Temporary Shelter

CHATROOM

Wednesday, September 5, 2012

CUF wataka mtaala wa mafunzo ya Polisi uangaliwe upya

THE   CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
Office of TheYouth Secretary General
P.O. Box  10979
Dar Es Salaam, Tanzania
http://www.cuf-or.tz
CUF/DSM/JUVCUF/002/1A/2012/0105/09/2012


MAUAJI YA RAIA NI MUHIMU MTAALA WA MAFUNZO YA POLISI KUANGALIWA UPYA.

SEKRETARIETI ya Vijana Chama cha Wananchi –CUF (JUVCUF) Taifa tunataka Serikali kupitia upya MTAALA wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwapa elimu ya maadili mema katika utendaji wao wakazi ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu na jinsi ya kukabiliana na changamoto ndogondogo kamaza Maandamano ya Raia na Mikutano yahadhara inayofanyika kwa Sasa, hasa kutokana na kukua kwa Demokrasia hapa nchini.
Tunaamini bila ya Serikali kukaa na kuliangalia nini polisi wanatakiwa wafundishwe wanapokabiliana na raia wasiokuwa na silaha wala kujua matumizi yake, hali itazidi kuwa mbaya hapa nchini sababu Polisi wataendelea kukosa maadili, wataua na kujeruhi raia jambo litalowafanya raia nao kutembea na silaha za moto kila watapokuwa kwenye mikutano yao ya hadhara au Maandamano, na ikifikia hapo nchi itakuwa imepoteza amani yake iliyodumu kwa nusu karne sasa na itasababisha nchi kuingia kwenye machafuko kama ilivyotokea katika mataifa ya Afrika Kaskazini ambapo ilifika mahali vijana walichoshwa na vitendo vya mauji ya raia na kuamua kuasi wakapambana  na Utawala hadi ukaanguka madarakani.
JUVCUF tunaamini kuwa Watanzania wengi hasa vijana wamekuwa wakiishi kwa utulivu huku wakilinda amani ya Taifa hili pamoja na matatizo makubwa ya umasikini yanowakabili kutokana na kukosekana kwa ajira za uhakika na kudumu kunakosababishwa na mfumo mbaya wa utawala na mipango hasi ya chama cha Mapinduzi.
Tunaiomba serikali kuwa makini na iwajengee uadilifu watendaji wake waliopo kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kuheshimu Mkataba wa kimataifa wa haki za Binadamu wa 1948 ili kulinda haki za msingi za binadamu hapa nchini.
Vijana wa CUF tunaendelea kulaani mauaji hayo yanayoendelea kufanywa na Polisi kwa kuwa yamekiuka haki ya msingi ya kuishi ya Marehemu Mwangosi kijana ambae alikuwa bado anahitaji kulitumikia Taifa lake.
Hivyo tunaomba Tume iliyoteuliwa iwe makini katika kuchunguza na kulifuatilia suala hili na iwe huru na yeyote aliyehusika atajwe na kufikishwa kwenye mikono ya sheria bila kujali nafasi, umaarufu au uwezo wa kifedha alionao.
Tunawaomba Vijana wajiunge na kushirikiana na CUF ili tulete mabadiliko yenye tija na manufaa kwa Vijana yatayolinda haki ya kila kijana ndani ya nchi na kupambana na kuondoa uonevu kama huo unaofanywa na polisi kwa maslahi ya watu wachache
Ashura Mustapha
Mkurugenzi wa Habari Secretarieti ya Vijana CUF-Taifa
0655 727341






0 comments:

TANGAZA NASI LEO

xx