STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY PRESS RELEASE Dodoma ...
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Dodoma
24.10.2012
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali
Mohamed Shein
ameutaka uongozi mpya wa UVCCM kuwa makamanda katika kuhakikisha
vijana wa CCM
wanakuwa mfano wa kutekeleza Ilani ya chama hicho na kukipa
ushindi katika chaguzi
zake zote zijazo ukiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango Dodoma, wakati
alipokuwa akifunga mkutano Mkuu wa nane wa Taifa wa Umoja wa
Vijana wa CCM, UVCCM.
Katika hotuba yake, Dk. Shein aliihakikishia Jumuiya hiyo kuwa
yeye na Rais wa
Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
wataendelea kutoa fursa
zaidi za uongozi kwa vijana kila inapoyumkinika.
Kutokana na hayo, Dk. Shein aliwataka vijana hao kwa upande wao
kuendelea
kukitumikia Chama hicho na kufanya kazi kwa moyo wote kwani vijana
hao ndio tegemeo
la ustawi wa CCM.
Aidha, Dk. Shein aliwaeleza vijana hao wa CCM kuwa propaganda
zinazofanywa na
wapinzani zinaweza kuhatarisha mshikamano wa kitaifa , hivyo ni
jukumu la UVCCM
kuhakikisha inajibu mapigo ya kila uzushi, ili wananchi wajue
ukweli badala ya
kuendelea kunyamaza kwa vile uongo ukizungumzwa sana unaweza
kuwapotosha watu.
Alieleza kuwa viongozi wote wa CCM wanatambua kuwa vijana
ndio nguvu kazi ya taifa
lolote na hivyo lazima Serikali yoyote iliyopo madarakani iwe na
mipango madhubuti
ya kuhakikisha vijana wanafanya shughuli zao kwa uhakika.
Dk. Shein aliuhakikishia mkutano huo Mkuu wa Taifa wa UVCCM kuwa
CCM itaendelea
kuzisimamia kikamilifu Serikali zote mbili kuwasaidia vijana ili
waweze kupata ajira
kwenye sekta rasmi na ile isiyokuwa rasmi.
Pia, aliwapongeza kwa kuanza mchakato wa kuanzisha Taasisi
ya Fedha inayojulikaa
kwa jina la Youth Microfinance Limited, inayojishugulisha na
mikopo midogo, mafunzo,
masoko na kuwaunganisha wajasiriamali katika mifuko ya Jamii.
Alieleza kuwa ushiriki wao mkubwa kuipigania CCM katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010
ndio uliofanikisha ushindi mkubwa wa kishindo wa chama hicho
katika pande zote mbili
za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Bila ya UVCCM kuwa madhubuti mimi na wenzangu katika CCM
tunaamini kwamba ushindi
huo usingekuwa wa kishindo kiasi hicho hata kama ungepatikana
kutokana na uimara,
mvuto pamoja na kupendwa kwa CCM na Watanzania walio
wengi”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar chini ya Serikali yenye
muundo wa Umoja wa
Kitaifa itaendelea kuwa na amani na utulivu licha ya hivi karibuni
kujitokeza
vikundi vya watu wachache wasiofuata misingi ya sheria na
kupelekea kufanya vitendo
vyenye kuhatarisha utulivu huo na kuwatia hofu wananachi.
Aliwahakikishia Wajumbe hao wa Mkutano Mkuu wa UVCCM kuwa
Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla zitaendelea kuwa mfano mzuri katika kudumisha amani na
utulivu
Dk. Shein hakuacha kutoa nasaha kwa viongozi wapya wa UVCCM
kuyatumia mapato
yanayotokana na vitega uchumi vya Jumuiya hiyo kwa kuekeza na
kamwe yasiwe chanzo
cha kuleta migogoro.
“Nimeambiwa kuanzia Januari 2013, UVCCM itaanza kuwa na mapato
yake yanayofikia dola
za Kimarekani 600,000 kwa mwka yanayotokana na vitega uchumi
vyake. Haya ni mapato
makubwa sana katika historia ya UVCCM”,alisisitiza Dk. Shein.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza mafanikio yaliopatikana
katika utekelezaji wa
Ilani ya CCM, nchini Tanzania katika Nyanja mbali mbali zikiwemo
afya, kilimo, maji,
barabara, elimu na sekta nyenginezo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamiazi Mkuu wa Uchaguzi huo
ambaye pia, ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Waziri wa Sera na Uratibu
Shughuli za Bunge Mhe.
Willium Lukuvi alimtangaza Sadifa Juma Khamis kuwa mshindi
kwa kupata kura 483
ambapo mpinzani wake Rashid Simai Msaraka amepata kura 263.
Lulu Mshamu Abdalla alijitoa katika kinyanganyiro hicho cha
kugombania nafasi hiyo
ya Uwenyekiti ambapo kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
ilichukuliwa na Mboni
Mohamed Mhita ambaye alipata kura 489 na kuwashinda Ally Salum na
Paul Cristian
aliyepata kura 241.
Katika uchaguzi huo pia nafasi mbali mbali ziligombaniwa zikiwemo
nafasi za
Halmashauri Kuu CCM Taifa kupitia UVCCM kutoka Bara ambapo
waliofanikiwa ni Petro
Magoti Itozwa, Benitho Michael Kunambi, Antony Peter Mavunde,
Fatma Jumbe Mwalim,
Jerry William Silaa na Deogratias Ndejembi.
Kwa upande wa nafasi ya Halmashauri Kuu kupitia UVCCM
Zanzibar ni Lulu Mshamu
Abdala, Michael Charles Bundala, Daud LKhamis Ismail, Shaka Hamidu
Shaka. Nafasi ya
Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa Zanzibar ni Omar Issa Ali, Wanu
Hafidh Ameir, Asya Ali
Khamis, Yohana Peter Martin na Mwanawewe Ussi Yahya.
Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa kutoka Tanzania Bara ni Halima
Abdallah Bulembo, Zainab
Othman Katimba,Ester Sato Makune, Gewe Rashid Gewe na Charles
Sylvester.
Naye Mwenyekiti mpya wa UVCCM, Sadifa Juma Khamis
Aliahidi uongozi uliotukuka na
kueleza kufarajika kwake na kuwapongeza vijana kwa kumpa nafasi
hiyo ambayo aliahidi
kwa mashirikiano ya pamoja kuendelesha gurudumu la umoja huo kwa
lengo la
kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Mapema uongozi uliomaliza muda wake chini ya ndugu Benno Malisa
ulitoa shukurani kwa
Rais pamoja na Wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
COMMENTS