazi akiwa naibu katibu mkuu na kwamba bila wao asingefika hapo alipo, akawashukuri pia wadau mbalimbali wakiwamo mabalozi kwa ushirikiano wa hali na mali waliompatiwa muda wote wa miaka mitano na nusu


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAMUAGA MIGIRO
MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAMUAGA MIGIRO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuuv_qSD2Q-eNRx9Fl0DKcS0e1gnfd_6NHTuvX7RtUAFCvj67Zis7tilQYbAPDnwKdDkYjXljq7tAN2XzgX8M2bdFNkGNpLWDf0uG_vvXVkVbI_7zRbyshs8rO8YPFzPjtVY1XxBlcbmM4/s320/un.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuuv_qSD2Q-eNRx9Fl0DKcS0e1gnfd_6NHTuvX7RtUAFCvj67Zis7tilQYbAPDnwKdDkYjXljq7tAN2XzgX8M2bdFNkGNpLWDf0uG_vvXVkVbI_7zRbyshs8rO8YPFzPjtVY1XxBlcbmM4/s72-c/un.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/06/mashirika-ya-kimataifa-yamuaga-migiro.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/06/mashirika-ya-kimataifa-yamuaga-migiro.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy