CHAMA Cha Mapinduzi
kimerejesha uongozi wa Jiji la Mwanza katika mikono yake baada ya kufanikiwa
kutwaa kiti cha umeya na Naibu meya.
Uchaguzi mpya uliofanyika
bada aya kugawanywa kwa Halmashauri ya Mwanza katika mapande mawili ya Mwanza
na Ilemela.
Uchaguzi wa Ilemela uliahirishwa
baada diwani wa Chadema aliyevuliwa uanachama na kamati kuu,
Ya chama hicho Henry
Matata kuweka pingamizi.
Akitangaza matokeo ya
uchaguzi, uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji,
Msimamizi wa uchaguzi,
Wilson Kabwe alisema mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula
alishinda nafasi ya umeya
baada ya kupata kura 11 na kumshinda upinzani wake kutoka
Chadema Charles
Chinchibera ambaye alipata kura nane.
Nafasi ya unaibu meya
ilichukuliwa na diwani wa kata ya Igogo, John Minja ambaye
alipata kura 10 na
kumbwaga mpinzani wake Diwani kata ya Mirongo (CUF), Daud Mkama
aliyepata kura nane.
Katika uchaguzi huo
Chadema iliingia mkataba na CUF wa kuachiana nafasi ya Unaibu
meya ambapo hata hivyo
walishindwa kuipata.
Kabla ya uchaguzi huo
kuanza majira ya saa saa 4 asubuhi, katika eneo la ofisi za
halmashauri ya jiji la
Mwanza kulionekana kuwepo kwa ulinzi mkali wa askari wa
kutuliza ghasia (FFU)
huku barabara ya kuelekea katika hospitali ya mkoa ya sekou
toure ikiwa imefungwa.
Walioruhusiwa kupita
katika barabara hiyo walikuwa ni madiwani, watumishi wa
halmashauri ya jiji la
Mwanza na waandishi wa ha
Na Grace Chilongola, Mwanza
Sept 8:HATIMAYE Halmashauri ya jiji la Mwanza imerudi chini ya uongozi wa CCM baada
ya kushinda nafasi ya Umeya na Unaibu meya katika uchaguzi uliofanyika jana kufuatia
kugawanywa na kuwa halmashauri mbili huku uchaguzi wa halmashauri ya manispaa ya
Ilemela ukiahirishwa baada diwani wa Chadema aliyevuliwa uanachama na kamati kuu,
Henry Matata kuweka pingamizi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi, uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya jiji,
Msimamizi wa uchaguzi, Wilson Kabwe alisema mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula
alishinda nafasi ya umeya baada ya kupata kura 11 na kumshinda upinzani wake kutoka
Chadema Charles Chinchibera ambaye alipata kura nane.
Nafasi ya unaibu meya ilichukuliwa na diwani wa kata ya Igogo, John Minja ambaye
alipata kura 10 na kumbwaga mpinzani wake Diwani kata ya Mirongo (CUF), Daud Mkama
aliyepata kura nane.
Katika uchaguzi huo Chadema iliingia mkataba na CUF na kuachiana nafasi ya Unaibu
meya ambapo hata hivyo walishindwa kuipata.
Kabla ya uchaguzi huo kuanza majira ya saa saa 4 asubuhi, katika eneo la ofisi za
halmashauri ya jiji la Mwanza kulionekana kuwepo kwa ulinzi mkali wa askari wa
kutuliza ghasia (FFU) huku barabara ya kuelekea katika hospitali ya mkoa ya sekou
toure ikiwa imefungwa.
Walioruhusiwa kupita katika barabara hiyo walikuwa ni madiwani, watumishi wa
halmashauri ya jiji la Mwanza na waandishi wa habari huku wengine wakitakiwa
kuzunguka.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa Nyamagana, Katibu wa Itikadi, siasa
na Uenezi wa CCM, Nape Mnauye alisema Chadema wamevuna walichopanda kwa ubabe wao.
“Hizi ni salamu kwa wana Chadema, Dk. Slaa alikuwepo hapa Mwanza alipoona upepo
mbaya jana (Juzi) usiku, ubabe wao umewafikisha hapo walipo,” alisema Nape na
kuongeza CCM bado ipo imara tofauti na Dk. Slaa anavyoona.
Alisema madiwani wameamua kuirudisha CCM kuliongoza jiji la Mwanza hivyo kuwaomba
washirikiane katika kuliletea jiji maendeleo kwa kuanza kukabiliana na changamoto ya
migogoro ya ardhi.








0 comments:
Post a Comment