USAJILI/PINGAMIZI DHIDI YA WACHEZAJI Musa Hassan Mgosi, Ayoub Hassan Isiko Mchezaji Musa Hassan Mgosi ameombewa usajili Ruvu JKT kut...
USAJILI/PINGAMIZI DHIDI
YA WACHEZAJI
Musa Hassan Mgosi, Ayoub
Hassan Isiko Mchezaji Musa Hassan
Mgosi ameombewa usajili Ruvu JKT kutoka DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC), na Ayoub Hassan Isiko ameombewa usajili
Mtibwa Sugar kutoka Bull
FC ya Uganda. Wachezaji hao hawaruhusiwi kuchezea timu hizo
mpaka Hati zao za
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) zitakapokuwa zimepatikana.
Toto dhidi ya Kagera
Sugar kumsaini Enyinna Darlinton Ariwodo
Toto Africans ilipinga
usajili wa Enyinna Darlinton kwa timu ya Kagera Sugar kwa vile bado ina mkataba wa
mchezaji huyo ambao unamalizika mwakani.
Kwa upande wake Kagera
Sugar ilisema imemsaini mchezaji huyo kwa vile Toto Africans imeshindwa kumlipa
mshahara ambapo kuna makubaliano rasmi kati ya Ariwodo kuwa klabu hiyo ikishindwa kumlipa
mshahara anaruhusiwa kuondoka.
Uamuzi wa Kamati ni kuwa
Ariwodo ni mchezaji halali wa Kagera Sugar kwa vile Toto Africans ilishindwa
kutimiza masharti ya mkataba.
Ramadhan Chombo ‘Redondo’
Redondo ameidhinishwa
kuchezea Simba kwa kuzingatia mchezo wa haki na uungwana (Fair
Play) baada ya klabu hiyo
na ile ya Azam kufikia makubaliano kuhusu mchezaji huyo.
Mchezaji David Luhende
kusajiliwa Yanga
Yanga ilikiri kutolipa
ada ya uhamisho ya sh. milioni 5 kama walivyokubaliana na
Kagera Sugar. Awali
waliipa Kagera Sugar hundi iliyogonga mwamba benki (bounced
cheque). Shauri hilo
lilimalizwa kwa Yanga imetakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku
21 kuanzia Septemba 10
mwaka huu.
Super Falcon dhidi ya
Edward Christopher kusaini Simba
Simba imepewa siku 21
kuanzia Septemba 10 mwaka huu iwe imeilipa Super Falcon fedha
za matunzo (compensation)
kwa vile ndiyo iliyomlea mchezaji Edward Christopher
aliyesajiliwa katika
klabu hiyo.
Toto Africans dhidi ya
Mohamed Soud kusajiliwa Coastal Union
Toto Africans iliweka
pingamizi kwa maelezo kuwa bado ina mkataba na mchezaji huyo.
Hivyo kwa msingi wa Fair
Play, mchezaji huyo ameidhinishwa Coastal Union baada ya
makubaliono kati ya
klabu.
Rollingstone dhidi ya
Kigi Makassy kusajiliwa Simba
Simba imetakiwa kuilipa
Rollingstone gharama za matunzo ilizoingia wakati ikiwa na
mchezaji huyo kwa
kuzingatia kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).
Super Falcon dhidi ya
Sultan Juma Shija kusajiliwa Coastal Union
Uamuzi wa Kamati ni kuwa
Shija atachezea Coastal Union, na kwa vile yuko chini ya
umri wa miaka 23, Coastal
Union itailipa Super Falcon fidia ya fedha ilizotumia
kumhudumia mchezaji huyo.
African Lyon dhidi ya
Razak Khalfan kusaini Coastal
Lyon imesema bado ina
mkataba na mchezaji huyo. Kamati imebaini kuwa mkataba wa
mchezaji huyo na Lyon
umemalizika, hivyo ni mchezaji halali wa Coastal Union.
Flamingo dhidi ya Kelvin
Friday kusajiliwa Azam
Friday ruksa kucheza
Azam, lakini klabu hiyo imepewa siku 21 kuanzia Septemba 10
mwaka huu kuilipa
Flamingo gharama za kuvunja mkataba.
Super Falcon dhidi ya
Robert Joseph Mkhotya kusaini African Lyon
Lyon imeagizwa kuilipa
Super Falcon sh. milioni moja ikiwa ni fidia ya kuvunja
mkataba wa mchezaji huyo
ambaye imemsajili. Fedha hizo zitalipwa kwa awamu nne
kutokana na makato ya
mlango yatakayofanywa na TFF. Falcon itapokea malipo hayo
kupitia TFF.
Oljoro JKT dhidi ya
Othman Hassan kusajiliwa Coastal
Kwa mujibu wa rekodi za
TFF, mkataba wa mchezaji huyo na Oljoro JKT unamalizika
mwakani. Hivyo, Othman
Hassan ni mchezaji halali wa Oljoro JKT kwa vile bado ana
mkataba na klabu hiyo.
Yanga dhidi ya Simba
kuacha wachezaji wanne
Kamati imetupa pingamizi
hizo kwa vile hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wachezaji
juu ya kuvunjiwa mikataba
yao. Wachezaji hao walioachwa na Simba ni Dan Mrwanda,
Haruna Shamte, Kanu
Mbiavanga na Lino Masombo.
Ikiwa wachezaji hao
watakuwa na malalamiko kuhusu kuvunjiwa mikataba suala hilo
litafikishwa katika
Kamati kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mbuyu Twite
Kwa mujibu wa Ibara ya
18(3) ya Kanuni za Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji wa
Kimataifa za FIFA, Yanga
ilifuata taratibu zote katika kumsajili Mbuyu Twite, hivyo
ni mchezaji wake halali.
Hata hivyo, kwa vile Yanga imekiri kuwa mchezaji huyo
alichukua dola 32,000 za Simba
na kukiri kuzirejesha, kwa msingi wa kanuni ya Fair
Play, Kamati imeipa Yanga
siku 21 iwe imelipa fedha hizo Simba.
Kelvin Yondani
Kwa mujibu wa Ibara ya
44(3) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF, Yanga
ilifuata taratibu zote
katika kumsajili Kelvin Yondani, hivyo ni mchezaji wake
halali.
Kwa vile Simba imesema
mchezaji huyo vilevile alisaini mkataba na klabu yao,
imetakiwa kupitia mamlaka
nyingine kuthibitisha hilo, na baada ya uthibitisho
iwasilishe malalamiko
yake kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji,
au mamlaka zozote za
kisheria kwa mujibu wa madai/lalamiko husika.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili
na Hadhi za Wachezaji
COMMENTS