Kipande tu cha umuhimu Leo kwa saa zaidi ya nne nilikuwa katika TIFPA-Media workshop on the Constitutional Review Processes pale Hot...
| Kipande tu cha umuhimu |
Leo kwa saa zaidi ya nne nilikuwa katika TIFPA-Media workshop
on the Constitutional Review Processes
pale Hotel Landmark, Ubungo Dar es Salaam.
Kulikuwa na mambo mengi ambayo yamezungumzwa kuhusu nafasi ya
waandishi na vyombo vya habari kusaidia taifa hili kupata katiba mpya.
| Mkude akitoa mada kuhusu vionjo vya katiba |
Pamoja na hayo kulikuwa na kusemana kwa wazi kuhusu kukosekana
kwa weledi na uadilifu miongoni mwa waandishi wa habari katika kufanikisha hilo
wakiwa wamejikita zaidi katika kile ambacho unaweza kukitafsiri kama
uanaharakati badala ya kazi ambao imejaa uwajibikaji na kuwasaidia watanzania
kupata majawabu na wala si majibu.
Baada ya mada zilizowasilishwa na Mzee Phili karashani na
Mkude wa TIFPA ilifika wakazi wa mazungumzo na watu kibao walisema maneno ambayo kama nilivyosema hapo juu.
Yaani Kimsingi katika warsha hiyo au tuseme semina, waandishi
wa habari nchini wametakiwa kuacha uanaharakati na kutekeleza wajibu wao katika
mchakato wa kuelekea Katiba mpya kwa uadilifu na uzalendo.
Kwangu mimi semina hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Sheria na
Haki za Binadamu cha TIFPA ( Tanzania IFP Alkumni Association) kwa ajili ya
wanabari na wasanii jijini Dar es salaam iliona haja ya waandishi kuachana na
unaharakati na kufuata weledi wa taaluma na kuwa wadilifu katika kuwapasha
habari wananchi kuhusiana na mchakato huo wakiwawezesha na si kuwatia maneno.
| Kipanya akizungumzia shida ya upelekaji mbovu wa maneno |
Akizungumzia changamoto za waandishi wa habari katika maeneo
takribani sita muhimu ya kwenye katiba, msanii wa vikaragosi, Masudi
Kipanya alisema sehemu kubwa ya
waandishi wanachukua maneno vibaya na kusababisha mitafaruku hali ambayo
haichangii kupatikana kwa katiba
inayostahili. Mahali fulani alisema anajisikia haya kuwa ndani ya
tasnia, mimi nikasema tuoshe matongtongo tuendelee na safari kwa namna
inavyostahili.
| Ngurumo akizungumza |
Naye Ensbert Ngurumo alisisitiza haja ya mawazo tofauti kuwa
pamoja kwa lengo la kujenga taifa na kuangalia falsafa ya uadilifu katika
maisha. Tuko waadilifu kiasi gani, tunaogopa nini? Unaogopa unapokosa uadilifu.
Naye Angel Msangi alisema kwamba wahariri wanatakiwa kusimamia
ukweli na uadilifu na kuacha ' bahasha
nene' zinazowafanya kupindisha maadili na kuwatumikia hao wenye bahasha.
Pamoja na kujadili masuala yanayohusu matatizo ya katiba
masuala ya sheria na haki za binadamu yalitakiwa kuwa wazi huku mfumo wa
muungano ukishauriwa kuangalia histioria, mahitaji ya sasa na siku za usoni.
| Tuangalie historia na sasa na yajayo... |
Mimi nilisema mfumo wa Muungano unapaswa kuangalia ukweli kuwa
dunia inajiunga kwa sababu za kiuchumi, lakini historia pia inazingatia
maungano ya watu huku hali ya kijiografia na mabadiliko ya hali ya hewa duniani
yanapaswa vile vile kuangaliwa kuhusu Muungano wa Tanzania.
umuhimu wa muungano ama hakika si katika ubinafsi bali ni kwanini
tunauhitaji sasa au baadaye katika mazingira ya kiuchumi na hata mabadiliko ya
hali ya hewa,urahisi wa kumudu mikikimikiki ya kiuchumi na kijiografia.
| viongozi..ukiukaji wa maadili |
Lakini nilizungumzia pia suala la viongozi kutokuwa pendwa,
hali inayotokana na kukiuka kwa undani kabisa
maadili ya uongozi miongoni mwa viongozi na kukosekana kwa hatua muafaka dhidi
ya wakiukaji. Inakuaje hasa unapokuwa na
oifisa wa TRA mathalani ambaye ana ghorofa kubwa katika kazi ambayo ameanza
juzi na hana mkopo.
| Shivji anatoa majawabu si jibu |
Lakini yote ni matokeo ya azimio la Zanzibar lililoua azimio
la Arusha lililokuwa likitaka uadilifu na kutojilimbikizia mali.
Aidha nilisema kwamba sioni kama Profesa Shvji anapingana na
kauli zake kuhusu muungano lakini anatoa majawabu kwa matatizo yaliyopo na wala
si jibu.
Katika semina mchokoza mada mwandishi wa habari veterani Phili
Karashani alihimiza kuangaliwa kwa vionjo halisi vya uzalendo kwani mazingira
ya sasa yanaonesha kwamba hakuna watanzania wenye ukereketwa.
Alitolea mifano watu wa
tanga wanapozungumza kufanikiwa ni kwenda Mombasa, Arusha ni kwenda Nairobi,
Bukoba ni kwenda Kampala, Kigoma ni kwenda Kigau au Bujumbura wakati wa Mbeya
ni kwenda Afrika Kusini ila wale wa Mtwara pengine kutokana na vita wao ni kuja
dar na kufanya umachinga wa bidhaa za
Kichina badala ya vinyago.
Katika mazingira hayo alihoji uzalendo.
Alisema wengi wa watu wanafikiria nje ya mipaka ya Tanzania
kwa mapumziko hata kufanyakazi na hivyo kimantiki hawaitendei haki nchi yao
lakini wakitaka yenyewe nchi iwatendee haki.
picha zote na Ahmad Michuzi wa jiachie blogspot
picha zote na Ahmad Michuzi wa jiachie blogspot
COMMENTS