TAARIFA KWA UMMA Pamoja na manispaa ya Kinondoni kutoa shilingi milioni moja na nusu tarehe 14 Septemba 2012 kwa ajili ya kufunga mi...
TAARIFA KWA UMMA
Pamoja na manispaa ya
Kinondoni kutoa shilingi milioni moja na nusu tarehe 14
Septemba 2012 kwa ajili
ya kufunga mita na kuanza kusukuma maji ya mradi wa Goba,
nitaendelea kuchukua
hatua za ziada za kuungana na wananchi katika kutaka
uwajibikaji wa watendaji
waliozembea na kusababisha matatizo hayo kudumu kwa muda
mrefu.
Izingatiwe kuwa kiasi
hicho ni nyongeza baada ya awali kutolewa milioni tatu na
Mfuko wa Maendeleo ya
Jimbo la Ubungo (CDCF) kwa ajili ya kuwezesha huduma ya maji
kupitia mradi huo
kurejea.
Ikumbukwe kuwa mwezi
Agosti 2011 maji yalikatwa kwenye kata ya Goba kutokana na
DAWASCO kuidai kamati ya
mradi wa maji shilingi milioni 18 na katika kufuatilia deni
hilo nilipata taarifa za
Kamati ya Maji kuwasilisha malalamiko DAWASCO ya
kutokukubaliana na
kiwango hicho cha deni na pia kwa Manispaa ya Kinondoni kuhusu
matatizo ya kiutendaji na
kifedha katika mradi huo wa maji ikiwemo ya upotevu wa
fedha.
Tarehe 5 Septemba 2011
niliwaunganisha wananchi kwa pamoja tukaandamana kwenda ofisi
ya DAWASCO makao makuu
ambapo tulikutana na mtendaji mkuu wa kampuni husika na
kufanya mazungumzo ambayo
yalisaidia baadhi ya hatua za msingi kuchukuliwa ikiwemo
DAWASCO kurejesha huduma
ya maji katika bomba kuu baada ya sehemu ya deni kulipwa na
makubaliano kufikiwa
kuhusu malipo ya kiwango kilichobaki.
Pia tarehe 24 Oktoba 2011
niliandika barua kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni
kutoa mwito wa hatua za
dharura kuchukuliwa ili kuhakikisha uhakiki unafanyika
wakati huo huo wananchi
wengine wanaendelea kupata huduma ya maji; lakini udhaifu wa
kiutendaji umefanya hatua
ziwe za kusuasua.
Hata hivyo, pamoja na
huduma ya maji kurejeshwa katika bomba kuu haikuweza
kusambazwa kwenye mabomba
ya wananchi pamoja na vioski vya kutolea huduma kwa sababu
ya udhaifu wa utendaji
katika ngazi ya kata na katika kamati ya maji hivyo tarehe 26
Januari 2012 niliwaunganisha
wananchi kufika Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya
hatua za haraka za
Mkurugenzi wa Manispaa.
Kufuatia hatua hiyo
Mkurugenzi wa Manispaa Fortunatus Fwema alifanya ziara katika
kata ya Goba tarehe 31
Januari 2012 na kuagiza kwamba ndani ya tano maji yatoke
katika kata hiyo na
kuagiza Mhandisi wa maji na timu yake waweke kambi katika kata
ya Goba mpaka maji yatoke
kwa gharama za halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Hata hivyo, muda huo
ulimalizika bila maji kupatikana na kikosi kazi kilikabidhiwa
jukumu tarehe 28 Februari
2012 kushughulikia kile kilichoelezwa kuwa ni kuanza
uchunguzi wa Bomba la
Maji kuanzia Tanki Bovu hadi kwenye tanki la Matosa ili
kubaini wizi, upotevu wa
maji na uharibifu wa miundombinu.
Katika kipindi cha kati
ya Februari mpaka Agosti 2012 nimefuatilia Manispaa kwa njia
mbalimbali na wakati wote
maelezo yamekuwa kazi hiyo inachukua muda mrefu kwa sababu
ya urekebishaji wa
miundombinu ambapo Manispaa ya Kinondoni ilikubali kutoa mita 15
pamoja na stendi za bomba
mpya kwa ajili ya kufunga katika bomba kubwa kwenye njia
zinazoelekea kwa wananchi
ili kudhibiti wizi na upotevu wa maji pamoja na kufanya
marekebisho katika
mabomba na gate-valves zilizohujumiwa.
Ikumbukwe kuwa matatizo
ya maji kata ya Goba yanafahamika kwa mamlaka zote husika
kuanzia Wizara ya Maji,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Manispaa ya Kinondoni na vyombo vya
dola kuanzia mwaka 2007
mpaka mwaka 2012 lakini hatua kamili hazijachukuliwa kwa
wakati.
Wananchi wa Goba
wamepoteza uvumilivu kwa kuwa hatua hazichukuliwi kwa haraka na
kutokana na hali hiyo
mbunge kama mwakilishi wa wananchi nimeumua kuungana nao
katika kutaka uwajibikaji
wa watendaji wote waliozembea na kusababisha matatizo hayo
kudumu kwa muda mrefu.
Nimefikia hatua hiyo kwa
sababu njia zote za kawaida kupitia vikao na mawasiliano ya
kiofisi zinaelekea
kukwamishwa na uzembe, hujuma na urasimu na udhaifu wa kiutendaji
katika ngazi mbalimbali.
Katika kushughulikia
masuala la maji kwenye kata ya Goba, narudia kusisitiza hatua
zifuatazo kuendelea
kuchukuliwa kwa haraka na mamlaka zifuatazo:
Mosi; Mamlaka za Manispaa
ya Kinondoni zikiongozwa na Meya na Mkurugenzi zinapaswa
kufuatilia kwa haraka
kuhakikisha maji yanarejeshwa Goba. Hatua hii iende sambamba
na kupanua wigo wa maji
Goba kwa kutekeleza kwa haraka upatikanaji wa maji kutoka
pia mradi wa maji toka
Madale Kisauke. Manispaa izingatie matatizo yaliyopo kwenye
miradi ya maji
inayoendeshwa na manispaa pamoja na kamati za wananchi au vyama vya
watumia maji katika
maeneo mbalimbali. Hivyo, pamoja na kuchukua hatua kuhusu mradi
wa maji wa Goba, Manispaa
ichukue hatua juu ya miradi iliyokwamba ukiwemo wa Mbezi
Msumi na Makabe. Pia,
Manispaa ya Kinondoni inapaswa kufanya mabadiliko kwenye idara
ya maji kwa kuwa ina
udhaifu mkubwa wa kiutendaji.
Pili; Wizara ya Maji,
Mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA) na Kampuni ya maji
safi na maji taka
(DAWASCO) zizingatie kwamba maeneo ya pembezoni ya Dar es salaam
ambayo awali yalikuwa
vijiji sasa ni mitaa yenye wakazi wengi. Hivyo, maeneo kama
kata ya Goba na mengine
ya pembezoni yanapaswa kuunganishwa moja kwa moja na mtandao
wa maji chini ya mamlaka
husika kwa mujibu wa sheria iliyounda DAWASA badala ya
mfumo uliopo ambalo
haulingani na mahitaji.
Tatu; vyombo vya ulinzi
na usalama vinapaswa kushughulikia vyanzo vya migogoro
badala ya kusubiri mpaka
matatizo yanapoibuka kwa kushughulikia kwa wakati
malalamiko yanayotolewa.
Mathalani, Jeshi la Polisi (Ofisi ya DCI) na TAKUKURU
wanapaswa kutoa kauli
kuhusu hatua zilizochukuliwa juu ya tuhuma za ufisadi na
ukiukwaji wa sheria
katika mradi wa maji Goba ambazo zimetolewa na wananchi kwa
mamlaka husika kuanzia
mwa 2007.
Mamlaka husika zizingatie
kuwa tarehe 27 Februari 2011 na 6 Machi 2011 nilifanya
mikutano na wananchi
katika kata ya Goba ambapo risala ya wananchi pamoja na ripoti
ya ukaguzi wa mradi wa
mradi wa maji Goba ya mwaka 2007 zilizosomwa ambazo zilieleza
bayana matatizo
yaliyokuwepo kwenye kamati ya maji pamoja na mradi kwa ujumla
ikiwemo yaliyohusu upotevu
wa fedha ambayo vyombo vya dola vilipatiwa taarifa lakini
hatua hazikuchukuliwa kwa
wakati.
John Mnyika (Mb)
19/09/2012
COMMENTS