TRIPPLE L ni moja ya sinema chache za Kiswahili ambazo unaweza kuzitazama na zikakuvutia kutokana na jinsi mchanganyiko wa uigizaji na wa...
TRIPPLE L ni moja ya sinema chache za Kiswahili ambazo unaweza kuzitazama na zikakuvutia kutokana na jinsi mchanganyiko wa uigizaji na waigizaji unavyoweza kukuweka katika kiti mpaka umalize CD ya pili.
Nasema hivyo kwa kuwa kuna sinema unaweza kuzitazama ukasema
ha ha ha nimeibiwa lakini sinema hii ya Tripple L unaweza kusema mhh inapendeza kuangalia,
wacha niendelee kuangalia.
Kupendeza huko kunatokana na CD namba moja kuwa makini na
taiti kukupa simulizi linalojishebedua kila unavyoipanda huku Walda akionesha
kweli kuwa mwanamke ambaye anaweza anachofanya.
Kwangu mimi ambaye wakati mwingine nashobokea picha za
mapenzi, filamu hii ina aina yake ya simulizi lenye kuhitaji fikira pana
kulielewa kutokana na wajihi wa Claud 112 njia nzima hadi mwisho.
Wakati Claud akionesha sura yenye kukosa furaha njia nzima,
Walda alionesha dhiki ya kuwa na waume
wawili wasiofahamiana kwamba wana mke
mmoja, japo walikuwa marafiki lakini kila mmoja akisema kwamba mke wake yuko
bize sana.
Claud aliweza kuisimulia hadithi hii kwa namna ya kusisimua
zaidi ambapo sababu za ndoa mbili kwa mke mmoja unaziona mwishoni kabisa huku
akitoa baraka tele katika msemo kwamba siri ni ya mmoja ukishaisimulia kwa
mwingine huwa si siri tena.
Zulfa alimsaliti bosi wake akaanika kila kitu kutokana na
penzi, hali ambayo ilimsababisha bibiye Lubna (Warda) kuzimika kwa muda
mwishoni mwa sinema kwa kubaini kwamba
amechambuliwa vya kutosha, hali
iliyomfanya alipoamka kusema ukweli kwa waume wake hao ambao walikuwa marafiki.
Claud pia anatupeleka katika simulizi za kimetafizikia kwa
kuwa Lubna aliota ndoto wale masekretari wake(kutoka olfisi mbili tofauti
anazomiliki) wanamweka pabaya na ikatokea kweli kuwa msaidizi wake mmoja Zulfa
ndiye anayeitosa siri kwa kuwa alishamweleza.
Naam, ni simulizi ambalo haliko kompliketedi lakini lina chuku
yake hasa kutokana na jinsi ambavyo watatu hao walivyokuwa wakiishi katika kaya
moja (mkike) bila kufahamu jinsi walivyowekwa kwa staili ya kufurahisha zaidi.
Pacho aliitumia vyema nafasi yake kwani alikuwa daktari hasa
mwenye mapepe katika mapenzi lakini anayejua kupenda na akiwa hana tatizo
kuliko Claud ambaye alisema wazi kwamba
wakati Limo (patcho) anafikiria magari na miundombinu yeye alikuwa
anafikiria miundombinu ya kumdhibiti mkewe.
Naam hadithi hii nimeipenda na amini usiamini imesimuliwa
tofauti na simulizi nyingine za mapenzi. Unaona shida ya mwanamke mwenye ndoa
mbili ila wote wawili inaonekana anawapenda kwa ukomo sawa.
Sinema hii ambayo pia inakupa kadhia ya nini kilisababisha
kuwapo kwa ndoa ya mke mmoja wanaume wawili, unapopewa mkanda wa nyuma wakati
Lubna yuko hospitalini na wanaume wote wawili wapo mbele yake, imepigwa vyema,
kutokana na picha zake kuzingatia muda na maeneo yaliyosanifiwa na hadithi.
Lubna alionesha uwezo hata wa kufadhaika, pale ambapo aliona
kabisa ipo haja ya kufadhaika na kuonesha hali ya kuwa mwanamke mfanyabiashara
mwenye nazo wakati akilazimika.
Washiriki wakuu katika sinema hii wameitendea haki kwelikweli
hasa kwa kuonesha uhalisia wa 'tension' katika nafasi walizoigiza na Limo akiwa
katika nafasi ya furaha.
Hadithi hii ya mke aliyeoa waume wawili akakaa nao hadi
mwishoni anapoanguka katika kutolewa kwa siri zake, wakati aliposikia maneno
yasiyostahili kusikiwa na kuamua kufumania, imechanganywa na hisia za
kibinadamu ambapo Limo na Libat
nwaliomuoa Lubna bila kujuana na
kutopewa penzi walilazimika kuwa na wapenzi wengine nje waliofanya nao
mapenzi.
Ni hisia za kibinadamu kwa kuwa haiwezekani uoe mke ambaye
hatimizi masharti ya ndoa akisingizia yuko bize wakati wote.
Nilipata bahati ya kuongea naye Issa Mussa (Claud 112) kuhusu
maana ya sinema yake hasa eneo la utajiri wa mkike mwenye ofisi mbili na
utajiri wa kutosha na ushirikina alioufanya ambapo kwanza alitakiwa kufanya mapenzi
na baba yake ikawa ameshafariki, kisha mganga anamwambia aolewe ndoa mbili
(hiki ndio kisa hasa) za watu wenye majina silabi ya mwanzo inayofanana na
silabi ya jina lake.
Hadithi hii inakuacha na swali moja nini kitatokea kwa utajiri
wake baada ya kuamua kuishi na Libat huku ajmaa yake Dk Limo akiridhia? Claud
alisema hadithi kama maisha ya biandamu haziishi na watu wataamua nini
kitatokea.
Naweza kusema hadithi inavutia, waigizaji wanavutia, uchukuaji
picha unavutia, hisia zinavutia na sijnema ina mvuto wa pekee kutokana na
mbwembwe kubwa na umakini wa waigizaji:Ama hakika, sinema za aina hii ni chache
lakini unaweza pasishaka hata ukikurupushwa uzingizini kutosita kuitaja sinema
ya Tripple L .
Waigizaji
Warda Walid kama Lubna
Irene Paul kama Zulfa
Halima Yahaya kama Rukiya
Limo kama Pacho mwamba
Libat kama Issa Mussa



COMMENTS