Leo huduma za tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeendelea kuimarika katika maeneo mengi. Taarifa kutoka Kurugenzi ya Tiba...
Leo huduma za tiba katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeendelea kuimarika katika
maeneo mengi. Taarifa
kutoka Kurugenzi ya Tiba (idara ya tiba, idara ya magonjwa ya
dharura, idara ya
wagonjwa wa nje, idara ya magonjwa ya afya ya akili, na idara ya
watoto) na Kurugenzi ya
Upasuaji (idara ya upasuaji, idara ya magonjwa ya wanawake,
idara ya meno, idara ya
magojwa ya masikio, pua na koo, idara ya macho, na idara ya
nusu kaputi) imeonyesha
kuimarika kwa huduma kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na
hali ilivyokuwa siku
chache zilizopita. Ifuatayo ni thathimini iliyofanyika kuanzia
asubuhi saa 2:00 hadi saa
11 jioni leo tarehe 4 Julaiy, 2012.
Kurugenzi ya Tiba
Idara ya Tiba: (Internal
Medicine)
Madaktari walioko katika
mafunzo kwa vitendo (Interns) 11wamefika kazini na kufanya
kazi. Registrar's wote
wamefanya kazi, Madaktari Bingwa wote wamefanya kazi. Service
ward rounds zimefanyika
pamoja na kliniki ya HIV imefanyika.
Idara ya Magonjwa ya
Dharura: (Emergency Medicine)
Madaktari
waliokuwepo ni Daktari Bingwa mmoja,
Registrars wawili na pamoja na
Interns wawili.
Idara ya Wagonjwa ya Nje
(Cold OPD)
Registrars wote walikuja
kazini na wawili wana ruhusa maalum. Wagonjwa wote
waliofika walionwa.
Idara ya Magonjwa ya Afya
ya Akili (Psychiatry and Mental Health)
Madaktari Bingwa wote
walikuwepo kazini isipokuwa mmoja ambaye yuko masomoni.
Kliniki zote zimefanyika,
wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa
Idara ya Watoto: (Pediatrics
and Child Health)
Madaktari Bingwa wote
wamekuja kazni na kufanya kazi. Interns
watatu nao walikuja
na kufanya kazi.
Kitengo cha Wagonjwa
Mahututi (ICU)
Huduma kwa wagonjwa wote
waliolazwa chumba cha wagojwa mahututi wameonwa
na
wanaendelea kuhudumiwa
chini ya uangalizi wa karibu..
Kurugenzi ya Upasuaji
Upasuaji leo umefanyika
na kuna ongezeko kubwa la madaktari lililojitokeza leo kwa
ajili ya kufanya upasuaji
katika vyumba vya upasuaji. Orodha ya wagonjwa
watakaofanyiwa upasuaji kesho
Alhamisi Julai 4, 2012 imeandaliwa na wagonjwa wote
wamefanyiwa taratibu zote
kwa ajili ya upasuaji ikiwemo kushauriwa na kukubali
kufanyiwa upasuaji,
kupimwa viwango au wingi wa damu kama inatosha mgonjwa kufanyiwa
upasuaji pamoja na
taratibu nyingine za tiba. Hata hivyo, wagonjwa bado ni wachache
wanaokuja kliniki na
waliolazwa wodini.
Idara ya Upasuaji:
(General Surgery)
Idara ya Upasuaji
wagonjwa walionwa na Madaktari bingwa tu, hapakuwa na Interns wala
Residents. Kliniki zote
zilizopangwa kufanyika leo zimefanyika hususani kliniki ya
masikio, pua na koo
(ENT), magonjwa ya wanawake, macho (ophthalmology), matumbo
(gastroentology), njia ya
haja ndogo kwa wanaume (urology), ngozi (skin), ART,
magonjwa ya moyo
(cardiovascular), meno, plastic surgery pamoja na pediatric
surgery. Aidha kliniki
zote kwa ajili ya wafanyakazi na wagonjwa wa kulipia
(private) zote
zimefanyika
Idara ya Magonjwa ya
Wanawake: (Obstetrics and Gynaecology)
Wagonjwa wote waliolazwa
wameonwa na Madaktari Bingwa kwa kushirikiana na Interns
wachache waliokuwepo.
Idara ya Meno: (Dental
Surgery)
Madaktari waliokuwa zamu
walipita round na waliona wagonjwa wote waliolazwa.
Idara ya Masikio, Pua na
Koo: (Otorhinolaryngology)
Makaktari Bingwa walipita
wodini kuona wagonjwa waliolazwa na kufanya upasuaji kwa
wagonjwa wawili.
Idara ya Nusu Kaputi:
(Anaesthesia)
Madaktari Bingwa na
wasaidizi wao walikuwepo na kuendelea na kazi kama kawaida.
Idara ya Macho:
(Ophthalmology)
Madaktari Bingwa waliona
wagonjwa wote waliolazwa wodini, waliendelea, kliniki na
kufanya upasuaji.
Vyumba vya upasuaji:
(Theatre)
*
Urology:
Walikuwa na orodha ya upasuaji na
walifanya
upasuaji wa mtu mmoja.
*
Pediatric Surgery:
Hawakuwa na orodha ya upasuaji kwa siku ya leo
*
Plastic Surgery:
Hawakuwa na orodha ya upasuaji.
*
Otorhinolaryngology (ENT) Walikuwa na orodha, walifanya upasuaji
kwa wagonjwa
wawili.
*
Macho: Wamefanya
zote zilizotakiwa
Kurugenzi ya Tiba
Shirikishi (Clinical Support Services)
Madaktari wa Radiolojia
wote nane walikuwepo kazini na wamefnya kazi. Hata hivyo
eneo hili halikuwa katika
mgomo. Upande wa Maabara: huduma zote ziliendelea
kutolewa. Pia eneo hili
halikuwa katika mgomo.
Idara ya Pharmacy yenye
iliendelea kufanya kazi na pia haikuwa katika mgomo. Idara
hii pia ina Interns 30 na kati yao watatu wako likizo
mmoja yuko likizo ya uzazi
waliobaki 27 wote
walikuwa kazini na kuchapa kazi.
Idara hii ina Wafamasia
12 ambapo 10 kati yao walikuwepo, na wawili wana likizo
maalumu. Pharmacy zote
zimefunguliwa na kufanya kazi. Eneo hili pia halikuwa kwenye
mgomo.
Kurugenzi ya Uuguzi na
Ubora (Nursing Services and Quality)
Wauguzi wote wanaotakiwa
kuwepo kazini wapo na wanaendelea na kazi. ha
Tathimini ya jumla:
Huduma zimeendelea
kuimarika. Wagonjwa ni wachache. Madaktari wengi wamerudi kazini
na wanachapa kazi.
.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 4, 2012
COMMENTS