MUHTASARI WA MKUTANO WA WADAU WA FILAMU TANZANIA ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS – KINONDONI MJINI DAR ES SALAAM 15 AGOST...
MUHTASARI
WA MKUTANO WA WADAU WA FILAMU TANZANIA
ULIOFANYIKA
KATIKA VIWANJA VYA LEADERS – KINONDONI MJINI
DAR
ES SALAAM 15 AGOST 2012.
Utangulizi.
Mheshimiwa
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Viongozi wa Vyama Wanachama wa
Shirikisho la Filamu na Wadau wa Filamu nchini.
Napenda
kuchukua fursa hii kwa kuwashukuru wote wale wote waliopata bahati ya
kuhudhuria katika mkutano ule ambao kwetu ni mkutano wa kihistoria.
Sababu
ya Kuwepo kwa Mkutano.
Mnamo
siku ya tarehe 7 Agost 2012 majira ya saa 11 jioni Shirikisho la Filamu
Tanzania , TAFF kwa ushirikiano wa pamoja na kampuni ya Usambazaji ya Steps
Entertaiment, Watayarishaji wa Filamu wa kampuni za Jerusalem Production, Nice
Entertainment , Chen Arts Creation , Nyerere the Power, CYG na Wasanii
Waongozaji kwa Ushirikiano wa Jeshi la Polisi na ofisi za TRA Makao makuu.
Tulifanikiwa kumkamata mtu ambaye inasadikiwa anadurufu kazi mbalimbali za
Wasanii wa Filamu na muziki wa taarabu na injili.
Mfanyabiashara
huyo haramu wa kazi Wasanii nchini Bwana Rigobert Masawe alikamatwa kwa
kushirikiana na raia mwema ambao hawakuridhikia na faida anayopata kutokana na
kufanya biashara haramu inayotokana na jasho la Wasanii .
Baada
ya kufanikiwa kumkamata Mtuhumiwa huyo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Shirikisho la Filamu – TAFF, iliitisha kikao cha dharura kwa Wasambazaji na
Watayarishaji wa Filamu wote ili kwa pamoja kutafuta namna ya kulishughulikia
jambo hili kwa haraka na kwa nguvu za Pamoja.
Katika
kikao hicho kilichofanyika 08/08/2012 ambacho kilikuwa cha Mafanikio
Watayarishaji na Wasambazaji wengi walihudhuria, baada ya majadiliano ya kina
na yenye busara ambayo yalionesha ushirikiano mkubwa katika kutetea hali hii,
Wajumbe walichangia mawazo mbalimbali na maazimio yalikuwa yafuatayo:
1.
Tufanye Mkutano na Waandishi wa Habari ili kuijulisha jamii na umma wa
Watanzania
kwamba jambo limezidi kuwa sugu na lisili la kificho na linafanyika
wazi
Bila ya woga.
2. Kufanya matembezi ya kulaani kushamiri kwa wizi
wa kazi za Sanaa Dhahiri
3.
Ili kuonesha kukerwa huko Wasanii na Wadau waliazimia kwamba kila mmoja awe
askari kanzu kwa jambo hili kwa makusudi bila ya hivyo filamu zitakosa mauzo
kama ilivyo kwa muziki hapa Tanzania kwa sasa.
Wajumbe
pia walikubaliana kwamba mambo yote yafanywe chini ya mwavuli wa TAFF kwa
sababu ndio muhimili wao.
Baada ya maazimio hayo iliundwa kamati ya
kusimamia na kupanga mkakati wa namna ya kutekeleza mkubaliano hayo, kamati hiyo
ilikuwa na Wajumbe wafuatao;
1. Simoni Mwakifwamba Rais wa TAFF.
2. Wilson Makubi Katibu Mtendaji wa TAFF.
3. Steven Mengele (Nyerere)
4. Simoni Mwapagata (Rado)
5. Jackob Steven (J.B)
6. Vicent Gibs (Gibs Media)
7. Vicent Kigosi ( Ray)
8. Issa Mussa (Cloud)
9. Mahsein Awadhi (Dr Chen)
10.
Asha Baraka
Kamati
ilikuwa na jukumu la kutafuta namna ya kufanikisha maazimio hayo na Kampuni za
Usambazaji na Watayarishaji zilikuwa tayari kusaidia baadhi ya maeneo katika
utekelezaj,i.
Mkutano
na Waandishi
Mheshimiwa
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo tarehe 10/08/2012 saa 5 mchana
asubuhi kamati ilifanikisha kutekeleza jukumu la kuongea na wa aandishi wa
habari kama maazimio yalivyopendekezwa. (taarifa kwa vyombo vya habari
imeambatanishwa).Mkutano ulifanyika katika Hotel ya Demagi Kinondoni ulikuwa na
mafanikio makubwa kwa sababu wadau mbalimbali walihudhuria pamoja na Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama Promotions Mh Alex Msama aliweza kufika na
aliipongeza TAFF kwa jitihada za makusudi iliyochukua kuokoa hali ambayo
inatishia uhai wa kazi za Wasanii wa Filamu nchini kama ilivyo katika Muziki
Wazungumzaji
wakuu katika mktano huo na Waandishi wa habari walikuwa ni Rais wa Shirikisho
la Filamu na Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movies.
Baada
ya Mkutano na Waandshi wa Habari TAFF ilifanya kikao na Wasambazaji wote pamoja
na kupitia chama cha Wasambazaji nchini TAFDA na ile kamati ya awali pamoja
kutafakari kwa pamoja juu ya matembezi ya kulaani wizi wa kazi za wasanii kikao
kilifanyika katika ofisi za TAFF zilizopo Magomeni.
Lakini
pamoja na Wajumbe wa kikao cha kwanza kupitisha maazimio ya kufanya matembezi
ya kulaani wizi bado Uongozi wa TAFF uliona kwamba hakuna ulazima sana wa
kufanya Matembezi hayo kwa kuwa Serikali tayari imeonesha nia ya kusaidia
tasnia hii na uzuri ni kwamba utekelezaji wake umeshaanza kupitia mpango wake
wa urasimishaji Wajumbe wote walikubaliana na hoja hiyo.
Kutokana
na hilo Shirikisho la Filamu ikaamua kusitisha suala la Matembezi badala yake
likafanya mkutano wa Kulaani wizi wa kazi sanaa katika viwanja vya
Leaders kwa makusudio na malengo yale yale yaliyoamuliwa katika kikao na
Wanakamati.
Wasambazaji
waliohudhuria ni Steps Entertainment, PiliPili Entertainment, Whatever
Production, Liro Promotion, Zito Entertainment, SSG Distribution, KAPICO, GMC ,
Papa Zii, Bajomba Production, Sas O entertainment, KIBIKI, Easy Media,
Bornagain Film Production,Mega Video na Wengineo wengi.
Kwa
kuona umuhimu wa hilo Wasamabazaji walipitisha azimio la kuchangia ili
kufanikisha mkutano huo na jumla ya Tshs 1,300,000/= ziliahidiwa na
kufanikisha mkutano huo.
Mkutano wa Kulaani Wizi wa Kazi za Sanaa.
Mheshimiwa
Waziri,Napenda kukujulisha kwamba miezi miwili iliyopita kabla ya tukio hili
kutokea Wadau mbalimbali wa tasnia ya Filamu na Muziki wameipongeza TAFF kwa
muenendo wake mzuri katika kusimamia majukumu yake pamoja na mapungufu makubwa
yaliyopo ikiwemo suala la tatizo la kifedha , lakini hawakusita kutushauri juu
ya mgogoro wa kifikra uliopo kati ya TAFF na kundi la wasanii wa Bongo Movie,
wengi walishauri kwamba ipo haja ya kufikia tamati kwa tatizo lenu sababu
nafasi tuliyonayo kwa jamii ni kubwa sana. TAFF iliupokea ushauri huo ilikuwa
inaufanyia kazi.
Mkutano
wa Wadau Kulaani Wizi huo, ulifanyika tarehe 15 Agost 2012 kuanzia saa 6 mchana
na kiukweli ni mkutano wa mafanikio kwa sababu pamoja na muda wa mkutano
ulikuwa wa jua kali lakini wadau walijitokeza wengi sana.
Mada
zilizozungumzwa katika mkutano huo ukiondoa mada kuu ya Kulaani Wizi wa kazi
za Sanaa ni zifuatazo:
a. Nafasi ya Wadau wa Filamu katika Urasimishaji
wa sanaa nchini
b. Umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wasanii
c. Umuhimu wa Wasanii katika mchakato mpya wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
d.
Umoja na Maadili ya Wasanii na katika kazi zetu.
Wazungumzaji
katika Mkutano huo Walikuwa ni
a. Rais wa Shirikisho
b.
Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie
Mratibu
Mkuu wa Mkutano huo walikuwa ni TAFF chini ya Usimamizi wa Katibu Mtendaji
Mkutano
ulifunguliwa saa 6:00 na Mkurugenzi wa kampuni ya Papa Zi kwa kuwashukuru wadu
wote wliohudhuria hapo pamoja na hali ya jua kuwa kali.
Lakini
pia aliwaomba wadau kwamba Jambo linalohusu umoja miongoni mwetu ni la muhimu
sana kuliko wanavyofikiria kwa sababu bila ya kuwa na umoja mambo mengi
hayatafanikiwa.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie.
Mwenyekiti
wa Kundi la Wasanii wa Bongo Movie Jackob Steven (J.B) alisema kwamba sasa ni
wakati wa Wasanii kuamka , kujitambua na kuacha tofauti zetu ambazo kimsingi
hazitusaidii kupiga hatua bali ni wakati wa kuungana ili kwa pamoja tuweze
kumpiga adui yetu kwa nguvu ya pamoja.
Lakini
pia aliupongeza uongozi wa TAFF kwa jitihada mbalimbali wanazofanya katika
kushughulikia matatizo ya Wasanii, kuwatetea wasanii na mambo muhimu
wanayopigania kwa niaba ya Wasanii wote hapa nchini.
J.B
aliendelea kusema kuwa Wasanii tusipoonesha ushirikiano na mshikamano wa kweli
maharamia wa kazi za filamu wataendelea kunufaika huku wenye haki tukiwa
palepale kwa sababu za kuendekeza matatizo yasiyo na tija kwetu. Lakini pia
alimuomba Rais wa Shirikisho la Filamu na Uongozi kwa ujumla walitazame suala
la mgogoro wetu kwa sababu unachangia kutumaliza wenyewe na aliomba wakati
umefika bifu hilo limalizike haraka iwezekanavyo kwa maslahi ya tasnia ya
filamu na sanaa kwa ujumla na anamini kwamba hakuna atayeweza kutusuluhisha
ikiwa sisi wenyewe hatuko tayari, wao kama Bongo Movie
wana tamka wazi kwamba hawana tatizo na Uongozi
wa Shirikisho na wanamtambua Rais wa Shirikisho na wako tayari
kufanya kazi pamoja .
Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania
Mheshimiwa
Waziri wa Habari,Vijana , Utamaduni na Michezo kabla ya kuanza kuzungumzia
ajenda kuhusu Mkutano huo aliwashukuru wadau wote waliohudhuria kwa sababu
anaamini wametambua wajibu na ummuhimu wa Shirikisho la Filamu Tanzania .
Lakini
pia alichukua fursa hiyo kujibu maelezo yaliyotolewa na J.B kuhusu mgogoro wa
Bongo Movie dhidi ya TAFF, Kabla ya yote alimuomba Mwenyekiti wa Bongo Movie na
viongozi wengine na Katibu wa Shirikisho na viongozi wengine wapande juu ya
jukwaa.
Alisema
kwamba anajisikia furaha na amani bila ya kutarajia kama J.B angetoa taarifa
hiyo mbele ya umma wa Wadau wa Filamu Tanzania siku hiyo, lakini kwa niaba ya
Kamati Kuu ya Shirikisho, Bodi ya Shirikisho la Filamu na Wanachama wote wa
Shirikisho la Filamu Tanzania, alitamka wazi kwamba ikiwa Rais wa Shirikisho au
Bodi ya Shirikisho na Wanachama waliwakosea Bongo Movie basi kwa niaba ya wote
anaomba tusamehewe lakini pia alisema na ikiwa Bongo Movie waliwakosea TAFF pia
kwa niaba ya uongozi mzima wa Shirikisho anatamka wazi kwamba tumewasamehe
hivyo anaomba tuzike na kusahau tofauti zetu leo na tuanze upya.
Baada
ya maelezo hayo ambayo yaliungwa mkono kwa wadau kupiga makofi kwa wingi sana
Rais wa TAFF, Simoni Mwakifwamba alimkaribisha J.B naye alisema kwamba kwa
niaba ya Uongozi wote wa Bongo Movie nao wamekubali msamaha uliotolewa na wao
wamewasamehe wale wote walio wakosea katika mchakato wa mgogoro huo na ameomba
tuanze upya mahusiano yetu kama ilivyo kuwa zamani wakati tunaanzisha TAFF na
wako tayari kushirikiana na TAFF kwa lolote wataloagizwa kufanya na kuanzia leo
wanamtambua Rais wa TAFF na uongozi wote kwa ujumla.
a.
Nafasi ya Wasanii wa Filamu katika Urasimishaji wa sekta ya Sanaa
Rais
wa TAFF alianza kwa kuishukuru serikali kwa kuweza kusikiliza kilio chetu
ambacho kimedumu zaidi ya miaka 20 sasa, lakini pia aliishukuru serikali kwa
kuifanya sanaa kuwa ni kazi rasmi ambayo itakuwa ni yenye mchango katika pato
la Serikali moja kwa moja. Kwa hiyo aliwataka Wasanii wa filamu kuakikisha kuwa
wanaitumia fursa ya urasimishaji huo kwa mambo yafuatayo:
i. Kuzalisha kazi bora zenye zitazokidhi viwango
vya soko la ndani na soko la kimataifa na zenye maadili
ii. Kuhakikisha kwamba kazi zote lazima ziwe
zimezingatia sheria zote za utayarishaji wa filamu kwabla ya kupelekwa sokoni.
iii. Wasambazaji na Watayarishaji wahakikishe
kwamba wanarekebisha mikataba yao kuwa ni yenye maslahi kwa Wasanii wote
wanaofanya nao kazi.
iv.
Kufichua Maharamia wa kazi za Wasanii ili kufichua uharamia wao.
b. Umuhimu wa Bima ya Afya
Rais
wa TAFF alisema kwamba sasa wakati umefika muda wa Wasanii kujiunga katika
mifuko
ya hifadhi ya jamii kwa lengo la kujiwekea akiba zitazo wasaidia katika
matatizo ya afya zao, mikopo kwa ajili kuendeleza kazi zetu na mengineyo lakini
alitumia fursa hiyo kusema kwamba NSSF wametaka TAFF kuingiza wanachama wake
kuingia katika mfuko huo, majadiliano yanaendelea yatapo kamilika wadau
watajulishwa kupitia vyama na makundi yao.
b.
Ushiriki wa Wasanii wa Filamu katika Katiba Mpya na Sensa 2012.
Rais
aliwataka Wasanii wa Filamu wote kuhakikisha kuwa pale kamati ya Katiba itapowa
fikia wahakikishe kuwa watajitokeza kwa wingi kwa ajili kutoa mapendekezo yetu
kwa sababu ni jambo muhimu na limekuja kwa wakati muafaka kwa hiyo si jambo la
kuzembea.Alisisitiza kwamba itakuwa ni aibu kwa vizazi vijavyo kwamba katika
madiliko ya Katiba mpya ya nchi Wasanii wa Filamu hawakushiriki kutoa maoni
yao, aliwaomba wajitokeze kwa wingi sana .
c.
Umoja na Maadili kwa Wasanii
Umoja
Rais
wa TAFF alisema kwamba katika umoja kwa kiasi Fulani tumeanza kufanikiwa
kwa
sababu ya Wasanii tumekuwa tukishirikiana katika matatizo mbalimbali lakini pia
anapongeza
tukio la kumaliza mgogoro uliokuwa kati ya Bongo Movie na TAFF kwa
siku
ya leo hivyo aliwataka wasanii kuwa wakweli na waaminifu miongoni mwetu.
Mwisho
aliwataka Wasanii kuhudhuria vikao mbalimbali vitavyoitishwa na vyama wanachama
au Shirikisho kwa sababu ya kupata taarifa muhimu.
Maadili
Rais
wa Shirikisho la Filamu, katika suala la maadili aliweka wazi kwamba Wasanii wa
Filamu mbele ya jamii tumechafuka sana. Tusijione tuko sawa tunapokuwa
wenyewe kwa wenyewe lakini mbele ya jamii hatusomeki vizuri. Katika hili
anaomba wasanii wote tushirikiane kujilinda na tabia zetu kwa lengo la kuleta
heshima mbele ya jamii.
Lakini
pia alisisitiza kwamba katika suala la maadili Shirikisho la Filamu
halitamvumilia hata mmoja miongoni mwa wale wataojitokeza kutuchafua na
atayejitokeza tutamshughulikia.ipasavyo.
d. Kukamatwa
kwa Mharamia wa Kazi za Wasanii
Kama
tulivyotangulia kusema hapo awali kwamba Bwana Masawe maarufu kwa jina la
Msukuma alikamatwa nyumbani kwake ambapo pia anafanya ofisi kwa ajili ya
kudurufu kazi mbalimbali za Wasanii. Kazi zilizokamatwa kwa haramia huyo ni
filamu ya Hatia (Tino) , Glory of Ramadhani (Ray), muziki wa Taarabu Mpenzi
Chokalte (Mzee Yusup).
Rais
wa TAFF aliwataka wasanii wote ili kuonesha mshikamano wa kweli lazima
tuhudhurie kwa wingi mahakamani bila ya kukosa pale kesi itapoanza kusikilizwa.
Kuonekana mahakamani kutasaidia kudhihirisha machungu kwa wezi wa kazi zetu na
endapo tusipojitokeza maana yake tumeridhika na maovu yanayofanywa na maharamia
hawa. Lakini pia kampeni itakuwa endelevu ikiwa ni sehemu ya kutekeleza tamko
na agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Gharibu
Billali alilolitoa Musoma katika Uzinduzi wa kanuni za sheria za filamu na
michezo ya kuigiza mwaka 2011 mwezi Octoba.
KUFUNGA MKUTANO
Harambee
Maalumu.
Baada
ya taarifa ya Rais wa Shirikisho Bwana Simoni Mwakifwamba kumaliza kuzungumza
Katibu wa Shirikisho la Filamu Bwana Wilson Makubi aliwashukuru wadau kwa
kuhudhuria mkutano huo lakini pia wadau waliomba kufanyike harambee ya
kuchangia gharama za kuendesha kesi hiyo. Wadau walikubali kuchangia na ilikuwa
kama ifuatavyo:
a.
Ahadi ya Usafiri kwenda mahakamani zilitolewa na kampuni zifuatazo;
i. Kampuni ya CYG chini ya Issa Mussa (Cloud )
ii. Kampuni ya Cheni Art Creation (Dr Cheni)
iii.
Nice Entartainment (Mtunisi)
b.
Ahadi ya Kuchangia Tshirt zenye ujumbe maalumu.
i.
Tuesday Kihangalla fulana 100
ii.
Dr Cheni fulana 50
iii.
Chriss Creation Fulana 100
iv.
Issa Mussa (Cloud) Fulana 200
v.
Christian Promoters fulana 50.
Jumla
ya Fulana ziliahidiwa kutolewa na wadau hao ni 500 Wasambazaji na Watayarishaji
walipendekeza kwamba fulana hizo mara baada ya kukamilika zitauzwa kwa gharama
ya shilingi 2000/= kila moja kuchangia gharama za uendeshaji wa Shirikisho la
Filamu Tanzani.
Fedha
Taslimu zilizochangwa zilikuwa ni Shilingi 75,000/= lakini pia wadau
waliwachangia Mzee Kankaa na Mzee Small jumla ya shilingi
150,000/= ili ziwasaidie katika matibabu yao na matumizi kwa kuwa Wazee wetu
hawa ni wagonjwa kwa muda mrefu sasa Mkutano ulifungwa saa 10 alasiri..
Ushauri
kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk Fenella
Mkangara tunaomba achukue hatua za makusudi kuwaita viongozi watatu wa kila
upande wa Shirikisho la Filamu Tanzania na Viongozi wa Bongo Movie kwa ajili ya
kuhitimisha na kusawazisha zaidi maelewano hayo kuimarisha tasnia.
Muhtasari
huu umepitiwa na:
SIMONI
J. MWAKIFWAMBA WILSON R. MAKUBI
RAIS
KATIBU MTENDAJI
TAREHE 18 AGOST 2012
COMMENTS