Bado nipo Mbeya maadili kasheshe kwelikweli

Mwezeshaji wa MCT Jackie Shirima,David Mbulumi na kaka Mkubwa talking notes Warsha  ya maadili ya uandishi  na azimio la Dar es sala...


Mwezeshaji wa MCT Jackie Shirima,David Mbulumi na kaka Mkubwa

talking notes
Warsha  ya maadili ya uandishi  na azimio la Dar es salaam kuhusu uhuru na uwajibikaji wa vyombo vya habari (Defir) kwa mkoa wa Mbeya
23-25Agosti  2012

Maana na umuhimu wa maadili ya uandishi wa habari
Kianzio:
Kuzaliwa kwa baraza la habari Juni 30,1995 kulilenga kutoa mwelekeo mpya kwa waandishi wa habari kutenga mashauri yao wenyewe na pia kuwa alama mahususi ya kitaaluma inayotoa mwelekeo ili kulinda weledi na ufanisi katika taaluma ya habari.
Aidha juhudi ya kuwapo kwa MCT kulikofanywa na watu takribani 13 kunatokana na hofu ambayo I dhahiri ya serikali kutaka kumeza uhuru wa habari kwa kutengeneza sheria ambazo zinatoa nguvu kubwa kwake na kukandamiza uhuru wa habari.
Hofu iliyotanda miongoni mwa watendaji wa serikali ilifanya Baraza hili kuchelewa kusajili hadi miaka miwili baadae na baada ya patashika kubwa. Baraza lilisajiliwa Mei 22,1997 na uzinduzi ulifanyika Agosti 16,1997 huku wadau wakisaini kuheshimu katiba ya baraza na kufanya kazi  kwa mujibu wa katiba za baraza na  kuheshimu maamuzi ya baraza .
Kitu kikubwa ni maadili ya uandishi wa habari na  kuheshimu maamuzi ya baraza kwa kuwa ni la hiari.
Maadili nini?
Maadili au kw akimombo ethics ni mambo ya msingi ambayo yanatawala tabia ya kikazi katika taaluma. Kanuni hizi husaidia jamii husika kutambua baya na zuri na kujenga misingi ya utendaji bora wa shughuli husika.
Tunaweza kusema kwamba ethics hutambulisha fanya hiki usifanye kile.
Mathalani mwandishi ameenda mahali amepewa fedha na chanzo cha habari. Katika maamuzi yake ana haya yafuatayo:.
Anaweza kuchukua fedha na kuamua asiandike habari
Anaweza kuchukua fedha na kuandika habari
Anaweza kukataa fedha na habari asiandike na
Anaweza kukataa fedha na akaandika habari
Ethics zinamtaka mwandishi wa habari afanye lililobora kabisa. Kwa hiyo katika hali ya kawaida kabisa atakataa kuchukua fedha na ataandika habari hiyo objectively.
Ufafanuzi zaidi kuhusu maadili:
Hakuna makubaliano ya kidunia kuhusu  dhana hii ya maadili ya habari katika tasnia ya habari, kila mtu anafanya kivyake akizingatia zaidi haja na utamaduni wa eneo. Kwa maneno mengine hakuna sheria Fulani mahususi katika fani hii kuhusu maadili katika dunia kwa ujumla wake.
Baadhi ya watu na taasisi zinasema wazi kwamba mazingira yalivyo duniani, vyombo vya habari haviwezi kupatana kuhusu hili la kanuni za maadili huku wanasheria wakionya kuhusiana na kanuni hizi, wakisema ipo hatari zinapotengenezwa na kufanyiwa kampeni za kutawala maisha na mazingira ya waandishi, wadau, serikali , wenye vyombo mpaka walaji.
Lakini katika miaka ya 1980 wakati wa mapitio ya Unesco kuhusu mabaraza ya habari ilibainika kwamba kuna mambo Fulani yanaingiliana duniani, lakini yanagusa hasa msingi wa maamuzi yaani ni ya kimoral zaidi.
Ipo msingi inayotawala Falsafa ya maadili . Kimsingi unaweza kusema inatokana na maagizo ya Mungu kwa Mungu kuna uzuri na kudai kufanyika kw amazuri; na pili wanafalsafa akina Plato ambao walisema ipo standadi yana uwiano wa mambo mazuri nje kabisa ya nadharia ya uzuri wa mungu, shida ni kuwa huo uwiano upo wapi? Msingi mwingine ni kuwa maadili yanatofautiana na mazingira, watu na utamaduni kinachoweza kufanyika nchi za magharibi si kile kinachofanyika nchi za kiarabu.
Lakini ukitazam kwa yote yanayofanya maadili kimsingi na matukio ya uwiano wa mvutano wa mbali na karibu wa mambo ambayo yanaitofautisha jamii na wapuuzi wengine ya kuwajibika na kujisikia vibaya unapokosa kutekeleza wajibu wako kiuhalali na bila woga na kwamba ndani yake kuna uzuri usiotakiwa kukoswa.
Mambo hayo ni kama:
1)     Honesty and fairness
