Temporary Shelter

CHATROOM

Wednesday, September 5, 2012

TAHADHARI YA KUWEPO KWA UGONJWA MPYA WA MAHINDI


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
TAHADHARI YA KUWEPO KWA UGONJWA MPYA WA MAHINDI

Tumepokea taarifa kutoka kwa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na Shirika la Kilimo na Chakula (Food and Agriculture Organization) juu ya kuwepo ugonjwa mpya wa mahindi unaojulikana kwa jina la “Maize Lethal Necrotic Disease (MLND)”. Ugonjwa huo unasababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalamu “Maize Chlorotic Mottle Virus (MCMV)” na “Sugarcane Mosaic Virus (SCMV)”.

Katika nchi jirani ya Kenya, ugonjwa huo ulianzia katika eneo la Bomet lililopo katika Bonde la Ufa ambapo ulisababisha asilimia 100 ya uharibifu kwa zao la mahindi lililokuwepo shambani. Kulingana na taarifa hiyo, hadi sasa ugonjwa umesambaa katika eneo kubwa ndani ya bonde la ufa na umeenea  katika wilaya 22 ambapo jumla ya hekta 16,000 za zao la mahindi zimeathirika. Hasara kutokana na ugonjwa huo inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 60 hadi 90.

Ili kukabiliana na hatari ya uwezekano wa ugonjwa huo kuingia nchini Tanzania, Wizara inawaarifu wadau wote wa kilimo nchini kuzingatia yafuatayo:

(i)                 Kwa kuwa inasemekana kuwa ugonjwa huo unaenezwa na mbegu na kwa kuwa Tanzania inaagiza kiasi kikubwa cha mbegu kutoka nje ya nchi, vibali vyote vinavyotolewa kuingiza mbegu hizo lazima ziwe hazina vimelea vya “Maize Lethal Necrotic Disease baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa maabara.

(ii)              Vilevile mbegu hizo kabla hazijaingizwa nchini sampuli ichukuliwe na kupelekwa kituo cha karantini cha Tropical Pesticide Research Institute (TPRI) kilichopo Arusha kwa ajiri ya kuhakiki. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuthibiti ugonjwa huo kuingia nchini.

(iii)            Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika zitatoa elimu ya jinsi ya kutambua ugonjwa huo na mbinu za kukabiliana nao.

(iv)            Wakuu wote wa Mikoa, Wadau wote wa mbegu, Wakulima na wananchi kwa ujumla katika mikoa inayolima mahindi kwa kutegemea umwagiliaji au kilimo cha msimu cha kutegema mvua wanapaswa kutoa taarifa mapema endapo dalili zisizo za kawaida zitaonekana katika mashamba ya mahindi.

(v)               Wakulima wote wanashauriwa kununua mbegu zilizothibitishwa ubora na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (Tanzania Official Seed Certification Institute - TOSCI). Sambamba na agizo hili, wauzaji na wasambazaji wa mbegu nchini wanaagizwa kuzingatia Sheria ya Mbegu ya Mwaka 2003, kinyume chake watachukuliwa hatua kali za kisheria.

(vi)            Your browser may not support display of this image.
Wananchi wote waliopo mipaka wanashauriwa kutokuhamisha au kubeba mahindi kiholela kutoka nchi jirani bila kufuata taratibu za kisheria. 
  
WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA

0 comments:

TANGAZA NASI LEO

xx