mnyika azungumzia ukazaji wa hukumu ya Dowans dhidi ya Tanesco

Jana tarehe 6 Septemba 2012 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetupa ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lililokuwa linaomba mahakama ...


Jana tarehe 6 Septemba 2012 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetupa ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) lililokuwa linaomba mahakama itoe amri ya kuzuia utekelezwaji wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo iliyoruhusu tuzo ya dola 65,812,630.03 za Marekani iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) mwaka 2010 kwa kampuni ya Dowans Holding SA (Costa Rica), sasa Dowans Tanzania Ltd isisajiliwe nchini.
Kufuatia huku hiyo nimetakiwa kutoa maoni yangu maoni kwa nafasi yangu ya  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na pia mbunge wa jimbo la Ubungo  ilipokuwepo Richmond, mitambo ya Dowans na sasa Symbions ambapo pia yapo makao makuu ya TANESCO.
Hivyo, serikali isitumie kizingizio cha maamuzi  ya jana kuharakisha mpango wa kuilipa kulipa Dowans kwa fedha za walipa kodi watanzania au kubebesha mzigo huo kwa wateja wa TANESCO na iwapo Serikali inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imezidiwa na Dowans kwa sababu ya kujiingiza katika mikataba mibovu inapaswa kuwabebesha deni hilo wazembe, mafisadi na waliokuwa wakihujumiana ndani ya Serikali waliosababisha hali hiyo.
Badala yake Serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo anapaswa kueleza ni hatua gani ilichukua kutoka TANESCO ilipowasilisha mahakama ya rufani taarifa ya kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi Septemba 28 mwaka 2011 iliyoruhusu tuzo hiyo isajiliwe.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aeleze ni kiasi cha fedha kilichotumika kwenye kuendesha kesi za Dowans, na IPTL mpaka sasa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya mawakili wa TANESCO na makampuni binafsi yanayotuhumiwa kusababisha mzigo mkubwa wa gharama za kesi ambazo serikali inashindwa kwa nyakati mbalimbali.
Ni muhimu umma ukafahamu kuwa kwa mwaka wa fedha 2011/2012 pekee jumla ya shilingi bilioni 10 zimetumika kwa ajili ya gharama za kuendesha kesi hizo kwa kuilipa
kampuni ya Rex Attorneys na Makampuni mengine ambayo kwa nyakati mbalimbali yamekuwa yakiiwakilisha serikali na TANESCO na kushindwa katika mahakama za kitaifa na kimataifa.
Hukumu ya jana inapaswa kuibua tena mjadala uliodumu kwa miaka minne kuanzia mwaka 2008  tangu yalipopitishwa maazimio 23 ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC ikiwemo kuhusu mkataba na Dowans.
Uamuzi huu wa mahakama unaibua mjadala mwingine kuhusu uwezo na dhamira ya wanasheria wa Serikali na TANESCO katika kesi hizi kwa kuzingatia mtiririko mzima wa masuala na matukio katika majadiliano ya mkataba wa Richmond na hatimaye Dowans kati ya mwaka 2006 mpaka 2012.
Katika mazingira haya namtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo kueleza kwa umma mabilioni mangapi yamelipwa na TANESCO mpaka hivi sasa kwa kampuni hiyo na nyingine na sababu za kuendelea kuilipa kampuni hiyo pamoja na kuwepo kwa uzembe wa wazi wenye kulisababishia hasara taifa.
Umma uzingatie kwamba gharama kama hizi za Dowans na mikataba mingine mibovu ndizo zinazoongeza mzigo wa gharama za uendeshaji za TANESCO na kuchangia katika ongezeko la bei ya umeme na ongezeko la gharama za maisha kwa ujumla.
Maelezo haya ni muhimu yakatolewa na Serikali kwa kina badala ya kuendelea kutoa kauli za ujumla bila kuchukua hatua za kusafisha safu yake ya kisheria ambayo imeingiza TANESCO katika mikataba mibovu na madeni makubwa.