2)    Duty to seek the views of the subject of any critical reportage in advance of publication or broadcast, duty to correct factual errors
3)    Duty not to fasify pictures or to use them in misleading fashion
4)    Duty to provide an opportunity to reply to critical opinion as well as to critical factual reportage
5)    Respect to privacy
6)    Duty to distinguish between facts,opinions and conjecture
7)    Duty not to discriminate or to inflame hatred on such grounds as race, nationality or gender
8)    Duty not to use dishonest means to obtain information except in special circumstances
9)    General standard of decency and taste
10)  Duty not to divulge confidential sources and
11)   Duty not to prejudice the guilt of an accused person and publish the dismissal of charges against or acquittal of any one about whom the paper/tv/radio previously report that charges had been filed or that a trial had commences
Na haya ndiyo yanatakiwa kuangaliwa na mwandishi wa habari ambaye ndiye anaeyewakilisha taaluma nyingine katika kufanikisha uchakataji wa habari
Kuna maelezo mengi ya nani ni mwandishi wa habari na katika hili  inatupasa kuelewa kuwa wanadamu wote ni waandishi wa habari kimsingi. Lakini ninapozungumzia mwandishi wa habari katika mafunzo haya, namzungumzia mtu ambaye amefunzwa namna ya kukusanya habari, kuzichakata na kuzisambaza kw akuzingatia kanuni na misingi ya uandishi wa habari.
Misingi hiyo inamtaka mwandishi wa habari kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia ukweli, uadilifu, umahiri na weledi pamoja na umakini  na uwajibikaji wa hali ya juu kwa umma, ili kujenga imani na uaminifu machoni kwa umma.
Ni wajibu pia wa msingi kwa wanahabari kuepuka tabia  za uchochezi wa vurugu, chuki na kukuza heshima ya binadamu.
Hiyo inatokana na ukweli kuwa Tasnia ya habari ipo kuhudumia umma. Na ndio maana pamoja na wafanyabiashara kuanzisha  makampuni ya habari kupata faida, vyombo vyao vinatakiwa kuhudumia maslahi ya  umma kwani tasnia ya habari ni mali ya umma.
Ili kutoa huduma hii kwa ufanisi wadau katika chumba cha habari kuanzia waandishi ,wahariri na wakuu wa vyombo vya habari wanapaswa kujua maana na umuhimu wa maadili  katika fani yao ili kudumisha na kuendeleza ubora wa kazi ya kupasha habari na kujenga imani kwa watu wanaowasoma au kuwasikiliza na hata kuwaona.
Maadili yakifuatwa
Kinachopaswa kudumishwa hapa ni maadili na kanuni za kazi yenyewe ambapo kama yatafuatwa ni dhahiri kutaepusha msuguano na kuleta uwiano sawa wa upashanaji habari kwa manufaa ya umma na taifa bila kujali chombo kinachotumika ni cha mfanyabiashara, dola au cha umma.
Ukiangalia kwenye azimio la Dar es salaam  (DEFIR) kifungu cha nane na tisa waandishi wa habari wakiwa na majukumu makubwa ya kuhabarisha wengine, wanatakiwa kutekeleza wajibu wao na majukumu yao ya kijamii kwa uadilifu mkubwa, umakini na umahiri unaolingana na viwango vya kitaalamu na maadili na kuelewa wakati wote kuwa wajibu na uwajibikaji wao ni kwa umma na kuwa wao ni watendaji wa umma wanaotoa huduma katika Nyanja nyeti ya utumishi kwa umma kwa minajili ya kujenga jamii ya kidemokrasia isiyo na ukandamizi isiyo na ubaguzi kwa misingi ya rangi,ukabila, jinsia na ulemavu na isiyo na uvunjaji wa haki za binadamu.
Mfano mahojiano ya Clouds na mwanafunzi aliyeandika mistari ya bongo fleva nini manufaa yake kwa taifa,mahojiano yalionesha kumtetea huyu mwanafunzi wa kidato cha nne, yumkini  maneno yake yakashawishi wanafunzi zaidi kudharau elimu kama msingi wa kuwa mtu bora katika fani chagua. Kama wazo lilikuwa kuonesha udhaifu wa mtoto mapokeo ya watoto ni tofauti sana kisaikolojia, pengine katika mahojiano walistahili kuwepo wazazi na wataalamu wa saikolojia.
Au kusema kwamba polisi hawana mawasiliano kunasaidia nini jamii kuweka wazi kwamba polisi ni kama wako watupu nahawawezi. Je hiyo kimantiki haiwezi kuchochea uhalifu? Kama ungelikaa kimya ukaiandika kama changamoto kwamba wanatakiwa kusaidiwa zaidi vifaa inakuaje. Isije ikawa kuongezeka kwa uhalifu kwa asilimia 3.9 kunatokana na kuweka wazi wazi matatizo ya lojistiki  ya jeshi la polisi.
Maadili kwa misingi mingine unaweza kusema  ni utekelezaji wa matakwa ya taaluma ili kuweka bayana ukweli, usahihi, haki na uhuru  bila kuonea upande wowote kwa kuzingatia miiko ya taaluma na bila kuumiza maslahi ya jamii.
Tujikumbushe
Mwandishi wa habari ni nani?
N
i mtu aliyefunzwa kitaalamu namna ya kukusanya habari na kuziandaa kwa ajili ya vyombo mbalimbali huku akiwajibika kwa umma.Anatakiwa:
a)    Kuleta usawa : hii kuelezea pande mbili zinazohusika na habari
b)    Kutofanya upendeleo yaani kuelezea upande mmoja wa habari
c)    Kuwa mwaminifu kwa kupunguza madhara bila kudhuru wengine
d)    Kutoa haki kwa kuhakikisha kila upande (unaolalamikiwa na ule unaolalamika) nafasi au huduma sawa ya kusema na kujitetea
e)    Kuhakikisha kuwa habari ina manufaa kwa umma, inahusu ustawi kwa ujumla wa maisha ya watu ni kusema ni public interest.
Juu ya yote waandishi wa habari lazima daima kukataa madai yasiyokuwa na mashiko kwa umma ambayo hutengeneza mitazamo finyu na kusababisha kufikiri kimakundi na kujifunga kimawazo.
>>Madhara ya kupinda maadili
Adhabu ya kutofuata kanuni na kuheshimu maadili hupatikana papo hapo mwandishi anapovunja. Adhabu hiyo ni kusongwa na moyo na kukosekana kwa amani kwamba amefanya makusudi  na pia kuivunjia heshima tasnia ya habari na pia kuiletea kashifa na madeni kampuni kwani ikishtakiwa inaweza kulipa na pia  kuonekana chombo kuwa cha hovyo na kinachokwenda kinyume na umuhimu wa tasnia ya habari.
Kwa waandishi upo uwezekano wa kushtakiwa na katika hili waandishi wapo waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya maadili na wapo wanaosubiri maafa kwani shauri lao linaangaliwa.
Pia mashauri yaliyopo barazani, kufa kwa baadhi ya magazeti kutokana na watu kuyashtaki na mengine kwa kukosa wasomaji kutokana na uandishi mbovu na wenye chuku.
NDIO KUSEMA
Mwandishi wa habari ambaye amefunzwa kitaalamu juu ya namna ya kukusanya habari na kuziandaa kwa ajili ya vyombo mbalimbali huku akiwajibika kwa umma.Anatakiwa:
a)    Kuleta usawa : hii kuelezea pande mbili zinazohusika na habari
b)    Kutofanya upendeleo yaani kuelezea upande mmoja wa habari
c)    Kuwa mwaminifu kwa kupunguza madhara bila kudhuru wengine
d)    Kutoa haki kwa kuhakikisha kila upande (unaolalamikiwa na ule unaolalamika) nafasi au huduma sawa ya kusema na kujitetea
e)    Kuhakikisha kuwa habari ina manufaa kwa umma, inahusu ustawi kwa ujumla wa maisha ya watu ni kusema ni public interest.
Lidia mapunda akiperuzi  gazeti wakati wa kuchambua habari zisizo na viwango katika magazeti.Picha kwa hisani ya  KALULUNGA.BLOGSPOT.COM kwa mapicha zaidi tembelea huko
Juu ya yote waandishi wa habari lazima daima kukataa madai yasiyokuwa na mashiko kwa umma ambayo hutengeneza mitazamo finyu na kusababisha kufikiri kimakundi na kujifunga kimawazo. JE TUNAFANYA HAYA/ AU TUNANG’ANG’ANIA kuvunja maadili kwa habari za makundi au watu binafsi au kujinufaisha wenyewe?
mwisho


COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Bado nipo Mbeya maadili kasheshe kwelikweli
Bado nipo Mbeya maadili kasheshe kwelikweli
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiheDMNlHrgDRhteVH4aWTXVf0P8jGTMfFkKfuUHe_AOrCoxsn0wXFCKkhZRu7g4TELShRdVrfFW66Rd4iZryUarzlTWMhbKHcw1oEUFBAVz6ktCfCnMY-yvgLLyYr4XZhktFdvXukwk1NQ/s320/wawezeshaji+wa+mct.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiheDMNlHrgDRhteVH4aWTXVf0P8jGTMfFkKfuUHe_AOrCoxsn0wXFCKkhZRu7g4TELShRdVrfFW66Rd4iZryUarzlTWMhbKHcw1oEUFBAVz6ktCfCnMY-yvgLLyYr4XZhktFdvXukwk1NQ/s72-c/wawezeshaji+wa+mct.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/08/bado-nipo-mbeya-maadili-kasheshe.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/08/bado-nipo-mbeya-maadili-kasheshe.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy