SINA uhakika na mikoani lakini sinema hii yenye pozi la mahaba kila kona, kila nukta ilileta mushkeri mkubwa wakati ilipoingia kat...
SINA uhakika na mikoani lakini sinema hii yenye pozi la mahaba
kila kona, kila nukta ilileta mushkeri mkubwa wakati ilipoingia katika majumba
ya sinema Dar es salaam.
Sizungumzii sinema nyingine ya mapenzi bali Yellow Emmanuelle.
Hamu ya kuzungumzia sinema hii ambayo si aksheni bali simulizi
la mapenzi ilitokana na udaku wa mtu mmoja aliyefika katika ofisi na kunitajia
mfululizo wa sinema zilizotoa raha kwa vijana katika miaka hiyo, vijana ambao
kwa leo hii wana umri wa ukaka.
Sinema hii ilipoingia nchini hata watu wa sensa kipindi kile
walipata taabu kubwa kuchop kwani walibakia wakishangaa kwa jinsi wanavyotaka
kufuata nadharia za eti utamaduni wetu hausemi hivyo na kujikuta wakipruni
dakika nyingi kiasi cha kuondoa utamu kwa wale wanaotaka kuiona kupitia majumba
yetu wakati huo ya Empire, empress, Avalon, Cameo, New Chox na kadhalika.
Yellow Emmanuele zipo nyingi lakini ninayotaka kukuambia mimi
ni ile ya Chai Lee ambayo ilileta taabu kubwa katika jiji la Dar watu wakanunua
tiketi kwa kupaa na kwa ajili ya utamu watu walikuwa wanaiangalia Empire
wanaisubiri Empress na wengine wapo Cameo na Chox na kiukweli walikuwa hawaishi
hamu, sinema ilikuwa tamu, mtoto mtamu na simulizi tamu.
Ni drama babu kubwa la mapenzi la mwaka 1977 ambalo pia
lilijulikana kama Il mondo dei sensi di Emy Won likitembea kama halikukatwa kwa
saa moja na dakika 39.Kwa Dar lilipigwa panga likawa kiasi kama cha saa limoja
tu.
Kwa kipindi kile walahi nakuambia Bitto Albertini ambaye ndiye
alikuwa akiongoza kikosi kilichotoa burudani cha Chai Lee kama Dokta Emy Wong
na Giuseppe Pambieri kama George Taylor
katika movie hili la mapenzi alikuwa amemudu kuleta muwashawasha miongoni mwa
watanzania.
Wengine waliokuwa katika sinema hiyo ni Ilona Staller kama
Helen Miller na Helga,Claudio Giorgi na Rik Battaglia
Simulizi hili ambalo ukilitazama kwa haraka unaweza kusema
kwamba ni la kipono lipo kwa rubani wa ndege ya Shirika la ndege la Uingereza
ambaye baada ya kujinafasi vya kutosha wakati anarejea nyumbani anakutana na
kisago kikali na wakora wa mji wa Hong Kong, alipozinduka alikuwa hospitalini
akitibiwa na binti bomba.
Binti huyo ambaye alikuwa Daktari mrembo ni Chai Lee
aliyekwenda kwa jina la Emy Wong. Jamaa anajikuta anampenda ghafla binti huyu
wa kichina, anayejua kupenda pia lakini alikuwa na kasoro moja alikuwa
anaheshimu tamaduni za Kiasia, kwamba ana mchumba ambaye hajawahi kumuona wala
kukutana naye faragha.
Ukiangalia kwa makini sinema hii utagundua kwamba Bitto
Albertini al maarufu kama Albert Thomas si tu hakutaka kutengeneza pono lakini
pia alitaka kuwa na sinema yenye msisimko wa pekee ambao utafanya ishu ya
mapenzi kuonekana kuwa na ladha inayostahili ya kutotegemewa ila unaikuta tu kwa
jinsi filamu inavyojifungua muda wote.
Naweza kusema hilo kwa kuwa mara tu sinema inapoanza baada ya
muda mfupi sana ukiangalia mandhari ya Hong Kong, unagundua kwamba unatazama
aina tofauti ya sinema miongoni mwa filamu za kipindi kile.
Pamoja na ukweli kuwa Albertini alishawahi kufanya kazi
nyingine kama "Emanuelle nera/Black Emanuelle" ya mwaka 1975, sinema
hii mpya ilikuwana utamu wa aina yake ambapo ilizingwa katika hisia na
grafiki za mapenzi zilizotulia sana.
Kutokana na umahiri wake waigizaji wa "Yellow
Emanuelle." walikuwa waigizaji bomba sana katika mitaa ya sinema za
kikubwa kwa ajili ya wakubwa. Kwani Ilona Staller alikuwa zaidi ya muigizaji
alikuwa mahiri sana katika sinema za watu wazima nchini Italia na Giuseppe
Pambieri akawa katika zile sinema za mapenzi ya kuchusha akiwa na Nico Fidenco
ndani ya mavitu ya wakubwa yanayotengeneza umatemate usiokuwa wa kawaida.
Katika sinema hii mapenzi ya Chai Lee kama Emy Wong na
Pambieri kama ukiyaangalia bila ya mpangilio ama hakika yatakupa ashira kwamba
yanatoka katika filamu nyingine kabisa si ile unayoitazama.Hii inatokana na
ukweli kuwa sehemu zao za mapenzi zilikuwa kali babu kubwa na hasa pale
walipofanya mapenzi katika chumba ambacho kilikuwa hakijakamilishwa vilivyo na
kilikusudiwa kuwa chumba cha kulala ilikuwa balaa tupu.
Chai Lee katika sinema hii alikuwa staa sana hasa kwa jinsi
alivyokuwa akionesha nini maana ya mapenzi ingawa mwisho wake umejaa utata,
japo sikumbuki vyema ilikuwa kuwaje vile. Lakini nataka kusema kwamba ilikuwa
moja ya filamu iliyotufanya wiki kadha tunajazana katika majumba ya sinema na
pengine ndio ilikuwa sinema za mwishomwisho kabla ya taifa hili kuanza
kushindwa kuagiza sinema toka nje hadi siku za karibuni ambapo CD zinaingia na
tunakosa uhondo wa milimita 35.
Kusema ukweli ilikuwa picha ya kutia raha, ladha na utamu wa
aina yake. Watu waliipenda kwani ilikuwa imechukua chati ya upigaji bora wa
sinema na wale wanaopenda masuala flani walifurahia sana kwa jinsi yalivyokuwa
ingawa wakati fulani unaguna kimya kimya.
NB ilitoka awali Spotileo

COMMENTS