Ikumbukwe pia kwamba iwapo hoja binafsi niliyoiwasilisha ofisi ya bunge mwaka 2011 kutaka utekelezaji wa maazimio yote yaliyobaki kuhusu mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ingejadiliwa bungeni, hatua zaidi zingechukuliwa kwa mafisadi na wahujumu uchumi waliohusika na Richmond, Dowans na masuala mengine ya kisheria yanayosababisha mzigo mkubwa kwa TANESCO na wananchi.
Kutokana na rekodi za maamuzi mbalimbali ya kimahakama kuanzia mwaka 2010 mpaka 2012 sasa inajulikana wazi kuwa Mkataba wa TANESCO na Richmond ulirithishwa kinyemela Oktoba 14, 2006 kwenda kwa Dowans huo kama inavyoononekana katika nyaraka za mahakama ambapo Dowans na Richmond zinadaiana huko Marekani; na kwa kuwa hilo lilifanyika bila kuitaarifu TANESCO kinyume na kifungu cha 15.12 cha Mkataba huo.
Kutokana na hukumu ya Dowans ushahidi umepatikana na kuwa mashahidi mbalimbali walioitwa mbele ya Kamati Teule ya Bunge na wakiwa chini ya kiapo walitoa taarifa za uongo kuwa mkataba kati ya Richmond na TANESCO ulihamishwa kwenda Dowans Disemba 23, 2006 na hivyo wahusika hao mbalimbali – wakiwemo wamiliki wa Richmond; walidanganya au kuficha ukweli mbele ya Kamati Teule na hivyo kuonesha dharau dhidi ya Bunge.
Hata Hivyo, masuala hayo hayawezi kujadiliwa bungeni mpaka kwanza mjadala husika uweze kufunguliwa; hivyo hoja binafsi niliyowasilisha ililenga kutaka uamuzi kubadilishwa na mjadala kufunguliwa ili kuongeza msukumo wa utekelezaji wa maazimio ya bunge na hivyo kuchangia katika mapitio ya mikataba yenye kuongeza mzigo wa gharama kwa watanzania;  kuweka mfumo wa kulihusisha bunge katika maandalizi ya mikataba mikubwa yenye maslahi ya taifa na kuwezesha uwajibikaji na hatua kamili kuchukuliwa kwa waliohusika na ufisadi na uzembe uliolisababishia hasara taifa.
Kufichwa kwa taarifa hizo muhimu ndiko kulichangia kukubaliwa kwa kampuni ya Dowans kuchukua Mkataba wa Richmond; wakati tayari ilikuwa imerithishwa kinyume cha mkataba wenyewe hivyo kuliingiza taifa katika deni kubwa ambalo serikali ilionyesha dhamira ya kutaka kulilipa kinyemela na linataka kugeuzwa kuwa  mzigo mkubwa migongoni mwa walipa kodi wa Tanzania katika utekelezaji wa maamuzi ya mahakama.
Hoja yangu pamoja na mambo mengine  ingependekeza bunge kuazimia kuweka muda usiopungua miezi mitatu kwa serikali kutekeleza Maazimio yote ya Bunge yaliyokuwa yamesalia katika sakata hili la Richmond ili mara moja na daima sakata hili la Richmond na Dowans limalizwe na kufungwa baada ya kutekeleza maazimio yote.
Haiwezekani taifa likawa kila wakati kwenye mjadala wa Richmond na Dowans; hali ambayo imefanya kwamba hata katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme unaouhusisha pia kampuni ya Symbion iliyonunua mitambo ya Dowans mianya imeachwa ambayo inaweza ikasababisha kesi zingine kama za IPTL, Richmond, Dowans iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuepusha hali hiyo.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
07/09/2012

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7051,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: mnyika azungumzia ukazaji wa hukumu ya Dowans dhidi ya Tanesco
mnyika azungumzia ukazaji wa hukumu ya Dowans dhidi ya Tanesco
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2012/09/mnyika-azungumzia-ukazaji-wa-hukumu-ya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/09/mnyika-azungumzia-ukazaji-wa-hukumu-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy